Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) BUNGE LA TANZANIA ______________ MAJADILIANO YA BUNGE _____________ MKUTANO WA NNE Kikao cha Arobaini na Nne - Tarehe 11 Agosti, 2011 (Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Naibu Spika ( Mhe. Job Y. Ndugai) Alisoma Dua HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na:- NAIBU WAZIRI WA HABARI, VIJANA, UTAMADUNI NA MICHEZO: Hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kwa mwaka wa fedha, 2011/2012. MHE. JENISTA J. MHAGAMA -MWENYEKITI WA KAMATI YA MAENDELEO YA JAMII: Taarifa ya Mwenyekiti wa Kamati ya Maendeleo ya Jamii kuhusu utekelezaji wa majukumu ya Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kwa mwaka 2010/2011, pamoja na maoni ya Kamati kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2011/2012. MHE. JOSEPH O. MBILINYI - MSEMAJI MKUU WA KAMBI YA UPINZANI KUHUSU WIZARA YA HABARI, VIJANA, UTAMADUNI NA MICHEZO: Taarifa ya Msemaji Mkuu wa Kambi ya Upinzani juu ya Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2011/2012. MASWALI KWA WAZIRI MKUU NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge leo ni Alhamisi, kufuatana na Kanuni tunaendelea kwenye kipindi cha maswali kwa Waziri Mkuu, siyo hotuba bali ni maswali. Swali la kwanza litaulizwa na Mheshimiwa Martha Moses Mlata. MHE. MARTHA M. MLATA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Mheshimiwa Waziri Mkuu sote tunakumbuka kwamba mwaka 2008 dunia ilikumbwa na mdororo wa uchumi. Lakini Mataifa makubwa kama Marekani na nchi zingine ikiwemo Tanzania iliweza kusaidia mabenki pamoja na watu waliokuwa na hisa kukabiliana na mdororo huo. Lakini sasa hivi Tanzania yetu pia imekumbwa na tatizo kubwa la mgao wa umeme. Wafanyabiashara wengi ambao wamekopa mitaji yao kwenye mabenki hususan wajasiriamali kama akinamama wanaofanya biashara ndogo ndogo, wanakabiliwa na tatizo hilo kwa sababu wao mikopo yao ni ya muda mfupi na wanatakiwa warudishe kwa mfano waliokopa Pride wanatakiwa kila baada ya wiki arudishe... NAIBU SPIKA: Sasa swali Mheshimiwa. MHE. MARTHA M. MLATA: Hivyo Mheshimiwa Waziri Mkuu, Serikali inatoa tamko gani kwa watu kama hawa kuwasaidia ili kuweza kukabiliana na mdororo huu? Ahsante. WAZIRI MKUU: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kwanza nimshukuru sana Mheshimiwa Martha Mlata kwa swali lake zuri na labda niseme tu kwamba, pengine si rahisi sana kwa Serikali kuweza kutoa kauli ya uhakika juu ya jambo hili. Wajasiriamali wako wengi na ukizua jambo hilo nadhani itakuwa ni kazi kubwa kweli kuweza kujua unamsaidia nani na kwa namna gani. Lakini 1 kama ni hili suala la pengine riba kwa kipindi hiki ambacho wameona kama kuna mdororo sana sana ninachoweza kusema hapa ni kwamba, pengine naweza nikasaidiwa tu na vyombo vinavyohusika Pride kwa maana hiyo na vyombo vingine kuwaomba kama inawezekana basi kwa kutambua hili angalau waweze kusukuma mbele ule muda wa marejesho ya mikopo hiyo. Nafikiri tunaweza tukazungumza na mabenki vile vile tukawasihi wakaliona hilo pengine hiyo ndiyo ingekuwa njia bora na rahisi ya kuweza kuwa-cover walio wengi. (Makofi) MHE. DKT. MARY M. MWANJELWA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Mheshimiwa Waziri Mkuu, kwa kuwa Jiji la Arusha lilikamilisha uchaguzi wake wa Meya na Kamati zake zote kwa mujibu na Kanuni za Serikali za Mitaa. Lakini hivi karibuni tumesikia tamko la CHADEMA kwamba wewe Mheshimiwa Waziri Mkuu pamoja na Kiongozi wa Kambi ya Upinzani, Mheshimiwa Mbowe mmeingia kwenye muafaka wa kutaka uchaguzi wa Meya pamoja na Kamati zote za pale Arusha urudiwe. Sasa Mheshimiwa Waziri Mkuu tunaomba utufafanulie kwenye Bunge hili Tukufu. Hizi taarifa zinazosemwa na CHADEMA je, ni za kweli au si za kweli? Ahsante. (Makofi) WAZIRI MKUU: Mheshimiwa Naibu Spika, namshukuru sana Mheshimiwa Mwanjelwa kwa jambo hili kwa sababu na mimi wakati niko Morogoro niliona tu sehemu ya taarifa hiyo kwenye runinga ya TBC, ikigusia suala kama hilo unalolizungumza. Lakini kuna baadhi ya magazeti vile vile ambao walikuja kuniona wakiulizia nini hasa kilichotokea. Nikajaribu kulifafanua. Kwa hiyo, nadhani hii ni fursa nzuri pengine Watanzania wajue kilichotokea ni nini. Mheshimiwa Naibu Spika, niliwahi kulisema hili jambo siku za nyuma kwamba kwa kadri tunavyolijua jambo hili uchaguzi ule ulifanyika, ulikamilika na ndiyo maana nilisema kama kulikuwa na mtu anaona hakutendewa haki njia rahisi na kiutaratibu wa kisheria ilikuwa ni kukata rufaa au kwenda kudai Mahakamani kile ambacho hukuridhika nacho. Bado naona ni msimamo wangu na ni msimamo wa Serikali kwa sababu ndiyo utaratibu ulivyo. (Makofi) Sasa juzi Jumamosi tarehe 6 baada ya kuwa nimeombwa na Mheshimiwa Mwenyekiti wa CHADEMA Mheshimiwa Mbowe, siku ya Ijumaa jioni kwamba angependa kuniona, nilikubali. Akaniomba kwamba naweza kuja na Katibu Mkuu, ndugu yangu Dokta Slaa, nikamwambia njoo naye tu. Kwa hiyo, Jumamosi asubuhi saa tatu walikuja kuniona. Kwa hiyo, walipofika katika mazungumzo yao likajitokeza suala la hali isiyoridhisha ya kisiasa katika Manispaa ya Arusha. Kwa maana kwamba vyama ambavyo ni vikubwa pale ni Chama cha Mapinduzi pamoja na CHADEMA. Wao waliona kama hali iliyopo pale haijatulia, bado haitoi fursa kubwa kwa chombo hiki kuweza kushughulika na mambo ya kiutendaji na kwa maslahi ya wananchi wa Manispaa. Kwa hiyo, nikawaambia kwamba okay fine kama ni suala linalogusa masuala ya siasa, hilo haliko ndani ya uwezo wangu mimi. Hapa tunachoweza kukubaliana tumwombe Msajili wa Vyama ambaye yeye ndiye amepewa jukumu la kuratibu na kuona matatizo yanayotokana na mambo kama haya ya mitafaruku kati ya vyama, pengine yeye huyo angeweza kutusaidia vizuri zaidi. Nikamwahidi kwamba nitamtafuta huyu bwana, nitamweleza kwamba wamekuja kuniona, rai yenu ndiyo hiyo. Yeye sasa ataandika barua kwenda Chama cha Mapinduzi, kwa Katibu Mkuu Taifa na CHADEMA, halafu vyombo hivi viwili vitatengeneza utaratibu wa namna ya kushughulikia au kukutanisha vyama hivi viwili. Mimi ndiye niliyesema kwamba naamini katika hatua zote itabidi kuwepo na timu ya pamoja pande zote at technical level ili waweze kubaini ni agenda gani mnataka kuzipeleka kwenye mazungumzo hayo. Agenda hizo zitapanda kwenda ngazi ya Taifa ili viongozi wa ngazi ya Taifa wakisharidhia utaratibu wa kuzungumza hicho walichokiita hali ya kuonekana kwamba kuna mtafaruku, hapajatulia kisiasa, liweze kuzungumzwa. Sasa, juzi nilipomsikia Mheshimiwa Mbowe kwenye TV, nikaona mmh mbona kwanza amekwenda mbali. Hili jambo lilikuwa ndiyo kwanza limeanza safari kwenda kwa Msajili. Lakini huku limetoka kana kwamba tumeshakaa, tumekubaliana, itakuwepo na timu ya Kitaifa. Haikuwa sahihi hata kidogo na nasema it is very unfortunate kwa jambo hili. (Makofi) Kwa hiyo namshukuru sana Mheshimiwa Mwanjelwa kwamba umelileta jambo hili kwa sababu ukweli wa mambo yalivyokuwa ndiyo hivyo. Sasa kama hilo ndiyo tafsiri yake nadhani it is wrong. (Makofi) 2 MHE. DKT. MARY M. MWANJELWA: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru. Mheshimiwa Waziri Mkuu, kwa kuwa sasa tumejua kwamba kauli zilizotolewa na CHADEMA zinazosemwa za Arusha siyo za kweli. Je, wewe kama Mheshimiwa Waziri Mkuu, una ushauri gani kwa Madiwani wote wa Arusha, wananchi wa Arusha na wale Madiwani ambao inadaiwa wamefukuzwa. Tunaomba tamko. (Makofi) WAZIRI MKUU: Labda niseme nilichokuwa nimemshauri Mheshimiwa Mbowe, kwa sababu aliniambia kwamba anakwenda kukutana na Kamati Kuu na kwamba agenda kubwa ni hii ya Madiwani sita. Nilichomshauri, nikamwambia ndugu yangu mnakwenda kuamua nini, hilo ni juu ya CHADEMA. Lakini nikasema panahitajika busara kubwa. Maana yangu ilikuwa ni kwamba wakati mnaomba pengine kuwepo na mazungumzo kati ya vyama hivi viwili kwa jambo ambalo linagusa hali ya kisiasa pale, fikra zangu ilikuwa ni kwamba, busara nzuri ilikuwa ni kuendelea na hali iliyokuwepo hadi hapo mtakapokuwa mmefikia hatua fulani. Sasa niliposikia kwamba wamefukuzwa, aah basi nikasema hata mazungumzo yenyewe sijui yatakuwaje sasa. Okay! (Makofi) Sasa nadhani tumejiingiza kwenye mtego mkubwa tu. Lakini kwa hili aliloliuliza, ninachoweza kushauri tu ni kwamba tufuate sheria. Kwa hiyo, Madiwani hawa kama wanaona hawakutendewa haki katika mchakato wa kufukuzwa kwao, njia rahisi waende Mahakamani. Wahoji uhalali, Mahakama ndiyo itakayowasaidia kuona kwamba walichofanyiwa ni sawa ama si sawa. Huo ndiyo ushauri wangu kwa Madiwani wote. (Makofi) NAIBU SPIKA: Ahsante sana, Madiwani wahoji kuchaguliwa kwa nguvu ya umma na kufukuzwa kwa nguvu ya Kamati ya Siasa. Swali linalofuata la Mheshimiwa Stephen Hilary Ngonyani. MHE. STEPHEN H. NGONYANI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana. Mheshimiwa Waziri Mkuu juzi Serikali ilitoa taarifa hapa Bungeni kwamba baada ya mchakato wa mafuta mpaka kufika juzi bei ya mafuta ingekuwa imeshuka na mafuta yamekuwa yako sawa na ulitoa tamko hapa kwamba yeyote ambaye atakuwa amekiuka misingi basi Serikali itamchukulia hatua. Sasa nataka kujua kwamba wale ambao wamekiuka misingi ya mafuta umewachukulia hatua gani? WAZIRI MKUU: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kumshukuru Mheshimiwa Ngonyani, Mjumbe wa Kamati mwenzangu, Kamati ile tunayojua wote hapa. (Makofi/Kicheko) Mheshimiwa Naibu Spika, jambo hili ni kubwa na wote limetugusa sana. Lakini nataka niliarifu Bunge lako Tukufu kwamba baada ya Bodi ya EWURA kutoa amri ambayo ilipaswa kuzingatiwa na vyombo vyote vinavyohusika katika sekta hiyo kutolewa na kuweka mwisho wa muda ule. Kwa taarifa nilizo nazo mimi mpaka jana saa 10 makampuni karibu yote hasa yale manne, yalikwishaanza kusambaza mafuta kutoka kwenye maghala. (Makofi) Lakini tutaendelea kulifuatilia kwa maana ya kuona sasa mafuta yanayotoka
Details
-
File Typepdf
-
Upload Time-
-
Content LanguagesEnglish
-
Upload UserAnonymous/Not logged-in
-
File Pages95 Page
-
File Size-