MKUTANO WA SABA Kikao Cha Nane – Tarehe 18 Aprili, 2017

MKUTANO WA SABA Kikao Cha Nane – Tarehe 18 Aprili, 2017

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ____________ MAJADILIANO YA BUNGE ____________ MKUTANO WA SABA Kikao cha Nane – Tarehe 18 Aprili, 2017 (Bunge Lilianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Spika (Mhe. Job Y. Ndugai) Alisoma Dua SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, tukae. Tunaendelea na Mkutano wetu wa Saba, Kikao cha leo ni Kikao cha Nane. Katibu! NDG. LAWRENCE MAKIGI – KATIBU MEZANI: Hati za kuwasilisha Mezani. HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na:- NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA: Hotuba ya Bajeti ya Ofisi ya Rais TAMISEMI kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018. WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA: Hotuba ya Bajeti ya Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018. 1 NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) MHE. JASSON S. RWEIKIZA – MWENYEKITI WA KAMATI YA UTAWALA NA SERIKALI ZA MITAA: Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa kuhusu utekelezaji wa majukumu ya Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017 pamoja na Maoni ya Kamati kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi hiyo kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018. Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa kuhusu utekelezaji wa majukumu ya Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017 pamoja na Maoni ya Kamati kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi hiyo kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018. MHE. RAPHAEL J. MICHAEL - MSEMAJI MKUU WA KAMBI YA UPINZANI KWA OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA: Taarifa ya Msemaji Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani kuhusu Ofisi ya Rais, TAMISEMI juu ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi hiyo kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018. MHE. CECILIA D. PARESSO - K.n.y. MSEMAJI MKUU WA KAMBI YA UPINZANI KWA OFISI YA RAIS, UTUMISHI NA UTAWALA BORA: Taarifa ya Msemaji Mkuu wa Kambi ya Upinzani kuhusu Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora juu ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi hiyo kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018. SPIKA: Katibu! NDG. LAWRENCE MAKIGI – KATIBU MEZANI: 2 NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) MASWALI NA MAJIBU Na. 60 Kuboresha Mfumo wa Taarifa za Kiutumishi na Mishahara (HCMIS) MHE. ABDALLAH D. CHIKOTA Aliuliza:- Je, ni lini Mfumo wa Taarifa za Watumishi LAWSON utaboreshwa na kuondoa dosari zilizopo sasa hivi kama vile watumishi wa Umma kuondolewa kwenye makato ya mikopo wakati hawajakamilisha malipo? WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA Alijibu:- Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Abdallah Dadi Chikota, Mbunge wa Jimbo la Nanyamba, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Spika, Mfumo wa Taarifa za Kiutumishi na Mishahara (Human Capital Management Informaton System) au kwa version nyingine ya LAWSON Version 9 unaotumika sasa kwa ajili ya kukusanya taarifa za kiutumishi na malipo ya mishahara ulianza kutumika mwaka 2012. Mheshimiwa Spika, ni kweli kwamba mfumo huu una changamoto ambazo zinasababisha watumiaji wasio waadilifu kuutumia vibaya kinyume na utaratibu ikiwemo kusitisha makato ya mkopo kabla mkopo wote haujamalizika kulipwa. Hii ilibainika kutokana na kaguzi za mara kwa mara zinazofanywa na Serikali ambapo hadi sasa watumishi wa aina hiyo wapatao 65 kutoka katika mamlaka za ajira 32 wamechukuliwa hatua mbalimbali baada ya kugundulika kuwa wametumia vibaya dhamana walizokabidhiwa. Mheshimiwa Spika, kutokana na changamoto hii, Serikali inaendelea na hatua za kuhamia kwenye toleo jipya 3 NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) la mfumo huu (LAWSON Version 11) ambao unatarajia kuwekwa mifumo zaidi ya udhibiti ili kuhakikisha kwamba maafisa wenye dhamana ya usimamizi wake hawafanyi mabadiliko yoyote bila kugundulika. Mheshimiwa Spika, usanifu wa mfumo huu ili kuweza kuhamia katika toleo jipya la LAWSON Version 11 unaendelea ambapo wataalam wetu wa Wakala wa Serikali Mtandao (EGA) ndio wamepewa jukumu la kusimamia usanifu na usimikaji wake. Baada ya maboresho haya miundombinu madhubuti ya kuzuia matumizi mabaya ya mfumo itaimarishwa. MHE. ABDALLAH D. CHIKOTA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi. Pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Waziri nina maswali mawili ya nyongeza. Ni wazi kwamba Mheshimiwa Waziri amekiri kwamba mfumo huu una upungufu na una changamoto nyingi ambazo nimeelezea mojawapo. Sasa nataka commitment ya Serikali kwamba hiyo Version 11 itaanza kutumika lini? Swali langu la kwanza. Mheshimiwa Spika, swali la pili; changamoto nyingine ya mfumo huu ni kwamba, unasimama peke yake (stand alone system) na wakati ukiangalia kwenye taasisi zetu, kwa mfano Mamlaka ya Serikali za Mitaa, kuna mifumo mingi, tulitegemea kwamba mifumo hii ingekuwa inaongea; kuna EPICA, kuna LGMD, sasa je, Mheshimiwa Waziri atanihakikishia kwamba mfumo huu mpya Lawson Version 11 utakuwa unaongea na mifumo mingine? (Makofi) WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru. Kwanza nimpongeze sana kwa namna ambavyo amekuwa akisimamia suala zima la management ya rasilimali watu katika utumishi wa umma na yeye mwenyewe pia alikuwa katika utumishi wa umma na tunafahamu mchango wake na tunauthamini. 4 NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) Mheshimiwa Spika, katika swali lake la kwanza, kwamba sasa Toleo hili la 11 ( Lawson Version 11) litaanza lini; nimhakikishie tu kwamba, katika Mwaka huu wa Fedha tumeshatenga Shilingi milioni 486 katika Idara yetu ya Usimamizi wa Rasilimali Watu pamoja na Idara yetu ya TEHAMA na nimhakikishie tu kwamba katika Mwaka huu wa Fedha suala hili litakamilika. Kama nilivyoeleza katika jibu langu la msingi, tumewakabidhi suala hili Wakala wa Serikali Mtandao ili waweze kusanifu na kusimamia usimikaji wake. Mheshimiwa Spika, katika swali lake la pili, kwamba ni lini sasa mfumo huu wa usimamizi wa rasilimali watu au taarifa za kiutumishi na mishahara utaweza kuzungumza na mifumo mingine kama mifumo ya kifedha kama EPICA na mingine; nimwambie tu kwamba tunaiona hoja yake na hata e-government wamekuwa wakifuatilia suala hili kwa makini sana, si tu katika suala zima la kuongea, hata katika kuhakikisha pia gharama za mifumo yenyewe na udurufu wa kuwa na mifumo mingi wakati kunaweza kukawa na mifumo michache ambayo inaweza ikazungumza. Mheshimiwa Spika, nimhakikishie tu kwamba pamoja na faida nyingine tutakazozipata tutakapoingia katika Lawson Version 11 ni pamoja na kuunganisha mifumo mingine kama EPICA lakini pia kuhakikisha Mifumo kama ya NECTA, NIDA, RITA pamoja na mingine nayo pia ni lazima izungumze na Mfumo wetu wa Lawson. SPIKA: Mheshimiwa Mwalimu Bilago, kuna shida gani ya Walimu tena huko! Swali la nyongeza! MHE. KASUKU S. BILAGO: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa kuniona. Wakati Serikali inafuatilia wafanyakazi hewa na ikagundua kwamba kulikuwa na wafanyakazi hewa wapatao 20,000, ni jambo sahihi na ni kweli kwamba Serikali hiyo iliwaondoa kwenye Mfumo wa Lawson wale waliopatikana kuwa hewa. Sasa nataka kujiuliza, na Waziri anisaidie, baada ya kugundua wafanyakazi 20,000 Serikali imekaa kimya habari ya ajira, naomba Serikali itoe kauli juu 5 NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) ya ajira ya wafanyakazi wakiwemo Walimu na Sekta nyingine za Idara ya Afya pamoja na Kilimo na kadhalika, naomba kauli ya Serikali. SPIKA: Swali hilo nalikataa kwa sababu leo ni siku ya Hotuba ya Mheshimiwa Waziri ili asianze kutoa yaliyo ndani ya hotuba yake lakini namuagiza Mheshimiwa Waziri katika kujibu hoja za Wabunge baadaye aichukue hoja hii iwe mojawapo ambayo ataifafanua, maana yake ni swali muhimu sana Mheshimiwa Mwalimu Bilago, sio kwamba nimelitupa, hapana, nimekuwekea akiba ili lije lijibiwe vizuri zaidi. Tunaendelea na Ofisi ya Mheshimiwa Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, swali la Mheshimiwa Zacharia Paulo Issaay, Mbunge wa Mbulu Mjini. Na. 61 Hali ya Maziwa Madogo Nchini MHE. ZACHARIA P. ISSAAY Aliuliza:- Maziwa Madogo nchini kama vile Ziwa dogo la asili la Tlawi katika Halmashauri ya Mji wa Mbulu yanaelekea kukauka kutokana na kuongezeka kwa magugu maji, kadhalika Ziwa Babati na Ziwa Manyara pia yana dalili ya kukauka na Mamlaka za Serikali za Mitaa hazina uwezo wa kuyaokoa:- (a) Je, Serikali haioni umuhimu wa kuyaokoa maziwa hayo muhimu katika ustawi wa nchi yetu na kizazi kijacho? (b) Je, kwa nini kusiwe na mpango kabambe wa Kitaifa kuyaokoa maziwa hayo? 6 NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) NAIBU WAZIRI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS, MUUNGANO NA MAZINGIRA Alijibu:- Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Zacharia Issaay, Mbunge wa Mbulu Mjini, lenye sehemu (a) na (b), kwa pamoja kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Spika, Serikali inaona umuhimu mkubwa wa kuokoa Ziwa dogo la Tlawi lililopo Halmashauri ya Mbulu na maziwa mengine kote nchini yanayokabiliwa na tishio la kukauka na magugu maji kutokana na kuongezeka kwa shughuli za binadamu hususan kilimo na ufugaji usio endelevu, uvuvi haramu na athari ya mabadiliko ya tabianchi. Mheshimiwa Spika, kutokana na umuhimu huo, mwaka 2008 Serikali iliandaa Mkakati wa Taifa wa Hatua za Haraka za Kuhifadhi Mazingira ya Bahari Ukanda wa Pwani, Maziwa, Mito na Mabwawa. Mkakati huu unaelekeza Wizara na sekta na halmashauri zote nchini kuchukua hatua za haraka kuzuia shughuli zote za binadamu kufanyika kandokando ya maziwa, mito na mabwawa ili kuzuia uharibifu wa mazingira unaoweza kusababisha kukauka kwa maziwa hayo. Mheshimiwa Spika, ili kunusuru Ziwa dogo la Tlawi, Serikali kupitia Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu imechukua hatua zifuatazo:- 1. Mradi wa DADP’s Wilaya ya Mbulu umetenga Shilingi milioni 100 katika mwaka wa fedha wa 2016/2017 kwa ajili ya kuondoa magugu maji katika Ziwa Tlawi. 2. Katika Bajeti ya Mwaka 2017/2018, Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu imepanga kutenga kiasi cha Shilingi 15,742,000 ili kutekeleza shughuli za kunusuru Ziwa Tlawi pamoja na kuainisha mipaka ya ziwa hilo, uvamizi wa watu katika shughuli za kilimo, kuhimiza kilimo endelevu pamoja na miinuko inayozunguka ziwa hilo, kutoa elimu kwa wananchi ya kuhifadhi 7 NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) mazingira na vyanzo vya maji, kuimarisha Kamati za Mazingira na ulinzi shirikishi kwa ziwa katika ngazi za kata, vijiji na mitaa.

View Full Text

Details

  • File Type
    pdf
  • Upload Time
    -
  • Content Languages
    English
  • Upload User
    Anonymous/Not logged-in
  • File Pages
    438 Page
  • File Size
    -

Download

Channel Download Status
Express Download Enable

Copyright

We respect the copyrights and intellectual property rights of all users. All uploaded documents are either original works of the uploader or authorized works of the rightful owners.

  • Not to be reproduced or distributed without explicit permission.
  • Not used for commercial purposes outside of approved use cases.
  • Not used to infringe on the rights of the original creators.
  • If you believe any content infringes your copyright, please contact us immediately.

Support

For help with questions, suggestions, or problems, please contact us