Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) BUNGE LA TANZANIA ________________ MAJADILIANO YA BUNGE _________________ MKUTANO WA NANE Kikao cha Arobaini na Tano – Tarehe 11 Agosti, 2012 (Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Mwenyekiti (Mhe. Musa Z. Azzan) Alisoma Dua HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI Hati Zifuatazo Ziliwasilishwa Mezani na:- NAIBU WAZIRI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS (K.n.y. WAZIRI WA NCHI, OFISI YA MKAMU WA RAIS (MAZINGIRA): Taarifa ya Mwaka ya Utendaji na Hesabu Zilizokaguliwa za Baraza la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira kwa Mwaka Ulioishia tarehe 30 Juni, 2011(The Annual Report and Audited Accounts of The National Environment Management Council (NEMC) for the Year ended 30th June, 2011). WAZIRI WA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI: Randama za makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kwa Mwaka wa Fedha, 2012/2013. HOJA ZA SERIKALI Makadirio ya Matumizi ya Serikali Kwa 2012/2013 Wizara ya Maliasili na Utalii MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge, tunaendelea na mjadala huu wa Maliasili na Utalii na sasa mchangiaji wetu wa kwanza atakuwa ni Mheshimiwa Mbarouk Salim Ali, Mheshimiwa Profesa Juma Kapuya. MHE. PROF. JUMA A. KAPUYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninashukuru sana kunipa nafasi na mimi niweze kuchangia hoja hii ya Wizara ya Maliasili na Utalii. Kwanza ninaomba kuwapongeza sana Mheshimiwa Waziri na timu yake kwa hotuba nzuri ambayo mmewasilisha na ambayo inatoa matumaini kwa wana Mazingira. Ninaomba niende moja kwa moja kwenye Hoja ya Hifadhi ya Misitu. Kila mtu anafahamu umuhimu wa misitu. Misitu ndiyo vyanzo vya maji na ukizingatia kule kwetu Urambo ambako tuna karibia 80% ya Hifadhi ya Misitu ya Mkoa wa Tabora ni kama Hifadhi ya maji ya Mkoa wa Tabora. Ni hifadhi ya maji yanayokwenda katika mto Malagarasi na katika ziwa Tanganyika ambayo ni 30%. Lakini pia misitu hii ndiyo inatengeneza hewa tunayovuta, misitu hii hutupa chakula, misitu hii ni vitega uchumi kwetu kwa sababu tunaitumia kuweka mizinga yetu ili tuweze kupata fedha, misitu hii vilevile ni kivutio kikubwa cha Watalii kwa hiyo, misitu ni kitu muhimu sana. (Makofi) Mheshimiwa Mwenyekiti, tatizo linakuja kwenye Management ya hifadhi za misitu na matatizo yenyewe tunaweza kuyagawa katika sehemu mbili. Tatizo la kisiasa na tatizo la uongozi. Hifadhi zimekuwepo toka wakati wa Mkoloni na wala zilikuwa hazina matatizo wakati tunapata Uhuru Watanganyika tulikuwa milioni sita na baadaye tukafika milioni tisa na sasa hivi tuna karibia milioni 45 kama itakavyokuja kuthibitishwa baadaye na sensa, kutokana na kuongezeka kwa watu kumekuwa na utaratibu unaoeleweka na Serikali watu wanapeleka maombi kupitia taratibu zinazoeleweka na maeneo yamekuwa yakiongezwa kupitia taratibu hizi. Pia taratibu zinazoeleweka ndiyo vinazaliwa vijiji kama Luyembe, Sungimlole, Kangeme, Kumbisiganga, Lumbe, Kakoko, Msinga na Ndiga katika Tarafa ya Kumbisiganga hivi ni vijiji ambavyo vimezaliwa kiutaratibu kabisa, lakini tatizo lilikuja kuzuka pale ambapo baadhi ya Wanasiasa tulianza kuona mapori haya kama vile tunaweza kuyatumia kama mtaji wa kisiasa hapo ndiyo tatizo kubwa lilikuja kuzuka. Kwamba kumbe kuna mapori yamekaa mtu anaweza kushawishi watu wakahamia pale wakajaa ili hatimaye baadae aje awatumie katika kumpigia kura na hili liko katika ngazi mbalimbali kazi za vitongoji, ngazi za vijiji na hata ngazi za Ubunge hili ndiyo limeleta sokomoko kubwa. Vijiji hivi ambavyo nimezungumza vilikuwa vinatambua kabisa kuwa jirani yetu ni msitu, jirani zetu ni wanyama pori hivyo waliishi kwa tahadhari hiyo lakini leo vurugu zimejaa katika misitu ya Urambo kwa sababu wavamizi wamejaa kwa kushawishiwa kisingizio kikubwa kinachotumika hapa wakishajazana katika misitu ile kwamba sisi hatujui mipaka, siyo kweli kabisa kuwa mipaka haijulikani kwa sababu ingekuwa mipaka haijulikani huko wanakokaa ingekuwa tumechanganyika na sisi wakazi wa zamani, wakazi asilia lakini ukienda katika maeneo hayo utakuta wamejaa wageni tena kuanzia mwaka 2000 mpaka 2010 hapa katikakati hapa. Mheshimiwa Mwenyekiti, ni wageni wa aina moja kazi yao ni moja ya ufugaji kabila lao ni moja na Chama chao ni kimoja kwamba wewe ukihamia huku na kuingia katika Chama hiki mimi nitakuwa mlinzi wako kuhakikisha kuwa unakaa hapa bila kubughudhiwa. Hii imeleta kasheshe kweli mtu anaposimama na kusema mipaka ni tatizo siyo kweli kwa mfano; pale Igagala tumeanzisha WMA inaitwa ISAWIMA kwenye jiwe la ISAWIMA lenyewe kuna mtu kaenda kujenga mji hivi ni kweli hajui mpaka kwa sababu jiwe liko pale linaonyesha kuwa hapa ndiyo mwanzo wa WMA lakini yeye kajenga pale hifadhi kwa hiyo, hili ukilinganisha na udhaifu wa uongozi na hapa ninazungumzia uongozi wa Serikali Kuu tunalo tatizo kubwa. (Makofi) Hifadhi hizi zilikuwepo toka wakati wa Mkoloni, Mkoloni alikuwa na utaratibu wa kuhakikisha kuwa kila baada ya miezi fulani anapita kukagua hivi sasa Hifadhi hizi hakuna anaye kagua watu wanakaa miaka 10, 12 mpaka 15 baadaye inakuja kuwa ni kero kubwa. Sasa hivi kwa kuwa tatizo limekuwa kubwa ndiyo Serikali imeanza kuzinduka ilikuwa imeachiwa Halmashauri, Halmashauri haiwezi, fedha ni kidogo na utalaam ni kidogo nguvu za maaskari ni kidogo matokeo yake ni kuwa misitu inakwisha na misitu inapokwisha athari zake hujitokeza moja kwa moja katika Wilaya yetu ya Urambo na katika Mkoa wetu wa Tabora mvua kwa sasa zimepungua karibia 50%, kulikuwa na mvua za milimita 1500, mpaka 1600 hivi sasa tunaishia milimita 800 tu, maji ya kunywa yamekuwa haba na kadhalika. Mheshimiwa Mwenyekiti, ukifika Urambo mwaka 1995 mpaka 2000 kuna eneo linaitwa Maboha na kuna eneo linaitwa Shela pale kulikuwa na Ziwa kubwa na watu walikuwa wakipita eneo lile kwa mitumbwi ndiyo maana 1997 tulipata ajali ya watu kupinduka na mtumbwi na watu karibia 30 walipoteza maisha. Ilikuwa ni kwaya inatoka sehemu moja ya eneo kwenda kuwatembelea waumini wenzao leo hii ukienda na kwa kuwa ardhi yetu ni tambarare unaweza kucheza mpira tu hakuna chochote ni vumbi tupu. Ninaishukuru sana Kamati ya Maliasili na Mazingira walipata nafasi kwenda kuangalia na wakathibitisha mambo mawili la kwanza, kwamba kumbe ni kweli katika vijiji hivi kuna eneo ambalo ni halali na eneo ambalo ni haramu. Kwa hiyo, hata operation ya kuchoma nyumba ilipokuja waliochomewa walikuwa ni wale ambao wako katika Shela haramu, Shela halali wananchi hawakuguswa kabisa. Lakini vilevile wakathibitisha kuwa zile propaganda za watu waliouawa karibia ishirini siyo kweli walitoa taarifa waliambiwa onyesheni makaburi lakini kaburi hata moja halikuonekana hili ni tatizo. Kwa sababu ya udhaifu huu Halmashauri ambayo inajitahidi inabidi itumie rasilimali zake tunaishiwa. Lakini pia kwa sababu watu hawa wameshajizatiti kule porini wanatuua sana na kututukana sana tarehe 4 Februari, 2011 kulikuwa na watu na ninaomba kwa idhini yako nisome ambao walikwenda kutoa taarifa kuwa eneo hili la North Lugala siyo halali ni msitu wa Hifadhi tunaomba muhame na operation inakuja badala ya kuwasilikiliza walichokifanya watu wale walioenda kutoa taarifa walipigwa na kuuawa kikatili na wafuatao waliuawa Ndugu Yasini Nyembe - VEO, Ndugu Makenzi Magida - Mwenyekiti wa Kitongoji, Ndugu Emmanuel Gabriel - Mgambo na Ndugu Ayo Ramadhani - Mgambo. Walionusurika kwa baraka za Mwenyezi Mungu walikuwa ni Ndugu Miraji Selemani, Ndugu Yasin Kapaya, Ndugu Ramadhani Amani, Ndugu Bahati Mlangila na Ndugu Nuhu Philipo. Hawa wote walikuwa wamekwenda kutoa elimu na kuwaasa wale watu watoke katika misitu ya Hifadhi, wakauawa kikatili. Mheshimiwa Mwenyekiti, kinachotuuma tumejitahidi sana sisi na Halmashauri, tumejitahidi sana na DC wetu kuieleza Serikali angalau wapate kifuta machozi familia za watu hawa mpaka leo hakuna hata senti tano, inauma na inasikitisha. Ninamwomba Mheshimkiwa Waziri wakati atakapokuwa anafanya majumuisho anielezee kuwa anakwenda kuzieleza nini familia hizi za watu hawa waliouawa na watu waliofanya mauaji mpaka leo hawajakamatwa. Ukiuliza Serikali unaambiwa utaratibu unafanyika inauma sana sisi ambao tumejitolea kulinda misitu hii na kulinda wanyama hawa hatutendewi haki ninakuomba sana Mheshimiwa Waziri hili unisaidie. Ushauri wangu ni kuwa Serikali hii Kuu iandae operation kabambe na katika operation hii wakawaondoe wavamizi walio katika misitu hii. Wakawaondoe wavamizi walio katika njia ya kupitia wanyama kutoka Ugala kuja Moyovozi ili uoto ule wa asili urudi katika hali yake ya asili. Ikisha fanya hivyo isiwe kama zimamoto waendelee kuwa wanasimamia kama ni suala la mipaka wachonge barabara kama ilivyokuwa zamani mimi nilikuwa ninaomba Mheshimiwa Waziri azingatie haya,lingine ni kuwa tunayo kampuni ya uwindaji inaitwa Robin Heart Safaris. Kampuni hii kule kwetu ukizungumzia misaada kwa wananchi kampuni hii haifanyi chochote kusaidia wananchi tunajiuliza hivi sisi faida yetu ni nini ukisikia wanayoyafanya kule Arusha wanafanya makubwa sana. Lakini huku ukiwaeleza shida wanakwambia mwaka 1995 tulitoa mabati na kukarabati madarasa mawili hivi toka mwaka 1995 mpaka leo 2012 hayo madarasa mawili ndiyo mwisho? Mheshimiwa Mkwenyekiti, tunamwomba Mheshimiwa Waziri kuwa mkataba wao utakapokwisha watu hawa usiwarudishe kwetu tena waelekee huko huko Arusha tutafutie wawekezaji wengine waje tukae nao. (Makofi/ Vicheko) Ndiyo, maana na sisi tunahitaji misaada kama wanavyohitaji wengine hizi Corporate Social Responsibilities lazima ziwepo katika maeneo yote na nilipokuwa nikizungumza suala la vijiji, vijiji kama hivi viko katika Kata ya Seleli, Kata ya Sasu na Kata ya Kashihi. Hawa nao vilevile kuna vijiji ambavyo vilikuwa vimezingatiwa kwa taratibu za Serikali navyo vilevile mnapoanza operation kubwa hii isiwe mtego wa panya kuingia
Details
-
File Typepdf
-
Upload Time-
-
Content LanguagesEnglish
-
Upload UserAnonymous/Not logged-in
-
File Pages350 Page
-
File Size-