MKUTANO WA SABA Kikao Cha Thelathini Na Mbili – Tarehe 23 Me

MKUTANO WA SABA Kikao Cha Thelathini Na Mbili – Tarehe 23 Me

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ____________ MAJADILIANO YA BUNGE ___________ MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Mbili – Tarehe 23 Mei, 2017 (Bunge Lilianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Mwenyekiti (Mhe. Mussa A. Zungu) Alisoma Dua MWENYEKITI: Tukae, Katibu. NDG. JOSHUA CHAMWELA – KATIBU MEZANI: Hati za Kuwasilisha mezani. HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na:- NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Maliasili na Utalii kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018. MHE. KHALIFA SALUM SULEIMAN (K.n.y. MHE. ATASHASTA J. NDITIYE - MWENYEKITI WA KAMATI YA ARDHI, MALIASILI NA UTALII): Taarifa ya Kamati ya Ardhi, Maliasili na Utalii kuhusu utekelezaji wa majukumu ya Wizara ya Maliasili na Utalii kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017 pamoja na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018. 1 NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) MHE. JOSEPH R. SELASINI (K.n. y. MHE. ESTHER N. MATIKO - MSEMAJI MKUU WA KAMBI YA UPINZANI KWA WIZARA YA MALIASILI NA UTALII): Taarifa ya Msemaji Mkuu wa Kambi ya Upinzani kuhusu Wizara ya Maliasili na Utalii juu ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018. MWENYEKITI: Ahsante, Katibu! NDG. JOSHUA CHAMWELA – KATIBU MEZANI: MASWALI NA MAJIBU MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge, tunaanza na Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, swali linaulizwa na Mheshimiwa Mgimwa, kwa niaba yake Mheshimiwa Kabati. Na. 254 Kupandisha Hadhi Barabara Inayounganisha Wilaya ya Mufindi na Wilaya ya Kilombero MHE. RITTA E. KABATI (K.n.y. MHE. MAHMOUD H. MGIMWA) aliuliza:- Mheshimiwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli alipokuwa Waziri wa Miundombinu aliahidi kupandisha hadhi barabara ya kutoka Mtiri – Ifwagi – Mdaburo, Ihanu, Isipi – Mpangatazara – Mpalla Mlimba ambayo inaunganisha Wilaya ya Mufindi na Wilaya ya Kilombero pia Mkoa wa Iringa na Morogoro. Je, ni lini Serikali itapandisha hadhi barabara hiyo muhimu kwa uchumi wa Wilaya ya Mufindi na Taifa kwa ujumla ambayo Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi imeshindwa kuihudumia wakati wote? 2 NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) NAIBU WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO alijibu:- Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Mahmoud Hassan Mgimwa, Mbunge wa Mufindi Kaskazini, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Mwenyekiti, barabara ya Mtili – Ifwagi – Mdaburo, Ihanu, Isipi – Mpangatazara – Mlimba ni barabara ya Wilaya inayohudumiwa na Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa kupitia Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi. Mheshimiwa Mwenyekiti, Wizara yangu inaifanyia kazi ahadi hiyo ya Serikali ya kuipandisha hadhi barabara hii na barabara nyingine nchini kwa kuzingatia vigezo vilivyoainishwa kwenye Sheria ya Barabara Na. 13 ya Mwaka 2007 na Kanuni za Menejimenti ya Barabara za mwaka 2009. Baada ya taratibu za kisheria kukamilika, Wizara yangu itamjulisha Mbunge pamoja na kutangaza barabara zilizopandishwa hadhi kwenye Gazeti la Serikali. MHE. RITTA E. KABATI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa kunipa nafasi niulize maswali tu madogo ya nyongeza. Kwa kuwa tumekuwa tukikaa katika vikao vya Bodi za Barabara mara nyingi sana hasa katika Mkoa wetu wa Iringa, barabara nyingi sana za Halmashauri zetu tunakuwa tukipeleka lakini hazipandishwi daraja. Je, ni vigezo gani sasa vinatumika maana utakuta sehemu nyingine barabara zinapandishwa lakini sehemu nyingine barabara nyingi hazipandishwi madaraja? Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, je, Serikali ina mpango gani wa kuongeza pesa kwenye Halmashauri kwa sababu Halmashauri nyingi barabara zake ni mbovu sana ili Halmashauri hizi ziweze kutengeneza barabara zake kwa kiwango? (Makofi) MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri majibu kwa kifupi. 3 NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) NAIBU WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO: Mheshimiwa Mwenyekiti, vigezo vya kupandisha hadhi barabara vimeainishwa katika Sheria ya Barabara pamoja na Kanuni zake kama ambavyo nilisema katika jibu langu la swali la msingi. Vigezo hivyo havijabadilika na kama tutataka kubadilisha tutakuja Bungeni kuvibadilisha. Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu kuongeza fedha; fedha nazo tumekubaliana kwamba Mfuko wa Barabara unagawa asilimia thelathini zinaenda kwenye Halmashauri na asilimia 70 zinaenda kuhudumia barabara za trunk road za mikoa. Sasa kama tunadhani kwamba formular hii kwa sasa labda haitufai bado ni suala la kuamua sisi Waheshimiwa Wabunge ndani ya Bunge hili Tukufu ili tuweze kubadilisha zile sheria ambazo tulikubaliana wenyewe. MWENYEKITI: Mheshimiwa wa Ushetu, jiandae Mheshimiwa Mbatia. MHE. ELIAS J. KWANDIKWA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kuniona ili nami niulize swali la nyongeza. Kwa kuwa hitaji la Mufindi Kaskazini linafanana na Ushetu na kwa kuwa Mheshimiwa Rais wetu Dkt. John Pombe Joseph Magufuli aliahidi kupandisha hadhi barabara hii inayounganisha mikoa mitatu; Mkoa wa Geita, Shinyanga na Tabora kwa kupitia maeneo ya Mbogwe, Mwabomba, Nyankende, Ubagwe, Uloa hadi Kaliua. Je, Serikali itaipandisha hadhi lini barabara hii? (Makofi) MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri, majibu. NAIBU WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO: Mheshimiwa Mwenyekiti, barabara hizo ni barabara tatu tofauti lakini zinazoungana na kwa hiyo nadhani tufuate tu utaratibu. Kwa hapa itabidi mikoa yote mitatu kwa vipande vyake ifuate taratibu za kuomba kupandisha hadhi hizo barabara. Kama tayari zimefuata taratibu hizo basi nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba 4 NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) maombi yake yatashughulikiwa kama ambavyo tumeongelea kwa barabara ambayo inaanzia Mtili – Ifwagi – Mdaburo na kuendelea. Utaratibu huo tutaufuata na maombi hayo tutayapitia kwa pamoja na zile zitakazotangazwa tutakuja kuwajulisha rasmi baada ya kutokea kwenye Gazeti la Serikali. MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa Mbatia. MHE. JAMES F. MBATIA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Kwa kuwa swali la msingi linaulizia ahadi ya Serikali na Mheshimiwa Dkt. Magufuli alivyokuwa Waziri wa Ujenzi aliahidi kukamilisha barabara ya Kawawa – Nduoni – Bakula – Marangu Mtoni ambayo ni barabara muhimu sana kwa ajili ya utalii, inajulikana kama utalii road. Alipokuwa anafanya kampeni wakati wa uchaguzi aliahidi pia kwamba itakamilika na imeshajengwa nusu tu kwa lami. Sasa ni lini Serikali itakamilisha barabara hii kwa maendeleo ya utalii na Serikali iweze kupata mapato. (Makofi) MWENYEKITI: Ni lini, anataka kujua. NAIBU WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO: Mheshimiwa Mwenyekiti, kama Waziri kivuli wa Wizara hii nadhani anafahamu na tumejadili, ingawa katika kipindi kifupi kidogo hakuwepo lakini nadhani anafahamu kwamba tumekuwa tukijadili utekelezaji wa ujenzi wa barabara mbalimbali na tumesema kwamba kwanza tuzikazanie zile ambazo zina madeni ili tuondokane na madeni na baada ya hapo tutaendelea na hizi zingine. Mheshimiwa Mwenyekiti, katika hizi zingine kipaumbele cha uhamasishaji wa utalii nacho tulikiweka. Kwa hiyo, nimshukuru alitusaidia kuweka hiki kipaumbele na hivyo mara tutakapomaliza barabara hizi ambazo zina mikataba ya muda mrefu zitafuata hizi barabara zinazohamasisha utalii na vile vile zinazohamasisha viwanda. 5 NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) MHE. VENANCE M. MWAMOTO: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nami niulize swali dogo tu la nyongeza. Kwa kuwa tatizo ambalo lipo kule Mufindi linafanana kabisa na kule Kilolo; barabara nyingi za Kilolo zimekuwa zikiahidiwa na hasa na Mheshimiwa Waziri. Sasa je, ni hatua gani ambazo inapaswa tuchukue endapo Mheshimiwa Waziri ameahidi kwa upande wa Serikali lakini utekelezaji haujafanyika? MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri kwa kifupi. NAIBU WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahadi ni dhamira, kwa hiyo tunapotoa ahadi tunaonesha dhamira ya kutaka kutekeleza hicho kitu. Hatua inayofuata baada ya kuwa na hiyo dhamira ni kutafuta fedha na mara fedha zitakapopatikana hii ahadi yetu tutaitekeleza. MWENYEKITI: Ahsante, umejibu vizuri. Waheshimiwa tunaendelea, Mheshimiwa Malocha. Na. 255 Ujenzi wa Barabara ya Kibaoni – Kasanga Hadi Mlowo - Songwe MHE. IGNAS A. MALOCHA aliuliza:- Barabara ya kutoka Kibaoni – Kasansa – Muze – Ilemba – Kilyamatundu – Kamsamba hadi Mlowo Mkoani Songwe inaunganisha Mikoa mitatu ya Katavi, Rukwa na Songwe; wananchi wa mikoa hiyo wamekuwa na maombi ya muda mrefu kutaka barabara hiyo itengenezwe kwa kiwango cha lami ili kuboresha maisha na kukuza uchumi wao na Taifa kwa ujumla:- Je, ni lini barabara hiyo itatengenezwa kwa kiwango cha lami? 6 NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) NAIBU WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO alijibu:- Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Ignas Aloyce Malocha, Mbunge wa Kwela, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Mwenyekiti, barabara ya Kibaoni – Kasansa ambayo ni kilometa 60.57 ni barabara ya mkoa inayohudumiwa na Wakala wa Barabara Tanzania Mkoa wa Katavi. Barabara ya Kasansa – Kilyamatundu ambayo ina urefu wa kilomita 178.48 ni barabara ya Mkoa inayohudumiwa na Wakala wa Barabara Tanzania Mkoa wa Rukwa; na barabara ya Kamsamba – Mlowo ambayo ina urefu wa kilomita 130 ni barabara ya mkoa inayohudumiwa na Wakala wa Barabara Tanzania Mkoa wa Songwe. Mheshimiwa Mwenyekiti, barabara hii ni kiungo sana kati ya mikoa hii mitatu ya Katavi, Rukwa na Songwe kwani inapita katika Bonde la Ziwa Rukwa ambalo ni maarufu sana kwa uzalishaji wa mazao ya kilimo na mifugo. Hali ya barabara hii ni nzuri kwa wastani ila inapitika kwa shida wakati wa masika katika baadhi ya maeneo. Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali kwa kufahamu umuhimu

View Full Text

Details

  • File Type
    pdf
  • Upload Time
    -
  • Content Languages
    English
  • Upload User
    Anonymous/Not logged-in
  • File Pages
    314 Page
  • File Size
    -

Download

Channel Download Status
Express Download Enable

Copyright

We respect the copyrights and intellectual property rights of all users. All uploaded documents are either original works of the uploader or authorized works of the rightful owners.

  • Not to be reproduced or distributed without explicit permission.
  • Not used for commercial purposes outside of approved use cases.
  • Not used to infringe on the rights of the original creators.
  • If you believe any content infringes your copyright, please contact us immediately.

Support

For help with questions, suggestions, or problems, please contact us