19 Desemba, 2013

19 Desemba, 2013

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) BUNGE LA TANZANIA __________ MAJADILIANO YA BUNGE __________ MKUTANO WA KUMI NA NNE Kikao cha Kumi na Tatu - Tarehe 19 Desemba, 2013 (Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Spika (Mhe. Anne S. Makinda) Alisoma Dua HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI Hati Zifuatazo Ziliwasilishwa Mezani na:- NAIBU WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI:- Taarifa ya Mwaka na Hesabu Zilizokaguliwa za Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) kwa Mwaka ulioishia Tarehe 30 Juni, 2012 (The Annual Report and Audited Accounts of the National Housing Corporation (NHC) for The Year ended 30th June, 2012). 1 Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) WAZIRI WA KAZI NA AJIRA:- Taarifa ya Mwaka ya Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Hifadhi ya Jamii (SSRA) kwa Mwaka 2011/2012 (The Annual Report of Social Security Regulatory Authority (SSRA) for the Year 2011/2012). MASWALI KWA WAZIRI MKUU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge leo ni siku ya Alhamisi, tunakuwa na Maswali kwa Waziri Mkuu. Kawaida yetu kama Kiongozi wa Upinzani yupo basi ndiye anayeanza. Naona sijamwona. Kwa hiyo, nitaanza na Mheshimiwa Murtaza Mangungu. Mheshimiwa Murtaza Mangungu. MHE. MURTAZA A. MANGUNGU: Nakushukuru sana Mheshimiwa Spika. Mheshimiwa Waziri Mkuu, kwa kipindi cha miaka ya 1970 kuja 1980 Serikali ilifanya jitihada kubwa sana kupanua elimu ya juu nchini. Lakini kutokana na matatizo ambayo hayajaelezeka kipindi kirefu hatujawekeza vya kutosha hivyo kuna upungufu mkubwa sana wa Wahadhiri katika Vyuo Vikuu hasa ukizingatia Sheria yetu ya ajira inatoa ukomo wa kustaafu siyo zaidi ya miaka 65 na maprofesa wote ambao ni full Professor wamezidi umri wa miaka 65. Je, Taifa letu tunalipeleka wapi katika Sekta hii ya Elimu? WAZIRI MKUU: Mheshimiwa Spika, naomba nimshukuru tu Mheshimiwa Murtaza Mangungu kwa swali lake zuri na labda nianze kwa kusema kwamba of course ni la Sera hili na si kwamba ni jambo linagusa sekta moja ya elimu kwa maana ya walimu hapana. Mfumo ulivyo sasa muhimili wa Mahakama ndiyo ambao umewekewa utaratibu wa kwenda mpaka miaka 65 na kwa ajili ya Majaji wa Mahakama ya rufaa. Lakini Majaji wengine nadhani tuko sawa sawa kama katika utumishi wa kawaida wa miaka 60. 2 Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) [WAZIRI MKUU] Kwa hiyo, walimu wengi na wenyewe wako kwenye kundi hilo la miaka 60. Isipokuwa kwa upande wa Vyuo vya Elimu ya Juu kilichopo kwa sasa ni kwamba anaruhusiwa kwa mkataba kuongezewa muda hadi miaka mitano, kwa miaka miwili, miwili, mmoja. Baada ya pale inakuwa ndiyo amefikia ukomo wake. Kwa hiyo, ni kama amefikia miaka 65 kama ilivyo kwa Majaji wa Rufaa. Sasa rai yake ni kwamba pengine katika mazingira tuliyonayo. Je, isingalikuwa busara pengine kupanua wigo tuongeze muda wa kustaafu ili tuweze pengine kuziba na kuwa na maprofesa wengi? Mimi nadhani ni rai nzuri. Inaweza ikaangaliwa, lakini iangaliwe kisera na lazima tutazame mfumo mzima unavyounganishwa na maeneo mengine yote ambayo yanagusa utumishi wa Umma. Lakini kwa upande mwingine alieleza vile vile kwamba inaonekana kwa sababu katika utaratibu wetu huu wa kukataa maprofesa inawezekana hatukuwekeza sana. Of course jitihada zimekuwepo muda wote na pengine kwa sasa naweza nikasema jitihada ni nzuri zaidi kwa sababu ukichukua Chuo cha Nelson Mandela pale ukachukua na Vyuo Vikuu vyenyewe sasa hivi walimu wengi tunaweza kuwapata ambao wanaweza kujiendeleza kwa njia ambayo ni pana zaidi kuliko iilvyokuwa siku za mwanzoni. Lakini bado pengine nitajaribukuzungumza na Waziri wa Utumishi pamoja na Waziri wa Elimu labda wakae waangalie hiyo rai na efect yake kwenye utumishi mpana wa Umma itakuwa ni nini. (Makofi) MHE. MURTAZA A. MANGUNGU: Nashukuru sana kwa majibu ya matumaini yaliyotolewa na Mheshimiwa Waziri Mkuu. Ningependa kuuliza swali moja la nyongeza. Wenzetu hawa ambao waliingia kwenye taaluma ya ufundishaji walikataa kazi zile za maslahi makubwa. 3 Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) [MHE. MURTAZA A. MANGUNGU] Lakini jambo la kusikitisha kabisa kwamba hawakuweza kulipwa pensheni. Mheshimiwa Rais, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, alitoa agizo kwa Serikali yake kwamba wastaafu hawa Wahandiri wa Vyuo Vikuu walipwe pensheni. Je, leo Serikali inatamka nini? WAZIRI MKUU: Mheshimiwa Spika, inawezekana nisiwe na jibu sasa kwa sababu ni kitu very specific kinalenga kinataka tutoe jibu la uhakika. Lakini ninaloweza kukubaliana tu ni kwamba Vyuo hivi vya Elimu ya Juu vina mfumo wake au scheme yake ya pensheni ambayo ndiyo wamekuwa wakiitumia kwa muda mrefu na kuna wakati hapo siku za nyuma nilipata nafasi ya kukutana nao kwenye mkutano mrefu mzuri. Lakini kulikuwa na mambo mawili. Moja ilikuwa ni kweli kwamba kulikuwa na maeneo ambayo yalikuwa na hitilafu katika malipo yao ambayo tulijaribu kukaa na kujaribu kuyatatua ili waweze kulipwa zile staili zao. Muda mrefu kidogo na maadam umeliuliza leo kwa sababu sijawahi kulipata hapo katikati labda unipe muda tu nita-cross check na wenzetu wa Elimu pale, tuone kama lile jambo lilikwisha na kama bado basi nitapata maelezo kwa nini ili tuweze kulimaliza. Lakini kimsingi tulishalifanyia kazi na tukakubaliana na ni maeneo mengi ambayo walikuwa wameyaleta yaliweza kutatuliwa bila tatizo kubwa. SPIKA: Ahsante sana. Waheshimiwa Wabunge kama tulivyosema maswali kwa Waziri Mkuu ni ya Sera. Mkiuliza Sekta kwa kweli it is just siyo sawa sawa. Maana yake unamwliza Waziri Mkuu wakati kuna wa Sector Minister. Tafadhali nawaombeni na muwe brief, tunaweza ku-cover watu wengi. Mheshimiwa Engineer James Francis Mbatia. 4 Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) MHE. JAMES F. MBATIA: Nashukuru Mheshimiwa Spika. Mheshimiwa waziri Mkuu, kasi ya kukua kwa majiji mengi duniani ni changamoto ambayo inatukumba hata kwetu sisi hapa Tanzania. Kwa mfano Jiji la Dar es Salaam kwanza ndiyo chanzo kikuu cha mapato kwa zaidi ya asilimia 80 fedha ya ndani tunaipata katika Jiji la Dar es Salaam. Kwa sasa msongamano wa magari katika Jiji la Dar es Salaam pamoja na majiji mengine yanayokuwa ni janga la kitaifa na linaingiza hasara kubwa sana katika Taifa letu. Kwa sasa Jiji la Dar es Salaam linaweza likatumika kwa usafiri wote yaani usafiri wa maji, reli, barabara, anga hata kwa tele-conferece katika kufanya majukumu mbalimbali. Je, Serikali kwa sasa hivi ina mkakati gani, kwa sasa licha ya mkakati ulioko wa mabasi yaendayo kwa kasi, ili kuondoa janga hili ambalo linatakiwa lipatiwe ufumbuzi wa kupambana na majanga? (Makofi) WAZIRI MKUU: Mheshimiwa Spika, nakubaliana kabisa na Mheshimiwa James Francis Mbatia kwamba msongamano uliopo Dar es Salaam kwa kweli ni adha kubwa. Kwanza kwa jamii yenyewe. Lakini kubwa zaidi hasa ni athari zake kwa uchumi kwa ujumla. Kwa sababu money hour loss inakuwa ni kubwa mno, kiwango cha masaa ambayo yanapotea pale ni mengi. Kwa hiyo, ni kweli ni concern genuine kwa kila Mtanzania na hasa sisi wakazi wa Dar es Salaam. Of course kwa upande wa Serikali tulikuja na lile wazo la mabasi yaendayo kasi, of course miradi imeanza kutengenezwa kujengwa. Lakini bado swali halitabadilika kwa sababu hiyo tu, hata kidogo. Kwa sababu lazima tukubali hilo kwamba idadi ya wakazi imeongezeka mno. Kwa hiyo magari vile vile yameongezeka katika Jiji letu la Dar es Salaam. 5 [WAZIRI MKUU] [MHE. MURTAZA A. MANGUNGU] Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) [WAZIRI MKUU] Sasa pengine tunachoweza labda na kumwahidi Mheshimiwa James Mbatia hapa unachohitaji kwanza ni kujaribu kuona katika muda huu mfupi katika hali tunayoiona pale, kwa sababu hata utengenezaji wa barabara nao umeongeza vile vile msongamono kwa kiasi kikubwa sana. Kwa hiyo, haja pengine ni Wizara ya Uchukuzi, wizara ya Fedha, TAMISEMI, Jiji lenyewe, Mambo ya Ndani ya Nchi, hawa wote pengine wakae mapema iwezekanavyo wajaribu kuona katika kipindi hiki cha muda mfupi ni hatua zipi zingeweza kuchukuliwa ili tuweze kuona namna ya kupunguza msongamano ambao sasa unaathiri sana shughuli za Serikali. Lakini wakati huo huo ni lazima tuendelee kama Serikali kuona jitihada hizi za kujaribu kujenga barabara sijui wanaziita za wapi za juu. Fly Overs, lazima zipewe msukumo mkubwa sana. Kwa sababu nchi nyingi zimepambana na tatizo hili. Lakini suluhu imekuwa ni katika kujaribu kupata hizo barabara zina uwezo wa kuweza kubeba magari, kuteremshwa kwenye maeneo mbalimbali. Sasa pale tunao mradi mmoja ule wa Ubungo lakini hauwezi ku-provide, hautatoa jibu kwa msongamano wa Jiji lote la Dar es Salaam. Kwa hiyo, nakubaliana na Mheshimiwa James Mbatia kuwa changamoto hii ni ya Serikali lakini ni yetu wote. Kwa hiyo, nadhani katika hatua hii ya mwanzo ngoja nikubali challenge hiyo tuone immediately nini tungeweza tukafanya pale. Lakini nadhani kwa muda mrefu itabidi Bunge nalo liendelee vile vile kushauri na kujaribu kuzungunza na Serikali tuendelee kulitafakari kwa pamoja ukuaji kwa kasi kwa miji na namna tunavyoweza kukabiliana na huu msongamano katika siku zinazokuja. (Makofi) SPIKA: Ahsante sana. Mheshimiwa Engineer James Francis Mbatia, swali la nyongeza kwa kifupi sana. 6 Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) MHE. JAMES F. MBATIA: Nashukuru Mheshimiwa Spika. Kwa kuwa ni vizuri kuwa na tahadhari, yaani kujikinga na majanga kabla ya janga lenyewe halijatokea na ucheleweshwaji wa kufanya maamuzi haya ulichukua miaka mingi kidogo tangu mwaka 1996 tuliwahi kulijadili Bungeni. Mheshimiwa Waziri Mkuu unaonaje kwamba Wizara hizi ulizozitaja ni sahihi kabisa zikakaa immediately na mimi na- declare interest mimi ni mtaalam wa majanga niko tayari kutoa ushauri wangu katika Wizara hizi? (Makofi) WAZIRI MKUU: Mimi nafikiri hilo mimi sina ugomvi nalo hata kidogo. Najua ndiyo eneo lako la fani. Kwa hiyo, kama utakuwa

View Full Text

Details

  • File Type
    pdf
  • Upload Time
    -
  • Content Languages
    English
  • Upload User
    Anonymous/Not logged-in
  • File Pages
    192 Page
  • File Size
    -

Download

Channel Download Status
Express Download Enable

Copyright

We respect the copyrights and intellectual property rights of all users. All uploaded documents are either original works of the uploader or authorized works of the rightful owners.

  • Not to be reproduced or distributed without explicit permission.
  • Not used for commercial purposes outside of approved use cases.
  • Not used to infringe on the rights of the original creators.
  • If you believe any content infringes your copyright, please contact us immediately.

Support

For help with questions, suggestions, or problems, please contact us