19 APRILI, 2013 BUNGE LA TANZANIA ________________ MAJADILIANO YA BUNGE ___________________ MKUTANO WA KUMI NA MOJA Kikao cha Tisa - Tarehe 19 Aprili, 2013 (Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Spika (Mhe. Anne S. Makinda) Alisoma Dua HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI Hati Zifuatazo Ziliwasilishwa Mezani na:- NAIBU WAZIRI WA KILIMO, CHAKULA NA USHIRIKA: Randama za Makadirio ya Matumizi ya Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika kwa Mwaka wa Fedha 2013/2014. WAZIRI WA NCHI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS, MAZINGIRA NA MUUNGANO: Hotuba ya Bajeti ya Waziri wa Nchi,Ofisi ya Makamu, Mazingira na Muungano, kwa mwaka wa fedha 2013/2014. 1 19 APRILI, 2013 MHE. FAKHARIA KHAMIS SHOMARI (K.n.y. MWENYEKITI WA KAMATI YA KATIBA, SHERIA NA UTAWALA): Taarifa ya Mwenyekiti wa Kamati ya Katiba, Sheria na Utawala Kuhusu Utekelezaji wa Majukumu ya Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano, kwa Mwaka wa Fedha 2013/2014. MHE. ESTER A. BULAYA (K.n.y. MWENYEKITI WA KAMATI YA ARDHI, MALIASILI NA MAZINGIRA): Taarifa ya Mwenyekiti wa Kamati ya Ardhi, Maliasili na Mazingira Kuhusu Utekelezaji wa Majukumu ya Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira, kwa Mwaka wa Fedha 2013/2014. MHE.PAULINE P. GEKUL (K.n.y.MSEMAJI MKUU WA KAMBI YA UPINZANI KWA OFISI YA MAKAMU WA RAIS, MUUNGANO: Taarifa ya Msemaji Mkuu wa Kambi ya Upinzani kwa Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano Kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi hiyo kwa Mwaka wa Fedha 2013/2014. MHE. CECILIA D. PARESSO (K.n.y. MSEMAJI MKUU WA KAMBI YA UPINZANI WA OFISI YA MAKAMU WA RAIS, MAZINGIRA: Taarifa ya Msemaji Mkuu wa Kambi ya Upinzani kwa Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira Kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi hiyo kwa Mwaka wa Fedha 2013/2014. 2 19 APRILI, 2013 MASWALI NA MAJIBU Na. 66 Kumaliza Tatizo la Madawati MHE. SARA M. ALLY aliuliza:- Kuna uhaba mkubwa wa madawati katika shule za msingi hali inayochangia wanafunzi kutokufanya vizuri katika masomo hayo:- Je, kwa nini Serikali haitoi kibali cha kuvuna miti ya kutosha na kutambua mafundi Seremala katika Halmashauri na kuwapa kazi ya kutengeneza madawati ili kumaliza tataizo hilo? NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (ELIMU) alijibu:- Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri Mkuu, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Sara Msafiri Ally kama ifuatavyo. Serikali inatambua umuhimu wa kuwa na madawati ya kutosha katika shule ili kuboresha mazingira ya kujifunzia na kufundishia. Hadi mwezi machi, 2013 shule za msingi na za Serikali zilikuwa zina mahitaji ya madawati 3,339,678; yaliyopo ni 2,029,310 na upungufu ni 1,310,675. Mheshimiwa Spika, Serikali imetoa fursa ya uvunaji wa miti ya asili na kupandwa kwa shughuli mbalimbali za kijamii ikiwa ni pamoja na utengenezaji wa madawati kwa ajili ya shule. Ili kudhibiti uvunaji holela Halmashauri zinatakiwa kufuata taratibu zilizowekwa za uvunaji misitu ikiwa ni pamoja kuomba vibali kutoka katika mamlaka husika katika Wilaya. Aidha, kutekeleza miradi ya kijamii Serikali imekuwa inasisitiza kutoa kipaumbele kutumia mafundi wenye sifa wa maeneo husika ikiwa ni sehemu ya ajira na kuinua kipato cha wanajamii wa maeneo miradi inapotekelezwa. 3 19 APRILI, 2013 Mheshimiwa Spika, katika juhudi za kumaliza tatizo la madawati nchini, Serikali imekuwa inapeleka fedha katika Halmashauri kwa ajili ya ununuzi na utengenezaji wa madawati. Mwaka 2010/2011 shilingi bilioni 3 zilipelekwa katika Halmashauri zote kwa ajili ya madawati ambapo Mkoa wa Mara ulipata shilingi milioni 197 na mwaka 2012/2013 shilingi bilioni 1 zilipelekwa katika Halmashauri zote kwa ajili ya madawati na Mkoa wa Mara ulipata milioni 68. Aidha, Serikali itatumia shilingi bilioni 18.4 zilizotokana na fidia ya ununuzi wa rada kwa ajili ununuzi wa madawati kwa Halmashauri zote nchini. Mheshimiwa Spika, Serikali inahimiza Mamlaka ya Serikali za Mitaa kutenga fedha katika mipango ya Bajeti kwa ajili ya miundombinu mbalimbali ya shule ikiwemo madawati na kuhakikisha fedha zinatolewa kwa ajili hiyo zinatumika ipasavyo. (Makofi) MHE. SARA M. ALLY: Mheshimiwa Spika,tumeshuhudia uvunaji wa miti na usafirishaji wa magogo nje ya nchi kupitia bandari ya Dar es salaam. Kwa nini Serikali isisitishe usafirishaji wa magogo nje ya nchi hadi hapo wanafunzi wote watakapo jitosheleza kwa madawati? La pili, kwa kuwa Serikali imekuja na mpango mpya wa kuhakikisha kila mwanafunzi anakaa kwenye dawati lake. Je, ni mkakati gani umeandaliwa na Serikali ili kuhakikisha kila mwanafunzi anafaidika na mpango huo? SPIKA: Waziri wa magogo simwoni lakini Naibu Waziri hebu jibu huko, ninaona ana wasiwasi kuzuia magogo ya wenzie, Mheshimiwa nani atajibu suala la magogo? Mheshimiwa Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii. 4 19 APRILI, 2013 NAIBU WAZIRI, MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Spika, Serikali inatambua kuwepo kwa magogo na magogo yapo ya aina mbili yale yanayopatikana kwa njia halali na yale ambayo yanapatikana kwa njia ambayo siyo halali na hatua mbali mbali zinachukuliwa ikiwa ni pamoja na kufanya msako na kuyakamata. Serikali imepiga marufuku na ninaomba nirudie kuwa, tumepiga marufuku usafirishaji wa aina yoyote wa magogo kwenda nje ya nchi kwasababu tungependa bidhaa zote za maliasili kwanza ziwekewe thamani hapa nchini kabla ya kusafirishwa nje ya nchi. (Makofi) SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri majibu ya sehemu nyingine. NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (ELIMU): Mheshimiwa Spika, ni kweli kuwa shule zetu zote za msingi na Serikali zina mahitaji makubwa ya madawati ili kutosheleza watoto wetu wote kukaa kwenye madawati kama ambavyo tunatarajia iwe. Kwa sasa mkakati tulio nao ni kuhakikisha kwamba tunaboresha upatikanaji wa madawati na kama ambavyo nimetoa kwenye jibu la msingi mahitaji ya shule za msingi, lakini pia katika eneo la sekondari mahitaji ya madawati sasa hivi ni milioni moja laki sita na arobaini na nane elfu, mia nane hamsini nane yaliyopo sasa hivi ni milioni moja laki mbili thelathini na moja elfu, mia nne arobaini na tunao upungufu wa madawati laki nne na kumi na saba elfu mia nne kumi na nane. Mheshimiwa Spika, kwa upungufu huu wa maeneo yote mawili na kwa kuwa tumetoa Mamlaka hizi kwa Serikali za Mitaa, kwa maana ya Halmashauri zote nchini ambazo zinamiliki shule hizi, zinao uwezo wa kuratibu vizuri fedha wanazojitengea kwenye Bajeti yao lakini ambazo sisi TAMISEMI huwa tunazipeleka kama nyongeza lakini pia kutumia Maliasili kwa wale ambao wana misitu hiyo, kuvuna 5 19 APRILI, 2013 mbao kwa taratibu zilizopo na nilipokuwa ninatoa mchango katika Bajeti ya Waziri Mkuu nilieleza kuwa Kamati ya uvunaji ya misitu iko katika kila Halmashauri na Mwenyekiti wa Kamati hiyo ni Mkuu wa Wilaya katika Halmashauri husika. Mheshimiwa Spika, kwa hiyo jambo hili halina matatizo na mkakati huu tukiusimamia wote kwa pamoja tunaweza kufanikiwa kuondoa tatizo la madawati nchini. (Makofi) MHE. ENG. RAMO M. MAKANI: Mheshimiwa Spika, ninakushukuru kwa kunipa fursa hii ya kuuliza swali la nyongeza. Hivi karibuni Serikali ilifanya operasheni maalum katika Wilaya ya Tunduru kupitia Wizara ya Malliasili operesheni ambayo ilipelekea uvunaji au ukamataji wa tani nyingi tu za mbao ambazo mpaka sasa zimelundikwa katika Ofisi ya Halmashauri na kwenye Ofisi ya Maliasili pale Wilayani. Je, Serikali itachukua hatua mahsusi sasa kutumia mbao zile zilizoko pale kwa ajili ya kupunguza angalau kidogo tatizo la madawati katika Halmashauri ya Tunduru? NAIBU WAZIRI, MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Spika, tumekuwa na utaratibu ambao ni endelevu kwamba shule au taasisi zinazohusika zinaruhusiwa kuomba vibali vya uvunaji wa mbao na hasa inapokuwa kwa ajili ya utengenezaji wa madawati, jambo ambalo kwanza tunalichukulia kama uongezaji wa thamani wa mbao na kwa ajili ya kuendeleza elimu hapa nchini. Ninaomba nilithibitishie Bunge lako Tukufu kuwa maombi hayo yatapewa kipaumbele. (Makofi) MHE. CHRITOWAJA G. MTINDA: Mheshimiwa Spika, ninaomba kuuliza swali moja la nyongeza. Kwa kuwa Naibu Waziri amekiri kuwa kuna upungufu mkubwa wa madawati na hili ni tatizo kwa shule zote Tanzania nzima. Je, Waziri haoni sasa kuwa kuna haja ya kutoa agizo maalum kwa Halmashauri zote ziweze kutoa tenda ya kutengeneza madawati katika vyuo vyetu vya VETA kuliko kutoa tenda kwa watu binafsi ambao wanatengeneza madawati kwa bei kubwa zaidi? 6 19 APRILI, 2013 NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (ELIMU): Mheshimiwa Spika, ni kweli na kama nilivyoeleza kwenye swali la msingi na namna ambavyo alikuwa amelihitaji Mheshimiwa Msafiri kuwatumia wajasiriamali kwenye eneo hilo. Haya mambo yote ni maamuzi ya Halmashauri yenyewe na kwa sasa tunavyo Vyuo Vya Ufundi, ziko Halmashauri zina Vyuo Vya Ufundi, lakini pia tuna VETA katika kila Mkoa. Kwa hiyo, ni jukumu la Halmashauri yenyewe kutambua umuhimu wa au kupeleka VETA kutengeneza madawati yote kwa pamoja au kutumia wajasiriamali walioko katika Halmashauri ambao wana uwezo tayari na walishasoma katika vyuo vya VETA ili watengeneze kwa gharama nafuu. (Makofi) Mheshimiwa Spika, jambo hili ni mipango ya Halmashuri yenyewe. (Makofi) SPIKA: Tunaendelea na swali linalofuata Mheshimiwa Meshack Opulukwa. Na. 67 Ukosefu wa Maji Safi MHE. MESHACK J. OPULUKWA aliuliza:- Mheshimiwa Spika, kabla ya kuuliza swali langu nilikuwa ninaomba Bunge lako Tukufu kulipa taarifa kwamba kumetokea mafuriko makubwa sana Meatu na mpaka tunapoongea hivi zaidi ya nyumba kumi zimeanguka na watu wamepoteza makazi. Aidha zaidi ya nyumba karibu 100 ziko mbioni kuanguka kutokana na kuwa na unyevunyevu mwingi kwenye matofali. 7 19 APRILI, 2013 Nilikuwa ninaomba Serikali yote kwasababu iko hapa iweze kuliangalia hili kwa ajili ya kuweza
Details
-
File Typepdf
-
Upload Time-
-
Content LanguagesEnglish
-
Upload UserAnonymous/Not logged-in
-
File Pages248 Page
-
File Size-