Constitution of Kenya Review Commission (Ckrc) Verbatim Report of Constituency Public Hearings, Marakwet West Constituency, Kapc
CONSTITUTION OF KENYA REVIEW COMMISSION (CKRC) VERBATIM REPORT OF CONSTITUENCY PUBLIC HEARINGS, MARAKWET WEST CONSTITUENCY, KAPCHEROP CATHOLIC HALL ON 2ND JULY 2002 CONSTITUENCY PUBLIC HEARINGS MARAKWET WEST CONSTITUENCY, KAPCHEROP CATHOLIC HALL HELD ON 2ND JULY, 2002 Present Com. Mrs. Alice Yano - Chairing Com. Isaac Lenaola Com. Prof. W. H. O. Okoth-Ogendo Secretariat in Attendance Triza Apondi - Programme Officer Jomo Nyambe - Asst. Programme Officer Martina Odhiambo - Verbatim Recorder Johnson Kasenge - 3Cs Member Meeting started at 10.00 a.m. with Com. Alice Yano on the chair. Fr. George Iregi: Tuungane pamoja tuweze kuombea nchi yetu na kuombea siku ya leo, kwa ajili ya yale yote ambayo tumekuja kujatenda. Kwa jina la Baba, na Mwana, na la Roho Mtakatifu, Amina. Baba mwema, Mungu wa milele uishiye daima. Tunakushukuru kwa ajili ya siku ya leo, tunakushukuru kwa ajili ya siku hii ambayo umeitenga hili tuje tuweze kama wananchi wa hapa, kuja kujiwakilisha, na kutoa mengi ambayo tunafaa kuyatoa kwa ajili ya Maendeleo mema ya nchi yetu. Tunakushukuru hasa sana kwa ajili ya safari njema umewajalia hawa wageni wetu, tunauliza Baba upate kuwapatia wao utulivu, utupatie nasi utulivu vile vile. Hili katika yote ambayo tutakayotenda, yote ambayo tutakayosema Baba, yawe yameongozwa na 2 Roho wako Mtakatifu, na katika yote, yaweze kutuongoza sisi kuwa wananchi bora zaidi wa Kenya, na katika yote, tuendelee kufurahia uhuru wetu, na kufurahia yale yote ambao Mungu wewe umetupatia sisi. Tunaomba basi siku ya leo iweze kuwa imebarikiwa, na uwabariki wote ambao wangali njiani wanakuja, hili sote kwa pamoja, tuweze kuunganika katika mkono mmoja, kwa ajili ya manufaa ya nchi yetu na manufaa ya maisha yetu.
[Show full text]