21 MAY 2019.Pmd

21 MAY 2019.Pmd

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ________ MAJADILIANO YA BUNGE _________ MKUTANO WA KUMI NA TANO Kikao cha Thelathini na Mbili – Tarehe 21 Mei, 2019 (Bunge Lilianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Mwenyekiti (Mhe.Najma Murtaza Giga) Alisoma Dua MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge, tukae. Katibu! NDG. MOSSY LUKUVI – KATIBU MEZANI: HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa mezani na:- NAIBU WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI: Hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Mifugo na Uvuvi kwa mwaka wa fedha 2019/2020. MHE. SIKUDHANI Y. CHIKAMBO - K.n.y. MWENYEKITI WA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE KILIMO, MIFUGO NA MAJI: Taarifa ya Kamati ya Kilimo, Mifugo na Maji kuhusu utekelezaji wa majukumu ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa mwaka wa fedha 2018/2019 pamoja na maoni ya Kamati juu ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2019/2020. 1 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) MHE. SUSAN A. J. LYIMO - K.n.y. MSEMAJI MKUU WA KAMBI RASMI YA UPINZANI BUNGENI KUHUSU MIFUGO NA UVUVI: Taarifa ya Msemaji Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani juu ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020. MWENYEKITI: Ahsante, Katibu tunaendelea. NDG. MOSSY LUKUVI – KATIBU MEZANI: MASWALI NA MAJIBU MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge tunaanza na Ofisi ya Rais TAMISEMI Mheshimiwa Semguruka Mbunge wa Viti Maalum alize swali lake. Na. 262 Kuonge Shule za Kidato cha Tano na Sita – Karagwe MHE. OLIVER D. SEMUGURUKA aliuliza:- Wilaya ya Karagwe ina Sekondari moja tu ya kidato cha Tano na Sita ambayo ni Bugene Sekondari. Je, ni lini Serikali itakamilisha ujenzi wa Sekondari za Nyabionza na Kituntu ili ziwe shule za kidato cha Tano na Sita? WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA alijibu:- Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Oliver Daniel Semuguruka Mbunge wa Viti Maalum kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali imepeleka kiasi cha shilingi milioni 190 katika shule Nyabionza kwa ajili ya ujenzi 2 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) wa madarasa mawili na mabweni mawili. Aidha, ujenzi na ukarabati wa maabara tatu, bweni moja la wasichana, maktaba, bwalo na jiko unaendelea kwa kutumia mapato ya ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe. Vilevile Shule ya Sekondari Kituntu, imepokea jumla ya shilingi milioni 52.5 ambazo zinatumika kwa ajili ya ujenzi wa madarasa mawili na bweni moja ambalo liko katika hatua ya umaliziaji. Kadhalika, halmashauri inaendelea na ujenzi wa maktaba moja, bweni moja la wavulana, madarasa mawili, bwalo la chakula na jiko kwa kutumia mapato ya ndani. Mheshimiwa Mwenyekiti, shughuli hizi za ujenzi wa miundombinu ni maandalizi ya kuzipandisha hadhi shule hizo mara tu zitakapokamilika ambapo zitasajiliwa na kupangiwa wanafunzi wa kidato cha tano. MWENYEKITI: Mheshimiwa Oliver swali la nyongeza. MHE. OLIVER D. SEMUGURUKA: Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na majibu mazuri ya Serikali ninayo maswali mawili ya nyongeza. (i) Je, Serikali itapeleka lini fedha ilizoahidi kwa ajili ya kujenga mabweni na maktaba pale Bugene Sekondari ambao ni A-level peke yake ya Serikali kwenye wilaya ya watu laki tatu na tisini? (ii) Je, Mheshimiwa Waziri upo tayari kuambatana na mimi pamoja na Mbunge wa Jimbo Mheshimiwa Bashungwa ili ukajionee mlundikano wa wanafunzi Bugene Sekondari kwa sababu ya upungufu wa mabweni? MWENYEKITI: Ahsante sana Mheshimiwa Oliver kwa maswali mafupi ya nyongeza ya kibunge kabisa Mheshimiwa Waziri majibu. WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la kwanza naomba nianze kujibu swali la pili kwa kwanza nipo 3 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) tayari tutaambatana pamoja hakika tutaenda kufanya kazi nzuri tu kule. Mheshimiwa Mwenyekiti, kifupi niseme nimpongeze sana Mheshimiwa Oliver, kwa sababu yeye na Mbunge Mheshimiwa Innocent wamekuwa wakipambana sana kuhakikisha Halmashauri ya Karagwe inafanya vizuri. Eneo hili ndio maana hata ile shule ya kwanza tuliyoipatia shilingi 190 ni kwa ajili ya maombi yao waliyoyaleta ofisi kuhakikisha tunasaidia wazi. Mheshimiwa Mwenyekiti, na upande wa Bugene sekondari tunajua ni wazi kweli idadi ya wanafunzi ni wengi, naomba nikuhakikishie Serikali itafanya kila liwezekanalo kuhakikisha tunaongeza fedha pale kwa ajili miundombinu ile iweze kuimarika vizuri tuweze kupokea watoto ambao tunatarajia si muda mrefu tutawatangaza. Kwa hiyo, hii ni commitment ya Serikali tutafanya kila liwezekanalo tutaongeza fedha kuimarisha miundombinu ya pale. MWENYEKITI: Mheshimiwa Mwita Getere. MHE. BONIPHACE M. GETERE: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushuru kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali, katika jimbo langu la Bunda kuna maboma ya maabara na hasa katika Shule ya Sekondari Salama. Mheshimiwa Waziri hatudhuliani ni ndugu yangu, katika ile shule kumekuwepo na maboma mawili ambayo kuna mabati na mbao zinaenda kuonza ni muda mrefu, wananchi hali yao ni mbaya wamekuwa na michango mingi kwenye maeneo mbalimbali. Nakuomba Waziri hili ni ombi rasmi nakuomba Waziri unisaidie kunipelekea milioni 30 tu kwenye shule ya sekondari salama ahsante. MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri majibu kwa ufupi. WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nichukue ombi la Mbunge Boniphace kwa sababu nikifahamu eneo lake lile kwa kweli kuna changamoto nyingi mbalimbali na nikiri wazi kwamba eneo hilo lazima tulipe 4 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) kipaumbele kwa sababu kuna fedha tu kidogo zinahitajika tutaangalia mfuko ukoje halafu tutashirikiana mimi na wewe kuangalia jinsi gani tutafanya kuhakikisha hiyo miundombinu ambayo wananchi wamejitolea isiweze kuharibika. MWENYEKITI: Mheshimiwa Leah Komanya. MHE. LEAH J. KOMANYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushuru shule ya wasichana Nyalanja yenye kidato cha tano na sita ina mchepuo mmoja tu lakini inayo madarasa sita zaidi ya miaka mitano hayatumiki. Je, Serikali haioni haja ya kutupatia bweni kwa ajili ya kuongeza mchepuo mwingine? MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri majibu kwa kifupi kwa swali hilo. WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kama kuna miundo mbinu kama hiyo, naomba nilichukue jambo hilo kwa sababu hivi sasa ukingalia tuna vijana wengi sana ambao kwa kweli ufaulu umeongezeka. Kwa mfano mwaka huu tuna vijana zaidi laki moja plus ambao wote wanatakiwa wape nafasi kwa ajili ya kidato cha tano na kuendelea. Kwa hiyo, kama kuna fursa kama hiyo ya madarasa yapo tutaangalia nini tufanye ikiwezekana tukatafute fedha kwa haraka tuongeze pale bweni kwa ajili kuhakikisha kwamba tunaongeza mchepuo mwingine vijana wengi wa kitanzania waweze kupata nafasi. MWENYEKITI: Mheshimiwa Maryam Msabaha. MHE. MARYAM SALUM MSABAHA: Mheshimiwa Mwenyekiti, sambamba na hilo wanafunzi wengi wa kike wamekuwa wakipata mimba katika mazingira magumu. Je, Serikali ina mikakati gani kujenga hostel za watoto wa kike ili wapate kujistiri waondokane na vishawishi vya barabarani? 5 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) MWENYEKITI: Haya ahsante, Mheshimiwa Waziri majibu ya swali hilo kwa kifupi. WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli ndio maana azma ya Serikali juzi juzi mwezi wa tatu Serikali imetoa takribani shilingi bilioni 54.6 ambayo katika hili lengo lake ni kujenga madarasa takribani 988 lakini mabweni mapya 210 kwa hiyo ni commitment ya Serikali kuhakikisha jinsi gani mabweni haya yanjengwa. Kwa hiyo, Mheshimiwa dada yangu naomba nikuhakikishie kwamba tutafanya kila liwezekano tutaangalia nini tufanye licha tunaanza kujenga mabweni 210 katika maeneo mbalimbali lakini juhudi ya Serikali itaendelea kuhakikisha vijana hawa wa kike tunawaondoa katika hali hatalishi zaidi hasa kwa watu ambao wana nia mbaya kuhakikisha wanaharibu future ya watoto wa kike. Kwa hiyo, tunaendelea kulichukua kwa ajili ya Serikali kulifanyia kazi. MWENYEKITI: Tunaendelea na Mheshimiwa Sebastian Simon Kapufi Mbunge wa Mpanda Mjini sasa aulize swali. Na. 263 Bajeti ya TARURA Mkoa wa Katavi MHE. SEBASTIAN S. KAPUFI aliuliza:- Katika Bajeti ya mwaka 2018/2019 Mkoa wa Katavi ulitengewa kiasi kidogo cha fedha kuliko mikoa yote. Je, Serikali iko tayari kuongeza mgao wa fedha kwa Mkoa wa Katavi kwa kuzingatia jiografia na kilomita za mtandao wa barabara? MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri, majibu ya swali hilo. WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA alijibu:- 6 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Sebastian Simon Kapufi Mbunge wa jimbo la Mpanda Mjini kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Mwenyekiti, Katika kupanga bajeti kwa ajili ya ujenzi na matengenezo ya barabara kwenye Mamlaka za Serikai za Mitaa. Serikali inazingatia vigezo mbalimbali ikiwemo kigezo cha mtandao wa barabara ullisajiliwa. Mkoa wa katavi katika mwaka wa fedha 2018/2019, uliidhinishiwa shilingi 3.62 kwa kuzingatia matandao wa barabara uliopo ambao ni kilomita 1,441.3. Vigezo vingine vinavyozingatiwa na pamoja na tabaka la barabara hali ya mtandao wa barabara, idadi ya magari yanayotumia barabara na idadi ya watu wanaohudumiwa na barabara husika. Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali kupitia bodi ya mfuko wa barabara inaendelea na zoezi la uhakiki wa mtandao wa barabara zinazosimamiwa na TARURA ili kuishauri Serikali kufanya mapitio ya mgawo wa fedha za mfuko wa barabara na kuhakikisha barabara zinazohudumiwa na TARURA zinatengewa bajeti ya kutosha kwa ajili ya matengenezo hayo. MWENYEKITI: Mheshimiwa Kapufi. MHE. SEBASTIANA S. KAFUPI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushuru pamoja na majibu mazuri ya Serikali

View Full Text

Details

  • File Type
    pdf
  • Upload Time
    -
  • Content Languages
    English
  • Upload User
    Anonymous/Not logged-in
  • File Pages
    310 Page
  • File Size
    -

Download

Channel Download Status
Express Download Enable

Copyright

We respect the copyrights and intellectual property rights of all users. All uploaded documents are either original works of the uploader or authorized works of the rightful owners.

  • Not to be reproduced or distributed without explicit permission.
  • Not used for commercial purposes outside of approved use cases.
  • Not used to infringe on the rights of the original creators.
  • If you believe any content infringes your copyright, please contact us immediately.

Support

For help with questions, suggestions, or problems, please contact us