NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA __________ MAJADILIANO YA BUNGE __________ MKUTANO WA TATU Kikao cha Tano – Tarehe 8 Aprili, 2021 (Bunge Lilianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Spika (Mhe. Job Y. Ndugai) Alisoma Dua SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, tukae. Waheshimiwa Wabunge, Asalaam Aleykum! Bwana Yesu asifiwe! Baada ya msimu wa Pasaka na sikukuu zake na jana tulikuwa na Kumbukumbu ya Mashujaa na kipekee kumkumbuka Mwanzilishi wa Taifa letu, Mzee Karume, sasa leo tunaendelea na kazi. Jamhuri ya Muungano wa Tanzania! WABUNGE FULANI: Kazi iendelee. SPIKA: Aah, kumbe mnajua! Jipigieni makofi basi, kazi iendelee. (Kicheko/Makofi) Katibu. NDG. STEPHEN KAGAIGAI – KATIBU WA BUNGE: HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na:- 1 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: (a) Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Taifa kwa Kipindi cha Miaka Mitano kuanzia 2021/2022 – 2025/2026 (The 3rd National Five Years Development Plan, 2021/22 – 2025/ 26); (b) Ripoti Kuu ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kuhusu Ukaguzi wa Taarifa za Fedha za Serikali Kuu kwa Mwaka wa Fedha ulioishia tarehe 30 Juni, 2020 (The Annual General Report of the Controller and Auditor General on the Central Government for the Financial Year Ended 30th June, 2020); (c) Ripoti Kuu ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kuhusu Ukaguzi wa Taarifa za Fedha za Miradi ya Maendeleo kwa Mwaka wa Fedha ulioishia tarehe 30 Juni, 2020 (The Annual General Report of the Controller and Auditor General on the Audit of Development Projects for the Financial Year Ended 30th June, 2020); (d) Ripoti Kuu ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kuhusu Ukaguzi wa Taarifa za Fedha za Mashirika ya Umma kwa Mwaka wa Fedha ulioishia tarehe 30 Juni, 2020 (The Annual General Report of the Controller and Auditor General on the Audit of Public Authorities and Other Bodies for the Financial Year Ended 30th June, 2020); (e) Ripoti ya jumla ya Ukaguzi wa Ufanisi na Ukaguzi Maalum kwa kipindi kinachoishia Tarehe 31 Machi, 2021 (The Annual General Report on the Performance and Specialised Audits for the Period Ending 31st March, 2021); (f) Ripoti ya Ukaguzi wa Ufanisi juu ya Usimamizi wa Mali zilizotelekezwa (Performance Audit on the Management of Unclaimed Assets); (g) Ripoti ya Ukaguzi wa Ufanisi juu ya Utekelezaji wa Udhibiti wa Uhamishaji wa Bei ya Mauziano ya Bidhaa au Huduma Baina ya Makampuni yenye Mahusiano 2 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) (Performance Audit on the Implementation of Controls over Transfer Pricing); (h) Ripoti ya Ukaguzi wa Ufanisi juu ya Usimamizi wa Ununuzi wa Pamoja wa Magari ya Serikali na Usambazaji wa Mafuta (Performance Audit on the Management of Procurement of Government Vehicles and Distribution of Fuel); (i) Ripoti ya Ukaguzi wa Ufanisi juu ya Usimamizi wa Misamaha ya Kodi kwenye Miradi ya Uwekezaji (Performance Audit on the Management of Tax Exemption on Investment Projects); na (j) Majumuisho ya Majibu ya Hoja na Mpango wa Kutekeleza Mapendekezo ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa Hesabu za Serikali Kuu na Mashirika ya Umma kwa Mwaka wa Fedha ulioishia tarehe 30 Juni, 2020. SPIKA: Ahsante sana Mheshimiwa Naibu Waziri Fedha, umeanza vyema, nakushukuru sana. (Makofi) Waheshimiwa Wabunge, bado ripoti zinaendelea kuja. Sasa ni ripoti kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, karibu sana Mheshimiwa Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu. NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, AJIRA, VIJANA, NA WATU WENYE ULEMAVU (MHE. PASCAL P. KATAMBI): (a) Ufuatiliaji wa Utekelezaji wa Mapendekezo ya Kaguzi za Ufanisi zilizofanyika na kuwasilishwa Bungeni mwezi Aprili, 2016 (Follow-Up on Implementation of the Controller and Auditor General’s Recommendations for Performance Audit Reports Issued and Tabled to Parliament in April, 2016); (b) Ripoti ya Ukaguzi wa Ufanisi juu ya Utekelezaji wa Mradi wa Uzalishaji Sukari wa Mbigiri (Performance Audit 3 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) on the Implementation of Mbigiri Sugar Production Project); na (c) Ripoti ya Ukaguzi wa Ufanisi juu ya Usimamizi wa Udhibiti wa Mafuriko (Performance Audit on Flood Control Measures); SPIKA: Ahsante sana. Sasa tuelekee TAMISEMI. Naibu Waziri wa TAMISEMI, Mheshimiwa David Silinde, tafadhali. NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DAVID E. SILINDE): (a) Ripoti Kuu ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kuhusu Ukaguzi wa Taarifa za Fedha za Serikali za Mitaa kwa Mwaka wa Fedha ulioishia tarehe 30 Juni, 2020 (The Annual General Report of the Controller and Auditor General on the Local Government Authorities for the Financial Year Ended 30th June, 2020); (b) Ripoti ya Ukaguzi wa Ufanisi juu ya Usimamizi wa Usafi wa Masoko ya Vyakula (Performance Audit on Hygiene Control in Food Markets); (c) Ripoti ya Ukaguzi wa Ufanisi juu ya Usimamizi wa Ujenzi wa Majengo ya Vituo vya Huduma za Afya Nchini (Performance Audit on the Management of Construction of Healthcare Facilities); (d) Ripoti ya Ukaguzi wa Ufanisi juu ya Ufuatiliaji na Usimamizi wa Miradi ya Ujenzi kwenye Sekta ya Elimu inayotekelezwa kwa njia ya “Force Account” (Performance Audit on Monitoring and Supervision of Construction Projects Implemented through Force Account in Education Sector); na (e) Taarifa ya Majibu ya Serikali na Mpango Kazi wa Utekelezaji wa Mapendekezo ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa Hesabu za Mamlaka za Serikali za Mitaa kwa Mwaka ulioishia tarehe 30 Juni, 2020. 4 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) SPIKA: Ahsante sana Mheshimiwa Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu. Nakushukuru sana Mheshimiwa Silinde. Waheshimiwa Wabunge, mtaona ripoti zipo nyingi, ndiyo maana tunasema ukiwa Mbunge lazima uwe na juhudi ya kusoma na kupitia vitu, utaona volume na volumes. Waheshimiwa Wabunge, sasa baada ya TAMISEMI kutupatia ripoti zao, niseme kwamba hatutakuwa na kipindi cha maswali kwa Mheshimiwa Waziri Mkuu kwa udhuru kidogo asubuhi hii. Kwa hiyo, tutaendelea na maswali ya kawaida. Waheshimiwa Wabunge, kabla ya hapo, niendelee kuwakumbusha kuendelea kujaza kipaumbele cha uchangiaji wetu katika kupitia mfumo wa Bunge mtandao unaopatikana katika dirisha la shughuli za Bunge. Wataalamu wa TEHAMA wapo katika maeneo ya ukumbi wetu, watakuwa wanapita humo. Kama unahitaji msaada wao, tafadhali unaweza ukawaambia, ushers hao wakakuitia ili uweze kuchagua ni Wizara gani ambazo ungependa upate nafasi ya uchangiaji. Kwa sababu ukisubiri siku hiyo, inawezekana katika maombi ambayo yako siku hiyo usipate nafasi. Nawe labda kama Mbunge ungependa sana Wizara fulani na Wizara fulani usikose kupata nafasi ya kuchangia kwa kusema. Waheshimiwa Wabunge, nadhani tunaelewana katika hilo, ili tusilaumiane mbele ya safari, bora uonyeshe vipaumbele vyako mapema ili tuwe navyo. Baada ya hilo, tunaendelea sasa. Katibu. NDG. STEPHEN KAGAIGAI – KATIBU WA BUNGE: Bado kuna hati hazijawasilishwa. SPIKA: Aah, kuna hati! Ooh, bado, bado. Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Utumishi na Utawala Bora). Samahani. 5 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS (UTUMISHI NA UTAWALA BORA): Ripoti Kuu ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kuhusu Ukaguzi wa Mifumo ya TEHAMA kwa mwaka wa fedha ulioishia tarehe 30 Juni, 2020 (The Annual General Report of the Controller and Auditor General on the Audit of Information Systems for the Financial Year Ended 30th June, 2020). SPIKA: Ahsante sana Mheshimiwa Deogratius Deo Ndejembi kwa uwasilishaji huo. Sasa twende na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mheshimiwa Hamad Hassan Chande, Mbunge wa Kojani, karibu sana Bungeni. NAIBU WAZIRI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS, (MUUNGANO NA MAZINGIRA): Mheshimiwa Spika, kwa kuwa ni mara ya mwanzo kusimama hapa naomba kwa idhini yako nimshukuru Mwenyezi Mungu Subhna-huwataala. Pili nimshukuru Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuniamini nami naahidi kujiaminisha. Kama mwana Falsafa alivyosema, wasia tatu ni vyema kuzingatiwa. Moja, unapoaminiwa ujiaminishe; pili, anapotajwa Mungu, basi usipite, mtangulize Mungu; na jambo la tatu subiri kichache upate kingi. Maana yake tutangulize subira. Ripoti ya Ukaguzi wa Ufanisi juu ya Udhibiti wa Uchafuzi unaotokana na Taka za Plastiki kwenye Bahari na Maziwa (Performance Audit on the Control of Plastic Wastes Pollution in Lakes and Ocean). SPIKA: Ahsante sana. Huyo ni Mbunge wa Kojani anaitwa Mheshimiwa Chande. Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi. Karibu sana Mheshimiwa Naibu Waziri. 6 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Ripoti ya Ukaguzi wa Ufanisi juu ya Uandikishaji na Utoaji wa Vitambulisho vya Taifa (Performance Audit on the Registration and Issuance of National Identification Cards). SPIKA: Ahsante sana Mheshimiwa Hamza Khamis Khamis, Mbunge wa Uzini. Waheshimiwa Wabunge, Watanzania wanataka kuwafahamu, ndiyo maana inanibidi niweke msisitizo. Ahsante sana. Mheshimiwa Khamis, Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi sasa, karibu sana Engineer. NAIBU WAZIRI WA UJENZI NA UCHUKUZI: (a) Ripoti ya Ukaguzi wa Ufanisi kuhusu Utekelezaji wa Mradi wa Awamu ya Pili ya Ujenzi wa Miundombinu ya Mabasi yaendayo kasi Dar es Salaam (Performance Audit on the Implementation of the Construction of Dar es Salaam Bus Rapid Transit (BRT) Infrastructure – Phase 2); na SPIKA: Ahsante sana. Huyo ni Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mheshimiwa Eng. Godfrey Kasekenya Msongwe, yeye ni Mbunge wa Ileje. Tunaendelea na Wizara ya Viwanda na Biashara. Ahsante. NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA: Ripoti ya Ukaguzi wa Ufanisi juu ya Usimamizi wa Mifumo ya Kudhibiti Ubora wa Vyakula
Details
-
File Typepdf
-
Upload Time-
-
Content LanguagesEnglish
-
Upload UserAnonymous/Not logged-in
-
File Pages241 Page
-
File Size-