NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ________ MAJADILIANO YA BUNGE _________ MKUTANO WA KUMI NA TANO Kikao cha Ishirini na Tisa – Tarehe 16 Mei, 2019 (Bunge Lilianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Spika (Mhe. Job Y. Ndugai) Alisoma Dua SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, tukae. Waheshimiwa Wabunge tunaendelea na Mkutano wetu wa Kumi na Tano, leo ni Kikao cha Ishirini na Tisa tangu tumeanza. Katibu! NDG. STEPHEN KAGAIGAI – KATIBU WA BUNGE: TAARIFA YA SPIKA SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, nina taarifa mbili muhimu, taarifa ya kwanza, ningependa leo kuwajulisheni kuhusu hatua iliyofikiwa katika ukaguzi wa hesabu za Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi, wengi tumezoea kuiita Ofisi ya CAG kwa mwaka wa fedha unaoishia tarehe 30 Juni, 2018. Waheshimiwa Wabunge, kwa mujibu wa kifungu cha 46(1) cha Sheria ya Ukaguzi wa Umma, Sheria Namba 11 ya mwaka 2008, Hesabu za CAG yaani za Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi zinapaswa kukaguliwa angalau mara moja kwa mwaka na kwamba Bunge kupitia Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) huwa lina jukumu la kuteua Mkaguzi wa kukagua hesabu za ofisi hiyo. Kwa maneno rahisi, Bunge ndiyo tunatafuta Mkaguzi wa Nje ambaye ndiye anakagua hesabu za Ofisi ya CAG. 1 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) Kwa hiyo, kazi hiyo ilishafanyika huko nyuma na Kampuni ya Mkaguzi inayoitwa EK-Mangesho and Company ilikwishakupatikana na imefanya kazi hiyo ya ukaguzi na imetuletea taarifa ya hesabu zilizokaguliwa za ofisi hiyo. Nimeona niwajulisheni ili muweze kufahamu katika hesabu zilizowekwa mezani wakati ule hesabu za Ofisi ya CAG mwenyewe huwa haziwekwi mezani pale, utaratibu wake ni huu ninaoueleza ambao kuna kuwa na External Auditor anakagua, nawataarifu sasa Bungeni kwamba nimeshapokea taarifa hiyo na nimeshaipitia, kuna mambo, lakini utaratibu ni kwamba tunapeleka kwenye Kamati ya PAC sasa. Kwa hiyo, kwa kuzingatia Sheria ya Ukaguzi hiyo, naipeleka taarifa hii kwenye Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) ili waipitie na kuichambua na mara watakapomaliza kazi hiyo ya uchambuzi watawasilisha uchambuzi huo kwangu na mengine yatakayofuata yatakuwa wakati huo utakapokuwa umewadia, ni kuwataarifuni tu kwamba katika masuala ya ukaguzi, hakuna ambaye anabaki, na hakuna anayejikagua mwenyewe, ila watu wanaangalia wenzao. Waheshimiwa Wabunge la pili, tunao Wawakilishi wetu katika Mabunge mbalimbali ambao baadhi yao tumewachagua ndani ya Bunge. Tuna wawakilishi ambao tunawapeleka katika Bunge la SADC, SADC PF, Wabunge wenzetu wako hapa, kuna Wawakilishi tunawapeleka kwenye Bunge la PAP (Pan African Parliament), Bunge la Afrika. Tuna Wawakilishi huwa tunawapeleka kwenye ACP EU (African Caribbean Pacific na EU, na pia kuna Wawakilishi tunawapeleka kwenye Bunge linaitwa Great Lakes (IGLSA)Bunge la Maziwa Makuu. Wawakilishi hawa, tunawachagua watuwakilishe katika Mabunge hayo na wamekuwa wakifanya kazi nzuri, lakini katika uwakilishi wa Bunge la Afrika, kumejitokeza matatizo makubwa, hasa kwa Mheshimiwa Stephen Masele. 2 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) Kuna matatizo makubwa sana ya kinidhamu, ambayo nisingependa kuyafafanua leo muda hautoshi, lakini tumelazimika kumtafuta Mheshimiwa Masele kumrudisha nyumbani, kuanzia Jumatatu, badala yake amekuwa akionesha kugoma na hata jana kwenye Bunge hilo, clips zinaonesha zimerushwa, baada ya kumwandikia kwamba arudi nyumbani ili aje ahudhurie kwenye Kamati ya Maadili hapa, amekuwa akilihutubia lile Bunge akisema japo ameitwa na Spika lakini ameambiwa na Waziri Mkuu a- disregard wito wa Spika, aendelee tu na mambo yake kule, kitu ambacho ni uongo na kutudhalilisha kama nchi, ni kiongozi ambaye amekuwa akifanya mambo ya hivyo hovyo, na ndiyo maana tumemuita kidogo kwenye Kamati ya Maadili, atufafanulie, huenda labda yuko sahihi, lakini kwa mtazamo wetu amekuwa akifanya mambo ambayo ni hatari kubwa ikiwemo kugonganisha mihimili, anapeleka kwenye Mhimili wa Serikali juu kabisa, maneno mengi ya uongo na ushahidi upo na kulidhalilisha Bunge, ni kiongozi amejisahau, hajui hata anatafuta kitu gani. Ukiacha hizo vurugu ambazo hivi sasa zinazoendelea kwenye Bunge lake huko, ambazo anaziongoza yeye mwenyewe ni vurugu kubwa, hilo halituhusu sana, sisi tunamuita kwa ajili ya mambo ya hapa nyhumbani ya utovu wa nidhamu. Sasa kwa kuwa tumekuwa tukimuita tangu jumatatu, hataki kurudi, ningependa kulifahamisha Bunge hili kwamba kwa niaba yenu na kwa mamlaka niliyonayo basi, nimemwandikia barua Rais wa PAP ya kusitisha uwakilishi tuliompatia Mheshimiwa Masele katika Bunge la PAP hadi hapo Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge itakapokamilisha uchunguzi wa tuhuma dhidi yake na kukamilisha taarifa yake. Kwa hiyo, kwa muda (temporarily suspension) ya Mheshimiwa Masele kuwa Mbunge wa Bunge la Afrika hadi hapo tutakapomalizana naye hapa na hapa kuna Kamati mbili zinamsubiri, Kamati Maalum hii ya Bunge ya Maadili, lakini pia Kamati ya Maadili ya Chama chake nayo kuna mambo inamuhitajia, kuja kuyajibu hapa nyumbani. 3 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) Kwa hiyo, kuanzia sasa yeye siyo Mbunge wa Bunge hilo tena, hadi tumalize masuala ya hapa nyumbani, ndiyo tutaamua wenyewe, mambo haya huwa tunaamua wenyewe, tunaendeleaje kuanzia hapo. Katibu! NDG. STEPHEN KAGAIGAI-KATIBU WA BUNGE: HATI ZA KUWASILISHA MEZANI SPIKA: Hati za Kuwasilisha Mezani, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa. Ooh! Samahani, tuna Waziri wa Kilimo kwanza, samahani sana, Waziri wa Kilimo, ulikaa mbali bwana, Mheshimiwa Naibu Waziri Kilimo, Mheshimiwa Bashungwa tafadhali, Innocent. NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Randama za Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Kilimo na Taasisi zake kwa mwaka wa fedha 2019/ 2020. SPIKA: Ahsante sana Naibu Waziri Kilimo, Mheshimiwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, naomba nikuite uweke mezani hati zako. WAZIRI WA ULINZI NA JESHI LA KUJENGA TAIFA: Hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa kwa mwaka wa fedha 2019/2020. SPIKA: Ahsante sana Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Hussein Mwinyi, tunakushukuru. Mwenyekiti wa Kamati ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, tafadhali. Kwa niaba yake, Mheshimiwa Bonnah Kaluwa. 4 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) MHE. BONNAH M. KALUWA - K.n.y MWENYEKITI WA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA MAMBO YA NJE, ULINZI NA USALAMA: Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge, Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama kuhusu utekelezaji wa bajeti, majukumu ya Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa kwa mwaka wa fedha 2018/2019 pamoja na Maoni ya Kamati kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2019/2020. SPIKA: Ahsante, Mheshimiwa Bonnah Kaluwa, Mbunge wa Segerea. Sasa naomba nimuite Msemaji Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzania Bungeni hukusu Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa. Mheshimiwa Joseph Selasini, tafadhali! MHE. JOSEPH R. SELASINI - MSEMAJI MKUU WA KAMBI RASMI YA UPINZANI BUNGENI KUHUSU WIZARA YA ULIZNI NA JESHI LA KUJENGA TAIFA: Taarifa ya Msemaji Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni kuhusu Wizara ya Ulizni na Jeshi la Kujenga Taifa juu ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2019/2020. SPIKA: Ahsante sana Mheshimiwa Selasini. Katibu. NDG. STEPHEN KAGAIGAI-KATIBU WA BUNGE: MASWALI NA MAJIBU SPIKA: Maswali, swali la kwanza linaelekea Ofisi ya Mheshimiwa Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa na litaulizwa na Mheshimiwa Sabreena Gabriel Sungura, Mbunge wa Viti Maalum, kwa niaba yake Mheshimiwa Susan. 5 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) Na. 239 Hitaji la Mashine ya Utra Sound Kituo cha Afya Ujiji MHE. SUSAN L. KIWANGA (K.n.y MHE. SABREENA H. SUNGURA) aliuliza:- Kituo cha Afya Ujiji kinahudumia zaidi ya wakazi 20,000 lakini kituo hicho hakina mashine ya ultrasound. Je, ni lini Serikali itapeleka mashine ya ultrasound katika kituo hicho? SPIKA: Ahsante sana, Mheshimiwa Naibu Waziri, TAMISEMI, Mheshimiwa, majibu ya swali hilo, vituo vya afya vinatakiwa viwe na ultrasound? Karibu. NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. JOSEPHAT S. KANDEGE) Alijibu:- Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (TAMISEMI), naomba kujibu swali la Mheshimiwa Sabreena Sungura, Mbunge wa Viti Maalum kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2018/19, Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma/Ujiji imeidhinisha kiasi cha Shilingi 15,475,254.28 kupitia Mradi wa Malipo kwa Ufanisi (Result Based Financing) kwa ajili ya ukarabati wa chumba kitakachotumika kwa huduma za mionzi na shilingi 45,000,000.00 zimetengwa kwa ajili ya ununuzi wa ultrasound. Fedha hizo zimepelekwa MSD kwa ajili ya taratibu za ununuzi wa kifaa hicho. Kwa sasa huduma ya Ultrasound inapatikana katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Maweni na Hospitali Teule ya Manispaa ya Baptist. SPIKA: Mheshimiwa Susan, swali la nyongeza. MHE. SUSAN L. KIWANGA: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa kunipa nafasi nipate kuuliza maswali mawili ya nyongeza. 6 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) Kwa kuwa suala la ultrasound katika vituo vya afya au Hospitali za Wilaya na Halmashauri, ni suala kubwa sana na halipatikani maeneo mengi nchini Tanzania na hii inaathiri kina mama na wanaokwenda katika Hospitali hizo kuangalia hali zao za kiafya hasa katika suala la tumbo. Je, ni lini sasa Serikali itaweka mkakati kupeleka ultrasound kwenye vituo vyote vya afya nchini Tanzania na Hospitali za Wilaya ili wanawake wapate huduma hizo katika hospitali nchini? (Makofi) Mheshimiwa Spika, katika Jimbo la Mlimba, Kituo cha Afya cha Mlimba kina ultrasound na mfuko wa Jimbo nilichukua nafasi mimi kumpeleka kwa kuomba na DMO kwenda kumsomesha mtaalam ambaye amesharudi na huduma hii inapatikana Kituo cha Afya
Details
-
File Typepdf
-
Upload Time-
-
Content LanguagesEnglish
-
Upload UserAnonymous/Not logged-in
-
File Pages268 Page
-
File Size-