Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) BUNGE LA TANZANIA _______________ MAJADILIANO YA BUNGE _________________ MKUTANO WA NNE Kikao cha Thelathini na Nane – Tarehe 2 Agosti, 2011 (Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Spika (Mhe. Anne S. Makinda) Alisoma Dua HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI Hati ifuatayo iliwasilishwa Mezani na:- WAZIRI WA UCHUKUZI (RELI, BANDARI NA USAFIRI WA MAJINI): Randama za Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Uchukuzi kwa Mwaka wa Fedha 2011/2012. MASWALI NA MAJIBU Na. 348 Uchimbaji wa Bwawa Jimboni Mbogwe MHE. AUGUSTINO M. MASELE aliuliza:- Serikali imewazuia Wananchi wa Kijiji cha Nsango, Kata ya Iponya, kunywesha maji mifugo yao katika mto ulioko katika Hifadhi ya Msitu wa Kigosi Muyowosi kwa ahadi kwamba kutakuwa na Mradi wa Uchimbaji wa Bwawa ambalo lingetoa huduma mbadala ya maji ya mto:- Je, ni lini Serikali itakamilisha uchimbaji wa bwawa hilo? NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (TAMISEMI) alijibu:- Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri Mkuu, ninaomba kujibu swali la Mheshimiwa Augustino Manyanda Masele, Mbunge wa Mbogwe, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Spika, ni kweli taratibu za hifadhi za wanyamapori haziruhusu shughuli zozote za kijamii kufanyika ndani ya hifadhi ikiwemo unyweshaji wa mifugo. Kutokana na sababu hiyo, Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe katika Mwaka wa Fedha wa 2010/2011, iliandaa andiko la Mradi wa Ujenzi wa Bwawa na kuliwasilisha kwenye Mfuko wa Wanyamapori wa Taifa, ikiomba kupatiwa shilingi milioni 78.1 kwa ajili ya kazi hiyo. Mfuko wa Wanyamapori wa Taifa ulikubali kutoa kiasi cha shilingi milioni 25 kwa kazi ya ujenzi wa bwawa hilo. Fedha hizo kiasi cha shilingi milioni 25 zilitolewa tarehe 13 Julai, 2010 na kuingizwa kwenye akaunti ya Halmashauri kwa ajili ya ujenzi wa bwawa katika Kijiji cha Nsango kilichopo katika Kata ya Iponya na siyo ndani ya Hifadhi ya Taifa. Mheshimiwa Spika, kutokana na upungufu huo, Halmashauri imepanga kutumia fedha hizo kwa ajili ya kuanza kujenga bwawa kwa kuanza na tuta, yaani charco darm embankment construction, litakalogharimu kiasi cha shilingi milioni 28.2, ambapo shilingi milioni 3.2 ni mchango wa Halmashauri. Kazi ya ujenzi inatarajiwa kuanza tarehe 22 Agosti, 2011. Aidha, Halmashauri inajitahidi kuimarisha makusanyo ya mapato ya ndani kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa bwawa hilo kwa mwaka 2011/2012. 1 MHE. AUGUSTINO M. MASELE: Mheshimiwa Spika, ninakushukuru kwa kunipatia nafasi ili niweze kumwuliza Mheshimiwa Naibu Waziri swali moja la nyongeza. Ningependa kujua ni kiasi gani cha pesa ambacho Serikali imepanga mwaka huu wa fedha ili kuweza kukamilisha ujenzi wa bwawa hili? NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (TAMISEMI): Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu, ninaomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Masele, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Spika, hela zilizoombwa na Halmashauri kwa ajili ya kusaidia zilikuwa shilingi milioni 78.1; hela zilizotolewa na Idara ya Wanyamapori zilikuwa ni shilingi milioni 25; na hela ambazo Halmashauri imesema kwamba, itaongeza pale ni shilingi milioni 3.1; jumla shilingi milioni 28.1. Hizo ndizo hela zilizotengwa kwa ajili ya kazi hiyo. Na. 349 Utafiti wa Volkano ya Mlima Kilimanjaro MHE. BETTY E. MACHANGU aliuliza:- Hifadhi ya Mlima Kilimanjaro ilianzishwa rasmi mwaka 1973 kwa lengo la kuhifadhi Mlima huo na maeneo yanayouzunguka; Mlima huo una vilele vitatu ambavyo ni Shira, Mawenzi na Kibo; Kilele cha Shira kina volcano iliyokufa na vile vya Kibo na Mawenzi vina volcano iliyolala:- Je, Seriklai imefanya utafiti wowote kuhusu volcano ya vilele vya Mawenzi na Kibo ili kujua kama kuna uwezekano wa kulipuka wakati wowote katika uhai wa volcano? WAZIRI WA NCHI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS (MAZINGIRA) alijibu:- Mheshimiwa Spika, kabla ya kujibu swali la Mheshimiwa Betty Eliezer Machangu, Mbunge wa Viti Maalum, ninaomba nitoe maelezo ya awali kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Spika, ninakubaliana na Mheshimiwa Mbunge kwamba, Hifadhi ya Mlima Kilimajaro (KINAPA), ilianzishwa mwaka 1973 kwa lengo la kuhifadhi Mlima huo na maeneo yanayozunguka. KINAPA ilitambuliwa na UNESCO mwaka 1987 kama Hifadhi ya Dunia (Global Natural Heritage Sites) na imekuwa na mafanikio makubwa katika kuhifadhi na kusaidia jamii inayozunguka katika Miradi mbalimbali; kwa mfano, kuelimisha Wananchi, ujenzi na ukarabati wa barabara, shule, vituo vya afya na Miradi mingine. Pamoja na mafanikio hayo, bado kuna changamoto kubwa ya uharibifu wa mazingira unaosababishwa na uvamizi wa hifadhi kwa ajili ya makazi, kilimo na mifugo. Mheshimiwa Spika, sasa ninaomba kujibu swali la Mheshimiwa Betty Eliezer Machangu, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo:- Kama alivyoeleza Mheshimiwa Machangu, Mlima Kilimanjaro una vilele vikubwa vitatu: Kibo urefu wa mita (5,895), Mawenzi (mita 5,149) na Shira (mita 3,962), juu ya usawa wa bahari. Vilele hivyo vilitokana na mlipuko mkubwa wa volcano miaka milioni moja iliyopita. Taarifa za Wataalam zimethibitisha kwamba, volcano za Mawezi na Shira zimekufa (Dead Volcano); maana yake hakuna uwezekano wa kulipuka tena kwenye vilele hivyo. Mheshimiwa Spika, kuhusu Kibo, volcano kwenye kilele hicho, inasemekana imelala, lakini kuna dalili halisi za uhai. Kwenye kasoko (crater) ya Kibo kuna chemchemi zinazofukuta, zenye majivu ya moto na kutoa gesi aina ya salfa. Tukio la mwisho kulipuka lilitokea miaka 200 iliyopita na kusababisha shimo (Ash Pit), ambalo lipo mpaka hivi leo. Mheshimiwa Spika, ninapenda kuliarifu Bunge lako Tukufu kuwa, hakuna utafiti wa kina uliofanywa kuangalia uwezekano wa kulipuka tena. Hata hivyo, kutokana na matukio ya milipuko 2 ya hivi karibuni, sehemu mbalimbali duniani, Serikali kupitia Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA), linakusudia kutafuta wataalam wa mlipuko wa volcano ili kufanya utafiti na kuangalia uwezekano wa kulipuka tena kwenye kilele hicho. Sasa hivi Wizara yangu ikishirikiana na TANAPA, ipo kwenye mchakato wa kutafuta mabingwa hao. MHE. BETTY E. MACHANGU: Mheshimiwa Spika, ninaomba kuuliza swali moja la nyongeza kama ifuatavyo:- Kwa vile tafiti duniani zinaonesha kwamba mpaka mwaka 2025 barafu ya Mlima Kilimanjaro itakuwa imeyeyuka. Je, Serikali imefanya tafiti zozote au inafanya mkakati gani kuunusuru Mlima huo na tatizo hilo? WAZIRI WA NCHI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS (MAZINGIRA): Mheshimiwa Spika, ninaomba kujibu swali la Mheshimiwa Betty Machangu, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Spika, ni kweli kabisa barafu ya Mlima Kilimanjaro inayeyuka na nilishawahi kujibu swali kama hili hapa Bungeni kwamba, tafiti mbalimbali zimefanyika ikiwemo University of Dar es Salaam, Mashirika mbalimbali na pia Shirika la Climate Change wamefanya tafiti na tafiti ya mwisho ilitolewa mwaka 2007 kwamba; ni kweli barafu ya Mlima Kilimanjaro itayayuka kutokana na climate change. Ninachoweza kusema ni kwamba, Wananchi wa Mkoa wa Kilimanjaro, wajitahidi sana na sisi wote tujitahidi kuutunza Mlima huu, kwa sababu kwanza, nimesema kabisa kuna kilele cha Kibo, volcano inaweza ikatokea kwa sababu bado volcano yake iko high. Kwa hiyo, tunapoendelea kuharibu zaidi huo Mlima, maana yake tunaleta madhara yaliyoko ndani ya Mlima ule chini kabisa na mengine yanayosababishwa na wanaadamu. Kwa hiyo, sisi wote kwa pamoja tujitahidi kuuhifadhi huo Mlima kwa kupanda miti ya kutosha ili kuunusuru usiendelee kulipuka na pia kusitokee madhara ambayo yanasababishwa na wanaadamu. Ahsante. Na. 350 Mgao wa Fedha za Wafadhili MHE. MARIAM SALUM MSABAHA aliuliza:- Wazanzibari wengi wanakerwa na matatizo ya Muungano kama vile mgao wa fedha zitokanazo na Wafadhili kwa ajili ya maendeleo:- Je, kwa nini misaada haitolewi kwa uwiano na wakati mwingine haiwafikii Wazanzibari? WAZIRI WA NCHI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS (MUUNGANO) alijibu:- Mheshimiwa Spika, kwa ruhusa yako, ninaomba kujibu swali namba 779, lililoulizwa na Mheshimiwa Mariam Salum Msabaha, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Spika, ni kweli kuwa zimekuwepo changamoto zilizojitokeza katika utekelezaji wa majukumu ya Muungano. Kati ya changamoto zilizojitokeza ni mgawanyo wa misaada na mikopo kutoka nje. Hata hivyo, suala la ugawaji wa misaada ya kibajeti inayotolewa na Wafadhili kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, limepatiwa ufumbuzi. Mheshimiwa Spika, ninapenda kuchukua nafasi hii kuwaarifu Waheshimiwa Wabunge kuwa, Zanzibar sasa inapata mgao wake wa fedha za misaada ya kibajeti na zimekuwa zikipitia Fungu 31 - Ofisi ya Mkamu wa Rais na kuwasilishwa kwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. Fedha hizo hutolewa kwa ajili ya nchi nzima. Mheshimiwa Spika, mgao wa fedha hizi hufuata formula iliyokubaliwa ya muda ya asilimia 4.5. Mheshimiwa Spika, kwa kutibitisha hayo niliyoyasema, ninaomba nisome takwimu za mgao wa fedha zilizokwenda Zanzibar kwa kipindi cha miaka mitano iliyopita. Katika mwaka wa fedha 3 2005/2006, Zanzibar ilipata mgao wa shilingi bilioni 18.6; 2006/2007 shilingi bilioni 23, 020,000; 2007/2008 shilingi bilioni 27,338,000; 2008/2009 shilingi bilioni 23, 040,000; na 2009/2010 shilingi bilioni 30, 200,000. Aidha, Serikali inaweka utaratibu wa namna bora ya kuhakikisha pande zote mbili za Muungano zinafaidika na fedha za misaada, mikopo na Miradi kutoka nje, kwa kuweka Mwongozo wa Ushirikishwaji wa Zanzibar katika Taasisi za Kimataifa. SPIKA: Mheshimiwa, hebu soma figure ya mwaka 2009/2010. WAZIRI WA NCHI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS (MUUNGANO): Mheshimiwa Spika, figure ya 2009/2010 ina marekebisho, siyo shilingi bilioni 50 bali ni shilingi bilioni 30. MHE. MARIAM SALUM MSABAHA: Mheshimiwa Spika, ninashukuru kwa majibu mazuri ya Waziri. Ninaomba kumwuliza maswali mawili ya nyongeza
Details
-
File Typepdf
-
Upload Time-
-
Content LanguagesEnglish
-
Upload UserAnonymous/Not logged-in
-
File Pages189 Page
-
File Size-