Nakala ya Mtandao (Online Document) BUNGE LA TANZANIA ________________ MAJADILIANO YA BUNGE _____________________ MKUTANO WA KUMI NA TANO Kikao cha Ishirini na Moja – Tarehe 29 Mei, 2014 (Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Spika (Mhe. Anne S. Makinda) Alisoma Dua HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI Hati Zifuatazo Ziliwasilishwa Mezani na :- NAIBU WAZIRI WA HABARI, VIJANA, UTAMADUNI NA MICHEZO: Hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kwa Mwaka wa Fedha 2014/2015. AIBU WAZIRI WA NISHATI NA MADINI: Hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Nishati na Madini kwa Mwaka wa Fedha 2014/2015. MHE. CAPT. JOHN D. KOMBA K.n.y. MWENYEKITI WA KAMATI YA MAENDELEO YA JAMII: Taarifa ya Mwenyekiti wa Kamati ya Maendeleo ya Jamii Kuhusu Utekelezaji wa Majukumu ya Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kwa Mwaka wa Fedha 2013/2014 na Maoni ya Kamati Kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo kwa Mwaka wa Fedha 2014/2015. MHE. JEROME D. BWANAUSI K.n.y. MWENYEKITI WA KAMATI YA NISHATI NA MADINI: Taarifa ya Mwenyekiti wa Kamati ya Nishati na Madini Kuhusu Utekelezaji wa Majukumu ya Wizara ya Nishati na Madini kwa Mwaka wa Fedha 2013/2014 1 Nakala ya Mtandao (Online Document) na Maoni ya Kamati Kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo kwa Mwaka wa Fedha 2014/2015. MHE. MOSES J. MACHALI (K.n.y. MSEMAJI MKUU WA KAMBI YA UPINZANI KWA WIZARA YA HABARI, VIJANA, UTAMADUNI NA MICHEZO): Taarifa ya Msemaji Mkuu wa Kambi ya Upinzani, kwa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo kwa Mwaka wa Fedha 2014/2015. MHE. RAJAB MBAROUK MOHAMED (K.n.y. MSEMAJI MKUU WA KAMBI YA UPINZANI KWA WIZARA YA NISHATI NA MADINI): Taarifa ya Msemaji Mkuu wa Kambi ya Upinzani, kwa Wizara ya Nishati na Madini Kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo kwa Mwaka wa Fedha 2014/2015. MASWALI KWA WAZIRI MKUU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, leo ni maswali kwa Waziri Mkuu bahati ninamwona Kiongozi wa Kambi ya Upinzani, kama ilivyo kwa mujibu wa Kanuni zetu yeye ndiye atakayeanza kumwuliza Maswali Waziri Mkuu. Mheshimiwa Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni. MHE. FREEMAN A. MBOWE: Mheshimiwa Spika, nashukuru sana kunipa nafasi ya kumwuliza Mheshimiwa Waziri Mkuu Maswali. Mheshimiwa Waziri Mkuu, wakati unahitimisha hoja ya Bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu, ulitanabaHisha kwamba, uchaguzi wa Serikali za Mitaa utafanyika kama ilivyo kawaida mwisho wa mwaka huu 2014. Vilevile, ulilifahamisha Taifa kwamba, wakati huo huo zoezi la uandikishaji wapiga kura katika utaratibu mpya wa biometric utakuwa unatumika. Mheshimiwa Waziri Mkuu kwa uzoefu wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Mwaka 2004 na zaidi Uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa mwaka 2009 ambao ulisimamiwa na Sheria ya Serikali za Mitaa, Sura ya 287 na Sheria ya Serikali za Miji, Sura ya 288, Uchaguzi huu uligubikwa na vurugu nyingi sana. Pia uliishawahi kutoa kauli huko nyuma kwamba, Serikali itaangalia upya sheria ile ili pengine kuifanyia marekebisho ya msingi kabla ya uchaguzi wa mwaka huu 2014 ili matatizo yale yasijirudie tena. 2 Nakala ya Mtandao (Online Document) Mheshimiwa Waziri Mkuu, ni miezi michache imebakia kabla ya Uchaguzi huo. Unaliambia nini Taifa kuhusu maandalizi ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Vijiji mwisho wa mwaka huu? (Makofi) WAZIRI MKUU: Mheshimiwa Spika, naomba tu kueleza kwa ufupi kwamba, mambo ambayo tumeishaanza kuyafanyia kazi; kwanza ni maandalizi tu ya kibajeti ambayo tulizungumza wakati wa kuhitimisha Bajeti ya Waziri Mkuu. Pili, huwa tunakuwa na utaratibu wa kushirikisha wadau wote wakati wa kuandaa Kanuni ambazo tunafikiria zinaweza zikasaidia katika kusimamia vizuri zoezi hili. Kwa hiyo, nalo tumeishaanza kuliangalia kwa maana ya kutafuta Kanuni za mara ya mwisho turekebishe mahali gani ili tuweze kwenda vizuri. Mheshimiwa Spika, tatu ni hili ambalo amelieleza. Ni kweli kwamba tulitoa hiyo kauli na tumeishaomba watu wa TAMISEMI waangalie kama kuna maeneo hasa ambayo tunafikiria pengine yangeweza kufanyiwa marekebisho kabla ya Uchaguzi Mkuu. Sasa kama yatabainika basi tutaleta hiyo rai mbele yetu. Wakati huo huo labda niseme tu kwamba, kwa sababu na ninyi ni wadau wakubwa kwa maana ya vyama vya Upinzani, ni rai yangu tu kwamba na ninyi mngeanza kulitazama vilevile kama kuna maeneo ambayo mnafikiria yangeweza kupendekezwa ili na yenyewe tuweze kuyachukua wakati tunajaribu kutazama na sisi upande wetu, tutashukuru vilevile. (Makofi) MHE. FREEMAN A. MBOWE: Mheshimiwa Waziri Mkuu, nakushukuru kwa majibu yako ya awali. Ni kweli sisi kama wadau muhimu yako maeneo mengi sana ambayo yanalalamikiwa katika Kanuni hizi ambazo mara ya mwisho zilitungwa mwaka 2009 na ni dhahiri tutatoa mapendekezo mengi tu ya mabadiliko katika Kanuni hizi ili kuufanya uchaguzi huu uwe huru na amani zaidi. Mheshimiwa Waziri Mkuu, hata hivyo, tatizo hapa siyo mapendekezo yetu, ila ni utayari wenu wa kukubali mapendekezo ambayo wadau watayatoa, kwa sababu tukikumbuka katika uchaguzi wa mwaka 2009 yako mapendekezo kadha wa kadha ambayo yalitolewa kwa Serikali lakini ikayapuuza na matokeo yake uchaguzi ule ukaghubikwa na vurugu nyingi. Sasa badala ya kusubiri wadau wapendekeze bila utaratibu unaoeleweka unaonaje kama leo utalipa Taifa taarifa kwamba, unakusudia kuita kikao cha wadau mapema sana ili mambo haya yajadiliwe mapema kabla hujafika hatua ya kumaliza Kanuni wewe na TAMISEMI ambao ni washindani katika zoezi hili? (Makofi) 3 Nakala ya Mtandao (Online Document) WAZIRI MKUU: Mheshimiwa Spika, mnaweza vilevile mkawa na Kanuni nzuri sana, lakini kama watu wenyewe ambao tunahusika na zoezi dhamira zetu nazo si nzuri, bado hiyo haiwezi kuwa ni tiba. (Makofi) Kwa hiyo, nadhani rai ya msingi hapa ni kwamba, sisi wote ambao ni washirika wakubwa katika zoezi hili pande zote mbili; upande wa Chama cha Mapinduzi, upande wa vyama vya Upinzani tufike mahali tuone kwamba, jambo hili ni letu wote na pale ambapo hapastahili kuwa na vurugu hakuna sababu ya kuwa na vurugu, vinginevyo nadhani rai yako kwangu haina tatizo hata kidogo. Tutajitahidi kuona wakati mwafaka, na hata ikibidi pengine kuanza na mawasiliano formal hivi, brain storming ya Kanuni zenyewe kwa ujumla wake halafu baadaye twende katika hatua sasa ya kuona ni maeneo gani ambayo tunafikiri tunaweza tukayafanya. Tutajitahidi kupitia TAMISEMI tuone wakati ambao tungeweza tukafanya hilo zoezi. (Makofi) SPIKA: Ahsante sana Mheshimiwa Waziri Mkuu kwa kumjibu Kiongozi wa Kambi ya Upinzani. Ninatamani wote walioamka asubuhi wamalizike na inawezekana tu kama maswali yetu yatakuwa mafupi na hoja zetu fupi na zingine siyo lazima ku- repeat. Kwa hiyo, ninaanza na Mheshimiwa Murtaza Mangungu. MHE. MURTAZA A. MANGUNGU: Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Mheshimiwa Waziri Mkuu, mwaka 1997 Serikali ilichukua uamuzi wa kuvunja Jiji la Dar es Salaam na liliendeshwa na Tume baadaye yakaja mapendekezo ya uanzishwaji wa Manispaa za Kinondoni, Ilala na Temeke. Hivi sasa kuna mkanganyiko mkubwa sana kwenye utekelezaji wa maamuzi kati ya Halmashauri hizo na Jiji. Je, ni lini Serikali itachukua uamuzi wa kuondoa mkanganyiko huu na kuweka mfumo ambao utasaidia kutekeleza majukumu ya Manispaa hizi kama inavyotakiwa? (Makofi) WAZIRI MKUU: Mheshimiwa Spika, ni kweli suala la mfumo au muundo wa Jiji na uhusiano wake na manispaa zile tatu kwa muda mrefu limekuwa ni tatizo 4 Nakala ya Mtandao (Online Document) ambalo linajitokeza mara kwa mara na ndiyo maana Serikali kwa nyakati imejaribu kuona ni muundo gani pengine ungeweza ukafaa. Mtakumbuka mara ya mwisho tulijaribu lakini yale mapendekezo bado hayakuweza kutatua lile tatizo na tukalazimika kurejea tena kwenye utaratibu huu wa sasa. Mheshimiwa Spika, sasa nafikiri ushauri wangu ingekuwa, tuombe Manispaa zile tatu ambazo ndiyo wadau wakubwa, pamoja na Jiji lenyewe pengine mngekuwa ndiyo chanzo cha kuibua fikra ambazo mnadhani zinaweza zikafaa kwa ajili ya muundo wa Jiji la Dar es Salaam. Mnaweza mkafanya hivyo, kwa kujaribu kutengeneza timu kwanza ya Wataalam, baadaye mkajaribu kutengeneza timu ya Madiwani lakini wa maeneo yote, lakini mtumie na uzoefu pengine wa maeneo mengine duniani kuona mifumo ya miji au majiji yalivyo na kuweza kuona ni namna gani nzuri tunaweza tukajaribu kuitumia hapa Dar es Salaam. Nadhani tukifanya hilo pengine litakuwa mwanzo mzuri kwa sababu ninyi ndiyo wadau wakubwa, badala ya kuanzia juu na kushuka chini. Tuanzie chini ili tuyalete juu tuone baadaye kama litakubalika. (Makofi) SPIKA: Mheshimiwa Mangungu swali la pili, fupi kabisa. MHE. MURTAZA A. MANGUNGU: Mheshimiwa Waziri Mkuu, nakushukuru sana kwa majibu mazuri yenye matumaini. Ningependa tu kujua kwamba, uko tayari kusimamia mwongozo na usimamizi wa jambo hili kwa maana hizo zitakuwa ni mamlaka ambazo mpaka sasa zinasuguana kama tunavyoona Jiji la Dar es Salaam linazidi kuwa chafu, mifereji ya maji machafu imefurika, kila mamlaka inasema hili ni jukumu la mwingine. Sasa kwa kipindi hiki cha mpito. Je, unatoa agizo gani na utayari wako wa kiasi gani kuweze kuzikutanisha mamlaka hizi na kulisimamia hili jambo chini ya ofisi yako? WAZIRI MKUU: Mheshimiwa Spika, ofisi yangu ndiyo kiongozi wa shughuli zote za Serikali za Mitaa, ndiyo maana ninalisema hili kwa sababu Manispaa hizi ziko chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu na Jiji lenyewe liko chini ya Ofisi Waziri Mkuu. Rai yangu ya msingi ni hiyo tu kwamba, tulianzishe kule chini ili muweze kubainisha maeneo ambayo mnayatazama kwamba, kwanza ni tatizo katika 5 Nakala ya Mtandao (Online Document) utekelezaji, tatizo kimfumo na kimuundo, yapande juu baada ya mjadala mpana kwenye mabaraza
Details
-
File Typepdf
-
Upload Time-
-
Content LanguagesEnglish
-
Upload UserAnonymous/Not logged-in
-
File Pages329 Page
-
File Size-