NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ______________ MAJADILIANO YA BUNGE ________ MKUTANO WA SITA Kikao cha Nne – Tarehe 3 Februari, 2017 (Bunge Lilianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Mwenyekiti (Mhe. Mussa A. Zungu) Alisoma Dua MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge tukae! Katibu! NDG. THEONEST RUHILABAKE - KATIBU MEZANI: HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na:- MHE. NAJMA MURTAZA GIGA - MWENYEKITI WA KAMATI YA BUNGE YA KATIBA NA SHERIA: Taarifa ya mwaka ya shughuli za Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria kwa kipindi cha kuanzia Januari, 2016 hadi Januari, 2017. MHE. ESTHER A. MAHAWE - K.n.y. MWENYEKITI WA KAMATI YA BUNGE YA UTAWALA NA SERIKALI ZA MITAA: Taarifa ya mwaka ya shughuli za Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa kwa kipindi cha kuanzia Januari, 2016 hadi Januari, 2017. MWENYEKITI: Ahsante! Katibu! NDG. THEONEST RUHILABAKE - KATIBU MEZANI: 1 NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT) MASWALI NA MAJIBU MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge, tunaanza na Ofisi ya Rais - TAMISEMI, Mheshimiwa Benardetha Mushashu. Na. 42 Madai Mbalimbali ya Walimu MHE. BENARDETHA K. MUSHASHU aliuliza:- Walimu wamekuwa wakiidai Serikali stahiki zao mbalimbali na tatizo hili la kutowalipa kwa muda muafaka limekuwa likijirudia rudia:- (a) Je, walimu wanadai stahiki zipi na kwa kiasi gani? (b) Je, Serikali imejipangaje kutatua tatizo hilo na kulimaliza kabisa? NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA alijibu:- Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Bernadetha Mushashu, Mbunge wa Viti Maalum lenye sehemu (a) na (b) kama ifuatavyo:- (a) Mheshimiwa Mwenyekiti, madai ya walimu yasiyo ya mishahara ni shilingi bilioni 26 hadi kufikia Desemba, 2016. Deni hili limeshahakikiwa na kuwasilishwa hazina kwa taratibu za mwisho ili liweze kulipwa. Aidha, madeni yanayotokana na mishahara ni shilingi bilioni 18.1. Uhakiki wa deni la shilingi bilioni 10 umekamilika na linasubiri kulipwa kupitia akaunti ya mtumishi anayedai. Deni linalobaki la shilingi bilioni 8.06 linaendelea kuhakikiwa ili liweze kulipwa. (b) Mheshimiwa Mwenyekiti, ili kudhibiti uzalishaji wa madeni, mamlaka za Serikali za Mitaa zimetakiwa kutohamisha walimu endapo hakuna bajeti iliyotengwa. Vilevile Serikali imeondoa kipengele kinachohitaji mwalimu akubali cheo chake kwanza ili aweze kulipwa mshahara wake mpya baada ya kupandishwa daraja jambo ambalo lilisababisha malimbikizo makubwa ya mishahara. Aidha, Serikali imeweka utaratibu wa kukusanya madeni katika Mamlaka za Serikali za Mitaa ili yaweze kupatikana, kuhakikiwa na kulipwa kwa walimu wanaoidai kwa wakati. 2 NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT) MWENYEKITI: Mheshimiwa Mushashu. MHE. BENARDETHA K. MUSHASHU: Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na majibu ya Mheshimiwa Naibu Waziri ninayo maswali mawili ya nyongeza. Mheshimiwa Mwenyekiti, miaka nenda, miaka rudi tofauti na kada nyingine za watumishi, kero imekuwa madeni ya walimu, madeni ya walimu. Leo hii mnatuambia kwamba madeni ya walimu yamefikia takribani shilingi bilioni 34 plus. Walimu hawa wanaidai Serikali wengine kama matibabu, likizo, kwa miaka zaidi ya mmoja hadi miwili. Walimu waliopandishwa mishahara miezi 12 iliyopita hadi leo hawajalipwa huo mshahara wanausikia harufu tu. Walimu wengine wamestaafu zaidi ya miezi sita hawajapata mafao yao. Ningependa kujua kwa kuwa sasa hivi Serikali mnasema mmeshahakiki ni lini, na mnipe tarehe na mwezi hawa walimu watakuwa wamelipwa haya madeni kwa sababu wamechoka kila siku madeni ya walimu? (Makofi) Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, kuna walimu waliosimamia mitihani mwaka 2015. Leo hii tunazungumza mwaka 2017, kwa nini hadi leo hawajalipwa na ni lini Serikali itakuwa imewalipa hiyo stahili yao? MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri. NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kama nilivyosema awali, kwanza tuweke kumbukumbu vizuri. Katika kada ambayo Serikali katika njia moja ua nyingine imekuwa ikishiriki vizuri sana katika ulipaji wa madeni ni kada ya walimu. Ukiangalia miaka mitatu mfululizo, trend ya malipo ya madeni ya walimu ambayo tulikuwa tumezungumza hapa katika Bunge kila wakati, kwa kweli Serikali inajitahidi sana. Na ndio maana katika kipindi cha sasa hata ukiangalia katika mwezi wa 11 uliopita huu kuna baadhi ya madeni ya walimu especially katika baadhi ya Wilaya, Halmashauri, kwa mfano kuna Temeke na Halmashauri zingine kulikuwa na outstanding deni karibuni ya shilingi bilioni moja nayo ililipwa vilevile. Mheshimiwa Mwenyekiti, ndio maana katika ulipaji wa madeni mapya mengine; ndio maana Serikali ilikuwa inafanya zoezi zima la uhakiki. Na bahati nzuri, ofisi yetu ya TAMISEMI pamoja na Ofisi ya Hazina ndio ilishiriki, na jambo hili sasa hivi limekamilika. Na ndio maana nimesema hapa siwezi kutoa deadline ni lini, deni hilo litalipwa lakini kwa sababu mchakato wa uhakika umekamilika, hili 3 NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT) deni la shilingi bilioni 26 ninaamini sasa hazina si muda mrefu mchakato wa malipo utaanza kuanza. Naomba Mheshimiwa Mbunge, najua uko makini katika hili lakini amini Serikali yako kwa vile zoezi la uhakiki ambalo lilikuwa ni changamoto limekamilika basi walimu hawa si muda mrefu wataweza kulipwa. Mheshimiwa Mwenyekiti, katika suala zima la deni la kusimamia mitihani na ndio maana nilisema deni hili lilikuwa ni miongoni mwa madeni haya ambayo yaliyohakikiwa ambayo takribani ilikuwa ni shilingi bilioni sita. Naomba tuondoe hofu walimu wangu katika mchakato wa sasa walimu hawa wote wataendelea kulipwa ili mradi kila mtu haki yake iweze kulipwa, na Serikali haitosita kuhakikisha inawahudumia vyema walimu wake kwa sababu italeta tija kubwa sana katika sekta ya elimu. MWENYEKITI: Ahsante! Mheshimiwa Hongoli ajiandae Mheshimiwa Masoud. MHE. JORAM I. HONGOLI: Mheshimiwa Mwenyekiti, asante sana kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza. Kwa kuwa kuna watumishi ambao walipandishwa daraja kama alivyosema muuliza swali wa kwanza, na kupokea mshahara mpya mwaka jana; na kisha hiyo mishahara ikasitishwa na sasa hivi watumishi hawa ambao ni walimu na watumishi wa afya kuna baadhi yao wameshastaafu, na wengine wanatarajia kustaafu miezi ijayo hii. Je, Serikali itatumia hesabu gani katika ku-calculate, itatumia mshahara upi? Ule wa zamani au mshahara mpya katika kukokotoa kile kiinua mgongo cha mwisho? Ahsante sana. MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri majibu kwa kifupi. WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YA UTUMISHI UMMA NA UTAWALA BORA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza kabisa kwa watumishi ambao walikuwa wameingia katika utumishi wa umma, halafu baadaye wakaambiwa warudi nyumbani, tumeshawarudisha watumishi 421 na kwa sasa tayari wameshalipwa takribani watumishi 379, 42 tumewarudishia waajiri wao ili waweze kukamilisha baadhi ya taratibu za ajira. 4 NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT) Mheshimiwa Mwenyekiti, katika hoja yake ya pili kwamba unakuta wengine wameshastaafu, lakini ni kiwango gani kitatumika katika kukokotoa mafao yao? Nipende tu kumhakikishia Mheshimiwa Mbunge na wote wanaosikiliza, kwa wale ambao wanastaafu wanapewa kipaumbele miezi miwili kabla ya tarehe ya kustaafu mishahara yao inarekebishwa na watakuwa wamepata katika cheo stahiki ili waweze kutokuathirika na mafao. MWENYEKITI: Mheshimiwa Masoud. MHE. MASOUD ABDALLAH SALIM: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. Nina swali moja dogo la nyongeza. Mheshimiwa Mwenyekiti, madai ya walimu yasiyo ya mshahara ni pamoja na deni la walimu kwa Serikali juu ya posho na kufundishia yaani teaching allowance ambayo ni ahadi ya Serikali tangu mwaka 2012 ambayo ilitolewa kule Mtwara siku ya Walimu Duniani. Je, Serikali ina mkakati gani wa ziada kuweza kuwalipa na kuwapatia fedha zao walimu hawa deni wanalolidai, posho la kufundishia yaani teaching allowance kwa haraka inavyowezekana? MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri! NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA YA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kama nilivyosema, kwa hali ya sasa tunachokifanya ni kuhakikisha kwa kadri iwezekano kusaidia sekta ya elimu. Ndio maana kabla sijajibu hili swali sasa hivi ukiangalia Serikali yetu kwa kazi kubwa waliyoifanya sasa hivi, mwanzo ukiangalia Walimu Wakuu, hata Waratibu wa Elimu mwanzo walikuwa hawalipwi hizi allowances. Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini Serikali hivi sasa toka mwaka jana kuanzia Waratibu wa Elimu, Wakuu wa Shule za Msingi na Wakuu wa Shule za Sekondari hivi sasa wote wanalipwa. Mheshimiwa Mwenyekiti, na kama kuna madeni mengine yoyote Serikali iko katika michakato mbalimbali kuyalipa madeni haya yote. Naomba niwahakikishie ndugu zangu Wabunge kwamba Serikali yetu jukumu letu kubwa ambalo tunalilenga sasa hivi, kwa sababu tunataka kuhakikisha ubora wa elimu lazima madeni haya yote yatalipwa na kama nilivyosema madeni yote ambayo yamehakikiwa kupitia Hazina yatalipwa madeni hayo. Tunataka walimu wetu wawe na morali ya kufanya kazi katika mazingira yao ya kazi. 5 NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT) MWENYEKITI: Waheshimiwa tunaendelea, Wizara ya hiyo hiyo Mheshimiwa Vedastus Mathayo Manyinyi, Mbunge wa Musoma Mjini. Na. 43 Upungufu wa Vyumba vya Madarasa na Maabara MHE.VEDASTUS M. MANYINYI aliuliza:- Baada ya Serikali kutoa tamko la elimu bure wananchi wamekuwa wagumu sana kutoa michango mbalimbali ya kuboresha elimu. Je, Serikali ina mikakati gani ya kumaliza tatizo la upungufu wa vyumba vya madarasa na vyumba vya maabara katika shule za msingi na sekondari? NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA alijibu:- Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri
Details
-
File Typepdf
-
Upload Time-
-
Content LanguagesEnglish
-
Upload UserAnonymous/Not logged-in
-
File Pages224 Page
-
File Size-