Nakala Ya Mtandao (Online Document)

Nakala Ya Mtandao (Online Document)

Nakala ya Mtandao (Online Document) BUNGE LA TANZAIA ____________ MAJADILIANO YA BUNGE __________ MKUTANO WA KUMI NA TISA Kikao cha Tisa- Tarehe 26 Machi, 2015 (Kikao Kilianza Saa 3.00 Asubuhi) D U A Mwenyekiti (Mhe. Lediana M. Mng’ong’o) Alisoma Dua MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge, Mheshimiwa Waziri Mkuu hayupo, kwa hiyo na maswali kwa Waziri Mkuu hayatakuwepo leo. Katibu! MASWALI YA KAWAIDA Na. 94 Kusuasua kwa Ujenzi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma MHE. FELISTER A. BURA aliuliza:- Ujenzi wa Ofisi ya Mkuu ya Mkoa wa Dodoma umeendelea kusuasua kwa muda mrefu. Je, Serikali ina mpango gani wa haraka kukamilisha ujenzi wa jengo hili? NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (TAMISEMI) alijibu:- Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Felister Aloyce Bura, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Mwenyekiti, ujenzi wa Ofisi ya Mkoa wa Dodoma ulianza mwaka 2009/2010 na ulitarajiwa kukamilika mwaka 2012/2013. Makadirio ya gharama ya ujenzi yalikuwa ni shilingi bilioni 15.2, lakini kwa sasa gharama hizo zinafikia shilingi bilioni 16.9. Kati ya fedha hizo Serikali imeshatoa shilingi bilioni 10.5. Utekelezaji wa mradi huu unafanyika kwa awamu, ambapo awamu inayoendelea ni ya nne. Mheshimiwa Mwenyekiti, kazi zinazofanyika ni ujenzi wa msingi, ujenzi wa mihimili mikuu ya jengo na msingi wa ujenzi wa ukumbi. Aidha, kazi zinazotekelezwa katika awamu ya nne ni ujenzi wa kuta, uwekaji wa milango na madirisha na mwendelezo wa kazi za umeme katika hatua ya ufungaji wa nyaya. Kazi nyingine zitakuwa ni ufungaji wa mfumo wa habari na mawasiliano yaani ICT awamu ya pili, umaliziaji katika sakafu hadi ghorofa ya pili na kuta za jengo lote, kukamilisha ujenzi wa ukumbi na kazi za mwanzo za mandhali. Mheshimiwa Mwenyekiti, awamu hii ya nne ilianza kutekelezwa tarehe 25/6/2014 na imepangwa kukamilika ndani ya kipindi cha miezi saba. Katika bajeti ya mwaka 2014/2015 zimetengwa shilingi bilioni tatu tayari Serikali imekwishatoa shilingi 1,104,413,000. 1 Nakala ya Mtandao (Online Document) Mheshimiwa Mwenyekiti, sababu kubwa ya ujenzi huo kuchukua miaka mitano badala ya miaka mitatu ni ufinyu wa bajeti inayotolewa kwa ajili ya kazi hiyo na fedha kutopelekwa katika muda muafaka. Hata hivyo, utekelezaji wa mradi huu unatarajiwa kukamilika mwaka huu wa fedha 2014/2015. Aidha, Ofisi ya Waziri Mkuu - TAMISEMI imeiandikia Wizara ya Fedha barua yenye Kumb Na. AB.39/156/01/114 ya terehe 19 Februari, 2015, kuikumbusha Wizara ya Fedha kutoa fedha za miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa. MHE. FELISTER A. BURA: Mheshimiwa Mwenyekiti, unaposema kwamba Dodoma ni Makao Makuu ni pamoja na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, jengo hili liliwahi kutembelewa na Kamati ya TAMISEMI na wakaiomba Serikali kwamba jengo hili sasa litengewe fedha za kutosha na jengo liweze kukamilika. Pamoja na kwamba tangu jengo hili lianze kujengwa kuna majengo mengi ya Serikali yameshakamilika, lakini Ofisi ya Mkuu wa Mkoa mpaka leo jengo hili linasua sua. Serikali inasema kwamba mradi huu utakamilika mwaka 2014/2015, lakini katika mwaka huu wa fedha Serikali imepeleka shilingi milioni 400 tu. Siyo kweli kwamba jengo hili litakamilika katika mwaka huu. Naomba kujua ni lini sasa Serikali angalau ipeleke shilingi bilioni tatu kama zilivyoombwa na Mkoa na kama Kamati ya TAMISEMI ilivyoomba? Swali la pili, kwa kuwa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii imeonesha nia na ina uwezo wa kusaidiana na Serikali yetu kukamilisha baadhi ya majengo ambayo Serikali itakubali kudhamini. Kwa mfano, NSSF, National Housing, PSPF na Mifuko mingine wakidhaminiwa na Serikali wana uwezo wa kukamilisha majengo yaliyokwama kama la Ofisi ya Mkuu wa Mkoa. Je, Serikali iko tayari kuidhamini Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wakajengewa na Mashirika haya na Hifadhi ya Jamii? NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA(TAMISEMI): Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza kwa ajili ya records, sasa hivi hapa natoka kwenye hiyo Ofisi inayozungumzwa na nimemwita Katibu Tawala wa Mkoa tulikuwa wote pale, Ndugu Rehema Madenge pamoja na watu wote wanaohusika na jambo hili tunalozungumza hapa. Tumekuwa tunafanya hivyo, tumekaa Ofisini tumezungumza nao. Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka niweke record vizuri, shilingi milioni 400 ambazo tumezitamka leo asubuhi hii nimethibitishiwa kwamba shilingi milioni 700 zimeingia wiki hii, ndiyo maana nataka nisahihishe takwimu zile ambazo zimeorodheshwa pale Mheshimiwa Bura achukue na nimemtaja mtu, hapa nimekuwa concrete, maana nimemtaja Katibu Tawala wa Mkoa, anaweza aka-cross check naye. Kwa hiyo, hela zilizokwenda kule ni bilioni moja milioni mia moja na nne ndizo ambazo zimeshaingia na wanazo which means kazi zitaendelea pale, nilitaka kusema hivyo. Mheshimiwa Mwenyekiti, hela ambazo zilitakiwa ziwe zimekwenda kwa ajili ya kazi yote hii kama hela zote zingekwenda kama zinavyotakiwa, zilikuwa ni shilingi bilioni kumi na sita na point. So far tumepeleka shilingi bilioni 10.5 ndizo zimeshapelekwa pale na kwa sababu ya inflation rate na vitu vingine hapa na kwa sababu watataka kuweka parking area na vitu vingine, wanahitaji shilingi bilioni 18 ambazo zinatakiwa pale. Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, nataka nimwambie Mheshimiwa Bura kwamba, nathamini sana, Mbunge huyu amekuwa anasukuma hili jambo kwa nguvu, ni haki yake kwa kweli afanye hivyo na tunamshukuru kwamba anafanya hivyo. Hata hivyo, nataka nimwambie kwamba dhamira ya Serikali iko pale pale, ilikuwa shilingi bilioni tano ndizo zilikuwa zinapelekwa pale, sasa hivi tunapeleka shilingi bilioni tatu. Kwa maneno kwamba kama hela tulizopeleka hapa sasa hivi ni shilingi bilioni 1.104, maana yake tunategemea kwamba tupeleke tena shilingi bilioni mbili na point. Ndiyo maana tumesema kwamba tutazungumza na Hazina na wamo humu ndani wanatusikia tukisema jambo hili. 2 Nakala ya Mtandao (Online Document) Mheshimiwa Mwenyekiti, nyumba ile inayojengwa pale ni nyumba yenye heshima kubwa, kwa maana ya kwamba siyo tu Ofisi ya Mkuu wa Mkoa itakuwa kule, kama kuna Wizara ambayo itakuwa ina tatizo la ofisi wanaweza wakapata pale. Kwa hiyo, ile inaitwa Government House ndiyo jina lake hasa, ni nyumba ya Serikali iko pale. Kwa hiyo, Mheshimiwa Felister Bura anazungumza kitu cha msingi sana. Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa ameleta hii aspect hapa, kwamba labda tungetumia LAPF, NSSF, National Housing wakatusaidia. Ninyi wote mnajua jambo hili, anayetakiwa kusema naam mimi nipo tayari, kudhamini jambo hili ni Wizara ya Fedha, siyo LAPF aseme niko tayari, NSSf aseme niko tayari au NHC aseme niko tayari, wao Wizara ya Fedha ndiyo wako humu ndani, ili hela hizi kama hazitalipwa atakayekuwa held responsible atakuwa ni Serikali na Mifuko hii imekuwa na kelele mnaifahamu. Mheshimiwa Mwenyekiti, nakuhakikishia nachukua wazo hili analolisema hapa, wamefanya hivyo Hombolo kwenye Chuo cha Serikali za Mitaa, tumefanya hivyo kwenye jengo hili, tumefanya hivyo UDOM. Kwa hiyo, ni jambo ambalo linawezekana tunaweza tukasema. Sasa hili litategemeana na Wizara ya Fedha itakavyofanya, lakini nakubaliana na mawazo mazuri aliyotoa Mheshimiwa Mbunge na tutayafanyia kazi. Na 95 Mchango kwa Ajili ya Kuandikisha Mwanafunzi MHE. DKT. ANTONY G. MBASSA (K.n.y. MHE. JOSHUA S. NASSARI) aliuliza:- Wazazi wanatozwa fedha pindi wanapokwenda kuwaandikisha watoto shuleni kama wanavyofanya Shule ya Msingi Upendo iliyopo Nsengony Kata ya King‟ori. (a) Je, michango hiyo inayotozwa kwa wazazi ni halali? (b) Kama ni halali, je, ni kiasi gani cha fedha anachopaswa kulipa mzazi kwani kiwango kinatofautiana baina ya shule na shule? (c) Kama si halali, je, Serikali inachukua hatua gani za kisheria dhidi ya walimu wanaokwamisha watoto wasipate haki yao ya Kikatiba? NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (ELIMU) alijibu:- Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Joshua Samweli Nassari, Mbunge wa Arumeru Mashariki, lenye sehemu (a), (b) na (c) kwa pamoja kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali kupitia Waraka wa Elimu Namba Nane (8) wa mwaka 2011, imetoa maelekezo kuwa uandikishaji wa wanafunzi kujiunga na darasa la kwanza au kidato cha kwanza unapaswa kufanywa bila masharti yoyote. Hivyo, michango yote inayotozwa wakati wa mwanafunzi kujiandikisha kuanza shule ni kinyume na taratibu na imepigwa marufuku. Hivyo, kimsingi hakuna kiasi chochote cha fedha ambacho mzazi au mlezi anapaswa kulipa anapompeleka mwanafunzi shuleni kama gharama ya kujiandikisha au gharama ya usajili. 3 Nakala ya Mtandao (Online Document) Mheshimiwa Mwenyekiti, Wizara imeziagiza Halmashauri zote nchini kuendelea na kuchukua hatua kwa Walimu Wakuu na Wakuu wa Shule wanaobainika kukiuka maelekezo haya na utaratibu wa uandikishaji. Kupitia Bunge lako natoa wito kwa wadau mbalimbali, wananchi na Waheshimiwa Wabunge kutoa taarifa inapotokea mwanafunzi au wanafunzi wanapoandikishwa kwa masharti ya kulipa fedha. Mheshimiwa Mwenyekiti, aidha, nitashirikiana na Mheshimiwa Mbunge kupata taarifa kamili za uwepo wa vitendo vya uandikishwaji wa darasa la kwanza wa wanafunzi katika Shule ya Msingi Upendo kwa masharti ya kulipa fedha ili hatua stahiki ziweze kuchukuliwa. MHE. DKT. ANTONY G. MBASSA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Kwa kuwa katika majibu ya msingi Mheshimiwa Naibu Waziri amesema kwamba wadau, wazazi na Wabunge wasaidie kutoa taarifa na hatua zichukuliwe. Hapa Mheshimiwa Mbunge ameshatoa taarifa kwa sababu ametaja shule husika na eneo husika, sasa sijui Mheshimiwa Waziri anahitaji tena taarifa zipi? Kinachohitajika hapa

View Full Text

Details

  • File Type
    pdf
  • Upload Time
    -
  • Content Languages
    English
  • Upload User
    Anonymous/Not logged-in
  • File Pages
    83 Page
  • File Size
    -

Download

Channel Download Status
Express Download Enable

Copyright

We respect the copyrights and intellectual property rights of all users. All uploaded documents are either original works of the uploader or authorized works of the rightful owners.

  • Not to be reproduced or distributed without explicit permission.
  • Not used for commercial purposes outside of approved use cases.
  • Not used to infringe on the rights of the original creators.
  • If you believe any content infringes your copyright, please contact us immediately.

Support

For help with questions, suggestions, or problems, please contact us