Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) BUNGE LA TANZANIA ________________ MAJADILIA NO YA BUNGE _______________ MKUTANO WA NNE Kikao cha Thelathini – Tarehe 26 Julai, 2006 (Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Spika (Mhe. Samuel J. Sitta) Alisoma Dua HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI Hati Zifuatazo Ziliwasilishwa Mezani:- NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Taarifa ya Mwaka na Hesabu Zilizokaguliwa za Taasisi ya Hifadhi za Bahari na Maeneo Tengefu kwa Mwaka Ulioishia Tarehe 30 Juni, 2004 (The Annual Report and Audited Accounts of the Marine Parks and Reserves Unit for the year ended 30th June, 2004). NAIBU WAZIRI WA ELIMU YA JUU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Taarifa ya Mwaka ya Utekelezaji wa Kazi za Chuo Kikuu Kishiriki cha Ardhi na Usanifu wa Majengo kwa Mwaka 2004/2005 (The Annual Report on the Activities of the University College of Lands and Architectural Studies for the year 2004/2005). NAIBU WAZIRI WA USALAMA WA RAIA: Hotuba ya Bajeti ya Waziri wa Usalama wa Raia kwa Mwaka wa Fedha 2006/2007. MHE. VITA R. KAWAWA (K.n.y. MWENYEKITI WA KAMATI YA ULINZI NA USALAMA): Maoni ya kamati ya Ulinzi na Usalama Kuhusu Utekelezaji wa Wizara ya Usalama wa Raia kwa Mwaka wa Fedha Uliopita pamoja na Maoni ya Kamati Kuhusu Makadirio ya Matumizi ya Wizara hiyo kwa Mwaka 2006/2007. 1 MHE. IBRAHIM MOHAMED SANYA - MSEMAJI MKUU WA KAMBI YA UPINZANI - KWA WIZARA YA USALAMA WA RAIA: Maoni ya Kambi ya Upinzani Kuhusu Utekelezaji wa Wizara ya Usalama wa Raia kwa Mwaka wa Fedha Uliopita pamoja na Maoni Kuhusu Makadirio ya Matumizi ya Wizara Hiyo kwa Mwaka 2006/2007. SPIKA: Kabla sijamwita Katibu ili tuingie hatua inayofuata. Kama kawaida tuna wageni hapa. Kwanza, wapo vijana watatu ambao ni watoto wa Mheshimiwa Mohamed Aboud Mohamed, Naibu Waziri wa Usalama wa Raia. Wa kwanza ni Aboud Mohamed, ndiye Mkubwa, wale pale, Aboud yule, halafu yupo Ahmed Mohamed Aboud na Ali Mohamed Aboud. Inasemekana kwamba mmoja wao anaandaliwa kuwa Mwanasiasa. (Makofi/Kicheko) Pia wageni wa Mheshimiwa Martha M. Mlata, ambao ni Madiwani saba (7) kutoka Tarafa za Ndago kule Wilaya ya Iramba, Singida. Madiwani wale pale. Karibuni sana Waheshimiwa Madiwani. (Makofi) Naona Vijana kutoka shule fulani lakini haikutangazwa ni shule ipi, lakini walimu na wanafunzi tunapenda kuwakaribisha sana muone jinsi Bunge lenu linavyofanya kazi ya Demokrasia. Karibuni sana. MASWALI NA MAJIBU Na. 280 Boma La Utete MHE. PROF. IDRIS A. MTULIA aliuliza:- Kwa kuwa Boma la Utete lina miaka zaidi ya 80; na kwa kuwa Boma hilo limejengwa na Wajerumani lakini sasa limeachwa kabisa kwa miaka mingi bila kufanyiwa ukarabati wa kutosha, limekuwa chafu sana kiasi cha kutia aibu:- (a) Je, Serikali itakubaliana nami kwamba, kuacha kulifanyia ukarabati unaostahili mara kwa mara ni kuidhalilisha Wizara husika na kuyashushia hadhi Makao Makuu ya Wilaya? (b) Je, Serikali itakuwa tayari kuahidi kuanza ukarabati huo mara moja? 2 NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA alijibu:- Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Prof. Idris Ali Mtulia, Mbunge wa Rufiji, kama ifuatavyo:- (a) Mheshimiwa Spika, nakubaliana na Mheshimiwa Mbunge kuwa Boma la Utete lina miaka mingi na lilijengwa wakati wa ukoloni na hivi sasa linahitaji kufanyiwa ukarabati mkubwa. Hata hivyo Serikali kupitia Bajeti za Mikoa imekuwa ikitenga fedha kidogo kidogo kulingana na uwezo wa fedha uliopo ili Maboma ya Wakuu wa Wilaya nchini yaweze kufanyiwa ukarabati ikiwa ni pamoja na Boma la Utete. Hivyo, naomba kumhakikishia Mheshimiwa Mbunge kwamba Serikali inatambua heshima na hadhi ya maboma ya Wakuu wa Wilaya kwamba ndiyo Makao Makuu ya Wilaya na kamwe suala la kudhalilisha Wizara halipo. Mheshimiwa Spika, tathmni iliyofanywa na Ofisi yangu mwaka 2004 inaonyesha kuwa baadhi ya Ofisi za Wakuu wa Wilaya ni chakavu na nyingine kutokuwa na thamani za kutosha ikiwa ni pamoja na Boma la Utete. Serikali inatambua umuhimu wa kulifanyia ukarabati boma hilo ili watumishi waweze kufanya kazi katika mazingira yanayofaa. (b) Mheshimiwa Spika, Serikali kwa kutambua umuhimu wa kuweka mazingira bora ya utendaji kazi, imeamua kuanza mara moja ukarabati wa Boma la Utete. Kazi hiyo inakadiriwa kugharimu Serikali jumla ya shilingi milioni 300. Katika Mwaka wa Fedha 2006/2007 Serikali imetenga kiasi cha shilingi milioni 90 ili kuanza awamu ya kwanza ya ukarabati huo. Mheshimiwa Spika, Serikali inapenda watumishi wake wote wawe na mazingira mazuri ya kazi, hivyo itaendelea kufanya ukarabati majengo kadri fedha zitakavyokuwa zinapatikana. MHE. PROF. IDRIS A. MTULIA: Mheshimiwa Spika, ahsante sana kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali moja la nyongeza. Mheshimiwa Spika, Boma la Utete halikujengwa kiholela, limejengwa katika uwanja wa vita vya Maji Maji ambako Kamanda wa Kijerumani aliuawa pale na Majugumbi Mzuzuri-jamii ya Mheshimiwa Dito. Sasa, it’s an Icon of resistance. Pale ni Waswahili wanatetea heshima ya Mswahili pale. Ninaomba Serikali ilitazame Boma lile kwa heshima; na kwa kuwa imekubali kukarabati. Je, Serikali safari hii itatumia Contractor makini? Kwa kawaida huletewa Contractor briefcase type. Ahsante sana. (Makofi) WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Spika, mimi nilidhani pengine jambo jema 3 kwa Mheshimiwa Prof. Idris A. Mtulia, ilikuwa kuishukuru Serikali kwa uamuzi wake mzuri sana wa kuanza kukarabati Boma. Mheshimiwa Spika, Boma lile kwa bahati nzuri mimi nimelitembelea mara mbili najua hali yake na nilichochea sana katika kujaribu kufanya uamuzi wa haraka ili kuweza kulibadilisha lifanane na Maboma mengine. Mheshimiwa Spika, kama alivyosema Mheshimiwa Naibu Waziri, tumedhamiria kufanya marekebisho ya msingi kabisa. Lakini nataka Mheshimiwa ajue kwamba masuala ya wakandarasi bado yatasimamiwa na Mkoa wa Pwani. Kwa hiyo mimi naomba Mheshimiwa Prof. Idris A. Mtulia ashirikiane na Mkuu wa Mkoa na timu yake pale waweze kupata mkandarasi mzuri ili aweze kufanya kazi ile vizuri na kwa matarajio ya Watanzania. MHE. ZAYNABU M. VULU: Mheshimiwa Spika, kwa kuwa Mkoa wa Pwani una Wilaya mbazo zimetimiza takriban miaka 100 na bado ziko nyuma kimaendeleo. Je, Serikali ina mpango gani katika kuinua na kwasaidia wananchi wa Wilaya hizo na wao waeze kupata maendeleo ambayo imepita zaidi ya miaka ya uhuru wetu? SPIKA: Hilo ni swali jipya, halihusiani na ile Ngome ya Utete. Kwa hiyo tunaendelea. Na. 281 Ukosefu wa Waganga na Wauguzi MHE. MARTHA M. MLATA aliuliza:- Kwa kuwa wananchi wa Singida katika baadhi ya vijiji wamejitolea kujenga Zahanati kwa kushirikiana na Mfuko wa TASAF ili kusogeza karibu huduma za matibabu; na kwa kuwa tangu Zahanati hizo zikamilike, bado hazifanyi kazi kwa kukosa Waganga na Wauguzi:- (a) Je, Serikali itapeleka lini Waganga na Wauguzi katika Zahanati za vijiji vya Wilaya ya Manyoni vya Mpapa, Mvumi, Chikombo, Hika na Mpandagani? (b) Je, kwa Serikali kutokupeleka Waganga katika Zahanati kwa takriban miezi kumi (10) haioni kwamba inadumaza moyo wa kujitolea kwenye miradi ya maendeleo? NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA alijibu:- 4 Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Martha M. Mlata, Mbunge wa Viti Maalum, lenye sehemu (a) na (b) kama ifuatavyo:- (a) Mheshimiwa Spika, ni kweli kwamba wananchi wa Wilaya ya Manyoni wakishirikiana na Mfuko wa TASAF wamejenga jumla ya Zahanati kumi na nne (14). Kutokana na uhaba wa watumishi waliopo katika Sekta ya Afya haikuwa rahisi kuhamisha watumishi kutoaka Zahanati zilizopo kwenda kufanya kazi katika Zahanati mpya zilizojegwa. Mheshimiwa Spika, hata hivyo katika mwaka wa fedha 2005/2006 Idara ya Afya Manyoni iliidhinishiwa Ikama ya Watumishi 298. Kati ya nafasi hizo, nafasi za ajira mpya za Waganga ni nne na 13 zilikuwa za Wauguzi. Mwaka 2006/2007 Ikama iliyopitishwa na Idara ya Afya, Waganga 23 na Wauguzi 17. Hivyo nafasi za ajira za Waganga ni 27 na nafasi za Wauguzi ni 30. Hivi sasa, Serikali imeamua kuajiri watumishi katika sekta ya Afya moja kwa moja kwa wale watakaohitimu vyuo na bila kufanya usaili. Hivyo ni matumaini yetu kuwa Zahanati zilizojengwa kwa nguvu za wananchi Wilayni Manyoni katika vijiji vya Mpapa, Mvumi, Chikombo, Hika na Mpandagani vitapata wataalam wanaohitajika. Nashauri Halmashauri ya Manyoni ifuate utaratibu unaotumika wa kupeleka maombi yote haya Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma ili ipatiwe wataalam wanaowahitaji kulingana na Ikama iliyopo. (b)Mheshimiwa Spika, kama nilivyoeleza katika kipengele (a) Halmashauri ya Manyoni mwaka 2005/2006 iliomba kuidhinishiwa Ikama ya watumishi kwa Zahanati mpya zilizopo ikiwa ni khatua ya kwanza ya kupata vibali vya ajira. Hivyo Serikali haikufanya makusudi kuchelewa kupeleka Waganga katika Zahanati husika. Mheshimiwa Spika, naomba kupitia Bunge lako Tukufu, kwanza niwapongeze wananchi wa Manyoni kwa kazi nzuri waliyoifanya ya kujenga Zahanati hizo, pia niwaombe wananchi hao wasivunjike moyo kushiriki katika shughuli za maendeleo yao pamoja na Serikali. Mheshimiwa Spika, kwa utaratibu uliopo sasa wa ajira kwa Sekta ya Afya kama nilivyosema tatizo hilo naamini litapungua. MHE. MARTHA M. MLATA: Mheshimiwa Spika, ahsante. Pamoja na majibu ya Mheshimiwa Naibu Waziri, naomba niulize maswali mawili madogo ya nyongeza:- (a) Kwa vile afya ya wananchi ni muhimu kwa uhai wao na pia kwa uchumi wa taifa letu, Je, Serikali haioni sasa umefika wakati wa kuwafundisha Waganga hawa pamoja na Manesi ili kukidhi haja za Zahanati zinazojengwa na wananchi wetu kwa wingi zaidi kwa kufuata Mfumo wa Wizara ya Elimu inavyofundisha walimu wake? (b) Kwa kuwa tatizo hili limekuwa ni kubwa hasa kwa Mkoa wa Singida, Waganga wengi na Wauguzi hawaendi kwa jinsi ilivyotakiwa. Je, Serikali itakubaliana nami kwamba iweke Mfumo mpya ili Serikali za Vijiji ziweze kupendekeza majina ya vijana ambao watapelekwa kuchukua mafunzo kwa ajili ya mkataba ili waweze kudumu katika Zahanati hizo? 5 NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Spika, natambua wazi kwamba afya ni muhimu kwa taifa letu kiuchumi na kwa kutambua hilo Serikali sasa hivi inaazma ya kuongeza idadi ya Wauguzi na Waganga katika Vyuo vyake. Kwa hiyo ni mpango mzuri tu ambao unafanywa na Serikali ili kuongeza hiyo idadi kama tulivyofanya kwenye mpango wa MMEM wa kuongeza walimu wengi.
Details
-
File Typepdf
-
Upload Time-
-
Content LanguagesEnglish
-
Upload UserAnonymous/Not logged-in
-
File Pages195 Page
-
File Size-