1 Bunge La Tanzania

1 Bunge La Tanzania

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) BUNGE LA TANZANIA _______________ MAJADILIANO YA BUNGE _______________ MKUTANO WA ISHIRINI Kikao cha Thelathini na sita – Tarehe 27 Julai, 2005 (Mkutano Ulianza saa Tatu Asubuhi) D U A Spika (Mhe. Pius Msekwa) Alisoma Dua HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI Hati zifuatavyo ziliwasilishwa Mezani na:- WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA: Taarifa ya Mwaka na Hesabu za Halmashauri ya Biashara ya Nje kwa Mwaka ulioishia tarehe 30 Juni, 2003 (The Annual Report and Accounts of the Board of External Trade (BET) for the year ended 30th June, 2003) Taarifa ya Mwaka na Hesabu za Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni kwa Mwaka ulioishia tarehe 30 Juni, 2003 (The Annual Report and Accounts of the Business Registrations and Licensing Agency (BRELA) for the year ended 30th June, 2003). WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Taarifa ya Mwaka na Hesabu za Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro kwa mwaka 2004 (The Annual Report and Account of the Ngorongoro Conservation Authority for the year 2004). Taarifa ya Mwaka na Hesabu zilizokaguliwa za Bodi ya Utalii Tanzania kwa Mwaka ulioishia tarehe 30 Juni, 2004 (The Annual Report and Audited Accounts of the Tanzania Tourist Board for the year ended 30th June, 2004). Taarifa ya Mwaka na Hesabu zilizokaguliwa za Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi Tanzania kwa Mwaka ulioshia tarehe 30 June, 2004 (The Annual Report and Audited 1 Accounts of the Tanzania Fisheries Research Institute for the year ended 30th June, 2004). NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA: Hotuba ya Bajeti Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kwa Mwaka wa Fedha 2005/2006. MWENYEKITI WA KAMATI YA MAMBO YA NCHI ZA NJE: Maoni ya Kamati ya Mambo ya Nchi za Nje kuhusu Utekelezaji wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kwa Mwaka wa Fedha uliopita, pamoja na Maoni ya Kamati ya Kuhusu Makadirio ya Matumizi ya Wizara hiyo kwa Mwaka 2005/2006. MSEMAJI MKUU WA KAMBI YA UPINZANI BUNGENI: Maoni ya Kambi ya Upinzani kuhusu utekelezaji wa Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kwa Mwaka wa Fedha uliopita, pamoja na maoni ya Kambi hiyo kuhusu makadirio ya Matumizi ya Wizara hiyo kwa mwaka 2005/2006. MASWALI NA MAJIBU Na. 343 Barabara Wilayani Serengeti MHE. PROF. JUMA MIKIDADI (K. n. y. DR. JAMES M. WANYANCHA) aliuliza:- Kwa kuwa, barabara muhimu Wilayani Serengeti kama vile barabara ya Nata – Mugumu; Mto Mara – Mugumu; Sirari Simba – Rung’abure; Mugumu – Fort Ikoma; Iramba – Mara ni za udongo na zinaharibika sana wakati wa mvua za masika:- (a) Je, ni lini Serikali itazitengeneza kwa kiwango cha lami, changarawe barabara hizo ili kuwaondolea kero ya usafiri wa maeneo hayo? (b) Je, kazi hiyo itaanza na kukamilika lini na itagharimu fedha kiasi gani? (c) Je, ni fedha kiasi gani kimetumika kuzitengeneza barabara hizo katika kipindi cha kuanzia mwaka 2000 – 2005 ikitajwa kila barabara. NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA alijibu:- 2 Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Dr. James Munanka Wanyancha, Mbunge wa Serengeti, lenye sehemu (a), (b) na (c) kama ifuatavyo:- (a) Mheshimiwa Spika, barabara za Mugumu - Fort Ikoma na Mugumu – Iramba zenye jumla ya kilometa 60 ziko chini ya uangalizi wa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti, na barabara za Silori Simba – Rung’abure, Nata – Mugumu na Mto Mara – Mugumu zenye jumla ya urefu wa kilometa 113 ziko chini ya uangalizi wa TANROADS Mkoa wa Mara. Barabara zote hizo ni za kiwango cha changarawe na udongo na kutokana na uwezo uliopo wa kifedha, kwa sasa Serikali haina mpango wa kuzitengeneza barabara hizo kwa kiwango cha lami. (b) Mheshimiwa Spika, gharama ya kujenga kilometa moja kwa kiwango cha changarawe ni shilingi milioni 18 – 20 na kwa kiwango cha lami nyembamba yaani surface dressing ni shilingi milioni 200. Kwa kujenga barabara zenye urefu wa kilometa 173, zitahitajika shilingi bilioni 3.46 kuzijenga kwa kiwango cha changarawe na shilingi bilioni 34.6 kuzijenga kwa kiwango cha lami nyembamba. Kiasi hiki ni kikubwa sana na Serikali haina uwezo wa kukitenga kwa sasa. (c) Mheshimiwa Spika, ili kupunguza kero hii kwa wananchi wanaotumia barabara hizi, Serikali imekuwa ikizifanyia matengenezo ya aina mbalimbali yakiwemo matengenezo ya sehemu korofi kwa kuziwekea changarawe kadri ya hali ya fedha ilivyoruhusu kati ya mwaka 2000 hadi sasa kama ifuatavyo:- Barabara ya Bukabwa – Sirari Simba – Rung’abure , imetumika jumla ya shilingi 344,209,000, barabara ya Tarime – Mugumu – Natta ni shilingi 595,016,000, barabara ya Mugumu – Fort Ikoma jumla ya shilingi 52,988,000 na barabara ya Mugumu (Nyansurura) – Iramba (Majimoto) shilingi 44,305,000. Kwa maelezo niliyoyatoa hapo juu yanaonyesha ni jinsi gani barabara za Wilaya ya Serengeti zinavyopewa umuhimu katika kuzifanyia matengenezo ili ziweze kupitika licha ya ufinyu wa Bajeti. Kwa upande wa TANROADS, mipango na utekelezaji katika matengenezo ya barabara haufuati mipaka ya kiutawala ya Wilaya bali hufuata mpangilio wa mtandao na urefu wa barabara husika kwani barabara yaweza kupita kwenye Wilaya mbili au zaidi. Hivyo, gharama zilizoonyeshwa hapo juu ni za urefu wa barabara yote inayohusika. Kwa barabara ya Mugumu hadi Iramba sehemu inayoshughulikiwa na Halmashauri ni kutoka Nyansurura hadi Majimoto. Sehemu zilizobaki zinashughulikiwa na Wakala wa barabara yaani TANROADS. Mheshimiwa Spika, kwa kuokoa muda nitampatia Mheshimiwa Mbunge nakala ya mchanganuo wa mwaka hadi mwaka kwa kila barabara iliyohusika kama alivyoomba katika kipindi alichohitaji. MHE. PROF. JUMA MIKIDADI: Mheshimiwa Spika, pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Naibu Waziri napenda kuuliza maswali mawili madogo ya 3 nyongeza kutokana na ufinyu wa bajeti na kutokana na hali ngumu za Halmashauri zetu kama vile ilivyokuwa ya Serengeti kushindwa barabara ya kutoka Nata mpaka Mugumu na Mto Mara mpaka Mugumu na hivyo hivyo basi katika Wilaya nyingine kwa mfano Wilaya yangu ya Rufiji kutoka Muhoro mpaka Mbwele kwa sababu ya madaraja ya Kipoka na Mberambe. Je Mheshimiwa Naibu Waziri haoni kwamba kuna ulazima wa hizi Halmashauri zetu zisaidiwe na Serikali Kuu hasa hasa Mfuko wa Barabara ili kutngeneza barabara hizo? Pili, je kutokana na kushindwa Halmashauri pia na kuomba msaada kutoka Serikali Kuu na mara kwa mara jambo hilo haliwezekani, haionekani kwamba kuna umuhimu sasa ili kizipa Halmashauri hizi nguvu za kuweza kukusanya mapato katika mambo yake na uchumi wake ili kuweza kufanya kazi nzuri ambayo inaweza ikasaidia kutengeneza barabara hizo? NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Spika, kama nilivyoeleza katika maelezo ya msingi, fedha ambazo zinatumika kutengeneza barabara nyingi hapa nchini ni sehemu ya mchango wa Serikali kupitia Mfuko wa Barabara, kwa hiyo kwa kadiri mfuko huu utakavyokuwa unakuwa kwa maana ya kukua kwa uchumi Serikali itaendelea kuongeza uwezo wa Halmashauri ili kuziwezesha kutoa huduma nzuri zaidi kwa upande wa barabara. Kuhusu swali la pili, ni kweli kwamba Halmashauri hizi zikiwezeshwa kukusanya mapato mengi zaidi zinaweza zikasaidia kuboresha mazingira yao kwa miundo mbinu na mambo mengine hata huduma za jamii kwa kiasi kikubwa, lakini tatizo hili la kifedha limekuwepo hata kabla hatujaondoa ushuru na baadhi ya kodi.Serikali imeendelea kutoa huduma ya kifedha kwa kuwa tunajua Halmashauri hizi hata zikiachiwa kiasi gani maadamu uchumi wetu bado ni mdogo, haujawa mpana kiasi cha bado tatizo hili litaendelea kuwepo. Kwa hiyo nadhani dhamira ya Serikali ni sahihi zaidi kuendelea kuzipa support mpaka hapo tutakapokuwa tumewezesha kutoa huduma ambayo ni bora zaidi. Na. 344 Tume ya Kushughulikia Kero za Walimu MHE. MWANNE I. MCHEMBA (K.n.y. MHE. MARIAM S. MFAK) aliuliza:- Kwa kuwa, Serikali imefanya kazi ya kuunda Tume ya Kushughulikia Kero za Walimu na kwamba, tume hiyo imepita katika Halmashauri zote na kuonana na walimu na viongozi wa Halmashauri hizo jambo lililowapa walimu imani kwamba, haki zao sasa zinashughulikiwa; na kwa kuwa, watumishi wa sekta na idara mbalimbali nao wanazo kero zinazofanana na zile za walimu wakiwemo na Makatibu Tarafa. 4 Je, Serikali itashughulikia lini kero za watumishi walioko katika sekta na idara mbalimbali kama Makatibu Tarafa, Afya, Kilimo, Maji na Mifugo, Maendeleo ya Jamii, Ushirika na kadhalika ili kuhakikisha kuwa haki zao zinalipwa. WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA alijibu:- Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swali la Mheshimia Mariamu Salum Mfaki, Mbunge Viti Maalum, ifuatavyo:- Mheshimiwa Spika, Tume anayoirejea Mheshimiwa Mbunge iliundwa na Mheshimiwa Waziri Mkuu na Wajumbe wake walikuwa ni baadhi ya Waheshimiwa Wabunge wa Bunge lako Tukufu. Majukumu ya tume hiyo ilikuwa ni kuainisha kero mbalimbali za walimu nchini kote. Mheshimiwa Spika, ninakubaliana na Mheshimiwa Mariamu Mfaki kuwa mbali na malalamiko kutoka kwa Walimu yapo pia malalamiko kutoka kwa watumishi wengine wa umma wakiwemo wa afya, kilimo, maji na mifugo, maendeleo ya jamii, ushirika, Makatibu Tarafa na kadhalika. Aidha, Serikali haijawatenga watumishi wa makundi mengine kwani malipo ya malalamiko mbalimbali yanaendelea kufanyika kwa watumishi wote na si walimu peke yao. Hadi kufikia tarehe 30/6/2005 jumla ya shilingi bilioni 18 zilikuwa zimetumika kulipia malimbikizo hayo na uhakiki wa malimbikizo yaliyobaki unaendelea kufanyika na baada ya kukamilika malipo yatafanyika. Mheshimiwa Spika, naomba watumishi wote wenye malalamiko na madai halali wayawasilishe kwa waajiri wao ili yashughulikiwe. Hata hivyo, siyo nia ya Serikali kuendelea kushughulikia masuala ya madai halali ya watumishi wake

View Full Text

Details

  • File Type
    pdf
  • Upload Time
    -
  • Content Languages
    English
  • Upload User
    Anonymous/Not logged-in
  • File Pages
    145 Page
  • File Size
    -

Download

Channel Download Status
Express Download Enable

Copyright

We respect the copyrights and intellectual property rights of all users. All uploaded documents are either original works of the uploader or authorized works of the rightful owners.

  • Not to be reproduced or distributed without explicit permission.
  • Not used for commercial purposes outside of approved use cases.
  • Not used to infringe on the rights of the original creators.
  • If you believe any content infringes your copyright, please contact us immediately.

Support

For help with questions, suggestions, or problems, please contact us