NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ________ MAJADILIANO YA BUNGE _________ MKUTANO WA KUMI NA NANE Kikao cha Sita – Tarehe 4 Februari, 2020 (Bunge Lilianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Mwenyekiti (Mhe. Najma Murtaza Giga) Alisoma Dua MWENYEKITI: Waheshimiwa tukae. Katibu tunaendelea Waheshimiwa Wabunge na Mkutano wetu wa Kumi na Nane, kikao cha leo ni kikao cha tano, Katibu NDG. RAMADHANI ISSA ABDALLAH – KATIBU MEZANI: HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati Zifuatazi Ziliwasilishwa Mezani na:- WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI, AJIRA, VIJANA NA WENYE ULEMAVU: Taarifa ya Matoleo ya Gazeti la Serikali pamoja na Nyongeza zake yaliyochapishwa tangu Mkutano wa Bunge uliopita kama ifuatavyo:- (i) Toleo Namba 46 la tarehe 8 Novemba, 2019 (ii) Toleo Namba 47 la tarehe 15 Novemba, 2019 (iii) Toleo Namba 48 la tarehe 22 Novemba, 2019 (iv) Toleo Namba 49 la tarehe 29 Novemba, 2019 (v) Toleo Namba 51 la tarehe 13 Desemba, 2019 (vi) Toleo Namba 52 la tarehe 20 Desemba, 2019 (vii) Toleo Namba 53 la tarehe 27 Desemba, 2019 (viii) Toleo Namba 1 la tarehe 3 Januari, 2020 (ix) Toleo Namba 2 la terehe 10 Januari, 2020 (x) Toleo Namba 3 la tarehe 17 Januari, 2020 (xi) Toleo Namba 4 la terehe 24 Januari, 2020 MHE. JASSON S. RWEIKIZA – MWENYEKITI WA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA UTAWALA NA SERIKALI ZA MITAA: Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za MItaa kuhuus shughuli za Kamati hii kwa Mwaka 2019. MHE. MOHAMED O. MCHENGERWA – MWENYEKITI WA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE KATIBA NA SHERIA: Taarifa ya Kmaati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria kuhusu shughuli zilizotekelezwa na Kamati hiyo kwa kipindi cha kuanzia Februari, 2019 hadi Januari, 2020. MHE. ANDREW J. CHENGE – MWENYEKITI WA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA SHERIA NDOGO: 1 NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT) Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria Ndogo kuhuus shughuli zilizotekelezwa kwa kipindi cha kuanzia Februari, 2019 hadi Januari, 2020. MWENYEKITI: Ahsante sana Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria Ndogo, Mheshimiwa Ntemi Chenge. Katibu tuendelee. NDG. RAMADHANI ISSA ABDALLAH – KATIBU MEZANI: MASWALI NA MAJIBU Na.66 Kuboresha Kituo cha Afya Kiagata – Butiama MHE. AMINA N. MAKILAGI aliuliza:- Je, Serikali ina mkakati gani wa kuboresha miundombinu ya Kituo cha Afya cha Kiagata kwani Wananchi wote wa Wilaya ya Butiama wanategemea Kituo hicho. NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. JOSEPHAT S. KANDEGE) alijibu:- Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Amina Nassor Makilagi, Mbunge wa Viti Maalum kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Mwenyeiti, katika mwaka wa fedha 2017/2028 Serikali iliidhinisha na kutoa kiasi cha shilingi milioni 400 kwa ajili ya kuboresha miundmbinu ya Kituo cha Afya cha Kiagati. Kazi zilizofanyika ni ujenzi wa nyumba ya mtumishi, wodi ya wazazi, jengo la maabara, jengo la mionzi, jengo la kuhifadhia maiti na kichomea taka. Aidha, Halmashauri ya Wilaya ya Butiama kupitia mapato yake ya ndani imetumia kiasi cha shilingi milioni 37.5 kwaajili ya kukamilisha miundombinu iliyosalia pamnoja na kununua Jokofu la kuhifadhia maiti. Mheshimiwa Mwenyekiti, KItuo hicho cha afya kwa sasa kinatoa huduma za upasuaji wa dharura, huduma za ultrasound, huduma za Mama na Mtoto na kulaza wagonjwa. MWENYEKITI: Mheshimiwa Amina swali la nyongeza. MHE. AMINA N. MAKILAGI: Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na majibu mazuri sana ya Mheshimiwa Naibu Waziri, Kaka yangu Kandege, pamoja na kuipongeza Serikali kwa kazi nzuri sana iliyofanya ya kuboresha hiki kituo muhimu cha Kiagata ambacho sasa kinatoa huduma kwa kiwango cha ufanisi, na pia kuishukuru Serikali kwa kazi nzuri sana iliyofanya ya kujenga vituo zaidi ya tisa katika Mkoa wa Mara, nina maswali mawili ya nyongeza kama ifuayavyo:- Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la kwanza; kwa kuwa kituo cha Kiagata na hata hospitali ya Wilaya ya Butiama ina upungufu wa wataalam kwa kiwango cha asilimia 70, kwamba pia lipo tatizo kubwa la wataalam wa mionzi lakini vilevile hakuna x-ray kwa Wilaya nzima ya Bitiama ikiwemo hospitali ya Wilaya na hata kituo cha Kiagata. Je, Serikali ina mkakati gani wa kuhakikisha inapeleka wataalam katika hospitali ya Butiama na Kituo cha Kiagata na hasa kipaumbele kikiwa ni wale watalam wa mionzi kwa ajili ya wakina Mama? 2 NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT) Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili; kwa kuwa Wilaya ya Butiama kwa mujibu wa sensa ina watu zaidi ya 200,003 na Butiama ni Wilaya ya kazi, watu wanakula wanashiba, population ya watu inaongezeka. Vilevile kwa kuwa Wilaya ya Butiama ina kata 18 na ina vitongoji 370 lakini Kituo cha Afya ni kimoja tu cha Kiagata ambacho kinahudumia hata wananchi wote wa Wilaya y Butiama; Tarafa ya Makongoro iko mbali na Kiagata, Wananchi wa Makongoro wanapata shida sana kwenda Kituo cha Afya cha Kiagata; (i) Ni mkakati gani sasa wa Serikali wa kuboresha Kituo cha Bisumwa ili kiwe sasa kituo cha afya, ili kisaidie Kata saba? (ii) Serikali ina mkakati gani wa kuboreshga Zahanati ya Kirumi ili sasa isaidie Kata sita? (iii) Na Serikali ina mkakati gani wa kuboresha Zahanati ya Buhemba ili iweze kusaidia wananchi wa Wilaya ya Butiama? Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kuwasilisha? MWENYEKITI: Mheshimiwa Naibu Waziri majibu ya maswali hayo mawili. NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. JOSEPHAT S. KANDEGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nijibu maswali mawili ya Mheshimiwa Amina Makilagi kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba uniruhusu nipokee pongezi ambazo ametoa kwa Serikali ya Awamu ya Tano kwa kazi inayofanya ya kupeleka huduma za afya jirani. Mheshimiwa Mwenyekiti, katika swali lake la kwanza, anaongelea suala zima la uharaka wa kuhakikisha kwamba wanakuwepo wataalam, na hasa wataalam wa mionzi, ili kazi nzuri iliyofanyika Kituo cha Kiagata iweze kutoa matunda. Naomba nitumie fursa hii kumuagiza Mganga Mkuu wa Wilaya, miongoni mwa wataalam waliopo ateue angalau mtaalam mmoja akasomee kazi ya mionzi ili huduma ianze kutolewa ili huduma ianze kutolewa wakati Serikali inafikiria kupeleka wengine. Mheshimiwa Mwenyekiti, ametaja kituo cha afya lakini na zahanati kama tatu, sina uhakika kama ni swali moja lakini naomba itoshe tu nimambie Mheshimiwa Makilagi, kazi kubwa, nzuri ambayo anaipigania kuhakikisha hasa akina mama wanapata huduma ya afya, sisi kama Serikali tuko pamoja na yeye. Naomba nitoe wito kwa halmashauri kuhakikisha kwamba maombi yote ambayo Mheshimiwa Amina Makilagi ameyatoa hapa yanazingatiwa katika bajeti hii ambayo inaandaliwa na sisi Serikali Kuu hakika hatutamuangusha. (Makofi) MWENYEKITI: Tunaendelea, Mheshimiwa Pascal Yohana Haonga Mbunge wa Mbozi sasa aulize swali lake Na. 67 Ujenzi wa Wodi ya Wakina Mama Wilaya ya Mbozi MHE. PASCAL Y. HAONGA aliuliza:- Wastani wa akinamama wanaojifungua kwa siku ni 18 - 20 katika Hospitali ya Wilaya ya Mbozi; licha ya idadi kubwa ya akinamama wanaojifungua, kuna ufinyu wa majengo mbalimbali ikiwepo na wodi ya akinamama. 3 NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT) (a) Je, ni lini Serikali itashughulikia ujenzi wa wodi ya akina mama katika hospitali hii? (b) Hospitali ya Wilaya ya Mbozi inatumika kama Hospitali ya Mkoa wa Songwe na haina maji safi na salama. Je, ni lini Serikali itapeleka huduma ya maji safi na salama katika hospitali hii? NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. JOSEPHAT S. KANDEGE) alijibu:- Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Pascal Yohana Haonga, Mbunge wa Mbozi lenye sehemu (a) na (b) kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Mwenyekiti, Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi imefanya tathmini na kubaini zinahitajika jumla ya shilingi milioni 37 kwa ajili ya upanuzi wa wodi ya akina mama wanaojifungua. Mradi huo umepewa kipambele katika mpango wa bajeti wa mwaka 2020/2021 ili kuanza ujenzi. Katika mwaka wa fedha 2019/2020 Halmashauri imeidhinishiwa jumla ya shilingi milioni 12 kwa ajili ya kuchimba kisima cha maji katika hospitali ya Wilaya ya Mbozi ili kutatua changamoto ya maji katika hospitali hiyo. MWENYEKITI: Mheshimiwa Haonga. MHE. PASCAL Y. HAONGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipa nafasi ya kuuliza maswali mawili ya nyongeza:- Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la kwanza; kwa kuwa katika majibu ya Serikali ni kwamba zimetengwa milioni 37 zitakazotumika katika kuboresha wodi ya akina mama wanaojifungua; na kwa kuwa wodi hiyo ni wodi ambayo kwa kweli akina mama wanapata shida, wanalala akina mama wawili katika kitanda kimoja na kuna msongamano mkubwa sana; Je, Serikali sasa inaweza ikatupa majibu rasmi wana Mbozi na wana Songwe kwamba hizo fedha ni lini sasa zitakwenda rasmi? Kwasababu tatizo hili si dogo, ni kubwa sana. Akina mama wanapata shida na wanaweza kupata magonjwa kwasababu kuna msongamano ambao kwa kweli si wa kawaida? Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili; kwa kuwa pia katika Hospitali hii ya Wilaya ya Mbozi ambayo pia inatumika kama Hospitali Teule ya Mkoa wa Songwe kuna tatizo la ufinyu wa OPD; na OPD iliyopo pale ni ndogo sana na kuna msomngamano mkubwa sana. Je, Serikali ipo tayari sasa kufanya upanuzi wa ile OPD ili iweze kuboreshwa na ichukue wagonjwa walio wengi zaidi kuliko hali iliyoko sasa ambayo wagonjwa ni wengi na OPD ni ndogo? MWENYEKITI: Mheshimiwa Naibu Waziri majibu. NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. JOSEPHAT S. KANDEGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nichukue fursa hii kujibu maswali yote mawili ya Mheshimiwa Haonga kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Mwenyekiti, katika majibu yangu ya msingi nimemwmbia Mheshimiwa Mbunge commitment ya Serikali kwamba katika bajeti ya mwaka 2020/2021 milioni 37 zimetengwa. Tafsiri yake ni nini? Ni kwamba hiyo inaonesha seriousness ya Serikali katika kuahidi na kuweka katika maandishi. Naomba Mheshimiwa Mbunge aendelee kuiamini Serikali, tukiahdi tunatekeleza. 4 NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT) Mheshimiwa Mwenyekiti, katika swali lake la pili anaongelea juu ya suala zima la ufinyu wa wodi, kwa maana kunakuwa na msongamano mkubwa wa wagonjwa katika ile hospitali ambayo inatumika kama ndiyo hospitali ya rufaa ya Mkoa.
Details
-
File Typepdf
-
Upload Time-
-
Content LanguagesEnglish
-
Upload UserAnonymous/Not logged-in
-
File Pages182 Page
-
File Size-