6 FEBRUARI, 2015 BUNGE LA TANZANIA __________________ MAJADILIANO YA BUNGE ____________________________ MKUTANO WA KUMI NA NANE Kikao cha Kumi – Tarehe 6 Februari, 2015 (Mkutano Ulianza Saa 3.00 Asubuhi) D U A Spika (Mhe. Anne S. Makinda) Alisoma Dua HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI Hati Zifuatazo Ziliwasilishwa Mezani na:- NAIBU WAZIRI WA FEDHA (MHE. MWIGULU L. N. MADELU): Muhtasari wa Tamko la Sera ya Fedha (Mapitio ya Nusu Mwaka), Februari, 2015. [The Monetary Policy Statement (The Mid-Year Review), February, 2015] SPIKA: Ahsante sana. Mwenyekiti wa Kamati Teule ya Bunge au Mwakilishi wake. Mwakilishi wake Mheshimiwa Magdalena Hamis Sakaya. 1 6 FEBRUARI, 2015 MHE. MAGDALENA HAMIS SAKAYA (K.n.y. MWENYEKITI WA KAMATI TEULE YA BUNGE): Taarifa ya Kamati Teule ya Bunge Iliyoundwa Kuchunguza na Kuchambua Sera Mbalimbali Zinazohusu Masuala ya Ardhi, Kilimo, Mifugo, Maji na Uwekezaji, ili Kubaini Kasoro Zilizomo Katika Matumizi ya Ardhi. SPIKA. Ahsante sana, Katibu tuendelee! MASWALI NA MAJIBU Na. 107 Wafungwa na Mahabusu Kutoruhusiwa Kupiga Kura MHE. EZEKIA D. WENJE aliuliza:- Mtu anapokuwa mfungwa/mahabusu hakumwondolei haki zake za msingi kama vile haki ya kuishi na haki ya uraia; na kwa kuwa moja ya sifa ya mtu kupiga kura ni uraia:- Je, ni kwa nini wafungwa na mahabusu wa nchi hii hawaruhusiwi kupiga kura? WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, URATIBU NA BUNGE alijibu:- Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri Mkuu napenda kujibu swali la Mheshimiwa Ezekiel Dibogo Wenje, kama ifuatavyo:- Ibara ya 1(5)ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977, inafafanua kuwa kila raia wa Tanzania aliyetimiza umri wa miaka 18 anayo haki ya kupiga kura katika uchaguzi unaofanywa Tanzania. 2 6 FEBRUARI, 2015 Hata hivyo, kwa mujibu wa ibara ya 5(2) ya Katiba hiyo na sheria za Uchaguzi, wafungwa wenye vifungo kuanzia miezi sita na kuendelea hawaruhusiwi kupiga kura. Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia Tume ya Taifa ya Uchaguzi, imeshaaza kufanya utafiti na mazungumzo na taasisi zinazohusika na kundi la wafungwa chini ya miezi sita na mahabusu ili kuweka utaratibu mzuri wa kuwawezesha kushiriki katika mchakato wa Uchaguzi kuanzia kuandikishwa katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura na kushiriki kwenye zoezi zima la uchaguzi. MHE. EZEKIA D. WENJE: Mheshimiwa Spika, nashukuru sana, baada ya kusoma majibu niliyopewa, ilibidi nichukue Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Katiba yetu, siyo kweli kwamba katika Ibara yake ya 5(2), inasema kwamba wafungwa waliofungwa kifungo cha zaidi ya miezi sita, wasiwe na uwezo wa kupiga kura. Ukisoma Katiba hiyo, Ibara ya 5(2) (c) inasema: Watu waliotiwa hatiani kwa makosa fulani ya jinai, siyo hata makosa yote ya jinai, lakini pia haijaweka limit ya kifungo. Mheshimiwa Spika, sasa maswali yangu ni kama ifuatavyo:- (1), Serikali imesema kwamba wameanza mazungumzo na wanaohusika, Tume ya Uchaguzi ya Taifa kuweka utaratibu wa hawa wafungwa kupiga kura. Je, Serikali inatupa commitment, kwamba katika huu uchaguzi unaokuja, mwaka huu na katika hata referendum, watakuwa wamemaliza huo mchakato, ili hao watu ambao wako gerezani pamoja na mahabusu, wapate hiyo haki yao ya msingi ya Kupiga Kura. (Makofi) 3 6 FEBRUARI, 2015 (2), Mheshimiwa Spika, ni dhahiri kwamba Katiba haisemi, haikatazi hawa watu Kupiga Kura, hata hawa watu waliofungwa zaidi ya labda miaka miwili, mwaka mmoja ambao hawajaua mtu, yaani ni makosa tu fulani fulani ya jinai, wengine wamefungwa labda kwa makosa ya madai, sasa hawa pia watawekewa utaratibu lini wa kupata haki yao ya msingi ya kupiga kura? WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, URATIBU NA BUNGE: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu maswali mawili ya Mheshimiwa Wenje, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Spika, unapopitia vifungu vile unavyosema Mheshimiwa Wenje, kifungu cha 5(1)(2), unapata yale makosa ambayo yanaweza kumfanya raia wa Tanzania asiweze kupiga kura, na wakati wa jibu langu la msingi nimesema, ukichukua Katiba, ukafuatilia pia na Sheria za Uchaguzi, zinatufikisha mahali ambapo ilikuwa si ruhusa kwa wafungwa kupata hiyo nafasi ya kuweza Kupiga Kura. Kwa hiyo, kwa swali lake la kwanza, commitment ya Serikali kama nilivyosema, kwa wafungwa wale ambao wamefungwa kifungo chini ya miezi sita, tayari mchakato umeshaanza wa kuangalia ni namna gani mwaka huu wanaweza wakasaidiwa na kuona wanapatiwa haki yao ya Kupiga Kura. Lakini baada ya kutathimini sheria na mambo yote ambayo yanawapelekea wao kupata haki hiyo. Mheshimiwa Spika, lakini kwa sababu Mheshimiwa Mbunge ametaka pia kujua na wale wengine ambao hawakuhukumiwa kwa makosa ya jinai, Serikali inasema nini kuhusu juu yao! Serikali itaendelea kuangalia Katiba na sheria mbalimbali na kama zitatufikisha katika hatua ya kuona kwamba wanastahili kupata haki hiyo ya kupiga kura, basi Serikali itafanya hivyo. 4 6 FEBRUARI, 2015 Kama itaona kwamba, kwa mujibu wa Katiba na kwa mujibu wa sheria mbalimbali, suala hilo litakuwa gumu, basi tutaendelea kuwa na mfumo utaratibu tulionao sasa. (Makofi) MHE. MARYAM SALUM MSABAHA: Mheshimiwa Spika, na mimi nimwulize Waziri swali la nyongeza. Kwa kuwa ndani ya mahabusu kuna wafungwa wengi wamo mle wengine wanasoma mpaka wanafika kuhitimu shahada ya sheria na wakirudi uraiani mnawatambuaje nao angalau wapate kazi za kuajiri kama wananchi wengine ambao wako uraiani? SPIKA: Kazi za kuajiriwa! WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, URATIBU NA BUNGE: Mheshimiwa Spika, namshukuru sana Mheshimiwa Maryam Msabaha, kwa swali la nyongeza. Mheshimiwa Spika, haki ya kujiajiri ama kuajiriwa katika nchi yetu ya Tanzania haimfungi mtu yeyote mahali popote na wakati wowote. Kama wako wafungwa, ambao katika kipindi chao cha kutumikia kifungo, wameweza kusoma na kupata taaluma mbalimbali, na mara wanapomaliza kifungo chao na kuwa raia huru nje ya magereza, tunawaomba tu, wafuate utaratibu wa kisheria wa nchi yetu, matangazo ya ajira za kuajiriwa yanatolewa kwa taratibu na Watanzania wote wanaruhusiwa kuomba na wote wataajiriwa kama wanazo sifa za kupatiwa ajira. Vile vile nichukue nafasi hi kuwahimiza wafungwa wanapotoka ndani ya kifungo chao, na kama wameweza kupata ujuzi na elimu zaidi ya ile walioyokuwa nayo, iko nafasi pia ya kupatiwa ushauri na wakaweza pia kujiajiri kutokana na taaluma walizonazo. (Makofi) 5 6 FEBRUARI, 2015 Na. 108 Kuwawezesha Wajasiriamali MHE. DKT. HENRY D. SHEKIFU aliuliza:- Suala la la kuwawezesha wajasiriamali na vikundi mbalimbali vya wananchi wanaohitaji kupambana na umasikini ni jambo muhimu sana:- (a) Je, Serikali ina mkakati gani wa dhati wa kuwawezesha wajasiriamali na vikundi mbalimbali vinavyohitaji msaada? (b) Je, kwa nini Serikali isianzishe chombo au benki ya wajasiriamali? WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, MAHUSIANO NA URATIBU alijibu:- Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Dkt. Henry Dafa Shekifu, Mbunge wa Lushoto, lenye sehemu (a) na (b) kama ifuatavyo:- (a) Mheshimiwa Spika, Serikali inawawezesha wajasiriamali na vikundi mbalimbali vinavyohitaji msaada kupitia sera ya uwezeshaji wananchi kiuchumi ya mwaka 2004 na sheria ya uwezeshaji wananchi kiuchumi namba sita ya mwaka 2004. Sera ya uwezeshaji wananchi kiuchumi, imeainisha nia ya Serikali ya kuweka mazingira mazuri ya upatikanaji kwa kuboresha vyanzo vya akiba na kuchukua hatua za kuondoa vikwazo mbalimbali ili kuwezesha mabenki kukopesha kikamilifu amana zilizopo na kwa gharama nafuu. Kutokana na sera hii, mipango ya miradi na mifuko mbalimbali imeanzishwa ili kuwawezesha wananchi kukopa kwa urahisi. 6 6 FEBRUARI, 2015 Mifano ya mipango na mifuko hiyo ni pamoja na Mpango wa Kuwadhamini Wajasiriamali Wadogo na wa kati unaosimamiwa na Benki Kuu ya Tanzania, Mpango wa Kuwawezesha Wananchi na kuongeza ajira. Mfuko wa Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi, Mradi wa kutoa Mikopo kwa Wajasiriamali Wadogo au Self, Mfuko wa Maendeleo ya Vijana, Mfuko wa Maendeleo ya Wananwake, Mfuko wa Rais wa Kujitegemea, Shirika la Maendeleo la Viwanda Vidogo MKURABITA, Mradi wa Kukuza Ushindani wa Sekta Binafsi na kadhalika. Aidha, umeanzishwa Mpango Kazi wa Serikali wa Kuboresha Mazingira ya Biashara na Uwekezaji Nchini kwa lengo la kuwapunguzia wajasiriamali muda na gharama za kuwekeza na kufanya biashara. (b) Mheshimiwa Spika, kwa kutambua umuhimu wa mikopo kwa wajasiriamali, Mwaka 2007 Serikali ilianzisha Benki ya Wanawake kwa lengo la kutoa mikopo kwa wajasiriamali. Kwa sasa Serikali inaendelea na mchakato wa kuanzisha Benki ya Majasiliamli katika sekta ya Kilimo pamoja na Biashara. Hata hivyo, utaratibu ulipo sasa, unaweshesha wakulima kuwapatia mikopo kupitia Benki ya Maendeleo ya Rasilimali, ambapo kumetengwa dirisha maalum kwa ajili ya mikopo ya pembejeo za kilimo. Mheshimiwa Spika, Serikali inatambua changamoto wanayokumbana nayo wajasiriamali wadogo wanapotaka kukopa kutoka katika taasisi za fedha, hasa zile za kibiashara. Hatua ya Serikali kuanzisha Benki ya Kilimo, Benki ya Wanawake na Dirisha la Kilimo katika Benki ya TIB ni kuwawezesha wajasiriamali wadogo kupata mikopo kwa urahisi. 7 6 FEBRUARI, 2015 Aidha Serikali kupitia Benki Kuu, inaendelea kufanya mazungumzo na wenye taasisi nyingine binafsi zinazotoa huduma za kifedha na mikopo ili kulegeza masharti ya kukopesha, likiwemo suala la riba za mikopo kuwa juu sana. (Makofi) MHE. DKT. HENRY D. SHEKIFU: Mheshimiwa Spika, nashukuru kwa majibu mazuri kiasi ya Waziri nina maswali madogo mawili ya nyongeza. Kwanza, ni ukweli usiopingika kwamba asilimia zaidi ya 60, ya wananchi wa nchi yetu ni vijana, na wao ndiyo wanahangaika kutafuta ajira, kutafuta mitaji. Waziri ameeleza vizuri kwamba iko sera. Je iliwahi kufanyika tathimini
Details
-
File Typepdf
-
Upload Time-
-
Content LanguagesEnglish
-
Upload UserAnonymous/Not logged-in
-
File Pages270 Page
-
File Size-