NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA __________ MAJADILIANO YA BUNGE __________ MKUTANO WA TATU Kikao cha Ishirini na Tisa – Tarehe 17 Mei, 2021 (Bunge Lilianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Naibu Spika (Mhe. Dkt. Tulia Ackson) Alisoma Dua NAIBU SPIKA: Waheshimiwa tukae. Katibu. NDG. MOSSY LUKUVI - KATIBU MEZANI: HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na:- NAIBU WAZIRI WA UJENZI NA UCHUKUZI (MHE. MWITA M. WAITARA): Hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi kwa mwaka wa fedha 2021/2022. NAIBU SPIKA: Ahsante sana. Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, Mheshimiwa Mtaturu. MHE. MIRAJI J. MTATURU K.n.y. MWENYEKITI WA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA MIUNDOMBINU: Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu kuhusu utekelezaji wa majukumu ya Wizara ya 1 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) Ujenzi na Uchukuzi kwa mwaka wa fedha 2020/2021 pamoja na Maoni ya Kamati kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022. NAIBU SPIKA: Ahsante sana. Tunaendelea, Katibu. NDG. MOSSY LUKUVI - KATIBU MEZANI: MASWALI NA MAJIBU NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, Maswali tutaanza na Ofisi ya Rais, TAMISEMI. Mheshimiwa Bryceson Magessa Tumaini Mbunge wa Busanda sasa aulize swali lake. Na. 243 Uhitaji wa Vituo vya Afya katika Jimbo la Busanda MHE. TUMAINI B. MAGESSA aliuliza:- Je, ni lini Serikali italipatia Jimbo la Busanda Vituo vya Afya hususan Tarafa ya Butundu na Tarafa ya Busanda? NAIBU SPIKA: Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, TAMISEMI Mheshimiwa Silinde, majibu. NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DAVID E. SILINDE) alijibu:- Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana. Kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Tumaini Bryceson Magessa, Mbunge wa Jimbo la Busanda, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Naibu Spika, Jimbo la Busanda katika Wilaya ya Geita lina Vituo vya Afya vitano ambapo vituo vya Afya vitatu vya Nyarugusu, Kashishi na Bukoli vipo katika Tarafa ya Busanda na Vituo vya Afya viwili vya Chikobe na Katoro vipo katika Tarafa ya Butundwe. 2 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) Mheshimiwa Naibu Spika, katika kuendelea kuboresha huduma za afya katika Wilaya ya Geita kuanzia mwaka wa fedha 2018/2019 hadi 2019/2020 Serikali imeipatia Halmashauri ya Wilaya ya Geita shilingi bilioni 2.8 kwa ajili ya ujenzi wa Hospitali ya Geita; shilingi bilioni 1.5 kwa ajili ya ujenzi wa Hospitali ya Katoro na shilingi milioni 400 kwa ajili ya ujenzi wa Kituo cha Afya Nyarugusu. Mheshimiwa Naibu Spika, katika mwaka wa fedha 2020/2021 Serikali imetenga shilingi milioni 500 kwa ajili ya ujenzi wa wodi tatu na shilingi milioni 500 kwa ajili ya ununuzi wa vifaa tiba katika Hospitali ya Wilaya ya Geita. Aidha, katika mwaka wa fedha 2021/2022, Serikali imetenga shilingi bilioni 1.9 kwa ajili ya kuendelea na ujenzi wa Hospitali ya Halmashauri ya Geita na Hospitali ya Katoro. Mheshimiwa Naibu Spika, katika mwaka wa fedha 2020/2021 Halmashauri ya Wilaya ya Geita imetengewa shilingi milioni 200 kwa ajili ya ukamilishaji wa maboma manne ya zahanati, yakiwemo maboma ya Zahanati za Lubanda na Bujura katika Jimbo la Busanda. Katika mwaka wa fedha 2021/2022 Halmashauri ya Wilaya ya Geita imetengewa fedha shilingi milioni 375 kwa ajili ya kuanza ujenzi wa Kituo cha Afya Isulwabutundwe na shilingi milioni 375 kwa ajili kuanza ujenzi wa Kituo cha Afya Butobela. Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali itaendelea kuimarisha miundombinu ya huduma za afya katika Jimbo la Busanda, ikiwemo kujenga zahanati, vituo vya afya na hospitali kwa kadri ya upatikanaji wa fedha. NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Bryceson Magessa, swali la nyongeza. MHE. TUMAINI B. MAGESSA: Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na majibu mazuri ya Serikali kutoka kwa Mheshimiwa Waziri, majibu haya yaliyotoka ni ya Wilaya ya Geita, nami maswali yangu yalikuwa yanaelekea Jimbo la Busanda. Kwa hiyo, nilipokee tu kwa sababu Jimbo la Busanda liko ndani ya Wilaya ya Geita, lakini mgawanyo wake inawezekana 3 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) Wilaya ya Geita usiwe ule ambao tunautarajia kuupata kule Busanda. Swali langu la kwanza la nyongeza: Je, Serikali ina mpango gani; kwa sababu sasa hivi kuna ramani mpya ya vituo vya afya na vituo vingi vinavyotajwa vina ramani ya zamani ikionekana wazi kwamba kuna upungufu mkubwa wa wodi za wanaume na wodi za wanawake: Je, Serikali ina mpango gani wa kufanya hivi vituo vya afya vijengwe kwa ramani hii mpya ya sasa? (Makofi) Swali la pili; pamoja na vituo vilivyotajwa, kuna upungufu mkubwa sana wa uimarishaji wa upatikanaji wa dawa kwenye vituo hivyo: Je, Serikali ina mpango gani kuhakikisha kwamba vituo hivi sasa vinaweza kuwahudumia wananchi na upatikanaji wa dawa ukawa kama uliokuwa unapatikana awali; kwa sababu, kwa miaka miwili sasa wananchi wana vituo vya afya lakini hawapati dawa kwa ajili ya kuwahudumia? (Makofi) NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, majibu. NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DAVID E. SILINDE): Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana. Swali la kwanza Mheshimiwa Mbunge alilokuwa anahitaji kufahamu ni juu ya ramani ambazo zimekuwa zikitolewa na Ofisi ya Rais, TAMISEMI kwenye ujenzi wa vituo vya afya kwamba, wakati mwingine haziendani na mahitaji. Mheshimiwa Naibu Spika, kitu kikubwa ambacho naweza nikamwambia Mheshimiwa Mbunge, zile ramani zilizoletwa katika maeneo husika ni minimum standards. Maboresho yanaweza yakafanyika kulingana na maeneo husikwa. Kwa hiyo, endapo kutakuwa na hitaji fulani, watu wa eneo husika wanaweza kufanya maboresho pamoja ikiwemo kuijulisha Ofisi ya Rais, TAMISEMI, nasi tutawapa ruhusa hiyo ili kuhakikisha hivyo vituo vinajengwa kulingana na mahitaji husika. (Makofi) 4 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) Mheshimiwa Naibu Spika, jambo la pili amezungumzia kwamba, tumekuwa na vituo lakini bado mahitaji ya dawa hayapatikani vya kutosha. Jambo hili nafikiri karibu Ofisi ya Rais, TAMISEMI kwa kushirikiana na Wizara ya Afya, Jinsia, Wazee na Watoto tumekuwa tukilijadili hili kila wakati na tumekuwa tukilitolea ufafanuzi. Kikubwa, wote tunafahamu kwamba, mahitaji kama bima za afya, fedha ambazo wananchi wanatoa pale pale, lakini kwa hivi karibuni Serikali imeongeza bajeti kubwa kwenye madawa na usimamizi wake mzuri. Kwa hiyo, tutaendelea kuongeza dawa katika vituo vyetu na tutaongeza vile vile usimamizi ili ziweze kuwafikia walengwa. Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana. (Makofi) NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Anne Kilango Malecela, swali la nyongeza. MHE. ANNE K. MALECELA: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru sana kupata nafasi hii. Kwa kuwa, Mkoa wa Kilimanjaro asilimia 40 ni Wilaya ya Same; na kwa kuwa Wilaya ya Same ina majimbo mawili; na Wilaya nzima ina Hospitali ya Wilaya moja: Je, Serikali haioni kwamba lile eneo ni kubwa sana, sasa upande wa Mashariki nao wapate japo Hospitali ya Wilaya moja? (Makofi) NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, majibu. NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DAVID E. SILINDE): Mheshimiwa Naibu Spika, sera yetu ya sasa ni kwamba kila Halmashauri ya Wilaya ipate hospitali yenye hadhi ya wilaya na ndio maana kwenye bajeti hata ya mwaka huu ambayo tumeipitisha mwaka 2021/2022 Serikali ya Awamu ya Sita imedhamiria kuhakikisha hata zile Halmashauri ambazo hazikuwa na hospitali za Halmashauri tutazijenga mwaka huu. Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, hili alilolileta hapa ni wazo kwamba angalau jimbo kwa imbo 5 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) liweze kupata lakini tutaendelea kuzingatia kuleta huduma bora za afya katika maeneo yote ikiwemo kujenga vituo vya afya na zahanati kuhakikisha huduma zinawafikia walengwa. Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, lengo la kwanza ni kuhakikisha kwamba tunamaliza kwanza Halmashauri zote halafu maombi mengine tutakuja kuyazingatia kulingana na mahitaji. Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. (Makofi) NAIBU SPIKA: Sawa. Tunaendelea na swali la Mheshimiwa Dkt. John Danielson Pallangyo, Mbunge wa Arumeru Mashariki. Na. 244 Serikali Kuunga Mkono Kushiriki katika Ujenzi wa Zahanati na Vituo vya Afya MHE. DKT. JOHN D. PALLANGYO aliuliza:- Je, ni lini Serikali itaunga mkono juhudi za wananchi katika ujenzi wa Zahanati na Vituo vya Afya Kata za Arumeru Mashariki. NAIBU SPIKA: Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, Mheshimiwa Silinde, majibu. NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DAVID E. SILINDE) alijibu:- Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana. Kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa John Danielson Pallangyo, Mbunge wa Arumeru Mashariki, kama ifuatavyo: - Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali imeendelea kuunga mkono jitihada za wananchi katika Halmashauri zote nchini kwa kutoa fedha kwa ajili ya ukamilishaji wa maboma ya 6 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) miundombinu ya afya kwa awamu kulingana na upatikanaji wa fedha. Katika mwaka wa fedha 2020/2021, Serikali imeipatia Halmashauri ya Wilaya ya Meru shilingi milioni 150 kwa ajili ya kukamilisha maboma ya Zahanati za Ngabobo, Shishtoni na Mikungani. Mheshimiwa Naibu Spika, aidha, katika mwaka wa fedha 2021/2022 Serikali imetenga shilingi milioni 150 kwa ajili ya kukamilisha maboma ya Zahanati za Ngejisosia, Imbaseni na Msitu wa Mbogo. Vilevile katika mwaka wa fedha 2021/2022 Halmashauri kupitia mapato yake ya ndani imetenga shilingi milioni 500 kwa ajili ya ujenzi wa Kituo cha Afya katika Kata ya Maroroni. Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali itaendelea kushirikiana na wananchi kuboresha miundombinu ya afya ikiwemo maboma ya zahanati na vituo vya afya
Details
-
File Typepdf
-
Upload Time-
-
Content LanguagesEnglish
-
Upload UserAnonymous/Not logged-in
-
File Pages384 Page
-
File Size-