NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ____________ MAJADILIANO YA BUNGE ___________ MKUTANO WA SABA Kikao cha Ishirini na Mbili – Tarehe 11 Mei, 2017 (Bunge Lilianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Naibu Spika (Mhe. Dkt. Tulia Ackson) Alisoma Dua NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, tukae. Katibu. NDG. CHARLES MLOKA – KATIBU MEZANI: MASWALI KWA WAZIRI MKUU NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, tutaanza na maswali kwa Mheshimiwa Waziri Mkuu. Waheshimiwa Wabunge, tutaanza na Mheshimiwa Freeman Aikaeli Mbowe, Kiongozi wa Upinzani Bungeni. MHE. FREEMAN A. MBOWE: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi ya kwanza ya kumuuliza Waziri Mkuu swali. Mheshimiwa Waziri Mkuu, Bunge kwa mujibu wa Katiba Ibara ya 63(2), ndicho chombo kikuu chenye mamlaka na wajibu wa kuisimamia na kuishauri Serikali. Katika Bunge hili, Bunge la Kumi na Mabunge mengine kadhaa, Bunge limekuwa linatoa Maazimio kadhaa kuitaka Serikali itoe taarifa na Serikali imekuwa inaahidi kutoa taarifa, lakini taarifa nyingi ambazo ni Maazimio ya Bunge yamekuwa hayatekelezwi na Serikali. 1 NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) Mheshimiwa Naibu Spika, kwa mfano, kuna Maazimio ya Bunge kuhusiana na Tokomeza mpaka leo Serikali haijaleta majibu. Kuna Maazimio ya Bunge kuhusiana na ESCROW na IPTL, Serikali mpaka leo haijatoa majibu. Kuna Maazimio ya Bunge kuhusu mabilioni ya Uswis, Serikali mpaka leo haijatoa majibu na Maazimio mengine mengi. (Makofi) Mheshimiwa Waziri Mkuu unaliambia nini Bunge na unaliambia nini Taifa. Wewe kama Kiongozi wa Serikali Bungeni, utapenda kusema kwamba Serikali inalidharau Bunge ama Serikali haina majibu ya kutoa? (Makofi) NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Waziri Mkuu majibu. WAZIRI MKUU: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nijibu swali la Mheshimiwa Freeman Aikaeli Mbowe, Mbunge wa Hai na Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza nataka nikuhakikishie kwamba Serikali inaheshimu sana Mhimili wa Bunge na inathamini sana maamuzi ya Mhimili huu wa Bunge na tutaendelea kushirikiana na Mhimili wa Bunge katika kupata ushauri na namna nzuri ya kuendesha Serikali kwa mapendekezo ambayo yanatolewa na Waheshimiwa Wabunge kupitia chombo cha Bunge. (Makofi) Mheshimiwa Naibu Spika, natambua vikao kadhaa huko awali kumekuwa na Maazimio yanayoitaka Serikali ilete maelezo, lakini baadhi ya maeneo ambayo yanatakiwa kuletwa hapa ni yale ambayo yanahitaji uchunguzi wa kina na uchunguzi huu unapokamilika ndipo unapoweza kuletwa Bungeni. Sasa yapo ambayo tunaona upo umuhimu wa kuyaleta ni pamoja na hayo uliyoyasema, nataka nikuahidi kwamba haya ambayo umeyatamka kwenye maeneo yanayogusa Wizara kadhaa ambazo zinatakiwa kuleta taarifa nitafanya ufuatiliaji, pale ambapo tutakuwa 2 NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) tumekamilisha uchunguzi wetu, nitayaleta kwa utaratibu ambao Bunge utakuwa umetoa maelekezo yake. Ahsante sana. (Makofi) NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Freeman Aikaeli Mbowe, swali la nyongeza. MHE. FREEMAN A. MBOWE: Mheshimiwa Naibu Spika, namshukuru Mheshimiwa Waziri Mkuu kwa majibu yake, ni ukweli usiopingika kwamba pale muda unapotumika au unapopita sana bila majibu hata status kutolewa katika Bunge, hoja hiyo huonekana kwamba imefifia umuhimu na ulazima wake. Mheshimiwa Waziri Mkuu, pamoja na kwamba umetoa ahadi ya kwamba Wizara zitashughulikia, unaweza ukatoa a firm commitment kwamba katika Bunge hili, kabla Bunge hili la Bajeti halijaisha, Serikali itapitia Hansard na kumbukumbu zote zinazohusiana na Maazimio yaliyopita ya Bunge halafu Serikali itoe status report na naomba itambulike hapa kwamba status report siyo lazima ndiyo iwe ripoti ya uchunguzi ya mwisho, angalau ituambie jambo hili limefikia hapa, limefanyiwa kazi moja, mbili, tatu, bado tutaletewa katika hatua ya baadae. Mheshimiwa Naibu Spika, angalau Bunge lipewe status ya Maazimio kadhaa ambayo ni mengi kwa kweli, ambayo yameshaazimiwa na Bunge hili, Mheshimiwa Waziri Mkuu, kwa sababu ya hiyo nia njema ya Serikali, unaweza ukatoa commitment hiyo? (Makofi) NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Waziri Mkuu, majibu. WAZIRI MKUU: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu swali la Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Naibu Spika, kama ambavyo nimeeleza awali kwamba masuala yote haya yanagusa maeneo mengi sana ambayo yanatakiwa ufuatiliaji wa kina na baadae 3 NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) nilieleza kwamba kila tukio linagusa Wizara kadhaa, kwa hiyo siwezi kusema kwamba katika Bunge hili nitakuja kuleta taarifa hiyo mpaka pale ambako nitakutana na Wizara, nijue wamefikia hatua gani, pia tutakutana na Mheshimiwa Spika ili tujue utaratibu mzima wa namna ya kupata hizo Hansard na kufanya mapitio. Tukijiridhisha na tukiona kwamba jambo hilo sasa linafaa kuletwa Bungeni na kwa kuwa liliazimiwa na Bunge, basi tutafanya maamuzi ya pamoja ya kuleta Taarifa hiyo Bungeni. (Makofi) NAIBU SPIKA: Ahsante sana. Waheshimiwa Wabunge, tutaendelea sasa na orodha. Mheshimiwa Jaku Hashim Ayoub, swali kwa Waziri Mkuu. MHE. JAKU HASHIM AYOUB: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana. Kwanza nimpongeze Mheshimiwa Waziri kwa umakini na utendaji wake na kilichonivutia zaidi anapotoka hapa akienda ofisini kwake haifiki hata dakika, watu anaokutana nao njiani anasalimiana nao ni jambo la kumpongeza sana Mheshimiwa Waziri bila kujali itikadi ya chama. Ninakupongeza sana, mara nyingi huwa nikikaa nje pale na nikienda kunywa chai ninakuona. (Makofi) Mheshimiwa Naibu Spika, Mheshimiwa Waziri Mkuu tunakaribiwa na Mwezi Mtukufu wa Ramadhani kama wiki mbili tu panapo majaaliwa tukifika, hali ya kusikitisha ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, sukari inahitajika kwa wingi matumizi yake. Hata wananchi wa Ruangwa na Peramiho wanahitaji sukari. Mwenyezi Mungu alitupa mtihani wa mvua, viwanda vyetu vya ndani havikuweza kuzalisha sukari ya kutosha na uchunguzi au harufu niliyoipata tunahitaji kama tani laki moja na ushee. (Makofi) Mheshimiwa Naibu Spika, jambo la kusikitisha kwa taarifa niliyo nayo ni kuwa mmetoa vibali vya tani 30,000 na baya zaidi kuna msemo Waislamu husema nguo ya Ijumaa hufuliwa Alhamisi na mvua hii pengine isikauke. Sasa hawa mliowapa vibali, sukari yao navyotegemea hata ikifika 4 NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) Ramadhani itakwisha, itawasaidia nini wananchi? Mnatumia utaratibu gani kuwapa vibali hawa watu, wanarudia ndiyo wale wale au na wengine? Kuna formula gani ili kuokoa hatua hii. Mheshimiwa Waziri Mkuu uko tayari kuleta watu angalau mwezi huu Mtukufu wa Ramadhani wakaingiza sukari kwa kipindi hiki ili kuokoa hii hali na janga hili lilivyo? Hii sukari mliyowapa vibali hata ikifika Ramadhani itakwisha, itasaidia nini kwa wananchi? (Makofi) NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Jaku, umeshauliza maswali manne tayari hapo uliposimama. Kwa hiyo, naomba umpe nafasi Mheshimiwa Waziri Mkuu aanze kujibu moja baada ya lingine. Mheshimiwa Waziri Mkuu. WAZIRI MKUU: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Jaku, Mbunge kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Naibu Spika, najua amezungumza mengi na yaliyotengeneza maswali mengi sana. jambo la msingi alilotaka kuzungumza hapa ni kupungua kwa sukari na mahitaji ya sukari nchini kwa sasa. Napenda niwathibitishie Watanzania kwamba Serikali iko macho na inajua maeneo gani yanahitaji kuboreshwa kulingana na mahitaji ambayo yanahitajika. Mheshimiwa Naibu Spika, kwa suala la sukari ni kweli nchi yetu hatuna uzalishaji wa kutosha wa sukari kutosheleza mahitaji ya Watanzania. Katika mwaka wa kilimo, mahitaji ya sukari nchini ni zaidi ya tani 420,000, lakini uzalishaji tulionao hapa nchini ni tani 320,000; kwa hiyo tunakuwa na mapungufu ya sukari inayohitajika ya tani laki moja na ikiwezekana zaidi kwa sababu ya ongezeko la watumiaji. Mheshimiwa Naibu Spika, kila mwaka tunao utaratibu wa kuagiza sukari na mwaka huu pia tumesahafanya hilo, tumeshaagiza sukari na mwaka huu tumeagiza sukari 5 NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) tunataka tuagize sukari ya tani 131,000 kwa mujibu wa takwimu zilizofanyiwa utafiti na Bodi ya Sukari, kati ya hizo tayari tumeshaagiza tani 80, kati ya tani 80 tayari zimeshaingia tani 35 na nyingine ziko bandarini. Hizi tani 35 tumeshaanza kuzigawa kwenye maeneo yote ya nchi ili ziweze kufika kwa wananchi ziweze kusaidia kupunguza gharama na bei. Mheshimwa Naibu Spika, pia kwa kuwa, tunakabiliwa na Mwezi Mtukufu wa Ramadhani ambapo watumiaji ni wengi, utaratibu wa kuagiza sukari zaidi kufikia malengo umeshaandaliwa. Watanzania tushirikiane kuwasihi wafanyabiashara ambao sasa hivi wamepandisha bei bila sababu na hii inaumiza sana Watanzania kwa sababu bei zilizopandishwa hazina umuhimu wowote kwa sababu uzalishaji tulionao na hii sukari pengo tunavyoleta nchini inataka tu bei zile ziendelee kuwa ambazo zinaweza kuhimilika na Watanzania wenzetu. Mheshimiwa Naibu Spika, iko mikakati ya kuongeza uzalishaji kufikia malengo. Natambua tuna viwanda vinne, Kagera Sugar, Kilombero, TPC na Mtibwa, tuna kiwanda cha tano kilichoko Tanzania Visiwani, Mahonda navyo pia vinasaidia uzalishaji. Mheshimiwa Naibu Spika, ili kuondoa tatizo la kuagiza sukari nje ya nchi, tumejiwekea utaratibu wa kukutana na wafanyabiashara wenye viwanda na kuwasihi kuongeza uzalishaji na tumeona jitihada kadhaa ambazo zinafanywa na wazalishaji. Bahati nzuri sana wiki moja iliyopita nilikuwa Mkoani Kilimanjaro, nimepata nafasi ya kutembelea kiwanda cha TPC ambacho kimeonesha mafanikio makubwa ya uzalishaji zaidi. Mwaka jana walizalisha tani 100,000 na sasa wameongeza tani 20,000, kwa hiyo, sasa hivi wamefikia uwezo wa kuzalisha tani 120,000 na msimu huu wa kilimo wataongeza tani nyingi zaidi, hivyo hivyo na viwanda vingine kama Kilombero na Mtibwa Sugar. Mheshimiwa
Details
-
File Typepdf
-
Upload Time-
-
Content LanguagesEnglish
-
Upload UserAnonymous/Not logged-in
-
File Pages182 Page
-
File Size-