NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA __________ MAJADILIANO YA BUNGE ___________ MKUTANO WA TATU Kikao cha Ishirini na Mbili – Tarehe 18 Mei, 2016 (Bunge Lilianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Naibu Spika (Mhe.Dkt. Tulia Ackson) Alisoma Dua NAIBU SPIKA: Katibu! NDG. NEEMA MSANGI - KATIBU MEZANI: HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa mezani na:- NAIBU WAZIRI WA NISHATI NA MADINI: Randama ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Nishati na Madini kwa mwaka wa Fedha 2016/2017. NAIBU SPIKA: Katibu! NDG. NEEMA MSANGI - KATIBU MEZANI: Maswali! MASWALI NA MAJIBU NAIBU SPIKA: Tutaanza na Ofisi ya Waziri Mkuu, Mheshimiwa Amina Nassoro Makilagi, Mbunge wa Viti Maalum, sasa aulize swali lake. Kwa niaba yake, Mheshimiwa Bura. Na. 184 Umuhimu wa Rasilimali Watu Katika Kukuza Uchumi wa Taifa MHE. FELISTER A. BURA (K.n.y. AMINA N. MAKILAGI) aliuliza:- 1 NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT) Je, Serikali ina mkakati gani wa kutumia rasilimali watu katika kukuza uchumi wa Taifa, hasa ikizingatiwa kuwa rasilimali hiyo ni muhimu sana katika kukuza uchumi wa Taifa? NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU (KAZI, VIJANA NA AJIRA) alijibu:- Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Amina Nassoro Makilagi kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali inatambua kuwa ili kukuza uchumi na kupunguza umaskini, matumizi ya rasilimali watu ni muhimu sana. Ili kuhakikisha kuwa rasilimali watu inawezeshwa na kutumika kukuza uchumi wa Taifa, Serikali imeweka mikakati ifuatayo:- (i) Serikali imeandaa mkakati wa Kitaifa wa kukuza ujuzi nchini ambao umelenga kutoa mafunzo ya vitendo yatakayofanyika maeneo ya kazi (apprenticeship and internship programs). Aidha, ili kuwapa vijana wengi fursa za mafunzo, Serikali imeanzisha program maaalum ya kutambua ujuzi uliopatikana kupitia mfumo usio rasmi na kuurasimisha kwa kutoa mafunzo ya muda mfupi kwa wale watakaobainika kuhitaji na kuwapa vyeti. Utaratibu huu unawapa fursa vijana wetu na kuendelea na mfumo rasmi wa mafunzo na pia kutambulika na waajiri au watoa kazi na hivyo kupata nafasi kuchangia katika kujenga uchumi wa Taifa. (ii) Kuhamasisha vijana wenye utaalam mbalimbali kushiriki katika shughuli za kiuchumi kwa kuweka mazingira bora ya uwekezaji katika sekta zenye uwezo mkubwa wa kuzalisha ajira hususan kilimo na biashara. Aidha, Serikali itajikita zaidi kuhamasisha na kuwezesha uwekezaji kwenye viwanda vidogo, vya kati na vikubwa ili kufikia lengo la asilimia 40 ya nguvu kazi nchini kuwa katika Sekta ya Viwanda ifikapo mwaka 2020, kupitia Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Miaka Mitano. Mheshimiwa Naibu Spika, hata hivyo, Serikali kupitia sekta na taasisi zake mbalimbali inaendelea kuhakikisha rasilimali watu iliyopo nchini inatumika sawasawa ili iweze kuchangia uchumi wa nchi. NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Bura, swali la nyongeza. MHE. FELISTER A. BURA: Mheshimiwa Naibu Spika, namshukuru sana Mheshimiwa Naibu Waziri kwa majibu yake mazuri, lakini pamoja na majibu hayo, nina maswali mawili madogo ya nyongeza. 2 NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT) Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kuwa vijana ndio nguvu kazi ya Taifa hili na kwa kuwa vyuo vikuu vinazalisha vijana asubuhi na jioni wenye elimu nzuri ya kufanya ujasiriamali, lakini tatizo ni wapi watapata mikopo kwa njia rahisi zaidi na kwa riba nafuu zaidi? Je, Serikali ina mpango gani wa kuwasaidia hawa vijana kupata mikopo kwa urahisi na kwa riba nafuu zaidi? Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili, kwa kuwa ajira ambayo ni rahisi kwa vijana na hasa kwa wanawake pia ni kilimo; lakini kilimo kinacholimwa kwa sasa hakina tija; kwanza, masoko hayapo kwa urahisi, mazao mengine yanaoza mashambani; lakini la pili, maeneo ya kulima. Vijiji vingi havijatenga maeneo kwa ajili ya kilimo kwa vijana na hata kwa wanawake ambao wameshajiunga kwenye vikundi mbalimbali. Je, Serikali iko tayari kutenga maeneo na kuzihimiza Halmashauri zetu kutenga maeneo kwa ajili ya vijana na hata kwa wanawake ambao wako tayari kuwa wajasiriamali kupitia kilimo? (Makofi) NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU (KAZI, VIJANA NA AJIRA) Mheshimiwa Naibu Spika, nikianza na la kwanza la mikopo na mitaji kwa wahitimu wa elimu ya vyuo vikuu na elimu ya juu, ni kweli natambua kwamba vijana wengi sasa hivi wanapenda kujishughulisha na shughuli za uzalishaji mali hasa kilimo, lakini changamoto kubwa wanayokutana nayo ni ukosefu wa mitaji na mikopo. Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali imeliangalia hili kwa macho mawili na katika mtazamo wa mbali kuhakikisha kwamba vijana hawa wanapata fursa ya mikopo na mitaji kwanza kabisa kupitia Mfuko wetu wa Maendeleo ya Vijana ambao umekuwa ukikopesha makundi mengi ya vijana kupitia SACCOS ambazo ziko katika Halmashauri zetu. Vilevile tumeendelea kuwa na msisitizo kwa kuwataka vijana hawa wajiunge katika makampuni na vikundi mbalimbali ili waweze kupata fursa ambazo zinatokana na mikopo na mitaji. Mheshimiwa Naibu Spika, pia tunayo program maalum sasa hivi kupitia Mfuko wa Uwezeshaji wa Wananchi Kiuchumi, ambapo tuna program ya Kijana Jiajiri inahusisha young graduates, wanaandika proposals zao wanazi-submit katika baraza na baadaye wanapatiwa mikopo na mitaji. Pia Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi imezungumza kuhusu kuwawezesha vijana wakae katika vikundi na makampuni kutumia fani zao na taaluma zao mbalimbali ili waweze kukopesheka. Mheshimiwa Naibu Spika, nitoe tu rai kwa vijana wote wale wa vyuo vikuu na wahitimu wa elimu ya juu kutumia fursa hii ya Mfuko wa Maendeleo ya Vijana na mikopo inayopita katika Halmashauri zetu kwa kukaa katika vikundi na makampuni. 3 NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT) Mheshimiwa Naibu Spika, pili, limeulizwa swali kwamba Serikali ina nia gani ya kutenga maeneo maalum kwa ajili ya shughuli za kilimo? Mwaka 2014, Wizara yetu ilikutana na Wakuu wa Mikoa wote nchi nzima hapa Dodoma na likatengenezwa azimio, ambapo moja kati ya kilichoamuliwa ni kutengeneza kitu kinaitwa Youth Special Economic Zone, ni ukanda maalum ambao utakuwa unasaidia utengaji wa maeneo kwa ajili ya shughuli za vijana. Mpaka sasa tayari ekari 8000 zimeshatengwa nchi nzima kwa ajili ya maeneo haya ili vijana waweze kufanya shughuli za kilimo na biashara. Mheshimiwa Naibu Spika, pia tumezungumza na Waziri wa Kilimo, yako mashamba makubwa ya Serikali ambayo wanayafanyia utaratibu sasa hivi nayo tuweze kuyatenga kwa ajili ya kuwagawia vijana waweze kufanya shughuli za uzalishaji mali. (Makofi) NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Bilago! MHE. KASUKU S. BILAGO: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kwa kunipa nafasi hii adimu. Pamoja na majibu yaliyotolewa na Naibu Waziri, ipo nguvu kazi nzuri sana katika nchi hii iliyotafuta ajira binafsi; vijana wa bodaboda. Hawa vijana wa bodaboda tunawatumia vizuri wakati wa uchaguzi, baada ya uchaguzi, wanapata misukosuko ya kufa mtu. Wanasumbuliwa na Polisi. Bodaboda wangu waliopo Kakonko na nchi nzima, hawa bodaboda tunawalindaje katika ajira zao hizi? Ahsante. (Makofi) NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU (KAZI, VIJANA NA AJIRA): Mheshimiwa Naibu Spika, hata mimi nataka nikiri kwamba kundi hili ni kundi ambalo kwa kiwango kikubwa sana, asilimia kubwa tuliopo hapa tuliwatumia katika kampeni zetu na ndio wametufanya tumefika katika jengo hili. Vile vile nataka nikiri tu kwamba, bodaboda ni biashara ambayo sisi tunaamini kwa kiwango kikubwa sana kwamba inasaidia katika kutatua changamoto za ukosefu wa ajira kwa vijana wetu. (Makofi) Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali katika eneo hili imefanyaje? Kwanza kabisa, Serikali kwa kushirikiana na mamlaka zile husika hasa mamlaka za Halmashauri ya Manispaa na Majiji, kwanza kabisa kutenga maeneo maalum na kuwatambua na kazi yao iheshimiwe. Pili, tuna program maalum kupitia Mfuko wa Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi pamoja na Mifuko ya Hifadhi ya Jamii ya ukopeshaji wa pikipiki, hizi bodaboda ili vijana wetu hawa ambao asilimia kubwa sana wanafanya kazi kwa watu wapate fursa ya kukopa wenyewe moja kwa moja na pikipiki zile ziwe mali zao na ziwasaidie katika kuinua uchumi wao. (Makofi) NAIBU SPIKA: Ofisi ya Rais, TAMISEMI. Mheshimiwa Boniventura Destery Kiswaga, Mbunge wa Magu, sasa aulize swali lake. 4 NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT) Na. 185 Kituo cha Afya Kisesa Kufanywa Hospitali MHE. BONIVENTURA D. KISWAGA aliuliza:- Kituo cha afya Kisesa kiliombewa kibali ili kipandishwe hadhi kuwa Hospitali kamili:- Je, ni lini Serikali itatoa kibali? NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (TAMISEMI) alijibu:- Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Boniventura Destery Kiswaga, Mbunge wa Magu, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Naibu Spika, kwa mujibu wa Sera ya Afya ya mwaka 2007, kila Wilaya inatakiwa kuwa na hospitali moja ya Wilaya na tayari hospitali hiyo ipo katika Wilaya ya Magu. Kituo cha Afya cha Kisesa kiliombewa kuboreshwa ili kiweze kutoa huduma za upasuaji mdogo kukidhi mahitaji hayo kwa wagonjwa badala ya kutegemea hospitali ya Wilaya pekee. Mheshimiwa Naibu Spika, ili kituo hicho kianze kutoa huduma za upasuaji, Serikali iko katika hatua za mwisho za umaliziaji wa ujenzi wa jengo la upasuaji, jengo la kuhifadhia maiti pamoja na chumba cha X-ray. Aidha, tayari X-ray machine imeshapatikana, inasubiri tu kufungwa baada ya kukamilika kwa ujenzi wa chumba cha X-ray. NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Kiswaga swali la nyongeza. MHE. BONIVENTURA D. KISWAGA: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru kwa majibu mazuri ya Serikali. Kwa kuwa Kituo hiki cha Afya kinahudumia maeneo makubwa katika eneo la Ilemela, Usagara Wilaya ya Misungwi, pamoja na Jimbo la Sumve
Details
-
File Typepdf
-
Upload Time-
-
Content LanguagesEnglish
-
Upload UserAnonymous/Not logged-in
-
File Pages187 Page
-
File Size-