NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ____________ MAJADILIANO YA BUNGE ___________ MKUTANO WA SABA Kikao cha Ishirini na Saba – Tarehe 17 Mei, 2017 (Bunge Lilianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Naibu Spika (Mhe. Dkt. Tulia Ackson) Alisoma Dua NAIBU SPIKA: Tukae. Katibu. NDG. THEONEST RUHILABAKE – KATIBU MEZANI: HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na:- WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji kwa mwaka wa fedha 2017/2018. MHE. MUSSA R. SIMA (K.n.y. MWENYEKITI WA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA VIWANDA, BIASHARA NA MAZINGIRA): Taarifa ya Kamati ya Viwanda, Biashara na Mazingira kuhusu utekelezaji wa majukumu ya Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji kwa mwaka wa fedha 2016/2017 pamoja na Maoni ya Kamati kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2017/2018. 1 NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) MHE. CECIL D. MWAMBE (K.n.y. MSEMAJI MKUU WA KAMBI YA UPINZANI KUHUSU WIZARA YA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI): Taarifa ya Msemaji Mkuu wa Kambi ya Upinzani kuhusu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji juu ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2017/2018. NAIBU SPIKA: Katibu. NDG. THEONEST RUHILABAKE – KATIBU MEZANI: MASWALI NA MAJIBU NAIBU SPIKA: Waheshimwa Wabunge, tutaanza na Ofisi ya Rais (TAMISEMI), Mheshimiwa Bernadeta Kasabago Mushashu, Mbunge wa Viti Maalum, kwa niaba yake Mheshimiwa Josephine Genzabuke. Na. 219 Madai ya Wazabuni MHE. JOSEPHINE J. GENZABUKE (K.n.y. MHE. BERNADETA K. MUSHASHU) aliuliza:- Wazabuni wanaotoa huduma shuleni wanaidai Serikali fedha nyingi kwa huduma walizotoa miaka iliyopita. (a) Je, Serikali inadaiwa fedha kiasi gani na kwa miaka ipi na wazabuni hao? (b) Je, ni lini madai hayo yatalipwa? NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais (TAMISEMI) majibu. 2 NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA alijibu:- Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (TAMISEMI), naomba kujibu swali la Mheshimiwa Bernadeta Kasabago Mushashu, Mbunge wa Viti Maalum, lenye sehemu (a) na (b) kama ifuatavyo:- (a) Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli kuwa wapo wazabuni mbalimbali ambao wanaidai Serikali baada ya kutoa huduma Serikalini. Wapo wazabuni waliotoa huduma za vyakula katika shule zenye wanafunzi wenye mahitaji maalum za msingi na shule za bweni za sekondari na wazabuni waliochapisha na kusambaza vitabu shuleni. Kiasi cha shilingi bilioni 54.86 zinadaiwa na wazabuni waliotoa huduma ya chakula, ambapo kiasi cha shilingi bilioni 9.907 ni za wazabuni waliotoa huduma ya uchapishaji na usambazaji wa vitabu vya shule za msingi. Hivyo jumla ya deni ni shilingi bilioni 64.767. (b) Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kuliarifu Bunge lako Tukufu kuwa madeni haya ni yale yaliyojitokeza kabla ya Serikali kuanza kutekeleza elimu msingi bila malipo. Kwa kutambua umuhimu wa kuwalipa wazabuni hawa Serikali kupitia Wizara ya Fedha imeshalipa jumla ya shilingi bilioni 13.239 hadi kufikia Mei, 2016. Wazabuni wengi ambao madeni yao hayajalipwa hadi sasa wataendelea kulipwa kwa awamu kwa kadri ya uwezo wa Serikali na upatikanaji wa fedha. Mheshimiwa Naibu Spika, tunawaomba wazabuni hawa wawe na uvumilivu kama ambavyo wamekuwa wakifanya wakati Serikali ikiendelea kulipa madeni haya ikiwa ni pamoja na madeni mengine ya ndani. NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Josephine Genzabuke, swali la nyongeza. MHE. JOSEPHINE J. GENZABUKE: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kwa kunipa nafasi ya kuuliza maswali. Pamoja 3 NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) na majibu mazuri ya Mheshimiwa Naibu Waziri, nina maswali mawili ya nyongeza. Mheshimiwa Naibu Spika, swali la kwanza, kwa kuwa wapo wazabuni ambao walitoa huduma hiyo ya kusambaza vyakula na vifaa mbalimbali katika shule zetu zikiwemo na shule za watoto wenye ulemavu, lakini wazabuni hao wengi wao wana miaka zaidi ya mitano hawajaweza kulipwa pesa yao na walio wengi wamekopa benki na wengine nyumba zao zimeuzwa na wengine ziko hatarini kuuzwa. Je, Serikali iko tayari kufanya uhakiki wa madeni hayo ili kuweza kuwalipa wazabuni hao? (Makofi) Mheshimiwa Naibu Spika, swali langu la pili, kwa kuwa wapo wazabuni wapya ambao walitoa huduma ya kusambaza vyakula shuleni wao wamelipwa lakini wazabuni wa zamani hawajalipwa. Je, Serikali iko tayari kuwalipa wazabuni wa zamani ambao walitoa huduma ya kusambaza vyakula shuleni ambao hawajalipwa lakini wapya wamelipwa? (Makofi) NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais (TAMISEMI), majibu. NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu swali la kwanza la kufanya uhakiki wa madeni haya ili walipwe, ndiyo maana nimesema kwamba ni kweli, kuna madeni mbalimbali hasa wazabuni waliotoa vyakula katika shule zetu kabla programu ya elimu bila malipo kuanza. Jambo hili kweli limesababisha wazabuni wengi kupata mtikisiko lakini ndiyo maana ilibidi Serikali kuyapitia madeni haya yote tukijua wazi kwamba lazima kuna mengine siyo sahihi maana katikati hapo tulibaini baadhi ya madeni mengine ni hewa. Kwa hiyo, Serikali imefanya mchakato wa ku-analyse madeni yote haya ili kutambua deni halisi la Serikali. Naomba niwahakikishie Waheshimiwa Wabunge na wazabuni wote waliotoa vyakula shuleni kwamba Serikali itafanya kila liwezekanalo kuwalipa. 4 NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) Mheshimiwa Naibu Spika, lakini katika hii concern kwa nini wazabuni wapya wanalipwa lakini wa zamani hawajalipwa ni kama nilivyosema kwamba utaratibu wa sasa tunapeleka fedha moja kwa moja kule shuleni. Kwa hiyo, kila mwezi mgao wa Serikali ukipeleka kule na fedha ya chakula inakuwepo. Ndiyo maana sasa hivi sitarajii sana kuona kwamba kuna wazabuni watadai kwa sababu fedha zote ambazo zinatakiwa zielekezwe katika ulipaji wa chakula tunazipeleka kila mwezi. Kwa hiyo, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba Serikali tunalibeba na sisi kama Watanzania na Serikali tutahakikisha kwamba wazabuni wetu wa ndani lazima tuwalinde ili waendelee kufanya biashara yao kwa sababu ndiyo watajenga uchumi wao katika nchi yetu hii. NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Lubeleje, swali la nyongeza. MHE. GEORGE M. LUBELEJE: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi ili niulize swali moja la nyongeza. Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kuwa wazabuni wanaohudumia chakula Mpwapwa High School, Mazai Girls’ School pamoja na Berege Secondary School form five na six sasa ni zaidi ya miaka miwili hawajalipwa na bado wanahudumia na wamekopa benki. Mheshimiwa Naibu Waziri amefika Mpwapwa sekondari na ameona hali ilivyo na wanataka kukamatiwa nyumba, je, hawa wazabuni watalipwa lini? NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais (TAMISEMI), majibu. NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Lubeleje, Senior MP wa Bunge hili kama ifuatavyo:- 5 NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli na kwa bahati mbaya kwa Halmashauri ya Mpwapwa siyo kesi ya wazabuni wa chakula peke yake isipokuwa kuna kesi ya wakandarasi mbalimbali ambao wamefanya kazi pale Mpwapwa lakini bado hawajalipwa. Hili napenda hasa nimuelekeze Mkurugenzi wetu wa Halmashauri ya Mpwapwa kwamba madeni mengine ambayo hayajalipwa ni suala la kuangalia Menejimenti ya Kurugenzi yake jinsi gani itafanya kuweza kuyalipa. Kwa hiyo, naomba nimhakikishie Mheshimiwa Lubeleje kwamba Mpwapwa ndiyo maeneo ya priority kwa sababu ofisini kwangu hata watu wa CRDB walifika kulalamikia Halmashauri ya Mpwapwa. Hata hivyo, ukiachia hizo fedha kutoenda lakini kuna mambo mengine ya ziada lazima tuyasimamie. Kwa hiyo, naomba nimhakikishie kwamba tutafanya kila liwezekanalo hasa kwa wazabuni wa Mpwapwa na maeneo mengine ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tuweze kuwalipa fedha hizi ili wasije wakataifishiwa mali zao na mabenki ambazo ziliwekwa kama dhamana wakati wanachukua mikopo. (Makofi) NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Sikudhani Chikambo, swali fupi. MHE. SIKUDHANI Y. CHIKAMBO: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Pamoja na majibu mazuri ya Naibu Waziri lakini napenda afahamu kwamba tunapozungumzia wazabuni tusisahau kwamba tunawazungumzia wafanyabiashara. Mara nyingi kama walivyosema wenzangu wafanyabiashara hawa wanapata pesa zao kutoka kwenye mabenki lakini maelezo yake anasema kwamba wale ambao hawajalipwa watalipwa pindi Serikali inapopata pesa. Napenda kujua ni lini? Ni vizuri jambo hili sasa likawekewa mkakati. NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri wa Fedha na Mipango majibu. NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali yetu inatambua umuhimu wa kuwalipa 6 NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) wazabuni hawa lakini kama alivyosema Mheshimwa Naibu Waziri wa TAMISEMI kwamba sasa hivi tuliji-engage kwenye kuyahakiki madeni haya. Waheshimiwa Wabunge, naomba niwaambie jambo moja kwamba Serikali ina nia njema. Tulipokea madeni haya kwa ajili ya shule tu ya shilingi bilioni 21.64 baada ya uhakiki tumekuta ni shilingi bilioni sita tu ambazo ni halali. Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, ndiyo maana Serikali inaomba muda maalum ili tuweze kumalizia uhakiki. Hii itasaidia Serikali kulipa yale madeni ambayo ni halali kwa ajili ya wazabuni waliotoa huduma na siyo kuwahi kulipa wakati kuna vitu vingine vya kufanya na tutajikuta tunalipa madeni hewa. Tunasisitiza dhamira ya Serikali ni njema na tutalipa madeni yote yale ambayo ni halali tu. NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Waziri, mtusaidie basi hayo madeni ambayo yako halali myalipe kwa sababu malalamiko yako mengi sana. Wabunge wanaandikiwa barua
Details
-
File Typepdf
-
Upload Time-
-
Content LanguagesEnglish
-
Upload UserAnonymous/Not logged-in
-
File Pages392 Page
-
File Size-