NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ________ MAJADILIANO YA BUNGE _________ MKUTANO WA TATU Kikao cha Kumi na Tisa – Tarehe 29 Aprili, 2021 (Bunge Lilianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Naibu Spika (Mhe. Dkt. Tulia Ackson) Alisoma Dua NAIBU SPIKA: Waheshimiwa, tukae. Katibu. NDG. MOSSY LUKUVI – KATIBU MEZANI: HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI Hati Zifuatazo Ziliwasilishwa Mezani na:- NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Randama za Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kwa mwaka wa fedha 2021/2022. NAIBU WAZIRI WA MADINI: Hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Madini kwa mwaka wa fedha 2021/2022. 1 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) MHE. SAADA MONSOUR HUSSEIN - K.n.y. MWENYEKITI WA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA NISHATI NA MADINI: Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini kuhusu utekelezaji wa Majukumu ya Wizara ya Madini kwa mwaka wa fedha 2020/2021 pamoja na Maoni ya Kamati kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2021/2022. NAIBU SPIKA: Ahsante sana. Katibu. NDG. MOSSY LUKUVI – KATIBU MEZANI: MASWALI NA MAJIBU SPIKA: Waheshimiwa maswali, tutaanza na Ofisi ya Rais, TAMISEMI, Mheshimiwa Simon Songe Lusengekile, Mbunge wa Busega, sasa aulize swali lake. Na. 158 Serikali Kukamilisha Ujenzi wa Zahanati – Busega MHE. SIMON S. LUSENGEKILE aliuliza:- Wananchi wa Kata ya Imalamate Wilayani Busega wamejenga zahanati na kumaliza maboma manne kwa maana ya zahanati moja kila kijiji:- Je, Serikali ina mpango gani wa kuwasaidia wananchi hao kuezeka maboma hayo ili waweze kupata huduma za afya kwenye zahanati hizo? NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri wa TAMISEMI, Mheshimiwa Dkt. Festo Dugange, majibu. NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE) alijibu:- 2 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Simon Songe Lusengekile, Mbunge wa Busega, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali imeendelea kuboresha miundombinu ya huduma za afya katika Wilaya ya Busega, ambapo katika Mwaka wa Fedha 2017/2018, Serikali iliipatia Halmashauri ya Wilaya ya Busega shilingi milioni 250 kwa ajili ya ukarabati wa Kituo cha Afya Nasa na kukiwezesha kuanza kutoa huduma za dharura za upasuaji. Mheshimiwa Naibu Spika, aidha, katika Mwaka wa Fedha 2018/2019 Serikali iliipatia halmashauri hiyo shilingi bilioni 1.8 kwa ajili ya ujenzi wa Hospitali ya Halmashauri. Vilevile, mwezi Februari, mwaka 2021 Serikali iliipatia Halmashauri ya Wilaya ya Busega shilingi milioni 500 kwa ajili ya ujenzi wa wodi tati katika Hospitali ya Halmashauri na imetenga shilingi milioni 500 katika bajeti ya mwaka 2020/2021 kwa ajili ya ununuzi wa vifaa tiba katika hospitali hiyo. Mheshimiwa Naibu Spika, mwezi Februari, 2021, Serikali imeipatia Halmashauri ya Wilaya ya Busega shilingi milioni 150 kwa ajili ya kukamilisha maboma ya Zahanati za Ng’wang’wenge, Sanga na Mkula. Vilevile, katika Mwaka wa Fedha 2021/2022, Serikali imetenga shilingi milioni 150 kwa ajili ya kukamilisha maboma ya Zahanati ya Imalamate, Ijutu na Busami katika Halmashauri ya Wilaya ya Busega. Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali itaendelea kuimarisha miundombinu ya huduma za afya katika Jimbo la Busega na nchini kote ili kuendelea kuboresha huduma za afya kwa wananchi. NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Simon Songe Lusengekile, swali la nyongeza. MHE. SIMON S. LUSENGEKILE: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana. Niishukuru Serikali kwa majibu mazuri ambayo Naibu Waziri amewasilisha, lakini nina maswali mawili ya 3 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) nyongeza. Swali la kwanza; wananchi wa Kata hii ya Imalamate yenye vijiji vitatu, kwa maana ya Mahwenge, Imalamate pamoja na Jisesa, wamejitolea sana kwa kujenga maboma ya kisasa ya zahanati. Je, Serikali haioni sasa umuhimu wa kuifanya kata hii kuwa moja ya kata za mfano ambazo wananchi wamejitolea kwa kujenga maboma haya ili waipatie kipaumbele cha kukamilisha maboma haya? Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili; je, Naibu Waziri yuko tayari sasa baada ya Bunge baada ya Bunge hili la Bajeti kuambatana pamoja nami ili kwenda kuwatembelea wananchi wa Kata ya Imalamate kuona kazi kubwa ambayo wameifanya ambayo itakuwa ya kuigwa katika nchi yetu? (Makofi) NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, majibu. NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Simon Songe Lusengekile, Mbunge wa Busega, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza, nianze kwa kumpongeza sana Mheshimiwa Simon Songe Lusengekile, Mbunge wa Busega, kwa kazi kubwa sana anayoifanya ya kuhakikisha anawasemea wananchi wake na kufuatilia miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo miradi ya huduma za afya. Pia niwapongeze sana wananchi wa Kata hii ya Imalamate na wananchi wa Busega kwa ujumla kwa kuendelea kuchangia nguvu zao katika ujenzi wa miundombinu ya kutoa huduma za afya kwa maana ya zahanati na vtuo vya afya. Mheshimiwa Naibu Spika, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba Serikali inatambua na inathamini kwamba wananchi hawa wameendelea kutoa nguvu zao. Na ni kweli, ni moja ya kata ambazo zimefanya vizuri katika ujenzi wa vituo vya afya na hivyo katika mwaka ujao wa fedha, 4 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) tumetenga shilingi milioni 150 kwa ajili ya maboma matatu katika Jimbo la Busega. Kwa hiyo bila shaka fedha hizi zitakwenda kukamilisha majengo haya katika Kata ya Imalamate. Mheshimiwa Naibu Spika, niko tayari kuambatana na Mheshimiwa Mbunge kwenda kushirikiana naye kuwahudumia wananchi wa Busega, lakini pia kutambua michango yao. Hivyo baada ya kikao hiki, tutapanga na Mheshimiwa Simon Songe tuweze kuona lini muda muafaka tutaambatana kwenda Jimboni kwake Busega. NAIBU SPIKA: Ahsante sana. Mheshimiwa Leah Jeremiah Komanya, swali la nyongeza. MHE. LEAH J. KOMANYA: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru. Wananchi wa Jimbo la Meatu wapo wanaotembea hadi kilometa 40 kwenda tu kufuata huduma za afya katika zahanati. Je, ni lini Halmashauri ya Wilaya ya Meatu italetewa fedha za kukamilisha maboma katika ule utaratibu wa kukamilisha maboma matatu kwa mwaka 2020/ 2021? NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, majibu. NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Leah Komanya, Mbunge wa Meatu, kama ifuatavyo: - Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza nampongeza sana Mheshimiwa Leah Komanya kwa kazi kubwa anayoifanya ya kuwasemea wananchi wa Meatu, lakini pia kuhakikisha miradi ya huduma za afya inakamilishwa na kusogeza huduma za afya karibu zaidi na wananchi. Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli kwamba Jimbo la Meatu ni jimbo kubwa na wananchi wanafuata huduma za 5 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) afya mbali kutoka kwenye makazi yao. Ndiyo maana Serikali imeweka mpango wa maendeleo ya afya msingi kuhakikisha tunajenga zahanati katika kila kijiji, vituo vya afya katika kata ili kusogeza huduma hizi kwa wananchi. Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nimhakikishie kwamba katika mwaka huu wa fedha 2020/2021, Serikali ilitenga shilingi bilioni 27.75 na tayari imekwishatoa shilingi bilioni 23 katika majimbo na wilaya zipatazo 133 kwa ajili ya ukamilishaji wa maboma matatu kwa kila halmashauri. Mheshimiwa Naibu Spika, pia nimhakikishie kabla ya mwisho wa mwaka huu wa fedha, Juni 30, Jimbo la Meatu pia litakuwa limepata fedha zile shilingi milioni 150 kwa ajili ya kukamilisha maboma hayo. Hili ni sambamba na majimbo na halmashauri zote ambazo bado hazijapata milioni 150, shughuli hiyo inaendelea kutekelezwa na kabla ya Juni 30, fedha hizo zitakuwa zimefikishwa katika majimbo hayo. NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Issa Ally Mchungahela, swali la nyongeza, amepotea. Mheshimiwa Boniventura Kiswaga, swali la nyongeza. MHE. BONIVENTURA D. KISWAGA: Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kuwa tatizo lililoko Busega linafanana kabisa na tatizo lililoko katika Jimbo la Magu. Jimbo la Magu lina vijiji 82, vijiji 40 vina zahanati, vijiji 42 havina zahanati. Tunavyo vijiji 21 ambavyo vimekamilisha maboma ya zahanati. Je, Serikali ina mpango gani wa kumalizia maboma hayo 21 ambayo yanahitaji bilioni moja na milioni 50 ili wananchi waweze kupata huduma kama inavyosema Ilani ya Chama Cha Mapinduzi kwamba kila kijiji kiwe na zahanati? NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, majibu. NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu swali la nyongeza 6 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) la Mheshimiwa Boniventura Kiswaga, Mbunge wa Magu, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli kwamba Serikali inaendelea kujenga vituo vya afya na zahanati katika vijiji na kazi kubwa imekwishafanyika nchini kote ikiwepo katika Jimbo la Magu. Hata hivyo, ni kweli kwamba bado kazi ni kubwa, bado kuna vijiji vingi na kata nyingi ambazo bado zinahitaji kujenga vituo vya afya na zahanati. Naomba nimhakikishie Mheshimiwa Kiswaga kwamba Serikali itaendelea kutenga fedha kila mwaka wa fedha kuhakikisha tunaendelea kujenga vituo vya afya na zahanati nchini kote, lakini pia katika Jimbo hili la Magu. Mheshimiwa Naibu Spika, nitambue kwamba katika mwaka huu wa fedha, tayari Jimbo la Magu limeshapelekewa milioni 150 kwa ajili ya kuchangia nguvu za wananchi kujenga na kukamilisha maboma matatu na katika mwaka ujao wa fedha pia imekwishatengewa shilingi milioni 150 kwa ajili ya kukamilisha maboma matatu
Details
-
File Typepdf
-
Upload Time-
-
Content LanguagesEnglish
-
Upload UserAnonymous/Not logged-in
-
File Pages292 Page
-
File Size-