January 27, 2016 COUNTY ASSEMBLY DEBATES 6

MOMBASA COUNTY ASSEMBLY HANSARD REPORT Wednesday, 27th January, 2016 The House met at 9:06am. (Hon. Speaker Mr. Rajwayi in the chair) PRAYERS

Hon. Speaker: You may have your seats Hon. Members.

Clerk there was unfinished business yesterday which was a motion; so the first business should be the Hon. from Port Reitz Ward, there was a motion by the Hon. Member for Port Reitz Ward; I think we should start with that.

COMMUNICATION FROM THE CHAIR

Hon. Members as we all know today the party leader of CORD and ODM is in town and he has a special business to do, so this House will only discuss one motion and then we will adjourn till the afternoon. Thank you.

PAPER

Yes Mheshimiwa Swaleh.

Hon. Mwalimu: Thank you Mr. Speaker Sir. Mr. Speaker Sir on behalf of the chairman who is doing some technicalities around...I hereby stand to lay a report; a paper before this Hon. House of which you are going to allocate the right time for it to be debated Mr. Speaker.

(Hon. Mwalimu lays paper)

Hon. Speaker: Thank you Hon. Fadhili. The report will be tabled next week to the business committee where we will give direction.

NOTICE OF MOTION

DISCLAIMER: The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor Page 1 January 27, 2016 COUNTY ASSEMBLY DEBATES 6

Hon. Speaker: Hon. Serah Nyamvula ….yes Hon. Akinyi?

Hon. (Ms.) Akinyi: Thank you Mr. Speaker Sir, due to unavoidable circumstances Hon. Nyamvula is not with us, she asked me to table this motion.

(Hon. (Ms.) Akinyi reads the Notice of Motion)

MAPPING OF TOURIST ATTRACTION SITES WITHIN THE COUNTY

THAT AWARE, Mombasa is one of the leading tourist destinations in the world.

FURTHER AWARE, that the fourth schedule part II 4(g) and 7(d) respectively have devolved museums and local tourism.

COGNIZANT of the fact that there are numerous historical sites and sites rich in cultural heritage within the county which if fully exploited can enable the county benefit from income generated in such sites.

NOTING THAT this can be realized by first mapping out a process which involves identification of historical and tourist sites within the county.

CONCERNED THAT the County government has not mapped out these sites, I urge this Assembly to resolve that:

1. The tourism department carries out a mapping exercise to enable them benefit from allocations made to museums.

2. The Department of Tourism after the mapping out the tourist attraction sites to vibrantly market those sites so as to add local revenue to our basket.

Thank you Mr. Speaker Sir, I beg to table the Notice of Motion.

(Hon. (Ms.) Akinyi ends reading the Notice of Motion and tables)

Hon. Speaker: Thank you, the House Business Committee will allocate proper time for it to be tabled.

DISCLAIMER: The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor Page 2 January 27, 2016 COUNTY ASSEMBLY DEBATES 6

MOTION

Mheshimiwa Fadhili Makarani?

Hon. Mwalimu: Ahsante Bwana Spika. Bwana Spika, mimi nasimama kuleta hoja ambayo ukikumbuka tarehe 23 mwezi wa Juni mwaka wa 2015 katika kikao cha 73 Mheshimiwa Spika Bunge hili lilikubaliana kwa pamoja kuwa wale wazee wote ambao wamefika miaka 60 na kuendelea waweze kuacha kazi zao Mheshimiwa Spika.

Mheshimiwa Spika twaelewa kuwa ndani ya Kaunti yetu kuna vijana ambao wanazo stakabadhi na wanao ujuzi wa kufanya kazi kama zile Mheshimiwa Spika, lakini la kusikitisha Mheshimiwa Spika ni kuwa vijana wetu ama vijana wengi wanashindwa ama inakuwa ni kigezo kigumu kwao kuweza kupata ajira kutokamana na uzembe kama huu wa wazee ambao wamefika miaka yao na hawataki kuwacha kazi na wako watu ndani ya Kaunti yetu hii ambao twawajua kwa majina, na ambao wamefika miaka na hawataki kuacha.

Mheshimiwa Spika mimi naomba Nyumba hii iweze kukubaliana kwa pamoja ya kuwa kitengo cha County Public Service Board (CPSB) ikishirikiana na County Assembly Service Board (CASB) walete ndani ya Nyumba hii wapewe muda kutokana na jambo hili linazidi kunyima vijana wetu ajira; pia linazidi kukiuka mkataba ambao Bunge hili lilipitisha.

Kwa haraka iwezekanavyo Mheshimiwa Spika kama tulivyokuwa tumepitisha kwa kikao chetu cha 73, majina yale yaweze kuletwa mbele ya Bunge letu Mheshimiwa Spika na hatua iweze kuchukuliwa haraka iwezekanavyo.

Mheshimiwa Spika nakuomba na nawaomba waheshimiwa wenzangu tukubaliane kwa pamoja kuwa tuliwahi pitisha hoja hii, tunaomba tu kupitia kiti chako, narudia Mheshimiwa Spika hoja hii tulipitisha kupitia kikao chetu cha 73, hoja hii ambayo nimeleta mimi ni utekelezwaji wa kile kikao cha 73.

Mheshimiwa Spika mimi naomba kupitia kiti chako utupe mwelekeo mwafaka wa njia ambayo itaweza ili kazi yetu ya Bunge letu isiweze kughadhabika na tuonekane Mheshimiwa Spika yale ambayo tunapitisha yanafanyiwa kazi. Ahsante Mheshimiwa Spika.

DISCLAIMER: The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor Page 3 January 27, 2016 COUNTY ASSEMBLY DEBATES 6

Hon. Speaker: Ahsante Mheshimiwa Fadhili Mwalimu, Mheshimiwa Hamisi Mwidani?

Hon. Mwidani: Ahsante Bwana Spika mimi nimesimama kuunga mkono…

Hon. Speaker: It has to be seconded first?

Hon. Mwidani: I arise here to second the motion.

(Question proposed)

Hon. Speaker: Members I put the question whether this motion should be debated in this House?

(Question put and agreed to)

Yes Mheshimiwa Fadhili.

Hon. Mwalimu: Mheshimiwa Spika mimi nafikiri nimekuwa mfasaha na wenzangu wamenielewa Mheshimiwa Spika lengo na madhumuni ya hoja yetu hii Mheshimiwa Spika ni utekelezaji wa yale maneno ambayo tuliyapitisha ndani ya Bunge letu.

Sote kwa pamoja katika kikao chetu cha 73 Mheshimiwa Spika na nimesema ni tarehe 23 mwezi wa Juni mwaka wa 2015. Nawaomba wenzangu tushirikiane pamoja tukubaliane maana haya ni mambo ambayo tulikuwa tushayapitisha, ninachokiomba sasa ni utekelezwaji, tunaomba kupitia kiti chako na naomba wenzangu pia tushikane pamoja tuhakikishe utekelezwaji wa mambo haya ambayo tulikuwa tumeyapitisha yanafanyika kwa maana tangu tulipoyapitisha bado kuna wale wanazidi kuzembea kwenye viti vile wanajifichaficha ndani ya watu Bwana Spika, hatujui ni vipi wanafanya kama mpaka wa leo wanaendelea kukaa na hali tulipitisha waweze kuacha nafasi zile vijana wetu waweze kuajiriwa. Ahsante, Bwana Spika.

Hon. Speaker: Yes Mheshimiwa Karisa Nzai Munyika?

Hon. Nzai: Ahsante Bwana Spika, nami pia nasimama kuunga mkono hoja ambayo imeletwa na Mheshimiwa Fadhili.

DISCLAIMER: The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor Page 4 January 27, 2016 COUNTY ASSEMBLY DEBATES 6

Mheshimiwa Spika ni jambo la kuonekana kuwa mtu ana heshima sababu wakati Mungu na wakati wa kustaafu umefika ni vyema kujitayarisha na kuweza kujikimu na kuanza kujipanga kwa ile miaka ambayo Mungu ameweza kukupatia na kama sisi wengine tunafahamu kwamba Mungu akikupa miaka kama miaka 70 na kama umekuwa mwema akupe zaidi lakini ile ambayo umeitumia kwa kazi haina haja ya kukaa hadi ulazimishwe kwenda ijapo ninavyofahamu ni kwamba kuna zile kesi ambazo ni spesheli; ni muhimu kwamba mtu ile kazi ambayo ameishikilia iweze kuwa ama tutoe ratiba ya kwamba kama mtu fulani katika kitengo fulani anachofanya imefika wakati wake, anaye msaidizi wake ampatie vilivyo ndiposa huduma zile zisije zikasimama maana kuna vitengo vingine mtu kama yule akiwa ameenda kazi hiyo itaathirika ama ikasimama kwa muda kabla kupatikane mtu mwingine.

Kwa hivyo tunasema kwamba katika sehemu zile spesheli peke yake kwanza kuna kitu inaitwa kandarasi yaani ‘contract’, kama kuna kandarasi ya mwaka mmoja ama miwili na ijapo mtu amepitisha na hiyo kazi aliyo nayo peke yake na haijapata mtu aliye na ujuzi wa kuendesha hiyo kazi Mheshimiwa Spika hiyo hali pia ifikiriwe. Ahsante sana Mheshimiwa Spika.

Hon. Speaker: Mheshimiwa Amur Murfad.

Hon. Murfad: Ahsante Mheshimiwa Spika hata mimi naunga mkono kwani huenda ikiwa una miaka 60 lakini shida iliyopo ni tunawatayarishia vipi hawa tunataka kuwapeleka kwenda zao wasiwe wanasimama kwenye barabara zetu ama baraza zetu wakitaka haki zao, je tumejipanga kivipi? Swali ni kwamba tumeshawasimamisha na inakuwa ni mateso, tumewaambia waende zao lakini yale marupurupu yao inakuwa ni mateso kupata haki zao lazima kuwe na mfumo maalum ya kuwa mtu anakwenda hakuna ambaye hataki kwenda, lakini kinachofanya mtu awe na ugumu mahali pa kwenda ni kwamba akishapewa barua ya kwenda yale marupurupu yake na haki zake itakuwa vigumu kupata.

Hii ndio shida ya kwamba watu hawataki kwenda Mheshimiwa Spika kwa sababu hakuna mfumo maalum Mheshimiwa Spika…

(Interruption)

DISCLAIMER: The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor Page 5 January 27, 2016 COUNTY ASSEMBLY DEBATES 6

Hon. Speaker: Yes Mheshimiwa Mary Akinyi?

Hon. (Ms.) Akinyi: Ahsante Mheshimiwa Spika. Mheshimiwa Spika ningependa kuuliza Bunge hili kama Mheshimiwa ambaye amesimama anaunga mkono ama anapinga?

Hon. Speaker: Yes Mheshimiwa elezea Nyumba hii kama unaunga?

Hon. Amur: Nafikiri Mheshimiwa hakusikia nikisema kuwa naunga kikamilifu, lakini nimesema mipango kabambe iwekwe katika ratiba tunataka kuwastaafisha hawa watu, je tumejipanga na pesa zao? Haki zao? Isiwe tunafuta watu kazi alafu wanabaki kwa ma ‘corridor’ wanakuja kutafuta haki zao. Hiyo ndio kitu ambayo inafanya…

(Interruption)

Hon. Speaker: Mheshimiwa Amur si kuhusu kustaafu ni umri wao, umri wa kustaafu.

Hon. Amur: Sawa Mheshimiwa Spika wamestaafu, lakini kustaafu huku inataka iwe na mpangilio kwamba wakati wamepewa barua za kustaafu na ombi zao pia ziwe ziko tayari ziambatane na ile barua ili mtu akitoka hapa atoke na roho safi.

Mheshimiwa Spika la pili wakati watu hawa wameenda kustaafu ni Bunge hili hili ama Kaunti hii iliyoajiri vijana kazi katika vitengo vya kuegesha magari, vitengo vya usalama barabarani yaani ‘traffic’, je vijana hawa washakuwa ‘confirmed’ kazini? Kwa sababu sisi tunatangaza kazi magazetini ilhali kuna vijana ambao tayari sisi tuliwaandika kazi Mheshimiwa Spika. Ahsante.

Hon. Speaker: Mheshimiwa Saad Faraj?

Hon. Faraj: Ahsante sana Mheshimiwa Spika kwa fursa hii. Mheshimiwa Spika nafikiri swala lilioko hapa ni kuzungumzia wale ambao kwamba wamefikisha umri wa kustaafu na mimi ningeomba Nyumba hii ikiwa kuna hoja ya aina nyengine yeyote ambayo yaweza kuwa yaambatana na swala kama hili, basi liletwe kama mswada au kama hoja iweze kuja kuzungumziwa; ama kwa hakika Mheshimiwa Spika hatuwezi kuacha watu ambao kwamba wamepita umri na bado wako kwa viti kwa sababu pale wale wataalamu walipopanga mwaka wa

DISCLAIMER: The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor Page 6 January 27, 2016 COUNTY ASSEMBLY DEBATES 6 kustaafu walikuwa wakifahamu kuwa kuna umri ambao ugemwezesha mwanadamu kutekeleza majukumu yake kama ilivyo.

Mheshimiwa Spika hata kule nyumbani kuna umri flani ukifika huwa ngoma huwezi tena kuicheza kwa hivyo kwa mfumo ule ule kwa sababu ni maumbile ya Mwenyezi Mungu na wala si maombi yetu sisi na ni makadirio yetu…

(Interruption)

Hon. Speaker: Yes Mheshimiwa Paul Onje what is it?

Hon. Onje: Ahsante sana Mheshimiwa Spika. Mheshimiwa Spika mimi nimesimama hapa nikiuliza Mheshimiwa mwenzangu ambaye alikuwa anaongea ni ngoma gani ambayo inashinda wanadamu wanapotimia miaka ya 60? Nataka nijue hiyo ni ngoma gani Mheshimiwa Spika, nataka nijue kama ni rumba tunaomba aeleze Jumba hili ni ngoma gani hizo.

Hon. Speaker: Yes Mheshimiwa Saad Faraj eleza Bunge hili ni ngoma gani?

Hon. Faraj: Mheshimiwa Spika nafikiri sote ni watu wazima; ile ngoma twaizungumzia sisi angechukua fursa baadaye atufafanulie lakini naamini mtu mzima yeyote ambaye yuko katika Nyumba hii anaweza kufahamu ngoma tunayozungumza ni ngoma gani.

Mheshimiwa Spika wakati hauko na sisi na sisi hatujipangii maisha na kila uchao sisi tunakaa tukihakikisha kuwa tukipigana kuwa watoto wetu, vijana wetu walioko nje waweze kupata fursa ya kuwakilisha na kufanya kazi katika sehemu tofauti tofauti, kila tukiangalia tunaona wazee wameshikilia zile nafasi na kila uchao tuna vijana ambao ni wasomi na wanatoka katika mji huu…

(Interruption)

Hon. Speaker: Mheshimiwa Mary?

DISCLAIMER: The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor Page 7 January 27, 2016 COUNTY ASSEMBLY DEBATES 6

Hon. (Ms.) Akinyi: Ahsante Mheshimiwa Spika. Mheshimiwa Spika nashangaa, Mheshimiwa ambaye amesimama anachangia si aeleze yale ambayo alikuwa anataka kueleza alafu yule ambaye alikuwa yuko katika hoja hiyo aendelee…

(Laughter)

… kwa sababu ni kama aliyekuwa anachangia hebu tueleze kama wewe ulikuwa umesimamia alafu urudi ukae chini alafu yule ambaye alikuwa anaendelea kuchangia aendelee kuchangia.

Hon. Speaker: Ok members am just reminding you the content of the prayer; members this motion was passed on 23rd of June, what we are talking out now is its implementation but the motion was passed so to save time we should not go back to the contents of the motion.

Please let’s not go back and debate the content of the motion that was passed let’s discuss the prayers of the game please, yes Hon. Saad?

Hon. Faraj: Mheshimiwa Spika nafikiri kuna utata; Mheshimiwa Mary aliona kuwa nimesimama ‘on a point of order’ lakini Mheshimiwa Amur alikuwa tayari amemaliza mimi anaendelea kuchangia mchango wangu hapo ndio kidogo nafikiri Mheshimiwa Mary alikuwa kidogo ametatizika.

Mheshimiwa Spika ni wajibu wetu tuhakikishe kuwa hili Jumba limefanya haki kwa wale vijana na wale wazee; na wale wazee hivi sasa kulingana na sheria na katiba iliyoko wapumzike waende wapumzike ili waweze kutoa fursa kwa wale vijana chipukizi walioinukia wenye ari mpya nguvu mpya kuja kuchangia katika uendeshaji wa hii Kaunti yetu ya Mombasa.

Hon. Speaker: Mheshimiwa Mary.

Hon. (Ms.) Akinyi: Ahsante Mheshimiwa Spika. Mheshimiwa Spika mimi pia nataka jambo hili likome na nataka wale wazee wote ambao wamefikia umri wa kustaafu wafuate mfano wa Karani mkuu wetu Tubmun Otieno ambaye alifika akaenda taratibu vizuri sasa zile senti zake kama vile Mheshimiwa Amur alivyosema…

(Members consulting loudly)

DISCLAIMER: The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor Page 8 January 27, 2016 COUNTY ASSEMBLY DEBATES 6

Hon. Speaker: Hon. Members order! Order! Hon. Members! Members you are reminded, am reminding you the prayer, let’s minimize the debate we don’t have time, time is running Mheshimiwa Mary?

Hon. (Ms.) Akinyi: ….Kwa hivyo wale ambao wametimia na hawataki kwenda kwa sababu wewe huwezi jua umri wa mtu waweza ona watu wengine wana miili tofauti tofauti, waweza kumuona ni mzee lakini ukija kuangalia kitambulisho chake bado ni kijana lakini wewe unaona pengine kama mfano Mheshimiwa Amur unaona pengine ni mzee lakini ukija kuangalia kitambulisho chake ukapata pengine ni kijana lakini wewe umekazana kuwa Mheshimiwa Amur amefika umri wa kustaafu aende zake.

Hon. Murfad: Mheshimiwa nasikitika kuona Mheshimiwa anasema mimi ni kijana, mimi si kijana mimi nishakomaa nishapita nusu karne kwa hivyo mimi sio kijana kijana ni wa miaka 18-35, kwa hivyo mimi nakalia bakshishi tu saa hii, kwa hivyo mimi sio kijana nataka ifahamike kwamba mimi si kijana nakalia ‘deposit’….

Hon. (Ms.) Akinyi: Kwa hivyo mimi Mheshimiwa Spika nilikuwa nataka na naomba tu Nyumba hii kama kuna mtu ambaye anajua na amefahamu kweli na ako na thibitisho kuwa kuna mtu ambaye amefika miaka 60 ambaye anatakikana astaafu hata kama hajastaafu amtaje astaafu alafu wale vijana pia waingizwe kazi.

Hon. Speaker: Mheshimiwa Hamisi Mwidani?

Hon. Mwidani: Ahsante Bwana Spika ni vizuri kuja hapa nafasi tuweze kuzungumzia jambo hili ambalo liko wazi kwa sababu ni changamoto hata sisi tutapelekwa kustaafu si ni 2017 sasa wengine wataenda staafu sasa hatuna budi, kwa hivyo aliyefika miaka 60 ni haki apatiwe nafasi Mheshimiwa kama hapa pia wengine tutakwenda kustaafu apatiwe hiyo nafasi.

Kwa hivyo hili ni jambo ambalo liko wazi si kwamba mtu anafutwa kabla wakati wa kustaafu. Mimi Bwana Spika ningeomba kwa heshima na wakati na kuwa wanawasiliana kwamba kuna boss wa chama ambaye tunataka kwenda kumsindikiza kwa hivyo tunaomba mtupitishie mswada ambao tunaweza kwenda kumpa ‘big boss’ wetu.

DISCLAIMER: The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor Page 9 January 27, 2016 COUNTY ASSEMBLY DEBATES 6

Kwa hivyo tunaomba Bwana Spika habari utakayoifanya tuweze kumaliza huu mswada na tuweze kuupitisha kuwa wale wazee wamefikisha miaka 60 wapewe waende mtaa na nina uhakika kustaafu kwao hakutaleta shida kwa sababu pesa sasa twaletewa wenyewe kwa Bunge, kwa hivyo hata pesa zao watalipwa kwa hivyo ni vizuri wapeane nafasi kuna vijana wengi ambao wanatafuta hiyo nafasi. Ahsante sana.

Hon. Speaker: Honorable Kizito Opeya two minutes please we are running out of time so please two minutes and then….

Hon. Opeya: Thank you Mr. Speaker, mine is just to say that this motion was passed on June 23rd 2015 now its 2016 obviously it shows we pass motions here now it’s time we make sure that we ensure that the these motions are implemented so that we don’t start repeating motions which were passed like several months ago.

It’s actually shameful that eight months ago they have not been implemented; they need to be followed up to make sure that when we pass something here it is implemented. Thank you, Mr. Speaker.

Hon. Speaker: Mheshimiwa Paul Onje two minutes and then Nassir two minutes and then Mheshimiwa Boma two minutes and then we wind up.

Hon. Onje: Ahsante Mheshimiwa Spika, mimi ningependa kuomba Bunge letu kupitia kiti chako kamati ya Leba waweze…..

Hon. Speaker: Unaunga mkono?

Hon. Onje: Yes naunga mkono…kamati ya Leba iweze kuwa na kikao kuitisha stakabadhi kutoka upande wa ‘executive in charge of labor’ ili wajue mwaka huu ni wangapi wamestaafu wapange ratiba wajue kabisa jinsi tunavyoambiwa hawa ambao wanaenda kustaafu lazima watayarishiwe kama ni kitita chao yaani ikifika tu pesa yao iwe iko kwenye akiba zao za benki waende sio mambo ya kuanza kutembea kwenye ‘corridors’ ukiuliza mimi najua huyu anastahili kustaafu manake kuna watu ambao wanafaa kufanya hiyo kazi. Ahsante sana.

DISCLAIMER: The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor Page 10 January 27, 2016 COUNTY ASSEMBLY DEBATES 6

Hon. Speaker: Yes Mheshimiwa Mwadziwe?

Hon. Mwadziwe: Ahsante sana Mheshimiwa Spika. Mheshimiwa Spika mimi ninaunga mkono mswada huu lakini nataka kuchangia nikisema kuwa ni kustaafisha hawa watu ama hawa watu kutoka.

Mheshimiwa Spika lazima kuwe na utaratibu; nasema hivyo kwa sababu Mheshimiwa Spika kuna wafanyi kazi wengine ambao wako ‘very sensitive areas’, kwa hiyo itabidi hao wazee wetu ambao wamefikisha umri wabakie ili kuweza kuwafundisha kazi hao vijana ili wanapotoka basi ule ujuzi wako nao tusije tukaikosa. Kwa mfano Mheshimiwa Spika naweza kukupa mfano kule hospitali kwetu mahali kama…

(Interruption)

Hon. Speaker: Mheshimiwa Paul Onje what is it?

Hon. Onje: Ahsante sana Mheshimiwa Spika. Mheshimiwa Spika nafikiri wakati ambapo tunachukua wafanyi kazi wanapitia njia ya ‘vetting’ na tunachukuwa wale waliohitimu na hatuchukui watu hapa, yule ambaye tunachukua tunajua ni mtu anafaa na anajua hiyo kazi kwa hivyo Bwana Spika mzee akifika wakati mzee aende nyumbani.

Mheshimiwa Mwinga: Mheshimiwa Spika nakubaliana sana na Mheshimiwa ndugu yangu Onje lakini kuna tofauti ya ujuzi wa huyo na ujuzi wake hata apate huwezi chukua mtu ametoka chuoni ukamuweka mahali kama hospitali kuu ya Coast general ukampa mgonjwa afanye upasuaji.

Kwa hiyo hii inahitaji Mheshimiwa Spika mtu afundishwe awe na ujuzi wa utenda kazi ile ili anapoachiwa mgonjwa aweze kumtibu kama inavyohitajika ama tutapata vijana ambao watakuwa wanaumiza watu wetu Mheshimiwa Spika. Ahsante.

Hon. Speaker: Yes Mheshimiwa Boma.

DISCLAIMER: The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor Page 11 January 27, 2016 COUNTY ASSEMBLY DEBATES 6

Hon. Boma: Ahsante sana Mheshimiwa Spika kwa kunipa nafasi ya kuweza kuchangia kuhusu swala hili. Mheshimiwa Spika nafikiri mswada huu ulipitishwa kitambo kitu kilichobaki ni utekelezaji kwa hivyo tuhakikishe kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Utekelezaji yaani ‘Implementation’…

(Laughter and applause)

….na kulingana na mfumo wa serikali mtu akifikisha miaka 60 tayari yuko tayari mshahara wao wakatika moja kwa moja, kwa hivyo mimi sioni haja ya kubishana hapa kwa sababu ukifikisha miaka 60 tayari pesa yako yakatika. Ahsante Bwana Spika.

Hon. Speaker: Mheshimiwa Patrick two minutes.

Hon. Siminyu: Mr. Speaker I don’t know if these things are done in the right way because I represent people who are working in the county and live in the estate. Mr. Speaker since I was elected I have seen many go home and the houses are still full and if there is evidence that there are people who are still working and they are in fact over-age, Mr. Speaker this matter has to be investigated thoroughly and we know who they are, because I have strong evidence that people are going home and need support for them to go home when its time…

What I’m trying to say is that people are going home and out of this motion we have evidence that there are people who have obtained the retirement age and they are still working; Mr. Speaker sir we need to have proper implementation so that we can see these people go home. Thank you Mr. Speaker sir.

(Question proposed)

Hon. Speaker: Thank you so much Mheshimiwa Patrick Siminyu this motion has been debated wisely and it was so I have no option but to put the question, members as many as of the opinion that this motion be passed and that the County Secretary and the Assembly Clerk to furbish this House with the names of elderly workers who have surpassed the age of 60 years.

(Question put and agreed to) DISCLAIMER: The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor Page 12 January 27, 2016 COUNTY ASSEMBLY DEBATES 6

This Assembly has passed that the County Secretary and the Assembly Clerk furnish this House with the names of those workers who are above 60 years before this House on Friday. Thank you very much.

ADJOURNMENT

Members this House stands adjourned until today in the afternoon.

The House rose at 9:43am.

DISCLAIMER: The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor Page 13