Majadiliano Ya Bunge ______

Majadiliano Ya Bunge ______

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) BUNGE LA TANZANIA _______________ MAJADILIANO YA BUNGE ______________ MKUTANO WA KUMI NA SITA Kikao cha Arobaini na Moja – Tarehe 29 Julai, 2009 (Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi) DUA Mwenyekiti (Mhe. Jenista J. Mhagama) Alisoma Dua HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na:- NAIBU WAZIRI WA AFYA NA USTAWI WA JAMII: Hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kwa Mwaka wa Fedha 2009/2010. MHE. DR. HAJI MWITA HAJI (K.n.y. MHE. OMARI S. KWAANGW’) – MWENYEKITI WA KAMATI YA HUDUMA ZA JAMII: Taarifa ya Kamati ya Huduma za Jamii kuhusu Utekelezaji wa Majukumu ya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kwa Mwaka 2008/2009 pamoja na maoni ya Kamati kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo kwa Mwaka wa Fedha 2009/2010. MHE. OMAR ALLY MZEE (K.n.y. MHE. DR. ALI TARAB ALI – MSEMAJI MKUU WA KAMBI YA UPINZANI KUHUSU WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII): Taarifa ya Msemaji Mkuu wa Kambi ya Upinzani kuhusu Makadirio ya Matumizi ya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kwa Mwaka wa Fedha 2009/2010. NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA UCHUMI – MHE. OMAR YUSSUF MZEE: Randama za Makadirio ya Wizara ya Fedha na Uchumi kwa Mwaka wa Fedha 2009/2010. MASWALI NA MAJIBU 1 Na. 299 Ujenzi wa Barabara za Manispaa ya Singida MHE. DIANA M. CHILOLO (K.n.y. MHE. MOHAMED G. DEWJI) aliuliza:- Kwa kuwa lengo mojawapo la Halmashauri ya Manispaa ya Singida ni kuhakikisha kuwa barabara zilizopo ndani ya Manispaa hiyo zinakuwa katika kiwango cha lami:- Je, Serikali ina mpango gani wa kuunga mkono jitihada za Manispaa katika ujenzi wa barabara hizo ? NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA alijibu:- Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Mohamed Gulam Dewji, Mbunge wa Singida Mjini, kama ifuatavyo:- Mhehimiwa Mwenyekiti, baadhi ya barabara za Halmashauri ya Manispaa ya Singida zilijengwa katika miaka ya tisini (1990’s) na kuendelea. Serikali inatambua umuhimu wa kuhakikisha kuwa barabara hizi zinaimarishwa kwa kujengwa kwa kiwango cha lami. Katika kuunga mkono juhudi za Halmashauri ya Manispaa ya Singida, Serikali kupitia Mfuko wa Barabara imefanya yafuatayo:- Katika mwaka 2007/2008, Halmashauri ya Manispaa ya Singida, ilipata shilingi milioni 100 kwa ajili ya ujenzi wa barabara ya VETA yenye urefu wa kilometa 1.0 kwa kiwango cha lami. Mwaka 2008/2009, Serikali ilitoa shilingi milioni 230 ili kukamilisha ujenzi wa barabara ya VETA. Mkandarasi Chico Engineering ambaye alikuwa anajenga barabara kuu ya Shelui-Singida alipewa kazi ya kujenga barabara ya VETA na ujenzi ulikamilika na iko katika hali nzuri. Mheshimiwa Mwenyekiti, mwaka wa fedha 2007/2008, Serikali pia ilitoa shilingi milioni 150 kwa ajili ya matengenezo maalum (periodic maintenance), kwa barabara za lami zilizopo na mwaka 2008/2009, Halmashauri ya Manispaa ya Singida, ilipatiwa shilingi milioni 250 kwa ajili ya matengenezo ya muda maalum kwa barabara za lami zenye urefu wa kilometa 2.1. Hivi sasa utekelezaji unaendelea kwa kujenga barabara ya Stanley yenye urefu wa kilometa 0.25 kwa kiwango cha lami kwa gharama ya shilingi milioni 97 na Mkandarasi Trust Engineering anafanya kazi hiyo. Aidha, kwa mwaka wa fedha 2009/2010 yaani hii tuliyopitisha, Serikali imeidhinisha kiasi cha shilingi milioni 220 kwa ajili ya kuendelea na matengenezo ya barabara ya lami katika Manispaa ya Singida. Msisitizo mkubwa wa Serikali ni kuunganisha barabara kati ya Wilaya na Wiilaya ili kurahisisha mawasiliano katika eneo hilo. 2 MHE. DIANA M. CHILOLO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Naibu Waziri, nina maswali mawili madogo ya nyongeza. La kwanza, kwa kuwa mji wa Singida unakua kila siku na una barabara nyingi sana za mitaa na kama alivyojibu Mheshimiwa Naibu Waziri, ni barabara moja tu mpaka sasa hivi ambayo imetengenezwa kwa kiwango cha lami na kila wanapoomba pesa, wanapewa chini ya zile walizoomba. Je, Serikali haioni sasa katika kuboresha Manispaa ya Singida, kuna kila sababu kutoa pesa zile zinazoombwa na Manispaa hiyo? (Makofi) Pili, kwa kuwa hata hiyo barabara ambayo imejengwa, haina hata mifereji ya kusafirisha maji, je, haoni kwamba sasa kuna sababu ya kutoa pesa mapema iwezekanavyo za kutengeneza mifereji ili barabara hiyo isije ikaharibiwa na maji? NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza, nataka niliweke hili vizuri ili Bunge lako liweze kupata picha kamili kwa sababu nakubaliana na anachosema Mheshimiwa Diana Chilolo, mji huu ni mji ambao unakua vizuri sana, Manispaa hii inakua vizuri sana na kama sisi wote tunavyofahamu iko katikati kwa kweli kwenye ile barabara kuu inayotoka Kusini mpaka Kaskazini. Kwa hiyo, anachozungumza hapa anazungumza jambo la msingi sana kwa sababu ni Manipaa ambayo inakua vizuri na ambayo ikiwekewa mazingira mazuri, itatusaidia sana katika maendeleo ya nchi nzima kwa ujumla wake. (Makofi) Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka tu niseme kwamba, barabara ya Karume ina kilomita 0.7 ambayo ilishakamilika, barabara ya Kawawa ina kilomita 0.6, ya Lumumba ina kilomita 0.4, Ipembe kilomita 0.4, Megeni kilomita 0.46, Soko kilomita 0.4, Boma Road kilomita 1.2, Stand kilomita 0.4 na VETA kilomita moja. Sasa anachosema hapa ni kwamba tunaisaidiaje hii barabara ambayo imekamilika na hizi zingine kwa maana ya kuziwekea mifereji. Mimi najua na Mheshimiwa Mgana Msindai, naona anasimama pale, najua ndiyo maswali yatakayoulizwa hapa, tatizo kubwa lililoko hapa na nimesoma takwimu hizi, Mheshimiwa Mwenyekiti ili lazima ujue tatizo. Tatizo kubwa tunalolipata hapa ni kwamba zikiwa kilomita ndogo ndogo hizi unazoziona hapa hata upatikanaji wa Mkandarasi unakuwa ni mgumu sana. Ndiyo tatizo kubwa tunalolipata pale Singida. Ikishakuwa kidogo kidogo hivi, inakuwa ni ngumu sana. Kwa hiyo, anachosema Mheshimiwa Chilolo na wanachosema Wabunge wa Singida ni kwamba at least uwe na package moja ambayo ni ndefu kama anavyosema hapa halafu uweze kutoa sasa kwa ajili ya Mkandarasi ili Mkandarasi aweze kupatikana. Hatuna tatizo na hilo. Tuwasiliane, tuangalie jinsi ambavyo tunaweza tukaziunganisha hizi barabara vizuri ili tuweze kumpata Mkandarasi. Hili la mifereji analolizungumza hapa ni la msingi sana Mheshimiwa Mwenyekiti. Naomba nimalizie. Ni la msingi kwa sababu ukijenga barabara kama hujaiwekea mifereji ya kuptishia maji ni kazi bure. Nataka nitoe rai hapa kwa Halmashauri zote, haina maana kwenda kilomita nyingi sana wakati huo hujaiwekea mifereji ya kutolea maji. Mifereji ya kutolea maji ni roho ya barabara. Kwa hiyo, mimi nakubaliana naye kwamba kuna 3 haja ya kuliangalia jambo hili, tutaangalia katika Bajeti yao kwamba tumepitisha kiasi gani ili tuweze kusaidia eneo hilo. (Makofi) MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge, nimemwona Mheshimiwa Waziri mwenye dhamana ya Miundombinu nchini, naomba nimpe nafasi. WAZIRI WA MAENDELEO YA MIUNDOMBINU: Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya majibu mazuri haya ya Mheshimiwa Naibu Waziri, naomba kutoa majibu ya ziada ama maelezo ya ziada kama ifuatavyo, kwamba Serikali Kuu inatambua umuhimu wa Manispaa ya Singida na katika kazi nyingi tunazozifanya, tumeweka mkakati kuhakikisha kwamba tunaboresha miundombinu ya barabara ndani ya Manispaa hiyo. Sasa hivi tunajenga ya Singida mpaka Babati na ndani yake tumeweka kilomita 1.3 kwa ajili ya ujenzi ndani ya Mji wa Singida kwa maana hiyo ni pamoja na mifereji hiyo. (Makofi) Lakini pia kwenye ujenzi wa barabara ya kwenda Shelui, tuliweka kilomita 1.3 pia ambayo imejengwa kwa lami. Kwa hiyo, tutaendelea kuhakikisha kwamba kila tunapojenga barabara kuu ambazo zinaenda kwenye Manispaa hii tutaingiza sehemu katika barabara za Manispaa. Nashukuru sana. (Makofi) MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge wa Singida, baada ya majibu hayo, bado tu? Haya swali la mwisho Mheshimiwa Nyalandu. MHE. LAZARO S. NYALANDU: Nakushukuru sana Mheshimiwa Mwenyekiti. Kwa kuwa Serikali ilionyesha nia kabisa ya kujenga barabara ya Singida Mjini kuiunganisha na Ilongero kwa lami hasa wakati mradi huu wa kwenda Mwanza-Singida unakamilika. Naomba tu Waziri awathibitishie watu wa Ilongero kama nia ile iko pale pale. NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Mwenyekiti, anazungumzia barabara ya Singida Mjini kwenda Ilongelo, naomba nikiri hapa kwamba hii barabara sijaijua vizuri. Kwa hiyo, nikiitamka tu hapa nikasema ni sawa sawa, nitakuwa siitendei haki. Namwomba Mheshimiwa Lazaro Nyalandu, tutawasiliana, tutakwenda kuangalia katika inventory zetu, hapa tunazungumzia barabara za lami ambazo gharama zake ni kubwa sana, siwezi kui-commit Serikali hapa, naomba niende nikaangalie vizuri barabara hii halafu baadaye tutaeleza. (Makofi) Na. 300 Wajibu wa Wakuu wa Idara Kufuata Kanuni na Sheria MHE. MWANAWETU S. ZARAFI aliuliza:- 4 Kwa kuwa Wakuu wa Idara katika Halmashauri za Wilaya/Miji wanatambua wajibu wao katika kufanya kazi zao na kwa kuwa kuna Kanuni na Sheria zinazowaongoza kutoa maamuzi:- (a) Je, kwa nini kunapotokea wizi au ubadhirifu wa fedha za umma, watendaji hao hawatumii Kanuni hizo na badala yake huungana na wanasiasa kupuuza na kuzibadlisha kesi za ubadhirifu hata kama kuna ushahidi wa kutosha? (b) Je, Serikali inasemaje kuhusu Wakuu wa Idara na wabadhirifu hao wa mali za umma? NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA alijibu:- Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Mwanawetu Said Zarafi, Mbunge wa Viti Maalum, lenye sehemu (a) na (b) kama ifuatavyo:- (a) Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli kuwa Wakuu wa

View Full Text

Details

  • File Type
    pdf
  • Upload Time
    -
  • Content Languages
    English
  • Upload User
    Anonymous/Not logged-in
  • File Pages
    196 Page
  • File Size
    -

Download

Channel Download Status
Express Download Enable

Copyright

We respect the copyrights and intellectual property rights of all users. All uploaded documents are either original works of the uploader or authorized works of the rightful owners.

  • Not to be reproduced or distributed without explicit permission.
  • Not used for commercial purposes outside of approved use cases.
  • Not used to infringe on the rights of the original creators.
  • If you believe any content infringes your copyright, please contact us immediately.

Support

For help with questions, suggestions, or problems, please contact us