Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) BUNGE LA TANZANIA _______________ MAJADILIANO YA BUNGE _______________ MKUTANO WA NNE Kikao cha Tisa – Tarehe 26 Juni, 2006 (Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Spika (Mhe. Samuel J. Sitta) Alisoma Dua HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa mezani na:- WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU (MHE JUMA J. AKUKWETI) Hotuba ya Bajeti ya Waziri Mkuu, kwa Mwaka wa Fedha 2006/2007. MHE. GEORGE M. LUBELEJE - MWENYEKITI WA KAMATI YA KATIBA, SHERIA NA UTAWALA:- Taarifa ya Kamati ya Katiba, Sheria na Utawala Kuhusu Utekelezaji wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa kwa mwaka wa Fedha uliopita pamoja na Maoni ya Kamati Kuhusu Makadirio ya Matumizi ya Ofisi hiyo kwa mwaka 2006/2007. MHE. DR. WILLBOD P. SLAA (K.n.y. HAMAD R. MOHAMED) - MSEMAJI WA UPINZANI KWA OFISI YA WAZIRI MKUU:- Taarifa ya Msemaji Mkuu wa Kambi ya Upinzani Kuhusu Hotuba ya Bajeti ya Waziri Mkuu kwa Mwaka wa Fedha 2006/2007. 1 SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, tunao wageni kadhaa. Naona Waheshimiwa Wabunge wamekuwa na Utamaduni mpya sasa wa kuleta majina mengi tu ya wageni wetu. Naomba sana ili tusiingiliane sana na kipindi cha maswali, basi niwatangaze mara baada ya kipindi cha maswali. Waheshimiwa Wabunge, ila ninalo tangazo na ni kawaida yangu kwamba yakitokea matukio mazuri tu kwa wenzetu Waheshimiwa Wabunge ni vizuri niweze kuwafahamisha. Nimearifiwa na Chama cha Mapinduzi kwamba jana Halmashauri Kuu ya Chama hicho ilifanya uteuzi wa uongozi mpya ndani ya Sekretarieti ya Chama na kwa kuwa wanne kati ya hao walioteuliwa au waliochaguliwa na Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM ni Waheshimiwa Wabunge wa Bunge hili nilikuwa naomba niweze kuwatambua kwa sababu ni wenzetu humu. Ninaviomba Vyama vingine inapotokea hivyo basi watuarifu hatutasita kuwatangaza. (Makofi) Wa kwanza ni Mheshimiwa Yusuf Rajab Makamba, Mbunge wa Kuteuliwa, ambaye amechaguliwa na NEC kuwa Katibu Mkuu wa CCM. Mwingine ni Mbunge wa Siha Mheshimiwa Aggrey Mwanri, huyu sasa Waheshimiwa Wabunge, ndiyo Katibu Mwenezi wa Taifa wa Chama cha Mapinduzi. Waheshimiwa Wabunge, mwingine ni Mbunge wa Igunga, Mheshimiwa Rostam Aziz huyu sasa ndiyo Mweka Hazina wa Chama cha Mapinduzi. Halafu upande wa Idara wenyewe wanaita Organization ameteuliwa Mheshimiwa Kidawa Hamid Salehe. Mheshimiwa Dr. Asha-Rose Migiro ameteuliwa kuwa ni Katibu wa Masuala ya Mambo ya Nje katika Chama cha Mapinduzi. Ahsanteni sana. (Makofi) Waheshimiwa Wabunge, kama nilivyotoa wito kwa wenzetu wa Vyama vyote vingine nadhani ni vizuri tuipongeze CCM kwa kutambua Hazina kubwa ya uwezo uliomo ndani ya Bunge letu hili. Tunaomba Vyama vyote vingine vinapotaka kupata watu madhubuti wa kuendesha mambo yao waangalie ndani ya Bunge hili. Ahsanteni sana. (Makofi) MASWALI NA MAJIBU Na. 78 Utekelezaji wa Sheria ya The Parliamentary Services Commission 1997 MHE. MOHAMED R. ABDALLAH aliuliza:- Kwa kuwa Bunge lilipitisha Sheria ya “The Parliamentary Services Commission Act” ya 11, 12 (1) na (3) inatoa madaraka kwa Bunge kuwa na Bajeti yake na kuisimamia na kwa kuwa mahitaji ya vifungu hivyo hayatekelezwi hivi sasa kama inavyotakiwa na hivyo sheria kutekelezwa bila ujumla wake:- (a) Je, ni nini sababu inayosababisha sheria hiyo isitekelezwe kwa ujumla wake? 2 (b) Je kwa nini Bunge lisiwe na Vote zake na kuzisimamia lenyewe kama ilivyo kwa Wizara za Serikali? NAIBU WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU(MHE. DR. LUKA J. SIYAME) alijibu:- Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu, naomba kabla ya kujibu swali la Mheshimiwa Mohamed Rished Abdallah, Mbunge wa Jimbo la Pangani, kutoa maelezo yafuatayo:- Mheshimiwa Spika, ni kweli kwamba mwaka 1997, Bunge lako Tukufu lilipitisha Sheria ya Tume ya Huduma za Bunge, yaani “The Parliamentary Services Commission Act, 1997 (Act No. 14 of 1997)” ambayo pamoja na mambo mengine, imeweka utaratibu wa kushughulikia fungu la fedha kwa ajili ya kikidhi mahitaji mbalimbali ya Bunge. Katika Sheria hiyo, kifungu cha 11 kinatamka bayana kuwa, fedha zinazohitajika kwa shughuli za Bunge zitalipwa na Hazina ikiwa makisio yake yamepitishwa na Bunge na kuwa fedha hizo zitatoka katika Mfuko Mkuu wa Serikali (i.e. Consolidated Fund). Aidha, kifungu cha 12(1), (2) na (3) kimetamka hatua mbalimbali za kuzingatiwa wakati wa kutayarisha Bajeti ya Bunge hadi kuidhinishwa na Bunge hili Tukufu. Mheshimiwa Spika, baada ya maelezo hayo, mafupi, naomba sasa kwa niaba ya Mhesimiwa Waziri Mkuu, kujibu swali la Mheshimiwa Mohamed Rished Abdallah, Mbunge wa Pangani, lenye sehemu (a) na (b) kama ifuatavyo:- (a) Kwa mujibu wa Sheria Na. 14 ya mwaka 1997, utaratibu unaotumika kuandaa Bajeti ya Ofisi ya Bunge unazingatia maelekezo ya Sheria hiyo kama nilivyobainisha katika maelezo ya ufafanuzi na Mheshimiwa Waziri Mkuu ndiye mwenye dhamana ya kuwasilisha makisio ya Bajeti hiyo kwenye Baraza la Mawaziri na hatimaye hapa Bungeni ili kuidhinishwa. Utaratibu huu ndio unaotumika kwa baadhi nchi za Jumuiya ya Madola ambazo zinatumia Mfumo uitwao Westminster. Miongoni mwa nchi hizo ni pamoja na Australia, India, Jamaica na Malaysia. (b) Bunge lina fungu lake kama ilivyo Wizara na Taasisi nyingine na linapewa fedha zinazohitajika kutoka katika Mfuko Mkuu wa Serikali yaani Consolidated Fund kupitia Fungu (Vote ) 42. Pia Mahakama ni Mhimili wa Dola kama ilivyo Bunge na yenyewe kwa mfumo unaotumika hivi sasa inapewa fedha kutoka Mfuko Mkuu wa Serikali kupitia Fungu 40. Mheshimiwa Spika, mfumo huu unalenga zaidi katika mgawanyo wa madaraka na majukumu kwa mihimili ya Dola iliyopo kama ilivyofafanuliwa ndani ya Katiba yetu ya Jamhuri ya Muungano ya mwaka 1977. MHE. MOHAMED RISHED ABDALLAH: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi niulize maswali mawili madogo ya nyongeza. 3 Mheshimiwa Spika, kwa kuwa sheria hii inatokana na Katiba ambayo ipo kwenye Cap.2. Mheshimiwa Spika, naomba ninukuu kidogo anasema: “This Act shall be read as one with the Constitution of the United Republic of Tanzania.” Kwa maelezo ya Mheshimiwa Naibu Waziri na procedure zote kwa ajili ya gharama za kuendeshea Bunge kama alivyoeleza. Mimi naamini kwamba utaratibu ule hauko wazi kama alivyosema Mheshimiwa Naibu Waziri kama vile tunavyopitisha bajeti za Wizara. Tunapitisha tu kifungu cha Bunge ili kupitisha gharama za Bunge. Hilo moja. La pili, sheria pia inatambua kuwepo kwa Waziri ambapo inasema: “ the Minister responsible for Parliamentary Affairs.” Mheshimiwa Spika, naomba niulize Waziri analisaidiaje Bunge katika kupanga na kuratibu shughuli za mafungu ya fedha kwa kuendeshea Bunge wakati sisi hatuoni kama kuna dalili hizo za Waziri kulisaidia Bunge katika shughuli zake za kila siku? Ahsante sana. (Makofi) WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU (MHE. JUMA J. AKUKWETI): Mheshimiwa Spika, kama tulivyojibu kwenye swali la msingi au jibu letu la msingi kuna mihimili mitatu ambayo yote inafanya kazi katika nchi hii moja. Kila mhimili unajitegemea katika masuala yake. Sasa inapofika wakati wa fedha kila mhimili unapanga Bajeti yake na baada ya kupanga Bajeti yake inapelekwa kule ambako inaweza kutafutiwa fedha na kwa hivi sasa ni Hazina na Hazina ndiyo baada ya kujua fedha ziko kiasi gani katika Taifa letu inagawa sasa zipi ziende wapi kutokana kwanza na mahitaji. Lakini pia mapato ya Taifa letu na kazi ya Waziri ni kuhakikisha hiyo process yenyewe. Mheshimiwa Spika, lakini Mheshimiwa Mbunge nadhani anafahamu katika sheria yetu kifungu 13 kinasema ifuatavyo na naomba nikisome moja kwa moja. Kifungu cha 13 katika sheria ya Bunge ambacho kina guide mambo ya Bunge kinasema hivi: “ The Commission shall from time to time prepare and recommend to the President the rates of salaries, allowances and other recommendations to be paid to Members of Parliament.” Nadhani utaratibu huu ni mzuri kwamba Bunge lenyewe baada ya mahitaji yake linapeleka moja kwa moja kwa Mheshimiwa Rais na Mheshimiwa Rais anatumia utaratibu wake ili kuhakikisha anakubali au anakataa yale maombi ya Bunge. Mimi nadhani huu ni utaratibu mzuri ili nguzo hizi tatu zisiweze kugongana, lakini wote tutatafuta fedha kwenye Mfuko mmoja kwa ajili ya Taifa letu. (Makofi) MHE KABWE Z. ZITTO: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza na wakati huo huo nitumie fursa hii kumpongeza Mheshimiwa Aggrey Mwanri kwa kuwa Katibu Mwenezi wa Chama, kweli kimepata mwenezi. (Makofi) Mheshimiwa Spika, swali langu ni dogo tu. Kwa kuwa matamkwa ya swali la msingi ni matamkwa ya Kisheria na matamkwa haya yameonekana kwamba hayafanyiki. Je, Serikali haioni kwamba imefika wakati muafaka Bunge liwe huru zaidi na kujipangia vote yake na Bajeti yake na kuisimamia yenyewe ili kuepuka kuwekwa chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu na chini ya Wizara ya Fedha? 4 WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU (MHE. JUMA J. AKUKWETI): Mheshimiwa Spika, nionavyo mimi utaratibu huu unafuata kabisa jinsi sheria inavyotaka. Mimi naomba niseme hivi Mheshimiwa Kabwe Zitto, kama nia ni kwamba kila nguzo ijipangie yenyewe basi kuna hatari ya nguzo hii ambayo ina mamlaka makubwa katika nchi yetu ikajipangia marupurupu makubwa kuliko hata kutoangalia nguzo zingine. Utaratibu unaotumika sasa ndiyo unaojenga haki ya mgawanyo sawasawa katika Taifa letu. Kuhakikisha Mahakama inapata kiasi chake ili isikwame na kuhakikisha kwamba Bunge linapata kiasi chake ili lisikwame na Executive inapata kiasi chake ili isikwame. Mheshimiwa Spika, nataka kumhakikishia Mheshimiwa Kabwe Zitto, kwamba kwa utaratibu huu mpaka sasa Bunge halijawahi kukwama kufanya kazi kwa sababu Executive haikutoa fedha. Na yeye tayari naweza kum-challenge aseme ni lini Bunge limeshindwa kufanya kazi kwa kukosa
Details
-
File Typepdf
-
Upload Time-
-
Content LanguagesEnglish
-
Upload UserAnonymous/Not logged-in
-
File Pages114 Page
-
File Size-