1458127047-Hs-7-2-20

1458127047-Hs-7-2-20

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) 11 APRILI, 2012 BUNGE LA TANZANIA _______________ MAJADILIANO YA BUNGE _______________ MKUTANO WA SABA Kikao cha Pili – Tarehe 11 Aprili, 2012 (Mkutano Uilianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Naibu Spika (Mhe. Job Y. Ndugai) Alisoma Dua MASWALI NA MAJIBU Na. 16 Miradi Inayohitaji Uwekezaji MHE. KABWE Z. ZITTO (K.n.y. MHE. HAMAD RASHID MOHAMED) aliuliza:- (a) Je, ni miradi mingapi na ya aina gani inayohitaji uwekezaji wa ama ubia na sekta binafsi na sekta binafsi peke yake? (b) Je, ni utaratibu gani mwekezaji aufuate ili asisumbuliwe kupata taarifa ya uwekezaji huu? WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, UWEKEZAJI NA UWEZESHAJI alijibu:- Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu naomba kujibu swali la Mheshimiwa Hamad 1 11 APRILI, 2012 Rashid Mohamed Mbunge wa Wawi, lenye sehemu (a) na (b) kama ifuatavyo:- (a) Mheshimiwa Naibu Spika, hadi sasa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kimepokea mapendekezo ya miradi 227 ya uwekezaji. Kati ya hiyo miradi 135 ni ya Ubia kati ya sekta ya Umma na Sekta binafsi kama ifuatavyo:- Miradi hiyo iko kwenye uzalishaji na usambazaji wa umeme miradi 29 usafiri kwa njia ya Reli 6 miradi ya ukarabati na ujenzi wa viwanja vya ndege 17, miradi ya ujenzi na ukarabati wa bandari 9 miradi ya kilimo 10, miundombinu ya majengo 9, maeneo maalum ya biashara (SEZ) 7 na miradi 48 kutoka Serikali za Mitaa. Aidha, miradi 92 imewasilishwa na sekta binafsi kwa mgawanyo ufuatao:- Viwanja kwa ajili ya uwekezaji wa viwanda 4, miradi ya kilimo 38, vitalu vya madini 13 shughuli za utalii 32, uwekezaji katika sekta ya elimu 2 na biashara 3. (b)Mheshimiwa Naibu Spika, ili mwekezaji asisumbuke kupata taarifa za uwekezaji anatakiwa afuate taratibu zilizowekwa chini ya sheria ya ubia baina ya sekta ya umma na sekta binafsi ya mwaka 2010 na kanuni zake za mwaka 2011 au sheria ya uwekezaji ya mwaka 1997 na Kanuni zake za mwaka 2002. Aidha, Serikali imeanzisha kitengo cha fedha (PPP- Financing Unit) chini ya Wizara ya Fedha mwezi Novemba, 2010 na Kitengo cha Uratibu (PPP- Coordination Unit) katika kituo cha Uwekezaji Tanzania mwezi Februari, 2012. uanzishwaji wa vitengo hivi utawezesha kufanyika uchambuzi wa kina wa miradi iliyopendekezwa kutoka katika mamlaka ya Serikali na sekta binafsi ikiwa ni pamoja na upembuzi yakinifu na masuala yanayohusiana na athari katika Bajeti ya Serikali (Fiscal Risk Assessment). 2 11 APRILI, 2012 MHE. KABWE Z. ZITTO: Mheshimiwa Naibu Spika, nilikuwa napenda kufahamu miradi ya reli ambayo imetajwa kama sehemu ya miradi iliyoorodheshwa ya ubia ni reli zipi na kwa utaratibu upi. Je, ni ule ule wa RITES ambao umeshindikana au ni miradi mipya kabisa ambayo inaanza? WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, UWEKEZAJI NA UWEZESHAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, namshukuru Mheshimiwa Kabwe Zitto kwa swali lake la nyongeza. Ameuliza juu ya miradi ya reli ambayo wawekezaji pengine wameonyesha nia ya kuwekeza kwa njia ya ubia au Wizara husika imeleta mapendekezo Ofisi ya Waziri Mkuu Kitengo cha Uwekezaji ni reli ambazo zipo ambazo wote tunajua kwamba zimezeeka na zinatakiwa zibadilishwe lakini pamoja na hayo kuna reli zingine ambazo ni mpya ambazo nazo wawekezaji wametaka kuwekeza. Kwa maelezo zaidi ya kina Mheshimiwa Kabwe Zitto anaweza kuja na tukampa maelezo zaidi ya kina ili aweze kuelewa na kama anaweza kutusaidia kusukuma basi nasi tutakushukuru. MHE. LUHAGA J. MPINA: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru kwa kunipa nafasi ili niweze kuuliza swali kama ifuatavyo:- Kwa kuwa miradi 10 ya kilimo aliyoitaja Mheshimiwa Waziri. Je, anaweza kunithibitishia kuwa ni pamoja na mradi muhimu sana wa Kiwanda cha Nyama cha Shinyanga, pamoja na ule wa kiwanda kikubwa cha nguo Shinyanga vitakuwepo kwenye uwekezaji wa ubia ambao tunauzungumza sasa hivi? ( Makofi ) WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, UWEKEZAJI NA UWEZESHAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, namshukuru Mheshimiwa Mpina, kwa swali la nyongeza. 3 11 APRILI, 2012 Mheshimiwa Naibu Spika, jana nilikuwa naongea na Mbunge wa Shinyanga Mjini na yeye ameniambia umuhimu na mimi naufahamu kwa sababu nilikuwa Waziri wa Viwanda umuhimu wa Kiwanda cha Nyama Shinyanga na Kiwanda cha Nguo kwa sababu Wasukuma wanalima pamba. Sasa sijakalili miradi yote ambayo ipo kwa sababu si rahisi kama nilivyozitaja ni nyingi. Lakini kama mradi huo haupo basi hata Mheshimiwa Mpina na Mheshimiwa Mbunge wa Shinyanga Mjini wanaweza wakauleta ili TIC iweze kuona kama kuna wawekezaji. Lakini nilivyoongea na Mheshimiwa Mbunge wa Shinyanga Mjini jana tuliongea ni vipi ambavyo tunaweza tukatafutia wawekezaji mradi huo hasa wa Kiwanda cha Nyama Shinyanga ambapo ng’ombe ni wengi wanafugwa kule na vile vile umuhimu wa kuwa na kiwanda cha nguo Shinyanga. Na. 17 Mgogoro wa Ardhi Kati ya Kata ya Ilagala na Magereza MHE. FELIX F. MKOSAMALI (K.n.y. MHE. DAVID ZACHARIA KAFULILA) aliuliza:- Mgogoro wa ardhi kati ya Wakazi wa kata ya Ilagala na Magereza unazidi kuwa mkubwa na kuhatarisha amani kwa wakazi wa eneo hilo . Je, Serikali inachukua hatua gani kulipat ia ufumbuzi tatizo hilo ili wananchi hao waweze kupata ardhi kwa ajili ya kilimo? 4 11 APRILI, 2012 NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (TAMISEMI) alijibu:- Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri Mkuu naomba kujibu swali la Mheshimiwa David Zacharia Kafulila, Mbunge wa Kigoma Kusini, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli kwamba kumekuwa na mgogoro wa ardhi baina ya Kijiji cha Ilagala na Gereza la Ilagala katika Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma. Mwaka 1968 uongozi wa Kijiji cha Ilagala ulitoa ekari 15,000 kwa taasisi ya magereza kwa ajili ya matumizi ya kilimo na ujenzi. Mgogoro ulioibuka ni madai ya Serikali ya Kijiji cha Ilagala kutaka kuongezewa eneo la ardhi kutokana na kuongezeka kwa idadi ya watu katika Kijiji hicho. Mheshimiwa Naibu Spika, eneo hili linamilikiwa kihalali na Gereza la Ilagala kutokana na idhini ya miliki iliyotolewa na Serikali ya Kijiji mwezi Machi, 1968. Magereza baada ya kupata eneo hilo walipima na kuweka mipaka mwaka 2003 ili kuzuia uvamizi unaoweza kujitokeza. Baada ya upimaji huo kukamilika ilibainika kuwa kitongoji cha Sambala ambacho kiko katika Kijiji cha Ilagala kipo ndani ya mipaka ya eneo linalomilikiwa na Magereza. Serikali ngazi ya Wilaya kwa kushirikiana na uongozi wa Magereza walikubaliana mipaka ya eneo hilo irekebishwe ili kitongoji cha Sambala na shule ya msingi viwe nje ya mipaka ya eneo la Magereza jambo ambalo Magereza walitekeleza. Mheshimiwa Naibu Spika, hata hivyo baada ya marekebisho hayo ya mipaka ilionekana kuna wananchi wachache waliokuwa na makazi na kuamriwa kuondoka. Serikali ya kijiji haikuridhia uamuzi huo na kufungua kesi kwenye Baraza la Ardhi na Nyumba la Wilaya kupinga agizo hilo la kuhama na hukumu ilitoka kwamba Magereza ndio wamiliki halali wa eneo hilo. 5 11 APRILI, 2012 Hata hivyo wananchi hao wameonyesha nia ya kukata rufaa Mahakama Kuu kupinga uamuzi uliotolewa na Baraza la Ardhi na Nyumba la Wilaya kwamba Gereza la Ilagala ndilo lenye umiliki halali wa ardhi hiyo lakini hadi sasa kwa maamuzi ya Baraza la Ardhi na Nyumba la Wilaya, Gereza la Ilagala ndiye mmiliki halali wa eneo husika. (Makofi) MHE. FELIX F. MKOSAMALI: Mheshimiwa Naibu Spika, nina maswali mawili kama ifuatavyo:- (a) Kwa kuwa Serikali ya Kijiji cha Ilagala ndio ilitoa eneo hilo na wananchi wamefukuzwa tu bila kuangalia haki ya kuishi wanakotaka kama Katiba ya nchi inavyosema. Je, Serikali haioni sasa kuna haja ya kukaa upya ili wananchi hawa waweze kurudishwa kwenye maeneo yao maana ni haki yao ya kikatiba? ( Makofi ) (b) Je, ni kwa nini Magereza inaendelea kuwa na msimamo mkali sana wakati jambo hili linapaswa kumalizwa kistaarabu ili waweze kuishi vizuri, askari Magereza na wananchi wa Kijiji kile? NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (TAMISEMI): Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu, ninaomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Felix Mkosamali, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Naibu Spika, asubuhi ya leo nimezungumza na Regional Commissioner wa Mkoa wa Kigoma nataka iingie kwenye rekodi Mheshimiwa Issa Machibya na tumeliangalia jambo hili. Kesi na faili zote na kila kitu ninacho hapa na mjadala huu ulivyohitimishwa ninavyo vyote hapa. 6 11 APRILI, 2012 Kwa hiyo, hapa wala si kwamba naibuka tu nakuja nasema hivi ninavyosema hapa kwamba nimepapasa papasa, nina documents zote ziko hapa. Kwamba wananchi hawa walifukuzwa pale wakawaambia ondokeni tu hivi si kweli hata kidogo. Mheshimiwa Felix Mkosamali, mimi naomba nikuweke vizuri pale wenyewe kijiji kilisema hivi tunakabidhi eneo hili kwa ajili ya Magereza, Magereza wakaenda waka-develop lile eneo. Baadaye ikaonekana lile eneo la Sambala linaonekana lipo katika eneo lile la magereza wakakubaliana kwamba eneo hilo liondolewa, yaani liwe skilled out likaondolewa. Wale wananchi wachache waliobaki kule ndani wakatolewa wakatakiwa waingie kwenye hilo eneo dogo yaani hiyo Sambala wakatoka pale wala hawakufukuzwa pale, baada ya hapo wakajisikia vibaya wakasema wanakwenda mahakamani, walipokwenda mahakamani nimesomea hapa kwamba mahakama bado ikaona Magereza ni mmiliki halali wa eneo lile kwa maana ya Serikali. Kwa hiyo, mimi ninachosema hapa mimi wala siyo msimamo wangu hapa huu, ni msimamo wa Serikali na wala wanaong’ang’ana hapa siyo nani wala nani ni Serikali. Ninachosema ni kwamba eneo hili ni mali ya Magereza. Mheshimiwa Naibu Spika, la pili msimamo huu siyo msimamo mkali ukiangalia proceedings na mambo yote yaliyozungumzwa hapa ni mambo tu yanayosema jinsi ambavyo nchi inatawaliwa tunazungumza habari ya good governance hapa kama tukishasema eneo hili ni kwa ajili ya shule ya msingi linakuwa ni eneo kwa ajili ya shule ya msingi. Kama kuna matatizo wananchi hawa hawana ardhi nimezungumza na Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa wa Kigoma na sasa hivi mnisisitizie wananchi hao waende kwa Mkuu wa Mkoa 7 11 APRILI, 2012 pale Kigoma bado ina ardhi ya kutosha watapatiwa mahali pa kukaa waende wakafanye kazi zao. Kwa hiyo, hakuna wasiwasi wowote, wala Serikali haijawa dormant hapa nawaomba wafanye hivyo kama wananisikiliza huko waliko waende wakamwone Mkuu wa Mkoa wa Kigoma.

View Full Text

Details

  • File Type
    pdf
  • Upload Time
    -
  • Content Languages
    English
  • Upload User
    Anonymous/Not logged-in
  • File Pages
    270 Page
  • File Size
    -

Download

Channel Download Status
Express Download Enable

Copyright

We respect the copyrights and intellectual property rights of all users. All uploaded documents are either original works of the uploader or authorized works of the rightful owners.

  • Not to be reproduced or distributed without explicit permission.
  • Not used for commercial purposes outside of approved use cases.
  • Not used to infringe on the rights of the original creators.
  • If you believe any content infringes your copyright, please contact us immediately.

Support

For help with questions, suggestions, or problems, please contact us