![Hii Ni Nakala Ya Mtandao (Online Document)](https://data.docslib.org/img/3a60ab92a6e30910dab9bd827208bcff-1.webp)
Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) BUNGE LA TANZANIA _____________ MAJADILIANO YA BUNGE ______________ MKUTANO WA NANE Kikao cha Ishirini na Tisa – Tarehe 21 Julai, 2012 (Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Naibu Spika (Mhe.Job Y. Ndugai) Alisoma Dua HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI Hati Ifuatayo Iliwasilishwa Mezani na:- NAIBU WAZIRI WA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA NA WATOTO: Mheshimiwa Naibu Spika, nianze kwa kuwatakia Ramadhani Karim Waislamu wote waliojaliwa kuanza Mwezi huu Mtukufu wa Ramadhani Inshallah Mwenyezi Mungu azikubali saumu zetu na azikubali toba zetu. Naomba sasa kuwasilisha Mezani Randama za Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto kwa mwaka wa Fedha, 2012/2013. HOJA ZA SERIKALI Makadirio ya Matumizi ya Serikali kwa 2012/2013 Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika (Majadiliano yanaendelea) NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge na mimi nichukue fursa hii kuwatakia kila la heri wale wote ambao wanaanza mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani tunawatakia kila la heri kama ambavyo tumekwisha ambiana na sisi Bungeni hapa maandalizi yote yamekamilika. Kila siku ambazo tutakuwa tukifanya kazi jioni tutamaliza kwa muda ule ambao Mheshimiwa wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu alitoa hoja jana na tukakubaliana na kutakuwa na futari katika kantini yetu ya Bunge kila siku jioni, sasa uchangiaji unaendelea naomba mchangiaji wetu wa kwanza awe Mheshimiwa Martha Mlata. (Makofi) MHE. MARTHA M. MLATA: Mheshimiwa Naibu Spika ninakushukuru kwa kunipa nafasi hii na mimi niwatakie heri Waislamu wote Tanzania kwa mwezi huu Mtukufu. Pamoja na salamu hizo za heri naomba pia niseme kwamba kuna karatasi ilikuja mezani kwako jana na ninaamini bahasha ile ilikataa kufunguka kwa hiyo naomba niseme kilichokuwemo ni kwamba kwa niaba ya Watanzania wote na wapenzi wote wa Yanga napenda kuipongeza Yanga kwa ushindi mkubwa iliyojipatia jana, baada ya salamu hizo na wewe nikutakie heri pia kwa mchezo wa Simba leo. (Makofi/Kicheko) NAIBU SPIKA: Mheshimiwa leo ni mjadala wa Kilimo, Chakula na Ushirika. (Makofi/Kicheko) MHE . MARTHA M. MLATA: Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya salamu hizo ninaomba sasa niingie kwenye hoja iliyoko mbele yetu sitakuwa nimetenda haki kwa kutoa pole kwa Watanzania wote kwa janga kubwa ambalo limetupata Watanzania wote tuwe na subira tumwombe Mwenyezi Mungu na kuwaombea heri wale wote walionusurika na wale wote waliopatwa na misiba. Lakini pia nitoe pole kwa Mama mzazi wa Yohana ambaye alifariki katika vurugu za kisiasa kwa sababu anatoka kwenye kijiji ninachotoka na ni jirani yangu na ni kijana ambaye alikua mwalimu wa kwaya yangu kwa hiyo, ninaomba nitoe pole hizo. Mheshimiwa Naibu Spika, naomba pia nitoe shukrani za dhati kabisa kwa Serikali na hasa kwa Waziri Mkuu baada ya mimi kuleta hoja ya mgogoro wa zao la alizeti Singida, Serikali iliingilia kati na mgogoro huo sasa umekwisha. Hali sasa hivi ni shwari na wafanya biashara pamoja na wakulima na wote ambao ni wadau wa zao hilo wanaendelea na shughuli zao kama kawaida. Ombi langu ni kwamba tunaomba Serikali iwe makini kuwatendea haki watu ambao wanajitoa kwa dhati kujikwamua kutoka kwenye hali ngumu ya maisha hasa wakulima ninaomba wakulima hawa na wafanyabiashara wote na wadau wote wa zao hili wasipatiwe bughudha, pamoja na kwamba zao hili la alizeti ndilo linaloongoza katika Mkoa wangu wa Singida kwa biashara na kwa kipato lakini bado Serikali haijaweka mikakati mizuri kwa kutoa pembejeo kwa sababu hata mbegu zinazopelekwa kule ambazo zinatumika sasa hivi ni aina mbili. Mheshimiwa Naibu Spika, lakini ninaamini kuna mbegu zingine kuna kituo cha kuzalisha mbegu Pambaa ambacho ni cha Serikali. Ninaiomba Serikali izidi kupeleka zana za kilimo kule ili waweze kuzalisha mbegu nyingi zaidi za kuweza kutosheleza katika Mkoa wa Singida na hata Mikoa jirani kwa sababu mbegu inayotoka pale Mpambaa ina ubora zaidi kuliko wanayoitumia wananchi wa Mkoa wa Singida. Pamoja na kumaliza mgogoro wa zao la alizeti Singida, bado kuna mgogoro mkubwa sana wa zao la mahindi katika Mkoa wa Singida. Historia ya zao la mahindi katika Mkoa wa Singida mimi nimeikuta ni zao ambalo kwetu sisi ni chakula na Mkoa wa Singida una zone tatu. Kuna zone ambazo zinaweza kulima zao la mahindi, zao la mtama, pamoja na uwele na mazao mengine lakini cha kushangaza Serikali ninaomba ilete majibu hapa ni takwimu zipi, ni wataalamu gani walioenda Mkoani Singida wakapima udongo wa Mkoa wa Singida na kusema kwamba zao la mahindi haliwezi kustawi na kulimwa Mkoani Singida. (Makofi) Kwa hali kama hiyo wananchi wamekuwa kwenye hali tete wakizuiwa kulima zao la mahindi hata takwimu zinazopatikana kwenye Mkoa wa Singida kwa zao la mahindi iwe pato au iwe takwimu tu kuwa Mkoa umezalisha kiasi gani haziingizwi na wala haziletwi kwenye RCC eti kwa sababu zao lile halitakiwi kulimwa Mkoani Singida. Ninaomba Mheshimiwa Waziri anakapokuja kujibu hoja zetu anieleze ni wataalamu gani. Mheshimiwa Naibu Spika, wataalamu walitumia nini kuona kuwa Mkoa ule haufai kulima zao la mahindi. Ninaomba kama hataleta mimi nitaomba nitoe shilingi ili kuonyesha kuwa wakulima wa zao la mahindi katika Mkoa wa Singida hawaungi Mkono Bajeti hii. Mheshimiwa Naibu Spika, zao la mahindi lililetewa pembejeo lakini pembejeo zile zikakataliwa eti kwa sababu zao hilo halitakiwi kulimwa Mkoani Singida. Ni kweli kuwa Mkoa wa Singida kuna maeneo ambayo yanastawisha mtama, uwele, ufuta na mazao mengine. Hivi mtu anapojitoa kulima ni Serikali gani ambayo inamzuia mtu na kukataa takwimu ambazo ni wazi kabisa na ni sahihi kabisa na ni sahihi kabisa zao lile hata mwaka huu vijana wengi na wakulima wengi wametoka kwenye umasikini kutokana na zao la mahindi. Ni zao la pili katika Mkoa wa Singida kwa biashara leo hii wakulima wanapigwa stop na Serikali. Mimi ninaishangaa sana Serikali ninaomba Waziri utakapoleta majibu yako ulete majibu fasaha na uniambie takwimu zake zikoje, pato lake likoje kwa sababu mimi binafsi nimeshindwa kupata takwimu ya zao hili kutokana na kwamba hata wataalamu wanaogopa kutoa takwimu na kuzungumzia zao hili kwa sababu watapata demotion kwa kuzungumzia na kusimamia zao hili. Ninaomba sana Serikali ije Mkoa wa Singida itusaidie kutatua mgogoro huu. Katika masuala ya umwagiliaji kuna scheme nyingi ambazo zimejengwa Mkoani Singida lakini scheme zile mimi bado mdogo leo ni Mbunge na ni Mbunge kwa kipindi cha mara ya pili ziko palepale tunapitisha Bajeti hapa ooh tutaleta kuna hela zimewekwa hivi hii Bajeti ambayo tunasomewa hapa sasa hivi kwanza mimi nilikuwa nataka kusema hii Bajeti ina ujumbe gani. Waziri amesoma anataka kutueleza nini kwenye hotuba yake hii aliyoitoa, maana mimi sielewi naomba ujumbe kamili juu ya hotuba hii kwamba ujumbe wake ni nini maana hata fedha zilizotengwa humu mimi naona ni kama kiini macho na ndiyo maana hata miradi au schemes zilizoko Mkoa wa Singida hazitekelezeki kwa sababu ya viini macho vilivyomo kwenye Bajeti husika kila mwaka. Mheshimiwa Naibu Spika, hivi inawezekanaje kweli wewe na Mke wako na familia yako mnapanga Bajeti kila mtoto unamwambia lete mahitaji yako halafu unamwambia Bajeti inakuwa ni 100,000 halafu unamwambia kuwa mimi nina 20,000 halafu unawaambia kuwa 80,000 nitakwenda kuomba kwa Mlata, nitakwenda kuomba kwa Mheshimiwa Joseph Selasini na mahali pengine, unajuaje kama utapata hizo hela? Hiyo ni Bajeti gani, kwa nini tunaletewa Bajeti ya kusubiri kupewa hela kwa watu mimi ninaomba pale tunapoweka kipaumbele kwenye jambo fulani fedha za kusubiri kupewa tusiziingize kwenye Bajeti tujue moja kwa moja kwamba hela zetu za ndani ndizo zitakazoweza kukomboa jambo letu tuliloliweka kwenye kipaumbele. Mheshimiwa Naibu Spika, mimi kwa kweli hapa niliposimama ninashindwa kuunga mkono hoja hii kwa sababu sina hakika Mwangeza kuna miundombinu ambayo ilishawekwa mpaka ina chakaa inasubiri mvua inyeshe ndiyo yale maji yapite hakuna mabwawa. Ukienda Kata ya Msingi kule vilevile naambiwa Mwanga kutakuwa sijui na mradi wa matone, matone gani kama mlishindwa kuendeleza miradi iliyopangwa miaka mingi hayo matone mtayaletaje mimi kwa kweli ninashindwa kuunga mkono hoja. Hapa juzi nimeuliza kuhusu suala la kilimo cha vitunguu nikaambiwa oh!tutawachimbieni mabwawa hapa hata sioni na kuwezesha watu sijui mashine, sijui kitu gani hazipo sasa mimi nitaungaje mkono hoja wakati watu walishapokea kwa furaha kabisa nilikuwa ninaomba sana Serikali tuwe makini katika kuweka Bajeti kwenye vipaumbele tusitegemee fedha za kuomba. Mheshimiwa Naibu Spika, lakini pia watendaji wetu hebu tutende haki kama fedha zimetolewa basi mtoe fedha ambazo zinakwenda kukidhi ule mradi, tusiwe tuna dokoadokoa halafu tunaacha tunawadanganya wananchi. (Makofi) Wakulima wa Mkoa wa Singida na Mikoa hii kama ya Dodoma Mikoa ambayo ni kame mnakaa mnapiga marufuku kulima mazao eti hayastawi kwenye ukame mnapigaje marufuku badala ya kusaidia zao, badala ya kusaidia wakulima chimbeni mabwawa wekeni miundombinu tuvune maji yanayomwagika kwa wakati mmoja mvua ikienda zake tunabaki na maji yetu badala ya kuwasaidia watu mnaanza kuwapiga marufuku mimi nashindwa kuelewa. (Makofi) Nilikuwa ninaomba pia pembejeo kwenye zao la mtama pamoja na mazao mengine kama uwele mimi naomba tupatiwe pembejeo hizi ili wale watu wanaolima mtama, wanaolima uwele na wao waweze kupata pembejeo. Mimi kwa kweli nitashindwa kabisa kuunga mkono hoja lakini nilikuwa ninaomba pia kuweza kuwawezesha wakulima waweze kupata mikopo. Kuna watu ni masikini wakulima bado wanatumia jembe la mkono, halafu unamwambia eti unazuia njaa, unazuia njaa gani umemwacha mtu analima kwa mkono kwa nini usimpelekee pembejeo za kujikwamua kulima eneo kubwa usidhani
Details
-
File Typepdf
-
Upload Time-
-
Content LanguagesEnglish
-
Upload UserAnonymous/Not logged-in
-
File Pages104 Page
-
File Size-