Hii Ni Nakala Ya Mtandao (Online Document)

Hii Ni Nakala Ya Mtandao (Online Document)

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) MAJADILIANO YA BUNGE __________ MKUTANO WA KUMI NA SITA ___________ Kikao cha Thelathini na Nne – Tarehe 21 Julai, 2009 (Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Naibu Spika (Mhe. Anne S. Makinda) Alisoma Dua HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na:- NAIBU WAZIRI WA KILIMO, CHAKULA NA USHIRIKA: Hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika kwa Mwaka wa Fedha 2009/2010. MHE. KHERI KHATIB AMEIR (K.n.y. MWENYEKITI WA KAMATI YA KILIMO, MIFUGO NA MAJI): Taarifa ya Kamati ya Kilimo, Mifugo na Maji kuhusu Utekelezaji wa Majukumu ya Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika kwa Mwaka 2008/2009 pamoja na maoni ya Kamati kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo kwa Mwaka wa Fedha 2009/2010. MHE. JUMA SAID OMAR (K.n.y. MSEMAJI MKUU WA UPINZANI KWA WIZARA YA KILIMO, CHAKULA NA USHIRIKA): Taarifa ya Msemaji Mkuu wa Kambi ya Upinzani Kuhusu Makadirio ya Matumizi ya Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika kwa Mwaka wa Fedha 2009/2010. NAIBU WAZIRI WA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI (MHE. GAUDENTIA M. KABAKA): Randama za Makadirio ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kwa Mwaka wa Fedha 2009/2010. MASWALI NA MAJIBU Na. 249 Hali ya Soko Kuu la Tabora Mjini MHE. SIRAJU J. KABOYONGA: Kwa kuwa soko kuu la Mjini Tabora ni la siku nyingi na limepitwa na wakati; kwa maana ya kwamba halina huduma nzuri za kuhifadhia bidhaa za wachuuzi, halina mpangilio mzuri kulingana na biashara zinazofanywa sokoji hapo; 1 hakuna huduma za vyoo kulingana na wingi wa wafanyabiashara na wanunuzi wanaohudumiwa hapo; na kwa kuwa gharama za matengenezo zinazohitajika sokoni hapo ni kubwa sana kuliko uwezo wa kifedha wa Manispaa ya Tabora pekee yake:- Je, kwa nini mradi huo usiingizwe kwenye orodha ya miradi inayostahili kufadhiliwa na Serikali Kuu ili soko hilo liweze kufanyiwa matengenezo yanayostahili na kulingana na mahitaji ya huduma zinazohitajika? NAIBU WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU (TAMISEMI) alijibu:- Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Siraju Juma Kaboyonga, Mbunge wa Tabora Mjini, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Naibu Spika, Soko Kuu la Mjini Tabora, lilianzishwa mwaka 1964 likiwa na uwezo wa kukidhi mahitaji ya idadi ya watu kwa wakati huo. Kutokana na ongezeko kubwa la watu, kwa sasa imekuwa vigumu kukidhi mahitaji kulingana na wingi wa wafanyabiashara waliopo. Mheshimiwa Naibu Spika, soko hilo ambalo linamilikiwa na Halmashauri ya Manispaa ya Tabora, kwa hivi sasa lina huduma ya choo kimoja ambacho kina matundu manane. Huduma hiyo haikidhi idadi ya wafanyabiashara 1,767 katika soko hilo na wanunuzi 30,000, ambao wanakadiriwa kuingia kwa siku katika soko hilo kutafuta mahitaji. Hivyo, Manispaa imepanga kujenga choo kingine chenye matundu 30 katika mwaka wa fedha 2010/2011. Hii ni kwa sababu, mwaka huu wa fedha bajeti ilikwishapitishwa. Hata hivyo, kwa sababu ni jukumu la Halmashauri kujenga masoko yake na mapato katika soko hilo ni wastani wa shilingi milioni 15 kwa mwezi, naishauri Halmashauri ya Manispaa ya Tabora, iangaliwe uwezekano wa kuboresha huduma ya soko hilo kwa kutumia mapato hayo. Serikali Kuu haina utaratibu wa kujenga masoko ya Halmashauri. MHE. SIRAJU J. KABOYONGA: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru tena kwa kunipa nafasi ya kuuliza maswali mawili madogo ya nyingeza. Kabla sijauliza, nimshukuru Mheshimiwa Naibu Waziri, kwa Majibu yake ambayo kwa kiasi fulani hayakuniridhisha. Majibu haya yamekuwa ya jumla jumla sana, wakati mimi nilikuwa na maswali very specific. Hata hivyo, naomba niuliuze maswali ya jumla kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Naibu Spika, Naibu Waziri amekiri kwamba, hali ya soko ni mbaya na ametuambia Manispaa ina mapato ya shilingi milioni 15 kwa mwezi. Kwa hiyo, itumie mapato hayo kurekebisha hali ya soko. Kwa hali ilivyo ukitaka kutengeneza lile soko, shilingi 15 milioni kwa mwezi hazitoshi. Kwa hiyo, naomba kuiuliza Serikali kupitia kwa Waziri Mkuu; je, itakuwa tayari Manispaa ya Tabora kupata mkopo kutoka Mashirika ya Hifadhi ya Jamii kuzingatia kwamba pato letu kwa mwezi ni milioni 15 basi tupate mkopo mkubwa utakaotuwezesha kulijenga upya lile soko kwa kutumia mapato hayo ya milioni 15 kwa mwezi? Swali la pili; Mheshimiwa Waziri amekiri kwamba hali ni mbaya, choo kilichopo kina matundu manane. Watu ndiyo hao kama alivyosema katika hali ya dharura. Je, Serikali haiwezi ikaisaidia kwa ruzuku Manispaa ya Tabora ikajenga vyoo vyenye matundu 30 kama suala la dharura kwa sababu kusubiri mpaka 2010/2011 hali inaweza kuwa mbaya sana? NAIBU WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU (TAMISEMI): Mheshimiwa Naibu Spika, Mheshimiwa Kaboyonga tulikuwa tunakaa pamoja na mimi sina mpango wa kujibu kitu chochote ambacho ni kinyume na unachotaka wewe. Hali ya soko 2 kutokuridhisha; ni kweli wakikaa mle ndani mvua zikinyesha wananyeshewa na jua likiwaka wanawakiwa. Kwa hiyo, mimi nakubaliana na yeye kabisa kwamba, kweli hali ya soko ni mbaya. Ninampongeza Mbunge kwamba, yeye anawashughulikia watu wake ili waweze kuwa na masoko mazuri. Kuwa na masoko mazuri, ndiyo mtindo wa kisasa wa kuishi, maana yake ni kwamba, biashara za watu zitakwenda. Mheshimiwa Kaboyonga ni Mwanauchumi na tunapozungumza hapa, anajua mambo ya uhasibu na anafahamu kila kitu. Ninachosema hapa ni kwamba, ninyi milioni 15 mnazipata kila mwezi na mimi nikitaka kukuletea takwimu hapa na nimezungumza na watu wa Tabora zote nimezipata ziko hapa. Wamelianzisha soko lile mwaka 1964. Ninachotaka kusema hapa ni kwamba, business inatakiwa i-break even, kama unaendesha biashara yoyote lazima uoneshe faida. Mheshimiwa Naibu Spika, umesema nisiongee sana; ninachotaka kusema hapa, tutasaidiana naye. Kuna LAPF, Loan’s Board katika TAMISEMI, vyote hivi ni vyombo ambavyo vinatoa mikopo. Yote hii bado utakwenda kwa akina Mkulo tena na bado twende kwa mwenye dhamana ya jambo hili, tukae mimi na wewe tuzungumze, tukiona kwamba mkopo huu unaweza ukapatikana kwa maana hiyo, unayoyazungumza hapo tutakuwa tumesaidiana. Sasa ruzuku ya dharura, Bajeti imepita hapa, Spika akatuuliza mnaunga mkono; wote tukaitikia tukasema ndiyo. Sasa nikikukubalia hapa nikasema tutatoa ruzuku ya dharura itatoka wapi maana tulishapitisha? (Kicheko) Na. 250 Shule za Kata katika Maeneo ya Wafugaji kuwa na Hosteli MHE. MICHAEL L. LAIZER aliuza:- Kwa kuwa Shule za Kata katika maeneo ya Wafugaji zinatakiwa ziwe na hosteli badala ya kuwa za kutwa kutokana na umbali uliopo kati ya vijiji na shule zenyewe:- Je, Serikali itachukua hatua gani kwa vile baadhi ya shule ziko mijini na zinafikika kwa shida sana? NAIBU WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU (TAMISEMI) alijibu:- Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Michael Lekule Laizer, Mbunge wa Longido, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali imekuwa ikitoa kipaumbele katika kuwapa elimu bora watoto wote nchini. Baada ya elimu ya msingi, wahitimu wanaofaulu hujiunga na elimu ya sekondari. Kwa kuwa wahitimu wa elimu ya msingi ni wengi, shule za sekondari za kutwa kwenye kata zilianzishwa nchini, ikiwa ni pamoja na kwenye maeneo ya wafugaji. Changamoto iliyopo ni kwamba, katika maeneo ya wafugaji, shule za kutwa huchukua wanafunzi wachache kwa sababu ya umbali kutoka nyumbani hadi shuleni. Katika Wilaya ya Longido, kuna shule tano za sekondari zilizojengwa na wananchi na shule nne zimesajiliwa mwaka huu wa 2009. Watoto wa jamii ya wafugaji, ambao kwa kawaida ni wahamiaji, hawawezi kusoma wakitoka nyumbani kutokana na umbali ambao katika vijiji vingine ni 3 zaidi ya kilometa ishirini na hakuna usafiri wa aina yoyote. Shule za Sekondari katika maeneo ya wafugaji, zinapaswa kuwa na hosteli ambazo hujengwa na wananchi kwa kushirikiana na Halmashauri husika. Mheshimiwa Naibu Spika, katika Wilaya ya Longido ni dhahiri kwamba, hosteli zilizopo ni chache kulingana na wingi wa wanafunzi. Ujenzi wa Hosteli katika shule mpya haujakamilika. Halmashauri ya Wilaya ya Longido, inaendelea kukamilisha ujenzi wa Hosteli katika shule hizo na ujenzi wa mabwalo ya chakula. MHE. MICHAEL L. LAIZER: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru kwa kunipa nafasi niulize maswali mawili ya nyongeza. Kwa kuwa majibu ya Mheshimiwa Naibu Waziri ni mazuri, napenda kuiambia Serikali kwamba, hali ya Wafugaji wa Longido kwa wakati huu ni mbaya sana, kutokana na ukame na kuna shule ambazo wanahitaji mabweni kwa haraka sana. Je, Serikali inaweze kusaidia kwa dharura kujenga mabweni hayo kutokana na hali halisi ya wafugaji kwa wakati huu ili wanafunzi waweze kupata mahali pa kulala? Kwa kuwa katika shule hizo bado hakuna mabwalo wala vitanda katika baadhi ya mabweni; je, Serikali itachukua hatua gani kuisaidia Halmashauri ya Wilaya ya Longido kwa sababu hali ya wafugaji wakati huu ni mbaya sana? NAIBU WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU (TAMISEMI): Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza, naomba ni-declare interest kwamba, mimi na Mheshimiwa Michael Laizer tunatoka mahali pamoja. Asilimilia 50 ya wapiga kura wangu ni hao anaowazungumza Mheshimiwa Laizer na wa Mheshimiwa Edward Lowassa tumepakana nao wote. Ninataka mjue hilo kwanza. Kwa hiyo, kumwambia mwezengu kwamba, hii habari haiwezekani na nini, najua itanidhuru mimi. (Kicheko) Ninachotaka kusema hapa ni kweli kabisa kwamba, jamii hizi za wafugaji mpaka Ngorongoro na kule Longido na Siha, zina matatizo makubwa yanayotokana na ukame kama anavyozungumza Mheshimiwa Laizer. Hili halina ubishi na ndiyo maana analeta rai maalum kwa Serikali. Ninataka niseme msimamo wa Serikali; maeneo haya ya pembezoni ambayo yanaonekana yana matatizo, tumekuwa na mkakati maalum wa kuwasaidia

View Full Text

Details

  • File Type
    pdf
  • Upload Time
    -
  • Content Languages
    English
  • Upload User
    Anonymous/Not logged-in
  • File Pages
    128 Page
  • File Size
    -

Download

Channel Download Status
Express Download Enable

Copyright

We respect the copyrights and intellectual property rights of all users. All uploaded documents are either original works of the uploader or authorized works of the rightful owners.

  • Not to be reproduced or distributed without explicit permission.
  • Not used for commercial purposes outside of approved use cases.
  • Not used to infringe on the rights of the original creators.
  • If you believe any content infringes your copyright, please contact us immediately.

Support

For help with questions, suggestions, or problems, please contact us