NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ____________ MAJADILIANO YA BUNGE ___________ MKUTANO WA TISA Kikao cha Sita – Tarehe 14 Novemba, 2017 (Bunge lilianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Naibu Spika (Mhe. Dkt. Tulia Ackson) Alisoma Dua NAIBU SPIKA: Tukae, Katibu. NDG. THEONEST RUHILABAKE – KATIBU MEZANI: HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa mezani na:- WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI, VIJANA, AJIRA NA WENYE ULEMAVU: Taarifa ya Matoleo ya Gazeti la Serikali pamoja na Nyongeza zake yaliyochapishwa tangu Mkutano wa Bunge uliopita kama ifuatavyo:- (i) Toleo Na. 35 la tarehe 01/09/2017 (ii) Toleo Na. 36 la tarehe 08/09/2017 (iii) Toleo Na. 37 la tarehe 15/09/2017 (iv) Toleo Na. 38 la tarehe 22/09/2017 (v) Toleo Na. 39 la tarehe 29/09/2017 (vi) Toleo Na. 40 la tarehe 06/10/2017 (vii) Toleo Na. 41 la tarehe 13/10/2017 1 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) (viii) Toleo Na. 42 la tarehe 20/10/2017 (ix) Toleo Na. 43 la tarehe 27/10/2017 NAIBU WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO (MHE. ENG. ATASHASTA J. NDITIYE): Maelezo ya Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kuhusu Muswada wa Sheria ya Shirika la Mawasiliano Tanzania wa Mwaka 2017 (The Tanzania Telecommunications Corporation Bill, 2017) MHE. HAWA M. CHAKOMA (K.n.y. MHE. NORMAN A.S. KING - MWENYEKITI WA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA MIUNDOMBINU): Maoni ya Kamati ya Miundombinu kuhusu Muswada wa Sheria ya Shirika la Mawasiliano Tanzania wa Mwaka 2017 (The Tanzania Telecommunications Corporation Bill, 2017) MHE. QAMBALO W. QULWI (K.n.y. MHE. JAMES F. MBATIA - MSEMAJI MKUU WA KAMBI RASMI YA UPINZANI WA WIZARA YA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO): Maoni ya Msemaji Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kuhusu Muswada wa Sheria ya Shirika la Mawasiliano Tanzania wa mwaka 2017 (The Tanzania Telecommunications Corporation Bill, 2017) NAIBU SPIKA: Katibu. NDG. THEONEST RUHILABAKE - KATIBU MEZANI: MASWALI NA MAJIBU NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, tunaendelea na maswali. Tutaanza na ofisi ya Waziri Mkuu Mheshimwa Sonia Jumaa Magogo, Mbunge wa Viti Maalum, sasa aulize swali lake. 2 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) Na. 68 Watumishi ambao Hawajaandikishwa Kwenye Mifuko ya Hifadhi ya Jamii MHE. SONIA J. MAGOGO aliuliza:- Je, Serikali ina mkakati gani dhidi ya waajiri ambao hawawaandikishi Watumishi wao katika Mifuko ya Hifadhi ya Jamii na kuwasababishia kukosa stahiki zao? NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, VIJANA NA AJIRA alijibu:- Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Sonia Jumaa Magogo, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Naibu Spika, mkakati wa Serikali katika kuhakikisha waajiri wote wanaandikisha wafanyakazi wao kwenye Mifuko ya Hifadhi ya Jamii ni kusimamia utekelezaji wa Sheria ya Usimamizi na Udhibiti wa Hifadhi ya Jamii Na. 8 ya Mwaka 2008, Kifungu cha 30 ambacho kimeweka utaratibu unaomtaka mwajiri kuwaandikisha watumishi wake katika Mifuko ya Hifadhi ya Jamii. Aidha, mwajiri anayekiuka matakwa ya kifungu hiki anastahili adhabu ya kulipa faini ya kiasi kisichozidi shilingi milioni ishirini kwa mujibu wa kifungu cha 55 cha Sheria ya Usimamizi na Udhibiti wa Hifadhi ya Jamii. Mheshimiwa Naibu Spika, katika kuimarisha usimamizi wa Sheria za Kazi, Serikali kupitia Bunge ilifanyia marekebisho ya Sheria ya Taasisi za Kazi Na. 7 ya mwaka 2004 ili kuimarisha mfumo wa kaguzi za kazi mahali pa kazi kwa kuruhusu kutoa adhabu za papo kwa papo kwa waajiri wanaokiuka matakwa ya sheria ikiwa ni pamoja na kutosajili au kuandikisha wafanyakazi katika Mifuko ya Hifadhi ya Jamii. NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Sonia Magogo, swali la nyongeza. 3 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) MHE. SONIA J. MAGOGO: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Je, Serikali ina mkakati gani juu ya vijana ambao wamekuwa wakipata ajira za muda mfupi na kushindwa kuendelea na ajira zile, lakini kwa kigezo cha umri wamekuwa wakishindwa kupata mafao yao ambayo yangeweza kuwasaidia katika kuendeleza maisha yao? Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili, kwa kuwa kumekuwa na tofauti ya pensheni za kila mwezi kutoka mfuko mmoja na mwingine. Je, Serikali ina mpango gani kuhakikisha wazee hawa wanaostaafu wanapata pensheni iliyo sawa ya kila mwezi na ambayo inaweza kuwasaidia kuendesha maisha yao? Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. (Makofi) NAIBU SPIKA: Kabla sijamwita Mheshimiwa Waziri, tukifuata mtindo huu wa kuuliza maswali, Waheshimiwa Wabunge tutapata muda wa kuuliza maswali mengi sana. Kwa hiyo Mheshimiwa, japokuwa ni Mbunge mgeni ameuliza vizuri sana. (Makofi) Mheshimiwa Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, majibu. NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, VIJANA NA AJIRA: Mheshimiwa Naibu Spika, katika swali lake la kwanza alikuwa anazungumzia kiujumla kuhusu fao la kujitoa na amewazungumzia vijana ambao bado hawajafikia umri wa kupokea pensheni. Mheshimiwa Naibu Spika, kama ambavyo tumesema awali katika Bunge lako kwamba Serikali inaendelea kulifanyia kazi suala hili la fao la kujitoa. Hivi sasa tupo katika utaratibu wa kushirikiana na wadau ili kutengeneza kwa pamoja mfumo mzuri ambao utawa-cover watu wote katika makundi tofauti tofauti. Hivyo nimwombe Mheshimiwa Mbunge, kwa sababu jambo hili bado linafanyiwa kazi na Serikali tutakuja na mpango mzuri wa kuweza kusaidia kutatua changamoto hii. 4 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) Mheshimiwa Naibu Spika, swali lake la pili kuhusu pensheni, tayari SSRA wameshatoa miongozo kwa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii kulipa kima cha chini cha pensheni sawa kwa mifuko yote na ambayo hivi sasa imeanza kutekelezwa. (Makofi) NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Waitara, swali la nyongeza. MHE. MWITA M. WAITARA: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi. Naomba niulize swali dogo la nyongeza. Hivi karibuni kumekuwa na maelekezo ya Mheshimiwa Rais kwamba Watumishi wa Umma wakiwemo na Walimu, wasihamishwe kutoka kituo kimoja kwenda kingine bila kuwa na malipo ama stahiki zao. Vilevile kumekuwa na uhamishaji huo unaendelea katika Halmashauri mbalimbali na sasa hivi ninavyozungumza kuna mgogoro mkubwa kati ya Walimu na katika Wilaya ya… NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Waitara, nimetoka kutoa ushauri sasa hivi. Muda hautatosha Wabunge wote wakianza kutoa maelezo. Uliza swali ili uweze kujibiwa. MHE. MWITA M. WAITARA: Mheshimiwa Naibu Spika, swali langu ni kwamba naomba nipate majibu ya Serikali, Rais ametoa maelekezo watumishi wa umma wasihamishwe kutoka kituo kimoja kwenda kingine bila malipo yao, lakini Wakurugenzi wameendelea kuhamisha walimu na watumishi… NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Waitara, nadhani sasa huna swali ndugu yangu kwa sababu unarudia maelezo uliyotoa mwanzo. Sasa hivi nimekwambia uliza swali, unaenda maelezo marefu. Naomba ukae. Mheshimiwa Mtolea. MHE. ABDALLAH A. MTOLEA: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi. Mheshimiwa Naibu Spika, katika sekta hizi zisizo rasmi na hapa nawalenga hasa wale wanaofanya kazi za 5 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) daladala kwa maana ya madereva wa madaladala na makondakta wao na hii ni sekta ambayo imeajiri vijana wengi na watu wengi. Kimsingi wana malalamiko mengi ya haki za wafanyakazi, kwamba hawapewi stahiki zao. Je, Mheshimiwa Naibu Waziri, atakuwa tayari kukutana na Madereva na Makondakta wa daladala ili asikilize kero zao na uweze kuzipeleka Serikali kwa ajili ya kuzishughulikia, ukianzia Temeke? (Makofi) NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, majibu. NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, VIJANA NA AJIRA: Mheshimiwa Naibu Spika, kazi hii kama Wizara tumekuwa tukiifanya, tutaendelea kuifanya na nimuahidi Mheshimiwa Mbunge kwamba nipo tayari kukutana nao na kujadiliana nao kuhusu haki ambazo zinawahusu. (Makofi) NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Lubeleje, swali la nyongeza. MHE. GEORGE M. LUBELEJE: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana kwa kunipa nafasi. Swali langu ni kwamba, kwa kuwa kuna waajiri ambao wanakata mshahara lakini hawapeleki fedha hizi kwenye Mifuko ya Hifadhi ya Jamii. Je, Serikali inawachukulia hatua gani? NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, majibu. NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, VIJANA NA AJIRA: Mheshimiwa Naibu Spika, kwa mujibu wa sheria kila mfanyakazi aliyeandikishwa na anayekatwa makato yake kwa ajili ya hifadhi ya jamii yanapaswa kuwasilishwa katika mfuko husika. Kinyume na kufanya hivyo ni kukiuka taratibu za kisheria. Mheshimiwa Naibu Spika, ndiyo maana baada ya kuziangalia sheria zetu tukafanya marekebisho ya mwaka 2016 katika Sheria Na. 7 ya Mwaka 2004 ambayo 6 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) inashughulikia masuala ya Taasisi za Kazi ambapo lengo lake ni ku-compound hizo fences na inapotokea mwajiri amekiuka taratibu hizi tutakachokifanya ni kwenda kumpiga faini ya papo kwa papo ili kufanya deterrence na kumpunguzia mzigo mfanyakazi lakini kumfanya mwajiri awe ana-comply na sheria. Mheshimiwa Naibu Spika, huo ndiyo mkakati wa Serikali kuhakikisha kwamba jambo hili linafanyika kwa mwajiri kuwasilisha mchango wa mwajiriwa wake ikiwa ni haki yake ya mchango ambao ni sehemu ya mshahara wake. NABU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, tunaendelea. Ofisi ya Rais, TAMISEMI, Mheshimiwa Mussa Ramadhani Sima, Mbunge wa Singida Mjini, sasa aulize swali lake. Na. 69 Hitaji la Vifaa Tiba – Hospitali ya Wilaya ya Singida MHE. MUSSA R. SIMA aliuliza:- Je, Serikali ina mpango gani wa kutoa vifaa tiba kwenye Hospitali ya Wilaya ya Singida Mjini au kituo cha afya Sokoine? NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. JOSEPHAT S. KANDEGE) alijibu:- Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,
Details
-
File Typepdf
-
Upload Time-
-
Content LanguagesEnglish
-
Upload UserAnonymous/Not logged-in
-
File Pages209 Page
-
File Size-