11 Aprili 2013

11 Aprili 2013

11 APRILI, 2013 BUNGE LA TANZANIA ________________ MAJADILIANO YA BUNGE ___________________ MKUTANO WA KUMI NA MOJA Kikao cha Tatu - Tarehe 11 Aprili, 2013 (Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Spika (Mhe. Anne S. Makinda) Alisoma Dua HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na:- WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (TAMISEMI): Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, kuhusu Ukaguzi wa Taarifa za Fedha za Mamlaka ya Serikali za Mitaa kwa Mwaka wa Fedha ulioishia tarehe 30 Juni, 2012. [The Annual General Report of the Controller and Auditor General on the Financial Statements of Local Government Authorities for the Financial Year ended 30th June, 2012]. 1 11 APRILI, 2013 Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Kuhusu Ukaguzi wa Ufanisi wa Usimamizi wa Mikataba ya Miradi ya Maendeleo ya Mamlaka ya Serikali za Mitaa kwa mwezi Machi, 2013. [The Report of the Controller and Auditor General on Contract Management of Development Projects in Local Government Authorities in Tanzania, March, 2013]. NAIBU WAZIRI WA FEDHA (MHE. SAADA MKUYA SALUM): Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, Kuhusu Taarifa za Fedha za Serikali Kuu kwa Mwaka wa Fedha ulioishia tarehe 30 Juni, 2012. [The Annual General Report of the Controller and Auditor General on the Financial Statements of the Central Government for the Year ended 30th June, 2012]. Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Kuhusu Ukaguzi wa Taarifa za Fedha za Miradi ya Maendeleo kwa Mwaka wa Fedha ulioishia tarehe 30 Juni, 2012. [The Annual General Report of the Controller and Auditor General on the Audit of the Financial Statements of Donor Funded Projects for the Year ended 30th June, 2012]. Ripoti ya Jumla ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, Kuhusu Ukaguzi wa Ufanisi na Maalum kwa kipindi kilichoishia tarehe 31 Machi, 2013. [The General Report of the Performance and Specialized Audits for the Period ended 31st March, 2013]. Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, kuhusu Ukaguzi wa Mashirika ya Umma kwa Mwaka wa Fedha 2011/2012. [The Annual General Report of the Controller and Auditor General on the Audit of Public Authorities and other Bodies for the Financial Year 2011/2012]. 2 11 APRILI, 2013 The Report of the Controller and Auditor General on the Performance of ICT Equipment in Public Sector, March, 2013. Taarifa ya Mwaka ya Utendaji wa Soko la Bima nchini kwa mwaka ulioishia tarehe 31 Desemba, 2011. [The Annual Report on Insurance Market Performance report for the year ended 31st December, 2011]. NAIBU WAZIRI WA KAZI NA AJIRA: Taarifa ya Madhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Kuhusu Ukaguzi wa Utendaji wa Masuala ya Afya na Usalama Maeneo ya Kazi nchini Tanzania, ya Januari, 2013. [The Report of the Controller and Auditor General on the Performance Audit Report on the Management of Occupational Health and Safety in Tanzania in January, 2013]. NAIBU WAZIRI WA MAENDELEO YA MIFUGO NA UVUVI: Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Kuhusu Ukaguzi wa Ufanisi wa Shughuli za Uvuvi katika Ziwa Viktoria ya Januari, 2013. [The Report of the Controller and Auditor General on the performance Audit Report on the Management of Fisheries Activities in Lake Victoria in January, 2013]. NAIBU WAZIRI WA KILIMO, CHAKULA NA USHIRIKA: Taarifa ya Mwaka na Hesabu zilizokaguliwa za Bodi ya Sukari Tanzania kwa Mwaka wa Fedha Ulioishia tarehe 30 Juni, 2012. [The Annual Report of Audited Accounts of Sugar Board of Tanzania for the Financial Year ended 30th June, 2012]. 3 11 APRILI, 2013 SPIKA: Katibu tuendelee! MHE. JOHN M. CHEYO: Mwongozo wa Spika. SPIKA: Mwongozo wa Spika. MHE. JOHN M. CHEYO: Mheshimiwa Spika, katika kipindi kilichopita tulipitisha hapa Sheria ambayo ilikuwa inaleta marekebisho kwa Sheria ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ambayo ilisema wakati Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali analeta ripoti hapa, Serikali pia concurrently kiingereza lazima pia waweke mezani majibu ya ripoti ya CAG. Leo tumekaa hapa tumepata ripoti, hatujapata majibu ya Serikali. Hii ndiyo kusema tunavunja sheria siku ya kwanza ambapo sheria hii inapaswa kuanza. Naomba mwongozo wako. (Makofi) SPIKA: Waziri au Mwanasheria Mkuu wa Serikali, inatosha tutajibu baadaye. Katibu! MASWALI NA MAJIBU Na. 20 Tatizo la Ajira Nchini MHE. VINCENT J. NYERERE aliuliza:- Kumekuwa na wimbi kubwa la Wahitimu wa Vyuo mbalimbali hapa nchini lakini hakuna ajira kwa wahitimu hao. Je, Serikali ina mpango gani wa kusitisha kutoa mikataba kwa wastaafu ili wahitimu wanaotoka vyuoni wapate ajira na kujenga nchi yao? 4 11 APRILI, 2013 WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, MENEJEMENTI YA UTUMISHI WA UMMA alijibu:- Mheshimiwa Spika, ni kweli kwamba wako wataalam wengi wanaohitimu katika vyuo mbalimbali hapa nchini. Wahitimu hao hupatiwa ajira kulingana na mahitaji ya nchi na pia kwa kuzingatia uwezo wa Bajeti ya Serikali. Mheshimiwa Spika, mikataba hutolewa na Serikali inapoonekana ni kwa manufaa ya Umma kufanya hivyo kutokana na mahitaji makubwa katika sekta husika. Kifungu 12.2 cha Waraka wa Rais Na. 1 wa mwaka 1998 kinatamka wazi kwamba endapo Utaalam wa Mtumishi unahitajika sana, Serikali inawajibika kumuomba mtumishi kuendelea kufanya kazi na siyo mstaafu mwenyewe kuomba. Kwa sasa Serikali inawapa mikataba wataalam wastaafu ambao sio rahisi kuwapata katika soko la ajira, hususan wataalam wa kada muhimu kama vile Walimu, Waganga, Wahandisi na Wahadhiri wa Vyuo Vikuu. Mheshimiwa Spika, kutokana na kuhitajika kwao, wataalam hawa wanapostaafu wanaendelea kutumiwa kwa kuwapa mikataba ya muda mfupi sambamba na kuajiri wahitimu wa vyuo mbalimbali. Kwa mantiki hiyo Serikali itaendelea kuajiri wastaafu katika kada hizo muhimu hadi hapo soko la ajira litakapojitosheleza. SPIKA: Waheshimiwa Wabunge kwa kulinda muda naomba maswali yenu ya nyongeza yawe mafupi na Mawaziri majibu yenu ya nyongeza yawe mafupi kwa sababu by saa Nne Kamili lazima nifunge mazungumzo na nikifunga hakuna msamaha kwa mtu yeyote. Mheshimiwa Nyerere swali la nyongeza. MHE. VINCENT J. NYERERE: Mheshimiwa Spika, ahsante. Kwa kuwa kazi za Wakuu wa Mikoa siyo za kitaalam na wengi ni wastaafu kutoka maeneo mengine, nini tamko la Serikali kuhusu ajira zao. 5 11 APRILI, 2013 SPIKA: Hayo ndiyo maswali ya nyongeza, Mheshimiwa Waziri wa Nchi majibu. WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, MENEJEMENTI YA UTUMISHI WA UMMA: Mheshimiwa Spika, naomba kumjibu Mheshimiwa Mheshimiwa Vincent Nyerere, swali lake la nyongeza, kama ifuatavyo. Mheshimiwa Spika, Wakuu wa Mikoa siyo watumishi wa Umma, wako kwenye upande wa watumishi wa kisiasa kama mlivyo Wabunge. MHE. LAIZER M. LEKULE: Mheshimiwa Spika, nashukuru kunipa nafasi niulize swali la nyongeza. Kwa kuwa wafanyakazi wengi wamestaafu na wengine wamefariki na Serikali kuwaacha watumishi wote wakiwa kaimu, kaimu, kaimu kwa kila Idara. Je, Serikali ina mpango gani wa kuziba nafasi hizo? SPIKA: Safi kabisa, haya ndiyo maswali ya nyongeza. Mheshimiwa Waziri wa Nchi, majibu. WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, MENEJEMENTI YA UTUMISHI WA UMMA: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Lekule M. Laizer kama ifuatavyo:- Nafasi mbadala huwa hazina matatizo yoyote, ni pale tu mtu anapostaafu Halmshauri husika inaleta taarifa kwetu Ofisi ya Rais, Menejementi ya Utumishi wa Umma. Tukiishapata tunatoa vibali mara moja ili nafasi kwa watumishi waliostaafu waweze kuajiri mara moja. Kwa hiyo, tatizo la nafasi mbadala huwa siyo kubwa sana kama ilivyo kwa watumishi ambao ni wa ajira mpya. MHE. VITA R. KAWAWA: Mheshimiwa Spika, ahsante sana kwa kunipa fursa hii ya kuuliza swali moja la nyongeza. 6 11 APRILI, 2013 Kwa kuwa ajira ni chache na ndiyo maana vijana wanakosa ajira na vijana kwa sasa wamefunguka kiakili wamekuwa wakijiajiri wenyewe lakini kikwazo ni mtaji. Je, Serikali iko tayari kuzungumza na benki ili kupunguza vigezo na riba ili vijana hawa waweze kupata mikopo na waweze kufanya kazi zao? (Makofi) SPIKA: Mheshimiwa Waziri wa Uwekezaji. WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, UWEKEZAJI NA UWEZESHAJI: Mheshimiwa Spika, kwa Niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejiment ya Utumishi wa Umma, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Kawawa kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Spika, analolitaka Mheshimiwa Mbunge ndivyo hivyo Serikali inajitahidi kufanya kupitia mfuko wa uwezeshaji wananchi kiuchumi. Serikali imeweka dhamana ya shilingi bilioni 2.1 lakini benki zinatoa mara tatu na pengine hata zaidi ya hapo. Kwa hiyo, tutajitahidi sana kwa wale ambao wanaleta andiko ambalo linaridhisha basi tutawaelekeza kwenye benki. Tukifanya hivyo nina hakika suala la ajira ya vijana pengine tatizo litakuwepo lakini litapungua kila tunavyoendelea. Mheshimiwa Spika, ahsante sana. MHE. MOSES J. MACHALI: Mheshimiwa Spika, nakushukuru. Katika majibu ya msingi ya Mheshimiwa Waziri ameeleza kwamba Walimu ni miongoni mwa kada muhimu za utumishi na hivi karibuni Serikali imetoa ajira kwa kada hii ya walimu isipokuwa wanafunzi waliosoma BED(Psychology) pale Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na vyuo vingine suala la kuajiriwa limekuwa ni tatizo. 7 11 APRILI, 2013 Nini kauli ya Serikali kuhusiana na watu hawa ambao wamesoma kada ya ualimu, Especially BED (Psychology), nini hatima yao katika suala zima la kuajiriwa? WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Moses J. Machali, kama ifuatavyo:- Ni kweli mwanzoni wakati tunawapangia ualimu wale ambao wamechukua BED tulikuwa hatujawapangia, lakini sasa hivi

View Full Text

Details

  • File Type
    pdf
  • Upload Time
    -
  • Content Languages
    English
  • Upload User
    Anonymous/Not logged-in
  • File Pages
    205 Page
  • File Size
    -

Download

Channel Download Status
Express Download Enable

Copyright

We respect the copyrights and intellectual property rights of all users. All uploaded documents are either original works of the uploader or authorized works of the rightful owners.

  • Not to be reproduced or distributed without explicit permission.
  • Not used for commercial purposes outside of approved use cases.
  • Not used to infringe on the rights of the original creators.
  • If you believe any content infringes your copyright, please contact us immediately.

Support

For help with questions, suggestions, or problems, please contact us