Toleo Na.1 // Februari 2020

Yaliyomo // Maduhuli ya Madini sasa rasmi Chunya yazidi kupaa Tume ya kuuza Madini ya bati nje... Na.04 ... Na.08

Madini Masoko ya Madini Mnada wa Kwanza wa yaingiza TZS Bilioni 58.8 Almasi Tangu Kupatikana ... Na.06 kwa Uhuru wa www.tumemadini.go.tz Wafanyika ... Na.13

Tume ya Madini 2020 www.tumemadini.go.tz /TAHARIRI

Salamu Kutoka kwa Maoni ya Mhariri Waziri wa Madini Tumeweza, Tunasonga mbele! Tume ya Madini Tumeweza!

Ni takriban Miaka miwili sasa imetimia tangu kuanzishwa kwa Ili kuhakikisha kuwa Sekta ya Madini inakuwa na Wizara ya Madini katika kipindi hiki cha Serikali ya Awamu ya mchango mkubwa kwenye ukuaji wa uchumi wa nchi, Tano. Katika miaka hii tumeshuhudia mafanikio kadhaa yaliyoji- Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dk. tokeza katika Sekta ya Madini nchini, ikiwemo ongezeko la Mapato John Pombe Magufuli ilifanya Mabadiliko ya Sheria ya yatokanayo na rasilimali madini, ukuaji wa Sekta ya Madini, Madini ya Mwaka 2017 yaliyopelekea uundwaji wa Uanzishwaji wa Masoko ya Madini, Udhibiti wa Rasilimali Madini Tume ya Madini na kuondoa Wakala wa Ukaguzi wa na Sekta kuwa mfano kwa Mataifa mengine, yote hayo yakitokana Madini Tanzania (TMAA). na Mabadiliko na usimamizi maduhubuti uliofanywa na Serikali hii. Tangu kuanzishwa kwa Tume ya Madini wananchi wengi wameshuhudia mabadiliko makubwa kwenye Aidha, Wizara imeendelea kusimamia na kutekeleza mikakati Sekta ya Madini ikiwa ni pamoja na ongezeko la kasi yake katika kuhakikisha kwamba Sekta ya madini inakua na ya utoaji wa leseni za madini ambapo hadi kufikia inachangia zaidi katika uchumi wa taifa, kuhamasisha uwekezaji katika kipindi cha Mwezi Februari 2020 jumla ya na uanzishwaji wa migodi mipya, kuhamasisha shughuli za leseni 7463 za madini zilitolewa. uongezaji thamani madini, kuwaendeleza wachimbaji wadogo na Leseni zilizotolewa ni pamoja na leseni za utafiti wa kuweka mazingira rafiki ya biashara ya madini ili ifanyike kwa madini 204, leseni za uchimbaji mdogo wa madini uwazi huku pande zote serikali na wadau wakinufaika. 5075 na leseni za uchimbaji wa kati wa madini, 42.

Vilevile, katika kuwaendeleza wachimbaji wadogo na kuhakiki- Leseni nyingine ni pamoja na leseni kubwa za sha kuwa wanakua kutoka uchimbaji mdogo kwenda wa Kati na biashara ya madini 586, leseni ndogo za biashara ya Hatimaye wakubwa, na kwa kuzingatia umuhimu wa wachimbaji madini 1514, leseni za uchenjuaji wa madini 38, leseni wadogo, Wizara imejenga Vituo Saba vya Umahiri katika mikoa za uyeyushaji wa madini 2 na leseni za usafishaji wa mbalimbali nchini na Vituo Vitatu vya Mfano kwa lengo la kuwap- madini 2. atia mafunzo wachimbaji waweze kuchimba kwa tija. Katika kuhakikisha wachimbaji wa madini wanakuwa Wizara ya Madini imeendelea kutoa fursa ya kukaa pamoja na na soko la madini la uhakika, Tume ya Madini wadau, kwa kujadili na kusikiliza changamoto ambazo zote ilianzisha masoko ya madini pamoja na vituo vya zinalenga katika kuboresha sekta hii iweze kuwa bora na yenye ununuzi wa madini ambapo mpaka sasa jumla ya manufaa zaidi kwa taifa. Hayo yamefanyika kupitia Mkutano wa masoko 28 na vituo vya ununuzi wa madini 25 nchini Sekta ya madini uliofanyika Mwaka 2019 na hivi karibuni kupitia yameanzishwa. Kupitia uanzishwaji wa masoko ya Mkutano wa Kimataifa wa Uwekezaji katika Sekta ya Madini madini tangu mwezi Machi 2019 hadi Desemba, 2019 Tanzania 2020: ambapo manufaa ya mikutano hiyo yameleta Serikali ilifanikiwa kukusanya jumla ya kiasi cha matokeo chanya. shilingi bilioni 58.8.

Aidha, kupitia wa mwaka huu tumeshuhudia uzinduzi wa Cheti Katika kuhakikisha kunakuwepo na udhibiti wa cha Uhalisi kwa Madini ya Bati, ni wazi kwamba madini haya kutosha katika utoroshwaji wa madini nchini, Serikali yanakwenda kuwa kichocheo kingine cha uchumi na biashara iliamua kujenga ukuta wa Mirerani katika eneo lenye kwa nchi yetu na mataifa mengine. Ni dhahiri kuwa, hii ni hatua uchimbaji wa madini ya tanzanite lililopo katika nyingine muhimu ya kiuchumi kwa taifa letu. Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara. Ukuta wa Mirerani ulipelekea ongezeko la uzalishaji wa Tanzan- Kadhalika, katika kuhakikisha Watanzania wanamiliki na ite kutoka kilo164.6 mwaka 2016 hadi kilo 2,772.2 kwa kushiriki uchumi wa Madini na katika kuhakikisha rasilimali mwaka 2019. madini zinazidi kulinufaisha taifa, hivi sasa Serikali ni Mbia Tume ilifanikiwa kwa kiasi kikubwa kutatua migogoro katika Kampuni ya Twiga Corporation Limited ambapo serikali ya wachimbaji wadogo wa madini maeneo mbalimbali inamiliki hisa ya asilimia 16. Haya kwetu kama Mataifa ni nchini pamoja na kutoa elimu kuhusu uchimbaji wa Mapinduzi makubwa. madini unaozingatia Sheria ya Madini na kanuni zake.

Aidha, anayestahili pongezi hizi zote siyo sisi Wizara ya Madini Kama njia moja ya wapo ya kuhabarisha umma bali pongezi hizi ni za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa kupitia vyombo vya habari ikiwamo televisheni, Tanzania Dk. kwa kuwa na maono ambayo magazeti, tovuti na mitandao ya kijamii, tumeanzisha yameiwezesha Sekta ya Madini Kubadilika na kulinufaisha Taifa jarida hili la Madini News ambalo tunaamini litakuwa kwa kipindi hiki kifupi. Ombi langu kwa Watanzania na hususan njia mojawapo ya kuhabarisha umma juu ya wadau wa madini kuendelea kushirikiana na serikali katika mafanikio ya Tume ya Madini. juhudi hizi za kuhakikisha sekta hii inakuwa namba moja katika kuchangia maendeleo, kukuza uchumi na kubadilisha maisha ya Tunakaribisha maoni na ushauri kwa wasomaji wetu watanzania. ambapo jarida hili litakuwa linatoka mara moja kwa kila mwezi.

Sekta ya Madini, Tumethubutu Tumeweza! Madini Yetu, Uchumi Wetu Tuyalinde!

Mhe. Doto Mashaka Biteko Prof. Shukrani E. Manya Waziri wa Madini Katibu Mtendaji Wizara ya Madini Tume ya Madini

Tume ya Madini 2 Toleo la Mtandaoni

Toleo Na.1 // Jamhuri ya Muungano wa Tanzania // Yaliyomo // Maduhuli ya Madini Februari Tanzania sasa rasmi Chunya yazidi kupaa 2020 Tume ya kuuza bati nje...Na.04 ...Na.08 Madini Masoko ya Madini Wafanyabiashara wadogo yaingiza Bilioni 58.8 wa madini Shinyanga kuuziwa ...Na.06 5% ya almasi na mgodi www.tumemadini.go.tz wa WDL...Na.13

Tume ya Madini 2020

Uzinduzi wa Hati Halisia ya Jadini ya bati... Na.1 Dkt. John Pombe Magufuli Madini News Rais wa Jamhuri ya Muungano Tolea Na.1 wa Tanzania Februari, 2020 HALIUZWI

KUHUSU SISI Tume ya Madini imeanzishwa chini ya Sheria ya Madini ya Mwaka 2010 kama ilivyorekebishwa na Sheria (Miscellaneous Amendment) Act Yaliyomo 2017. Tume ilianzishwa kupitia Gazeti la /HABARI NA MATUKIO Serikali Namba 27 iliyotolewa tarehe 7 Julai, 2017.

Tume imechukua majukumu yote 1 Tanzania Sasa Rasmi Kuuza Madini ya Bati Nje . . . . . 04 ya kiutendaji ambayo yalikuwa yakifanywa na Idara ya Madini 2 Masoko ya Madini yaingiza TZS Bilioni 58.8 - Profesa Manya . . . . 06 chini ya Wizara ya Nishati na Madini na kazi zote ambazo 3 Maduhuli ya Madini Chunya yazidi kupaa . . . . 08 zilikuwa zikifanywa na Wakala wa Ukaguzi wa Madini wa Tanzania 4 Mnada wa Kwanza wa Almasi Tangu Kupatikana kwa Uhuru (TMAA) na Kitengo cha Uchambuzi wa Almasi (TANSORT). wa Tanganyika Wafanyika . . . . 13 Lengo la Tume ni kuimarisha 5 Migodi mipya ya kati mbioni kuanza- Prof. Manya . . . . 11 usimamizi wa Sekta ya Madini na kuhakikisha Serikali inafaidika 6 Wizara Yakabidhiwa Kituo cha Pamoja Cha kutokana na mapato yanayopatika- Biashara- Mirerani . . . . 15 na kwa namna endelevu.

7 Kurugenzi ya Huduma za Tume yafanya Mageuzi, DIRA Tume ya Madini . . . . 16 Kuwa Taasisi inayoongoza katika Sekta ya Madini Afrika.

DHIMA /PICHA NA MATUKIO Kuchochea na kurekebisha Sekta ya Uchimbaji Madini ili kuhakikisha inatoa mchango endelevu na wenye tija katika uchumi wa Taifa. 8 Matukio na Picha, Februari 2020 . . . . 17-22

Mhariri Mkuu Prof. Shukrani E. Manya

Mhariri Msaidizi Greyson Mwase

Wajumbe William Mtinya George Kaseza Mha. Yahya Samamba Dkt. Abdulrahman Mwanga Asteria Muhozya Andendekisye Mbije

Msanifu Jarida Kelvin Kanje

3 Tume ya Madini #1 /HABARI NA MATUKIO

Tanzania Sasa Rasmi Kuuza Madini ya Bati Nje Asteria Muhozya na Tito Mselem, DSM

Uzinduzi wa Cheti cha Uhalisia ulifanywa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, mbele ya hadhira ya washiriki zaidi ya 1,000 kutoka ndani na nje ya nchi waliohudhuria Mkutano wa Kimataifa katika Sekta ya Madini Tanzania 2020 wakiwemo Mawaziri kutoka nchi za ICGLR, Sekretarieti ya ICGLR, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, , Wadau wa Madini, Wataalam wabobe- zi kutoka Sekta zinazojifungamanisha na Sekta ya Madini, huku Mwamini wa Muunganiko wa Bara la Afrika kutoka nchini Kenya, Prof. Patrick Lumumba akiwa kivutio kwenye mkutano huo .

Mkutano wa Kimataifa wa Uwekezaji katika Sekta ya Madini ulifanyika tarehe 22 hadi 23 Februari, 2020 na kutanguliwa na Maonesho ya Madini mbalimbali yanayopatikana nchini yakiwemo ya Vito, Viwandani na Nishati.

Yazindua Cheti Akifunga mkutano huo uliokuwa na kaulimbiu ‘’Uwekezaji na Ushirikiano Endelevu katika Sekta ya Madini,’’ Waziri Mkuu, cha Uhalisia kwa Majaliwa aliieleza hadhira kuwa Tanzania inakuwa nchi ya nne kutimiza vigezo kwa kutoa Cheti za Uhalisi kwa madini hayo Madini wakati wa kuyauza baada ya nchi za DRC, Rwanda na Burundi. ya 3T’s Waziri Mkuu Majaliwa aliongeza kuwa, Serikali ya Tanzania itaendelea kutekeleza makubaliano yote ya Nchi za Maziwa Tanzania kwa mara nyingine imeingia katika historia Makuu kwa lengo la kuboresha sekta ya madini huku akizitaka kwenye biashara ya Madini ya Bati baada ya kuwa miongo- nchi wanachama kubuni maeneo mapya yatayowezesha serikali ni mwa nchi zilizokidhi Vigezo vya kusafirisha Madini hayo hizo kunufaika kupitia rasilimali madini. nje ya nchi. Tukio hilo la Kihistoria lilifanyika Februari 23, 2020, baada ya Serikali kuzindua rasmi Cheti cha Uhalisia Vilevile, aliziasa nchi Wanachama wa ICGLR kuhakikisha miku- kwa Madini ya 3T’s yani Tungsten, Tantulum na Tin. tano hiyo inakuwa endelevu ili itumike kama njia ya kutangaza fursa za uwekezaji katika sekta ya madini zilizopo Afrika na Kimsingi, Cheti hicho hutolewa kwa nchi mwanachama kuhakikisha mikutano hiyo inazaa matunda yatakayosaidia baada ya kukidhi vigezo vilivyoainishwa ambapo katika kuipeleka mbele sekta ya madini. maeneo kumi ya makubaliano, suala la Madini ni itifaki ya tano ambayo inahusu udhibiti wa uvunaji haramu wa Aliongeza kwamba, serikali imeridhika na utendaji wa wizara ya Madini. Madini na Tume ya Madini ambapo mafanikio ya utendaji huo yanaonekana ikiwemo kuongezeka kwa mapato yatokanayo na Taarifa zilizotolewa kwa nyakati tofauti hivi karibuni na madini, kukua kwa mchango wa sekta ya madini, udhibiti wa Viongozi Waandamizi wa Wizara ya Madini akiwemo utoroshaji wa madini na kueleza kuwa hali hiyo imeleta mageuzi Waziri wa Madini, , Naibu Waziri Stanslaus makubwa katika sekta husika. Nyongo, Katibu Mkuu wa Madini Prof. Simon Msanjila na Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini Prof. , ‘’Ndugu washiriki, mafanikio yote yaliyotokea kwenye sekta ya walieleza kuwa, vigezo hivyo vinalenga kuhakikisha madini chanzo chake ni Bunge. Kwenye nchi zilizopo hapa, madini hayo hayatumiki kwenye kuchochea vita na chukueni haya’’, alisema. migogoro katika nchi husika na badala yake yalenge katika kuzinufaisha nchi hizo.

Tume ya Madini 4 Awali, akizungumza katika mkutano ‘’Uzinduzi huu ni hatua kubwa ya mabadiliko, huo, Waziri wa Madini Doto Biteko lakini sisi sote tunahitaji kupambana kwa alisema mkutano huo ulilenga katika pamoja ili kulinda rasilimali zetu,’’ alisema kutoa fursa kwa wadau kutambua fursa balozi Muburi. za uwekezaji zilizopo nchini, kujenga ushirikiano wa kibiashara miongoni Muburi aliongeza kuwa, rasilimali madini mwa wadau, kuwasikiliza wadau na katika nchi nyingine zimekuwa chanzo cha kujua namna ya kuzifanyia kazi migogoro na badala ya rasilimali hiyo kutumi- changamoto zilizopo katika sekta ka kama biashara imekuwa chanzo cha kuzal- husika. isha wakimbizi. Alizitaka nchi wanachama kuhakikisha zinaendeleza juhudi za kuhakiki- Aidha, alisema kwamba, mkutano huo sha rasilimali madini zinaleta Amani Afrika umetumika kutangaza mafanikio ya badala ya kuwa chanzo cha matatizo. sekta kufuatia mabadiliko yaliyofanywa katika sheria ya madini ikiwemo kutoa ‘’Tanzania imekuwa nchi kiongozi barani mrejesho wa utekelezaji wa maazimio Afrika kuleta Amani tangu enzi za Hayati yaliyofikiwa katika Mkutano wa Sekta baba wa Taifa Mwl. . Kukiwa na ya Madini uliofanyika Mwaka 2019 na amani katika nchi jirani, majirani mnaishi kuwashirikisha wadau mbalimbali wa vizuri,’’ aliongeza Balozi Muburi. madini nchini. Aidha, aliongeza kwamba sekretarieti hiyo Naye, Spika wa Bunge la Jamhuri ya itaendelea kuzisaidia nchi wanachama wa Muungano wa Tanzania, Job Ndugai, umoja huo kuhakikisha sekta za madini akizungumza katika mkutano huo, katika nchi hizo zinaendelea na kuwa na tija aliipongeza Serikali kwa mabadiliko kwa nchi wanachama. ambayo yametokea kwenye sekta ya madini na kuipongeza Sekretarieti ya Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Mawaziri ICGLR kwa kuweka misingi mizuri wa Nchi za Maziwa Makuu na Waziri wa kuhakikisha nchi wanachama zinanu- Maendeleo ya Nishati na Madini wa Jamhuri faika na rasilimali zao ikiwemo kudhibi- ya Uganda alizitaka nchi wanachama ti migogoro inayotokana na madini hayo. kuhakikisha zinakuwa na mfumo jumuishi Aliwataka watanzania kutokuwa ambao utaweka sura moja kwa wawekezaji watazamaji katika kushiriki na kumiliki wote watakaowekeza katika nchi wanachama. uchumi wa madini na kueleza kuwa, Alisema nchi wanachama zinapaswa tayari Rais wa Jamhuri ya Muungano kuhakikisha kwamba zinakomesha vitendo wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli vya uhalifu na migogoro inayosababishwa na ameweka misingi inayowapa nafasi ya uwepo wa madini hayo. kumiliki uchumi huo. Kwa mujibu wa Katibu Mtendaji wa Tume ya ‘’ Afrika bado haina kampuni kubwa za Madini Prof. Shukrani Manya, akizungumza madini zote ni za kigeni, huko nyuma katika kipindi cha Morning Trumpet kinacho- tulikuwa tunaibiwa sana, Rais amey- rushwa na luninga ya AZAM, alisema aweka chini hayo yote na sisi bunge kwamba Cheti hicho cha uhalisi kilichotolewa tukamuunga mkono,’’ alisema Spika kinaonesha mnyororo mzima wa madini ya Ndugai. bati tangu hatua za mahali yanapochimbwa, anayechimba, mahali mtaji wa mchimbaji Kwa upande wake, Katibu Mtendaji wa unapotoka, soko analouzia, anayenunua na Seretarieti ya ICGLR, Balozi Zachary namna yanavyosafirishwa. Muburi alisema kwamba, cheti hicho cha uhalisia kwa Tanzania ni ishara Aliongeza kwamba lengo ni kuhakikisha kwa wanunuzi wa madini hayo kuwa madini hayo hayana mkono wa ufadhili Tanzania sasa inao uhalali wa kuuza kuchochea mgogoro katika nchi za maziwa madini hayo na hivyo kuzitaka nchi makuu na hayahusishi uhalifu wowote. nyingine kuiga mfano ili kuwezesha usafirishaji halali wa madini ya bati.

5 Tume ya Madini #1 Masoko ya Madini yaingiza TZS Bilioni 58.8 - Profesa Manya

Na Greyson Mwase

Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini, ..Watendaji kutoka Tume ya Madini na Aliongeza kuwa, katika kuimarisha Profesa Shukrani Manya amesema kuwa, Mawaziri na wawakilishi wa Mawaziri udhibiti wa utoroshwaji wa madini, tangu kuanzishwa kwa masoko ya madini kutoka katika nchi za Ukanda wa Maziwa Serikali kupitia Wizara ya Madini iliamua mapema Machi, 2019 hadi Desemba, 2019, Makuu. kujenga ukuta wa Mirerani hali iliyopele- masoko hayo yameiingizia Serikali kiasi kea kuongezeka kwa uzalishaji wa cha shilingi bilioni 58.8 Akielezea mafanikio ya masoko 28 ya tanzanite kutoka kilo 164.6 mwaka 2016 madini na vituo 25 vya ununuzi wa hadi kilo 2,772.2 kwa mwaka 2019. Profesa Manya aliyasema hayo tarehe 23 madini yaliyoanzishwa tangu mwezi Februari, 2020 kwenye Mkutano wa Machi 2019 hadi Desemba, 2019 Profesa Akielezea mikakati ya Tume ya Madini Kimataifa hukusu Uwekezaji kwenye Manya alisema Serikali imekusanya kiasi kwenye uboreshaji wa huduma zinaz- Sekta ya Madini jijini Dar es Salaam cha shilingi bilioni 58.8 otolewa na masoko ya Madini, Profesa uliokutanisha wadau wa madini kutoka Manya alisema sambamba na kuboresha ndani na nje ya nchi. Akielezea mafanikio ya Soko la Madini la miundombinu kwenye masoko ya madini, Geita, Profesa Manya alisema tangu Tume pia imenunua vifaa vya kupima Waliohudhuria katika mkutano huo wa uanzishwaji wa soko, kiwango cha mauzo madini na kupeleka wataalam nje ya nchi siku mbili walikuwa ni pamoja na Waziri kimeongezeka kutoka kilo 100 mwaka kwa ajili ya kusomea masuala ya wa Madini, Doto Biteko, Naibu Waziri wa 2018 hadi kilo 500 kwa mwezi mwaka uthaminishaji wa madini ya vito. Madini, , Katibu Mkuu 2019. wa Wizara ya Madini, Profesa Simon Msanjila...inaendelea

Tume ya Madini 6 www.tumemadini.go.tz Maduhuli ya Madini Chunya Yazidi Kupaa

Hadi kufikia Januari 31 yafikia bilioni 24.1 sawa na lengo la asilimia 128 ya lengo la mwaka. Mwenyekiti Tume ya Madini apongeza Mkuu wa Wilaya, Afisa Madini Mkazi

Na Greyson Mwase Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Chunya, Godson Kamihanda ameeleza kuwa kuanzia kipindi cha mwaka wa fedha 2019/2020 kilichoanza Julai, 2019 hadi Januari 31, 2020, ofisi yake imefanikiwa kukusanya jumla ya kiasi cha shilingi bilioni 24.173 ikiwa ni sawa na asilimia 128 ya lengo la ofisi kwa mwaka wa fedha 2019/2020 ambalo lilikuwa ni shilingi bilioni 18.861.

Kamihanda aliyasema hayo leo tarehe 13 Februari, 2020 kwenye ziara ya Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula Wilayani Chunya mkoani Mbeya yenye lengo la kufuatilia maelekezo aliyoyatoa katika ziara yake aliyoifanya awali nchini kati ya tarehe 29 Oktoba, 2019 na tarehe 03 Novemba, 2019, kukagua shughuli za uchimbaji wa madini, kusikiliza na kutatua kero mbalimbali za wachimbaji wa madini.

Alisema kuwa maduhuli yamechangiwa na uanzishwaji wa Soko la Madini Chunya pamoja na vituo vidogo tisa vya ununuzi mdogo wa madini vilivyopo katika maeneo ya Makongolosi, Matundasi, Itumbi, Chunya Mjini, Sangambi, Godima, Igundu na Shoga na vituo vingine vilivyopo katika maeneo ya Mkwajuni na Saza katika Wilaya ya Songwe.

Aliongeza kuwa ili kuhakikisha biashara ya madini inakuwa na mchango mkubwa kwenye makusanyo ya maduhuli Chunya, kwa mwaka wa fedha 2019/2020 ofisi yake ilitoa leseni 105 za ununuzi mdogo wa madini ya dhahabu kwa wale ambao walikubali kukaa katika vituo vidogo vya ununuzi wa madini.

Alisema pia ofisi yake ilitoa leseni 34 za ununuzi mkubwa wa madini katika kipindi cha kuanzia mwezi Julai, 2019 hadi Januari, 2020 tofauti na mwaka 2018/2019 ambapo ni leseni tisa tu zilitolewa.

Alisema kuwa, kukua kwa biashara ya madini Chunya kumetokana na elimu ya uhamasishaji ambayo imekuwa ikifanywa na Ofisi yake tangu kuzinduliwa kwa Soko la Madini Chunya mnamo tarehe 02 Mei, 2019 na Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Profesa Simon Msanjila ikiwa ni siku tano baada ya Rais John Magufuli kutoa siku saba za kuhakikisha soko husika limefunguliwa.

Leseni 34 za ununuzi mkubwa wa madini Wananchi wameanza kuwa na uelewa mkubwa wa zimetolewa katika kipindi cha kuanzia mwezi Julai, umuhimu wa kutumia masoko ya madini na kuwa walinzi 2019 hadi Januari, 2020 tofauti na mwaka wa rasilimali za madini huku wakilipa kodi mbalimbali 2018/2019 ambapo ni leseni 9 tu zilitolewa. Serikalini.

Godson Kamihanda Mhandisi Maryprisca Mahundi Afisa Madini Mkazi Mkuu wa Wilaya Mkoa wa Kimadini Chunya ya Chunya

8 Tume ya Madini #1 Katika hatua nyingine, Kamihanda aliongeza kuwa ili Wakati huo huo Mwenyekiti wa Tume ya Madini alimpongeza kuhakikisha usimamizi unaimarishwa kwenye vituo vya Mkuu wa Wilaya ya Chunya Mhandisi Maryprisca Mahundi na ununuzi wa madini, ofisi yake ilishirikisha viongozi wa kata Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Chunya, Godson Kamihanda ambao wamekuwa mstari wa mbele kusimamia biashara ikiwa kwa usimamizi mzuri wa masoko ya madini hali iliyopelekea ni pamoja na kuwasilisha taarifa zote kwa maafisa wa Tume ya maduhuli ya Serikali kupaa. Madini ambao wamekuwepo kwenye soko kuu la madini. Akielezea mikakati ya Tume ya Madini katika kuboresha Naye Mkuu wa Wilaya ya Chunya, Mhandisi Maryprisca huduma kwenye Ofisi za Maafisa Madini Wakazi wa Mikoa, Mahundi alisema kuwa Ofisi yake imekuwa ikisimamia kwa Profesa Kikula alisema Serikali imeongeza wataalam kwenye karibu sana suala la usalama kwenye biashara ya madini ikiwa Ofisi za Madini, vitendea kazi ikiwa ni pamoja na magari na ni pamoja na kutoa elimu kwa wafanyabiashara wa madini. mashine za kupima madini kwenye masoko ya madini yaliyoanzishwa. Alisema kuwa, wananchi wameanza kuwa na uelewa mkubwa wa umuhimu wa kutumia masoko ya madini na kuwa walinzi Aidha, Profesa Kikula alifanya ziara katika vituo vya ununuzi wa rasilimali za madini huku wakilipa kodi mbalimbali wa madini vilivyopo katika eneo la Makongolosi na kuwataka Serikalini. wafanyabiashara wadogo kuwa wazalendo na waaminifu kwenye biashara ya madini huku wakilipa kodi mbalimbali Mbali na kupongeza juhudi zinazofanywa na Rais wa Jamhuri Serikalini. ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Magufuli kwenye Sekta ya Madini, alisema kuwa kabla ya maboresho kwenye Sekta ya Pia Profesa Kikula alitembelea Kampuni za Uchenjuaji wa Madini wachimbaji wa madini wasio waaminifu walikuwa Dhahabu za PM na Otta Mining Limited zilizopo katika eneo la wakitorosha madini hali iliyoikosesha Serikali mapato yake. Makongolosi na Kampuni ya Uchimbaji na Uchenjuaji wa Dhahabu ya Sunshine iliyopo katika eneo la Matundasi Wilayani Chunya Mkoani Mbeya

Tume ya Madini 9 ZIARA YA MWENYEKITI WA TUME YA MADINI PROFESA IDRIS KIKULA CHUNYA,13 FEBRUARI, 2019.

Mkuu wa Wilaya ya Chunya, Mhandisi Maryprisca Mahundi (mbele) akimwongoza Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula ( wa pili) kwenye ziara katika 05 Kampuni ya Uchenjuaji wa Dhahabu ya Otter iliyopo katika eneo la Makongolosi Wilayani Chunya Mkoani Mbeya.

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula (kushoto) akiangalia namna 01 upimaji wa madini ya dhahabu unavyofa- nyika katika kituo cha ununuzi wa madini cha Makongolosi kilichopo Wilayani Chunya Mkoani Mbeya. Kulia ni mmoja wa wauzaji katika duka linalomilikiwa na Sitta Malase, Philemon Boniphace.

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula (kushoto) akitoa maelekezo kwa Afisa Madini Mkazi wa Chunya, 02 Mhandisi Godson Kamihanda (wa pili kulia) katika Kiwanda cha Uchenjuaji Dhahabu cha PM kilichopo katika eneo la Makongolo- si Wilayani Chunya Mkoani Mbeya. Katikati ni Mkuu wa Wilaya ya Chunya, Mhandisi Maryprisca Mahundi.

Kutoka kulia waliosimama Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula na 03 Mkuu wa Wilaya ya Chunya, Mhandisi Maryprisca Mahundi wakiangalia namna uchenjuaji wa dhahabu unavyofanyika katika Kiwanda cha Uchenjuaji Dhahabu cha PM kilichopo katika eneo la Makongolo- si Wilayani Chunya Mkoani Mbeya.

Mkuu wa Wilaya ya Chunya, Mhandisi Maryprisca Mahundi akizungumza na Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa 04 Idris Kikula pamoja na timu yake (hawapo pichani) ofisini kwake mara baada ya kuwasili wilayani Chunya kwa ajili ya ukaguzi wa shughuli za madini, kusikiliza na kutatua kero za wachimbaji wa madini.

10 Tume ya Madini #1 Migodi mipya ya kati mbioni kuanza- Prof. Manya

Na Asteria Muhozya, Dar es Salaam

Katika jitihada za kuhakikisha Tanzania Prof. Manya aliyasema hayo wakati akitoa Akizungumzia swali alilouli- inakuwa nchi ya Viwanda na hatimaye tathmini ya Mkutano wa Kimataifa wa zwa kuhusu mvutano wa kufikia uchumi wa Kati ifikapo Mwaka Uwekezaji katika Sekta ya Madini ambao Barrick na Serikali alisema 2025 na kama inavyoeleza Dira ya Maen- aliuelezea kuwa ulikuwa na mafanikio, awali wawekezaji wengi deleo ya Taifa, hivi karibuni Serikali ilitan- kwani walioshiriki wameondoka na kitu walionesha kusita lakini gaza kuwa, kabla ya Uchaguzi Mkuu wa cha ziada. baada ya muafaka wengi Mwezi Oktoba, 2020 Migodi Mipya Miwili wameelewa na wame- ya Kati itakuwa imeanzishwa nchini. Akieleza lengo la mkutano huo, alisema hamasika kuja kuwekeza ulilenga kueleza fursa za uwekezaji zilizo- nchini. Hayo yalisemwa Februari 25, 2020 na po katika Sekta ya Madini nchini na Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini Prof. kuieleza Dunia kuwa fursa za uwekezaji Tume ya Madini imepata Shukrani Manya wakati akizungumza zipo, huku Serikali na washiriki wa maombi mengi ya Leseni kwenye Kipindi cha Morning Trumpet mkutano wakipata fursa ya kuzungumza. kutoka nje. Aliongeza kinachorushwa kupitia Luninga ya AZAM. kwamba baada ya muafaka Akizungumzia Cheti cha Uhalisia kwa na Barrick sasa Serikali inao Aidha, uanzishwaji wa migodi hiyo unak- Madini ya 3T’s yajulikanayo kama Tung- wawakilishi kwenye nafasi wenda sambamba na Malengo ya Wizara sten, Tantulum na Tin alisema kwamba za maamuzi na huku ikiwa ya Madini ya kuhakikisha inahamasisha cheti hicho ni hatua kubwa kwa serikali ya mbia katika migodi inayomi- uanzishwaji wa migodi nchini ikiwemo ile Tanzania kwani hivi sasa madini hayo ya likiwa na kampuni hiyo. ya uongezaji thamani madini ili shughuli bati yatatambuliwa kuwa yanatoka Tanza- hizo ziweze kufanyika nchini badala ya nia pale yatakaposafirishwa. Akizungumzia kuhusu madini ghafi kusafirishwa nje suala masuala mengine hususan ambalo mbali ya kujenga uchumi wa nchi Alifafanua kuwa, cheti hicho kilichotolewa utoroshaji wa madini, linasaidia kuzalisha ajira. katika Mkutano huo kinaonesha mnyororo alisema hasara anayopata ‘’Mgodi mmoja utakuwa wa Madini ya mzima wa madini ya bati, tangu yanapo- mtu anayetorosha madini ni Kinywe (graphite) ambao upo Wilayani chimbwa, anayeyachimba, namna yana- kubwa sana kuliko anavyo- Ruangwa na mwingine ni wa madini vyosafirishwa, mahali mtaji wa mchimbaji paswa kulipa kodi na kusema mazito ya baharini (heavy mineral sands’ unapotokea, soko analouzia na anay- ‘’ Tukikukamata tunachukua ambao uko Kigamboni jijini Dar es enunua madini hayo . kila kitu. Kwanini upate Salaam,’’ alisema Prof. Manya. hasara ya kufilisiwa kuliko ‘’Lengo ni kuhakikisha madini hayo kulipa kodi unayostahili Alisema mbali na migodi hiyo ya Kati, hayana mkono wa ufadhili kuchochea kulipa?”. tayari serikali imekwishatoa Leseni za migogoro katika Nchi za Maziwa Makuu Migodi miwili mikubwa ya kuchimba na hayahusishi uhalifu wowote’’ alisema Kuhusu masuala ya madini ya dhahabu na madini ya Rare Prof. Manya. mazingira, alisema wakati Earth Elements na kuongeza kwamba, wataalam wa Tume ya tangu miaka ya 2000 serikali haijaanzisha Akizungumzia historia ya uanzishwaji wa Madini wanapokwenda migodi mipya mikubwa. cheti hicho, alisema kwamba tangu kwenye shughuli za ukaguzi Mwaka 2004 kumekuwa na Jukwaa la wa mazingira, wanaambat- Aliongeza kwamba hata baada ya Mareke- Nchi za Ukanda wa Maziwa Makuu, ana na wataalam kutoka bisho ya Sheria ya Madini, wawekezaji International Conference on the Great taasisi nyingine na kwamba wengi wameendelea kuja kuwekeza Lakes Region (ICGLR) ambapo ukanda huo kumekuwapo ushirikiano nchini, huku taasisi inayohusika kutoa umekuwa na migogoro kutokana na mkubwa kutoka kwa taasisi Leseni za Madini ambayo ni Tume ya baadhi ya watu kuchukua fedha zinazoto- za serikali zinazosimamia Madini ikipokea maombi mengi kutoka kana na Madini hayo ya 3T’s kufadhili masuala ya mazingira. kwa wawekezaji wa nje. migogoro kwenye nchi wanachama.

Tume ya Madini 11 www.tumemadini.go.tz Mnada wa Kwanza wa Almasi Tangu Kupatikana kwa Uhuru wa Tanganyika Wafanyika Wafanyabiashara wa madini wapongeza Wizara ya Madini, Tume ya Madini Na Greyson Mwase, Shinyanga

Tume ya Madini kupitia Ofisi ya Afisa Madini Mkazi wa Alisema mgodi wa WDL ulianza kwa kujenga kituo ndani ya eneo lake Mkoa wa Shinyanga tarehe 18 Februari 2020 iliweka historia ambapo kwa kuanzia mnada umeanza kufanyikia hapo. ya nchi baada ya kufanya mnada wa asilimia tano ya madini ya Almasi kutoka Mgodi wa Williamson Diamond Limited Kaseza aliwataka wafanyabiashara wadogo wa madini ya almasi na uliopo mkoani dhahabu nchini kuyatumia masoko yaliyoanzishwa hivi karibuni. Shinyanga. Wakizungumza katika nyakati tofauti wafanyabiashara wadogo wa Akizungumza kupitia mahojiano maalum, Meneja wa madini ya almasi waliipongeza Serikali kupitia Wizara ya Madini na Biashara ya Madini wa Tume ya Madini, George Kaseza Tume ya Madini na kuongeza kuwa mbali na kujipatia kipato alisema kuwa uuzaji wa asilimia tano ya almasi kutoka wataanza kulipa kodi mbalimbali Serikalini. mgodi wa WDL ni matokeo ya maelekezo yaliyotolewa na Waziri wa Madini, Doto Biteko kupitia mkutano wake aliou- fanya mwaka jana na wadau wa madini mkoani Shinyanga.

Alieleza kuwa, kupitia mkutano husika ilikubalika mgodi wa WDL kuuza asilimia tano ya almasi yake kwa wafanyabi- ashara wadogo wa madini ili waweze kwenda kuuza kwenye Soko la Kimataifa la Dhahabu na Almasi la Shinyanga na kujipatia kipato huku wakilipa kodi mbalimbali Serikalini.

Tume ya Madini 13 Uzinduzi wa Hati Halisia ya Jadini ya bati... Na.1

www.tumemadini.go.tz Wizara Yakabidhiwa Kituo cha Pamoja Cha Biashara- Mirerani Na Issa Mtuwa, Mirerani

Waziri wa Madini Doto Biteko hivi karibuni ‘’Kama mazingira hayatakuwa rafiki sio “Ndugu zangu, nafurahi kuhusu mchango alikabidhiwa Kituo cha Pamoja cha Uchim- dhambi mtu kwenda kuuza Arusha kwa wenu, sisi kama wizara tunautambua, baji na Biashara ya Madini ya Tanzanite- kufuata utaratibu. Mazingira yaliyowekwa kubwa zaidi nawaomba tuzidi kuwa wazal- Mirerani (One Stop Center) kutoka kwa kwenye soko la Arusha ni mazingira endo kama ambavyo Mhe. Rais Dkt. John Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa mazuri na mpaka sasa tunahitaji kuongeza Pombe Magufuli ameamua kuwa mzalendo (JKT) Dk. mkoani jengo kutokana na uwepo wa watu wengi kuhusu raslimali hizi na sisi tuendeelee Manyara, wilaya ya Simanjiro. kufanya shughuli hizo za madini,’’ alisema kumuunga mkono,” alisema Biteko. Biteko. Kwa upande wa Waziri wa Ulinzi na JKT, Kabla ya kufanyika kwa makabidhiano ya Biteko aliongeza kuwa, awali, wachimbaji Dk. Hussein Mwinyi, aliwashukuru viongo- Kituo hicho, Waziri Biteko na Waziri wakubwa walikuwa wamesusa kuchimba zi wa Wizara ya Madini kwa kuwapa heshi- Mwinyi walipatiwa maelekezo kuhusu madini, badala yake wachimbaji wadogo ma kubwa ya kujenga miundombinu mbal- mfumo wa ufungaji wa kamera kwenye waliendelea kuchimba madini ambapo imbali ya sekta ya Madini. ukuta unaozunguka migodi ya Tanzanite shughuli zao zimepelekea kuchangia “Pamoja na hayo, nawashukuru maofisa Mirerani na namna zitakavyokuwa zinafa- mapato kwa wingi katika sekta ya madini. wa jeshi na askari wengine ambao wame- nya kazi. Mhandisi Liberatus Bikulanchi fanikisha ujenzi wa kituo hiki cha pamoja kutoka kwa Wakala wa Ufundi na Umeme Aliongeza kuwa, Kampuni ya Tanzanite- cha kisasa ambacho tunawakabidhi hivi (TEMESA) Dodoma, aliwaeleza Mawaziri One, kabla ya kufunga mgodi huo, ilikuwa punde. Ni ishara nzuri ya kufanya kazi ya hao kuwa kamera zilizofungwa zina uwezo inachangia mapato kwa kiasi cha Tsh. pamoja chini ya wizara mbili tofauti ni wa kuona mbali na kuona chochote nje ya bilioni 1.1. imani yangu wizara yangu tutaendelea ukuta na mahali popote. Hata hivyo, alisema kampuni hiyo na kufanyakazi na nyie kadri nafasi za namna wachimbaji wengine wakubwa walipoacha hiyo zitakapokuwa zinapatikana” alisema Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Waziri kuendelea na uchimbaji, wachimbaji Dkt. Mwinyi Biteko alisema hakuna sababu ya wafany- wadogo waliwapita kwa kuongeza mapato Naye, Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Manyara, abishara kwenda kuuza Tanzanite popote hadi kufikia jumla ya Sh. bilioni 2.7 kwa Chelestino Mofuga, alimpongeza Waziri wakati kituo hicho kipo na kina mahitaji mwaka. Biteko kwa kazi nzuri anayoifanya kwenye yote ya kuwezesha biashara ya madini ya sekta ya madini na kuelezwa kuwa, sekta tanzanite kufanyika katika eneo hilo. hiyo kwa sasa inatambulika rasmi kwa kuingiza mapato mengi nchini huku wachimbaji wadogo wakiwa ni sehemu ya uchangiaji huo.

Waziri wa Madini Doto Biteko (kushoto) akimkabidhi Mfano wa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Dkt. Hussein Baadhi ya Picha zinazoonesha matukio ya maeneo mbalimbali Ufunguo wa Jengo la Kituo cha Pamoja cha Uchimbaji na Mwinyi (kushoto) akimkabidhi mfano wa ufunguo wa Kituo cha ndani na nje ya ukuta kwa wakati mmoja zikiwa ndani kwenye Biashara ya Madini ya Tanzanite (One Stop Centre) Katibu Pamoja cha Uchimbaji na Biashara ya Madini ya Tanzanite chumba cha mfumo wa picha ndani ya jengo Mirerani. Mtendaji wa Tume ya Madini Prof. Shukrani Manya, (kulia) (One Stop Centre) Waziri wa Madini Doto Biteko (kulia) Mirerani. mara baada ya kukabidhiwa na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt. Hussein Mwinyi.

15 Tume ya Madini #1 Akizungumzia masoko ya madini Kurugenzi ya Huduma za Tume 28 pamoja na vituo 25 vya ununu- zi wa madini yaliyoanzishwa yafanya mageuzi, Tume ya Madini nchini tangu mapema Machi, 2019 Mtinya alisema Tume ya Madini mpaka sasa imeshanunua mashine za kupima madini (XRF machines) 24 pamoja na mizani kwa ajili ya kupima madini mbal- imbali yanayoletwa na wafanya- biashara wa madini kwenye masoko kabla ya kutozwa kodi mbalimbali na vifaa hivi vitasam- bazwa hivi karibuni.

Katika hatua nyingine, Mtinya akielezea mafanikio yaliyopatika- na tangu kuanzishwa kwa masoko ya madini, alisema kuwa kati ya kipindi cha Mwezi Machi, 2019 hadi Desemba, 2019 Serikali ilifanikiwa kukusanya jumla ya kiasi cha shilingi bilioni 58.8. kutoka katika masoko hayo.

Mkurugenzi wa Huduma za Tume, William Mtinya Aliongeza kuwa, katika kuhakiki- sha huduma katika masoko ya madini zinaboreshwa, Tume ya Ajira 188 zamwagwa, lengo kuboresha utendaji kazi Madini imeanza uboreshaji wa Vifaa vyamwagwa yakiwemo magari 36 mizani na mashine miundombinu pamoja na za kupima madini 24 kuwapeleka wataalam wake Mkurugenzi wa Huduma za Tume, Wiliam Alisema kuwa, kuanzishwa kwa ofisi husika kwenda kusomea masuala ya Mtinya amesema kuwa tangu kuanzishwa kumepelekea huduma za utoaji wa leseni kufanyika uthaminishaji wa madini nchini kwa Tume ya Madini, Tume imefanikiwa kwa wakati ikiwa ni pamoja na kurahisisha zoezi la India wanaotarajia kumaliza kutoa ajira 188 na kununua vitendea kazi ukusanyaji wa maduhuli na kodi mbalimbali za masomo yao mwezi Mei, 2020. ikiwa ni pamoja na magari 36 na mashine za Serikali. kupima madini (XRF machines) 24 lengo likiwa ni kuboresha mazingira ya kazi na Alifafanua kuwa, ili kuhakikisha watumishi wanao- kuimarisha Sekta ya Madini. fanya kazi katika Ofisi za Maafisa Madini Wakazi wa Mikoa na Maafisa Migodi Wakazi wanafanya kazi Mtinya aliyazungumza hayo tarehe 26 kwa ufanisi na kuongeza kasi ya ukusanyaji wa Februari, 2020 kupitia mahojiano maalum maduhuli katika mikoa husika na kwenye masoko Tume ya Madini alipokuwa akizungumzia mafanikio ya ya madini, Tume ya Madini iliamua kununua magari imefanikiwa kutoa ajira Tume ya Madini tangu kuanzishwa kwake 36 ambapo mpaka sasa magari 32 yameshakabidhi- 188 na kununua vitendea mapema Mei, 2018. wa na kusambazwa kwenye ofisi za madini zilizopo kazi ikiwa ni pamoja na Alisema mara baada ya uanzishwaji wa mkoani. magari 36 na mashine 24 Tume ya Madini, hatua ya kwanza iliyofany- Mpaka sasa tumeshapokea magari 32 na kuyasam- za kupima madini (XRF wa ilikuwa ni uanzishwaji wa Ofisi za Maafi- baza katika mikoa yote, magari manne yaliyobaki machines) lengo likiwa ni sa Madini Wakazi wa Mikoa na Ofisi za tunatarajia kuyapokea mwishoni mwa mwezi Aprili kuboresha mazingira ya Maafisa Migodi Wakazi kwenye migodi 2020, lengo letu ni kuhakikisha watumishi waliopo kazi na kuimarisha Sekta mikubwa na ya kati ya madini lengo likiwa mikoani wanafanya kazi kwa ubunifu na kufaniki- ya Madini. ni kusogeza huduma karibu na wachimbaji sha uvukaji wa lengo la ukusanyaji wa maduhuli na wafanyabiashara wa madini. kwa mwaka wa fedha 2019/2020 ambalo ni la shilingi bilioni bilioni 470.

Tume ya Madini 16

/PICHA NA MATUKIO Mkutano wa Kimataifa wa Madini Dar es Salaam 22-23 Februari 2020

Kutoka kushoto (waliosimama nyuma) Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Stella Manyanya, Naibu Waziri wa Nishati, 01 Subira Mgalu, Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Costantine Kanyasu, Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughu- likia Uwekezaji, , na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), , wakiwa katika picha ya pamoja na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa mara baada ya kufunga Mkutano wa Kimataifa wa Uwekezaji kwenye Sekta ya Madini uliofanyika jijini Dar es Salaam kuanzia tarehe 22 hadi 23 Februari, 2020.

Viongozi wa Tume ya Madini wakiwa katika picha ya pamoja na Waziri Mkuu wa 02 Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa mara baada ya kufunga Mkutano wa Kimataifa wa Uwekezaji kwenye Sekta ya Madini uliofanyika jijini Dar es Salaam kuanzia tarehe 22 hadi 23 Februari, 2020.

Viongozi wa Wizara ya Madini wakiwa katika picha ya pamoja na Waziri Mkuu wa 03 Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa mara baada ya kufunga Mkutano wa Kimataifa wa Uwekezaji kwenye Sekta ya Madini uliofanyika jijini Dar es Salaam kuanzia tarehe 22 hadi 23 Februari, 2020

Waziri wa Madini, Doto Biteko akizungumza katika Mkutano wa 04 Kimataifa wa Uwekezaji kwenye Sekta ya Madini uliofanyika jijini Dar es Salaam kuanzia tarehe 22 hadi 23 Februari, 2020

Tume ya Madini 17 Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo, tarehe 19 Februari,2020 alikutana na kuzungumza na wahariri wa Vyombo vya 05 Habari jijini Dar es Salaam ikiwa ni Maandalizi ya Kuelekea katika Mkutano wa Kimataifa wa Uwekezaji katika Sekta ya Madini Tanzania 2020, uliofanyika tarehe 22 na 23 Februari, 2020.

Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo akisisitiza jambo katika kikao na wahariri wa Vyombo vya Habari jijini Dar es Salaam ikiwa ni Maandalizi 06 ya Kuelekea katika Mkutano wa Kimataifa wa Uwekezaji katika Sekta ya Madini Tanzania 2020, uliofanyika tarehe 22 na 23 Februari, 2020.

Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo akizungumza katika Mkutano wa Kimatai- 07 fa wa Uwekezaji kwenye Sekta ya Madini uliofanyika jijini Dar es Salaam kuanzia tarehe 22 hadi 23 Februari, 2020.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini Prof. Simon Msanjila akifafanua jambo 08 katika Mkutano huo.

18 Tume ya Madini #1 Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula akizungumzia mafanikio ya 09 Sekta ya Madini kwenye Mkutano wa Kimataifa wa Uwekezaji kwenye Sekta ya Madini uliofanyika jijini Dar es Salaam kuanzia tarehe 22 hadi 23 Februari, 2020.

Kamishna wa Tume ya Madini, Profesa Abdulkarim Mruma akielezea fursa 10 zilizopo kwenye Sekta ya Madini Tanzania

Kutoka kulia makamishna wa Tume ya Madini, Dk. Athanas Macheyeki na Haroun 11 Kinega wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zinawasilishwa kwenye mkutano huo.

Viongozi wa Tume ya Madini wakifuatilia hotuba iliyokuwa inatolewa na Waziri wa Madini, Doto Biteko (hayupo pichani) 12 kwenye mkutano huo.

Tume ya Madini 19 Viongozi wa Tume ya Madini wakifuatilia hotuba iliyokuwa inatolewa na Waziri wa Madini, Doto Biteko (hayupo pichani) 13 kwenye mkutano huo

Wadau wa madini (kulia) wakipata maelezo kuhusu shughuli zinazofanywa na Tume 14 ya Madini kwenye banda la Tume ya Madini katika maonesho hayo.

Kutoka kushoto, Meneja Habari na Mawasi- liano wa Tume ya Madini, Greyson Mwase, Mkurugenzi wa Huduma za Tume ya Madini, William Mtinya, Afisa Mazingira 15 wa Tume ya Madini, Monica Augustino na mchimbaji wa madini ya vito, Idd Pazi wakiwa katika picha ya pamoja kwenye maonesho yaliyofanyika katika mkutano huo.

Mkurugenzi wa Huduma za Tume ya Madini, William Mtinya (wa pili kulia) 16 akiwa katika picha ya pamoja na timu iliyoshiriki katika maonesho yaliyofanyika katika mkutano huo.

20 Tume ya Madini #1 Wadau wa Madini Walivyosema Kuhusu Uwekezaji Kwenye Sekta ya Madini Tanzania

Kuna haja ya kuwekeza kwenye RasilimaliWatu. Tukianza kufikiria kuwekeza kwenye teknolojia, elimu na ujuzi katika Sekta hii, tutafika mbali. Kuna tabia ya kubweteka, mazingira ya rushwa na uzembe ambayo wakati mwingine yanatukwamisha. Nchi zenye utajiri mwingi ndizo zenye uchumi kidogo, Nchi kama Korea Kusini ina kiasi kidogo sana cha madini lakini ndiyo nchi mzalishaji mkubwa wa Steel duniani

Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Prof.

Katika Kampuni kubwa 10 Duniani za Madini hakuna hata moja inayotoka Afrika. Afrika inazalisha isichokitumia na kutumia isichokizalisha. Tatizo la Afrika ni kutofikiria nje ya boksi. Wananchi hawali GDP, Afrika iige Tanzania Prof. Patrik Lumumba

Naipongeza Serikali ya Awamu ya Tano kwa dhati kabisa, tulikaa hapa tarehe kama ya leo Mhe. Rais alitupa nafasi ya kukaa zaidi kujadili changamoto zetu. Nampongeza Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini Mhe. Dustan Kitandula alilisimamia hili ndani ya siku 17 mapendekezo yetu yakapitishwa na Bunge. Tunapongeza Utendaji wako Mhe. Waziri na wote Wizarani, na yote yanaonekana leo. Mhe. Umetengeneza mazingira ya siku hii iwe ya kiuwekezaji. Kwa asilimia kubwa changamoto tulizokuwa nazo kwenye sekta ya Madini asilimia 80 zimetatuliwa. Sheria ya Madini sasa ni rafiki kwetu sisi wachimbaji wa Madini.

Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wachimbaji wa Madini Tanzania (FEMATA), John Bina

Baada ya Mkutano wenye Afya wa mwaka 2019, tumeshuhudia mapato yakiongezeka, masoko ya madini kufunguliwa, kuongezeka kwa utii wa Sheria, kusingekuwa na mafanikio kama kusingekuwa na mjadala wa wazi. Leo pia tunakutana tunatarajia baada ya kutoka hapa lengo letu ni kuongeza hatua ambayo itakuwa na mafanikio kwa pande zote sisi sote na Serikali. Kwetu sisi huo ndio uchimbaji endelevu.

Mwakilishi wa Shirikisho la Wachimbaji Wakubwa wa Madini Tanzania, (TCM), Simon Shayo

Tumefarijika sana kwa Mabadiliko ya Sheria ya Madini, tumeona Masoko ya Madini yameanzishwa Tanzania katika maeneo yenye Madini. Tumeona faida japo kuna changamoto ndogo ndogo ambazo Mhe Waziri ungetusaidia. Tunaamini Mhe. Waziri ukitusaidia, Sekta ya Madini itakuwa uti wa mgongo kwa uchumi wa Nchi. Naiomba Serikali iweke mfumo rahisi utakaowawezesha wafanyabiashara wa Madini kusafirisha na kuuza Madini yao nje ya nchi, lengo ni kuinua Sekta ya Madini

Mwenyekiti wa Wafanyabiashara wa Madini Tanzania (TAMIDA), Sam Mollel

Tume ya Madini 21 Wamiliki wa Migodi ya Madini ninawataka kufuata kanuni za afya kwa wafanyakazi ili kodi wanazolipa zitumike kwa ajili ya maendeleo na si kutibu wafanyakazi baada ya kupata maradhi ambayo yanaweza kuepukika

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Serikali kupitia Tume ya Madini itahakikisha inarasimisha wachimbaji wa madini wasio rasmi kwa kuwahamasisha kuunda vikundi na kuwapatia leseni za uchimbaji wa madini ili uchimbaji wao uwe na tija na kulipa kodi mbalimbali Serikalini. Ninawataka wachimbaji wa madini nchini kuhakikisha wanachimba kwa kufuata Sheria ya Madini na Kanuni zake

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula

Tume ya Madini 22 Tume ya Madini 2020 | Toleo Na.1

Jarida la Mtandaoni MAWASILIANO Tume ya Telegramu "MADINI" Simu: + 255-26 2320051 Nukushi: +255 26 2322282 Madini Barua pepe: [email protected] S. L. P 2292 , DODOMA. www.tumemadiuni.go.tz