NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA _________ MAJADILIANO YA BUNGE _________ MKUTANO WA KUMI NA TANO Kikao cha Thelathini na Tano – Tarehe 24 Mei, 2019 (Bunge Lilianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Naibu Spika (Mhe. Dkt. Tulia Ackson) Alisoma Dua NAIBU SPIKA: Waheshimiwa tukae. Katibu! NDG. RAMADHANI ISSA ABDALLAH – KATIBU MEZANI: HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati Zifuatazo Ziliwasilishwa Mezani na:- WAZIRI WA MADINI: Randama za Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Madini kwa mwaka wa fedha 2019/2020. NAIBU SPIKA: Ahsante. Katibu! NDG. RAMADHAN ISSA ABDALLAH – KATIBU MEZANI: MASWALI NA MAJIBU NAIBU SPIKA: Maswali Waheshimiwa Wabunge, tutaanza na Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mheshimiwa Rashid Abdallah Shangazi Mbunge wa Mlalalo c kwa niaba yake Mheshimiwa Mary Chatanda. 1 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) Na. 287 Kuugawa Mkoa wa Tanga MHE. MARY P. CHATANDA (K.n.y MHE. RASHID A. SHANGAZI) aliuliza:- Mkoa wa Tanga ndiyo Mkoa wenye halmashauri nyingi zaidi kwa sasa ukiwa na jumla ya halmashauri kumi na moja:- Je, Serikali haioni sasa ni wakati muafaka wa kuugawa mkoa huo ili kurahisisha shughuli za utawala na maendeleo? NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri Ofisi ya Rais, TAMISEMI, majibu. NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA - MHE. MWITA M. WAITARA alijibu:- Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Nchi ofisi ya Rais-TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Rashid Abdallah Shangazi Mbunge wa Mlalo kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali inatambua kuwa Mkoa wa Tanga ndio mkoa wenye halmashauri nyingi zaidi kwa sasa ukiwa na jumla ya halmashauri 11. Hata hivyo, kipaumbele cha Serikali kwa sasa ni kuimarisha maeneo ya utawala yaliyopo yaliyoanzishwa katika miaka ya hivi karibuni kwa miundombinu na huduma mbalimbali ili kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi kabla ya kuanzisha maeneo mengine mapya. Hivyo, naomba Mheshimiwa Mbunge avute subira wakati Serikali ikitekeleza azma ya kuimarisha maeneo yake yaliyopo ambayo yana upungufu wa miundombinu na huduma mbalimbali muhimu kwa ajili ya kuwahudumia wananchi wetu. NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Ally Keissy swali la nyongeza. 2 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) MHE. ALLY K. MOHAMED: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana. Nchi yetu kwa sasa ina miundombinu mizuri kuliko enzi za ukoloni au enzi zilizopita. Je, Serikali inaonaje kwa muda huu kupunguza idadi ya wilaya, idadi ya majimbo ya mikoa ili Serikali ipate pesa, i-save pesa kwa ajili ya kupunguza idadi ya mikoa, idadi ya majimbo na idadi ya wilaya? NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais- TAMISEMI majibu. NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Naibu Spika, tumemsikia Mheshimiwa Ally Keissy kwa maoni yake na mtazamo wake lakini maeneo haya kiutawala yakiwepo majimbo ya uchaguzi ya Waheshimiwa Wabunge hawa wapendwa, wilaya, mikoa na maeneo mengine ya kata na vijiji yanaanzishwa kwa mujibu wa sheria. Mheshimiwa Naibu Spika, sasa utakapofika wakati wa kuona kwamba kwa hilo wazo la Mheshimiwa Keissy ni muhimu kufanyiwa kazi tutalifanyia kazi. Kwa sasa msimamo ni kwamba tutaendelea kuimarisha maeneo yaliyopo kujenga miundombinu, kupeleka huduma mbalimbali za kijamii ili watu wote waweze kupata maisha ambayo ni bora zaidi. NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Oran Njeza swali la nyongeza. MHE. ORAN M. NJEZA: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru sana ningependa kuuliza swali la nyongeza mji mdogo wa Mbalizi ulipewa mamlaka miaka 15 iliyopita na sasa hivi ina wakazi zaidi ya 100,000 na pia uwanja wa kimataifa wa Songwe uko katika eneo hilo. Sasa ni lini Mji mdogo wa Mbalizi utapewa hadhi ya kuwa Halmashauri ya Mji wa Mbalizi? NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais- TAMISEMI majibu. 3 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Naibu Spika, kama nilivyosema kwenye jibu langu la msingi ni kwamba kwa sasa tunaendelea kuimarisha maeneo ya kiutawala yaliyoanzishwa. Wanapozungumzia kuanzisha halmashauri maana yake unaongezea miundombinu unahitaji huduma ya ukubwa zaidi na watendaji watakuwepo na majengo yataongezeka. Mheshimiwa Naibu Spika, naomba Mheshimiwa Mbunge aendelee kuvumilia tuimarishe kwanza hii miji midog iliyopo halmashauri zetu na katika nchi hii kuna mikoa mingi pia bado haina majengo ya kutosha ya kuwa mikoa na watendaji wengine. Tuna upungufu wa miundombinu katika halmashauri zetu pia Waheshimiwa Wabunge wenyewe bado wanadai ofisi za Wabunge hazijajengwa. Kwa hiyo, nadhani ukiangalia mahitaji yaliyopo na kuongeza eneo la utawala nadhani tupeane muda kidogo tutekeleze haya yaliyopo tukamilishe tutazingatia baadaye maoni yake, ahsante. NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Ezekiel Maige swali la nyongeza MHE. EZEKIEL M. MAIGE: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru sana kwa kunipa nafasi kwa kiasi kikubwa swali langu linafanana na Mheshimiwa Njeza kumekuwepo confusion ya kuongeza maeneo na kupandisha hadhi. Mkoa wa Shinyanga tulishamaliza mchakato wa kupendekeza mji wa Kahama uwe manispaa na sifa zote tunakidhi na kigezo kikubwa kimekuwa ni suala la mapato ambayo halmashauri ya Manispaa ya Kahama ina uwezo wa kujiendesha kwa hiyo si changamoto kwa Serikali. Pia Mji wa Isaka na tulishafikisha wizarani je, ni lini Wizara kwa mtazamo maalum inaweza ikaruhusu Halmashauri ya Mji wa Isaka pamoja na Halmashauri ya Manispaa ya Kahama itaanza? NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Waziri, Ofisi ya Rais- TAMISEMI majibu. 4 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza naomba nimpongeze Naibu wangu kwa ufafanuzi mzuri sana. Katika swali hili lakini tunafahamu kwamba nishukuru Mheshimiwa Maige kwa concern yake; tuna maeneo makubwa matatu kwanza, kuna Halmashauri ya Mji wa Geita, Kahama, pamoja na Halmashauri ya Mji wa Kibaha ambao sasa iko katika suala la kufanya tathmini ya kuhakikisha kuzipandisha katika hadhi ya manispaa. Kwa hiyo lakini kuna utaratibu sasa hivi ambao tunaendelea kuufanya kwanza kutoanzisha maeneo mapya lakini hilo suala zima la hadhi tutalifanyia kazi pale jambo litakapoiva vizuri mtapata mrejesho Waheshimiwa Wabunge. NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge tuendelee na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mheshimiwa Bupe Nelson Mwakangata, Mbunge wa Viti Maalum sasa aulize swali lake. Na. 288 Ujenzi wa Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Rukwa MHE. BUPE N. MWAKANG’ATA aliuliza:- Je, ni lini Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Rukwa itaanza kujengwa? NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto majibu. WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO alijibu:- Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Bupe Nelson Mwakang’ata Mbunge wa Viti Maalum kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Naibu Spika, Mkoa wa Rukwa unao Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Sumbawanga inayotoa huduma 5 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) za rufaa kwa halmashauri nne za mkoa huo hadi sasa. Hata hivyo hospitali hiyo inayo changamoto ya ufinyu wa nafasi kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu mipya ya kutolea huduma za afya ili kukidhi mahitaji ya wananchi. Kutokana na changamoto hiyo Ofisi ya Mkoa wa Rukwa imeshapata eneo jipya la ukubwa wa hekari 100 lililopo Milanzi ndani ya Manispaa ya Sumbawanga litakalotumika kwa ajili ya ujenzi wa hospitali mpya ya rufaa ya mkoa. Mheshimiwa Naibu Spika, ujenzi huu utaanza baada ya kumalizika ujenzi wa hospitali za rufaa katika mikoa mipya ya Katavi, Songwe, Njombe, Simiyu na Geita. NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Bupe Mwakangata swali la nyongeza. MHE. BUPE N. MWAKANG’ATA: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru kwa kunipa nafasi ya kuuliza maswali mawili ya nyongeza. Kwanza naipongeza Serikali kwa kutujengea hospitali za wilaya tatu katika Mkoa wa Rukwa, lakini katika hizo wilaya tatu bado wilaya moja ya Sumbawanga mjini haijapatiwa hospitali ya wilaya. Je, ni lini sasa itajengewa hospitali ya wilaya? Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili ni lini Serikali sasa itapeleka fedha za ukarabati hospitali hii ya mkoa ambayo inatumika kwa sasa? NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto majibu. WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO: Mheshimiwa Naibu Spika, nimpongeze sana Mheshimiwa Bupe Mwakangata kwa kazi nzuri ambayo anafanya katika kufuatilia upatikanaji wa huduma za afya katika Mkoa wa Rukwa hasa huduma ya afya ya mama na mtoto naamini wanawake wa Mkoa wa Rukwa wamemuona na wameiona kazi yake nzuri. 6 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu ni lini tutajenga hospitali ya wilaya katika wilaya moja ambayo haijapata hospitali, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - TAMISEMI kama alivyoeleza tumeanza hospitali 67 mwaka huu katika bajeti ziko hospitali 28 kwa hiyo, tuombe tu uvumilivu kwa wananchi ambao hawajapata hospitali moja ya wilaya, Serikali ya Awamu ya Tano ni Serikali ya vitendo ni Serikali ya kutekeleza kwa hiyo tutajenga hospitali. Mheshimiwa Naibu Spika, lakini naomba nitoe angalizo kwa sababu pia tunataka kujenga hospitali mpya ya Mkoa wa Rukwa. Kwa hiyo, ningeomba subira tukimaliza ujenzi wa mikoa mitano mipya kutekeleza ilani hii ya uchaguzi 2015/2020. Kwa hiyo, ile hospitali ya mkoa sasa tutaikabidhi kwa hospitali ya manispaa ya Sumbawanga kama tulivyofanya kwa Shinyanga na Singida ndio tutafanya hivyo, tukimaliza hospitali mpya hizi zilizokuwa zinatumika za mikao zitakabidhiwa katika manispaa. Sasa ni lini tutapeleka fedha ya ukarabati tumepata fedha takribani shilingi bilioni 14 kutoka mfuko wa Dunia wa kupambana na UKIMWI, TB na Malaria
Details
-
File Typepdf
-
Upload Time-
-
Content LanguagesEnglish
-
Upload UserAnonymous/Not logged-in
-
File Pages214 Page
-
File Size-