Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) BUNGE LA TANZANIA ______________ MAJADILIANO YA BUNGE _____________ MKUTANO WA NNE KIKAO CHA NNE – TAREHE 14 JUNI, 2011 (Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Spika (Mhe. Anne S. Makinda) Alisoma Dua MASWALI NA MAJIBU Na. 37 Ardhi Iliyotolewa Kujenga Shule ya Msingi Kiraracha MHE. AUGUSTINO L. MREMA aliuliza:- Mzee Pauli Sananga Lekule wa Kijiji cha Kiraracha, Kata ya Marangu, Wilaya ya Moshi Vijijini, alitoa ardhi yake ikatumika kujenga shule ya msingi Kiraracha, Marangu miaka 10 iliyopita akiahidiwa na Serikali kupewa eneo jingine kama fidia lakini mpaka sasa hajapewa eneo jingine kama fidia jambo lililomfanya aione Serikali haikumtendea haki. Je, ni lini Serikali itamlipa haki yake kutokana na makubaliano hayo? NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (ELIMU) alijibu:- Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Augustino Lyatonga Mrema, Mbunge wa Vunjo kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Spika, Serikali inatambua kuwa Ndugu Pauli Sananga Lekule wa Kijiji cha Kiraracha, Kata ya Marangu Magharibi, alitoa ardhi yake kwa ajili ya ujenzi wa shule ya msingi Kiraracha, Kata ya Marangu Magharibi kwa ahadi ya kufidiwa eneo lililoko Njia panda. Aidha eneo ambalo Halmashauri ya Wilaya ya Moshi ilitarajia kumfudia Ndugu Lekule lipo katika mgogoro na kesi bado inaendelea Mahakama Kuu. 1 Mheshimiwa Spika, kwa kuwa eneo lililopimwa viwanja na kutarajia mlalamikaji lipo katika mgogoro wa kisheria kati ya Halmashauri na wananchi, Serikali inaendelea kufuatilia mwenendo wa kesi na mara shauri litakapomalizika Mahakamani mhusika atapewa eneo lake. Mheshimiwa Spika, katika jitihada za Serikali kuhakikisha shauri hili haliendelei kuchukua muda mrefu, Halmashauri ya Wilaya ya Moshi imeunda timu kwa ajili ya kufuatilia na kuharakisha shauri hili ili ikiwezekana limalizike nje ya Mahakama ili Ndugu Lekule Sananga aweze kupata haki yake mapema. (Makofi) MHE. AUGUSTINE L. MREMA: Mheshimiwa Spika, pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Naibu Waziri, naomba kuuliza maswali yafuatayo:- Kwanza huyu Mzee Pauli Sananga Lekule amekuwa mtu muungwana sana, mkarimu sana. Kwa miaka kumi iliyopita akakubali heka zake nne zichukuliwe na Serikali ya kijiji cha Kiraracha. Hatukuwa na eneo jingine la kujenga shule, miaka kumi imemalizika, watoto wake wamemzingira wanataka urithi, wanataka haki zao. Sasa Serikali kukaa miaka kumi yule mtu hajapata haki zake na tunamwambia kwa sababu ya kesi iliyoko Mahakamani ina uhusiano gani na yeye? Kwanini yeye mwenyewe alikuwa tayari kufidiwa shilingi milioni 40 amalizane na Serikali tumpe haki yake kiwanja tuchukue na shule imeshafika darasa la saba na yeye alikuwa tayari kusema kwamba kama hamtaki kunilipa ondoeni shule yenu nipeni ardhi yangu? Sasa kwanini Serikali haitaki kulinda heshima yake ikapatana na yule mwananchi na raia wa kawaida pale kijijini mkampa haki yake milioni 40 ni kitu gani mbele ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Naomba apewe fidia yake tuachane na yeye. Baada ya kusema hayo naomba nimwulize Waziri Serikali itafanya nini? NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (ELIMU): Mheshimiwa Spika, kwanza lazima nitambue hekima aliyonayo mwananchi ule Bwana Pauli, Sananga Lekule ni kweli amekuwa mvumilivu kwa kipindi chote cha miaka kumi na Mheshimiwa Mbunge anatambua migogoro ya ardhi iliyoko Kilimanjaro. Kilimanjaro kuna tatizo la ardhi na maeneo yote yana migogoro. Lakini katika hili Serikali inayo nia njema ya kumlipa Bwana Lekule kwa sababu kipindi kile toka mwaka 2000 eneo lile lilipopimwa mwaka 2001 wale wananchi walianza mgogoro na ile kesi ilifunguliwa. Mwaka 2003 tukategemea ile kesi ingeweza kwisha lakini ilishindikana kwisha na sisi tukawa tunasubiri maamuzi ya Mahakama kwa kipindi chote hiki kufikia mwaka jana tukawa tumepanga utaratibu mwingine. Tunalo eneo jingine pale Kiraracha la Halmashauri ya Wilaya, lile eneo tumeliombea kibali Wizara ya Ardhi ili tubadilishe matumizi na tayari wameshatukubalia ndiyo makubaliano ya msingi ya kumrudishia ili tuweze kumrudishia ardhi yake. (Makofi) 2 Hatua tuliyofikia sasa huku tukisubiri kesi ile Mahakamani lakini tumeunda Tume kuomba Mahakama ile kesi irudi tuzungumze huku nyumbani ili tuweze kumlipa haki yake ya msingi. Lakini kama itashindikana suala la Mahakama tuna uhakika eneo ambalo tumeshapata kibali cha kubadilisha matumizi ya ardhi kwenye eneo ambalo tumeliombea, bado tuna uhakika wa kumlipa ardhi yake. Suala la kumlipa milioni 40 Ndugu Pauli Lekule hajawahi kutuandikia barua ya kuomba kulipwa milioni 40, atakapoandika sasa tunaweza tukazungumza kwa nia ya kutaka kumlipa thamani ya ardhi yake ili asiweze kupoteza haki yake ya msingi. (Makofi) Na. 38 Shule za Kata MHE. PHILIPA J. MTURANO aliuliza:- Shule nyingi za Kata zilizoanzishwa, licha ta kuwezesha wanafunzi wengi zaidi kujiunga nazo lakini shule hizo zina upungufu mkubwa wa vitendea kazi na walimu wenye sifa stahiki:- (a)Je, Serikali ina mpango wa kuzipatia shule hizo walimu wa kutosha wenye sifa stahiki na vitendea kazi vya kutosha? (b)Je, Serikali inasema nini juu ya kuwarudishia walimu Teaching Allowance hususani kwa walimu wa Shule za Msingi na Sekondari kama motisha kwa watumishi hao ili kuinua ari yao ya kufanya kazi? NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (ELIMU) alijibu:- Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Philipa Maturano, Mbunge wa Vti Maalum, lenye sehemu (a) na (b) kama ifuatavyo:- (a)Mheshimiwa Spika, mpango wa kuzipatia Shule za Kata Walimu wenye sifa stahiki ni bayana na Serikali imejipanga kufanya hivyo kwa kuongeza udahili wa walimu wanafunzi katika Vyuo mbalimbali. Kwa kuendelea na juhudi hiyo hiyo katika mwaka 2010/2011 jumla ya walimu 9226 wameajiriwa na Serikali na miongoni mwao wamepangwa katika Shule za Kata. Aidha, Serikali inaendelea kuhamasisha watu binafsi na mashirika yasiyo ya kiserikali kuanzisha Vyuo vya Ualimu ikiwa ni njia mojawapo ya kuongeza udahili wa walimu. Kwa mwaka 2011/2012 jumla ya walimu wanaotarajiwa kuhitimu vyuo mbalimbali nchini ni 19,031 (shahada 12,649 na 3 stashahada 7,382). Serikali itaendelea kuwaajiri walimu hao kadri wanavyohitimu na kufaulu. Mheshimiwa Spika, katika utekelezaji wa malengo na mikakati ya mpango wa maendeleo wa Elimu ya Sekondari awamu ya II (MMES II) Serikali imekusudia kuongeza upatikanaji wa vifaa vya kufundisha na kujifunzia katika masoo yote na ngazi zote ifikapo 2013 kwa kupeleka nusu ya fedha za ruzuku ya uendeshaji na fedha kutoka Benki ya Dunia kwa ajili ya kununulia vitabu na vifaa vya maabara. (b)Mheshimiwa Spika, Serikali inatambua ukubwa wa kazi ya walimu pamoja na mchango mkubwa unaoutoa kwa jamii na changamoto zinazomzunguka katika kutoa elimu nchini. Serikali imeendelea maslahi, mishahara na stahili za walimu ili kuwapa ari ya kufanya kazi ni azima ya Serikali pia kuboresha posho na maslahi kwa walimu wapya wanaoripoti kazini. Aidha Serikali itaendelea kuboresha maslahi na mishahara ya walimu watumishi wengine kadri uwezo Serikali unavyoruhusu. MHE. PHILIPA J. MTURANO: Mheshimiwa Spika, nakushukuru. Kuna walimu ambao wana miaka zaidi mitatu tangu wamehitimu katika vyuo vya Ualimu mpaka sasa hawajaajiriwa. Katika jibu la msingi Mheshimiwa Waziri amesema kwamba Serikali inaongeza udahili. Je, hawa ambao wako majumbani na hawajaajiriwa mpaka sasa Serikali inasemaji. Swali la pili, kwa kuwa Shule hizi za Kata, zinachukua watoto wengi na baadhi yao wanatoka maeneo ya mbali na wengi ni wakike je, Serikali inasemaje kujenga hosteli ili kupunguza mamba ambazo watoto wakike wanazipata wanapokuwa wanahangaika kuhusu masuala ya usafiri? NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (ELIMU): Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Mbunge kwa sasa hatuna uhakika kama kuna mwalimu yoyote aliyepata mafunzo ya ualimu na yuko mtaani hana ajira. Kwa sababu idadi kubwa ya walimu wote ambao wamehitimu mafunzo ya ualimu iwe ni kwa Diploma na Digrii, tulitoa nafasi na kuwashukuru, tulitoa nafasi mwezi Februari na tukawaajiri 9226 kutokana nakuajiri waliotoka vyuoni lakini pia walioko kwenye soko. Tunaamini wale wote walioomba ndiyo waliajiriwa. Idadi ndogo ya vijana waliomaliza vyuo vya ualimu hawajakamilisha kufaulu masomo ya mtihani kwenye vyuo vyao. Mkakati wa Serikali tunaajiri mwalimu ambaye amehitimu lakini awe amefaulu masomo yote, hiyo ndiyo sifa ya kwanza ya kuajiriwa mwalimu kwa sasa. Swali la pili la ujenzi wa hostel ni kweli. Serikali ina mpango wa kujenga hostel kwenye shule zetu na moja kati ya mambo yaliyoko kwenye package ya MMES ni pamoja na ujenzi wa hestel kwenye shule zetu za sekondari. 4 Kwa hiyo Waheshimiwa Wabunge na Watanzania wote tunamatumaini kwamba ujenzi wa hostel utakuwepo kwenye shule za sekondari lakini tuendelee kushirikiana na kamati zetu zile za Ward C kwenye Kata zetu na Kamati za ujenzi kuratibu mipango hiyo kwenye vijiji vyetu ili tuweze kujenga zile hostel na hatimaye tuokoe mazingira ya watoto wa kike. MHE. MARIAM N. KISANGI: Mheshimiwa Spika, ahsante. Pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Waziri nina swali moja la nyongeza. Serikali inatambua kuwa Walimu ni Jeshi kubwa kama majeshi mengine ambapo walimu wanapambana na adui ujinga. Je, Serikali ina mkakati gani wa kuwapunguzia walimu kodi za vifaa vya ujenzi ili nao wapate makazi bora? SPIKA: Swali jingine kabisa. Haya Mheshimiwa Naibu Waziri majibu. NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (ELIMU): Mheshimiwa Spika, nilipokuwa nazungumzia Mpango
Details
-
File Typepdf
-
Upload Time-
-
Content LanguagesEnglish
-
Upload UserAnonymous/Not logged-in
-
File Pages203 Page
-
File Size-