Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) BUNGE LA TANZANIA ___________ MAJADILIANO YA BUNGE ___________ MKUTANO WA KUMI NA NNE Kikao cha Kumi na Moja – Tarehe 17 Desemba, 2013 (Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Mwenyekiti (Mhe. Mussa Z. Azzan) Alisoma Dua HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na:- MHE. JOSEPHINE J. NGENZABUKE (K.n.y. MWENYEKITI WA KAMATI YA BUNGE YA UCHUMI, VIWANDA NA BIASHARA): Taarifa ya Kamati ya Bunge ya Uchumi, Viwanda na Biashara Kuhusu Utekelezaji wa Shughuli zake kwa Mwaka 2013. MHE. LUCKSON N. MWANJALE (K.n.y. MWENYEKITI WA KAMATI YA BUNGE YA MASUALA YA UKIMWI): Taarifa ya Kamati ya Bunge ya Masuala ya Ukimwi Kuhusu Utekelezaji wa Shughuli zake kwa Mwaka 2013. 1 Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) MASWALI NA MAJIBU Na. 120 Kuleta Walimu na Kujenga Nyumba Zao MHE. MWIGULU L. N. MADELU (K.n.y. MHE. DKT. HAMISI A. KIGWANGALLA) aliuliza:- Kwa kutumia jitihada binafsi na Mfuko wa Jimbo, Mbunge wa Jimbo la Nzega ameanzisha ujenzi wa shule tatu za Kidato cha Tano na Sita:- (a) Je, ni lini Serikali itaunga mkono jitihada hizi kwa kujenga nyumba za Walimu kwenye shule hizo? (b) Je, Serikali itakuwa tayari kuleta Walimu na kusajili shule hizo? NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (TAMISEMI) alijibu:- Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Dkt. Hamisi Andrea Kigwangalla, Mbunge wa Nzega, lenye sehemu (a) na (b), kama ifuatavyo:- (a) Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza kabisa, naomba nimpongeze sana Mheshimiwa Dkt. Hamisi Andrea Kigwangalla, kwa jitihada anazozifanya kuboresha utoaji wa elimu nchini. Serikali itaendelea kuunga mkono jitihada hizi kupitia Mipango ya Maendeleo ya Elimu ya Msingi na Sekondari na kutenga fedha kila mwaka kupitia Mpango wa Bajeti za Halmashauri. Mheshimiwa Mwenyekiti, kati ya mwaka 2010 na 2013, kupitia Awamu ya Pili ya Mpango wa Maendeleo wa Elimu ya Sekondari (MMES II), Serikali imetoa jumla ya shilingi bilioni 11.9 katika Mamlaka za Serikali za Mitaa kwa ajili ya ujezi wa nyumba za walimu na Halmashauri ya Wilaya ya 2 Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) [NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, (TAMISEMI)] Nzega ilipatiwa shilingi milioni 72 zilizonufaisha Shule za Sekondari za Budushi, Undomo, Shigamba na Milambo Itobo. Kupitia Mfumo wa kugawa ruzuku ya maendeleo katika Mamlaka za Serikali za Mitaa (LGCDG), mwaka 2013/ 2014 Halmashauri ya Wilaya ya Nzega imepokea shilingi milioni 420 na kati ya hizo shilingi milioni 105 zimepangwa kupelekwa katika ujenzi wa nyumba za walimu. (b) Mheshimiwa Mwenyekiti, Shule za Sekondari Puge na Chifu Ngelengi zinazotarajiwa kuwa za Kidato cha Tano hazijakamilisha vigezo vya kuweza kusajiliwa na kupokea wanafunzi wa Kidato cha Tano kwa kukosa madarasa ya kutosha, vyoo, mabweni, maabara na samani. Halmashauri ya Wilaya ya Nzega imeshauriwa kutumia vyanzo vya mapato vya ndani na kuweka kipaumbele kupitia bajeti za Halmashauri ili kukamilisha mahitaji muhimu katika shule hizi. Aidha, napenda niwahakikishie Wananchi wa Nzega kuwa, mara vigezo vyote vitakapokamilika ikiwemo kuwa na miundombinu muhimu, Serikali itakuwa tayari kushirikiana na Mheshimiwa Mbunge katika kuharakisha usajili wa shule hizo na kuzipatia walimu wa kutosha. MWENYEKITI: Mheshimiwa Mwigulu Nchemba! MHE. MWIGULU L. N. MADELU: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza, nashukuru kwa majibu ya Mheshimiwa Naibu Waziri, lakini niseme kwamba, kuna maeneo mengi sana ambayo jitihada za Wananchi zimefikia kiwango ambacho zikiungwa mkono shule zile zingesajiliwa na zingeanza kutumika mapema zaidi. Yapo maeneo mengi ambako Wananchi wamejitahidi na wameshajenga kwa kiwango hicho, lakini kutokana na ukomo wa bajeti wa Halmashauri, shule hizo zinachukua muda kukamilika kwa sababu Wananchi walewale wanatakiwa washughulike kwenye sekta zingine pia. Je, ni kwa nini basi Serikali isitoe kipaumbele kwa maeneo ambayo Wananchi wameshaonesha njia kwa kiwango hicho kwa kutenga bajeti maalum ya kuunga 3 Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) [MHE. MWIGULU L. N. MADELU] mkono maeneo ambayo yameshaonesha jitihada badala ya kuziachia tu Halmashauri na kusababisha majengo ambayo Wananchi wametumia jitihada kubwa kuyajenga yabaki bila kutumika kwa kipindi kirefu kwa sababu wanasubiri kujikusanya upya na kutengeneza maeneo hayo kama ilivyo eneo la Kichangani pale Misigiri? MWENYEKITI: Mheshimiwa Naibu Waziri! NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (TAMISEMI): Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Mwigulu Nchemba, ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi na Mbunge wa Iramba, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Mwenyekiti, nakubaliana na Mheshimiwa Mwingulu Nchemba, anachosema ni kweli kama kuna mahali na ndivyo ilivyo katika nchi yetu kwamba Wananchi wamejitoa, wametoa nguvu zao, wamefanya kazi, unachotegemea Halmashauri hizi zitaungwa mkono na Serikali na ndivyo vitu ambavyo nimekuwa navieleza hapa. Hili eneo analolisema sijalipata vizuri kwamba liko Iramba au kule Nzega, lakini haitaondoa maudhui ya jibu. Mheshimiwa Mwenyekiti, hii Halmashauri ya Nzega tunayoizungumza ukiangalia katika mapato yake, fedha zimekwenda kule na nimesema katika MMES II shilingi milioni 105 zimeelekezwa katika eneo hilo na katika Local Government Capital Development Grant wamepelekewa fedha pia shilingi milioni 72, lakini hazikuenda sasa katika shule hizi ambazo Dkt. Hamisi Kigwangalla anazizungumzia. Pia nataka nitoe taarifa hapa kwamba, kupitia mrabaha ambao umetokana na machimbo, Halmashauri hii imepata shilingi bilioni 2.3, sikumbuki vizuri ile figure lakini at least najua kuna fedha zimepatikana pale na hizi ni own source ambazo kama tunazungumza habari ya elimu, duniani kote sasa hivi investment kubwa ya Mataifa makubwa yote inapelekwa katika kitu kinachoitwa elimu. 4 Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) [NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, (TAMISEMI)] Maoni yangu na ya Ofisi ya Waziri Mkuu ni kwamba, hawa wakae wafikirie jinsi ambavyo wanaweza wakatumia sehemu fulani ya mrabaha ule ikasaidia katika jambo lile wakati Serikali tukiendelea na jitihada hizi za kusaidia kama anavyoshauri Mheshimiwa Nchemba. MWENYEKITI: Tunaendelea na swali lingine, Mheshimiwa Felix Mkosamali! Na. 121 Wabunge Kualikwa Kwenye Vikao vya Halmashauri MHE. MOSES J. MACHALI (K.n.y. MHE. FELIX F. MKOSAMALI) aliuliza:- Baadhi ya Wabunge wamekuwa hawapati taarifa za kila siku za Halmashauri ikiwa ni pamoja na kutoalikwa kwenye baadhi ya vikao hata wakiwa Majimboni:- (a) Je, kwa nini Makatibu wa Wabunge wasiwe wanaalikwa katika vikao ikiwa Wabunge hawapo Majimboni na walipwe posho? (b) Je, kwa nini Serikali isiagize Halmashauri zote nchini kufanya hivyo ili Wabunge wapate taarifa za Halmashauri zao? NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (TAMISEMI) alijibu:- Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Felix Francis Mkosamali, Mbunge wa Muhambwe, lenye sehemu (a) na (b), kama ifuatavyo:- (a) Mheshimiwa Mwenyekiti, Halmashauri zote nchini huendesha vikao vyake kwa kuzingatia Kanuni za Kudumu zilizotungwa chini ya Kifungu cha 70 cha Sheria ya 5 Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) [NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, (TAMISEMI)] Serikali za Mitaa (Mamlaka za Wilaya) Sura ya 287 na Kifungu cha 42 (1) cha Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka za Miji) Sura ya 288. Mheshimiwa Mwenyekiti, Halmashauri zote huandaa ratiba ya vikao vya Mabaraza kwa mwaka mzima na ratiba hiyo hukabidhiwa Wajumbe wote. Aidha, Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI) imefanya mapitio upya ya Kanuni za Kudumu za Halmashauri ambapo imeongeza Kifungu cha 6 (ii) na 7 (ii) ambacho kinatamka kuwa, Mikutano yote ya Baraza la Madiwani itapangwa na Baraza la Madiwani kwa kuzingatia Vikao vya Bunge ili kuwawezesha Waheshimiwa Wabunge kuhudhuria Mikutano ya Baraza la Madiwani. Endapo italazimika kuitishwa kwa Mikutano hiyo ya Baraza wakati Vikao vya Bunge vinaendelea, Mkurugenzi Mtendaji atamjulisha au atawajulisha Wabunge husika kuhusu kikao hicho ili waweze kuhudhuria. (b) Mheshimiwa Mwenyekiti, Kanuni zinaelekeza kwamba, Wajumbe wa Vikao vya Halmashauri ni Waheshimiwa Wabunge pamoja na Waheshimiwa Madiwani katika maeneo yao. Hata hivyo, Makatibu wa Wabunge hawazuiliwi kuhudhuria Vikao vya Mabaraza ya Madiwani, ambavyo vinaruhusu Wananchi wote kuhudhuria ingawa hawatapewa fursa ya kuhoji jambo lolote wala kulipwa posho kwa kuwa wao siyo Wajumbe. Kwa hiyo, itakuwa ni vigumu kuziagiza Halmashauri kuwaalika Makatibu wa Wabunge kwani kufanya hivyo itakuwa inaenda kinyume na taratibu zilizoelezwa katika jibu (a). (Makofi) MWENYEKITI: Mheshimiwa Machali! MHE. MOSES J. MACHALI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa kunipa fursa niulize maswali mawili madogo ya nyongeza. (i) Kwa kuwa baadhi ya Halmashauri zimekuwa zinaandaa vikao makusudi kabisa na pengine Wabunge hatupati taarifa; kwa mfano, katika Halmashauri yangu na 6 Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) [MHE. MOSES J. MACHALI] hata katika Halmashauri ya Wilaya ya Wilaya ya Kibondo ambako Mheshimiwa Felix Mkosamali anatokea na ndiyo maana ameuliza swali hili. Serikali inatoa kauli gani kuhusiana na Halmashauri hizi kuzingatia ratiba za Wabunge? (Makofi) (ii) Ameeleza kwamba Makatibu wa Waheshimiwa Wabunge ni ruhusa kuhudhuria kwenye vikao hivi, lakini hawatalipwa posho kama Wananchi wengine wa kawaida; lakini Watendaji mbalimbali kwa mfano Watendaji wa Kata na Maafisa Tarafa katika Halmashauri yangu huwa wanaalikwa na kuhudhuria
Details
-
File Typepdf
-
Upload Time-
-
Content LanguagesEnglish
-
Upload UserAnonymous/Not logged-in
-
File Pages222 Page
-
File Size-