NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ____________ MAJADILIANO YA BUNGE ___________ MKUTANO WA KUMI NA MOJA Kikao cha Hamsini na Mbili – Tarehe 18 Juni, 2018 (Bunge Lilianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Spika (Mhe. Job Y. Ndugai) Alisoma Dua SPIKA: Waheshimiwa Wabunge tukae. Katibu! NDG. STEPHEN KAGAIGAI - KATIBU WA BUNGE: HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na:- MHE. HAWA A. GHASIA - MWENYEKITI WA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA BAJETI:- Taarifa ya Kamati ya Bajeti kuhusu Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2017 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019, pamoja na Tathmini ya utekelezaji wa Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 na Mapendekezo ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019. SPIKA: Ahsante sana Mheshimiwa Mwenyekiti wa Bajeti, Mheshimiwa Hawa Ghasia. Katibu. 1 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) NDG. STEPHEN KAGAIGAI – KATIBU WA BUNGE: MASWALI NA MAJIBU Na. 438 Hitaji la Gari la Wagonjwa Kituo cha Afya Mgungulu MHE. MENDRAD L. KIGOLA aliuliza:- Je, ni lini Serikali itapeleka gari ya kuwahudumia wagonjwa katika kituo cha Afya cha Magunguli –Mgololo? NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. JOSEPHAT S. KANDEGE) alijibu:- Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Menrald Lutengano Kigola, Mbunge wa Mufindi Kusini, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Spika, gari la wagonjwa kwa ajili ya Kituo cha Afya Magungulu - Mgololo kilichopo kata ya Magungulu imekwishapatikana. Gari hili lilitolewa na Mheshimiwa Rais wakati anatoa msaada wa magari ya wagonjwa kwa halmashauri mbalimbali hapa nchini mnamo mwezi Machi, 2018 na taratibu za usajili zinaendelea. Mheshimiwa Spika, hata hivyo, kwa kutambua uhitaji wa gari katika kituo hiki, gari hili limepelekwa kituoni moja kwa moja na kuanza kutumika huku taratibu za usajili wake zikiwa zinaendelea. Ni matumaini yetu kuwa gari hili, litasaidia kuleta wepesi kwa wananchi kufikia huduma za afya pale mahitaji yatakapo yanajitokeza. SPIKA: Mheshimiwa Kigola swali la nyongeza nimekuona. MHE. MENDRAD L. KIGOLA: Mheshimiwa Spika, kwanza nichukue nafasi hii kwa kumshukuru sana Makamu wa Rais 2 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) alipokuwa amekuja kwenye jimbo langu na mimi nilimwomba Ambulance siku ile na utekelezaji umefanyika nashukuru sana. Swali langu la kwanza kule jimboni kwangu nina vituo vya afya kama vitatu ambavyo viko vijijini sana hakuna magari kwa mfano pale Mninga na Mtwango ni vituo vikubwa sasa. Je, Serikali itanisaidia tena kuniletea (Ambulance katika hivyo vijiji viwili ambao wananchi wanapata shida sana? Mheshimiwa Spika, swali langu la pili, nina tatizo kubwa sana la watumishi wa Afya kwenye vituo vyangu vya afya na zahanati kwenye jimbo langu. Je, Wizara ya Afya ina utaratibu gani wa kuhakikisha kwamba watumishi wa Afya tunaweza kuwapata? SPIKA: Majibu ya maswali hayo mawili, Mheshimiwa Naibu Waziri Tawala za Mkoa na Serikali za Mitaa. NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. JOSEPHAT S. KANDEGE): Mheshimiwa Spika, kwanza kwa niaba ya Serikali naomba nipokee shukrani ambazo zimetolewa na Mheshimiwa Mbunge. Katika suala lake la kwanza, anaongelea vituo vya afya vingine viwili ambavyo viko mbali sana na vina uhitaji mkubwa wa magari ya Ambulance. Mheshimiwa Spika, naomba nimwakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba ni azma ya Serikali pale ambapo gari zinapatikana tutazisambaza na hasa tutazingatia maeneo yenye uhitaji mkubwa sana. Sasa kama na eneo la kwake litakuwa miongoni mwa hayo maeneo ambayo yana uhitaji mkubwa hakika sisi tutatekeleza hilo, lakini ni vizuri pia akatambua kwamba kuna baadhi ya maeneo ambayo hawakupata hata hiyo gari ambayo yeye amepata kwa hiyo kwa kadri gari zitakapopatika tutafuata uwiano unaotakiwa ili haki iweze kutendeka. Mheshimiwa Spika, katika swali lake la pili, anaongelea juu ya vituo vyake vya afya kutokuwa na watumishi wa kutosha, naomba nimhakikishe Mheshimiwa Mbunge sasa hivi Ofisi ya Rais, TAMISEMI tumeshatangaza 3 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) nafasi 6,180,000 na naamini pale ambapo watakuwa wameajiriwa na eneo la kwake litaweza kufikiriwa kupelekewa. SPIKA: Tunaendelea na swali linalofuata la Desderius John Mipata Mbunge wa Nkasi Kusini. Na.439 Barabara ya Namanyere- Ninde MHE. DESDERIUS J. MIPATA aliuliza:- Serikali imetumia zaidi ya shilingi milioni 350 kuimarisha barabara ya Namanyere – Ninde yenye urefu wa kilomita 67, lakini fedha hazikutosha kukamilisha barabara hiyo:- Je, Serikali itatenga fedha zaidi kukamilisha barabara hiyo? NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. JOSEPHAT S. KANDEGE) alijibu:- Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Desderius John Mipata, Mbunge wa Jimbo la Nkasi Kusini, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Spika, Barabara ya Namanyere- Ninde yenye urefu wa kilomita 67, kwa mara ya kwanza iliibuliwa na mradi wa TASAF Awamu ya I mwaka 2005/2006 kwa kulima barabara hiyo kwa kutumia nguvu kazi ya wananchi. Kwa kipindi chote hadi mwaka 2014/2015, barabara haikufunguka kwa kukosa miundombinu muhimu kama vile madaraja na makalvati. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2014/2015, Serikali ilitenga fedha jumla ya shilingi milioni 375.3 kwa ajili ya kuifanyia matengenezo ambapo fedha hizo zilitumika kwa kufyeka barabara na kuondoa miti katika barabara yote, 4 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) kuilima barabara kwa urefu wa kilomita 25 kwa kiwango cha udongo, kujenga Makalvati 15 pamoja na kujenga madaraja manne. Kati ya madaraja manne yaliyojengwa, mawili yapo katika Mito ya Lwafi na Ninde, hivyo matengenezo hayo yamewezesha barabara hiyo kufunguka kwa urefu wa kilomita 25 tu. Mheshimiwa Spika, kulingana na upatikanaji wa fedha, Serikali imeendelea kutenga fedha kwa ajili ya kufanyia matengenezo barabara hiyo ambapo mwaka wa fedha 2015/2016, shilingi milioni 44.58 zilitengwa kwa ajili ya kufanya matengenezo ya muda maalum kwa urefu wa kilomita 20. Aidha, mwaka wa fedha 2016/2017, kiasi cha shilingi milioni 20 zilitumika kuimarisha sehemu korofi zenye urefu wa mita 500. Mheshimiwa Spika, Serikali itaendelea kuifungua barabara hii kadri fedha zitakavyokuwa zinapatikana ili kusaidia wananchi wanaotumia barabara hii katika suala zima la usafiri. SPIKA: Mheshimiwa Mipata swali la nyongeza, MHE. DESDERIUS J. MIPATA: Mheshimiwa Spika, ahsante sana kufuatia majibu ya Serikali tayari barabara hii imetumia zaidi ya milioni 439.8 katika jitihada ya kutaka kuifungua. hata hivyo, mwaka huu haijatengewa fedha na wanasema itaendelea kuitengea fedha kadri fedha itakavyozidi kupatikana. Je, Serikali haioni kwamba kwa kufanya hivi inachelewa na fedha ambazo tayari imesha-invest kwenye barabara hizi zitakosa thamani? Mheshimiwa Spika, swali la pili, kufuatia mvua nyingi zilizonyesha katika Mkoa wa Rukwa kuna barabara katika Jimbo la Nkasi Kusini zimefunga kabisa. Barabara hizo ni pamoja na Kisula - Malongo Junction - Katongolo- Namasi- Ninde - Kanakala na tayari TARURA imeleta taarifa ya orodha ya barabara hii. Je, ni lini fedha sasa zitatolewa kwa ajili ya kwenda kurudisha miundombinu ili iweze kutumika? 5 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri, Josephat Kandege majibu ya maswali hayo. NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. JOSEPHAT S. KANDEGE: Mheshimiwa Spika, naomba kwanza uniruhusu kipekee nimpongeze sana Mheshimiwa Mipata barabara hii amekuwa akiipigania kwa nguvu zake zote na ndiyo maana Serikali imesikia kilio chake na hicho kiasi cha pesa kikaanza kutumika. Mheshimiwa Spika, naomba nimhakikishie kama ambavyo yeye mwenyewe amesema itakuwa si busara kwa Serikali kuweza pesa bila kupata matunda kwa sababu matunda yanayotarajiwa ni barabara kufunguka. Hata hivyo, naye atakubaliana nami kwamba barabara hii haikuwepo kabisa na kazi kubwa ambayo imekwishafanya kuhusiana na ujenzi wa madaraja pamoja na yale makalvati hakika pesa ikipatikana kipande ambacho kimebaki kitaweza kufunguliwa na wananchi waweze kupita kwenye hiyo barabara. Mheshimiwa Spika, katika swali lake la pili, anaongelea baada ya mvua kunyesha kumekuwa na uharibifu katika barabara hizo ambazo amezitaja na bahati nzuri TARURA walishaleta makisio ya nini ambacho kinatakiwa kutumika. Naomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge pesa ambazo zilitengwa kwa ajili ya emergence almost zote zilishakwisha na theluthi mbili ya pesa hizo zilitumika katika kurudishia miundombinu katika Mkoa wa Dar es Salaam. Mheshimiwa Spika, pia naomba nimhakikishie kwa sababu bajeti ilishapitishwa naamini muda siyo mrefu pesa ikianza kupatikana na eneo la kwake litaweza kufunguliwa hizo barabara. SPIKA: Tuendelee na Utumishi na Utawala Bora swali la Mheshimiwa Ruth Hiyob Mollel, kwa niaba yake! Mheshimiwa Selasini. 6 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) Na. 440 Watumishi wa Umma kuzingatia Kanuni na Sheria za Utumishi wa Umma MHE. JOSEPH R.SELASINI - (K.n.y MHE. RUTH H. MOLLEL) aliuliza:- Serikali ya Awamu ya Tano inajinasibu kuzingati Utawala wa Sheria, Kanuni na taratibu katika Utumishi wa Umma. Hata hivyo, kuna ushahidi kuwa baadhi ya viongozi wanakiuka maadili na taratibu lakini wameachwa pasipo kuchukuliwa hatua zozote za kinidhamu:- (a) Je, tunaweza kujenga uchumi imara bila Watumishi wa Umma kuzingatia Kanuni na Sheria za Utumishi wa Umma? (b) Je, Serikali ina mkakati gani kuhakikisha Taifa linadumisha umoja ulioasisiwa na Baba wa Taifa? WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS (UTUMISHI NA UTAWALA BORA) alijibu:- Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Ruth Hiyob Mollel,
Details
-
File Typepdf
-
Upload Time-
-
Content LanguagesEnglish
-
Upload UserAnonymous/Not logged-in
-
File Pages227 Page
-
File Size-