Nakala ya Mtandano (Online Document) BUNGE LA TANZANIA _________________ MAJADILIANO YA BUNGE ___________________ MKUTANO WA KUMI NA TISA Kikao cha Saba – Tarehe 24 Machi, 2015 (Mkutano Ulianza Saa 3.00 Asubuhi) D U A Spika (Mhe. Anne S. Makinda) Alisoma Dua SPIKA: Waheshimiwa Wabunge tukae. Katibu! HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI Hati Zifuatazo Ziliwasilishwa Mezani na:- WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA URATIBU NA BUNGE: Taarifa ya Matoleo yote ya Gazeti la Serikali, Pamoja na Nyongeza zake zilizochapishwa tangu Kikao cha Mwisho cha Mkutano wa Bunge uliopita kama ifuatavyo:- 1. Toleo la Gazeti Namba 6 la tarehe 6 Februari, 2015 2. Toleo la Gazeti Namba 7 la tarehe 13 Februari, 2015 3. Toleo la Gazeti Namba 8 la tarehe 20 Februari, 2015 4. Toleo la Gazeti Namba 9 la tarehe 27 Februari, 2015 5. Toleo la Gazeti Namba 10 la tarehe 6 Machi, 2015 6. Toleo la Gazeti Namba 11 la tarehe 13 Machi, 2015 NAIBU WAZIRI WA FEDHA (MHE. ADAM K. MALIMA): Taarifa ya Utendaji wa Soko la Bima kwa Mwaka Ulioishia tarehe 31 Desemba, 2013 (The Annual Insurance Market Performance Report for the Year ended 31st December, 2013). 1 Nakala ya Mtandano (Online Document) MASWALI NA MAJIBU Na. 67 Kupanua Mradi wa Maji Uroki – Bomang’ombe MHE. GRACE S. KIWELU (K.n.y. FREEMAN A. MBOWE) aliuliza:- Kata ya Hai katika Jimbo la Hai, inayokadiriwa kuwa na wakazi wasiopungua elfu hamsini (50,000) inapata huduma ya maji kutoka mradi wa maji wa Uroki Bomang‟ombe ambao ulijengwa na Serikali ya Ujerumani kwa kushirikiana na Kanisa ka KKKT. Awali mradi huu ulikadiriwa kuhudumia watu wapatao elfu kumi na tano (15,000) tu. Kwa kuwa idadi ya watu imeongezeka kwa kiasi kikubwa kinyume na maotoe ya awali. Je, ni lini Serikali itapanua mradi huu ili kukabiliana na upungufu mkubwa wa maji unaosababishwa na ongezeko hilo la watu. NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA, (TAMISEMI): Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu naomba kujibu swali la Mheshimiwa Freeman A. Mbowe, Mbunge wa Hai, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Spika, Mji wa hai unahudumiwa na Mradi wa Maji wa Uroki-Bomang‟ombe. Mradi huu unayo jumuiya moja ya watumia maji ya Uroki Bomang‟ombe inayohudumia vijiji 14 ambavyo ni Shari, Mamba, Kyeeri, Uswaa, Sawe, Sonu, Ngira, Roo, Kware, Kwa Sadala, Chekimaji, Sanya-Station, Chemka, Rundugai na Mji Mdogo wa Hai. Ni kweli kwamba mahitaji ya maji kwa sasa ni makubwa ikilinganishwa na uwezo wa mradi kuhudumia maeneo hayo. Mheshimiwa Spika, kwa kutambua ukubwa wa tatizo la maji kwa wananchi wa maeneo hayo, tayari Serikali imefanya upya usanifu wa mradi na kubaini kwamba zinahitajika shilingi bilioni 9.9 ili kukamilisha upanuzi wa mradi huo. Wizara ya Maji imepanga kutekeleza mradi huu kwa awamu katika awamu ya pili ya utekelezaji Programu ya Maendeleo ya Sekta ya Maji ambayo itatekelezwa kwa miaka mitano kuanzia mwaka 2014/2015. Utekelezaji wa mradi huu utaanza mara baada ya fedha zinazohitajika kupatikana. MHE. GRACE S. KIWELU: Mheshimiwa Spika, ahsante sana, nina swali moja la nyongeza. Majibu ya Naibu Waziri yanasema ukamilishaji wa mradi huu utakamilika mpaka fedha zitakapopatikana. Kwa kuwa tunakwenda mwisho wa Bajeti hii ya 2014/2015 na fedha hizo hazijapatikana, nini kauli ya Serikali kwa wananchi wa Bomang‟ombe hususani wanawake ambao wanapata shida kutafuta maji hayo? NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri Mkuu naomba kujibu swali la Mheshimiwa Grace Kiwelu, kama ifuatavyo:- Kama ambavyo amejibu Mheshimiwa Naibu Waziri ni kwamba mradi huu ulitengewa fedha mwaka jana katika Bajeti shilingi milioni 225 baadaye Mji huu ukatangazwa Mji Mdogo. Kwa hiyo kutakuwa na Mamlaka ya Maji ambayo inatakiwa kuundwa. Kwa hiyo, mradi huu sasa ulikadiriwa kuwa na watu 10000 sasa utakuwa na watu 50000. Kwa hiyo, ndiyo maana 2 Nakala ya Mtandano (Online Document) tumefanya usanifu upya na tutaingiza katika Bajeti inayokuja. Lakini fedha kwa ajili ya mradi wa awali tulishazituma na zimepelekwa katika vijiji vingine katika Wilaya ya Hai. SPIKA: Sikuona wengine, Mheshimiwa Selemani Jafo, nimekuona. MHE. SELEMANI SAID JAFO: Mheshimiwa Spika, ahsante. Mheshimiwa Spika, kwanza niishukuru Serikali kwa kuhakikisha kwamba inashughulikia miradi ya maji. Hivi sasa mvua za masika zimeanza lakini katika Tanzania yetu hii kulikuwa na miradi ya maji ya World Bank ambayo mingine ilikuwa inahusisha ujengaji wa marambo. Kwa mfano, mradi wa Chole ambao Mheshimiwa Naibu Waziri aliutembelea, lakini miradi kama hiyo iko sehemu mbalimbali Tanzania. Mheshimiwa Spika, mvua inaponyesha malambo yale hayajakamilika hivi sasa kutokana na ukosekanaji wa fedha na wakandarasi wametoka site. Ina maana kwamba mradi wa shilingi 1.5 billion tutapata variationya 1.8 baadaye. Sasa Serikali ina mpango gani wa kuhakikisha kwamba hii miradi ya marambo ambayo iko haijakamilika na wakandarasi wako site itoe pesa za haraka wakandarasi warudi site ili mradi tusije tukapoteza pesa na miradi ikashindwa kabisa kutekelezeka? NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Jafo kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Spika, nakubaliana naye na nimefika katika bwawa hili la Chole kuna kazi kubwa imefanyika na sasa kuna ucheleweshaji tu wa malipo. Kama nilivyosema jana na juzi kwamba mara tupatapo fedha tutatoa kipaumbele kwa miradi inayoendelea ili iweze kukamilika. Na. 68 Kushindwa Kutekelezwa kwa Miradi ya Maendeleo Katika Halmashauri MHE. DAVID E. SILINDE aliuliza:- Miradi mingi ya Maendeleo inayopangwa na Halmashauri zetu imekuwa ikishindwa kutekelezwa kwa kila mwaka licha ya Bajeti zinazopangwa kupitishwa na Bunge. Je, kwa nini Bajeti hizo za Halmashauri hazitekelezwi kwa kadiri fedha zinavyopangwa na Bunge? NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (TAMISEMI): Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri Mkuu naomba kujibu swali la Mheshimiwa David Ernest Silinde, Mbunge wa Mbozi Magharibi, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Spika, utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo katika Halmashauri nchini huzingatia vipaumbele na Bajeti inayopitishwa na Bunge kila mwaka. Sehemu kubwa ya fedha zinazotumika kutekeleza miradi hiyo zinatokana na ruzuku kutoka Serikali Kuu na Mapato ya Ndani ya Halmashauri. Mheshimiwa Spika, sababu za kutokufikiwa kwa malengo ya utekelezaji wa baadhi ya Miradi ya Maendeleo katika Halmashauri nchini ni Halmashauri hizo kuchelewa kupokea au 3 Nakala ya Mtandano (Online Document) kupokea fedha pungufu hasa zile zinazotoka kwa wahisani na Halmashauri zenyewe kutokufikia malengo ya makusanyo ya mapato ya ndani ya kila mwaka kutokana na sababu mbalimbali. Kwa mfano, Halmashauri ya Wilaya ya Momba katika Bajeti yake ya Mwaka 2013/2014 iliidhinishiwa ruzuku kutoka Serikali Kuu ya shilingi bilioni 4.65 lakini ilipokea shilingi bilioni 3.65 ambayo ni sawa sawa na asilimia 78 na katika Bajeti ya mwaka 2014/2015 Halmashauri hii iliidhinishiwa shilingi bilioni 5.1 na imeshapokea shilingi bilioni 2.3 sawa na asilimia 46 hadi Februari, 2015. Kwa upande wa Mapato ya Ndani, Halmashauri hii katika mwaka wa fedha 2013/2014 ilikadiria kukusanya shilingi bilioni 1.6 lakini ilifanikiwa kukusanya shilingi bilioni 1.15 sawa na asilimia 71 ya Makisio. Mheshimiwa Spika, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) inaendelea kuzijengea uwezo Halmashauri ili kuongeza Mapato ya Makusanyo ya ndani ambapo asilimia 60 ya fedha hizo zinatakiwa kutumika kutekeleza Miradi ya Maendeleo. Kupitia mradi wa miji ya kimkakati yaani Tanzania Strategic Cities Project tayari Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI imeanzisha mfumo wa utambuzi wa majengo ambayo yanastaili kulipiwa kodi. Mradi wa kielektroniki unaojulikana kama Local Government Revenue Collection Information System. Lengo la mfumo huu ni kuziwezesha Halmashauri kuwa na takwimu sahihi za majengo ili kuongeza mapato yanayotokana na kodi za majengo. MHE. DAVI E. SILINDE: Mheshimiwa Spika, ahsante sana kwa kunipatia nafasi niulize maswali mawili madogo ya nyongeza. Ikiwa Mheshimiwa Waziri amekiri kabisa kwamba karibu kila mwaka Serikali imeshindwa kupeleka Bajeti kwa asilimia 100, sasa itueleze ni lini sasa Serikali itakuwa na uwezo wa kupeleka asilimia 100 ya Bajeti tunayopanga na Bunge kwenda katika Halmashauri zote nchini. (b) Kwa kuwa mara nyingi kama unavyoona kwenye swali langu hapo alipouliza mpaka sasa amepeleka asilimia 46 tu katika Halmashauri ya Momba na tumebakiza miezi mitatu kuingia kwenye mwaka mpya wa fedha. Sasa Serikali itueleze ni kwa nini imekuwa karibu miezi tisa ya Bajeti nzima haipeleki fedha ila mwishoni mwishoni ndiyo inaenda kubaka mpaka kufikia asilimi 70 au 80? Je, yaani hizo fedha zinapatikana mwishoni na siyo mwanzoni? Kwa hiyo, Serikali itueleze kwa nini fedha hizo zinapatikana mwishoni? NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA, (TAMISEMI): Mheshimiwa Spika, ninaomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa David Ernest Silinde, Mbunge wa Mbozi Magharibi, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Spika, concerns anazozileta Mheshimiwa Mbunge sisi wote tunakubaliana nazo. Halmashauri zote katika nchi yetu ya Tanzania hakuna ambayo imepokea asilimia 100 na ni kweli anachosema, huyu anazungumza habari ya Momba, Momba ambayo ni Halmashauri mpya imeanza mwaka 2013/2014. Bajeti ni mpango wa Serikali unaokuonyesha hela zitakazopatikana na hela zitakavyotumika. 4 Nakala ya Mtandano (Online Document) Ni kweli kabisa kwamba hapa sisi tunavyomsikiliza Waziri wa Fedha akizungumza hapa anasema asilimia 40 ya mapato ya Serikali so far tulikuwa tunategemea wahisani kutoka nje na asilimia 60 ndizo ambazo zinatoka kutoka humu
Details
-
File Typepdf
-
Upload Time-
-
Content LanguagesEnglish
-
Upload UserAnonymous/Not logged-in
-
File Pages120 Page
-
File Size-