Majadiliano Ya Bunge Mkutano Wa Kumi Na Mbili

Majadiliano Ya Bunge Mkutano Wa Kumi Na Mbili

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) BUNGE LA TANZANIA ______________ MAJADILIANO YA BUNGE ______________ MKUTANO WA KUMI NA MBILI Kikao cha Kumi na Moja – Tarehe 25 Juni, 2008 (Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Spika (Mhe. Samuel J. Sitta) Alisoma Dua MASWALI NA MAJIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge kama ilivyo ada swali la kwanza kwa leo linaelekezwa Ofisi ya Mheshimiwa Waziri Mkuu na linaulizwa na Mheshimiwa Clement Beatus Lyamba, Mbunge wa Mikumi. Na. 94 Ombi la Kufuta Hati Miliki ya Mashamba – Kilosa MHE. CLEMENT B. LYAMBA aliuliza:- Kwa kuwa, mashamba makubwa yaliyoko katika Majimbo ya Mikumi na Kilosa yametekelezwa na wamiliki kwa miaka mingi sasa; na kwa kuwa, wanavijiji waliokuwa vibarua, enzi hizo, wamezaliana na kuongezeka sana na hivyo kukosa maeneo ya kulima hali inayosababisha wahitaji maeneo hayo ili wajishughulishe na kilimo na hivyo kupunguza umaskini na kujiletea maisha bora:- Je, Serikali imefikia hatua gani kuhusu ombi la Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa lililowasilishwa Ofisi ya Waziri Mkuu la kuzifuta hati miliki za mashamba hayo ambayo orodha yake iliambatanishwa katika barua hiyo? NAIBU WAZIRI OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA alijibu:- Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu naomba kujibu swali la Mheshimiwa Clement Lyamba, Mbunge wa Mikumi, kama ifuatavyo:- 1 Mheshimiwa Spika, Mkoa wa Morogoro unayo mashamba makubwa yaliyomilikishwa kisheria lakini hayaendelezwi kama ilivyotarajiwa. Hali hii imekuwa ni kikwazo katika kufanikisha malengo na juhudi za Serikali za kuinua uchumi na kuongeza pato la Taifa kutokana na shughuli zilizotarajiwa kufanywa katika mashamba hayo; kuongezeka kwa kipato cha wananchi kutokana na ajira inayoweza kupatikana katika mashamba hayo. Aidha, kutokana na kukosa haki ya kuyatumia mashamba hayo maeneo hayo yamekuwa ni chanzo cha kuibuka kwa migogoro mingi ya ardhi pale baadhi ya wananchi ama wameyatumia au kuyavamia kwa lengo la kufanya shughuli mbalimbali za maendeleo. Mheshimiwa Spika, Serikali ilikwishatoa maelekezo kwa Uongozi wa Mkoa wa Morogoro kuandaa orodha ya mashamba yasiyoendelezwa ili kuiwezesha Serikali kufuta Hati Miliki za mashamba hayo. Mkoa umetekeleza maelekezo hayo baada ya Halmashauri kukamilisha taratibu muhimu za kisheria zinazohitajika kufanywa. Ofisi ya Waziri Mkuu, TAMISEMI imepokea taarifa ya Mkoa yenye mapendekezo ya:- · Kufuta miliki za mashamba 138 na ambayo yana ukubwa wa hekta zaidi ya 187,600. · Ugawaji upya wa mashamba kwa wanaoyahitaji. Katika taarifa hiyo, Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa imependekeza kufutwa kwa miliki za mashamba 39 yenye ukubwa wa hekari 34,350. Kwa kuwa wamiliki wa mashamba makubwa hawako Morogoro tu Ofisi ya Waziri Mkuu – TAMISEMI, imeziagiza Halmashauri zote nchini kuwasilisha Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi taarifa kuhusu mashamba yanayohodhiwa bila kuendelezwa ili hatua za kufuta miliki zao zichukuliwe. Maagizo hayo yamo kwenye barua Kumb. Na. CHA. 203/307/01/43 ya tarehe 28 Februari, 2008 na yalitumwa kwa Makatibu Tawala wa Mikoa yote nchini. Kwa kuzingatia taratibu za kisheria zinazohitajika kufanywa, Halmashauri zinaendelea na utekelezaji wa maagizo hayo. (Makofi) Mheshimiwa Spika, Ofisi yangu inatekeleza maelekezo haya ya Serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali muhimu ikiwa ni pamoja na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika, Wizara ya Fedha na Uchumi, Tume ya Kurekebisha Mashirika ya Umma na Kituo cha Uwekezaji. Utaratibu huu wa kushirikisha wadau hao una lengo la kuiepusha Serikali kwenye gharama kubwa za fidia na utatuzi wa migogoro baada ya Hati Miliki za mashamba hayo kufutwa na pia kurahisisha na kuweka utaratibu mzuri na wa haki wa kugawa maeneo ya mashamba haya kwa wanaoyahitaji. Hivyo, napenda kumshauri Mheshimiwa Mbunge kuwa na subira wakati Serikali ikiendelea kulifanyia kazi suala hili. Baada ya kukamilika kwa kazi hiyo Waheshimiwa Wabunge watafahamishwa matokeo ya kazi hiyo. MHE. CLEMENT B. LYAMBA: Mheshimiwa Spika, namshukuru sana Mheshimiwa Naibu Waziri kwa majibu yake yenye kutia matumaini kwa wananchi na wanavijiji katika maeneo husika hasa katika Kata za Masanze, Kilangali, Mabwelebwele, 2 Tindiga, Malui, Zombwe na Ulaya. Pamoja na majibu hayo naomba Mheshimiwa Waziri aweze kutoa time frame anayodhani ni muafaka ambapo anafikiri hatua hizo alizozieleza zitakuwa zimekamilika, kwa sababu wanavijiji wana shauku kubwa sana ya kuweza kuanza shughuli hizo za kujiinua kiuchumi kwa kilimo. Swali la pili, ni kwamba je, Serikali inaweza kutoa ahadi ya kutoa mwongozo katika ugawaji wa mashamba hayo wapewe vipaumbele wanavijiji wadogo wadogo, wakulima wanaozunguka mashamba hayo kabla ya kuwafikiria wafanyakazi na wafanyabiashara wengine wengi wanaweza pia kutoa maoni kama hayo? Ahsante Mheshimiwa Spika. NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Spika, katika swali hili la kwanza anataka kujua kwamba tunaweza tukachukua muda gani katika zoezi hili, ili liweze kuharakishwa na wananchi waweze kupata hiyo huduma ambayo wanataka kuipata kwa maana ya kupatiwa mashamba. Nimeeleza mchakato mzima ambao unahitajika hapa kwa ajili ya kazi hii na hapa tunazungumza mambo makubwa. Unazungumza juu ya kwamba unam-involve Rais wa nchi katika maana ya kufuta hatimiliki. Ninaamini kwamba zoezi hili sisi tutajitahidi kama Wizara kuhakikisha kwamba tunafanya haraka iwezekanavyo ili liweze kukamilika. Siamini kwamba ninaweza nikatamka hapa kwamba litachukua muda gani likaelezwa. Lakini naeleza tu nia ya Wizara katika maana ni kwamba tutahakikisha tunafanya haraka iwezekanavyo ili zoezi hili liweze kukamilika. Mheshimiwa Spika, kuhusu swali la pili la kwanza ninaweza kutoa maelekezo hapa kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu ili wakulima wadogo wadogo waweze kuangaliwa kwa karibu zaidi. Hii mimi sidhani kama nina tatizo nalo kwa sababu nchi hii ni nchi ya wakulima na wafanyakazi na humu ndani mna wafanyakazi na wakulima wa nchi hii. Kama kuna haja ya kuona kwamba tunafanya hivyo katika Ilani ya Uchaguzi wa Chama cha Mapinduzi tunatamka wazi wazi kwamba watapewa fursa za mwanzo mwanzo kwa maana ya kutumia ushirika. Kwa hiyo, naamini kwamba zoezi hili likikamilika hapa Serikali itahakikisha kwamba tunawasaidia wakulima wadogo wadogo ili waweze kupata mashamba haya kwa ajili ya kuweza kujikimu. Tusipofanya hivyo maana yake ni kwamba hawa wataendelea kuwa ni vibarua katika nchi yetu kitu ambacho ni kinyume kabisa na siasa yetu ya Ujamaa na Kujitegemea. (Makofi) MHE. JOHN S. MALECELA: Mheshimiwa Spika, baada ya majibu mazuri ya Naibu Waziri ningependa kuuliza swali moja la nyongeza. Serikali inayo mashamba makubwa sana katika Wilaya ya Kilombero ambazo ni sehemu za huko huko alikouliza Mbunge. Kuna shamba la Rwipa, Kotako, Rwipa ilikuwa tutengeneze sukari tukishirikiana na Wa-Cuba. Kotako ilikuwa tutengeneze shamba kubwa tukishirikiana na watu wa Korea, halafu Chita ni shamba ambalo kubwa sana walipewa JKT lakini 3 hawakuweza mpaka sasa hawaja-develop hata robo. Je, katika ardhi hizi ambazo ni kubwa sana Serikali inasema nini nazo zigawiwe kama jibu la kwanza? WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU: Mheshimiwa Spika, Mkoa wa Morogoro umeshajipanga vizuri sana tena mchakato wao umeshakamilika wa mashamba yote ya Mkoa wa Morogoro likiwepo shamba la Rwipa, Chita na mashamba mengineo. Mgawanyo wa mashamba hayo kwa upande wa Morogoro tayari wameshaweka mapendekezo kwamba ni ekari ngapi wapewe wanavijiji, ekari ngapi wapewe wawekezaji. Kwa hiyo, mchakato wa Mkoa wa Morogoro kwa ujumla umeshakamilika na mashamba hayo yatagawanywa kulingana na vipaumbele vya Mkoa vilivyoona. (Makofi) Pia niongezee kwamba Mkoa wa Morogoro tayari zoezi hili limeshakamilika. Kwa hiyo, wao wako mbele kwamba imeshafika Wizarani, Wizarani tumeshakaa pamoja na kukaa tayari tumeshaweka mapendekezo ya nini kifanyike ili yaende kwa Mheshimiwa Rais. Nitoe rai kwa mikoa mingine ambayo tumeiandikia yenye mashamba kama hayo wahakikishe kwamba mchakato uanzie kwenye Wilaya uingie kwenye RCCs ili mashamba makubwa ambayo wamepewa wawekezaji na hawajayatumia waweze kutuletea mapendekezo ili tuyapeleke mbele ili Rais aweze kutengua hatimiliki za hao wanaomiliki mashamba makubwa ambayo mpaka sasa hivi hayajafanyiwa kazi. Kwa mfano Mkoa wa Tanga una mashamba mengi ambayo yamechukuliwa na wawekezaji lakini mpaka sasa hivi hayajafanyiwa chochote. Kwa hiyo niwaombe Waheshimiwa Wabunge mshirikiane na Halmashauri husika ili kuhakikisha kwamba mchakato huu unafanyika haraka kama ulivyofanyika kwa Mkoa wa Morogoro. (Makofi) SPIKA: Waheshimiwa Wabunge tunaendelea. Bado tuko Ofisi ya Mheshimiwa Waziri Mkuu. Swali sasa linaulizwa na Mheshimiwa Felix Kijiko, Mbunge wa Muhambwe. Na. 95 Kituo cha Afya Kifura Kupatiwa Gari MHE. FELIX N. KIJIKO aliuliza:- Kwa kuwa, vituo vya afya vilivyoko Kibondo vilikuwa vikipata msaada wa magari toka Mashirika ya kuhudumia Wakimbizi hasa IRC; na kwa kuwa, Mashirika hayo sasa yamefunga shughuli zao na kwamba, kituo cha afya cha Kifura bado hakina gari la kuhudumia wagonjwa licha ya kuahidiwa kupewa gari siku nyingi:- Je, Serikali itakisaidiaje kituo hiki cha afya kupata gari ili kupunguza tatizo la vifo hasa vya akina mama wajawazito ambao hufariki kutokana na kushindwa kufika hospitalini kwa wakati? NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA alijibu:- 4 Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Felix Ntibenda Kijiko, Mbunge wa Muhambwe kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Spika, Kituo cha Afya cha Kifura kiko umbali wa kilometa 32 toka

View Full Text

Details

  • File Type
    pdf
  • Upload Time
    -
  • Content Languages
    English
  • Upload User
    Anonymous/Not logged-in
  • File Pages
    110 Page
  • File Size
    -

Download

Channel Download Status
Express Download Enable

Copyright

We respect the copyrights and intellectual property rights of all users. All uploaded documents are either original works of the uploader or authorized works of the rightful owners.

  • Not to be reproduced or distributed without explicit permission.
  • Not used for commercial purposes outside of approved use cases.
  • Not used to infringe on the rights of the original creators.
  • If you believe any content infringes your copyright, please contact us immediately.

Support

For help with questions, suggestions, or problems, please contact us