NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ____________ MAJADILIANO YA BUNGE ___________ MKUTANO WA KUMI NA MOJA Kikao cha Ishirini na Sita – Tarehe 10 Mei, 2018 (Bunge Lilianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Spika (Mhe. Job Y. Ndugai) Alisoma Dua SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, tukae. Tunaendelea na Kikao cha Ishirini na Sita cha Mkutano wetu huu wa Kumi na Moja. Katibu. NDG. STEPHEN N. KAGAIGAI-KATIBU WA BUNGE: HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019. MAKAMU MWENYEKITI WA KAMATI YA VIWANDA, BIASHARA NA MAZINGIRA - MHE. INNOCENT L. BASHUNGWA: Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira kuhusu Utekelezaji wa Majukumu ya 1 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 pamoja na Maoni ya Kamati kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019. SPIKA: Ahsante sana Mheshimwa Makamu Mwenyekiti. Katibu. NDG. STEPHEN N. KAGAIGAI-KATIBU WA BUNGE: MASWALI KWA WAZIRI MKUU SPIKA: Maswali kwa Mheshimiwa Waziri Mkuu. (Makofi) Swali la kwanza litaulizwa na Mheshimiwa Richard Mganga Ndassa, Mbunge wa Jimbo la Sumve, swali fupi tafadhali. MHE. RICHARD M. NDASSA: Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Kwa idhini yako, naomba uniruhusu niungane na Watanzania wenzangu kwa kuipongeza sana Serengeti Boys baada ya kushinda. (Makofi) SPIKA: Mheshimiwa Ndassa, moja kwa moja kwenye swali. MHE. RICHARD M. NDASSA: Mheshimiwa Spika, Tanzania imepewa heshima kubwa ya kuandaa mashindano ya vijana chini ya umri wa miaka 17, AFCON U17. Swali langu kwa Mheshimiwa Waziri Mkuu, Serikali imejipangaje kufanikisha mashindano hayo? SPIKA: Mheshimiwa Waziri Mkuu, majibu tafadhali. WAZIRI MKUU: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Ndassa, Mbunge wa Sumve, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Ndassa amezungumzia vijana ambao 2 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) wameshinda hivi karibuni Kombe la Afrika Mashariki lakini pia na hawa ambao tunawaandaa kwa mashindano ya Afrika. Kwanza, nitumie nafasi hii kuwapongeza sana vijana wetu wa umri chini ya miaka 17 kwa ushindi mzuri, mkubwa walioupata kule Burundi na ambao pia wataendelea mbele. (Makofi) Mheshimiwa Spika, mbili, tunayo timu ya chini ya miaka 19 ambayo itatuwakilisha kwa kucheza Kombe la AFCON kama ambavyo ameeleza sambamba na heshima ambayo nchi yetu imepewa ya kuendesha mashindano ya chini ya umri wa miaka 19 ambayo yatafanyika 2019. Kwa ujumla wake, timu hizi zote ambazo tunazo kwa sasa ambazo zinacheza kwenye ngazi ya Kimataifa ni jukumu letu kama Serikali kuziandaa. Mimi nataka nitumie nafasi hii kulipongeza sana Shirikisho la Soka Tanzania kwa pamoja na Serikali kupitia Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kwamba wamefikia hatua nzuri baada ya kupata heshima hii kufanya maandalizi na maandalizi yanaendelea. Maandalizi haya, kwanza timu zenyewe tunaziandaa na ninazo taarifa, moja kati ya maandalizi ambayo tunayafanya kwa timu hii ambayo itatuwakilisha tunaipeleka nchini Sweden kwa ajili ya kupata ufundi na maarifa zaidi ili kujihakikishia kwamba michezo yote itakayokuja mwakani tutaweza kushinda. (Makofi) Mheshimiwa Spika, sambamba na hayo, tunajiandaa huku ndani kupata viwanja ambavyo vitatumika kuchezea Kombe lile, lakini pili, maeneo ambayo yatafikiwa na wageni wetu kwa sababu tutakuwa na wageni wengi na mambo yote ambayo yanahusiana na afya, usafiri wao ndani ya nchi, haya yote yanaendelea kufanyiwa maandalizi. Kwa hiyo, nataka niwahakikishie Watanzania maandalizi juu ya michezo yetu ya Kimataifa ambayo pia tumepata heshima ya kucheza hapa nchi yote yanaendelea kama kawaida. Mheshimiwa Spika, nitoe wito kwa Watanzania, pamoja na kazi nzuri iliyofanywa na Wizara na Shirikisho la Soka Tanzania, nawasihi Watanzania tuendelee kuziunga mkono timu zetu zote zinazofikia ngazi za Kimataifa ili ziweze 3 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) kufanya vizuri na nchi yetu iendelee kupata heshima. Pia kwa kufanya hilo, mashindano mengi mengine ambayo yatakuja, basi yaelekezwe nchini Tanzania ili tuweze kupata tija kwa uwepo wa michezo hiyo hapa kwetu Tanzania. (Makofi) Mheshimiwa Spika, ahsante sana. SPIKA: Ahsante sana. Mheshimiwa Ndassa, swali fupi sana tafadhali. MHE. RICHARD M. NDASSA: Mheshimiwa Spika, sawa nitauliza swali fupi sana. Kupitia mashindano haya na kwa sababu kutakuwa na wageni wengi kutoka nje na kwa sababu tunazo fursa za utalii, je, TANAPA na Ngorogoro watashirikishwa namna gani? (Makofi) WAZIRI MKUU: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Ndassa, Mbunge wa Sumve, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Spika, kama ambavyo nimeeleza heshima ambayo tumeipata ya kuendesha mashindano ya dunia hapa kwetu mwakani nayo pia ni fursa kwetu na ziko nyingi ikiwemo na hiyo ya kutangaza vivutio vyetu lakini kuwapeleka wageni wetu kwenye vivutio vile ili tuweze kujipatia fedha. Ni kweli tumeamua kutangaza na mipango ambayo Wizara ya Maliasili inayo sasa ni ya kuimarisha sekta ya utalii kikamilifu kwa kutangaza mapori na vivutio vyote vilivyopo nchini. (Makofi) Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, tutatumia fursa kama hii, kwanza, kwenye viwanja vyake. Pili, kwenye matangazo ya radio na television, lazima tuvionyeshe wakati wote wageni wakiwa hapa. Tatu, kutoa fursa kwao angalau timu moja, mbili, tatu kuwapeleka Kigoma huko wakaone sokwe mtu; tuwapeleke Serengeti na Selou wakaone utalii wa huko na tuwapeleke Kilwa wakaone majengo ya zamani yaliyokaliwa na Waarabu na maeneo mengine yote yenye vivutio vyetu. (Makofi) 4 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) Mheshimiwa Spika, ni matumaini yetu kwamba nafasi hii tutaitumia vizuri na kimsingi niliposema tunafanya maandalizi ni pamoja na kutangaza vivutio vya ndani. Kwa hiyo, nawasihi Watanzania sasa tutumie fursa hii, kila mmoja mwenye sekta ambayo anaona ujio wao utamletea faraja basi ajipange vizuri ili wakati ule wageni wanapoingia aweze kuitumia. Kama unaimarisha sekta ya usafirishaji, kama unaimarisha sekta ya vyakula, kama pia una sekta ambazo unadhani wanahitaji mavazi na kila kitu, ni fursa kwetu Watanzania kutumia matukio kama haya ambayo pia Serikali inaendelea kuyavutia nchini kwetu ili yafungue milango kwa Watanzania wote. Mheshimiwa Spika, ahsante sana. (Makofi) SPIKA: Ahsante sana. Twende CUF, Mheshimiwa Vedasto Edgar Ngombale. MHE. VEDASTO E. NGOMBALE: Mheshimiwa Spika, nashukuru kwa kunipa nafasi. Mheshimiwa Spika, Serikali ilitoa maelekezo kwamba katika msimu huu wa mwaka 2018/2019 zao la ufuta litanunuliwa katika mfumo wa stakabadhi ghalani. Mpaka sasa navyozungumza, ufuta uko tayari, wakulima wameshavuna na wengine wameshauza. Pia maelekezo ya Serikali pia yalisisitiza mikoa yote inayolima zao la ufuta ijiandae kwa mfumo wa stakabadhi ghalani. Je, ni nini tamko la Serikali maana iko kimya na mpaka sasa wafanyabiashara na wakulima hawajui nini kinachoendelea? SPIKA: Majibu ya swali hilo, Mheshimiwa Waziri Mkuu tafadhali. WAZIRI MKUU: Mheshimiwa Spika, naomba nijubu swali la Mheshimiwa Vedasto Ngombale, Mbunge wa Kilwa Kaskazini, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Spika, ni kweli kwamba tumeweka utaratibu wa masoko ya mazao yetu yote nchini . Tumeanza 5 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) na mazao matano lakini pia tumeanza kuingia kwenye mazao haya ambayo yanaonekana yanazalishwa kwa wingi ambayo pia yanatuletea tija kwa wakulima lakini hata kwa Serikali kwa ujumla wake ikiwemo na zao la ufuta. Tumetoa maelekezo kwa Wizara ya Kilimo iratibu vizuri mikoa yote inayolima ufuta. Zao hili mwaka huu litauzwa kwa njia ya mnada ili kuzuia mfanyabiashara mmoja mmoja kwenda kuwarubuni wakulima na kusababisha kupata bei ndogo. (Makofi) Mheshimiwa Spika, tunapotoa maelekezo maana yake kila mmoja anayewajibika kwenye eneo hili lazima afanye kazi yake. Tumetoa maelekezo maalum pia kwa Wakuu wa Mikoa wote wakutane na Wizara na of course Wizara inawajibu wa kuwaita iandae utaratibu na utaratibu huu uende sasa kwa wakulima waelimishwe, waeleweshwe namna nzuri ya kusimamia jambo hili na halmashauri zisimamie kwa karibu kuhakikisha kwamba wakulima ndani ya halmashauri zile hawadhulumiwi na hawauzi kwa bei ndogo ili iweze kuwapatia tija. (Makofi) Mheshimiwa Spika, kwa maelekezo haya na kwa swali lako sasa Wizara ya Kilimo wamesikia, Wakuu wa Mikoa wamesikia na wilaya zinazolima ufuta kwa sababu siyo nchi nzima wanalima ufuta, sasa wajipange wahakikishe wanaratibu vizuri kupitia Maafisa Ushirika na Maafisa Kilimo kuwatambua wakulima na maeneo watakayouza kama mnada ili wakusanye mazao, watangaze siku moja, wanunuzi waje, bei ipatikane wakulima wapate faida, ndiyo mkakati wa Serikali. Wizara ipo na itasimamia jambo hili. (Makofi) SPIKA: Tunaendelea. Mheshimiwa Saed Kubenea, CHADEMA. MHE. SAED A. KUBENEA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi hii. Mheshimiwa Spika, sera ya Serikali ni kila mtu kuabudu dini anayoitaka na kutokuingilia dini ya mtu mwingine. Katiba 6 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) yetu, Ibara ya 3(1) inasema Serikali yetu haina dini isipokuwa watu wana dini. Mheshimiwa Spika, Serikali imetoa kibali kwa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) kuratibu zoezi zima la hija kwa mwaka huu. Kwa msingi huo imeziacha taasisi nyingine ambazo zilikuwa zinapeleka Mahujaji Makkah zisifanye kazi hiyo ikiwemo Kamisheni ya Wakfu na Mali ya Amana - Zanzibar ambayo nayo inatakiwa iratibiwe na BAKWATA. Mheshimiwa Spika, swali langu kwa Mheshimiwa Waziri Mkuu, nini msimamo wa Serikali sasa kwa kuwa suala hili limeleta sintofahamu na gharama za kupeleka Mahujaji Makkah kupitia
Details
-
File Typepdf
-
Upload Time-
-
Content LanguagesEnglish
-
Upload UserAnonymous/Not logged-in
-
File Pages351 Page
-
File Size-