TUMUUNGE MKONO

RAIS

Lameck Amos Hulilo

i

Copyright © 2019 Lameck Amos Hulilo

Simu: +255 715 403 214 / +255 767 238 675 Barua Pepe: [email protected] Facebook: www.facebook.com/lameckah Youtube: www.youtube.com/user/lameckamos Toleo la kwanza 2019

ISBN: 978-9987-844-26-5

Kimechapishwa na

Mpango Mkakati Technologies www.mpangomkakati.co.tz [email protected] 0715403214/ 0767238675

Haki Zote Zimehifadhiwa. Hakuna sehemu yoyote ya kitabu hiki ambayo inaruhusiwa kutolewa upya au kuhamishwa kwa namna au njia yoyote; kielektroniki au kiufundi au kwa kutoa nakala (photocopy), kurekodi kwa namna yoyote ya kuhifadhi habari au kurudishia tena bila ruhusa ya maandishi kutoka kwa mwandishi

ii

Kitabu hiki ninakitabaruku kwa Rais wetu wa Jamhuri ya Muungano wa ndugu Dkt. John Joseph Pombe Magufuli ambaye amekuwa msitari wa mbele katika kuhakikisha watanzania wanakuwa salama. “Nakuombea Maisha marefu na Mungu akutie nguvu ili upate kutimiza kile chema ambacho alikukusudia nacho hata akaridhia uwe Rais wetu kwa awamu hii. Watanzania tunakupenda, tunakukubali na tumekuelewa. Hakika awamu awamu ya tano imefana sana kwa uwepo wako Piga kazi baba, hapa kazi tu.”

Lameck Amos Hulilo

iii

YALIYOMO SHUKRANI ...... vii UTANGULIZI ...... viii SURA YA KWANZA ...... 1 RAIS NI NANI? ...... 1 AWAMU ZILIZOTANGULIA ...... 4 AWAMU YA TANO ...... 17 SURA YA PILI ...... 29 TANZANIA KWA UFUPI ...... 29 SURA YA TATU ...... 32 SISI WATANZANIA ...... 32 TUTAIFANYIA NINI NCHI YETU? ...... 34 HATIMA YETU...... 34 TUKO WAPI? ...... 35 TUNA NINI? ...... 36 CHANGAMOTO ZINAZOTUKABILI ...... 37 MAADUI ZETU ...... 37 TUNAHITAJI KIONGOZI WA NAMNA GANI ...... 38 TOFAUTI ZETU ZISIWE MTAJI WA KUTUGAWA ...... 39 MIGONGANO YA KISIASA ...... 39 TOFAUTI ZA KIDINI(KIIMANI) ...... 42 TOFAUTI ZA KIKABILA ...... 42

iv

TOFAUTI ZA KIUCHUMI/ KIPATO ...... 42 TOFAUTI ZA MADARAKA NA VYEO ...... 43 TOFAUTI ZA KIELIMU ...... 43 SURA YA NNE ...... 44 MATUMAINI MAPYA ...... 44 HOTUBA YA KWANZA YA RAIS MAGUFULI BUNGENI ...... 44 SURA YA TANO ...... 84 JICHO LA MBALI ...... 84 SURA YA SITA ...... 85 HAPA KAZI TU ...... 85 SURA YA SABA ...... 98 MAONI YA WATU MBALIMBALI...... 98 SURA YA NANE ...... 102 KWA NINI TUMUUNGE MKONO? ...... 102 SURA YA TISA ...... 107 TUMUUNGE MKONO SASA ...... 107 WAJIBU WETU KAMA WANACHI ...... 107 WASANII NA WANA MICHEZO ...... 111 VYOMBO VYA HABARI ...... 113 TAASISI ZA DINI ...... 114 ASASI ZA KIRAIA ...... 117 WAFANYA BIASHARA ...... 117

v

WAKULIMA ...... 118 WANAFUNZI ...... 118 VYAMA VYA SIASA NA WANA SIASA ...... 119 FAMILIA ...... 120 WAFANYA KAZI ...... 121 WAVUVI ...... 122 WAFUGAJI ...... 122 VIJANA ...... 122 SURA YA KUMI ...... 124 NUKUU ZA RAIS MAGUFULI ...... 124 SURA YA KUMI NA MOJA ...... 127 TUIOMBEE NCHI YETU ...... 127 MAMBO YA KUOMBEA ...... 128 REJEA ...... 130

vi

SHUKRANI

Namshukukuru Mungu kwa zawadi ya maisha na nguvu yake isiyowezakuzuilika inayotenda kazi ndani yangu ili makusudi yake yapate kutimizwa sawasawa na yeye mwenyewe apendavyo.

Pia nawashukuru wazazi wangu Mch. Amos T. Hulilo Pamoja na mama Theopista T. Hulilo (Mrs.), mke wangu na rafiki yangu wa karibu Ridness, Wakwe zangu Bw. Na Bi Isaya Gerana, walezi, wachungaji, walimu wangu wa ngazi zote za taaluma kiroho na kimwili, washauri, washirika wa kibiashara, timu yote ya Mpango Mkakati Technologies ndugu jamaa na marafiki kwa mchango wao wa thamani sana. Mungu awabariki sana kwa kazi kubwa wanayoifanya kuzidi kunitia moyo, kunikosoa, kunionya, kunifundisha na zaidi sana kuniombea ili kusudi la Mungu ndani yangu lipate kutimizwa. Mungu awabariki sana.

Mwisho, lakini si kwa umuhimu nikushukuru wewe unayesoma Makala hii ili ujipatie maarifa.

vii

UTANGULIZI Nimekiandika kitabu hiki mahususi kama rai yangu kuwaomba na kuwakumbusha watanzania wenzangu juu ya wajibu tulionao wa kumuunga mkono rais wetu. Tunapaswa kuelewa kuwa nguvu ya kiongozi haiko kwenye mamlaka aliyonayo wala nafasi yake bali ni kwa watu ambao ndiyo chanzo cha mamlaka na nafasi hiyo. Kwa mujibu wa mfumo wa kidemokrasia ambao ndiyo unatumika katika kuwapata viongozi wetu ambapo watu huchaguliwa na wananchi. Tukumbuke pia ili kuweza kuifikisha nchi yetu mahali tunapotaka ifike katika nyanja zote kwa ajili yetu na vizazi vijavyo hatuna budi kusimama pamoja na viongozi wetu ili kuchochea moto wa maendeleo waliouwasha. Nikukaribishe tuungane pamoja katika kitabu hiki ili tujifunze pamoja na tukumbushane wajibu wetu wa kuwaunga mkono viongozi wetu hasa mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye ndiye mhimili mkuu wa uongozi katika nchi yetu.

viii

SURA YA KWANZA RAIS NI NANI? Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 katika sura ya pili sehemu ya kwanza ibara ya 33 kifungu cha kwanza inaelezea kutakuwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano. Inaendelea kwenye sehemu ndogo ya pili kuelezea kuwa Rais atakuwa mkuu wa nchi, kiongozi wa Serikali na Amiri Jeshi mkuu. Haya yote yanamuelezea Rais kama kiongozi wa ngazi ya juu kabisa wa nchi yetu. Nimeanza kwa kunukuu vifungu hivyo ili uelewe Rais ni nani na ana nafasi gani kwako kama mwananchi na ana nafasi gani katika nchi maana ili uweze kumuunga mkono mtu ni muhimu ukamuelewa kwanza. Usichanganywe na maneno na propaganda za kisiasa ukafikiri Rais ni wa (CCM) hapana Rais ni Rais wa watanzania anatuongoza mimi na wewe bila kujali itikadi za vyama vyetu, dini, kabila n.k. Katiba inaposema atakuwa mkuu wa nchi maana yake Rais ndiyo kiongozi wa juu wa nchi yetu kwa mujibu wa katiba. Katiba pia inamtambulisha kama kiongozi wa serikali kwa maana ya kuwa anahusika na mambo yote ya kiutawala na vilevile anatambuliwa kama Amiri Jeshi Mkuu kwa maana ya kwamba ndiyo kiongozi mkuu wa majeshi yetu ya ulinzi na usalama. Mpaka hapo unaweza kuiona na kuitambua nafasi na mamlaka ya Rais ambaye tumempa dhamana ya kutuongoza kwa kipindi cha miaka

1 mitano kama katiba yetu inavyoelekeza. Hivyo basi unavyomtazama Rais usimtazame kwa mlengo wa chama, kabila, dini, kanda n.k bali unapaswa kumtazama kama kiongozi mkuu wa nchi yetu vinginevyo hayo mambo mengine ya kiitikadi yatakuchanganya endapo utayapa nafasi kwa namna isiyo sawasawa. Ukiendelea mbele zaidi katika katiba yetu kwenye ibara ya 35 kifungu cha kwanza utaona namna inavyoelezea shughuli za utendaji kazi kupitia watumishi kwa niaba ya Rais. Hii ni kwamba kiongozi wetu hawezi kufanya majukumu yote peke yake hivyo mamlaka yake iko pia kupitia watu wengine kupitia nafasi mbalimbli za utumishi wa uma. Kumbe Rais haishii ikulu tu lakini mamlaka yake imejigwanya kupitia watendaji mbalimbali ambao wanamsaidia katika ngazi mbalimbalim kwenye utumishi wa uma maana yake ukiwaona hao na kuwaunga mkono basi umemuunga mkono Rais na ukiwakwamisha hao maana yake umemkwamisha Rais. Pia ukisoma ibara ya 36 kifungu kidogo cha pili unaweza kuona pia katiba imempa mamlaka Rais ya kuteua wasidizi wake kenye nafasi mbalimbali. Ndiyo maana kuna nafasi ambazo kupatikana kwake ni mpaka mtu ateuliwe na Rais. Hii pia inampa nguvu na unafuu Rais unaomwezesha kumudu kujigawanya katika mamlaka zake za kiutendaji. Baadhi ya watu ambao ni wateule wa Rais ni Mawaziri, Wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya, majaji, wakurugemzi n.k. Hawa usiwaone wala

2 kuwachukulia kama watu wa kawaida lakini ndani yao wanakuwa wamebeba mamlaka ya urais hivyo ukiwaunga mkono hawa umemuunga mkono Rais na ukiwakwamisha hawa umemkwamisha Rais. Unaweza kufanya rejea na kuisoma vizuri katiba yetu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lakini ninataka kukuonesha jinsi ambavyo mamlaka ya urais ilivyo pana na namna ambavyo imesambaa. Hivyo hii si nafasi ya kubeza, kuifanyia mzaha, wala kuifikiria kwa udogo bali ni nafasi ya kuheshimiwa, kutakiwa heri, kusahauriwa, kusaidiwa kwa namna njema maana kwa mujibu wa katiba yetu unapozungumzia nchi yetu kwa ujumla wake. Endapo tutafanya mengi kumkera na kumvuruga mtu aliyevikwa mamlaka hii kisheria tukidhani kuna la maana tunalofanya tujue tunamnyima utulivu mtu huyu wa kufanya yale ambayo ndiyo sababu ya sisi kumpa dhamana ya kutuongoza katika nafasi hiyo kubwa kuliko zote na ikiwa atafanya lolote kujihami au kutukomoa kwa kutumia mamlaka aliyonayo kisheria kwa mujibu wa katiba tutakaopata madhara ni sisi kama nchi au wananchi na si yeye kama mtu mmoja.

3

AWAMU ZILIZOTANGULIA Tulipo patakuwa hapana maana nzuri sana kama tutasahau tulikotoka ni wapi. Vilevile tulipo hapatakuwa na historia yenye mashko kama tunawasahau wale waliotuongoza kutoka huko na kutufikisha hapa ttulipo leo. Niseme wazi tu pamoja na changamoto nyingi ambazo tumekuwa nazo kama taifa wazee hawa waliifanya kazi kubwa ya kutufanya tufike tulipo pasipo machafuko wala uvunjifu wa Amani na tumeweza kuiona awamu ya tano. Ni tofauti nay ale ambayo tumekuwa tukiyashuhudia katika mataifa mengine. Hii ni ishara ya kutokuwa wabinafsi vinginevyo wangeweza kufanya lolote ambalo pengine leo tungekuwa wakimbizi ndani ya nchi zingine. Ninapozungumzia kazi kubwa iliyofanywa na rais siwezi kuwasahau watangulizi wake maana bila hao pia rais wetu angekuwa na wakati mgumu sana kuliko ule alionao kwa sasa. Tunapaswa kuelewa kuwa kila unapoona mambo mazuri yanafanyika basi ujue pia kuna waliotangualia. Pia tunapaswa kuwa nazo shukrani kwa marais waliotangulia maana bila wao tusingekuwa hapa tulipo leo. Tunaelewa wazi ni jukumu la kila mtanzania kuhakikisha amani yetu inadumu lakini bila kuwa na viongozi wenye weredi na hekima ni vigumu sana kulinda na kudumisha Amani hii. Tunagazie kwa ufupi machache ya kihistoria kuhusu hawa viongozi wetu wa awamu zilizopita maana bila awamu ya kwanza, ya pili ya tatu na ile ya nne hakuna awamu ya

4 tano. Hapa ninamaanisha kuwa tunayaona kwa awamu hii ya tano ni mwendelezo wa awamu zilizotangulia.

MWL J.K NYERERE, BABA WA TAIFA RAIS WA AWAMU YA KWANZA (1961-1985)

Julius Kambarage Nyerere alizaliwa mwaka 13 April 1922 na alifariki dunia tarehe 14 October 1999. Alikuwa mwana harakati aliyeongoza harakati za kupinga utawala wa kikoloni. Alikuwa waziri mkuu wa Tanganyika kuanzia mwaka 1961 hadi 1962 na kisha akawa rais kuanzia 1963-1964, baada ya hapo aliiongoza Jamhuri ya muungano wa Tanzania kama Rais kuanzia mwaka 1964 hadi 1985 alipoamua kung’atuka kwa hiari yake. Pia mwalimu J. K Nyerere ni miongoni mwa wanachama wanzilishi wa chama cha TANU(Tanganyika African National Union) ambacho mwaka 1977 kiliungana na ASP(Afro Shirazy Party) cha kuunda Chama Cha Mapinduzi(CCM) ambacho katika hicho alishika

5 nafasi ya mwenyekiti wa chama mpaka mnamo mwaka 1990 ambacho mpaka sasa bado ndiyo chama tawala nchini Tanzania akiwa Rais kuanzia 1964 to 1985. Mwalmu alitoa kipaumbele kwa falsafa ya ujamaa na kujitegemea. Alizaliwa huko Butiama wakati wa utawala wa wakoloni wa kiingereza nchini Tanganyika, Nyerere alikuwa mtoto wa Chifu wa Kizanaki. Baada ya kumaliza shule alisoma Elimu ya juu katika chuo cha Makelele Uganda na baadaye chuo kikuu cha Edinburgh huko Scotland Uingereza. Mnamo mwaka 1952 alirudi Tanganyika, akaoa na alifanya kazi kama mwalimu. Mwaka 1954, alisaidia juhudi za uanzishwaji wa chama cha TANU, ambapo kupitia hicho aliongoza harakati za kudai uhuru wa Tanganyika kutoka kwa utawala wa waingereza. Kutokana na mchango wa kiongozi wa kutafuta uhuru wa India Mahatma Gandhi, Nyerere alisisitiza mgomo usi0o na fujo zozote ili kutimiza lengo lake. Alichaguliwa kwenye baraza la wawakilishi katika uchaguzi wa mwaka 1958-1959, baada ya hapo Nyerere aliiongoza TANU kuibuka na ushindi kwenye uchguzi mkuu wa mwaka 1960 na ndipo alipopata nafasi ya kuwa Waziri Mkuu wa Tanganyika. Katika mazungumzo na serikali ya Kiingereza ikapelekea Tanganyika kujipatia uhuru wake mnamo mwaka 1961. Mnamo mwaka 1962 Tanzania ilikuwa Jamhuri, huku mwalimu Nyerere akichaguliwa kuwa Rais wa kwanza wa Jamhuri ya Tanganyika.

6

Utawala wake ulitilia mkazo kwenye ukombozi wa nchi nyingi za kiafrika kutoka mikononi mwa wakoloni huku akihamasisha umoja miongoni mwa nchi za kiafrika. Alisisitiza kuundwa kwa Serikali za chama kimoja na vilevile alipelekea kuundwa kwa jumuiaya ya Afrika Mashariki kati ya nchi za Tanganyika, kenya na Uganda. Kufuatia kwa mapinduzi ya Zanzibar mnamo mwaka 1964, visiwa vya Zanzibar viliungana na Tanganyika ili kutengeneza Tanzania. Nyerere alitilia mkazo kwenye kushamirisha sera ya ujamaa na kujitegemea.

Mnamo mwaka 1967, Nyerere alikuja na azimio la Arusha ambalo lilielezea vizuri maono yake ya kijamaa. Hapo ndipo Mabenki, Viwanda vikubwa na makampuni yalibinafsishwa na serikali; elimu na huduma za afya zilipanuliwa kwa kiwango kikubwa. Kulikuwa na mkazo mkubwa kwenye maendeleo ya kilimo kupitia kuundwa kwa jumuiya za wakulima, ingawaje mapinduzi haya ya kilimo yalipelekea kwenye uzalishaji hafifu wa chakula na kupelekea Tanzania kutegemea misaada ya chakula kutoka nchi za nje. Serikali yake ilichangia kwa kiasi kikubwa kwenye utoaji wa elimu na misaada kwa makundi ya wapigania uhuru wa nchi za kusini mwa Afrika. Mnanamo mwaka 1978-1979 mwalimu aliongoza vita dhidi ya nduli Id Amini dada wa Uganda na kufanikiwa kumuondoa madarakani. Mnamao mwaka 1985 mwalimu Nyerere alitangaza kung’atuka kwenye kiti cha urais huku nafasi yake ikichukuliwa na Ali Hassan Mwinyi. Aliendelea kubakia kwenye nafasi ya mwenyekiti wa

7 chama cha mapinduzi mpaka mnamo mwaka 1990, akishughukishughullikia mabadiliko ya uanzishwaji wa mfumo wa vyama vingi na baadaye alikuwa akishughulika kama mpatanishi wa kusaidia kumaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Burundi. Nyerere alikuwa kiongozi wa kipekee. Alijipatia heshima ndani ya bara la Afrika hasa katika mkakati wake wa kusaidia nchi nyinginezo za kusini mwa Afrika zinapata uhuru wake lakini pia anasifika sana kwa kuhakikisha watanzania wanaungana na kuwa kitu kimoja jambo ambalo mataifa mengine ya jirani na Afrika kwa ujumla yameshindwa baada ya kujipatia uhuru wao. Nyerere anaendelea na ataendelea kukumbukwa na kuenziwa na watanzania na dunia kwa ujumla kwa mengi mazuri aliyoyfanya na anabaki kuwa baba wa Taifa la Tanzania na siku ya kifo chake imeingizwa kwenye siku za mapumziko ya umma pasipo kufanya kazi ili kumuenzi kiongozi huyu mashurui ambaye ni shujaa wa watanzania na Afrika kwa ujumla. Maeneo ya kumbukumbu: • Uwanaja wa ndege wa kimataifa wa Julius nyerere uliopo jijini Dar es salaam. • UDSM Mwl. Julius Nyerere Campus • Ukumbi wa iikutano wa kimataifa wa Julius nyerere ulipo jijini Dar es salaam • Nyerere Square Dodoma • Chuo kikuu cha kumbukumbu ya Mwl. Nyerere

8

ALLY HASSAN MWINYI RAIS WA WAMU YA PILI(1985-1995)

Ali Hassan Mwinyi alizaliwa tarehe 8 Mei 1925 katika kijiji cha Kivure Mkoani wa Pwani Tanzania. Ni mwanasiasa wa Tanzania aliyekuwa Rais wa pili wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutoka mwaka 1985 hadi mwaka 1995. Nafasi alizo wahi kushika kabla ya kuwa Rais ni pamoja na Waziri wa mambo ya ndani na vilevile amewahi kua makamu wa Rais. Pia alikuwa mwenyekiti wa chama Tawala chama cha mapinduzi CCM kutoka mwaka 1990 hadi 1996. Katika kipindi cha Mwinyi ndipo mambo mengi sana yaliyokuwa kwenye sera za kijamaa za mwalimu Nyerere yalipobadilishwa. Alipunguza baadhi ya masharti kwenye uingizwaji wa bidhaa za aina mbali mbali nchini kutoka nchi nyingine lakini pia alichochea ukuaji wa sekta binafsi. Ni katika kipindi chake ambapo mfumo wa kisiasa wa nchi yetu ulibadilika kutoka kwenye nchi ya

9 demokraisa ya chama kimoja kuingia kwenye nchi ya demokrasia ya vyama vingi. Mara zote huyu huwa anakumbukwa kwa jina maarufu la mzee Rukhsa. Baadhi ya maeneo ya kumbukumbu:-

• Barabara ya Ali Hassan Mwinyi, mojawapo ya barabara kubwa jijini Dar salaam. • Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi Tabora. • Shule: o The Ali Hassan Mwinyi Islamic Secondary School iliyoko mkoani Tabora o The Mwinyi Secondary School iliyoko mkoa wa Pwani.

10

BENJAMIN WILIAM MKAPA RAIS WA AWAMU YA TATU (1995-2005)

Mkapa alizaliwa mnamo mwaka 1938 huko ndanda Mtwara karibu na Masasi maeneo ya kusini mwa Tanzania bara. Alihitimu elimu yake ya juu kutoka chuo kikuu cha Makelele huko Uganda mnamo mwaka 1962 akipata shahada yake katika masuala ya Lugha ya Kingereza. Pia alipata Shahada ya pili katika chuo kikuu cha Columbia katika msuala ya Mambo ya Kimataifa(International Affairs) mnamo mwaka 1963. Nafasi alizowahi kushika ni pamoja na katibu tawala wa mkoa wa Dodoma na waziri wa Sayansi, Teknolojia na Elimu ya juu. Aliwahi pia kuwa waziri wa mambo ya nje kutoka mwaka 1977 hadi 1980 na vilevile akashika nafasi hiyo hiyo tena kuanzia mwaka 1984 hadi 1990. Mnamo mwaka 1995, mkapa alichaguliwa kuwa Rais wa awamu ya tatu ya serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Vileveile alifaulu kushinda uchaguzi kwenye kipindi cha pili cha kugombea kwake mnamo mwaka 2000 ambapo aliongoza na kumaliza kipindi chake

11

Desembea mnamo mwaka 2005. Katika kipindi chake mkapa anakumbukwa kwa sera yake ya ubinafsishaji wa mashirika ya umma pamoja na uanzishwaji wa soko wa soko huria. Sera hii iliungwa mkono sana na Benki ya dunia na Shirika la Fedha la kimataifa ambapo ilipelekea kufutwa kwa baadhi ya madeni ya Tanzania kwa nchi za nje. Baadhi ya vitu ambavyo vimebaki kama kumbukumbu ya Rais Benjamini William Mkapa:-

• Ukumbi wa Benjamini mkapa ulioko mtaa wa Sokomatola jijini Mbeya • Barabara ya Benjamin Mkapa iliyoko Zanzibar ambayo inayaunganisha maeneo ya Mtoni Kidatu na Uwanaja wa ndege wa Abeid Aman Karume kupitia Daraja Bovu. • Daraja la Mkapa, Daraja refu kuliko yote nchini lenye urefu wa mita 970 lililoko huko Mtwara. • Benjamini William Mkapa Pension Tower, mojawapo ya majengo marefu nchini. • Eneo maalum la uwekezaji wa kiuchumi la Benjmini William Mkapa(Benjamini William Mkpa Special Economic Zone) • Shule ya Sekondari Mereran B W Mkapa iliyoko mkoani Manyara. • Shule ya sekondari ya Benjamin William Mkapa iliyoko Dar es salaam. • Hospitali ya Benjamin William Mkapa iliyoko Dodoma.

12

DK. JAKAYA MRISHO KIKWETE RAIS WA AWAMU YA NNE (2005-2015)

Jakaya Mrisho Kikwete alizaliwa tarehe 7 Oktoba 1950 katika kijiji cha Msoga kilichoko Bagamoyo nchini Tanzania. Ni mwanasiasa wa Tanzania aliyepata nafasi ya kuwa Rais wa awamu ya nne wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa vipind viwili kutokea mwaka 2005 hadi 2010 na kutokea mwaka 2010-2015. Kabla ya kuchaguliwa kuwa Rais alipata nafasi ya kuwa waziri wa Mambo ya nje kutoka mwaka 1995 hadi mwaka 2005 chini ya uongozi wa Rais aliyemtangulia mhe. Benjamini William Mkapa. Pia alitumika kama mwnyekiti wa jumuia ya umoja wa Afrika mwaka 2008 hadi 2009 na vilevile kama mwenye kiti wa umoja wan chi za kusini mwa Afrika(SADC) MWAKA 2012-2013. Kati ya mwaka 1959 na 1963 Kikwete alisoma Shule ya Mshingi Karatu kabla ya kuijunga na middle School katika shule ya Tengeru mwaka 1962 hadi 1965. Baada ya kutoka Tengeru Kikwete alijiunga na Kibaha Sekondari

13 kwa masomo ya O-Level kuanzia mwaka 1966 hadi 1969 na kisha akajiunga na Tanga Techical Sekondari kwa masomo ya A-Level. Alihitimu chuo kikuu cha Dar es salaam mnamo mwaka 1975 akintunukiwa shgahada ya kwanza ya uchumi katika kilimo(Agrieconomics) Kama kada wa chama Kikwete alipata fursa ya kushiaka nafasi mbali mbali ndani ya chama. Wakati TANU na ASP vilipoungana kuunda CCM mwaka 1977, Kikwete alipelekwa Zanzibar ili kusimamia utengenezaji mpya wa mambo ya kimuundo na kiutawala ya chama kisiwani humo. Manao mwaka 1980 alirudishwa Dar es salam makao makuu ili kusimmia idara ya ulinzi na usalama wa cham,a cha mapinduzi kabla ya kuhamishiwa huko Tabora mnamo mwaka 1981-1984 na kisha Singida na Nachingwea mnamo mwaka 1986-1988 na kisha wilaya ya Masasi mnamo mwaka 1988 katika maeneo ya kusini mwa Tanzania Lindi na Mtwara. Mnamo mwaka 1988 alichaguliwa kujiunga na Serikali kuu. Mwaka 1994, katika umri wa miaka 44, alikuwa miongoni mwa waziri wa fedha wenye umri mdogo katika historia ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Desemba 1995, aliteuliwa na Rais Benjmini William Mkapa kuwa Waziri wa Mambo ya nje na ushirikiano wa Kimataifa. Alishika nafasi hii kwa miaka kumi mpaka alipochaguliwa kuwa Rais wa awamu ya nne wa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Desemba 2005 na hivyo kuweka rekodi ya kuwa waziri aliyekaa muda mrefu kwenye nafasi ya waziri wa wizara ya mambo ya nje. Katika kipindi chake cha uwaziri wa mambo ya nje Tanzania ilitoa mchango mkubwa sana katika kutafuta

14 usuluhishi wa amani katika nchi za mazia makuu hususani ni katika Jamhuri ya Burundi na Jamhuri ya kidemokraia ya Kongo(DRC) ambao walikuwa wakikabiliwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe. Kikwete pia alihusika kwa sehemu kubwa katika ujenzi mpya wa Jumuiaya ya Afrika Mashariki. Mara nyingi alihusika kwenye michakato ya uanzishwaji wa umoja wa forodha kati ya nchi tatu za Afrika Mashariki yaani Tanzania, Kenya na Uganda ambapo mara nyingi alishika nafasi ya mwenyekiti kwenye baraza la mawaziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Kikwete alishiriki kwenye uanzishwaji na akawa mwenyekiti mwenza wa Helsinki Process on Globalisation and Democracy. Tarehe 4 Mei 2005 kikwete aliibuka kidedea miongoni mwa wanachama 11 wa CCM waliojitupa kwenye kinyang’angiro cha kupendekezwa kugombea urais mwanka 2005. Baada ya uchaguzi mmkuu wa terhehe 14 Deemba 2005, alitangazwa mshindi na tume ya uchaguzi ana mnamo tarehe 17 Desemba 2005 aliapishwa kuwa Rais wa wamu ya nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tarehe 25 Desemba 2005. Baadhi ya maeneo ya kumbukumbu ya Dk. Jakaya Mrisho Kikwete:-

• Daraja la Kikwete lenye urefu wa mita 275 lililoko magharibi mwa Tanzaia. • Kitu cha vijana cha michezo cha Jakaya M Kikwete kilichoo jijini Dar es salaam.

15

• Taasis ya moyo ya Jakaya Kikwete(Jakaya Kikwete Cardiac Institute - JKCI), iliyoko Hospitali ya Taifa ya Mhimbili. • Barabara ya urafiki ya Kikwete yenye urefu kwa kilomita 12 itakayojengwa kutoka ukonga Banana wilaya ya Ilala hadi Chamazi wilaya ya Temke jijini Dar es salaam. • Shule:

o Shule ya Msingi ya Jakaya Kikwete iliyoko wilaya ya Muleba mkoani Kagera. o Shule ya Sekondari ya Jakaya Kikwete iliyoko Mbulu mkoani Manayara. o J. M. Kikwete Shule ya Sekondari iliyoko wilaya ya Mbozi mkoani Mbeya.

16

AWAMU YA TANO

MHE. DK. JOHN POMBE MAGUFULI RAIS WA AWAMU YA TANO (2015-)

John Joseph Pombe Magufuli alizaliwa trehe 29 Oktoba 1959. Ni mwanasiasa Mtanzania na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzana aliyeingia madarakani tangu mwaka 2015. Vilevile ni mwenyekiti wa Jumuiya ya maenedeleo ya nchi za kusini mwa afrika. (SADC). Kwa mara ya kwanza alichaguliwa kama mbunge mnamo mwaka 1995, alifanya kazi kwenye baraza la mawaziri kama naibu waziri wa kazi mnamo mwaka 1995 mpaka mwaka 2000, Waziri wa Kazi toka mwaka 2000 hadi 2006, waziri wa ardhi na makazi kutoka mwaka 2006 hadi

17

2008, Waziri wa mifugo na uvuvi toka mwaka 2008 hadi 2010 na kisha tena kama waziri wa kazi kwa mara ya pili kuanzia mwaka 2010 hadi 2015. Wakati alipogombea kwa tiketi ya chama cha mapinduzi CCM katika uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 2015 alishinda na kuapishwa kuwa Rais tarehe 5 Oktoba 2015. Utawala wa maguguli umekuwa na mkazo mkubwa katika kupambana dhidi ya vitendo vya rushwa na matumizi mabaya ya fedha, madaraka na ofisi za serikali. John Joseph Pombe Magufuli alianza elimu yake ya msingi katika shule ya msingi Chato kutoka mwaka 1967 hadi 1974 na kisha akajiunga na Katoke Seminary huko Biharamulo kwa elimu yake ya Sekondari kutoka mwaka 1975 hadi mwaka 1977 kabla ya kuhamia Lake Sekondari mnamo mwaka 1977 na kuhimtimu hapo mwaka 1978. Alijiunga na Mkwawa High School kwa masomo ya A- level mwaka 1979 na kuhitimu mnamo mwaka 1981. Mwaka huo huo alijiunga na Chuo cha ualimu cha Mkwawa akisomea masomo ya Diploma ya Sayansi akijikita katika Masomo ya Chemia, Hesabu na Elimu. Magufuli alipata Shahada yake ya kwanza ya Sayanasi ya Elimu katika Chemia na Hesabu kama masomo ya kufundishia kutoka chuo kikuu cha Dar es salaam mnamo mwaka 1988. Vilevile alipata Sahahada yake ya pili 1994 na ?Shahada ya uzamivu mwaka 2009 kutoka chuo hicho hicho cha Dar es salaam. alijiingiza kwenye siasa baada ya kuutumiki aumma kwa kipindi kifupi kama mwalimu katika shule ya Sengerema Sekondari kati ya mwaka 1982 na 1983 wakati alipofundsha masomo ya hesabu na

18 chemia. Baada ya hapo aliacha kazi yake ya ualimu na akaajiriwa na chama cha ushirika cha Nyanza kama mkemia wa kiwanda. Alifanya kazi hapo kuanzia mwaka 1989 hadi mwaka 1995, alipochaguliwa na wananchi kuwa mbunge wa jimbo la Chato. Alichaguliwa kama naibu waziri wa kazi katika kipindi chake cha kwanza cha ubunge. Mwaka 2000 aligombea tena na kushinda na akafanikiwa kuteuliwa kwenye nafasi ya waziri wa kazi akitokea kwenye nafasi ya naibu waziri. Baada ya Rais Jakaya Kikwete kuingia madarakani alimhamishia Magufuli kwenye wizara ya ardhi na makazi tarehe 4 Januari 2006. Vilevile alifanya kazi kama waziri wa mifugo na uvuvi kutoka 2008 hadi 2010 na baada ya hapo alirudishwa kwenye wizara ya kazi kutoka mwaka 2010 hadi 2015. Tarehe 12 Julai 2015 Magufuli alitangazwa kuwa mgombea wa urais mwaka 2015 kupitia tiketi ya chama cha mapinduzi CCM baada ya kupata kura nyingi za maoni na kumshinda aliyekuwa Waziri wa Katiba na Sheria Bi Asha-Rose Migiro na balozi wa umoja wa Afrika Bi amina Salum Ali ambao walipendekezwa kupigiwa kura za maoni ndani ya chama. Ingawaje Magufuli alipata upinzani mkubwa kutoka kwa mwanachama wa zamani wa CCM ndugu ambaye aligombea kupitia Muungano wa vyama vya upinzani(UKAWA) katika uchaguzi uliofanyika tarehe 25 Oktoba 2015, Magufuli alitangazwa mshindi na

19 tume ya uchaguzi way Taifa tarehe 29 Otoba 2015 akiIbuka kidedea kwa kupata asilimia 58 ya kura zote zilizopigwa. Mgombe mwenza wake Bi Samia suluhu Pia alitngazwa kuwa makamu wa Rais. Aliapishwa tarehe 5 Novemba 2015 kuwa Rais wa Jamhuri ya Muunga no wa Tanzani. Baada ya kuingia madarakani, moja kwa moja magufuli alianza kutekeleza sera na mkakati wa kudhibiti matumizi mabaya ndani ya serikali, kama vile kutoruhusu safari za nje zisizo na tija yoyote kwa watumishi wa umma, kutumia usafiri wa bei rahisi na sehemu za vikao, kupunguza idadi ya ujumbe wa watu waliotakiwa kwenda ziara za kimafunzo katika Jumiya ya madora kutoka watu 50 hadi watu 4, kupunguza ufadhili wa ruzuku inayotolewa kwa ajili ya maadhimisho ya siku ya UKIMWI duniani na badala yake fedha hizo zikaelekezwa kwenye mapambano ya kimatibabu dhidi ya UKIMWI, na kupiga marufuku matukio, sherehe na maadhimisho yasiyo na tija yaliyokuwa yakifanywa na taasisi za serikali mfano alipuguza bajeti ya sherehe ya chakula cha jioni ikulu kwa ajili ya kushekea kuingia kwa mhula mpya wa bunge na badala yake vilitumika vitafunwa na vinywaji vya bei ndogo. Vilevile Rais Magufuli alipunguza mshahala wake kutoka 15,000/= usd hadi 4,000/= USD kwa mwezi yaani kutoka shlingi million 34 za kitanzania hadi shilingi hadi shilingi milioni 9.2 za kitanzania. Vilevile magufuli alisitisha sherehe za maadhimisho ya uhuru mwaka 2015 badala yake watu wajihusihse kwenye shughuli za usafi wa maeneo mbali mbali yanayowazunguka ili kupunguza majanga ya milipuko ya kipindupindu. Lakini hakuishai hapo tu hata yeye mwenye

20 we alishiriki kwaenye shughuli za usafi na pia akasema, “ Ni aibu sana kutumia kiasi kikubwa cha pesa kusherekea sherehe za miaka 54 ya uhuru wakati watu wanakufa kwa kipindupindu”. Gharama zilizookolewa dhidi ya kufanyika kwa maadhimisho ya sherehe za uhuru wa miaka 54 ziliekezw kwenye uboreshaji wa huduma za afya na usafi nchini. Taehe 10 Desemba 2015 zaidi ya mwezi mmoja baada ya kuapishwa Rais Magufuli alitangaza Baraza lake ambalo alilipunguza kutoka baraza lenye wizara 30 kwa mujibu wa awamu ilipita na kutengeneza baraza lililokuwa na wizara 19 tu ili kupunguza gharama ambazo serikali ilikuwa ikiingia kwa kuwa na wizara nyingi na mawaziri wengi vile vile. Tarehe 12 April Magufuli alifanya ziara yake ya kwanza ya nje ya nchi kwa kutembelea nchi ya Rwanda ambpo alikutana na rais wananchi hiyo Paul Kagame ambapo alizingua daraja jipya na kituo kipya cha ofisi ya uhamiaji mpakani maeneo ya Rusumo. Vilevile alihudhuria kumbukumbu ya 22 ya mauaji ya kimbari yaliyotokea huko Rwanda mnamo mwaka 1994. Julai 2016 Tanzania ilipiga marufuku matumizi ya shisha, ambapo Rais magufuli alielezea madhara ya kiafya yanayotokana na uvutaji wa shisha kwa vijana ambao ndiyo nguvu kazi ya Taifa. Mwezi Machi 1, 2017 Tanzania ilipiga marufuku ushafirishaji wa madini ambayo hayajachenjuliwa ili kuchochea uchenjuaji wa madini hapapa ndani. Sheria za mikataba ya madini zimefanyiwa marekebisho ili kuipa serikali nguvu ya kuzungumza au kuivunja pale

21 itakapogundulika kuna kitu chochote ambacho si sahihi katika mikataba hiyo.

MHE. MAMA SAMIA SULUHU MAKAMU WA RAIS WA AWAMU YA TANO(2015-)

Samia Hassan Suluhu alizaliwa tarehe 27 Januari 1960. Ni mwanasiasa wa kitanzania. Samia ni Mbunge wa Jimbo la Makunduchi huko Tanzania Visiwani(Zanzibar) tangu mwaka 2010 na amekuwa Waziri wa ofisi ya makamowa Rais katika mambo ya muungano tangu mwaka 2010. Samia amekuwa mwanamke wa kwanza kushika nafasi ya makamu wa Rais nchini Tanzania. Alitangazwa kuwa makamu wa Rais mnamo mwaka 2015 wakati ambapo Rais Magufuli aliposhinda uchaguzi mkuu na kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

22

Kabla ya hapo aliitumikia serikali kama waziri katika Serikli ya mapinduzi ya zanzibara katika kipindi cha Rais Amani Karume. Mwaka 2014 alichaguliwa kuwa makamu mwenyekiti wa baraza la wawakilishi akipewa majukumu ya kuongoza mchakato wa utengenezaji wa katiba mpya. Baada ya kumaliza elimu yake ya Sekondari mwaka 1977, aliajiliwa na wizara ya mipango na maendeleo kama kalani. Alichukua kozi nyingi fupi fupi katika muda wake wa ziada. Mwaka 1986 allihitimu kutoka kwenye taasisi ya Uratibu wa maendeleo ambayo kwa sasa inafahmika kama Chuo kikuu cha Mzumbe akipata advance diploma in public administration.

Baada ya kuhitimu aliajiliwa kwenye mradi uliokuwa chini ya Shirika la Chakula la umoja wa mataifa(World Food Programme). Kati ya mwaka 1992 na 1994, alijiunga na chuop kikuu cha Manchester na akahitimu kwa kupata postgraduate diploma ya mambo ya uchumi. Manamo mwaka 2015 alipata shahada yake ya pili katika Maendeleo ya jamii kiuchumi kupitia progam shirikishi kati ya Chuo Huria cha Tanzania na Southern New Hampshire University. Mwaka 2000 aliamua kuanza kufanya siasa. Alichaguliwa kama mbunge wa viti maalum kwenye baraza la wawakilishi Zanzibar na alichaguliwa kuwa waziri na Rais Amani Karume. Alikuwa waziri pekee mwanamke baraza hilo. Mwaka 2015 alichaguliwa tena na akateuliwa kuwa waziri tena. Mwaka 2010 alijitosa kwenye kinyang’anyiro cha uchaguzi akigombea ubunge jimbo la Makunduchi na

23 akashinda kwa zaidi ya 80%. Rais Kikwete alimteua kuwa waziri wa mambo ya Muungano. Julai 2015 mgombea wa urais wa chama cha mapinduci ndugu John Pombe Magufuli alimchagua ili awe mgombea mwenza wake katika uchaguzi mkuu wa mwaka huo na kumfanya kuwa mgombea mwenza wa kwanza mwanamke katika historia ya chama hicho. Na hii ikamplekea yeye kuwa makamo wa kwanza wa rais mwanamke katika historia ya nchi yetu.

KASSIMU MAJALIWA WAZIRI MKUU(2015-)

Kassim Majaliwa Majaliwa alizaliwa tarehe 22 Mwezi desemba 1961. Ni mwanasiasa wa kitazania ambaye amepata nafasi ya kuwa waziri mkuu tangu mwaka 2015 ambapo alichaguliwa na Rais magufuli baada ya uchaguzi

24 mkuu wa mwaka 2015. Yeye ni mwanachama wa chama tawala chama cha mapidnuzi CCM na amekuwa mbunge wa Ruangwa tangu mwaka 2010. Alimaliza elimu yake ya sekondari katika Shule ya Kogonsera mwaka 1983. Baada ya hapo alifanya kazi kama mwalimu hadi mwaka 1999. Katika mahangaiko ya kusaka elimu alipata diploma ya ualimu kutoka Chupo cha mafunzo ya ualimu Mtwara mwaka 1993 na kisha baada ya hapo alipata Shahada ya kwanza ya elimu kutoka chuo Kikuu cha Dar es salaam mwaka 1998. Alijiunga na vyama vya wafanya biashara na kisha akafanya kazi kama katibu wa wilaya na kisha katibu wa mkoa katika Chama cha Waalimu Tanzania kati ya mwka 1999 na 2006. Alichaguliwa kuwa mkuu wa wilaya ya Urambo mwaka 2006. Alibakia katika majukumu haya mapaka alipochaguiwa kuwa mbunge wa Ruangwa mwaka 2010. Kwa mara ya kwanza Majaliwa alichaguliwa kuwa mbunge wa jimbo la Ruangwa manamo mwaka 2010 kwa tiketi ya chama cha mapinduzi ccm. Alipata nafasi ya kuwa naibu waziri ofisi ya waziri mkuu, utawala bora na serikali za mitaa kuanzia mwaka 2010 hadi 2015. Katika uchaguzi wa mwaka 2015, Majaliwa alichaguliwa tena kuwa Mbunge wa Ruangwa akimbwaga chini mpinzani wake Omari Makota wa chama cha wananchi CUF kwa kupata kura 31,281 ambapo Omari alipata kura 25,536. Baada ya John Pombe Magufuli kuapishwa kama Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mnamo mwaka 2015

25 alimteua Majaliwa kuwa waziri mkuu tarehe 19 Novemba 2015. Uteuzi wake ilikuwa ni jambo ambalo halikutarajiwa na wengi na hata kwake yeye mwenyewe ukizingatia kuwa alikuwa ni mwanasiasa mpya kwenye siasa za uchaguzi. Uteuzi wake ulitokana na unyenyekevu wake, uaminifu, maadili ya kazi vilevile sababu za ukanda maana waziri mkuu mppya alitarajiwa kutokea maeneno ya kusini mahali ambapo hata Majaliwa ndipo anapotoka. Uzoefu wake katika elimu kama mwalimu, mtaalumu wa vyama vya ushirika wa biashara na kama naibu waziri ulitarajiwa kuwa msaada mkubwa katika serikali ya Rais Magufuli ambayo ilitilia mkazo katika kuleta mageuzi na mapinduzi makubwa kweye sekta mbalimbali. Japo kuna waliopinga uteuzi wake lakini ndani ya muda mfupi majali alionyesha utendaji usio wa kawaida katika nafasi yake.

DK. ALI MOHAMED SHEIN RAIS WA ZANZIBAR

26

Ali Mohamed Shein alizaliwa tarehe 13 Machi 1948. Huyu ni Rais wa saba wa Serikali ya mapinduzi ya Zanzibar. Kabla ya kuwa Rais alikuwa makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuanzia mwaka 2001 hadi mwaka 2010. Kwa asili Dk. Shein anatokea visiwa vya Pemba na ni mwanachama wa chama tawala chama cha mapinduzi ccm. Yeye ni Daktari kwa taaluma.

Shein alimaliza elimu yake ya Sekondari katika Chuo cha Lumumba huko visiwani Zanzibar. Mwaka 1969-1970 alijiunga na Voronezh State University, USSR kwa masomo ya sekondari ya juu kabla ya kujiunga na masomo ya shahada ya kwanza kutoka mwaka 1970 hadi 1975 katika chuo kikuu cha Odessa huko USSR. Mwaka 1984 hadi 1988 Shein alipata shahada yake ya uzamili katika Medical Biochemisry kutoka chuo kikuu cha masuala ya utabibu cha Newcastle huko Uingereza. Mnamo mwaka 1995 Shein alipata shahada yake ya uzamivu katika masuala ya Clinical Biochemistry and Metabolic Medicine, akibobea kwenye, “inborn Errors of Metabolism”. Pia alifanya kozi ya masuala ya HIV/ AIDS katika nchi zinazoendelea kutoka Chuo kikuu cha East Anglia mnamo mwaka 1995. Shein alifanya kazi kama Karani katika Wizara ya Elimu na kama msaidizi makmu katibu mkuu kutoka May 1969 mpaka Septemba 1969. Mwaka 1976 hadi 1984alikuwa mkuu wa idara ya Diagnosis and the department of Ptgy katika wizara ya Afya.

27

Alikuwa pia bingwa wa masuala ya vipimo na mkuu wa idara ya Pathology katika wizara ya Afya kuanzia 1989 hadi 1991. Kuanzia Novemba 1991 hadi Julai 1995 Sein alitumika kama Programme Manager, AIDS prevention Project katika wizara ya afya na mshauri wa wizara katika masuala ya maaabara na vipimo. Shein aliteuliw na Rais wa Zanzibar kuwa mjumbe wa baraza la wawakilishi tarehe 29 Oktoba 1995 ambapo aliteuliwa kuwa Naibu waziri wa Afya tarehe 12 Novemba 1995. Kuanzia tarehe 6 November 2000 alikuwa mjumbe wa baraza la wawakilishi akiwakilisha jimbo la Mkanyageni huko Zanzibar kabla ya kuteul;iwa kuwa waziri wan chi Office ya Rais, katiba na utawala bora huko Zanzibar tarehe 22 November 2000 na baada ya hapo kuwa makamo wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Julai 2001. 1966 alikuwa mwanachama wa umoja wa vijana ndani ya ASP(Afro-Shirazi Party). Jan-Desemba 1969 alikuwa katibu wa habari ndani ya umoja huo. Lumumba College 1968- katibu wa ASPYL, Zanzibar Sekondari. 1969- Mwanachama wa ASP. Shein alitangazwa na Chama tawala CCM tarehe 9 Julai 2010 kama mgombea wa urais kwa tiketi ya CCM huko Zanzibar. Alishinda uchaguzi huo na kuwa Rais wa kwanza kutokea katika visiwa vya Pemba.

28

SURA YA PILI TANZANIA KWA UFUPI Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni nchi inayopatikana Afrika mashariki kwenye ukanda wa nchi za maziwa makuu barani Afrika. Nchi hii ni matokeo ya Muungano wa nchi mbili yaani Tanganyika iliyopata uhuru wake tarehe 9 Desemba 1961 na Zanzibar iliyopata uhuru wake tarehe 12 Januari 1964 na kisha zote kuamua kuungana kutengeneza nchi moja mnamo mwaka 1964 ambayo ndiyo ilipewa jina jipya la Tanzania. Kwa upande wa kaskazini imepakana na Uganda. kwa upande wa kaskazini mashariki imepakana na Kenya. Inapakana na visiwa vya Comoro vilivyo ndani ya bahari ya Hindi kwa upande wa mashariki. Upande wa kusini imepakana nan chi za Msumbiji na Malawi; Kusini magharibi inapakana na nchi ya Zambia. Na Upande wa magharibi inapakana na Rwanda, Burundi na Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo. Kwa hiyo kijiographia Tanzania inazungukwa na nchi tisa barani Afrika. Nchi hii inasifika kwa kuwa na vitu vingi vizuri ambavyo vimepelekea iwe na maeneno mengi ya kitalii kama vile mlima Kilimanjaro ambao ni mlima mrefu kuliko yote Afrika unaopatikana upande wa Kaskazini Mashariki mwa Tanzania mkoani Kilimanjaro. Sehemu za maziwa makubwa yote Afrika zinapatikana ndani ya Tanzania. Ambapo upande wa Kaskazini na magharibi linapatika ziwa Victoria ambalo ni ziwa kubwa

29 kuliko yote Afrika, Ziwa Tanganyika ambalo ni ziwa lenye kina kirefu kuliko yote afrika ambalo linasifika kwa kuwa kuwa na samaki wa kipekee. Kwa upande wa kusini linapatikana Ziwa Nyasa. Tanzania ina makabila zaidi ya mia moja kitu kinachoifanya kuwa nchi yenye makabila mengi zaidi Afrika mashariki. Lugha ya Taifa ni Kiswahii na lugha nyingine haya inayotumika kiofisi na kibiashara ni kingereza. Kiswahili hutumika kwenye vikao vya bunge, kwenye mahakama na kama lugha ya kufundishia kwenye shule za msingi. Kingereza kinatumika kwenye biashara za kimataifa, kwenye mambo ya dipromasia, mahakama kuu na kama lugha ya kufundishia kwenye shule za sekondari, shule za upili, vyuo vya kati na vyuo vikuu. Kwa mujibu wa takwimu za sasa Tanzania inakadiriwa kuwa na wakazi milioni 57.3 waliotapakaa kwenye eneo la kilomita za mraba 947,303. Mji mkuu wa Tanzania Dodoma ambapo kwa sasa ndipo ambapo shughuli za ofisi kuu zote za serikali zimehamishiwa kutoka jijini Dar es salaam. Tanzania bara ina jumla ya mikoa 30 ambayo ni Mwanza, Dodoma, Dar es salaam, Pwani, Shinyanga, Ruvuma, Rukwa, Mbeya, Iringa, Njombe, Geita, Simiyu, Mororgoro, Arusha, Kilimanjaro, Manyara, Tabora, Kigoma, Katavi, Tanga, Singida, Lindi, Mtwara, Mara. Tunasifika kwa kuwa na madini kama vile dhahabu, almasi, chuma, tanzanite n.k

30

Tanzania ni miongoni mwa nchi zinazoongoza kwa utalii duniani ikiwa na sehemu mbalimbali za vivutio kama vile Serengeti, Selou n.k

31

SURA YA TATU SISI WATANZANIA

Katika hafla iliyowaleta pamoja viongozi wa Dini na mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda Mch. Anthony Lusekelo maarufu kama Mzee wa upako alisema maneno yafuatayo, “Duniani amini usiamini na hasa hapa Tanzania hakuna sisi nzuri ziko sisi nyingi tu; sisi fulani, sisi fulani, kabila fulani, dhehebu fulani, ukoo fulani, dini fulani lakini hakuna sisi nzuri kama sisi watanzania. Hiyo ndiyo sisi yenye nguvu kuliko zote, Sisi watanzania”

32

Kwa mujibu katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ibara ya 8 kifungu cha kwanza:- “(a) Wananchi ndio msingi wa mamlaka yote, na Serikali itapata madaraka na mamlaka yake yote kutoka kwa wananchi kwa mujibu wa katiba hii. (b) Lengo kuu la Serikali litakuwa ni ustawi wa wananchi. (c) Serikali itawajibika kwa wananchi. (d) Wananchi watashiriki katika shughuli za Serikali yao kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii.” Nguvu ya kiongozi haiko kwenye sera nzuri za chama chake bali ni watu anaowaongoza. Hivyo basi tunapaswa kuelewa kuwa sisi ndiyo tunaoweza kumpa nguvu Rais wetu. Tukitambua kuwa sisis ndiyo nguvu ya kiongozi wetu tusiruhusu walaghai na wasiopenda maendeleo yetu watutumie vibaya. Tunapaswa kuelewa kwamba kanuni ya nguvu inasema, “nguvu haiwezi kuharibiwa wala kutengenezwa lakini inaweza kubadilishwa toka kwenye mfumo mmoja kwenda mwingine”. Wananchi ndiyo nguvu na wanapoamua kusimama na kiongozi wao katika yale mema yote yanayohusu nchi yao wanamfanya kiongozi wao anakuwa na nguvu ya kuwaongoza ili kuwapa maendeleo. Tukiwa kama raia wazalendo ambao tumefaulu kujipambanua na tumejielewa sisi ni akina nani, tuna nini na tunataka nini hatuna budi kukataa kutumiwa vibaya na watu wasio na mapenzi mema na nchi yetu ambao wengi

33 wanapambana katika mengi si kwa ajili yetu bali kwa maslahi yao binafsi badala yake kwa uzalendo wetu tujitoe kuwa msitari wa mbele kupigania maendeleo. TUTAIFANYIA NINI NCHI YETU? Tunapoizungumzia Tanzania kama Taifa na hatima yake ni muhimu kila mmoja ajitazame katika jicho la kilicho chema anachoweza kufanya kwa ajili ya taifa hili na si kwa jicho la kiongozi gani atatufanyia nini ili yeye pamoja na viongozi waweze kwenda bega kwa bega katika kuhakikisha yale yote mema kwa ajili ya nchi yetu yanatekelezeka. Usijiulize Tanzania itakufanyia nini bali kila siku jiulize wewe unatakiwa kuifanyia nini Tanzania ili iwe vile wewe unavyotaka iwe kupitia mchango wa kile unachokifanya. Kuwaza na kujiuliza utaifanyia nini Tanzania badala ya kujiuliza itakufanyia nini ndiyo tafsiri halisi ya moyo wa kizalendo unaopaswa kuwa ndani ya mtanazania yeyote.

HATIMA YETU Ni muhimu kujikumbusha na kuijua hatima yetu kama taifa. Tungependa kufika wapi? Tungependa vizazi vyetu vifike wapi? Tukiyajua hayo hatutafanya mchezo. Kila mmoja wetu akiifahamu nini hatima tunayoitafuta kama watanzania hatakuwa na ujasiri wa kupinga kile ambacho kinafanywa na mtukufu Rais kwa ajili yetu. Kumbuka kama ulijenga vibaya ukitaka kujenga vizuri ni sharti ubomoe ili ujenge tena hivyo basi ikiwa tulifika mahali

34 fulani na imetulazimu kubomoa mahali fulani ili tujenge vizuri kwa ajili ya hatima yetu hatuna budi kufanya hivyo. Ni muhimu tufike mahali kama watanzania tuelewe nini hatima yetu kama Taifa. Hii itatusaidia kujua ya kuyakubali na ya kuyakataa lakini hii itatusaidia kuona mazuri yanayofanyika na kuyaunga mkono na vile vile kujitoa na kusimama bila uoga kupinga mabaya na kuwakemea mawakala wa mambo mabaya yanayoweza kuharibu taifa letu. Pia tunapaswa kujua kuwa hatima ya taifa letu haiko mikononi mwa wageni wala mtu yeyote yule isipokuwa mikononi mwetu wenyewe hivyo basi tukilielewa hilo tutajua kuwa wenye wajibu wa kujenga au kubomoa ni sisi wenyewe.

TUKO WAPI? Ni muhimu kujua tulipo ni wapi. Lazima tujue tuko hatua gani kiuchumi, kimaendeleo, kielimu, kiafya n.k na kisha tukubaliane na maazimio ya kuondoka tulipo kuelekea kule tunapopataka ambapo ndiyo hatima yetu. Kama hatufahamu tulipo ni wapi ni ngumu kukubaliana tunapoambiwa hapatufai na vilevile ni ngumu kujua tunahitaji nini. Wakati mwingine inatubidi kukubali maumivu na gharama tutakazoingia ili tu tuweze kupiga hatua kutoka hapa tulipo. Tukifahamu tulipo ni wapi kama nchi basi ni rahisi sana kuujua wajibu wetu na kuukubali ili tujenge taifa lenye taswira ambayo tunaitaka kitaifa na kimataifa.

35

Na ili tuweze kuyajua haya ni muhimu kila mmoja wetu afuatilie taarifa mbalimbali zinazotolewa na serikali pamoja na taasisi zake maana ndizo zenye dhamana ya kutupa taarifa halisi ili tusizolewe na uvumi wa mambo ya kizushi yanayoenezwa mitaani bila utaratibu kutoka kwenye vyanzo ambavyo si vya uhakika ikiwa sehemu ya agenda za kutubomoa za wale wasiyo na mapenzi mema na sisi. TUNA NINI? Ni lazima tujue tuna nini kama watanzania ili tuweze kujua ni namna gani tumebarikiwa na namna ya kukitumia kile ambacho tumebarikiwa nacho kutoka tulipo kwenda hatua nyingine. Tunazo rasilimali kama madini, mbuga za wanyama, mito maziwa, tuna lugha inayotuunganisha pmaoja lugha ya Kiswahili, tuna ardhi yenye rutuba, mlima mrefu kuliko yote. Tuna amani, hiki si kitu kidogo ndugu zangu na ni cha kulinda kuliko vyote tulivyonavyo maana kikitoweka hiki hatutakuwa na pa kukimbilia na wala hatutakuwa na nafasi ya kutumia tuliyonayo. Tulichonacho ndicho kinachoweza kutusaidia tusichokuwa nacho haijalishi ni kizuri kiasi gani hakiwezi kutusaidia. Lakini zaidi sana tuna Rais shupavu, mpenda maendeleo na mtetezi wa wanyonge mheshimiwa Dk. John Joseph Pombe Magufuli. Hii ni sehemu ndogo tu ya vile vingi tulivyonavyo na ambavyo tukivitumia vizuri vinaweza kutufanya tuifurahie nchi tuliyopea na Mungu kama urithi wetu.

36

CHANGAMOTO ZINAZOTUKABILI Ni muhimu kuzijua changamoto zinazotukabili kama Taifa kwa pale tulipo ili tuzitumie kama ngazi au daraja la kujenga aina ya taifa tunalolitaka. Ni vema kujua tunauhitaji wa elimu, afya bora, ulinzi, maji safi, makazi bora, miundo mbinu kama barabara n.k

MAADUI ZETU Lazima tujue kama taifa tunao maadui wasiopenda maendeleo yetu. Hawa wapo wale wa nje na wale wa ndani ambao ni vibaraka wa adui zetu wa nje na wale ambao wanajali sana maslahi yao binafsi. Pamoja na yote hayo tuna maadui ambao tulisawahi kutahadharishwa na baba wa Taifa Mwl. J. K Nyerere tangu hapo awali na hawa si wengine bali ujinga, maradhi na umaskini. Tukifaulu kukabiliana na hawa tutakuwa na kazi ndogo sana ya kupambana na wale maadui wa nje na wale wa ndani ambao ni vibaraka wa wale wa nje. Hivyo basi kama unavyofahamu ndugu yangu wahenga walisema umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu. Tunapogawanyika kwa maneno ya wale wasiopenda maendeleo yetu kama taifa tunajiingiza katika nafasi ya kuwa dhaifu lakini tunapoungana pamoja na kusmama na Rais wetu kwenye mambo ambayo yamebeba maslahi mapana ya taifa letu tunaweza kuwa na nguvu za kusonga mbele kama Taifa na kuweza kujiletea maendeleo yetu wenyewe na yale yatakayodumu mpaka vizazi vijavyo.

37

Tunawatambua adui zetu hawa wakuu lakini ni lazima tutambue uwepo wa maadui wengine ambao ni mazalia ya hawa ambao wanatuzuia kupambana na hawa

TUNAHITAJI NINI? Ni lazima tujue tunahitaji nini kwa sasa ndiyo tutaweza kujua nani ni sahihi kwetu au nani wa kumuunga mkono akipatikana miongoni mwetu. Tunahitaji elimu bora, maji safi, miundombinu, huduma bora za afya, uongozi bora, watu wazalendo, siasa safi n.k

TUNAHITAJI KIONGOZI WA NAMNA GANI Ni muhimu kujiuliza tunahitaji kongozi wa namna gani. Kwa kufanya hivyo tutajiridhisha juu ya sababu za uamuzi wetu wa kumuunga mkono. Ni lazima kujiuliza kiongozi yupo ili iweje na je! asipokuwepo nini kitaharibika na akiwepo kama hayupo madahara yake ni nini. Hizi ni baadhi ya sababu ambazo zitapelekea sisi kujua ni kiongozi gani tunayemtaka au tuliyemataka:- 1. Anayejua Shida za watu 2. Asiyetanguliza mbele maslahi yake 3. Mpenda maendeleo 4. Mpenda haki

38

5. Kiongozi shupavu ambaye hayuko tayari kufungama na makundi ya walanguzi na wezi wanaotamani kuuza kila kilichomo kwenye nchi yetu bila kujali urithi wa vizazi vijavyo. 6.Awe kiongozi wa wananchi na si kiongozi wa chama fulani wala kundi fulani la watu wenye maslahi yao binafsi. 7. Awe tayari kujitoa kuwatumikia wanachi katika hali zote tunazopitia kama nchi. 8. Awe tayari kuweka mbele maslahi yanayoendana na yale ambayo ndiyo uhitaji wetu mkubwa. 9. Awe mchapa kazi 10. Msikivu na anayeweza kushaurika pia. 11. Anayeweza kutekeleza ahadi alizotoa kwa wananchi wakati wa kuwaomba ridhaa ya kuwaongoza (wakati wa kampeni) 12. Awe na moyo wa uvumilivu maana kuwaongoza watanzania inahitaji uvumilivu.

TOFAUTI ZETU ZISIWE MTAJI WA KUTUGAWA MIGONGANO YA KISIASA Kama wananchi tunapaswa kuwa wanachama wa maendeleo. Simaanishi kuwa wale ambao wameamua kuwa wanachama wa vyama vya siasa miongoni mwetu

39 wasiwe lakini ninachomaanisha hapa ni kuwa tunapaswa kutanguliza mbele maslahi ya kimaendeleo kuliko maslahi ya kisiasa. Mara nyingi sana kinachotuvuruga katika mengi hata kiasi cha kuwafanya baadhi ya viongozi wetu waonekane hawafai huwa ni migongano ya kisiasa hususani ni baadhi ya watanzania wenzetu wanaoendekeza siasa chafu zisizo na tija kwa malengo yao binafsi ya kujitafutia kibali kwa wanachi. Wana siasa inabidi wafikie mahali pa kuelewa kuwa watanzania si wajinga wa kuzolewa na siasa za kizushi na kuchafuana lakini kama wakijitokeza kwa namna ambayo ni sawa na kwa hoja za kueleweka na zenye ushawishi kwa wakati sahihi watakubaliwa lakini si zile siasa za kupinga kila linalofanywa na serikali hata yale mema ya wazi kabisa. Ni lazima tuwe makini kwenye hii migongano ya kisiasa na madai ya kisiasa ya baadhi ya wanasiasa na makundi ya kisiasa ili kuziba mianya ya siasa inayoweza kupelekea kuvurugika kwa amani yetu na kutupotezea muda ambao tungeweza kuutumia kwa ajili ya maendeleo yetu wenyewe. Wanaofanya siasa tuwaache wafanye siasa kwa utaratibu wa kisiasa kwa mujibu wa katiba yetu lakini tusikubali kutumika kisiasa kuzuia maendeleo kwa kujihusisha na mambo ambayo ni kinyume cha katiba na sheria za nchi yetu kwa ajili ya kutafuta matakwa ya wanasiasa au vikundi vya kisiasa ambavyo vinatafuta kuteka nguvu na hisia za wananchi kwa matumizi yasiyo na afya kwa maendeleo ya nchi yetu. Kumbuka nchi yetu ni nchi inayoendelea hivyo changamoto zake ni nyingi mno kwa

40 hiyo kila mtu akiamua kuwa mpinzani muonyesha matatizo hakuna asiyeweza kuyaona. Lakini pia tutambue kuwa kwa wingi wa matatizo yetu hatuwezi kuyamaliza kwa mara moja hivyo basi tunaanza kushughulika na moja baada ya jingine mpaka hapo yakatakapokwisha. Kwa hiyo mtu akikujia kwa mlango wa kuonyesha tatizo ambalo halijashughulikiwa na vema akatoa mapendekezo juu ya nini alipenda kifanyike na kwa namna gani ambayo haiwezi kupelekea uvunjifu wa amani. Kama taifa tunazo changamoto mbali mbali zinazotukabili hivyo ni vema kuzijua na kujikita katika kuzikabili ili tuweze kusonga mbele katika nyanja mbali mbali. Katika harakati za kupambana na changamoto zetu tukae tukijua tunao watu tuliowachagua kama wawakilishi wetu katika kuongoza jahazi la utatuzi wa changamoto hizi. Mmojawapo wa hawa ni mheshimiwa rais ambaye anakesha usiku na mchana kuhakikisha anapunguza changamoto zetu. Hivyo katika kupambana na changamoto hizi hatutafaulu kama hatutaungana naye kwa moyo mmoja. Tungekuwa na busara kama kwa uwingi wa changamoto tulizonazo tungepunguza migongano yetu ya kisiasa isiyo na tija na kumsumbua Rais bila utaratibu ila tukapambana kwenye mambo yenye tija na si yale yatakayomchafua kitaifa na kimataifa.

41

TOFAUTI ZA KIDINI(KIIMANI) Kwenye mambo ya imani ni vema tukashindana kwa imani. Si vyema kukoseana heshima, kudharilishana au kutukanana kwa sababu ya tofauti zetu za kiimani. Kila mmoja wetu atimize haki yake ya kikatiba ya uhuru wa kuabudu pasipo kuingilia uhuru wa mwingine ili tupate ujasiri wa kusimama pamoja kusukuma mbele gurudumu la maendeleo.

TOFAUTI ZA KIKABILA Makabila yetu yatusaidie kutunza na kuenzi utamaduni wa mtanzania lakini yasiwe chanzo cha kubaguana na kutengana. Ni vyema tukaenzi na kujitahidi kuendeleza kile alichotuachia mwalimu Nyerere na marais wengine wa awamu zilizotangulia kwa kudumisha misingi ya umoja, upendo, amani na mshikamano bila kujali tofauti zetu kwa mlengo mmoja ama mwingine ili tuendelee kuwa taifa moja na lenye nguvu.

TOFAUTI ZA KIUCHUMI/ KIPATO Kutofautiana kwa vipato vyetu kusiwe sababu ya kutugawa wala kutufanya tuone kuwa wenye nacho ndiyo wamesababisha wasionacho wakose lakini tudumishe misingi ya umoja na ushirikianao bila kubaguana kwa mwenye nacho na asiyekuwa nacho. Maendeleo ni yetu sote tusiendekeze matabaka maana hayo ni sumu ya maendeleo.

42

TOFAUTI ZA MADARAKA NA VYEO Ni jambo jema kuheshimiana kila mmoja na mwingine hata kama tumetofatiana kwa vyeo. Mwenye cheo au madaraka amheshimu asiyenayo na asiye na cheo wala madaraka amheshimu mwenye nacho maana haya ni maisha inaweza kutokea mwenye cheo akakipoteza na asiye nachoakawa nacho.

TOFAUTI ZA KIELIMU Tusiendekeze makundi ya waliosoma na wasiosoma bali tujue wazi kuwa waliosoma na wasiosoma wote ni watanzania na wajibu wa elimu ni kutuondolea ujinga ili tuweze kumudu kutatua matatizo yetu na kuboresha maisha yetu. Tukilitambua hili itatusiadia kuunganga pamoja chini ya uongozi wa Rais wetu makini ili tujenge aina ya nchi tunayoitaka na tutakayoifurahia. Wenye elimu na wasio na elimu sote tunahitajiana katika kuiletea nchi yetu maendeleo.

43

SURA YA NNE MATUMAINI MAPYA

HOTUBA YA KWANZA YA RAIS MAGUFULI BUNGENI

Mhemishia Job Ndugai Spika wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhemishimiwa Dk. Akson Tulia Naibu spika, Mheshimiwa Samia Suluhu makamo wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dk. Ali Mohamed Shein Rais wa Zanzibar, Waheshimiwa marais wastafu walioko hapa, Mheshimiwa Balozi Id makamo wa pili wa Rais wa Zanziba, Mheshimiwa Waziri mkuu wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Waheshimiwa viongozi wote mliohudhuria katika bunge hili, yawezekana ikawa ni vigumu kuwataja wote loakini nataka nitamke tu kwamba itifaki imezingatiwa. Mheshimiwa spika niko hapa leo kutimiza matakwa ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ibara ya 91

44 ibara ndogo ya kwanza inayonitaka kulihutubi abunge na kulifungua rasmi bunge hili. Naomba nimshukuru mwenyezi Mungu kwa kutujalia uzima na afya njema na kutuwezesha kuwepo hapa siku ya leo. Aidha nitumie fursa hii kuwakumbuka wenzetu ambao kwa namna na nafasi mbali mbali walishiriki katika mchakato wa uchaguzi huu kwa bahati mbaya walipoteza maisha yao kabla mchakato haujamalizika. Kwa hao wote nwaliotangulia mbele ya haki ninamuomba mwenyezi Mungu azilaze roho zao na awape pumziko la amani. Mheshimiwa spika nitumie nafasi kuwapa pole pia ndugu na jamaa ambao ndugu zao walifariki na wengine kupata ulemavu katika mchakato wa uchaguzi huu. Pia natoa pongezi kwako wewe mheshimiwa spika Job Ndugai na mheshimiwa naibu spika Dk. Akson Tulia kwa kuchaguliwa kwenu kuongoza bunge la 11. Kwa kweli meshimiwa spika nakupongeza sana na uspika wako umeanza kuonekana sasa hivi. Lakini pia napenda niwapongeze waheshimiwa wabunge ambao kwa imani kubwa kwako na kwa naibu spika wameweza kuwachagua ili muweze kuongoza katika bunge hili la kumi na moja. Napenda pia mheshimiwa spika niwapongeze waheshimiwa wabunge wote wa vyama vyote waliochaguliwa kuwa wabunge wa bunge hili la 11. Aidha nitumie nafasi hii kuwapongeza wale wote waliochaguliwa katika nafasi za udiwani katika kata mbalimbali kote nchini. Natoa pongezi hizi kwa dhati kabisa kwa sababu kuu mbili; kwanza ni kwa sababu ushindani katika uchaguzi wa mwaka huu ulikuwa ni mkubwa sana kuanzia ndani ya vyama vyetu na baadaye katika uchaguzi mkuu uliohusisha na kushindanisha wagombea toka vyama tofauti lakini pia nawapongeza

45 kwa sababu wananchi wamewapa imani na ridhaa ya kuwawakilisha kaika kipindi ambacho matarajio yao kwa awamu ya tano ya uongozi wa nchi yetu ni makubwa sana. Kule kuchaguliwa kwenu waheshimiwa wabunge kunadhihirisha ni kwa namna gani wananchi wa Tanzania wa vyama vyote wanavyowaamini na kuwapenda na wana matumaini makubwa ya kwamba mtawafanyia kazi kubwa. Hongereni sana waheshimiwa wabunge. Sisi sote watatupima kwa namna tutakavyokidhi kiu na matarajio yao. Na sote tuliahidi kuwatumiakia wananchi na kutokana na utumishi wetu kwao tuweze kutatua matatizo mbalimbali na kuongoza mabadiliko makubwa ya kiutendaji, usimamizi wa matumizi wa mali ya umma na rasilimali za Taifa na ugawaji wa rasilimali hizo kwa haki. Mimi pamoja na mheshimiwa Suluhu makamo wa Rais wa Jamhuri ya Tanzania tuliwaahidi wananchi kuwa tutawatumikia na tutahakikisha kuwa katika utumishi wetu tutawajali wananchi wote bila kujali itikadi za vyama vyao lakini zaidi wanachi wa kawaida. Tunaamini na ninyi mliahidi hivyohivyo kwamba mtawatumikia watanzania wote katika kutatua matatizo yao. Na daima tukumbuke kuwa kazi zetu na mipango yetu yote tutakayoipanga na kuisimamia italenga katika kuwanufaisha watu wote. Mheshimiwa spika niwahakikishie tu wanachi kuwa mambo tuliyoyaahidi tutayatekeleza kweli kweli. Sikusudii kurejea mambo yote niliyoyaahidi katika hotuba yangu hii ya leo lakini nataka niwatoe wasiwasi kabisa wananchi wote kwamba tuliyoyahidi tumeyaahidi na ahadi ni deni. Nataka wananchi mtuamini kuwa sikutoa ahadi hii ili nipigiwe kura ya kuwa raisi bali niliwaahidi kwa lengo la kuwatumikia na kuwafanyia kazi na hicho ndicho

46 nitakachofanya. Ni imani yangu kwamba waheshimiwa wabunge pamoja na waheshimiwa madiwani pia watafanya hivyohivyo kama ambavyotumeahidi sisi. Napenda pia kutoa shukrani zangu za dhati kabisa kwa watanzania wote. Tulijiandikisha kwa wingi sana kwa ajili ya kupiga kura, tulishiriki na kufuatilia kwa karibu sana kampeni za uchaguzi na tukajitokeza kwa wingi siku ya kupiga kura kinyume na ilivyotabiriwa na wasiotutakia mema. Hakuna siku iliyokuwa ya utulivu mkubwa na amani kama siku ya tarehe 25 Oktoba tulipokwenda kupiga kura. Hata baada ya matokeo kuanza kutangazwa tulionyesha utulivu mkubwa na hata pale ambapo matokeo yalipotangazwa na yakawa sivyo baadhi yetu walivyotarajia bado tuliyapokea kwa hali ya utulivu na uungwana mkubwa. Wale waliotarajia kuwa tutafarakana wameondoka wakiwa wamefadhaika sana huku wakijiuliza, “hivi hawa ndiyo watanzania?, Ni waafrika wa namna gani” . Ndugu zangu watanzania kwa mara nyingine tena tumedhihirisha kwetu sisi wenyewe na kwa Afrika na dunia nzima kwamba sisi ni kisiwa cha amani katika bahari iliyochafuliwa. Tunayo haja ya kujipongeza na kujiwekea nadhiri kuwa tutaendelea kuidumisha hali hii na kuilinda amani ya nchi yetu. Ombi langu kwa vyama vya siasa na wanasiasa na wana siasa wa vyama vyote na viongozi wa dini kutimiza wajibu wetu wa kuilea Amani ya nchi yetu. Mheshimiwa spika napenda kuchukua nafasi hii kumpongeza mheshimiwa Zito ambaye yeye hakufanyia fujo bunge lako na yuko hapa. Hii ndiyo Tanzania ninayoitaka Tanzania ya watanzania wote. Lengo la watanzania ni kutatua matatizo yao siyo kupiga kelele na kuzomea. Lakini Mheshimiwa spika hii nilitaka kuchomeka tu kidogo lakini napenda niungane na ninyi

47 pamoja na watanzania wote kuvipongeza vyombo vyetu vya ulinzi na usalama. Na ninaposema vyombo vya ulinzi nza usalama namaanisha jeshi la wananchi wa Tanzania, jeshi la polisi, magereza, uhamiaji, usalama wa Taifa pamoja na mgambo ambao ni jeshi la akiba letu hapa Tanzania kwa jinsi walivyoshiriki katika kuhakikisha nchi yetu inaendelea kuwa salama katika kipindi chote cha uchaguzi. Nawapongeza pia tume ya uchaguzi kwa namna walivyosimamia zoezi zima la uchaguzi toka hatua ya awali ya kujiandikisha hadi siku ya kupiga kura na kutangaza matokeo, ninawapongeza sana. Wametimiza wajibu wao kwa weledi na umahiri mkubwa katika mazingira magumu na yenye changamoto nyingi. Hongereni hongereni sana Tume ya uchaguzi. Mheshimiwa spika, waheshimiwa wabunge naomba kwa namna ya pekee niwashukuru viongozi wakuu wa nchi yetu waliotangulia kwa kazi kubwa na nzuri waliyoifanya katika nchi yetu. Natambua mchango wa waasisi wa taifa letu, Mwl. Julius Nyerere na Mzee Karume kwa kujenga misingi imara ya umoja mshikamano na amani ya nchi yetu. Mzee mwinyi kwa jina lingine anaitwa mzee rukhsa, kwa kuleta mabadiliko ya kiuchumi na kisiasa na kuijenga misingi yake. Mzee Mkapa au lingine mzee wa ukweli na uwazi kwa kupanua na kuimarisha misnig ya uchumi na siasa ya nchi yetu. Na mzee Kikwete ambaye ni mzee wa maisha bora, kwa kuendeleza misingi hiyo na kupanua fursa mbalimbali kwa wananchi kujiletea maendeleo yao. Wamefanya kazi kubwa, nawashukuru sana na ninawatakia uzee mwema na maisha marefu ili tuzidi kuchuma busara zao. Mheshimiwa spika tumeingia kwenye uchaguzi wamoja, tumeshindana katika kampeni tukiwa wamoja na

48 tumemaliza uchaguzi wetu tukiwa wamoja, nataka niwahakikishie waheshimiwa wabunge na watanzania kwa ujumla kwamba serikali ya awamu ya tano itaendelea kulinda kwa nguvu na uwezo wote tunu hizi za umoja na amani. Hatutakuwa na simile kwa mtu au kikundi chochote ambacho kitataka kuvuruga umoja na amani yetu kwa misingi ya udini, kwa misingi ya rangi, kwa misingi ya ukabila, au kwa misingi ya vyama au ukanda. Mheshimiwa spika wakati wa kampeni yako maeneo yaliyojitokeza kwa kulalamikiwa sana na wananchi. Ningependa niyataje baadahi ya maeneo yaliyolalamikiwa. Maeneo hayo ambalo kubwa sana ni rushwa. Suala la rushwa limelalamikiwa sana takriban katika maeneo yote yanayowagusa wananchi. Eneo lingine lililolalamikiwa liko ndani ya TAMISEMI, Upotevu wa mapato kushindwa kukusanya kodi, ubadhirifu, matumizi mabaya ya fedha na utekelezaji wa baadhi ya miradi chini ya viwango, wizi, uzembe n.k. Eneo lingine lililolalamikiwa na wanachi wakati tukizunguka wakati tukiomba kura na ninyi ni mashahidi waheshimiwa wabunge ni ardhi kuhusu migogoro ya wakulima na wafugaji, viwanja, kuhodhi maeneo bila kuendeleza, mipango miji, kujenga maeno ya wazi n.k. Eneo lingine ni eneo la bandari rushwa, wizi, ubadhirifu na urasimu. Ninataka niyataje haya maeneo yote ili sisi wote tuondoke tukijua kwamba haya ni maeneo yanayolalamikiwa ili tukishatoka hapa tukafanye kazi kwa pamoja kutatua matatizo haya. Eneo lingine lililojitokeza kulalamikiwa sana na wananchi ni matatizo ya maji, kiwango cha chini cha upatikanaji wa maji safi na salama lakini huduma za maji kupatikana mbali na makazi n.k. Eneo lingine ni TRA; ukwepaji kodi, rushwa, ubadhirifu, urasimu na

49 upotevu wa mapato kwa kushindwa kukusanya kodi hasa kodi zinazotakiwa kulipwa na wafanyabiashara wakubwa. Eneo lingine ni TANESCO. Katika TANESCO pamekua na suala la kukatikakatika kwa umeme mara kwa mara na uwepo umeme wa mgao hilo nao limelalamikiwa na wananchi wetu. Eneo lingine ni maliasili na utalii; pamekuwa na ujangili ambao lazima idara husika inashiriki. Haiwezekani meno ya tembo makubwa kiasi hicho yakashikiwe ulaya, yamepita hapa bila wahusika wa idara yenyewe kuhusika kwa aina moja au nyingine. Lakini pia kuna migogoro ya mipaka kati ya vijiji na hifadhi na upotevu wa mapato n.k. Lakini mengine yaliyolalamikiwa na wananchi wetu ni huduma za afya kwa maana ya hospitali; huduma kuwa mbali na wahitaji, ukosefu wa madawa, hujuma kwenye vifaa vya vipimo, msongamano wa wagonjwa na tozo zisizostahili, lugha mbaya za watumishi kwa wagonjwa, uhaba wa majengo, uhaba wa vitendea kazi, rasilimali watu na fedha na kushindwa kukusanya mapato yanayowahusu n.k. Mheshimiwa spika na waheshimiwa wabunge inanibidi haya yote niyataje ili tujue tunaanzia wapi na tunaenda wapi. Nisipoyataja nitakuwa mnafiki na mimi staki niwe mnafiki kwa sababu msemakweli ni mpenzi wa Mungu. Suala lingine linalolalamikiwa ni uhamiaji na ajira; Kutoa hovyo hati za uraia, vibali vya kuishi nchini kwa wageni, kushindwa kusimamia ajira za wageni hususani kwa kazi zinazoweza kufanywa na wazawa n.k. Suala la elimu nalo limelalamikiwa kwa kuwa na uhaba wa vifaa vya kujifunzia na kufundishia, michango mingi isiyo ya lazima, malalamiko ya walimu yasiyoisha, mazingira ya kusomea ikiwa ni pamoja na majengo madawati, ukosefu wa nyumba za walimu n.k. Eneo lingine ambalo

50 limelalamikiwa, polisi; malalamiko ya wananchi kubambikwa kesi, upendeleo, madai ya askari kutotimizwa, ukosefu wa nyumba za maaskari, ukosefu wa vitendea kazi vya kisasa n.k. Hili pia linaendana na zimamoto kuchelewa kufika kwenye matukio na saa nyingine wanapofika kwenye matukio wanafika wanatakiwa wafike na maji lakini hata maji hawana na wakati wako kwenye tukio. Eneo lingine ni mizani, kucheleweshwa kwa magari yanayosafiri katika mizani yetu kwa malengo ya kupata rushwa. Mahakama, natambua jitihada za mahakama katika kushugulikia suala la mlundikano wa kesi hata hivyo bado kumekuwa na malalamiko mengi juu ya ucheleweshaji wa kesi katika mahakama zetu. Suala la madini nalo limelalamikiwa; wenyeji kutofaidika, vilio vya wachimbaji wadogo wadogo kutengewa maeneo ya uchimbaji na kupatiwa mikopo, kutolipa kodi stahiki, usumbufu wa kulipa fidia n.k. Eneo lingine ni kilimo na mifugo; uhaba wa pembejeo za mifugo na kilimo, tatizo la masoko, kukopwa mazao ya wakulima, ukosefu wa watalaam wa ugani, upungufu wa maghala, mabwawa, malambo, majosho n.k. Eneo la uvuvi napo ni vifaa duni na masoko, uvuvi haramu, uwekezaji mdogo katika sekta ya uvuvi hususani viwanda vya mazao ya uvuvi n.k na hasa katika ukanda wa bahari kwa sababu katika ukanda wa bahari ukianzia Moa kule Tanga hadi msimbati kule Mtwara kuna zaidi ya kilomita 1422 lakini katika eneo lote lile la ukanda hakuna viwanda vikubwa vya samaki ambavyo vingeweza kuzalisha uchumi katika nchi yetu. Eneo lingine ni reli; uchakavu wa miundombinu ya nchi, kutokuwepo kwa usafiri wa uhaki wa reli,upungufu wa bandari kavu, mizigo mingi kusafirishwa kwa barabara n.k. Eneo lingine

51 ni ATC. Shirika la ndege lipo, wafanyakazi wako zaidi ya 200 na wanalipwa mishahara ila ndege ni moja tu wanayohangaika nayo. Suala lingine ni katika makundi maalum; haki za wazee, walemavu, wanawake na watoto zimekuwa zikikiukwa. Lakini pia wafanyakazi, wasanii na wana michezo. Mzigo wa kodi kwa wafanyakazi, haki na maslahi yao n.k. Kero hizi ni lazima tuzishughulikie kwa nguvu zetu zote. Wizara, ofisi na taasisi husika zijipange zipasavyo kutatua kero hizi. Nimezitaja baadhi ya kero hizi ili nanyi waheshimiwa wabunge mzitambue na mshikamane na kushirikiana na serikali na wadau mbalimbali katika kuhakikisha kwamba tunazitafutia majawabu ya haraka. Lakini pamoja na kero hizo tutashughulkia pia mambo yafuatayo: Suala ambalo tutalishughulikia ni pamoja na kuimarisha muungano. Mheshimiwa spika nilipoapa kuwa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania niliapa kuulinda muungano wa nchi yetu. Hata bila kiapo mimi ni muumini wa dhati wa muugano wetu wa kipekee uliounganisha nchi mbili zilizokuwa huru za jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya watu wa Zanzibar tena kwa hiari na kwa wino wa karamu na si mtutu kama miungano mingine duniani. Naamini kwa dhati ya moyo wangu kuwa muungano wetu ndiyo umoja wetu, amani yetu na salama yetu. Ninayo kila sababu ya kulinda na kuenzi muungano wetu adhimu na adimu. Ni adhma yangu kuwaona wananchi wa Zanzibar na bara wakifurahia matunda ya muunga wetu badala ya kuwa kikwazo kwa ustawi wao na ustawi wa nchi yetu. Aidha kwa kushikirikiana na serikali ya mapinduzi ya Zanzibar na wadau wa siasa hususani vyama vya kafu na CCM tutahakikisha kuwa majaribu ya kisiasa yanayoikabili Zanzibar yanamalizika salama na

52 amani. Tunamuomba mwenyezi Mungu atujalie busara na hekima tumalize kwa utulivu na amani . Na serikali nitakayoiunda itafanya hilo lililo ndani ya uwezo wake kuendelea kuimarifa muungano wetu. Na nina faraja kubwa kuwa mheshimiwa Samia Suluhu makamo wa Rais anao uzoefu mkubwa kutokana na nafasi yake ya awali ya waziri wa nchi ofisi ya makamo wa rais anayeshughulikia muungano na pia akiwa makamo mwenyekiti a bunge la katiba. Mimi pamoja na makamu wa raisi mama Samia Suluhu na rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein tutahakikisha tunasimamia na kuimarisha muungano wetu. Suala lingine ambalo ningependa nilizungumzie hapa ni suala la kuimarisha mihimili ya serikali. Mheshimiwa spita serikali ya awamu ya tano itaheshimu na kuendeleza utamaduni mzuri uliojengeka nchini kwa kuheshimu mihimili ya dola. Tutafanya hivyo kwa kuhakikisha kuwa mihimili yetu ya bunge na Mahakama inapata fedha za kutosha kuendesha shughuli zake kwa uhuru Kupitia mfuko wa bunge na mfuko wa mahakama. Kwa upande wa bunge tutahakikisha fedha za mfuko wa maendeleo ya jimbo zinapatikana kwa wakati ili waheshimiwa wabunge mkashirikiane na wananchi wetu kusukuma maendeleo ya maeneo mnakotoka. Na kwa upande wa mahakama tutalipa uzito mkubwa suala la uboreshaji wa mahakama kwa kusogeza huduma za mahakama karibu na wananchi na kuongeza kasi ya utoaji haki na kuboresha mslahi ya watumshi wa mahakama zetu. Kuhusu suala la mchakato wa katiba. Mheshimiwa spika serikali yangu imepokea kiporo cha mchakato wa katiba ambao haukuweza kukamilika katika awamu iliyopita kutokana na kutokukamilika kwa wakati kwa zoezi la unadikishji wa wapiga kura. Napenda

53 kuwahakikisha kuwa tunatambua na kuthamini kazi kubwa ya kizalendo liliyofanya na wananchi walioshiriki hatua ya awali ya ukusanyaji wa maoni kuhusu Katiba mpya. Lakini pia tunatambua kazi nzuri ya tume ya marekebisho ya katiba na bunge la katiba lililotupatia katiba inayopendekezwa. Tutatekeleza wajibu wetu kama ulivyoainishwa katika sheria ya marekebisho ya katiba. Tunapenda mtuamini hivyo. Mheshimiwa spika kuhusu suala la uchumi na matarajio ya wananchi serikali ya awamu ya tano inaingia madarakani kukiwa na misingi imara ya kiuchumi iliyojengwa katika awamu inayomaliza muda wake ya mzee Kikwete. Uchumi wa nchi yetu umekuwa ukiimarika na kukua kwa wastani wa 7%. Katika kipindi hicho fursa mbalimbali za kiuchumi zilizoko nchini mwetu zimezidi kufunguliwa. Hii ni kutokana na jitihada zilizofanywa na serikali za awamu zilizopita za kujenga miundo mbinu ya kiuchumi kama vile barabara, uimarishaji wa bandari, uimarishaji wa reli na ukuzaji wa sekta za mawasiliano ya simu na mitandao, ukuzaji wa uongezaji wa uwezo wa watu wa kuzalisha na kusambaza umeme. Napenda kuwahakikishia kuwa tutaendeleza na kuimarisha ujenzi wa miundiombinu mipya na kuimarisha iliyopo ili kuvutia na kushawishi wawekezaji wa ndani na wa nje. Mheshimiwa spika nasema hivi kwa sababu miongoni mwa ahadi tulizoziahidi kwa watanzania ni kuendeleza ujenzi wa barabara mbalimbali za kuunganisha miji yetu mikuu ya mikoa na wilaya, barabara ziendazo kwenye maeneo muhimu ya kimkakati ya kiuchumi lakini na upanuaji wa barabara za miji kama vile Dar es salaam kwa kujenga flyover barabara za pete n.k. Uboreshaji wa barabara na njia nyingine za kiuchumi na ushafirishaji

54 kuingia na kutoka Dar es salaam ni muhimu sana kwa sababu bandari ya Dar es salaam ni lango kuu la biashara kwa nchi yetu na nchi jirani. Mheshimiwa spika katika jitihada hizo za kuboresha na kuimarisha miundombinu ya kiuchumi serikali ya awamu ya tano katika kipindi cha mika mitano ijayo itaongeza nguvu zake katika ujenzi wa reli mpya katika kiwango cha kimataifa yaani standard gauge. Reli ambazo tumekusudia zianze kujengwa ni ile ya kutoka Dar es salaa, Tabora, kigoma, hadi Mwanza. Reli ya kutoka uvinza msongati kule Burundi na isaka kigari Rwanda. Reli ya kutoka Mtwara Songea Mbambabay na matawi ya kwenda Mchuchuma hadi Liganga ambapo ni maeneo ya uzalishaji na pale tunaweza tukaboost uchumi wetu. Lakini Reli ya kutoka Kariuwa Mpanda hadi Kalema. Mheshimiwa spika nchi yetu pia imejaliwa kuwa na madini na maliasili nyingi. Ugunduzi wa gesi asilia umeongeza matumaini ya watu wetu wengi juu ya uwezo wetu wa kiuchumi katika miaka ijayo. Serikali itahakikisha kwamba madini na maliasili zetu zinatumika kwa manufaa ya taifa letu kwa kusimamia sheria na taratibu zilizopo. Aidha napenda kuipongeza kwa dhati kabisa serikali ya rais Jakaya Mrisho Kikwete na bunge la kumi ambapo mheshimiwa spika wewe ulikuwa naibu spika kwa kupitisha sheria ya usimamizi wa mapato ya mafuta na gesi yaani the oil and gas revenue management act yam waka 2015. Serikali yangu itasimamia utekelezaji wa sheria hiyo kwa uamininu na umakini mkubwa. Kuhusu suala la ujenzi wa viwanda. Mheshimiwa spika serikali ya awamu ya tano itaweka mkazo mkubwa katika ujenzi wa viwanda. Natambua kwamba sekta binafsi ndiyo muhimili mkubwa wa kujenga uchumi wa viwanda.

55

Hatuna njia nyingine kama kweli tunataka kujenga msingi wa uchumi endelevu katika nchi yetu utakaopaisha uchumi na maisha ya watu wetu. Dira ya maendeleo ya mwanaka 2020 inatutaka tuwe nchi ya watu wenye kipato cha kati. Tunaweza tukafika huko na dalili zipo lakini pia tunaweza tukafika huko kitakwimu tu wakati ukweli na uhalisia wa mambo ni tofauti. Utofauti ninaouzungumzia ni pale takwimu zitakapoonyesha kwamba sisi ni nchi ya kipato cha kati wakati mapato halisi na hali za maisha za watu wetu hazifaninani na takwimu hizo. Tamaa yangu ambayo ninaamini pia ni tamaa yenu na kwa kweli jitihada za serikali ya awamu ya tano zitakuwa katika kujenga uchumi wa kipato cha kati ambapo sura na maisha ya watanzainia walio wengi yafananefanane na nchi ya kipato cha kati. Njia moja ya kutufikisha huko ni uendelezaji wa viwanda. Ndiyo maana mheshimiwa spika tutahakikisha suala la viwanda linasimamiwa vizuri na tunafanikiwa, ndiyo lengo kubwa. Kwamba tulisimamie kwa makini na tufanikiwe. Lakini matarajio yangu ni kwamba Bunge lako tukufu litatuunga mkono mimi na serikali nitakayoiunda katika kufikia lengo hili. Mheshimiwa spika kama nilivyosema wakati wa kampeni na ninataka nirudie hapa, tutaanza na viwanda vilivyopo na kuhakikisha vinafanya kazi. Wale wote ambao walibinafsishwa viwanda vilivyokuwa vya umma kwa makubaliano kwamba wataviendeleza niliwakata wafanye hivyo mapema. Na kwa hapa nataka nisisitze wito wangu huo kwao najua huko nyuma ufuatiliaji na usimammizi wa utekelezaji wa mikataba ya namna hiyo umekuwa ukilegalega na watu wamejifanyia mambo wanavyotaka. Wako walioacha kabisa uzalishaji na kufumua hata mitambo ya uzalishaji. Mimi niliahidi na ninataka niseme

56 hapa kwa wazi kabisa kwamba wale waliobinafsishwa viwanda hivyo waanze kazi, waanze kazi mara moja. Wakishindwa basi tutatoa viwanda hivyo kwa kuzingatia sheria na taratibu za nchi na kuwapa watu wengine wenye nia ya kuviendeleza viwanda hivyo. Hatuwezi kuwa na watu wanaojiita wawekezaji tunawapa viwanda vyetu halafu wanaviatamia tu kama mayai. Mimi hilo sitalikubali na wala sitalivumilia nimeieleza ofisi ya msajili wa hazina kuanza kushughulikia suala hili mara moja na naomba bunge lako tukufu mheshimiwa spika lituunge mkono katika hili ili tuweze kwenda mbele. Tumewadekeza sana. Viko viwanda vingine wanafugia mbuzi mle na walipewa kwa ajili ya msingi kwamba watakapopewa vile viwanda waweze kuviendeleza tutengeneze ajira vijana wetu wapate ajira na tujenge uchumi wetu kwenda mbele lakini hawakufanya hivyo. Kwa hiyo ni lazima tuchukue hatua na hatua tutachukua haraka. Mheshimiwa spika njia ya pili ya kuendeleza viwanda ni kuhimiza na kushawishi wawekezaji kuwekezea katika maeneo mbalimbali ya nchi yetu. Kama nilivyoeleza miundo mbinu ya kufanya hivyo tayari ipo na baada ya muda itakuwa bora zaidi. Najua wapo watu wanaotaka kuwekeza Tanzania sasa katika viwanda na wamekuwepo hata miaka ya nyuma kidogo lakini wakati mwingine sisis humu humu tukiwemo sisi viongozi kwa kushirikiana na wafanya biashara matapeli na walaghai tumehujumu mipango ya shauku za wawekezaji wa namna hiyo. Pamoja na shauku na utayari wao wa kuwekeza Tanzania tumewawekea vikwazo na kuwapiga vita na hivyo kuwalazimisha kwenda kuwekeza katika nchi za jirani. Sisi katika serikali ya awamu ya tano tutajitahidi sana

57 kuondoa usumbufu na urasimu wa namna hiyo na kuongeza bidii ya kuwashawishi wawekezaji wa ndani na wa nje kuja kuwekeza viwanda hapa nchini. Na hili niseme kwa watendaji wa serikali ambao kwa njia moja ama nyingine watashiriki kukwamisha wawekezaji wawe wa ndani au wa nje katika kuwekeza katika nchi hii hatutakuwa na nafasi nao. Mheshimiwa Spika, waheshimiwa wabunge ni lazima sasa tujue ni viwanda vya aina gani hasa ambavyo tunavyotaka kuviwekeza. Sura ya kwanza ya viwanda tunvyokusudia ni vile ambavyo sehemu kubwa ya malighafi yake itatoka ndani husuani ni kwenye sekta za kilimo, mifugo, uvuvi na madini na maliasili nyingine. Viwanda vya aina hii tutavipa fursa ya kujenga mfumo wa uzalishaji ndani ya nchi uliofungamana na kushikamana. Viwanda vya aina hii vitahitaji na kutegemea malighafi kutoka kwa wazalishaji wa sekta nilizozitaja hapo mwanzoni na kwa kufanya hivyo wazalishaji hao watakuwa na soko la uhakika humuhumu ndani ya nchi yetu. Sura ya pili ya viwanda hivi ni kuzalisha bidhaa ambazo zinatumiwa na watu wengi humu nchini yaani mass consumption yaani bidhaa kama vile nguo, viatu, mafuta ya kupikia n.k. Ninalizungumza hili kwa sababu nikitoa mfano tu Tanzania tuna zaidi ya ng’ombe karibu milioni 22, 23 na ninafikiri tuko wa pili baada ya Ethiopia na tunashindanashindana na Sudan. Lakini hebu angalia bidhaa hata za viatu tu zinazozalishwa hapa, tunaagiza viatu kutoka nje kwenye nchi ambazo hazina ng’ombe. Tungeweza tukawa na viwanda vya ngozi, tukawa na viwanda vya viatu, viwanda vya mikanda, viwanda vya pochi, viwanda vya kofia n.k. Kwa njia hiyo tutakuwa

58 tumeongeza thamani ya mazao yetu ya mifugo lakini pia tukawa tumetengeneza ajira kwa watu wetu kwa kuwa na viwanda vya ngozi, viwanda vya viatu n.k. Kwa hiyo viwanda hivi vitakuwa na uhakika wa soko la ndani kabla ya kufikiria soko la nje. Viwanda hivi vitatarajiwa kuzalisha ziada kwa ajili ya soko la nje na yote mawili yakitokea yaani kuzalisha kwa ajili ya soko la ndani na nje itatuongezea akiba yetu ya fedha za kigeni na kutuwezesha kutekeleza na kuendeleza mipango mingine kwa ajili ya ustawi wa uchumi wetu. Sura ya tatu ya viwanda ninavyokusudia ni kuzalisha ajira nyingi. Shabaha yetu ni kuwa ifikapo mwaka 2020 idadi ya ajira itokanayo na viwanda ifikie 40% ya ajira zote zitakazokuwepo nchini wakati huo. Na hii pia ndiyo reflection ya irani yetu ya uchaguzi tuliyoinadi sisi wote wheshimiwa wabunge na wananchi kuiamini na ndiyo maana tukachaguliwa. Mheshimiwa spika nimeamua kulisema hili kwa kirefu sana kwa sababu ili tufanikiwe ni lazima tuelewane na tusaidiane kulisukuma kwa pamoja jambo hili. Suala lingine ambalo ningependa nilisisitize hapa ni suala la kilimo, mifugo na uvuvi. Mheshimiwa spika sekta nyingine ambazo lazima tutazitilia mkazo mkubwa na kuziendeleza ni kilimo, mifugo na uvuvi. Tutaziangalia sekta hizi kwa mtazamo wa kibiashara na viwanda kwa lengo la kuwa na viwanda vya kisasa vya kuongeza thamani ya mazao yatokanayo na kilimo, mifugo na uvuvi. Nchi yetu kwa kiasi kikubwa ni nchi ya kilimo, ufugaji na uvuvi hii inatokana na ukweli kwamba sehemu kubwa ya watu wetu wapatao75% wanaishi vijijini na wanategemea kilimo, ufugaji na uvuvi kwa ajili ya maisha yao. Wakulima, wafugaji na wavuvi wanatumia zana na mbinu duni katika shughuli zao na wanazalisha zaidi ya

59 asilimia 95 ya chakula chote kinacholiwa hapa nchini na kutoa mchango wa 25% kwenye pato la taifa yaani GDP na asilimia 30 ya mapato yetu ya fedha za kigeni. Kwa takwimu hizi chache ni wazi kwamaba mchango wa sekta ya kilimo, mifugo na uvuvi katika uchumi wetu na maisha yetu ni mkubwa sana, nichukue nafasi hii kuwapongeza na kuwashukuru wakulima, wafugaji na wavuvi wote wa Tanzania kwa mchango wao mkubwa katika maisha yetu na uchumi wa nchi yetu. Nataka kuahidi kwao wakulima, wafugaji na wavuvi sitawaangusha. Mheshimiwa spika pamoja na umuhimu wa kilimo, mifugo na uvuvi katika uchumi wetu wakulima, wafugaji na wavuvi wetu wengi bado ni watu maskini mapato yao yao chini na maisha ni duni. Lengo letu ni kuimarisha sekta hizi ili ziweze kutoa mchango mkubwa zaidi katika uchumi wa nchi lakini pia ziweze kuwanufaisha wakulima, wafugaji na wavuvi katika kuyabadili maisha yao. Tukiweza kuboresha sekta hizi vijana wengi zaidi watavutiwa kujiunga nazo na hivyo kupunguza tatizo la upatikanaji wa ajira. Nataka niwahakiishie wakulima, wafugaji na wavuvi wetu kwamba ahadi zetu kwao tutahakikisha zinatekelezwa. Serikali ya awamu ya tano itazisimamia kwa dhati ahadi hizo ili kuhakikisha kwamba kilimo, ufugaj na uvuvi unakuwa wa kisasa zaidi na wenye tija zaidi. Baadhi ya mambo ambayo tuliahidi kuyatekeleza ni pamoja na kuwapatia mafunzo ya kilimo, ufugaji, uvuvi wa kisasa ikiwa pamoja na ufugaji wa samaki. Lakini pia kuwapatia pembejeo wakulima wetu. Tutawapatia zana za kisasa za kilimo, ufugaji, na uvuvi. Tutawapatia wataalam wa ugani. Tutatwawezesha kupata masoko ya uhakika ya mazao yao. Tutawapatia mikopo na kwa hili benki ya kilimo itasaidia sana kufikia lengo hili. Tutaondoa ushuru

60 wa kodi na kero mbalimbali za mazao ya kilimo, mifugo na uvuvi zinazosababisha bei ya mazao hayo kuwa chini. Mfano kahawa, nilipokuwa Kagera wakulima wa kahawa na ndiyo maana wakulima wote wa Kagera wanataka kawaha yao wakaiuze Uganda. Lakini tulipouliza wana kodi zaidi ya 26 na kwa kuzingatia kuwa na kodi hizo zaidi ya 26 bei wanayopewa wakulima wa kahawa kule Kagera na maeneo mengine inakuwa ndogozaidi ukilinganisha na bei wanayopewa katika nchi ya jirani ya Uganda. Na ndiyo maana wananchi wanakuwa wanachukua hata risk hata ya kwenda kuzama kwenye maji lakini wawe wanasafirisha kahawa. Sasa ndiyo maana nasema makodi makodi haya ya hovyohovyo ambayo ni ya kero kero kwa wakulima wetu katika mazao ya kahawa, mahindi, chai, pamba, korosho, mkonge, ngozi, nyama, maziwa na samaki tutahakikisha tutayaondoa kama si kuyapunguza kwa kiasi kikubwa sana. Lakini pia tutahakikisha umiliki wa ardhi na kuwaondolea usumbufu kwa wao kutokuondolewa kwenye ardhi zao kupisha wawekezaji. Lakini tutahakikisha kwamba migogoro ya ardhi baina ya wakulima na wafugaji tunaitatua na kuikomesha kwa kuhakikisha kuwa vyanzo vya misingi vya migogoro hiyo tunaviondoa haraka. Lakini tutahakikisha kwamba tatizo la wavuvi kuvamiwavamiwa na majambazi hasa sehemu za kigoma kule na uvuvi haramu linashughulikiwa kiamilifu. Mheshimiwa spika katika tatizo la umaskini na ajira nimezungumzia umuhimu wa kuendeleza viwanda, kilimo, mifugo na uvuvi kwa sababu matatizo makubwa mawili yanayoikabili nchi yetu kwa sasa kwanza ni tatizo la umaskini na pili ni tatizo la ajira. Ni kweli uchumi wetu umekuwa ukikuwa kwa kasi ya kuridhisha lakini kasi hiyo haijawiana na kasi ya kuondoa umaskini na uzalishaji wa

61 ajira za kutosha kwa vijana wetu wanaoingia kwenye soko la ajira la kila mwaka. Mheshimiwa spika kwa mujibu wa takwimu zilizopo zaidi ya asilimia 28.2 ya watanzania ni maskini na kwamba kwa namna na kadiri uchumi wetu unavyokuwa pengo baina ya mtajiri walionacho na maskini wasionacho linazidi kukua. Tukiendelea hivi tunavyoendelea sasa hatutakuwa tunaitakia mema nchi yetu kwa sababu mgawanyiko mkubwa wa kimapato na tofauti kubwa za kimaisha baina ya matajiri na maskini ukiachwa uendelee na kuzidi kukua utachochea chuki na uhasama baina ya walionacho na wasionacho. Kwa hiyo mheshimiwa spika ni lazima tujidhatiti na kutumia akili, maarifa na nguvu zetu zote kukabiliana na kuibadilisha hali hii kwanza lazima tushughulikie umasini wa watu wetu na njia moja kama nilivyokwishaeleza ni uendelezaji wa sekta ya viwanda na uboreshaji wa sekta za kilimo, mifugo na uvuvi. Lakini tatizo la pili hilo la ajira kama nilivyokwisha kugusia ukuaji wa uchumi wetu haujaenda sambamba na kasi ya watu wanaoingia kwenye soko la ajira kila mwaka. Tatizo hili la ajira ni kwa vijana wote waliosoma viwango mbalimbali vya elimu na wasio na ujuzi, hii ina maana kwamba sekta zinazochangia kukua kwa uchumi wa nchi yetu sizo zinazozalisha ajra kwa wingi ndiyo maana kuweka msisitizo kwenye sekta ya viwanda hasa vile vinavyoajiri watu wengi na sekta ya kilimo, uvuvi na mifugo ambavyo ndivyo mwajiri mkubwa hivi sasa. Mheshimiwa spika pamoja na kuweka msisitizo katika viwanda, kilimo, mifugo na uvuvi hatuna budi kuwezesha vijana wetu kuanzisha shughuli mbalimbali za uzalishaji kwa viwango mbalimbali. Ili hili liwezekane na sisi tutalifanya linahitaji mambo mawili makubwa, kwanza

62 kuandaa vijana wetu vizuri kielimu na kiujuzi. Hatuna budi kuweka mkazo katika viwango vya ubora vya elimu na stadi za kazi wanazopata vijana wetu. Nalisema hili kwa sababu hatuwezi kuzungumzia uendelezaji wa viwanda ikiwa hatujaandaa vijana wenye uwezo na ujuzi na stadi za ufanya kazi hizo kwa ubora na ufanisi wa hali ya juu. Hatuwezi kutaka kuwekeza katika viwanda vya nguo au samani ikiwa hatuna wahandisi wa mitambo wazuri, wabunifu wazuri na wenye viwango vinavyotakiwa kukabiliana na tatizo hilo. Aidha hatuwezi kuwa na vijana wenye uthubutu wa kuanzisha shughuli za uzalishaji kama hawana elimu na maarifa ya kubuni miradi na kuiendeleza. Kwa hiyo tutaelekeza nguvu zetu katika kuhakikisha kuwa shule na vyuo vyetu katika ngazi mbalimbali vinafundisha na kutoa vijana wenye viwango vya hali ya juu vya elimu, maarifa, ujuzi na ufundi. Mheshimiwa Spika pili ni suala la wawezeshaji vijana hasa wale watakaotaka kujiajiri. Katika kutekeleza lengo hili serikali ya awamu ya tano itachukua na kutekeleza hatua mbalimbali ikiwemo kuwawezesha vijana wanaohitimu elimu ya juu na vyuo vya ufundi kupata mitaji ya kuwasidia kuanzisha makampuni yao kulingana na fani walizozisomea. Lakini pia tutawawezesha vijana kuanzisha SACOSS zao na kupiti aSACOSS hizo kuwawezesha kupata mikopo. Lakini pia kuwawezesha vijana wajisiliamali kujiunga na mifuko ya hifadhi ya jamii ili waweze kupata mikopo na kunufaika na mafao mengine katika mifuko hiyo. Mheshimiwa spika tatu ni kuzitambua na kuziheshimu kazi na shughuli mbalimbali zinazofanywa na makundi mbalimbali ya kina mama na vijana. Hapa namanisha shughuli za kina Mama lishe, wachuuzi mbalimbali, machinga, waendesha bodaboda,

63 waendesha maguta na vijana wa kike na wa kiume wanaojitafutia kazi mbalimbali halali za kujipatia mapato kwa ajili ya kuendeshamaisha yao. Shughuli za makundi haya zinatusaidia sana katika kupunguza makundi ya vijana wetu ambao wangekaa tu na kuzururazurura hovyo bila shughuli za kufanya. Na kwa kuwa kwa sasa uwezo wetu wa kuwapatia ajira tofauti ni mdogo ni jukumu letu kuwasidai na kuwawezesha kufanya shughuli zao kwa ulivu bila bugudha. Niliahidi na na ninataka niahidi na nirudie hapa kwamba serikali ya awamu ya tano ikishirkiana na halmashauri zetu, wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya itaweka mipango na taratibu nzuri na rafiki kwa aina ya shughuli ambazo baadhi nimezigusia . Aidha ushuru usiyo wa lazima na wenye usumbufu kwa wafanyabiashara wadogowadogo utokananao na shughuli nilizozitaja hapo tutaziondoa. Ninaamini ikiwa tutaweza kuongeza ukusanyaji wa mapato na kuziba mianya ya wakwepaji wakubwa wa kodi ambao huipotezea serikali mamilini na mabilioni ya fedha tutakuwa hatuna sababu ya kufukuzana na akina mama ntilie na vijana mitaani katika kukusanya kodi. Kodi ambazo hatuzikusanyi ni nyingi ambazo zingeweza zikaendesha uchumi wa nchi hii badala ya kukaa na kusumbuana na wanyonge ambao wanajitafutia riziki yao kwa ajili ya kuishi. Kwa hiyo niwatake viongozi wateuliwa waliochini ya mamalaka yangu wakalisimamie hili badala ya kuwanyanyasa wananchi wa hali ya chini wanaojitafutia maisha yao. Na ikiwezekana waweze kuandaa maeneo maalum kwa ajili ya kufanya boiashara, hata ulaya wanafanya hivyo badala ya kila mahali mtu anapokwenda ni kufukuzwa na hata wakichukua chakula

64 wanakila wao kwa hiyo haya hatuwezi kuyaacha yakaendelea kufanyia hivyo. Kuhusu suala la afya mheshimiwa spika dhamira ya kujenga uchumi wa kisasa na sula la kupambana na umaskini inakwenda sambamba na sula la kuwa na wananchi wenye afya bora. Kwa kutambua ukweli huu na mahitaji ya huduma bora za wananchi wetu serikali ya wamu ya tano itahakikisha wanachi wanapata huduma bora za afya kwa kufanya baadhi ya mambo yafuatayo. Kwanza ni kuimrisha huduma za afya kwa pale zilipo na kuanzisha pale amabpo hazipo. Lengo ni kuhakikisha kuwa kila kijiji kinakuwa na zahanati, kila kata inakuwa na kituo cha afya, kila wilaya inakua na hospitali na kila mkoa unakuwa na hospitali ya rufaa. Lakini pili tutaimarisha na kuboresha huduma za afya kwa kuongeza utaalam katika Nyanja za afya kwa kuwapatia mafunzo watumishi wake ndani na nje ya nchi na kwa kuzipatia vigfaa bora na vya kisasa hospitali, vituo vya afya na zahanati zetu. Lengo la kufanya hivyo ni kuwezesha upatikanaji wa huduma mahususi hapahapa nchini na hivyo kutolazimika kupeleka watu wetu kutibiwa nje ya nchi. Kwa sababu imekuwa ni kawaida kila mtu akiumwa hata mafua ni kwenda nje wakati kumbe wangeweza kutibiwa hapa vizuri na wakapona na tukasevu hela zitatumika kutengeneza mambo mengine ya faida ya nchi yetu. Lakini tatu tutaongeza bajeti ya dawa na kuboresha mfumo wa upatikanaji. Ili kuhakikisha dawa zinapatikana katika hospitali, vituo vya afya na zahanati zetu, aidha tutahamasisha wanachi wajiunge na bima ya afya. Kuhusu suala la elimu, mheshimiwa spika natambua juhudi kubwa zimetumika katika upanuzi wa elimu ya

65 awali, msingi, sekondari na vyuo vikuu. Serikali ya awamu ya tano itajielekeza katika kuongeza ubora wa elimu inayotolewa ikiwa ni pamoja na kuongeza mkazo katika masomo ya sayansi. Aidha tutahakikisha kwamba vifaa vya kufundishia na kujifunzia vinapatikana ikiwa ni pamoja na maabara, vitabu, madawati n.k. Tutahakikisha kuanzia Januari mwakani elimu kuanzia darasa la kwanza hadi kidato cha nne inatolewa bure. Na ninaposema bure maana yake nina maana ya bure wahusika wasije wakatumia suala la kusema bure halafu waanze kutengeneza mamichango ya ajabu ajabu ya kuwatoza wanafunzi wale. Ni lazima tuanzie mahali kwamba tunaposema bure maana yake ni bure kweli. Lakini kama tulivyoahidi kwenye kampeni tutahakikisha kwamba wanafunzi wengi zaidi wa elimu ya juu wanapata mikopo kwa wakati. Tutashughulikia maslahi na kero za walimu wa ngazi zote ikiwa ni pamoja na kujenga nyumba za walimu vijini na kuiunga mkono benki ya walimu ili iweze kuwanufaisha zaidi. Kuhusu suala la maji, mheshimiwa spika wakati wa kampeni nimekutana na malalako mengi sana ya ukosefu wa maji. Serikali ya wamu ya tano itahakiisha inaongeza kiwango cha upatikanaji wa maji kufikia asilimia 85 kwa maeneo ya vijijini na 95 katika maeneo ya mijini ifiikapo mwaka 2020. Tutakamilisha miradi iliyokwishaanza na kuanzisha miradi mipya mikubwa na midogo ya maji kutoka katika mito, maziwa, vyanzo vingine mbalimbali ambavyovitakuwa vya uhakika vya maji ikiwa ni pamoja na kuvuna maji ya mvua. Tunatakana tuwatue akina mama ndoo kichwani. Tunatambua umaskini hauwezi kuondoka nchini kama wananchi hawapati maji safi na salama.

66

Suala lingine mheshimiwa spika ni suala la umeme. Mheshimiwa suala la upatikanaji wa umeme limeendelea kuwa tatizo katika nchi yetu pamoja na jitihada kubwa zilizofanywa na serikali zilizopita. Hatuwezi kuzungumzia suala la kujenga viwanda wakati umeme hautoshi. Serikali yangu itahakikisha kwamba umeme unapatikana wa kutosha na wa uhakika. Tutakamilisha miradi ya umeme iliyopo na kujenga mingine mingi mipya ili wananchi wengi zaidi wanufaike na nishati ya umeme na viwanda vingi zaidi vidogo, vikubwa na vya kati viweze kupata umeme. Lakini na hujuma zile ndogongogo zinazofanywa a atendaji wa sekta ya umeme. Kwa mfano wakati mvua zinaponyesha halafu watu wanalipwa hela kwa mfano pale Mtera wanayafungulia maji usiku halafu levo yake haifiki kwa wakati kila siku kunakuwa na maji hayatoshi hizi tutazisimamia kikamilifu. Kwa sababu pamekuwa na mtindo huo, watu wanapokata kusaplai majenereta yao au kununua mafuta ya bei ya juu wanalipwa wale wanaohusika pale Mtera kwenye maji wanayafungulia maji usiku yanamwagiki kwa hiyo levo inayotakiwa haifikiwi kwa hiyo kila siku levo ya maji ile inakuwa haifiki. Tutadili nao na mimi ninawaambia nitadili nao kwelikweli. Kuhusu suala la madawa ya kulevya. Mheshimiwa Spika madawa ya kulevya yamekuwa ni janga kubwa kwa taifa letu na kundi linaloathirika zaidi ni vijana wa kiume na wa kike familia nyingi zimeathirika na nguvu kazi ya taifa imepotea. Tutashughulika mtandao huo unaojihusisha na mtandao huo bila ajizi. Tutawatafuta wale wakubwa wanaohusika na madawa ya kulevya badala ya kuhangaika na dagaa. Na ninaposema nasema kweli

67 naomba bunge mnisaidie na Mungu anilinde na mwendelee kuniombea. Mheshimiwa spika masuala mengine tunayoyawekea mkazo katika utawala wa awamu ya tano ambayo ninaamini yatasiadia katika kujenga uchumi wetu ni opamoja masuala ya utalii, mawasiliano, madini, ardhi makazi, ujenzi, miundo mbinu, bandari, barabara, utunzani wa mazingira, vijana, wanawake, watu wenye ulemavu, wazee, wafanyakazi, wasanii, wanamichezo, wanahabari, wafanyabiashara, wawekezaji, wajasiriamali, sekta binafsi n.k. ni vigumu kutaja wote wahusika tutakayoshughulika nayo katika kujenga uchumi wetu. Utekelezaji wa masuala haya umefafanuliwa vizuri katika irani ya CCM yam waka 2015. Mapambano dhidi ya rushwa na ufisadi. Mheshimiwa spika, Jambo moja nililolisemea kwa nguvu kubwa wakati wa kampeni ni mapambano dhidi ya rushwa na ufisadi. Sikufanya hivyo kwa sababu nilitaka tu kuwarubuni wananchi ili wanipe kura zao na kunifanya kuwa rais wao. Niliongea jambo hili kwa dhati kabisa na nilichokisema na kuahidi wananchi ndicho hasa nilichokusudia. Mheshimiwa spika wananchi wanachukia sana rushwa na ufisadi na wamechoshwa wamechoshwa sana na vitendo hivyo. Mimi pia nachukia rushwa na ufisadi. Sifurahishwi kabisa na vitendo vya rushwa na ufisadi vinavyoendelea hapa nchini. Vitendo vya rushwa na ufisadi vinawanyima haki wananchi na kuitia hasara serikali kwa mabilioni ya fedha ambazo zingeweza kutumika kwa ajili ya kujenga miradi ya maendeleo kwa ajili ya watu wetu.Mheshimiwa spika chama changu cha Mapinduzi kimejengwa katika misingi ya kukataa rushwa na ufisadi. Ndiyo maana moja

68 ya imani kuu za CCM ni ile inayosema rushwa ni adui wa haki sitatoa rushwa wala kupokea rushwa. Ingawaje sina uhkika sana kama sasa hivi ndani ya chama chetu hawapokei na kutoa rushwa. Kwa mtanzania mwaminifu kwa imani yake hatakuwa na kigugumizi katika kuwa mstari wa mbele katika kupambana na rushwa na ufisadi. Mheshimiwa spika mmoja wa waasisi wa Taifa letu aliwahi kuifananisha rushwa na ufisadi kama adui mkubwa wa watu akiongea bungeni mwezi Mei 1960 mwalimu Nyerere alisema yafuatayo na ninaomba kunukuu, “rushwa na ufisadi havina budi kushughulikiwa bila huruma kwa sababu naamini wakati wa amani rushwa na ufisadi ni adui mkubwa kwa ustawi wa watu kuliko vita ”. Mheshimiwa Spika haya ni maneno makali ya mtu na kiongozi aliyechukia na kuikeme rushwa katika maisha yake yote ya uongozi. Ni maneno yanayotukumbusha tu nini kinaweza kikatutokea kama taifa endapo tutaendeleza rushwa na ufisadi. Chuki ya wanachi dhidi ya rushwa na ufisadi ni dhahiri .wamechoka kabisa, wamechoka sana, hawakao tayari kuvumilia upuuzi wa serikali inayoonea haya rushwa na kulea mafisadi. Mheshimiwa spika mimi nimewaahidi wananchi na ninataka nirejee ahadi yangu kwao mbele ya bunge hili tukufu kwamba nitapambana na rushwa na ufisadi bila kigugumizi na bila haya yoyote. Dawa ya jipu ni kulitumbua na mimi nimejipa kazi ya kuwa mtumbua jipu. Nimejipa kazi ya kuwa mtumbua jipu. Najua kutumua jipu kuna maumivu lakini babati mbaya halina dawa nyingine hivyo ninawaomba waheshimiwa wabunge na watanzania wote kwanza mniombee na mniunge mkono wakati ninapotumbua majipu haya. Mheshimiwa spika makofi haya yanaashiria kwamba mtaniunga mkono

69 wakati nikitumbua majipu. Mheshimiwa spika nafahamu ugumu wa vita niliyoamua kuipigana. Nasema nafahamu ugumu na changamoto zake kwa sababu wanaojihushisha na rushwa si watu wadogowadogo. Vitendo vya rushwa na ufisadi vyenye madhara makubwa kwa nchi na ustawi wa nchi yetu hutendwa na watu wenye dhamana kubwa za uongozi na utumishi ambazo wamezipata kutokana na ridhaa ya watu. Kwa hivyo ili niweze kufanikiwa lazima nipate ushirikiano mkubwa toka kwa bunge lako tukufu na vyombo vingine vilivyopo na vyenye majukumu ya kupambana na vitendo hivi vya rushwa. Aidha tutashinda vita hii endapo wananchi pia watatuunga mkono. Lakini sina mashaka kuwa kwa vile wao wananchi kwa wingi wao wanachukia rushwa na ufisadi watakuwa tayari kutoa ushirikiano wao katika mapambano haya dhidi ya rushwa na ufisadi. Hivyo mheshimiwa spika katika kushughulikia tatizo hili hili nimeahidi kuunda mahakama ya rushwa na ufisadi. Ni matumaini yangu vyombo husika katika jambo hili havitanikwamisha. Aidha nataka niahidi mbele ya bunge lako tukufu kwamba kiongozi yoyote wa kuteuliwa ambaye mimi nitakuwa nimemteua kwa mamlaka niliyonayo kikatiba na ninayo mamlaka ya kumwajibisha pindi tu nikibaini na kujiridhisha kuwa anajihusihsa na vitendo vya rushwa pamoja na ufisadi nitamtimua mara moja wala sitakuwa na kigugumizi. Na baada ya mimi kuchukua hatua hizo za kumtia hatua na taratibu zingine za kisheria zitafuata. Nataka twende mbele ili watanzania wote hasa watanzania wa maisha ya chini waweze kufaidika na matunda ya nchi yao Tanzania. Tanzania ni tajiri, Tanzani ina kila kitu, tukisimama imara kwa pamoja na tukamtanguliza Mungu mbele tutafanikiwa kwa kuwa na

70 maisha mazuri. Mheshimiwa spika ninachotaka kusema hapa ni kwamba serikali yangu itafuatilia kwa karibu mienendo ya viongozi na watendaji wake ili kubaini kwa haraka nani anajihushisha na vitendo vya rushwa na ufisadi na tukijiridhisha hatutasubiri tutachukua hatua. na imani yangu wengine pia katika ngazi mbalimbali mtafanya hivyo. Bila kufanya hivyo rushwa na ufisadi vitazoeleka na kuwa wimbo unaoburudisha badala ya kuwa wimbo unaoudhi na kukera. Mheshimiwa spika Kuhusu suala la muundo wa serikali na utumishi. Nilipokuwa nazunguka na kuzungumza na wananchi wakati wa kampeni za uchaguzi niliahidi nitaunda serikali ndogo ya wachapakazi. Aidha niliahidi pia kuunda serikali ambayo itawatumikia watu na hasa wanachi wa kawaida. Serikali nitakayoiunda nataka iwe inwahudumia wananchi kwa haraka na siyo kuwasumbuasumbua na kuwazungusha. Natoa rai kwa watumishi wa serikali hasa ambao ni wazembe na wazivu wajiandae. Tumewavumilia kwa muda mrefu nafikiri wakati wa kuvumiliana sasa umekwisha. Wametuchezea vya kutosha wakati kwa kutuchezea sasa umekwisha. Wametuchakachua vya kutosha wakati wa kutuchakachua sasa umekwisha. Kwa sababu watumishi wa aina hiyo hawatavumiliwa katika serikali nitakayoiongoza. Lugha za hiyo ni changamoto, tutashughulikia, tuko kwenye mchakato, tunaendelea hazitavumiliwa katika serikali ya awamu ya tano. Mimi nataka watu iwe kazi tu. Hatuwezi kulea watu ambao wanalipwa mishahala lakini hawafanyi kazi wanazotakiwa kufanya au wamegeuza ofisi za umma kuwa ni mahali pa kuchuma bila kufanya kazi. Mheshimiwa spika pamoja na kuwataka watumishi wa serikali kufanya kazi hatuna budi kuyaangalia na

71 kuboresha mishahara na maslahi yao pamoja na mazingira yao ya kufanyia kazi kwa kuwapatia vitendeakazi bora na vya kisasa. Na jambo moja tutakalolitekeleza ni kuangalia namna ya kupunguza kodi ya mapato katika mishahara ya wafanyakazi yaani PAYEE. Pia tutajitahidi kuwatambua na kuwapa motisha wafanyakazi wachapakazi ili hii iact kama motivating agent. Lakini pia kadiri uchumi utakavyokuwaunaendelea tuaangalia namna ya kuboresha maslahi yao. Kwa sababu na kila afanyaey kazi hana budi kulipwa mshahara mzuri. Kuhusu suala la kuongeza mapato na kupunguza matumizi. Mheshimiwa spika kwa zaidi ya miaka mitatu sasa ukusanyaji wa mapato umekuwa chini ya makadirio kwa sababu mbalimbali. Serikali ya awamu ya tano itaongeza nguvu katika upanuzi wa wigo wa kodi na kuongeza ufanisi katika ukusanyaji wa mapato. Tutahakikisha kwamba kila mtu anayestahili kulipa kodi analipa kodi stahiki. Hatutasita kumchukilia hatua mtu yeyote atakayekwepa kulipa kodi. Tunawaomba wananchi mhakikishe mnapewa risti kila mnaponunua bidhaa au huduma. Kodi ni kitu muhimu na kimetajwa hata katika vitabu. Kwa hiyo ni lazima tulipe kodi. Na ndiyo maana nasisitiza mtu unaponunua bidhaa yoyote lazima upewe risti. Lakini pia tutahakikisha kwamba Kila senti inayoongezeka katika mapato ya serikali inaelekezwa katika kutoa huduma bora zaidi kwa wananchi. Tutajitahidi kuziba mianya ya upotevu wa fedha za serikali ambayo inaipunguzia serikali uwezo wake wa kuwahudumia wananchi. Mheshimiwa Spika nitataja baadhi tu ya maeneo ambayo tutayasimamia kwa lengo la kupunguza matumizi yasiyo ya lazima na kuziba mianya ya ufujaji wa fedha za

72 serikali. Kwanza ni safari zote zisizo za lazima nje ya nchi tutazidhibiti na tumekwishaanza. Badala yake tutawatumia mabalozi wetu kutuwakilisha kwenye mikutano ya aina hiyo na pale inapolazimu kiongozi au mtumishi mwandamizi kusafiri tutahakikisha kwamba haandamani na msululu wa watu wengi ambao hawana umhumi wala shughuli za kufanya katika safari hizo. Katika kusisitiza hili napenda niwape takwimu za fedha zilizotumika ndani ya serikali na mashirika ya umma na taasisi nyingne za serikali kati ya mwaka 2013/14 na 2014/15. Jumla ya shilingi bilioni 356.324 zilitumika kwa ajili ya safari za nje kama ifuatavyo: Tiketi za ndege zilitumika shilingi bilioni 183.16. Mafunzo ya nje ya nchi zilitumika shilingi bilioni 68.612. Posho za kujikimu PER DM zilitumika shilingi biloni 104.552. Wizara na taasisi zilizoongoza kwa matumizi ya safari za nje ni pamoja na Bunge, wizara ya mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa, wizara ya fedha, ofisi ya waziri mkuu, ofisi ya taifa ukaguzi wa hesabu za serikali NAOT, wizara ya mambo ya ndani n.k. Hizi fedha zingeweza kutumika vizuri kuboresha huduma za maisha ya wanachi wa hali ya chini kama afya, maji, elimu n.k. Fedha nilizozitaja hapa kwa mfano fedha hizi zingetosha kutengeneza barabara ya kilomita 400 ya lami. Kwa hiyo mheshimiwa Serukamba na barabara yake ya kigoma ile ambayo in kilomita 200 tu zimebaki ingekuwa ni lami na ukaenda mpaka Uvinza ingekuwa ni lami tungekuwa tunaelekea Mpanda. Lakini zimetumika kwa safari za nje. Lakini tujiulize zingeweza kutengeneza zahananti ngapi, zingeweza kutengeneza nyumba za walimu ngapi, zingeweza kutengeneza madawati mangapi, zingeweza kununua madawa hospitalini tani ngapi n.k. hivyo tunapodhibiti safari za nje

73 tunawaomba waheshimiwa wabunge kwa heshima kubwa sana na watanzania wote mtuelewe na mtuunge mkono. Pili tutahakikisha tunadhibiti safari na ziara za mafunzo nje ya nchi zinazogharamiwa na serikali ambazo yangeweza kupatikana hapa nchini. Unaweza ukawa na utaratibu mzuri tu badala ya kutuma kikundi cha watu kwenda kufundishwa kule mleteni huyo mwalimu anayewafundisha aje awafundishie hapa. Mmlipe mtu moja badala ya kulipa grupu la watu kwenda kufundishiwa huko. Lakini cha ajabu siku hizi kinachofanyika hata bodi badala ya kukaa bodi Tanzania kujadili mambo yao wanakwenda Ulaya kwenda kukaa bodi, board meeting. Ni mambo ya ajabu ya aibu. Na ndiyo maana ndugu zangu waheshimiwa wabunge napenda mnielewe na lazima niliseme nisipolisema nitakuwa mnafiki na mimi sitaki niwe mnafiki kwani msema kweli ni mpenzi wa Mungu. Sisi wote hapa tuliopo hapa tumewaahidi watanzania wa maisha ya chini kule tulikotoka tuwatekelezee yale wanayoyahitaji. Nyinyi wote waheshimiwa wabunge ni mashahidi mmeona shida za wananchi wetu huko vijijini. Wana shida kweli kweli na sisi wote hapa tumeahidi kwamba tutatatua shida zao. Hatuwezi tukazitatua shida hizo kwa mtindo huu wa kusafirisafiri na kuwa na matumizi ya hovyohovyo ndani ya serikali, taasisi na vitu vingine. Kwa hiyo ninapoyasema haya ninayasema kwa uchungu mkubwa. Kwamba tuna wajibu wa kufanya haya ili Tanzania yetu ineemeke, ili Tanzania yetu inde mbele, ili wananchi wetu waweze kufaidika, ili wananchi wetu tuwaondolee kero za ajabu ambazo zimekuwa zinawatesa katika maisha yao. Wapo watu yaani kwao kusafiri nje ameshasafiri zaidi nje

74 kuliko hata kwenda kwao kumsalimu baba yake na mama yake. Tatu Tutadhibiti warsha semina, makongamano na matamasha ambayo kwakweli yanatumia fedha nyingi tu za serikali lakini hayana tija na wala hayaongezi ufanisi katika utekelezaji na usimamizi wa sera na mipango ya serikali. Siku hizi kwenye mawizara wakitaka kukutana mahali lazima watafute hotel wakati wizarani kuna ukumbi. Wangeweza hata wakatukatima kwenye miti wakazungumza yale ambayo wanataka kuyazungumza. Lakini pia Tutasimiamia kwa ukamilifu sheria za manunuzi ya umma ili kuhakikisha kwamba mianya yote ya upotevu wa fedha za umma unaotokana na sheria ya manunuzi tunaiziba. Hii sheria ya manunuzi ni mdudu mwingine mbaya mbaya mbaya sana. Unaweza ukakuta nyumba ambayo ingeweza ikajengwa kwa milioni 30 kwa sheria ya manunuzi itajengwa kwa milioni 200. Maofisa wetu masurufu wanaokaa kwenye mawizara unaweza ukakuta karamu ya biki inayonunuliwa kwa shilingi elfu moja imenunuliwa shilingi elfu kumi. Sheria hii imekuwa ni mbaya kwa matumizi ndani ya serikali lakini katika meneo mbalimbali. Nina uhakika waheshimiwa wabunge pakiletwa mswaada wa kubadilisha hii sheria nina uhakika hamtachelewa kuupitisha. Mheshimiwa spika tano tutasimamia na kudhibiti ukiukwaji wa maagizo na maelekezo mbalimbali yaliyokwishatolewa na serikali siku za nyuma kuhusu ununuzi wa bidhaa kama samani kwa ajili ya matumizi ya serikali. Samani zote kwa ajili ya matumizi ya serikali zinatakiwa ziwe zilezile zinazozalishwa hapahapa nchini. Serikli ya awamu ya tano itasimamia kwa karibu na

75 kudhibiti ununuzi wa magari ya gharama kwa ajili ya viongozi na watumishi waandamizi wa serikali. Kwa sababu unakuta mtu ni Engineer unatakatiwa kwenda kukagua barababara badala ya kuwa na pikapu unataka kununua V8. Sasa ni lazima tubadilishe huo mwenendo. Saba, tutandelea kuchunguza na kudhibiti matumizi ya serikali na taasisi zake zote yasiyo na tija kwa uchumi wa taifa letu. Mheshimiwa spika mambo ni mengi lakini kwa ajili hiyo vipaumbele vya serikali ninayotarajia kuiunda vitakuwa kupunguza urasimu ili kuongeza kasi ya utekelezaji wa maamuzi na miradi ya serikali, kubana matumizi kwa kupunguza yale ambayo kutokana na hali yetu ya uchumi kwa sasa yanaweza kuepukika na kurejesha nidhamu ya serikali na utumishi wa umma kwa kuongeza uwazi na uwajibikaji. Tutatekeleza vipaumbele hivyo kwa kufanya pamoja na mambo mengine kupunguza ukubwa wa baraza la mawaziri, kuongeza usimamizi katika ukusanyaji wa mapato ya kodi na maduhuli ya serikali kwa kuziba mianya ya ukwepaji kodi na tutahakikisha kwamba wale wote wanaotakiwa kulipa kodi wanalipa ipasavyo. Tutaongeza nidhamu ya matumizi ya serikali ili kuhakikisha fedha zinazookolewa zinakwenda kwenye miradi ya maendeleo na kusimamia sheria, kanuni na taratibu za uwajibikaji kwa viongozi na watumishi wa umma ili wawajibike kwa wananchi ambao ndiyo wateja na waajiri wao wakuu wa utumishi wa umma. Serikali ya awamu ya tano itaendelea kubainisha maeneo mengine ya matumizi yasiyo ya lazima ambayo yanaigharimu serikali fedha nyingi na kuyadhibiti. Aidha nitoe wito kwa watanzinia wote kila moja wetu afanye kazi. Awe

76 shambani, ofisini, kiwandani, sokoni, kwenye bustani n.k. badala ya tabia ya sasa iliyojengeka ya watanzania kutokupenda kufanya kazi na hivyo kupoteza muda mwingi vijiweni. Muda ambao ungetumika kufanya kazi. Na ndiyo maana kauli mbiu yangu ni, “hapa kazi tu”. Mheshimiwa spika kuhusu masuala ya mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa nchi yetu imepata mafanikio makubwa katika nyanja za dipromasia na ushirikiano wa kimataifa katika awamu zilizotangulia za uongozi. Serikali yangu itaendeleza sifa hiyo kwa kujenga juu ya msingi imara uliowekwa na zilizotangulia hasa awamu ya nne chini ya mheshimiwa Dk. Jakaya Mrisho Kikwete. Tutaendelea kuwa waumini na tuaendeleza sera ya ujirani mwema na nchi zinazotuzunguka kwa lengo la ustawi wa watu wetu na maslahi mapana ya nchi yetu. Tutaendelea kuwa waaminifu wa utangamano wa jumuiya ya Afrika mashariki na daima tutatekeleza wajibu wetu kwa mujibu wa mkataba wa uanzishwaji wa jumuiya ya Afrika mashariki itifaki zake na maamuzi ya vikao vya nchi wanachama tutaendelea kuyatekeleza matakwa na mkataba huu kwa kujenga utangamano wetu hatua kwa hatua. Mheshimiwa spika Tanzania itaendelea kuwa mwanachama mwaminifu wa jumuiya ya maendeleo ya kusini mwa Afrika SADC na kuendelea kushirikiana kwa karibu na nchi wanachama ambao tuna uhusiano nao wa kihistoria na kindugu. Lakini pia tutaendelea kuamini katika umoja wa Afrika na azma ya ndoto ya waasisi wetu ya kuunganisha bara la Afrika. Tutaendelea pia kushiriki kikamilifu katika Jumuiya ya nchi za Maziwa makuu ICGLR na kushirikiana na nchi wanachama wenzetu kutafuta majawabu ya kudumu ya amani usalama na maendeleo katika maeneo ya maziwa makuu.

77

Tutaendeleza na kustawisha mahusiano na marafiki zetu wote magharibi, mashariki ya kati kwa lengo la kushirikiana na maslahi ya nchi yetu kwa watu wetu. Tutapenda kutumia fursa nzuri za mahusiano yetu mazuri kisiasa kukuza mahusiano yetu ya uchumi kwa kutumia dipromasia yetu ya uchumi. Tutafanya hivyo pia kwa uhusiano wa mataifa kwa kuendeleza mahusiano yetu na Umoja wa mataifa na taasisi zake, jumuiya ya madora, benki ya dunia, shrika la fedha duniani, benki ya maendeleo ya Afrika n.k. Aidha tutazitaka balozi zetu zionyeshe matunda yanayolingana na thamani ya fedha tunazowapelekea hususani katika kkuvutia uwekezaji, biashara, utalii, mchango wao katika ukuzaji wa sekta ya viwanda n.k. Tunataka kuona dipromasia yetu na sera yetu ya nje ikijibu changamoto zetu za ndani za ajira, miundombinu, masoko ya mazao ya wakulima, viwanda n.k. Mheshimiwa spika, waheshimiwa wabunge naomba basi kabla ya kuhitimisha nitoe wito kwa waheshimiwa wabunge na bunge hili ambalo najua lina historia ya kuweka hisitoria ya kuwa kitu kimoja na kuweka maslahi ya taifa mbele. Kama kuna kitu ambacho wananchi wanachukia ni lugha za vijembe, mipasho, ushabiki wa vyama bungeni, kwanza tukumbuke wote bila kujali itikadi za vyama vyetu sisi ni kitu kimoja. Na pili tumechanguliwa kuwawakilisha wenzetu baada ya miaka mitano kila mmoja atarudi kwenye jimbo lake kuomba kura na huko atapimwa kwa maendeleo aliyoyapeleka. Ningewaomba tusimame pamoja, Tanzania ni yetu sote, tutangulize maslahi ya nchi mbele. Na kwa mara ya kwanza watanzania waone bunge tofauti na siyo bunge la kuzomea, kutoka nje kutukanana na mipasho n.k. ndiyo

78 maana kwa dhati kabisa nimempongeza mheshimiwa Zitto. Mhe. Zito umekomaa ninajua hata kwenu kule Kigoma wamekuchagua wana CCM. Ni lazima sasa tujenge dhana ya kutanguliza maslahi ya watanzania tunaowaongoza badala ya maslahi ya kuzomea yanaaibisha bunge hili. Bunge ni chombo muhimu sana katika mihimili ya taifa letu. Tunaitwa waheshimiwa wabunge kwa heshima ya dhamana tuliyopewa na bunge hili tukufu. Tutunze heshima hiyo ili tuzidi kuheshimiwa. Aidha napenda kusisitiza kuwa kazi iliyoko mbele yetu ni kubwa matarajio na matumaini ya watanzania waliotuchagua na kutupa ridhaa ya kuwaongoza katika kipindi cha miaka ijayo ni makubwa mno. Tuna wajibu wa kuyatimiza, wanachotaka kuona ni nchi yetu kupiga hatua kubwa za maendeleo zitakazojibu matumaini yao na kutatua shida na kero za wanachi wetu. Nyie na mimi baada ya miaka mitano toka sasa tutapimwa kwa namna tutakavyokuwa tumetekeleza mambo ambayo tumewaahidi watanzania wenzetu. Mimi nina Imani kabisa kwa ushirikiano wenu na kwa kufanya kazi kwa bidii na ubunifu tutaweza kutimiza ndoto za watanzania wenzetu. Mheshimiwa spika niliona hili nilizungumze kwa sababu na mimi nimewahi kuwa mbunge katika kipindi cha miaka yangu ishirini katika bunge hili. Niwaombe sana watanzania wote, niwaombe sana wabunge wote, kikubwa ambacho kiko mbele yetu sisi watanzania ni kutimiza haja za wananchi wetu kwa kuwafanyia kazi. Wanahitaji kuona maji yanapatikana. Wanahitaji kuona Babarabara zinajengwa. Wanahitaji kuona hospitali zipo. Wanahitaji kuona mashule yapo. Wanahitaji kuona kila kitu ambacho wanakihitaji kwa maisha yao. Sasa tukiutumia muda wetu wa bunge wakati tuna wajibu wa

79 kuiongoza serikali itimize wajibu wake tukafanya mambo kama ambayo yamejitokeza leo ya aibu hayatatusaidia kuwasaidia watanzania waliotutuma. Mheshimiwa spika nimejitahidi kuzungumza kwa uchache lakini napenda nikushukuru sana tena mheshimiwa spika, mheshimiwa naibu spika, waheshimiwa viongozi wote tuliokaribishwa kuingia kwenye ukumbi huu na kushuhudia yote yaliyojitokeza na mmeona tuna kazi kubwa kwa sababu bado tuna watoto wengi, muendelee kuwavumilia na kuwafundisha na watanzania wameona. Baada ya kusema haya napenda basi nitamke kwamba ninalifungua rasmi bunge la kumi na moja la Jamahuri ya Muungano wa Tanzania. Asanteni sana kwa kunisikiliza. Mungu libariki bunge hili, Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Afrika asanteni sana.

Kupitia hotuba hii moyo wa kizalendo na wenye kuleta matumaini ndipo ulipojifunua kupitia mengi ambayo mheshimiwa rais aliyasema ambayo yalidhirihisha dhamira yake ya dhati ya kuwavusha watanzania na kuwatoa kwenye matatizo mbali mbali. Ukiangalia mengi ambayo mheshimiwa rais Dk. John Pombe Magufuli aliyazungumza ndiyo aliyoyafanya, ndiyo aliyoyasimamia, ndiyo aliyoyapigania kwa moyo wake wote na kwa nguvu zake zote kwa mapenzi mema aliyonayo juu ya nchi yetu. Hotuba hii inaweza kuwa kipimo cha aina ya kiongozi ambaye Mungu ametubariki kuwa naye kwa kipindi kama hiki. Mtu ambaye anasimamia anachokisema, mtu ambaye anaguswa sana na maisha ya watu hasa wale wa hali ya chini, mtu

80 mwenye kiu ya kuona taifa letu lenye vyanzo vingi vya utajiri likipiga hatua na kuingia kwenye eneo ambalo litawafanya wananchi wake wawe na maisha ambayo ndiyo stahili yao kwa rasilimali ambazo Mungu amewajalia kuwa nazo. Wakati hotuba hii inasomwa nan a mheshimiwa Rais bungeni alikuwa hata hajamaliza mwezi tangu kuchaguliwa lakini ukiangalia mpaka sasa maeneo ambayo ameyagusa hata wewe utakuwa ni shahidi kuwa mtu huyu anastahili kuungwa mkono kwa yote anayoyafanya kwa ajili ya wanyonge wa taifa hili ambao kwa muda mrefu walinyongwa lakini haki yao hawakupewa kama wahenga wanavyosema, “mnyonge, mnyongeni lakini haki yake mpeni”. Katika hotuba hi mheshimiwa aligusia maeneno mengi ambayo mpaka baadhi yamekwisha kufanyiwa kazi kwa kiwango kikubwa. Tunaweza kuona suala la elimu bure, miradi ya ujenzi wa miundombinu kama barabara, sula la shirika la ndege kufufliwa, suala la uwajibikaji wa viongozi wa serikali n.k. Kila ninapoisoma hutuba hii ninapata matumaini mapya kwa kuona kuwa rais magufuli anakiishi kile ananchokisema hivyo ni mtu anayefaa kuaminiwa ba kuungwa mkono katika jitihada zake za dhati ya kuifikisha nchi zetu katika nchi ya uchumi wa kati inayoendeshwa kwa viwanda chini ya serikali ya awamu ya tano.

81

SURA YA TANO MATENDO YENYE MGUSO

ZIARA YA KUSHTUKIZA KATIKA GEREZA LA BUTIMBA MWANZA

Hili ni miongoni mwa mambo yaliyogusa hisia za wengi lakini ilionyesha ni kwa kiwango gani rais magufuli ni rais wa wanyonge. Baada ya ziara hii baadhi ya watu waliobambikiziwa kesi walipata haki zao. Lakini hii ilikuwa ni faraja kwa wafungwa kujiona kuwa wanayekiongozi anayejali makundi ya aina zote.

82

MAMA ALIYEIBIWA MIFUGO ALIPWA NA RPC BAADA YA MTUHUMIWA KUACHIWA Baada ya huyu mama kibiwa mifugo yake mtuhumiwa alitatikwa kulipa kiasi cha shilingi milioni kumi na mbili lakini siku ya kulipa ilipofika askari walimwachi. Baada ya rais kumsikiliza alimwagiza RPC kumlipa kiasi cha shilingi milioni 15 kama fidia ya wizi wa n’gombe hao wapatao 25. Hii inaonesha namna ambavyo rais magufuli amekuwa ni rais na mtetezi wa wanyonge. Agizo hili lilitolewa kutokana na uzembe wa polisi. Hii inaonesha namna ambavyo pia kumekuwa na uwajibishwaji wa moja kwa moja wa viongozi wa serikali na watendaji wa ngzi mbalimbali.

83

SURA YA SITA JICHO LA MBALI Ni lazima tujitahidi kuona mbali. Tusisubiri wanasiasa ndiyo watusaidie kuona mbali lakini kuona mbali ni wajibu wa kila mwananchi na njia pekee ya kuona mbali ni kusafiri kwa njia ya mawazo na fikra. Naamini kila mtanzani akijitahidi kusafirisha macho yake ya kifikra kuna mambo mengi hatutayakubali. Kama tunaangalia karibu ni ngumu kumtambua aina ya kiongozi anayetufaa ni rahisi kuangukia kwenye mikono ya walaghai watakao tudanganya kwa mambo ya muda mfupi lakini tukijitahidi kuona mbali basi tunaweza kuyakataa baadhi ya mambo ambayo yanaonekana ni mazuri kwa sasa lakini mbeleni yanaweza kutufanya tukalia na kuomboleza. Hitaji letu kubwa limekuwa kupata kiongozi ambaye anaweza kuona mbali na kwa kuona mbali huko akawa na ujasiri wa kuyakataa baadhi ya mambo ambayo wajanja na wezi katika nchi yetu wanajaribu kuyapenyeza. Sisi pia tukiwa na jicho la mbali kama mtu mmoja mmoja tutakuwa tumefaulu kujenga mazingira ya kumwelewa na kumuunga mkono yule ambaye anatuongoza kwa muono wake wa mbali lakini vinginevyo tunaweza tukajikuta tunakuwa kikwazo kwake kwa sababu hatuwezi kumwelewa kwa namna anavyojaribu kutuelezea maono yake ya mbali.

84

SURA YA SABA HAPA KAZI TU

Hapa kazi tu ni kauli mbiu ya serikali ya awamu ya tano chini ya uongozi wa Rais makini Dk. John Pombe Magufuli. Hii ni serikali inayoundwa na chama cha mapinduzi. Serikali hii ni mahususi kwa ajili ya kuleta ustawi wa wananchi. Kwa hiyo iliwekwa madakani na wananchi na ipo madarakani kwa ajili ya wananchi. Na kila mtu amekuwa shahidi kwa namna inavyowajibika kwa ueledi ili kupelekea maendeleo ya nchi na ustawi wa wananchi. Serikali hii inaundwa na wizara zifuatazo ambazo zimekuwa msitari wa mbele usiku na mchana katika kuhakikisha wananchi wanapata maendeleo: KILIMO, OFISI YA RAIS, TAMISEMI, UTUMISHI NA UTAWALA BORA, MADINI, OFISI YA MAKAMO WA RAIS MASUALA YA MUUNGANO NA MAZINGIRA, OFISI YA WAZIRI MKUU SERA, BUNGE, KAZI VIJANA, AJIRA NA WALEMAVU, MIFUGO NA UVUVI, SHERIA Na KATIBA, ULINZI NA JESHI LA KUJENGA TAIFA, ELIMU SAYANSI TEKNOLOJIA NA UFUNDI, NISHATI, FEDHA NA MIPANGO, MAMBO YA NJE, USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARAKI, KIKANDA NA KIMATAIFA, AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA , WAZEE NA WATOTO, MAMBO YA NDANI, VIWANDA BIASHARA NA UWEKEZAJI, HABARI,

85

UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO, ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI, MAJI NA UMWAGILIAJI, UJENZI UCHUKUZI NA MAWASILIANO.

Kuna haja ya sisi kama wananchi kuzitambua na kila mara kuikumbuka kazi kubwa inayofanywa na serikali ya awamu ya tano chini ya Rais wetu ili tusijetukadondokea mikononi mwa walaghai wanaojaribu kutushawishi kwamba hakuna kilichofanyika. Kuna mengi yaliyofanyika mpaka sasa na macho ya wengi yameyashuhudia hata kama yote hayajaisha lakini walau kwa hatua kadhaa ambazo zimetupa kuona matokeo dhahiri ni vyema tukawa na moyo wa shukrani na wa kupongeza kwa ajili ya serikali ya awamu ya tano chini ya uongozi wa Rais Dk. John Pombe Magufuli kiongozi mwenye dhamira ya dhati ya kuitoa nchi yetu hapa tulipo na kutufikisha kwenye nchi ya uchumi wa kati inayoendeshwa kwa viwanda ifikapo mwaka 2025. 1. BARABARA NA MADARAJA

86

Serikali ya awamu ya tano imejipambanua zaidi katika ujenzi wa miundombinu tofauti na awamu zote ambapo kwa mara ya kwanza kumekuwepo na ujenzi wa barabara za juu zaidi ya nne jiji Dar es salaam. Hadi sasa imefanikiwa kufanikisha ujenzi wa fly oiver tazara maarufu kama Daraja la Mfugare uliogharimu zaidi ya shilingi bilioni 95. Vivlevile ujenziwa flyover ubungo ambao unatarajia kugharimu zaidi ya shilingo bilioni 188.71 bado unaendelea mpaka sasa. Pamoja na hayo ujenziwa barabara nchi nzima zaidi ya kilomita 2115 za rami kwa gharama ya trillion 5.37 ukiendelea mpaka sasa. Hii inadhirisha ai utendaji kazi wa rais. Pia serikali imegfanikisha kuanza ujenizi wa bara bara ya njia nane kati ya kimara Dar salaam na kibaha mkoa wa pwani uyenye urefu wa wa kilomit a19.2 .u jenzi huu utagharimu shiingi bilioni 141.56 pia utahusiha ujenzi wa barabara za juu katika maeneo ya kibamba ccm kwenye makutano ya

87 barabra inayokwenda bunju na hospopitali ya taifa ya muhimbili tawi la mloganzira. Miradi mingine ni ujenzi wa Daraja la kigongo busisi katika ziwa Victoria ambalo litakuwa lefu kuliko yote Afrika mashariki na kati kwa ghama ya shilingi billion 696.2 na ujensi wa daraja la Salenda jijini Dr es salaam kwa gharama ya shilingi bilioni 270.

2. SHIRIKA LA RELI

Ujenzi wa reli mpya ya kisasa katika kiwango cha kimataifa Standard Gauge Railway(SGR) kutoka Dar es salaam, Tabora hadi Kigoma. Lakini pia Mwanza na Tabora Mpanda yenye urefu wa kilomita 1219 inayotarajiwa kugharimu zaidi ya shilingi trillion 7.6 na uboreshaji wa njia za reli za zamani. Hili ni mojawapo ya dalili zinazotumiwa katika kuangalia dalili zitakazopelekea kuinukia kwa uchumi wa Taifa letu. Hii

88 ni tofauti na awamu iliyopita ambapo Rais mstaafu Jakaya Kiwete aliwahi kuiri kuwa alikuwa na mpango wa kujenga reli mpya lakini haikuwa ya kutumia umeme kama ambavyo Rais wa awamu ya tano amefanya. Kampuni ya Rasilimali za reli nchini RAHACO ndiyo inatekeleza mradi huo kutoka Dar es salaam kwenda Isaka na mwannza. UJenzi huo umegawanyika katika awamu ndogo nne 1. Dar es salaam hadi Morogoro; 2. Morogoro hadi Makotopora 3. Makotopora hadi Tabora 4. Tabora hadi Mwanza. Kwa mujibu wa mkurugenzi mtendaji wa RAHACO Mhandisi. Masanja Kadogosa jumla ya makandarasi wane wanaendelea na ujenzi usiku na mchana ili kukamiilisaha ujenzi wa reli hiyo yenye upana wa mita 1.345 na ambao utarushusu tereni kutembea kwa kilomita 160 kwa saa.

3. SHIRIKA LA NDEGE

89

Awamu zilizopita lilishindwa kuendesha shirika la ndege kwa sbabu mbali mbali lakini kwa awamu hii mambo yamekuwa ni tofauti. Hadi sasa ndege sabab zimekwisha nunuliwa katika utekelezaji wa mpango wa kuwa na ndege ifikapo mwaka 2021 tnagu kuanziwa kwa shirika hili mwaka 1977. Chini ya mpango wa kufufa shirika hili mpka sasa ndege 6 zimekwisha kununuliwa ambayo imepelekea idadi ya ndege kuwa 7. Ndege hizi zimnunuliwa kulingana na mpango wa biashara wa shirika hili. Rais kikwete alikili kuwa rais Magufuli ni jasiri kutokana na ujasiri wake wa kulifufua shirika hili. Wakati wa Baba wa Taifa tulikuwa na ndege 14. Ununuzi wa ndege umeenda sambamba na ujenzi na ukarabati wa viwanja mbali mbali vya ndege 15 kwa gharama ya shilling trillion 1.9 kujenga na kunua rada 4 katika mikoa ya Mbeya, Dar es salaam, Mwanza na Kilimanjaro kwa shilingi bilioni 67.3.

90

4. ELIMU

Kupitia mpango huu ndoto za wengi zimepata mwangaza maana elimu haitakuwa ya wenye nacho peke yao. Serikali imefanikiwa khakiisha fedha za mikopo way wanafunzi wa elimu ya juu natoka kwa wakati. Mna vilevil kiwango cha wanafunzi wanaopewa mikopo kimeongezeka. Tangu rai aingie madarakani zaidi ya shilingi trillion 1.62 zimekwihsa tolewa. Uandikishwaji wa wanafunzi wa elimu ya msingi umeongezeak na mpaka sasa kiasi cha shilingi biloni 945.987 zimekwisha tumika. Vilevile serikali imefanikiwa kukarabati shule kongwe 62 ujenzi wa madarasa, maabara na nyumba za walimu kwa shilingi bilioni 308.1

91

5. HUDUMA ZA AFYA.

Sehemu ya majengo ya kituo cha afya cha Matemanga kilichoko wilayani Tunduru mkoani Ruvuma kilichofanyiwa ukarabati uliogharimu shilingi milioni 500 za kitanzania. Sambamba na ukarabati na ujenzi wa vituo vya afya pia serikali ya awamu ya tano imewezesha utaratibu wa wananchi wa kawaida kumudu kulipia bima za afya ambazo kwa mtu mmoja mmoja inagharimu shilling 40,000/= na shilingi 150,000/= kwa watu sita wa familia moja. Hii imerahisisha watu wengi hususani wajasiriamali kupata namna ya kumudu gharama za matibabu. Ili kumuunga mkono Rais katika hili ni muhimu tujitokeze kwa wingi kufuta utaratibu utakaotuwezesha kupata bima za afya kwa wale tusionazo.

92

Tmeona juhudi kubwa zilzifanywa katika kuboresha huduma za afya. Kwa mjuibu wa waziri wa Tamisemi mhe. mpaka ssasa katika sekta ya Afya kuna ujenziwa vituo vya afya 352, zahanati 30, hospitali 67 ukarabati wa hospitali 21 za zamani kwa shilingi bilioni 321. Pia vifaa mbali mbali vya hospitali vimenunuliwa kwa gharama ya shilingi bilioni 64. Yote haya ni matunda ya juhudi za srikli kwa kushirikiana na bunge ili kuongeza bajeti ya wizara ya afya.

6. UKUSANYAJI WA MAPATO Hivi sasa tunavyoongea mamlaka ya mapato inakusanya wastani shilingi trilioni 1.3 kila mwezi ikiwa ni matokeo ya kuziba mianya ya upotevu ambayo ilikuwa ikipelekea nchi kupoteza asilimia 8 mpaka 10 ya mapato kila mwezi. Serikali ya awamu ya tano imefanikiwa kuongeza ukusanyaji wa mapato kutoka trilioni 9.9 ktika awamu ya nne hadi kufikia trillion 14 kwa mwaka katika awamu ya tano. Imefanikiwa kuongeza asatan wa mwezi wa mapatao kutoka wastani wa shilingi billion 850 kwa mwzei kwa mwaka 2015 hadi kufikiwa wastani wa trillion 1.3 kwa mwezi kwa sasa. Unaweza kuona ongezeko na utofauti wa miaka iliyo pitakimapato kama ifuatavyo; 2015/2016- trilion 12.5 2016/ 2017-trilion 14.4, 2017/ 2018-trilion 15.5. Mapato yote yaliyokusanywa kwa miaka mitatu mfululizo ni trillion 42.4. Tangu TRA ilipoanza kufanya kazi julai mos 1996 mapema mwezi huu imevunja rekodi kwa kukusanya trillion 1.76 mwezi septemba 2019

93 makusanyo ambayo ni sawa na ufanisi wa asilimia 97.2 ya lengo la TRA kukusanya shilling trillion 1.81 iliyojiwekea TRA yakilinganisha n septemba 2018 makusanyo hayo yameongezeka kwa asilimia 29.81 hivyo kuzidi ufanisi wa miezi yote ya robo ya kwanza yam waka huu wa fedha. Ongezeko hili la ukusanyaji mapato ni hatua kubwa nchini ambalo ka kiwango kikubwa limechangiwa na kudhibiti mianya ya ukwepaji wa kodi na umma kumwelewa rais na kuamua kumuunga mkono. 7. MAJI Sekta ya maji imeboreshwa . Desemba mwaka jana Rais alizindua ujenzi wa maji wa thamani ya ziaid ya shilingi bilioni 520 naotekelezwa kwa ushirikiano katik ya serikali na beki ya maendeleo ya Afrika AFDB. 8. NISHATI YA UMEME Umeme mto Rufiji maarufu kama stigrous gouge. Richa ya kupigwa vita na jumuiya za kimataifa rais magufuli amefanikiwa kuanza ujenzi wa mradi wa Bwawa la kualisha umeme katika bonde la mto Rufiji stigrouz gouge ambao unagharimu shilling trillion 6.5. Mradi huo uliopewa jina la mwalimu yerer ulikwamba kwa muda wa zidi ya miaka 4o. hata hivyo Decsenmba mwaka jana serikali ilishasaini mkataba na kmpuni ya Arab contrctors ya misri ambayo inatekeleza mrdi huo utakao gharimu shilingi trtrillion.558 na unatarajia kuzalisha meghawat 2100. Mradi huo ulikwama kutekelezwa tangu miaka ya 1970 kutoka kwa mashirika na wadau mbali mbali wa masuala ya mazingira.

94

9. NIDHAMU SERIKALINI Watumishi wengi walikuwa wakifaya kazi kwa mazoea na kukiuka maadili ya kazi kwa kujihusihsa na vitendo vya rushwa na mambo mengine ambayo hayakuwa sawia. Alifanikiwa kutokomeza watumishi hwea kitu ambacho kiliishabasihia serikali hasara kwa kulipa malipo hewa. Vilevile alikomesha safari za kiholeala za nje. 10. MIGOGORO YA ARDHI Seriukali ya awamu ya tano imesuluhisha migogoro mingi ya ardh ambayo kwa kiwango kikubwa ilikuwa imeshamiri kwenye miko yay a migogoro na manyara. Hili lilienda sambaba na kufuta baadhi ya maeneo tengefu. Mapori tengefu 12 yamefunta ili kunemeen=shja vijni zaidi ya 900. 11. USIMAMIZI THABITI WA RASILIMALI Usimamizi thabiti a rasilimali za Taifa letu ni mojawapo ya jambo ambalo rais magufului amefaulu sana. Hata yeye binafsi husema kua Tanzania sin chi maskini. Mojawapo ya mambo ambay ameyafanya ni kushinikiza marekebisho mpaya ya sheria ya kodi ya madini. Kupitia marekebisho hayo Rais ameiamuru kampuni ya kuchimba madhni bariki kuafiki marekbisho hayo ambapo pamoja na hayo yamepelekea kufutwa kwa kampuni ya ACACIA na kuunda kampuni nyingine ya Twiga mining kwa ubia wa serikali na kampun ya Barick. Yote hayo yalikuwa ni matokeo ya Rais Magufuli kuunda tume ya mabingwa na wanasheria waliobobea katika mambo ya madini mbayo

95 ilichunguza makontena 77 ya makininia ambayo yalibainka kuwa na kiwango kibkubwa cha madini togfaitui na vile ilivyokuwa inatazamiwa.

12. MAKAO MAKUU DODOMA Zaidi ya watuishi 5136 wanatarajiwa kuhamia Dodoma. 13. UJENZI WA VIWANDA MOJWAPO YA AENA MUHIMU YA Rais Mgufuli ni kuifanya Tanzania inakuwa nchi ya wviwanda. Mpaka sasa viwanda vikubwa na vidogo zaidi ya 3000 vimekwish kuinduliwa na vinafanya kazi.

14. USAFIRI WA MAJINI Upande wa usafri wa majini rais magufuli amejenga meli katika ziwa victori ana ziwa nyasa kwa shiliongi bioni 172.3. vilevle amepanua bandari ya Dar es slaam, Mtwara na Tanga kwa shilingi trioni 1.2. tofauti n awamu zotre zxilizopita awamu ya tano imefanikisha kuanza ujenzi wa meli mbili kubwa mpya na za kisasa katiaka ziwa Victoria na ziwa Tanganyika ujenzi unaotekeleza na kampuni kutoka Jamhuri ya watu wa korea pamoja na kukarabati meli tano ambazo ni Mv Victioria, Mv Butyama, Mv Liemba, Mv umoja na Mv Serengeti.

96

15. DAWA ZA KULEVYA Matumizi ya dawa za kulevya ni tattizo sugu llilokuwa likisumbua taifa letu. Rais magugfuli alifanikiwa kuanzisha mapambano dhidi ya madawa ya kulevya mabmapo alianzisha mamlaka yua kudhibiti madawa ya kulevya.

97

SURA YA NANE MAONI YA WATU MBALIMBALI 1. “Pongezi kubwa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Rais John Pombe Magufuli kwa ushujaa wake usiokuwa wa kawaida katika Sekta ya madini. Wapo watu ambao wakisikia Rais anapongezwa wao masikio yanawasha wanapenda kuona anapingwa tu. Muungwana kwa kawaida hawezi kupinga kila jambo wakati wote. Hata kama una hoja fulani ukiwa muungwana tafuta mazuri kwanza ya kupongeza halafu ndipo unapoweza kuleta hoja yako. Mtu ambaye atakuwa anapinga tu kila jambo kama vile hakuna lolote lililo zuri huyo atakuwa siyo muungwana atakuwa ni mkorofi. Tanzania ni nchi ya waungwana, ukishakuwa mkorofi hata kama ulikuwa na hoja inakuwa ni vigumu kusikilizwa. Kwa nini namuita shujaa Rais Magufuli katika eneo la sekta ya madini? Kwa sababu kwa miaka mingi nchi hii imekuwa watu wanaimba wimbo wa nchi maskini nchi maskini lakini Rais Magufuli amesimama na kutaja tena na tena kwamba nchi yetu ni tajiri na tena akazungumza kuwa nchi yetu inaweza kuwa nchi inayoweza kusaidia nchi nyingine. Huu ni ushujaa. Naomba mheshimiwa undelee kulizungumza hili tena na tena mpaka kila mtanzania abadilishe mtazamo wake maana umaskini unaanza katika fikra mpaka tufikie kila mahali kila mtu anazungumzia nchi yetu ni tajiri siyo nchi maskini na kwa kufanya hivyo tunaumba kitu kikubwa sana.

98

Ukishaingia tu katika habari ya kuhakikisha matunda ya nchi yanabaki kuwa faida ya taifa umetangaza vita. Na kile anachosema wakati wote kwamba kuna vita ya kiuchumi kwa mtu yoyote wa rohoni anawezakuelewa vita inayotangazwa. Kwa hiyo katika maombi ambayo tunaenda kuomba sasa kumkabidhi Rais JPM mikononi mwa Mungu kwamba ampiganie vita hii na zaidi sana alifanye taifa hili kuweza kuneemeka kama alivyokusudia. ”, ASKOFU ZAKARIA KAKOBE

2. “Mungu aliyekupa mambo haya akakujalie kuyatimiza maana nguvu ya mfalme ni watu wake nan a mfalme pasipo uwezesho toka kwa Mungu hakuna linalotendeka. Mungu akupe maono ya kufanikisha kazi hii. Nilitumia miaka 15 nikilia tupate mtu ambaye kwa kiasi anafanana na kichaa kichaa hivi anayeipenda Tanzania, anawapenda watanzania, anaijua Tanzania, anaitakia mema Tanzania kufanya isimame na kutimiza maono ya Mungu. Mungu akupe Baraka zake” ASKOFU JOSEPHAT MWINGIRA

3. “Tanzania ni nchi ya saba duniani kwa vyanzo vya utajiri utajiri ukitoa zile sita maana yake Tanzania ni nchi ya kwanza, ni nchi ya pili duniani kwa utalii ukitoa Brazil ni nchi ya kwanza kwa utalii ndiyo maana Serkali naipongeza kuchukua maamuzi ya kununua ndege itakuza uchumi wan chi yetu sana” MCH. ANTHONY LUSEKELO(MZEE WA UPAKO)

99

4. “Napenda utendaji kazi wa Rais, naona nidhamu kazini imerudi, watu wanaheshimiana. Yeye ni binadamu siyo Mungu kwamba anafanya kila kitu kiko sawa japokuwa kuna vitu ambavyo vianweza visiwe sawa lakini ninampenda kwa sababu ni kiongozi mwenye maamuzi ya kijasiri. Hiyo ni moja kati ya vitu ambavyo ninavipenda kwa Magufuli. Kiujumla tu niseme anashika nafasi yake vizuri kama Rais, anafanya kazi nzuri”, NAY WA MITEGO (MWANA MZIKI) 5. “Nikikuangalia nauona moyo wako jinsi ambavyo unatamani kuliona taifa hili likienda viwango vingine na umejitahidi sana. Kila mwenye machoameona na kila mwenye masikio amesikia. Nimezunguka karibu nchi nzima kila ninakokwenda vumbi linatimuka mabarabara yanajengwa vitu vingi vinafanyika. Kwa hiyo sioni woga wala mashaka kusema haya kokote ninakokwenda kwa kazi nzuri unayoifanya Rais wetu. Mimi niseme kwa niaba ya wale ambao hawawezi kukufikia kwa sababu hat mimi nimeipata kwa bahati na sina uhakika kama nitaipata tena kwamba mhe. Rais mimi niwe mdomo wao wale ambao hawawezi kukufikia niseme lugha moja tu TUMEKUELEWA. Watanzania tumekuelewa. Hata wale ambao hawataki kusema kwa midomo yao wamesema kimoyomoyo kwamba Rais wamekuelewa ndiyo maana nilipopata mwaliko huu niliarisha shughuli zangu zote ili nije niseme tu nimekuelewa.” MCH. DANIEL MGOGO 6. “Serikalini kumebadilika watu wanafanya kazi kwa nidhamu. Tunakokwenda ni pazuri kuliko tulip oleo

100

Ninamatumaini kwamba tutafanya vizuri sana na serikali itafanya vizuri sana kuliko kule tulikotokea. Mwendo huu ni mchakamchaka si mwendo wa wazembe…” ASKOFU JOSEPHAT GWAJIMA 7. “Mimi mkenya mlipata raisi Tanzania ingawa kwa sasa amwezi ona mazuri yake siku kitoja mtayasifia akuna raisi kwaii dunia asie na mapungufu yake wala mwanadam yeyote ameipinga Tanzania msasa sawasawa hadi wamejielewa ingwa kwaza waliona kama ni kuonewa ila sasa wanajivunia matuda walio na ufaham wanajua wamepata raisi jembe hakika makufuli kiboko ya Tanzania maedeleo mtayaelewa tuu hata kama amyajui napenda vile unavio jiyoa kwa wanainji wako raisi makufuli MUNGU Azidii kukupa maharifa uiyongoze tazania” MAGY NZIOKA (KENYA) 8.

101

SURA YA TISA KWA NINI TUMUUNGE MKONO?

Tunaweza kuona kuwa Rais ni kazi rahisi hata kiasi cha kuiongelea kirahisi lakini ni kazi nzito inayohitaji moyo wa kujitolea zaidi kuliko mtu anayetafuta matakwa yake mwenyewe(faida zake mwenye ili ajinufaishe). Ikiwa inahitaji mtu ambaye ana moyo wa kujitolea yaani moyo uliobeba watu zaidi na wenye kutanguliza mbele maslahi ya wananchi na nchi kwa ujumla basi ni dhahiri kuwa kila anachokifanya kitakuwa kwa ajili ya watu hawa na ili mambo yaende sawa mtu mwenye mamlaka ya cheo cha Rais hana budi kuungwa mkono. Kwa mujibu wa katiba ya nchi Rais anatambulishwa kama mkuu wa nchi basi kwa sababu nchi ni yetu na yeye anakuwa mkuu wetu hivyo basi hatuna budi kumuunga

102 mkono kwa sababu yeye ni mkuu wetu. Kushindwa kwake ni kushindwa kwetu, aibu yake ni aibu yetu, kuchafuka kwake ni kuchafuka kwetu, kufanikiwa kwake ni kufanikiwa kwetu, kufanya vizuri kwake ni kufanya vizuri kwetu n.k maana yeye ni kiongozi wetu mkuu kama nchi. Tukumbuke kuwa nguvu ya kiongozi ni watu wake maana yake kama watu hawako tayari kusimama na kiongozi wao, kumlinda na kumtetea dhidi ya watu wenye nia ovu na wasio na mapenzi mema na nchi yao ni dhahiri kuwa watu hawa ni watu wasiojitambua wanaompa mtu nafasi ambayo ni nyeti na inayogusa maisha yao kutoka kila upande lakini hawako tayari kusimama naye ili wajenge nchi yao chini ya uongozi wake. Kwa mujibu wa katiba yetu Rais ni kiongozi mkuu wa Serikali. Kwa mujibu wa mfumo wa demokrasia ya vyama vingi ambao sisi ndiyo tunaufuata kwa sasa chama kinachoshinda uchaguzi ndicho kinachounda serikali na serikali hiyo ndiyo inakuwa na wajibu au mamlaka ya kusimamia shughuli zote za maendeleo ya nchi na watu wake. Hivyo basi inapokuja kwenye suala la utendaji wa mambo mbalimbali husuani ni taasisi za serikali na miradi mbalimbali ya maendeleo. Hapa pia tunaowajibu mkubwa wa kumuunga Rais mkono katika kuhakikisha shughuli zote zinaenda sawa maana hapa ndipo palipo na moyo wa shughuli zote za kimaendeleo. Kwa mujibu wa katiba yetu vilevile Rais ni Amiri Jeshi Mkuu yaani kiongozi mkuu wa majeshi yetu ya ulinzi na usalama. Suala la usalama wetu si jambo la mchezo. Tanzania inafahamika kama kisiwa cha amani duniani.

103

Tunao wajibu wa kumuunga Rais wetu mkono ili kuhakikisha nchi yetu inaendelea kuwa mahali pa amani. Katika hili tusilete mchezo kabisa maana ikiwa hatutasimama katika nafasi zetu tunaweza kujikuta katika machafuko na mambo mengine mabaya. Unapaswa kufahamu kuwa ni muhimu kusimama na kiongozi wetu mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama ili amani yetu iendelee kudumu. Sababu nyingine ya kumuunga mkono Rais ni kujua kuwa yeye kama kiongozi wetu mkuu ndiye anayetuunganisha sote tukiachilia mbali utofauti wa itikadi zetu kisiasa, utofauti wa Imani zetu, utofauti wa makabila yetu lakini katika yote hayo tunahitaji kumuunga mkono Rais bila kuyaangalia hayo ili kumfanya apate utulivu wa kutuongoza vizuri kwenye maendeleo ambayo yenyewe kwa asili yake hayana chama, kabila, dini n.k Sababu nyingine ni kwa sababu tulilidhia kikatiba awe Rais wetu yaani tulimchagua. Mtu akishafaulu kushinda uchaguzi hatuna budi kuachana na itikadi zetu na kusimama naye maana kama wengi wetu wamemchagua basi ni sisi wote tunakuwa tumemchagua. Sababu nyingine ya kutufanya tumuunge mkono zaidi ni dalili njema ambazo ametuonyesha katika utendaji wake tangu kuingia madarakani. Ikiwa mtu anafanya kazi nzuri na ametuonyesha njia nzuri ya kule anakotupeleka tunahitaji nini tena zaidi ya maendeleo. Tunahitaji nini tena zaidi ya miundombinu bora ya barabara, reli, usafiri wa anga, huduma za afya n.k. Haya ndiyo mambo ambayo

104 tunapaswa kuyaunga mkono na kuyapongeza ili baada ya muda tuondokane na adha za usafiri mbaya, shida za maji n.k. Tunahitaji nini zaidi ya kuona wanyonge wanapata haki zao, wanaoonewa hawaonewi tena n.k. Nafikiri wengi wetu tukijiuliza ni kiongozi wa namna gani tunayemtaka tutaona tuna sababu za kumuunga mkono Rais wa namna hii kwa kipindi chote ambacho atakuwepo madarakani kwa mujibu wa katiba. Sababu nyingine ni vizazi vyetu watoto wetu na watoto wa watoto wetu. Hapa nina maana kuwa hata kama wewe hutaguswa sana na matunda ya yale yanayofanyika leo kumbuka una watoto kesho na kesho kutwa watakuta mazingira mazuri kwa sababu kuna kiongozi mzuri ulumuunga mkono. Vita dhidi ya ufisadi, rushwa, wizi wa rasilimali, madawa ya kulevya, ukandamizaji na unyonyaji wa kiuchumi. Haya ndiyo mambo ambayo yanatesa nchi nyingi za kiafrika na ndiyo sababu kubwa nyingi haziendelei lakini viongozi wake ni matajiri wakubwa kwa sababu ya usaliti. Sasa ukipata mtu ambaye ana ujasiri wa kukomesha au kupunguza kwa kiwango kikubwa vitendo vilivyoainishwa hapo juu unataka kiongozi wa namna gani. Maana usifikiri ni kazi rahisi kuvamia magenge ya wala rushwa na mafisadi, kufyeka mapori ya maharamia wa kiuchumi inahitaji ujasiri na kama umepewa neema ya kuwa na kiongozi wa namna hii huna budi kumuunga mkono.

105

Kutoa nafasi pia kwa vijana kuongoza. Vijana ndiyo wenye nguvu na wenye uwezo wa kufanya mambo kwa nguvu na wa haraka. Ni vizuri kumunga mkono kiongozi anayetoa nafasi kwa vijana katika harakati za kujenga nchi yetu. Ikiwa vijana wanashirikishwa kwa kiwango kikubwa tunakuwa na mazingira mazuri ya kuwa na maendeleo endelevu. Kero za wanachi zinapewa kipaumbele na kutatuliwa. Ni muhimu kumuunga mkono kiongozi anayetoa kipaumbele kwenye usikilizwaji na utatuliwaji wa kero za wananchi.

Kiongozi asiyejilimbikizia mali.

Kiongozi asiendekeza matumizi mabaya ya rasilimali hasa fedha kwa namna isiyo sawasawa kitu ambacho kimesaidia mambo mengi ya msingi kupewa kipaumbele kwenye mgao wa kifedha. Ili maendeleo yawepo ni lazima tuwe na nguvu ya fedha lakini tatizo si kuwa na nguvu ya fedha tu ila kupata mtu atakaye hakikisha fedha zinakwenda maeneo sahihi kuliko kuishia kwenye matumbo ya watu wenye tamaa wasio na huruma wala uchungu wowote na nchi yetu.

Kiongozi ambaye ameongeza kiwango cha uwajibikaji wa viongozi wengine, watumishi wa uma na kupandisha heshima ya serikali.

106

SURA YA KUMI TUMUUNGE MKONO SASA

WAJIBU WETU KAMA WANACHI Sasa ni wakati wetu wa kutangaza na kujitokeza kumuunga mkono Rais bila kuona aibu maana ni Rais wetu na anayoyafanya ni kwa ajili yetu na watoto wetu. Tumuunge mkono kwenye kukemea vitendo vya rushwa. Tuseme hapana mahali popote tunapoona vitendo vya rushwa. Tumuunge mkono kwenye ujenzi wa miundo mbinu. Tumuunge mkono kwenye kukemea vitendo viovu. Wajibu wa kujenga Tanzania ni ya watanzania wenyewe hivyo tunapowachagua viongozi tuwape ushirikiano. Ni vyema tukawaunga mkono viongozi wetu katika masuala yote muhimu yanayogusa maslahi yetu kwa

107 namna moja ama nyingine. Ikiwa tutatoa ushirikiano wa kutosha viongozi wengi hawatakuwa na ujasiri wa kufanya yasiyofaa maana hakuna atakayeyabariki lakini pia itakuwa ni rahi kuwashughulikia mara tu tutakapowagundua kwa kufuata utaratibu ambao tumejiwekea kikatiba. Hata kama si wote tuliompigia kura kumchagua hata kama hatokei kwenye chama chetu, dini yetu, kabila letu n.k lakini akishafanikiwa kuwa Rais wetu hatuna budi kumtambua na kumuunga mkono ili atufikishe pale ambapo tunatamani atufikishe. Hatupaswi kufuatisha propaganda za kisiasa ila tunapaswa kusimama pamoja na Rais wetu ili aweze kufanya yale ambayo yamebeba maslahi yetu. MITANDAO YA KIJAMII Uwepo wa mitandao ya kijamii ni mojawapo ya viashiria vya hatua kubwa za kimaendeleo hususani katika eneo la Sayansi na Teknolojia. Vilevile katika kipindi tulichonacho mitandao ya kijamii imeteka hisia na akili za watu wengi sana lakini zaidi imefaulu kuwaleta watu karibu na kuwa chombo muhimu cha mawasiliano miongoni mwa wananchi hata wananchi na Serikali. Ni vema tukafahamu kuwa tuna wajibu wa kuitumia vizuri mitandao hii kwa ajili ya maendeleo yetu. Tusiitumie kama chombo cha kupeleka taarifa zitakazotufanya tugombane na tuchukiane bali itusaidie kuwa karibu zaidi kwa ajili ya maslahi mapana ya Taifa letu. Pia iwe nyenzo

108 itakayotusaidia kufanya mema yanayounga mkono juhudi za wazi za Serikali yetu ya awamu ya tano chini ya kiongozi makini, mwadilifu na mwenye weredi Rais John Joseph Pombe Magufuli. Tuwe makini na matumizi yake pia tukitambua wazi kuwa iko sheria ya matumizi ya mitandao ili tusijetukajikuta tunaingia matatizoni. Tunapaswa kuelewa wazi kuwa sheria hii hijawekwa wazi kwa ajli ya kumkomoa au kumtega mtu yeyote lakini ni katika kuboresha utaratibu wa namna tunavyokwenda kama Taifa la watu wanojitambua na kujielewa. Lakini pia sheria hii ni mahususi kwa ajili ya kutulinda sisi wenyewe dhidi ya maadui ambao wanaweza kujipenyeza kupitia baadhi yetu na kutaka kutugawa kwa kupitia matumizi ya mitandao kitu ambacho kinaweza kuhatarisha Amani yetu. Ni vyema kuijua sheria hii ya mtandao kwa mtu yeyote anayetumia mtandao ili usije ukaingia hatiani kwa makossa ambayo chanzo chake ni kutojua yaani ujinga. Tuitumie mitandao hii kuelimisha, kuhamasishana na kupashana habari njema juu ya Taifa letu wenyewe na si kusambaza mambo ambayo yanatuchafua sisi wenyewe. Tusisambaze habari za uongo, uzushi na zile za kuchfuana maana hakuna tunayemfaidisha zaidi ya kulibomoa Taifa letu kwa matendo kama hayo ambayo ni ya kishenzi nay a watu wasio wastarabu na wasiolitakia Taifa let mema. Kumbuka kumvua nguo ama kumdharirisha kiongozi mtandaoni ni kujidharirisha mwenyewe maana kwa nchi kama hii yenye mfumo wa kidemokrasia kiongozi aliyeko madarakani anakuwakilisha wewe hivyo unapaswa kumlindia heshima na likiwako jambo lislo sahihi juu

109 yake fuata utaratibu uliowekwa kikatiba ili lipate kumalizwa. Ibara ya 3 ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kifungu cha kwanza, “Jamhuri ya Muungano ni nchi ya kidemokrasia nay a kijamaa, isiyokuwa na dini, yenye kufuata mfumo wa vyama vingi vya siasa” Ibara ya 8 ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kifungu cha kwanza kifungu kidogo (a), “Wananchi ndiyo msingi wa mamlaka yote, na Serikali itapata madaraka na mamlaka yake yote kutok kwa wananchi kwa mujibu wa katiba hii” Watanzania ni watu ambao tumelelewa kwa maadili na nidhamu ya hali ya juu na sifa hii tunayo hata kwa mataifa mengine hivyo tusikubali kuipoteza kwa kubebelea tabia za kishenzi zisizo na maana ambazo pengine tunaziiga kutoka mataifa mengine tukidhani zitatusaidia kumbe hata wale tunaowaiga wanatushangaa tumeingiwa nan a kitu gani cha ajabu hata kiasi cha kuacha utamaduni wetu mzuri. Unapoongelea jambo loloe hata kama ni mtandao basi tumia lugha nzuri ya staha ambayo haitaibua chuki wala kuleta mkanganyiko ili tusitumie muda mwingi kwenye malumbano yasiyo na tija badala yake tutumie muda wetu kujenga nchi yetu. Pia ni vema tukajua kuwa si kila jambo linalotuhusu tunapaswa kulijadili mtandaoni lakini tutumie njia sahihi kuweza kulifikisha mahali husika maana kupiga kelele na kupayuka bila utaratibu haitusaidii.

110

Jambo jingine la kuongezea na kukumbusha ni kuwa tunapaswa kuwa makini sana na namna tunavyotumia hii mitandao maana tunaweza kuona viwango vya utalii vinashuka, wawekezaji wanapungua wakati mwingine tukadhani ni uzembe wa serikali kumbe ni matokeo yay ale tunayoyafanya kule mitandao. Tujue jambo moja kuwa hii nchi ni ya kwetu na tunao wajibu wa kuilinda kama wanacnchi si kwenye mipaka ya kijiografia lakini hata mitandaoni pia kwa hisia tunazojaribu kuzionyesha ni kile tunachojaribu kuionyesha dunia kwamba mtanzania ni mtu wa namna gani kupitia mtandao. Ibara ya 28 ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania yam waka 1977 kifungu cha kwanza, “Kila raia ana wajibu wa kulinda, kuhifadhi na kudumisha uhuru, mamlaka, ardhi na umoja wa taifa”

WASANII NA WANA MICHEZO Sanaa na michezo ni nyenzo muhimu sana katika kuhamasisha na kuchochea maendeleo. Mbali na kuimba, kuandika, kuigiza n.k kuhusu mapenzi na mambo mengine yanayoweza kuteka hisia na kukonga nyoyo za mashabiki lakini pia tusisahau kuwa kuna umuhimu mkubwa wa kutunga nyimbo, maigizo, hadithi n.k ambazo zitaleta hamasa kubwa na kuongeza chachu ya wananchi kupenda maendeleo na kushiriki shughuli za maendeleo maana hiki ndiyo kilio chetu kama taifa na kama tukiendelea hata kazi za wasanii zitongezeka motisha ili kufikia thamani inayolingana na kile kinachotolewa.

111

Tunaweza kukumbuka huko zamani wakati wa mwalimu Nyerere nyimbo nyingi zilitungwa na kuimbwa ili kusamasisha maendeleo. Pia tuwe makini na wachache miongoni mwetu wanaojaribu kupenyeza mbegu za chuki kupitia Sanaa na michezo iwe kwa tungo zenye kuchochea chuki au mmomonyoko wa maadili ya watanzani, hao tusiache kuwakemea bila aibu maana tukiwaonea aibu tutakuja kushtuka wametufikisha mahali amabapo hatuwezi kujinasua tena kutoka kwenye majanga. Kwa wale ndugu zangu wa Sanaa ya uchekeshaji tusiishie kuchekesha watu tu kwenye mambo ambayo mengine ni ya kipumbavu kiasi kwamba hamwezi kukaa kama familia mkatazama kazi ya msanii lakini tubuni mbinu pia za kuchekesha kwa namna ambazo zitaibua hisia za watu kuhusu msitakabari mzima wa maendeleo yetu ili tusitengeneze kizazi cha wajinga na wapumbavu wanaolelewa na Sanaa za kipuuzi. Vivyo hivyo kwa ndugu zangu wahamasishaji(motivational speakers and life coaches) tusiwahamasishe na kuwatia moyo watu kwa habari ya ustawi wao binafsi lakini tuwatie moyo kuwa wazalendo wa nchi yao na kuangalia namna wanawezakuunga mkono juhudi za maendeleo maana ndivyo watakavyoweza kutengeneza mazingira mazuri ya ustawi wa ndoto na maono yao. Vilabu vya michezo ya aina zote hususani mpira wa miguu, mpira wa kikapu, wakimbia riadha n.k tujitahidi pia kubuni njia ambazo zinaweza kuchochea moto wa maendeo kupitia michezo. Pia wananchi tujitoe kuunga mkono michezo ikibidi hata kwa kutoa pesa zetu ili

112 tuongeze nguvu kwenye michezo ambayo kwa sasa ni ajira pia. Tuchochee moto wa maendeleo ambao umekolea sana hivi sasa ili kutoa taswira njema ya nchi yetu kitaifa na kimataifa na tuweze kushinda hila za wale wachache wasiotutakia mema ambao hatuwezi kuwashinda kwa maeneo lakini kwa vitendo vya kimaendeleo.

VYOMBO VYA HABARI Nitoe wito na rai yangu kwa vyombo vyote vya habari kwa maana ya wamiliki na watangazaji au wandaaji wa vipindi. Ninatambua kazi kubwa inayofanywa na vyombo vya hivi lakini kwa pamoja tukishirikiana na watanzania tusitoe mwanya kwa habari ambazo hazileti afya kwa taifa letu ila tujitahidi kuwekeza kwenye habari zitakazoendelea kuibua shauku ya kuunga mkono juhudi za maendeleo ili tujenge nchi yetu. Tujitoe kwa hali na mali kusimama na Rais wetu, viongozi wa ngazi mbali mbali na watendaji wengine wa taasisi mbalimbali za serikali kuhakikisha taifa letu linapiga hatua zaidi kuelekea mahali pazuri zaidi patakapotupa fursa ya kufanya kazi vizrui zaidi. Vilevile tujilinde na watu wabaya ambao lengo lao ni kupenyeza habari mbaya zitakazotufanya tuondoke kwenye lengo letu ambalo ni kuliendeleza taifa letu. Lakini pia tuseme hapana kwa wana habari ambao wanaweza kutumiwa kwa namna moja ama nyingine kutuvuruga au kuwapa wananchi habari za kipotoshaji

113 ambazo zinaweza kuwaondolea utulivu na kuwafanya wasiiamini Serikali makini iliyoko madarakani chini ya Rais mzalendo, Kipenzi cha watanzania, mtetezi wa wanyonge, mchapa kazi, mwenye uchungu na watanzania, mtanguliza maslahi ya watanzania mbele, Rais jembe na tingatinga la maendeleo Rais John Joseph Pombe Magufuli.

TAASISI ZA DINI Ibara ya 3 ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania yam waka 1977 ibara ndogo ya kwanza, “Jamhuri ya Muungano ni nchi ya kidemokrasia nay a kijamaa, isiyokuwa na dini, yenye kufuata mfumo wa vyama vyingi vya siasa” Ibara ya 19 ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania yam waka 1977 ibara ndogo ya kwanza, “Kila mtu anastahili kuwa na uhuru wa mawazo, Imani na uchaguzi katika mambo ya dini, pamoja na uhuru wa watu kubadilisha dini au Imani yake” Nchi yetu haina dini lakini imetoa uhuru wa kikatiba wa haki ya kuabudu na haki na mtu kuwa na dini anayoitaka. Hiki ndicho kitu kilichopelekea uwepo wa dini na madhehebu mbalimbali ndani ya nchi yetu kila watu kwa imani yao. Vilevile pamoja na nchi yetu kutokuwa na dini lakini pia haijafunga milango ya kushirikiana na dinia au madhehebu mbalimbali katika mambo ya maendeleo yaani ustawi wa watu ndiyo maana imeruhusu mashirika na taasisi za dini kujenga shule, vituo vya afya n.k. Ni

114 vema taasisi za dini zikajitadi kwa kiwango kikubwa kuzingatia ustawi wa wananchi si katika mambo ya rohoni tu bali hata yale ya mwilini ambayo yatapelekea waumini wao au wahsirika wao kuimarika zaidi rohoni. Kwa njia hii Rais wetu na Serikali yake kuna mahali hatapata shida. Taasisi za dini zinapaswa kuwa kiunganishi kizuri kati ya waumini wake na Serikali kwa maana ya kuwafundisha waumini wao kuwa na utii kwa viongozi wa Serikali lakini pia umuhimu wa kushiriki kwenye miradi ya maendeleo na vilevile kuwakumbusha waumini kuwa serikali si adui wa wananchi kama baadhi ya wanasiasa wanavyofanya bali ni chombo kilichopewa dhamana ya kuhakikisha kunakuwa na ustawi wa wananchi kama katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania yam waka 1977 inavyosema kwenye ibara ya 8 ibara ndogo ya kwanza kifungu a, b, c na d:- (a),“Wananchi ndo msingi wa mamlaka yote, na Serikali itapata madaraka na mamlaka yake yote kutoka kwa wananchi kwa mujibu wa katiba hii” (b), “lengo kuu la Serikali litakuwa ni ustawi wa wananchi” (c), “Serikali itawajibika kwa wananchi” (d), “Wananchi watashiriki katika shughuli za Serikali yao kwa mujibu wa masharti ya katiba hii”

Nafikiri ifike wakati kabla hatujailaumu na kuishutumu Serikali kwa namna moja ama nyingine sisi pia tujue tuna

115 nafasi ya kufanya jambo. Tushirikiane na Serikali ili kuhakikisha mambo yanakwenda sawa. Tumuombee Rais. Tumshauri hata kama hajatuomba ushauri, si lazima kuitwa ikulu ila tunaweza kuandika barua za kushauri na kutoa mawazo yetu pia. Lakini si lazima kupeleka mawazo yetu ikulu lakini tukiwashauri vizuri wateule wa Rais ambao tuko karibu nao tutakuwa tumemshauri Rais maana wao wanamwakilisha yeye kwenye mamlaka za kiutendaji. Tusiwavumilie viongozi au waumini wenzetu wenzetu wa dini wanaotaka kupenyeza itikadi za kutufarakanisha kitu ambacho kinaweza kuvuruga amani na na umoja wetu hivyo tuwakemee kabla hawajafikiwa na mkono wa Serikali. Lakini tuone pia namna ambavyo katiba imetutambua basi na sisi tumpe ushirikiano Rais na Serikali yake ili mambo ya kimaendeleo ndani ya taifa letu yapate kusonga mbele. Kuna mambo ambayo tunapaswa kuhakiksha kama tasisi za dini tunasimama bega kwa bega na serikali kwa ajili ya ustawi wa wananchi miongoni mwao wakiwa ni wale ambao wapo kwenye taasisi zetu za dini. Kuna mambo kama elimu, afya, miradi ya maji, elimu ya uraia n.k huu ni wajibu wetu sote. Lakini pia tusichoke kuiunga mkono katika kukemea vitendo viouvu kama vile rushwa, madawa ya kulevya, wizi, uhaini n.k na mambo mengine mengi ambayo kushamiri kwake ndiyo kudhoofika kwa taifa letu kwenye nyanja mbalimbali. Cha muhimu sana tusichoke kuiombea nchi yetu na viongozi wetu vilevile tuwahimize waumini wetu kufanya hivyo kila siku katika sala na maombi yao.

116

ASASI ZA KIRAIA Asasi za kiraia pia zisibaki nyuma kusimama pamoja na Rais wetu pamoja na Serikali yake ya awamu ya tano katika kuhakikisha wananchi wanapata maendeleo. Niwapongeze kwa kazi kubwa ambayo mmekuwa mkiifanya lakini niwakumbushe kuwa tunayo kazi kubwa bado mbel yetu tusichoke kutoa elimu na kutoa muda wetu kushiriki mikakati na utekelezaji wa miradi ya maendeleo. Tuwe msitari wa mbele katika kuwaunga mkono viongozi wetu n ahata kuwasemea vizuri kwa wananchi. Tusiingie kwenye mikumbo ya ushabiki wa kisiasa ili tuepuke nchi yetu kuingia kwenye migogoro. Tuache vilivyosajiliwa kama vyama vya siasa vifanye siasa na sisi ambao ni asasi za kiraia tusimame na wananchi katika kuhakikisha maendeleo yanapatikana na wananchi wanakuwa na mazingira mazuri.

WAFANYA BIASHARA Tunao wajibu mkubwa wa kushiriki kwenye mikakati na mipango kazi ya uborehwaji wa mazingira yetu ya kibiashara maana kupitia kodi zetu ndiyo miradi mingi ya kimaendeleo inafadhiriwa. Hivyo basi tujue kwamba ikiwa tutajihusisha ni vitendo vyovyote ambavyo vitalegeza ushirika wetu na serikali maana yake kwa namna moja ama nyingine tutakuwa tunakwamisha maendeleo. Kama tunavyoona Rais amejitahidi kukaa na sisi na kututengenezea mazingira mazuri ya kujadili naye basi tusi muanguhshe ili tuweze kwenda mbele zaidi. Likitokea jambo lolote ni vyema kufuata utaratibu wa

117 kisheria tusifuate mikumbo ya wtu wachache wanaotaka kutumia njia zinazoweza kupelekea ghasia na vurugu kwa kuibua hisia za watu kwa namna isiyo sawasawa. Maana tukimuunga mkono rais kwa haya anayoyafanya tutafany biashara kwa urahisi maana miundombinu inayojenga itatusaidia kuokoa muda lakini pia kutufanya tuweze kufikika katika Nyanja zote za kimawasiliano na uchukuzi. Kwa namna moja ama nyingine kasi hii ya kimaendeleo itachangia sana ukuaji wa kibiashara.

WAKULIMA Wakulima tusibaki nyuma huu ndiyo wakati wa kilimo chenye tija na ambacho kitatupa hatua kimaendeleo. Tunaweza kuona namna ambavyo serikali inafanya kazi kwa bidii kupitia wizara ya kilimo ili kuhakikisha kilimo kinakaa sawa maana kilimo ndiyo uti wa mgongo wa uchumi wetu. Tujitokeze kutumia fursa mbalimbali za kilimo na kuunga mkono harakati mbalimbali za kilimo zinazobuniwa na wataalam mbali mbali kwa ajili ya kuwasaidia wakulima.

WANAFUNZI Wanafunzi hatupaswi kuwa nyuma maana tumeona mazuri yanayofanywa na serikali ya awamu ya tano kwa ajili yetu hata kama haijawa vile tunavyotaka walau sasa hata ambao waliondoa majina yao kwenye wale watakaopata elimu kwa sababu ya umaskini sasa wanaipata nah ii ndiyo sera ya elimu bure ya serikali ya

118 awamu ya tano chini ya tingatinga la maendeleo Rasi John Joseph Pombe Magufuli makishirikiana na Makamo wa Rais Mama Samia Suru na Waziri Mkuu makini na muwajibikaji Kassim Majaliwa na viongozi wengine wengi wenye njaa na kiu kubwa ya maendeleo kwa ajili ya wananchi wa Tanzania. Huu ni mwanzo tu ila kuna mengi mazuri yanakuja. Tusidanganyike tukajihusisha kwenye mambo ya kishenzi ambayo yatatufanya tukose eli na tukaligeuza taifa letu taifa la watu wajinga. Kwa fursa hii tuliyoipata ni muhimu kutambua kuwa na fursa adhimu na njia pekee ya kumuunga mkono Rais ni kuhakikisha tunajituma vizuri kwenye masomo yetu tukitambua kuwa elimu ni mkombozi wetu na kama tukiitafuta na kuipata sawasawa hatutakuwa watumwa wa watu wa mataifa mengine. Lakini pia tukipata elimu tutafanikiwa kujiokoa kutoka kwenye meno makali ya wajanja wachache wanaojinufaisha kwa mgongo wa ujinga wetu kwenye maeneo mbalimbali. VYAMA VYA SIASA NA WANA SIASA Kuwa mpinzani haina maana kupinga kila kitu lakini katika kuwa kwetu au kutambulika kwa baadhi ya vyama vya kisiasa isitusahaulishe hatima yetu ni moja na tunayo hatima ya kimaendeleo kama taifa na inapokuja kwenye hiyo hakuna chama, kabila dini wala chochote lakini sote tunakuwa wananchama wa maendeo na sera yetu na wimbo wetu unakuwa ni maendeleo. Tusiegemee kwenye upande tu wa kuifanya serikali ionekane haifanyi kazi lakini penye mazuri yanayofanyika tupongeze na

119 tuwahimize wananchi kuyalinda na kuyatunza. Hata kama unatatafuta nafasi ya kuongoza basi tufanye siasa zenye tija na si zile zitakazopelekea vurugu na machafuko. Tusitamani kabisa vurugu na machafuko maana tunayo mifano ya majirani zetu namna ambavyo mewagharimu na wengine inavyoendelea kuwagharimu. Sikatai suala la kuikosoa Serikali na Rais kwa mujibu wa mambo ya kisiasa lakini suing mkono na sitabariki jambo lolote linalomvua nguo Rais wetu a Serikali yetu kwa maslahi ya mwanasiasa fulani au kundi fulani la kisiasa ambalo linapambana kuitafuta maslahi yake lenyewe na si wananchi. Maana unapomchafua Rais umeichafua nchi na umewachafua wananchi pia. Ninaamini ziko njia nzuri tu za kufanya siasa pasipo kuiathiri nchi wala wananchi nab ado tukaeleweka nafikiri tuzitumie hizo ikiwa kweli tuna nia njema na mapenzi mema na taifa letu.

FAMILIA Ninapozungumzia familia ninazungumzia sehemu ya chini kabisa ya uongozi wan chi yetu baada ya kutoka kwenye sehemu ya mtu mmoja mmoja ambayo inachangia uwepo wa sisi kama taifa. Ninaziomba familia pia zishiriki katika kumuunga mkono Rais kwanza kwa kumuombea heri na fanaka katika kipindi tulichompa kutuongoza lakini pia kupitia mkazo wa malezi bora kwa watoto. Ukiona mtoto haheshimu wazazi wake nyumbani ni ngumusana kumheshimu kiongozi. Hili litusaidie pia kuona umuhimu wa kuwafundisha watoto wetu kuheshimu viongozi tangu wakiwa wadogo wajue Rais ni

120 nani nchi ni nini ikibidi kila mzazi awe na picha ya Rais aliyepo madarkani kwa wakati huska na picha inayoonesha nchi yetu ilivyo na mikoa yake ili watoto wetu waijue nchi yetu. Tuwakanye na kuwaonya watoto wetu kutojihusisha na mambo ambayo hayaleti afya kwenye taifa letu. Maana yakiwako mambo ya uvumi nay a hatari lakini yasiyo ya kweli wanaoyachoea kwa namna moja ama nyingine baadhi ni watoto wetu baadhi ni mama zetu n.k Kwa kifupi ninamaanisha kuwa kama familia zitahakikisha zinasimama pamoja kumuunga mkono Rais pamoja na watengaji wake basi tunao ujasiri wa kupinga hatua za kimaendeleo kifua mbele. Ni vizuri kukumbushana, kurekebishana na kukemeana katika ngazi ya familia kuhusiana na masuala mazima ya ustawi wa taifa letu.

WAFANYA KAZI Wafanya kazi tujitoe kwa bidi tujue kazi tunazozifanya ni kwa ajili yetu yaani tunajenga nchi yetu wenyewe. Kwa kulitambua hili ni muhimu tukafanya kazi kizalendo zaidi na kwa uhuru bila hofu ya kutumbuliwa. Lakini tusipolielewa hili tunaweza kupambana na misukosuko n ahata kutumbuliwa pia. Tukifanya kazi kwa weredi na kwa bidi ni rahisi kutengeneza mazingira ya kuboreshwa kwa stahiki zetu lakini tukiendekeza vitendo vya rushwa na uzembe maana yake tunajiharibia wenyewe kwa kudahani tunawahabia wananchi kumbe hata sisi wenyewe ni wananchi, watoto wetu, wake na waume zetu,

121 wajomba zetu, baba zetu na mama zetu, majirani zetu n.k ni wananchi pia.

WAVUVI Wavuvi pia ni muhimu tukamuunga mkono ili kuwezesha urahisi wa kuwekwa saawa kwa mikakati ambayo itatusaidia kunufaika na rasilimali zetu lakini pia kufanya urithi wa samamk tulionao uendelee kuwepo hata kwa ajili ya vizazi vijavyo.

WAFUGAJI Wafugaji pia tunayo sababu ya kumuunga mkono rais maana bila ushiriki wetu itakuwa ni vigumu kuwezesha mikakati na sela zilizolenga kuboresha ufugaji na mazao yanayotoka na ufugaji kufanyiwa kazi ipasavyo ili pia nchi yetu iweze kusonga mbele kupitia mchango wa wavuvi.

VIJANA Kundi hili nimeliandika hapa pia maana ni kundi linalokabiliwa na hatari nyingi. Lakini mbali na hayo yote vijana ni nguvu kazi ya Taifa maana yake ni kuwa Taifa lisilo na vijana ni taifa maskini na ambalo leo yake haipo. Tusikubali kutumiwa vibaya na watu wasio na nia njema lakini tuwe na utayari wa kujitoa kushiriki shughuli za maendeleo maana tunaye Rais anayetambua nafai ya vija.

122

Tunaweza kuona kwenye uteuzi wa nafasi mbalimbali kuna vijana wengi wanatuwakilisha hivyo basi tumuunge mkono kwenye mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na kutorishika kukaa tu ila tujitume kwenye kazi mbalimbali za kiuzalishaji mali ili taifa letu liwe na uchumi mzuri.

123

SURA YA KUMI NA MOJA NUKUU ZA RAIS MAGUFULI

1. Ninafanya haya ndugu zangu kwa ajili yenu. Mlinichagua bure ni lazima niwahudumie bure. Mafisadi wameifikisha mahali pabaya nchi yetu nchi hii ni tajiri haitakiwi kuchezewa.

2. Ni aibu fedha zinatafutwa na watanzania kwa ajili ya kupata maji halafu fedha hizo zinapotea.

3. Sikuchaguliwa kwa ajili ya kuonekana sura nzuri si ajabu hata mke wangu ananiona sura yangu mbaya lakini nataka tufanye kazi kwa ajili ya watanzania. 4. Tuache kufikiria sana kwamba misaada ya nje ndiyo itatusaidia. 5. Katika Afrika kutoka kaskazini mpaka kusini kutoka mashariki mpaka magharibi tukisimama pamoja kwa lengo moja tu la neno maendeleo nchi za Afrika tunaweza tukafanya maajabu. 6. Ni lazima sasa waafrika tuamke inawezekana migogoro mingine inaletelezwa kwa makusudi kwa sababu tunaonekana kuwa dhaifu sana. 7. Hakuna kiongozi duniani atakayekuja awe anawagawia hela mfukoni. 8. Ni kawaida duniani unaweza ukafanya kazi nzuri watu wengine wasione uzuri wa kazi yako. Duniani

124

tumeumbwa hivyo wako watu ambao ni vigumu kushukuru, wako watu ambao hata ungewabeba kiasi gani ni vigumu kushukuru, wako watu haka kama ungemvushwa kwenye mto ni vigumu kushukuru. 9. Ndugu zangu naomba mniamini mambo ya mateso kwa wananchi hayana chama. 10. Mimi nimeamua kuwa sadaka ya watanzania 11. Kazi hii ni ngumu ni ya ajabu kila mmoja anajitahidi haya tunayoyafanya tusiyafanye lakini nawashukuru mnaendelea kuniombea. Endeleeni kutuombea lengo letu ni la kuwasiaidia ninyi lengo letu ni kuwasaidia ninyi. 12. Mtu akijaribu kusimamia ukweli anachukiwa. 13. Ukweli huwa unabaki ni ukweli unaweza ukauchelewesha, unaweza ukaufungafunga lakini ukweli huwa unajulikana. 14. Huu si wakati wa kufanya upumbavu nasema ukweli ndani ya utawala wangu tunataka mambo yaende sawasawa. 15. Saa nyingine huwa sipendi kuchukia Mungu anisamehe tu lakini mambo mengine yanaudhi kweli. 16. Ni lazima tufike amhali tuambizane ukweli. 17. Lazima tujifunze kuwahudumia hawa akina mama na akina baba watu maskini. 18. Ndugu zangu kazi ya uongozi ni msalaba ni mateso. 19. Ninaomba ndugu zangu tuishi kwa amani na upendo mkubwa.

125

20. Ni jambo la kujitoa na kufanya na mimi nawaambia ndugu zangu watanzania tunaweza sana. Wala msije mkawa na wasiwasi tunaweza na fedha zipo. 21. Hatutajikomboa kwa kutegemea wao ni lazima tuamue. 22. Wafadhili ni wewe una madini na kila kitu 23. Tatizo letu lilikuwa kushindwa kujiamini. 24. Msema kweli ni mpenzi wa Mungu na mi sitaki kwenda kuhukumiwa kwa kuyafumbia macho yasiyoijenga Tanzania. 25. Deni langu kwenu ni kufanya kazi tu, mchana nitafanya kazi usiku nitafanya kazi, nikiwa nimekaa nitafanya kazi, nikichuchumaa nitafanya kazi, nilala kifudifudi nitafanya kazi, nikiwa chali nitafanya kazi, lengo langu ni kuifanya Tanzania iwe Tanzania ya maendeleo ya kweli. 26. Muendelee kuniombea ili nitakapopata urais kwanaza nisiswe na kiburi, nisije nikawa nimesahau nilikotoka, siku zote nimtangulize Mungu, niwaheshimu watanzania wote, nisiwabague kutokana na vyama vyao, nisiwabague kutokana na dini zao wala nisiwabague kutokana na makabila yao mimi nifanye kazi kazi kazi kazi kazi. 27. Nataka tuwe na mbadiliko ya kweli. 28. Hiyo ndiyo serikali ninayotaka kuiunda serikali yenye kujali shida za wananchi, serikali inayojali maisha ya watanzania hasa watanzania wanyonge.

126

SURA YA KUMI NA MBILI TUIOMBEE NCHI YETU Tunapaswa kusimama imara na kumwombea Rais wetu nan chi yetu yote kwa ujumla. Maana sisi kama wanadamu hatuwezi lakini kwa mkono wa Mungu hatuwezi kushindwa. Tunapomuombea raisi tukumbuke kuliombea taifa letu pia na viongozi wengine. Nitoe wito kwa watanzania wenzangu kuliombea taifa letu na viongozi wake pamoja na wananchi wote kwa ujumla ili Mungu atutangulie na kutufanikisha katika yote. Katiba ya nchi yetu inasema wazi kuwa nchi yetu haina dini. Kutokuwa na dini si tatizo lakini tatizo ni kutokuwa na Mungu. Ninaamini kuwa taifa letu linaamini katika Mungu na ndiyo maana limetoa haki na uhuru wake katika kuabudu kila mmoja kwa Imani yake. Katika maombi haya kumbuka kuwaombea viongozi wetu, Serikali, Bunge, mahakama, mipaka ya nchi, rasilimali zetu, Amani, upendo, mshikamano n.k maana maeneo haya yakikaa sawasawa tunasonga mbele bila shida yoyote. Kama kweli unaitakaia nchi yako mema basi utachukua muda kuiombea maana mengine yanayotokea unaweza kuona tatizo ni viongozi au wananchi wenyewe kumbe tatizo ni mambo ya ulimwengu wa roho

127

MAMBO YA KUOMBEA 1. Ombea nchi yote kwa ujumla mpaka rasilimali a. katika hili eneo omba toba kwa ajili ya nchi yetu mambo ambayoyamefanyika ndani yake b. Ombea ardhi yetu iendelee kuwa na rutuba na ile iliyochoka ipate rutuba. c. Ombea rasilimali kama madini. Mshukuru Mungu kwa ajili ya zawadi na utajiri huu. Mwambie Mungu ayafanye kuwa Baraka kwetu na si chanzo cha laana. d. Ombea mito, maziwa, bahari, misitu n.k ambayo Mungu ametujalia kuwa nayo. e. Ombea mikoa , wilaya, tarafa, vitongoji, vijiji na mitaa. 2. Omba kwa ajili ya viongozi wa ngazi zote kuanzia rais mpaka mjumbe wa nyumba kumi. 3. Ombea muungano uendelee kuimarika. 4. Ombea watendaji wa Serikali katika sekta mbalimbali watende haki, wajitenge na rushwa na watekeleze majukumu yao kama inavyotakiwa. 5. Ombea wananchi wote wakulima, wafanya biashara, wafanya kazi, watoto na vijana n ahata wagonjwa pia na wasio na cha kufanya Mungu awakumbuke. 6. Liombee Bunge letu tukufu 7. Ombea mahakama

128

8. Omba kwa ajili ya nchi jirani zetu na bara la Afrika kwaujumla na dunia yote ili kusiwe na mambo ambayo yatatuathiri na sisi. 9. Ombea uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu pia uwe wa huru, haki na ufanyike kwa Amani. 10. Ombea hifadhi za Taifa na vivutio mbalimbali vya utalii tulivyonavyo. 11. Ombea bandari zetu: Bandari ya Dar es Salaam, Bandari ya Mtwara, Bandari ya Tanga na Bandari nyinginezo zilizoko kwenye maziwa mbali mbali nchini.

129

REJEA Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania yam waka 1977 www.youtube.com https://en.wikipedia.org

130