Nakala Ya Mtandao (Online Document)

Nakala Ya Mtandao (Online Document)

NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ________ MAJADILIANO YA BUNGE _________ MKUTANO WA KUMI NA NANE Kikao cha Tisa – Tarehe 7 Februari, 2020 (Bunge Lilianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Naibu Spika (Mhe. Dkt. Tulia Ackson) Alisoma Dua NAIBU SIKA: Waheshimiwa tukae. Katibu. NDG. JOSHUA CHAMWELA - KATIBU MEZANI: HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na:- NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Maelezo ya Waziri wa Fedha na Mipango kuhusu Azimio la Kufuta Hasara itokanayo na Maduhuli ya Madeni ya Nyuma ya Ada na Leseni za Magari, Riba na Adhabu kwa Kipindi kinachoishia tarehe 30 Juni, 2019. Muhtasari wa Tamko la Sera ya Fedha (Mapitio ya Nusu Mwaka 2019/2020) [Monetary Policy Statement (The Mid-Year Review 2019/2020)]. MHE. STANSLAUS S. MABULA - K.n.y. MWENYEKITI WA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA HESABU ZA SERIKALI: Maoni ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali kuhusu Azimio la Kufuta Hasara itokanayo na maduhuli ya madeni ya nyuma ya ada na leseni za magari, riba na adhabu kwa kipindi kinachoishia tarehe 30 Juni, 2019. MHE. IMMACULATE S. SEMESI - K.n.y. MSEMAJI MKUU WA KAMBI RASMI YA UPINZANI KWA WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO: Maoni ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni kuhusu Azimio la Kufuta Hasara itokanayo na maduhuli ya madeni ya nyuma ya ada na leseni za magari, riba na adhabu kwa kipindi kinachoishia tarehe 30 Juni, 2019. WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA: Maelezo ya Waziri wa Katiba na Sheria kuhusu Muswada wa Sheria ya Usuluhishi wa Mwaka 2020 (The Arbitration Bill, 2020). 1 NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT) MHE. ZAINAB A. KATIMBA - K.n.y. MWENYEKITI WA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA SHERIA NDOGO: Maoni ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria Ndogo kuhusu Muswada wa Sheria ya Usuluhishi wa Mwaka 2020 (The Arbitration Bill, 2020). MHE. SALOME W. MAKAMBA - MSEMAJI MKUU WA KAMBI RASMI YA UPINZANI JUU YA WIZARA YA KATIBA NA SHERIA: Maoni ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni kuhusu Muswada wa Sheria ya Usuluhishi wa Mwaka 2020 (The Arbitration Bill, 2020). NAIBU SPIKA: Ahsante, Katibu. NDG. JOSHUA CHAMWELA - KATIBU MEZANI: MASWALI NA MAJIBU NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, tutaanza na Ofisi ya Waziri Mkuu, Mheshimiwa Grace Victor Tendega, Mbunge wa Viti Maalum sasa aulize swali lake. Na. 105 Agizo La Kukamatwa Vijana Wanaocheza “Pool Table” MHE. GRACE V. TENDEGA aliuliza:- Wakati akiwaapisha Wakuu wa Mikoa tarehe 15/03/2016 Mhe. Rais alitoa agizo la kuwakamata vijana wote watakaokutwa wakicheza mchezo wa “pool table” na kuwapeleka kambini wakalime:- (a) Je, Serikali imeandaa kambi ngapi na kujua huduma za kujikimu kwa vijana hao wakati watakapokuwa wakiendelea na shughuli za kilimo na kipindi cha kusubiri mavuno yao? (b) Je, Serikali ina mpango mkakati gani wa kupunguza tatizo la ajira kwa vijana ili kuondokana na wimbi la vijana kuzurura na kushinda bila kufanya kazi? (c) Je, Serikali imefanya sensa na kujua ni vijana wangapi wanaofanya kazi usiku na kupumzika mchana au mchana na kupumzika usiku ili kubaini wazururaji wa mchana na wanaocheza “pool table” mchana kwa sababu ya kukosa ajira? NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, majibu. NAIBU WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, VIJANA NA AJIRA alijibu:- Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Grace Victor Tendega, Mbunge wa Viti Maalum, lenye sehemu (a), (b) na (c) kama ifuatavyo:- (a) Mheshimiwa Naibu Spika, msingi wa agizo la Mheshimiwa Rais wa Awamu ya Tano Dkt. John Pombe Magufuli kuzuia vijana kucheza “pool table” wakati wa kazi umelenga kusisitiza na kuimarisha dhana na tabia ya kila mwenye uwezo wa kufanya kazi anafanya kazi 2 NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT) katika sekta mbalimbali za kiuchumi ili kuchangia kukuza pato la Taifa na kupunguza umaskini. Katika kuhakikisha kwamba vijana wanashiriki kwenye shughuli za kiuchumi, Serikali kupitia Tawala za Mikoa na Wilaya imetenga maeneo maalum ya uzalishaji mali kwa vijana ambapo jumla ya ekari 217,882 zimeelekezwa katika kukidhi mahitaji ya shughuli za kilimo, ufugaji, viwanda na biashara ndogo. Mheshimiwa Naibu Spika, uwepo wa Vituo vya Maendeleo ya Vijana na Majengo ya Viwanda “Industrial Sheds” umesaidia kuwapa mafunzo vijana na kuwajengea uwezo wa kuongeza thamani katika mazao ya kilimo. (b) Mheshimiwa Naibu Spika, katika kukabiliana na tatizo la ukosefu wa ajira kuwa vijana, Serikali imeendelea kutekeleza mikakati ifuatayo:- (i) Kuwajengea vijana ujuzi kupitia Programu ya Kukuza Ujuzi Nchini ili vijana kutumia ujuzi wa mafunzo mbalimbali kujiajiri na kuajiri vijana wengine. Kwa mwaka huu wa fedha, Serikali inatekeleza mafunzo ya stadi mbalimbali za kazi ambapo jumla ya vijana 49,265 watanufaika. (ii) Kuweka mazingira bora ya uwekezaji nchini ili kuvutia uwekezaji mkubwa kwenye sekta zenye uwezo mkubwa wa kuzalisha ajira hususani kilimo, ufugaji, madini na viwanda. (iii) Utekelezaji wa dhana ya local content katika miradi mikubwa ya kimkakati ya Serikali katika maeneo ya uchukuzi, nishati na miundombinu ya barabara na reli. (iv) Kuwezesha vikundi vya vijana kupitia zabuni za manunuzi ya ndani kwenye kila Halmashauri za Manispaa na Wilaya nchini Tanzania kupitia Akaunti Maalum kama mabadiliko ya mwaka 2016 ya Sheria ya PPRA yanavyoelekeza. (v) Uwezeshwaji kiuchumi kwa vijana kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Vijana na mikopo ya asilimia 10 za mapato ya ndani ya Halmashauri. (c) Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali imelipokea wazo la kujua vijana wanaofanya kazi usiku na wanaofanya kazi mchana. Hivyo suala hili litawasilishwa katika Mamlaka ya Takwimu ili lizingatiwe katika sensa ya watu na makazi itakayofanyika mwaka 2022. NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Grace Tendega, swali la nyongeza. MHE. GRACE V. TENDEGA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kwa kunipa nafasi niulize maswali mawili ya nyongeza. Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza, nasikitika sana swali langu halijajibiwa kama nilivyokuwa nimeuliza. Katika majibu ya Naibu Waziri anasema kwamba wao wametenga zaidi ya ekari 217 ambazo ziko katika mikoa mbalimbali lakini hajaainisha ni mikoa ipi na wilaya zipi makambi hayo yapo ili tuweze kujua kwa sababu sisi ndiyo wawakilishi wa hao vijana na tunawaona jinsi ambavyo wanapata adha huko tuliko. (Makofi) Mheshimiwa Naibu Spika, wamesema kwamba kuna programu mbalimbali na mazingira ambayo wamewawezesha, ni program zipi na mazingira yepi ambayo wameyaweka ili hawa vijana tukawaona wanafanya kazi. Amekiri kabisa hakuna hata sensa waliokwisha kuifanya ya kufahamu ni vijana wangapi ambao wanafanya kazi hizo mchana na usiku kwa maana ya kwamba hakuna wanachokijua kuhusu vijana wetu na tunawaona wakiwa wako na hali ngumu na hawana ajira na ajira hazijapatikana. Ahsante. (Makofi) 3 NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT) NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, majibu. NAIBU WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, VIJANA NA AJIRA: Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Grace Victor Tendega (Viti Maalum), kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Naibu Spika, katika eneo lake la kwanza amehoji kwa nini hatujaainisha maeneo yote ya ekari 217,882 ambayo yametengwa. Katika utaratibu wa uwasilishaji wa majibu nimetoa majibu ya jumla kuonyesha ekeri zilizotengwa lakini bado hii haizuii Mheshimiwa Mbunge kupata taarifa ya maeneo ambayo yametengwa. Kupitia TAMISEMI tutawasilisha orodha ya maeneo yote haya ambayo yametengwa ili Waheshimiwa Wabunge pia wafahamu ardhi ambayo imetengwa kwa ajili ya shughuli za vijana kwa ajili ya kilimo, viwanda na ufugaji. Mheshimiwa Naibu Spika, la pili anahoji kuhusu program ambazo tunaziendesha. Ofisi ya Waziri Mkuu kwa 2016/2021 tunaendesha Programu Maalum ya Ukuzaji Ujuzi Vijana yenye lengo la kuwafikia vijana milioni 4.4 kwa mwaka 2021 ili vijana hawa wapate ujuzi waweze kujiajiri na kuajiri vijana wengine. Mheshimiwa Naibu Spika, kwa sababu ameomba azisikie program, kwa ruhusa yako naomba nimtajie chache tu ili ibaki kwenye kumbukumbu sahihi za Bunge hili. Program ya kwanza ambayo tunaifanya inaitwa RPL (Recognition of Prior Learning), ni mfumo wa Urasimishaji wa Ujuzi kwa vijana wenye ujuzi ambao hawajapitia mfumo rasmi wa mafunzo ya ufundi. Ukienda leo mtaani kuna vijana wanajua kupaka rangi au kutengeneza magari lakini hawajawahi kusoma VETA wala Don Bosco. Serikali inachokifanya inarasimisha ujuzi wao na kuwapatia vyeti. (Makofi) Mheshimiwa Naibu Spika, tuna Program ya Greenhouse ambapo kila wilaya tunawafikia vijana 100 katika awamu ya kwanza. Mpaka sasa nchi nzima tumeshafikia vijana 18,800. (Makofi) Mheshimiwa Naibu Spika, tuna Program ya Mafunzo ya Ufundi kupitia vyuo vya Don Bosco na vyuo shirikishi. Takribani vijana 8,800 katika awamu ya kwanza wamenufaika na tunaendelea na awamu ya pili. (Makofi) Mheshimiwa Naibu Spika, tuna program ambayo inaendeshwa DIT Mwanza ya Viatu na Bidhaa za Ngozi ambako vijana wanapata mafunzo na kuweza kunufaika. (Makofi) Mheshimiwa Naibu Spika, program ziko nyingi sana kwa sababu ya muda, naomba niishie hapa lakini Mheshimiwa Mbunge atapata taarifa zaidi. NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu. WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI, VIJANA, AJIRA NA WENYE ULEMAVU: Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu, nampongeza sana Mheshimiwa Naibu Waziri kwa majibu mazuri tena ya kina kabisa. (Makofi) Mheshimiwa Naibu Spika, nataka kuongeza jambo dogo tu, Mheshimiwa Tendega amelalamika hapa kwamba hakuna chochote kinachofanyika na haelewi chochote. Ili kumsaidia zaidi Mheshimiwa Mbunge akumbuke kwamba kila tunapopitisha bajeti za Serikali kila Wizara inaeleza program zote

View Full Text

Details

  • File Type
    pdf
  • Upload Time
    -
  • Content Languages
    English
  • Upload User
    Anonymous/Not logged-in
  • File Pages
    215 Page
  • File Size
    -

Download

Channel Download Status
Express Download Enable

Copyright

We respect the copyrights and intellectual property rights of all users. All uploaded documents are either original works of the uploader or authorized works of the rightful owners.

  • Not to be reproduced or distributed without explicit permission.
  • Not used for commercial purposes outside of approved use cases.
  • Not used to infringe on the rights of the original creators.
  • If you believe any content infringes your copyright, please contact us immediately.

Support

For help with questions, suggestions, or problems, please contact us