IGIZO

By Ombeni Pallangyo

Sunga Secondary School Play for the Celebration of World Malaria Day

Presented at Mambo Primary School April 25, 2013

In collaboration with Jane Teas, Peace Volunteer

Wahusika:

Mwandishi wa habari

Mzee Mbia

Mama Abeseto

Mzee Mitomingi

Daktari

Mama Inda

Kaboi

Mabala

Chausika

Angel

Mandhari:

Kijiji katika nchi ya Tanzania, Afrika Mashariki “Siama”

NB Sio Majina Sahihi, majina yametolewa kwenye vitabu vya fasihi

Mbele ya jukwaa mtungazaji anasimama mbele na kutambulisha kuwa leo ni siku ya maadhimisho. Malaria duniani Takriban ulimwengu mzima inaathimisha siku hii. Anasema takribun watu 675,000 hufa kwa ugonjwa huu wengi wao ni watoto wa chini ya umri wa miake 5 na wagonjwa wa ukimwi. Mbele yenu kuna familia mbili ambazo kati ya familia hizo moja inatumia chandarua wakati familia ya pili yam zee mitomingi hawatumii.

Mzee Mbia (Ni asubuhi anamka) Aaaah! Khaua Mama Abeselo hebu amkeni kumekucha, amkeni amkeri.

Mama Abeselo: Mh! Shakamoo! Mzee Mbia: Marahabaa! Umeamkaje?

Mama Abeselo: Salama.

Mzee Mbia: Ah! Leo hawa mbu wamenisumbua.

Mama Abeselo: Sijui tufanyeje maana hata mimi sijalala kabisaa!

Mzee Mbia: Sasa mimi nitawakomesha nitachukua safuleti nitalifunga kwenye madirisha ili wasiingie.

Mama Abeselo: Labda itasaidia.

Mzee Mbia: (Anaaga). Sasa mimi ngoja niende kwanza kijiweni kubadilishana mawazo na wazee wanzangu au siyo?

(Anaondoka huku akionekana ni mwenye mzigo wa mawazo. Anakutana na mzee mtomingi).

Mzee Mitomingi: Ooh! Mzee mbia, upo?

Muzee Mbia: Nipo mzee, Mambo yanaendaje.

Mzee Mitoming: Mh! Hivyo hivyo tu. Yaani basi tu. Vipi jana umetizama ile game mpaka mwisho?

Mzee Mbia: Ndio, lakini mambo yamekuwa zigzag kabisaa!

Mzee Mitimingi: Kwanini mzee?

Mzee Mbia: Hah! Kwa sababu mambo yalienda mvangemvanga.

Mzee Mitomingi: Kha! Kha! Khauu! (akiangua kicheko mzee mbia anamwingilia).

Mzee Mbia: Lakini naonei kuna tangazo hapo hebu tulione (wanalitizama wote wawili).

Mzee Mitomingi: Ah! Ni tangazo la hii serikali ya michongo.

Mzee Mbia: (Anaonekana aliesisimka) Ah! Hapana, hebu! Hebu! Mwezi huu kutatolewa vyanfarua pale zahanuti bure. Hii ni nzuri serikali inatupenda.

Mzee Mitomingi: Ha! Vyandarua vyenyewe ni vitu gani kama sio choko choko tu.

Mzee Mbia: Hiki kimechorwa kwenye hii picha bwana na watu wamelala ndani kwa ajili ya kujizuia didi ya mbu wanaoeneza malaria.

Mzee Mitomingi: Mbona ni kama chambo cha kuvulia samaki.

Mzee Mbia: Hapana sio hivyo lakini naona ni vyema tukaenda huko zahanati tukamuone daktari.

Mzee Mitomingi: Haya basi baadae. Mzee Mbia: Haya mzee nisalimie shemeji (wanaachana kila mmoja anashika njia yake. Huku mzee mbia akionekana mwenye furaha. Anafika nyumbani ).

Mzee Mbia: (kwa shangwe kubwa) Hodi! Hodi!

Mama Abeselo: Ha! Mume wangu mbona furaha hivyo kuna nini tena?

Mzee Mbia: (Anaelezea).

Saso mbona unaharaka kama makamasi! Mke wangu,

Mama Abeselo: Lazima niwe na haraka. Kwani ngoja ngoja yaumiza matumbo. Au vipi mume wangu.

Mzee Mbia: Sawa, sawa ni hivi Nimeenda kule kitaani kwetu, yaani kule kijiweni. Nimeona tangazo linalo waomba wananchi wote wafike pale zahanati kuchukua vyandarua bule.

Mama Abeselo: Kwa hiyo umekuja twende.

Mzee Mbia: Ndio, nimeona ni vyema twende wote maana usipo ziba ufa utajenga ukuta.

Mama Abeselo: Na wazee wasema liwezekanalo leo lisingoje kesho. Si ndiyo?

(Wanawaaga watoto wao na kuelekea zahanati, Wanaingia)

Wote wawili: Hodi! Hodi!

Daktari: Karibu, pita, ingia ndani.

Wote wawili: Za saa hizi daktari.

Daktari: Salama, poleni, ni wasaidie nini?

Mzee Mbia: Ahsante, daktari, nimeona tangazo kuhusu ugawaji wa vyandarua.

Daktari: Ndio vyandarua vipo vinatolewa hapa bure.

Mama Abeselo: Tunaweza kuchukua sasa hivi daktari?

Daktari: Ndio, (anatoa na kuwapa). Matumizi ni hivi, kifunge kila jioni saa kumi na mbili na kifungue asubuhi unapo amka.

Wote wawili: Ahsante daktari.

Daktari: Karibuni tena

(Mzee mitomingi anaaga familia yake kwamba anaenda zahanati iti kuelezwa juu ya huo ugari wa vyandarua).

Mzee Mitoming: Haya mimi ninaenda. Fanyeni shughuli zote sawa ee? Wote ndani: Haya mzee.

(akiwa njiani mwenyewe)

Mzee Mitomingi: Yaani hii serikali, nimeache shughuli zangu eti nifuata vyandurua si kusumbuana huku.

(anafika zahanati?).

Hodi ndani

Daktari: Karibu, ingia ndani mzee.

Mzee Mitomingi: Ahsante, daktari.

Daktari: Pole! Haya, niambie tatizo.

Mzee Mitomingi: Mimeona tangazo kwamba kunatolewa vyandarua hapa zahanati leo.

Daktari: Ndio, tunatoa vyandarua bure

Mzee Mitoming: Daktari, chandarua ninini?

Daktari: Ni aina ya kitambaa ambacho kinamatundu madogo. Nguo hii hutumika kujifunika usiku ili mbu ambao wanaeneza malaria wasikung’ute na kukuambukiza malaria.

Mzee Mitoming: Yaani daktari mbu anaeneza malaria?

Daktari: Ndio, mbu jike anaeitwa anofelesi huanza kuwauma watu kuanzia saa 8 usiku wa manane. Mbu hao, hutoa viini vya malaria kutoka kwa mtu mmoja ambaye ameathirika kwenda kwa mtu ambaye hajaathirika

Mzee Mitomingi: kwa iyo ukijifunika ndio hawakuumi

Daktari: Ndio, malaria inazuilika pindi tu tukishirikiana na kuchukua hatua madam sisi sote tukibuni za kuwatokemeza mbu, kufyaka vichaka vinauyozunguka nyumba zetu, kufukia vidimbwi na mifereji maji ya machaful pamoja na kutumia vyandarua ambavyo tunawapeni leo hii.

Mzee Mitomingi: Nigaie vingi maana nina watoto lukaki.

Daktari: Sawa, hamna shida, shika hivi hapa.

Mzee Mitomingi: Ahsante sana daktari.

Daktari: Karibu sana, halafu unaingia ndani no hakikisha hamna hatu sehemu moja ambayo ipo wazi.

Mzee Mitomingi: Sawa daktari, kwa heri.

(Anaondoka akiwa ni mwenye mshangao). Ha! Yaani mbu amuuwe mtu.

(Anafika nyumbani)

Hodi.

Mama Inda: Karibu mume wangu.

Mzee Mitomingi: Nimeshaakaribia, natokea kule zahanati nimepewa hivyo vyandarua hiviv hapa.

Mamainda: Mbona ni kama chekecheke.

Mzee Mitomingi: Ndio mke wangu. Halafu zinanonekana kuwa zinafaa kuvulia samaki.

Kaboi: Ndio baba hizi zinavua hata wale samaki wadogo wadogo.

Mabala: Zinafaa pia kutengeneza kibanda cha kuku.

Chausiku: Pia naona baba, zinafaa kutengeneza na kushonea mapazia.

Angel: Ed! Mimi nitashona gauni kilemba pia.

Mzee Mitoming: Redio wangangu, viyote hivyo vinafaa na kwa sababu ni vingi kila mmoja atapata mahitaji yake yaani, mapazia, vitambaa, magauni, vyambo kwa ajili ya kuvulia na hata kwenye mabanda ya kuku.

Kaboi: Baba, baba!

Mzee Mitomingi: Ndio mwanangu.

Kaboi: Tena itafaa twende leoleo usiku.

Mzee Mitomingi: Ndio le oleo, ya kesho ni mengine.

(huku wengine wachana wao waneondelea kwenda kuvua usiku huo)

(kwa upande wa mzee mbia wanalala)

Mzee Mbia: Sasa jamani ni usiku tufunge chandaru kama tulivyo elekezwa na daktari.

Mama Abeselo: Ndio mume wangu lakini mbona bado mapema

Mzee Mbia: Ha! Hapana daktari alisema saa 12 jioni.

Wote wawili: Sawa, haya tushushe huku

Mzee Mbia: Haya, watoto nao tuhakikishe wamelala ndani.

Mamba Abeselo: Haya, watoto wazuri ingieni ndani mlale Watoto: Sawa mama.

Mama Abeselo: Usiku mnono.

(mzee Mitomingi na watoto wake wauua samaki)

Mzee Mitomingi: Leo wanaonelea wengi kweli.

Kabo: Huyo mkubwa kwdi

Mabala: Baba mwakuu tutanenepa

Mzee Mitomingi: Na kutajiriba pia maana hali mbayo sana.

(wanamaliza kuvua wanarudi nyumbani jiani wanakutana na mzee mbia)

Mzee Ambia: Mtumeee! Mzee vipi mbona umeshika vyandaru mkono na umevichafua hivyo.

Mzee Mitomingi: tunatokei Kuvudia.

Mzee Mbia: Mzee acha ujinga na ukale wako mbona hivi tumepewa iti kujikinga dhidi ya malaria.

Kaboi: Mzee tumekata kimoja tukaninginiza kwenye mlango na kwenye dirisha ili mbu wasiingie.

Mzee Mbia: Hapana hiyo siyo jinsi inavyo tulaiwa.

Mzee Mitomingi: Basi mzee mimi hiyo ndiyo daktari aliyonielekeza.

Wote: Ah mzee tuache huo ni wiuu usiko tu?

Mzee Mbia: Ah sorikari. Huu ni ujinga.

Kaboi: Baba, Yule mzee anawiuu sana Yule

Mabala: Halafu ni mchani sana Yule.

Mzee Mitomingi: Halafu anajifanyu anajua sana yale.

(Mi usiku wa piti ziku inayofuata) motto mmoja anaumwa na mwingine pia hali yake si nzuri nyumbani kwa Mzee Mitomingi)

Kaboi: Dada! Dada vipi mbona unatepika.

Mabala: Khaa! Khaa! (nae anatepika).

Angel: (Akiwa anatetemeba na kutapika) kamuite mama.

Mzee Mitomingi: Haya nini nwanangu.

Maminda: Ha! Jamani nani kawaruga watoto wangu. Mzee MitomingI: Tablal labda ni jirani wet

Mamainda: Tuwapeleke kwa Sangatiti mganga mashuhuri)

Mzee Mitomingi: Haya tuwashikeni.

(Vlanaenda kwa mganga wa kwenyeji)

Mganga: Puuu! Puuu! Nasikia halafu ya mzaga wangu. Wizuuu! Wizuuu!

Mamainda: tusaidie mfalme wetu, wato wangu wame no ywa.

Mke wa mganga: Nkweii! Nkweii do haya waetei.

Mganga: Puuu! Puuu ni kale te kuku mrefu kidoli ambaye akipita mtaani anakonyeza konyeza, demu wako wa zamani, mkojo wa jogoo mzee, macho zi ya samaki, na mate ya mzimu mrembo.

Mzee Mitomingi: Ha! Mganya sitaweza?

Mganga: Basi kalete bwanza kuku mwenpe na mweusi.

Mke wamganga: Na chupa ya asali

Mganga: Hanakaaa! Puuu! Puuu! Wanauwawa ukichelewa.

(Wanapeleleka kuku lakini watoto hawaponi)

Mzee Mitomingi: Kuku tumeleke lakini watoto ba do holi si nzuri mke wanga vipi

Mamainda: Tume haribu masharti

Mzee Mitomingi: Ngoja niende hape kijiweni kwanza kupata ushuvi sawa?

(Anaenda kwa mzee mbia)

Mzee Mitomingi: Haya. Mzee upo?

Mzee Mbia: Ndio, mbona mbio asubuhi hii.

Mzee Mitomingi: Watoto wangu wanaumwa.

Mzee Mbia: Malaria, kipindupindu au nini.

Mzee Mitomingi: Twende ukawaune.

Mzee Mbia: Hayu twende lakini ngoja, mke wanga ngoja niende kwa mzee mitomingi kuna tetizo.

(Wanafiba)

Mzee Mbia: Kichwa kinauma. Angel: Ndio.

Kaboi: Halafu ana inapepo ana onge mwenyewe.

Mzee Mbia: Huu ni ugonjwa wa malaria tuwashibe tuwapelike hospitali

(Wanafiba hospital)

Daktari: Tume wapima watoto wana sumbulia na malaria.

Mzee Mitomingi: Tusaidie daktari

Daktari: Umetumia chanderua.

Mzee Mitomingi: Ah! Ah! Hapana.

Daktari: Ndio Sababu.

Mwisho