NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ____________ MAJADILIANO YA BUNGE ___________ MKUTANO WA KUMI NA MOJA Kikao cha Kumi na Sita– Tarehe 24 Aprili, 2018 (Bunge Lilianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Spika (Mhe. Job Y. Ndungai) Alisoma Dua SPIKA: Waheshimiwa Wabunge tukae. Waheshimiwa Wabunge tunaendelea na Mkutano wetu wa Kumi na Moja leo ni Kikao cha Kumi na Sita, Katibu. NDG. PAMELA PALLANGYO – KATIBU MEZANI: MASWALI NA MAJIBU SPIKA: Tunaanza na Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, swali la kwanza linaulizwa na Mheshimiwa Mbunge wa Babati Mjini, Mheshimiwa Pauline Gekul. Na. 125 Hitaji la Maji Safi na Salama Kata ya Sigino - Babati MHE. PAULINE P. GEKUL aliuliza:- Kata ya Sigino na Vijiji vyake vyote katika Jimbo la Babati Mjini haina kabisa maji safi na salama:- Je, ni nini mkakati wa Serikali wa kuipatia maji safi na salama Kata hiyo pamoja na Vijiji vyake? 1 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. JOSEPH G. KAKUNDA) alijibu:- Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI naomba kujibu swali la Mheshimiwa Pauline Philip Gekul, Mbunge wa Babati Mjini, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Spika, ni kweli kwamba vijiji vyote vinne katika Kata ya Sigino ndani ya Halmashauri ya Mji wa Babati vyenye wakazi 11,895 havina huduma ya maji safi na salama. Hata hivyo ziko hatua mahsusi zinazoendele. Mnamo tarehe 29 Mei, 2017, Halmashauri ya Mji wa Babati ilisaini mkataba wa Sh.487,470,000 kujenga mradi wa maji katika Kijiji cha Imbilili ambao ulipangwa kukamilika tarehe 30 Juni, 2018 lakini Mkandarasi Black Lion Limited amebainika kuwa na uwezo mdogo kwani hadi sasa ametekeleza kazi kwa asilimia saba tu. Naishauri Halmashauri ambapo Mheshimiwa Pauline Gekul ni Diwani, itathmini haraka hali hiyo na ichukue hatua haraka kwa manufaa ya wananchi. Mheshimiwa Spika, hatua nyingine kubwa inayoendela ni utekelezaji wa mkataba kati ya Halmashauri na Mkandarasi Maswi Drilling Company Limited kuchimba visima virefu katika Vijiji vya Sigino, Singu na Haraa kwa shilingi milioni 94.5 ambao umefikia asilimia 25 na utakamilika tarehe 30 Juni, 2018. Usanifu na ulazaji wa mabomba yakayosambaza huduma za maji safi na salama kwa wananchi utaanza mwaka 2018/2019 kwa kutumia Sh.611,137,000 ambazo zimetengwa kutekeleza mradi huo. Ahsante. SPIKA: Swali la nyongeza Mheshimiwa Pauline Gekul. MHE. PAULINE P. GEKUL: Mheshimiwa Spika, ninakushukuru naomba niulize maswali mawili ya nyongeza. Mheshimiwa Spika, ni kweli majibu hayo aliyotoa Mheshimiwa Naibu Waziri ni ya kweli kabisa kwa hatua ambazo zinaendelea katika Halmashauri, lakini huyu Mkandarasi Maswi kimsingi amekuwa akitusumbua sasa 2 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) muda mrefu kweli amekuwa akitoa sababu mbalimbali kwamba sijui ni masika hawezi kutafuta haya maji. Sasa naomba kwa sababu ilikuwa ni commitment ya Waziri wa Maji alifika katika Kata hii na katika kijiji hiki, je, Wizara hii pamoja na Wizara ya Maji wanaweza wakatupa ushirikiano DDCA wakatusaidia, kwa sababu wao wanafahamu ni wapi maji yanapatikana badala ya huyu Maswi akaendelea kutusumbua na wananchi wale wakapata maji? Mheshimiwa Spika, swali la pili, nakubaliana na Mheshimiwa Naibu Waziri kwamba huyu Mkandarasi wa awali anayechimba maji katika Kijiji cha Imbilili kwa kweli amekuwa akitusumbua sana, lakini hayo tutayafanyia kazi kwenye Baraza letu kama alivyoshauri. Naomba nifahamu Wizara iko tayari sasa kuangalia bili tunazolipa za maji katika Mji wetu wa Babati kwa sababu wananchi wetu wakilalamika sana, pamoja na upungufu wa maji lakini wanatozwa bili kubwa sana za maji. Je, Wizara hii na Wizara ya Maji mko tayari ku-review bili ambazo wananchi wa Babati wanalipa? SPIKA: Mheshimiwa Pauline maswali yako mengi ni yenu wenyewe Halmashauri, kwani Wizara ya Maji ndiyo inapanga bei za maji kwenye huko Halmashauri? Mheshimiwa Naibu Waziri majibu. NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. JOSEPH G. KAKUNDA): Mheshimiwa Spika, swali la kwanza, kitaalam ni kweli kwamba huwezi kufanya utafiti mpya wa maji chini ya ardhi hasa kama unataka kuchimba visima wakati huu wa masika. Kwa hiyo, kama Mkandarasi ameomba muda kidogo apewe ambapo yupo asilimia 25 kwa sasa hivi, kama anapewa muda wa mwezi wa Tano anaweza akachukua muda wa mwezi mmoja kumalizia visima vile ambavyo alikuwa anachimba kwenye vile vijiji na ikiwezekana mwezi wa Sita au mwezi wa Saba akamaliza kazi ya kuchimba visima. Nashauri kitaalam apewe muda wa mwezi wa Tano na Sita ili kusudi aweze kukamilisha kazi yake vizuri. Mheshimiwa Spika, kama Mkandarasi huyu Maswi 3 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) ataondolewa sasa hivi halafu wakaanza mchakato mpya wa kumpata kazi mtu mwingine wanaweza wakachukua miezi sita kukamilisha kumpata Mkandarasi ambayo itakuwa ni siyo faida sana kwa wananchi. Kwa hiyo, nashauri avumiliwe kidogo kwa kipindi hiki cha miezi miwili ama mitatu ili aweze kukamilisha kazi yake. Wizarani tutasukuma ili kusudi aweze kufanya kazi yake kitaalam zaidi. Mheshimiwa Spika, swali la pili, ningependa kuisifu sana Mamlaka ya Maji Mjini Babati, kama ambavyo imesifiwa pale ambapo Waziri Mkuu alienda mwaka juzi waliisifu wao wenyewe BUWASA kwamba inafanya kazi nzuri na hata Mheshimiwa Diwani Sumaye ambaye anatoka kwenye Kata ile ya Sigino ambako hakuna maji kabisa, mbele ya Mheshimiwa Waziri Mkuu alisema kwamba bwana kwa kweli tunashukuru wenzetu wa Mjini Babati wanapata maji vizuri, tatizo hapo ni bili. Mheshimiwa Spika, ili kusudi ianzishwe bili, EWURA kabla hawajaidhinisha huwa wanafanya kitu kinaitwa mkutano wa wadau, wanajadili, wakishakubaliana wadau ndiyo bili ile inaidhinishwa. Kwa hiyo, nashauri Halmashauri kama inaona kwamba bili ni kubwa basi wawasiliane na EWURA kwa barua rasmi ili kusudi suala hilo liweze kutatuliwa. Mheshimiwa Spika, ahsante. SPIKA: Tunaendelea Waheshimiwa Wabunge na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, swali la Mheshimiwa Pascal Yohana Haonga Mbunge wa Mbozi kwa niaba yake, Mheshimiwa Selasini. Na. 126 Changamoto Zinazokabili Shule za Watu Binafsi MHE. JOESPH R. SELASINI (K.n.y. MHE. PASCAL Y. HAONGA) aliuliza:- Shule za Watu Binafsi zinatoa huduma ya elimu kama 4 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) zilivyo Shule za Umma, lakini kwa muda mrefu zimekuwa zikikabiliwa na changamoto nyingi sana ikiwa ni pamoja na kodi ya majengo (property tax), tozo ya fire, kodi ya ardhi na kodi nyinginezo:- (a) Je, Serikali haioni sasa ni wakati muafaka wa kuondoa baadhi ya kodi zisizokuwa na tija ambazo zimekuwa kero kwa shule za watu binafsi? (b) Je, Serikali haioni ni wakati sasa wa kuzipatia ruzuku shule binafsi kwa sababu zinashirikiana na Serikali kupunguza tatizo la ajira? NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA alijibu:- Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Pascal Yohana Hasunga, Mbunge wa Mbozi, lenye sehemu (a) na (b) kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Spika, Serikali inatambua na kuthamini mchango wa sekta binafsi katika maendeleo ya elimu nchini ambapo hadi sasa jumla ya shule za msingi 1,432 kati ya shule 17,583 zinamilikiwa na sekta binafsi. Aidha jumla ya shule za sekondari 1,250 kati ya shule 4,885 zinamilikiwa na sekta binafsi. Vilevile kati ya vyuo vikuu 34, vyuo 22 vinamilikiwa na sekta binafsi. Kwa mchanganuo huo ni dhahiri kuwa sekta binafsi ina mchango mkubwa katika kuongeza fursa na ubora wa elimu nchini. Mheshimiwa Spika, Serikali imekuwa ikishirikiana na wamiliki wa shule binafsi kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili ikiwemo kodi na tozo. Katika kutatua changamoto hizo hadi kufikia sasa Serikali imeweza kuondoa tozo ya uendelezaji ujuzi (Skills Development Levy-SDL) tozo ya zimamoto, kodi ya mabango na tozo ya usalama mahali pa kazi (OSHA). Mheshimiwa Spika, hii ikiwa ni hatua ya Serikali 5 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) kuhakikisha kuwa sekta binafsi inakuwa na mazingira rafiki na wezeshi katika kuwaletea Watanzania maendeleo. Hivyo, Serikali kwa kushirikiana na umoja wa wamiliki wa shule binafsi itaendelea kujadiliana na kutatua changamoto zinawakabili ili kuvutia uwekezaji katika sekta ya elimu nchini. Mheshimiwa Spika, kuhusu kuzipatia ruzuku shule binafsi, Serikali itaendela kuboresha mazingira ya Taasisi za Fedha ili sekta binafsi iweze kupata mitaji kwa gharama nafuu huku Serikali ikiendelea kupunguza changamoto zilizopo katika shule za umma. SPIKA: Mheshimiwa Selasini nilikuona. MHE. JOSEPH R. SELASINI: Mheshimiwa Spika, nnakushukuru na nashukuru kwa majibu ya Serikali. Kabla sijauliza maswali mawili ya nyongeza naomba tu jina la muuliza swali lisomeke kama Pascal Yohana Haonga siyo Pascal Yohana Hasunga. Baada ya masahihisho hayo kidogo naomba niulize maswali yangu mawili ya nyongeza kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Spika, swali la kwanza, mara nyingi Serikali imekuwa ikizungumzia na kutoa matamko kuhusu ada zinazopangwa na shule za binafsi ikionesha kana kwamba Serikali ina mpango wa kuweka kiwango fulani cha ada bila kuzingatia gharama ambazo shule hizi zinaingia katika kusomesha wale watoto na kuendesha shule zao. Je, kwa nini Serikali isiwaachie wamiliki wakapanga hizi ada wenyewe ili wazazi ambao wanaweza wakamudu ada hizo waenda kwenye shule bila kikwazo? Mheshimiwa Spika, swali la pili, mara nyingi shule zinapanga taratibu zao za namna ya kuwafanya hawa watoto waweze kufaulu, kwa mfano, kuwawekea mitihani kutoka kwenye daraja fulani kwenda kwenye daraja fulani, lakini Serikali pia inaonesha haifurahishwi na jambo hili. Je, kwa nini Serikali isiache hizi shule zikapanga utaratibu wa kuwafanya hawa watoto waweze kufaulu kulingana
Details
-
File Typepdf
-
Upload Time-
-
Content LanguagesEnglish
-
Upload UserAnonymous/Not logged-in
-
File Pages201 Page
-
File Size-