Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) BUNGE LA TANZANIA ______________ MAJADILIANO YA BUNGE _____________ MKUTANO WA SITA Kikao cha Pili – Tarehe 1 Februari, 2012 (Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi) DUA Spika (Mhe. Anne S. Makinda) Alisoma Dua MASWALI Na. 16 Ujenzi Usiokidhi Viwango Hospitali ya Wilaya ya Himo- Moshi Vijijini na Mawenzi MHE. BETTY E. MACHANGU aliuliza:- Kwa kawaida Mkandarasi anayejenga hospitali au jengo lolote lile hupewa ramani za michoro ya majengo husika lakini ni jambo la kushangaza kwamba majengo ya hospitali ya Wilaya inayojengwa Himo imeonesha upungufu mwingi, kwa mfano, vyumba vya maabara vilitakiwa kuwa saba (7) lakini vimejengwa vyumba viwili (2), idara ya macho vilitakiwa vyumba vitatu (3) lakini kimejengwa chumba kimoja (1) na katika hospitali ya Mkoa, Mawenzi jengo la operation la hospitali hiyo limejengwa katika viwango duni:- (a) Je, Serikali itafanya nini kwa ujenzi huo ulio chini ya viwango uliokwishajengwa kwenye hospitali hizo mbili? (b) Je, ni hatua gani zinazochukuliwa kwa wahusika wa matatizo haya? NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU-TAMISEMI alijibu:- Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Betty Eliezer Machangu, Mbunge wa Viti Maalum, lenye sehemu (a) na (b) kama ifuatavyo:- (a) Mheshimiwa Spika, hospitali ya Wilaya - Himo inatokana na kupandishwa hadhi kwa kilichokuwa Kituo cha Afya cha Himo. Ujenzi unaoendelea unalenga kuongeza majengo katika Hospitali hiyo kwa kuzingatia viwango vilivyowekwa na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii. Ujenzi unafanyika kwa awamu ambapo awamu ya kwanza imegharimu shilingi milioni 175. Awamu ya pili itagharimu shilingi milioni 319 ikihusisha ujenzi wa jengo la Utawala, Huduma ya Mama na Mtoto, jengo la X-Ray na uzio wa choo cha nje. Kwa mantiki hiyo ujenzi utakapokamilika jengo litakuwa na vyumba saba vya maabara na vitatu vya Idara ya macho kwa kuzingatia ramani iliyotolewa na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii. 1 Mheshimiwa Spika, tarehe 25 Oktoba, 2011 Ofisi ya Waziri Mkuu - TAMISEMI ilifanya ziara katika hospitali ya Mkoa wa Mawenzi akiwemo Mheshimiwa Grace Kiwelu Mbunge wa Viti Maalum kutoka Mkoa wa Kilimanjaro. Ziara hiyo ilibaini upungufu kadhaa ukiwemo ujenzi wa jengo la upasuaji kutozingatia michoro iliyotolewa na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii na kusababisha jengo kufanyiwa marekebisho kukidhi vigezo vilivyowekwa na Wizara. Mshauri wa ujenzi huo alikuwa ni Wakala wa Majengo ya Serikali (TBA). Baada ya kubaini upungufu huo Ofisi ya Waziri Mkuu - TAMISEMI ilitoa maelekezo kwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Kilimanjaro kuhakikisha upungufu uliojitokeza unafanyiwa kazi haraka. Aidha, Ofisi ya Waziri Mkuu - TAMISEMI ilimuagiza Katibu Tawala huyo awasiliane na Katibu Mkuu, TAMISEMI ili awasiliane na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi ambayo wakala wa majengo iko chini yake. (b) Mheshimiwa Spika, kutokana na usimamizi mbovu wa Wakala wa Majengo ya Serikali (TBA) katika ujenzi wa jengo hilo, Wizara ya Ujenzi ilifahamishwa kuhakikisha hatua zinachukuliwa dhidi ya Mhandisi Mshauri aliyeshindwa kusimamia ujenzi wa jengo hilo kwa kuzingatia michoro iliyoidhinishwa na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii. MHE. BETTY E. MACHANGU: Mheshimiwa Spika, naomba kuuliza maswali mawili ya nyongeza kama ifuatavyo:- Kwa kuwa Serikali imejiwekea mkakati wa kuzifanya hospitali za Mikoa ziwe za rufaa na kwa kuwa hali ya kuzidiwa wagonjwa katika hospitali ya Mawenzi ni kubwa sana na kwa kuwa hospitali ya KCMC inazidiwa kutokana na ubovu wa tatizo la hospitali ya Mawenzi. Kwanza, je, Serikali iko tayari sasa kuharakisha mpango wake wa kuifanya hospitali ya Mawenzi kuwa ya rufaa katika mpango wake wa maendeleo 2012/2012? Swali la pili, kwa kuwa ujenzi wa wodi ya wanawake na majengo mengine ya hospitali ya Mawenzi umechukua muda kwa sababu ya kujengwa vipande vipande na kwa kuwa wanawake wengi wanaotaka kujifungua wanasongamana katika vitanda na hata kulala chini, Serikali haioni kwamba inapata hasara kwa sababu ya mfumuko wa bei yaani inflation na kwamba wanawake hawa hawatendewi haki? NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU- TAMISEMI: Mheshimiwa Spika, hili la hospitali za Mikoa kuwa hospitali za rufaa wala sio jambo la kujadiliana hapa kwa sababu kisera lilishakubalika kwamba hospitali zote za Mkoa ziwe hospitali za rufaa katika Mikoa kwa maana ya kwamba, tumeanzisha vituo vingi vya afya na zahanati na kadhalika. Kinachotakiwa tu hapa sasa ni kuingiza katika mipango ya Mkoa kwa maana ya Regional Consultative Committee ili tuweze kuona sasa operationalisation ya mawazo hayo mazuri ambayo anayazungumzia Mheshimiwa Betty Machangu. Mheshimiwa Spika, la pili hili analozungumza la wodi hii na kwa bahati mbaya sana wakati ule tulipokwenda pale katika hospitali ya Mawenzi tulikuwa tumemuomba Mheshimiwa Betty Machangu pia aweze kufika, lakini kwa kweli kwenye majukumu aliyokuwa nayo alishindwa kufika, l akini ni kweli kabisa kwamba tumeiona hiyo wodi ya akinamama, ni wodi ambayo ukiiangalia utafurahi wewe mwenyewe. Ni kubwa lakini nazungumza habari ya bilioni 12, sasa bilioni 12 na hela zinazopitishwa hapa ni hela kidogo sana, hela tunazojua kwamba zimepelekwa katika ile hospitali ni bilioni 1.3 sasa unaweza ukaona kwamba ni kweli kabisa anavyosema vifaa vitapanda bei lakini tatizo ninaloliona hapa ni ufinyu wa bajeti. Hata hivyo, tuko tayari kukaa na Mheshimiwa Betty Machangu tufikirie wote kwa pamoja kwamba tufanye nini. Tatizo lililoko la msingi pale ni kwamba, kuna miradi mingi pale, kwa hiyo inafika mahali sasa una-scatter sasa resources, kwa hiyo, unashindwa kufika mahali. Nadhani ana mawazo wazuri na tunaweza tukakaa naye, tukaona kwamba tupeleke labda upande mmoja ili tuweze kuondoa tatizo hilo na ndivyo tulivyoliona na Mheshimiwa Grace Kiwelu wakati tulipokwenda pale. MHE. AUGUSTINO L. MREMA: Mheshimiwa Spika, naomba kumwuliza Naibu Waziri kuhusu ujenzi wa hospitali ya Wilaya iliyopo Himo. 2 SPIKA: Hospitali gani tena? MHE. AUGUSTINO L. MREMA: Mheshimiwa Spika, Hospitali ya Himo ameitaja hapa kwenye swali la msingi la Betty Machangu, hiyo ni hospitali iliyoko katika Jimbo langu. Mwaka jana mwezi Januari nakumbuka niliuliza swali kuhusu ujenzi na kazi inayofanyika pale kwenye hospitali ya Himo na nikauliza hospitali hiyo itakamilika lini. Waziri alijibu kwamba ikifika mwezi wa Mei mwaka jana itakuwa imekamilika, lakini juzi nimepita pale nimekuta hakuna kinachoendelea, ningemwomba Waziri kama ana maelezo ni kwa nini hospitali ile haijaanza kazi? Swali la pili… SPIKA: Huwezi kuuliza maswali mawili Mheshimiwa, ni swali moja tu kwa sababu sio swali lako. NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU- TAMISEMI: Mheshimiwa Spika, anachosema Mheshimiwa Lyatonga Mrema ni kweli kabisa kwamba, ndivyo tulivyokuwa tumedhania, kile kituo ni kituo ambacho kimekuwa transform ed, ilikuwa sio kazi ambayo imeanza moja kwa moja, ni kwamba tulisema kituo hiki kibadilishwe matumizi, kiwe hospitali ya Wilaya. Pale kumekuwa kuna matatizo pia kwamba Mkandarasi na nafikiri labda ndiyo swali alilotaka kuuliza na hivi asubuhi, nimezungumza na DED na nikamwambia kwamba ni hatua gani zinazochukuliwa. Kesho watakwenda kwenye PMU watazungumzia zaidi kwa undani hii hali ya kusuasua ambayo Mheshimiwa Lyatonga Mrema anaizungumzia hapa. Matumaini yangu ni kwamba, sasa Halmashauri kwa kutumia sheria na taratibu zilizowekwa watatafakari upya mkataba ambao wameingia pale kwa sababu ni kweli kama anavyosema kwamba speed inayokwenda pale ni ndogo na kwa hiyo, kushindwa kufikia lengo lile la kwamba sasa kituo kiwe kimeanza kazi. MHE. ANNA K. MALECELA: Mheshimiwa Spika, nashukuru kupata nafasi. Namwuliza Mheshimiwa Naibu Waziri. Kwa kuwa nimekuwa nafuatilia sana ziara yake aliyokuwa anaifanya kat ika baadhi ya Mikoa na kwamba yeye mwenyewe aliona kwamba majengo mengi yanajengwa chini ya kiwango na akawa anafoka. Je, Serikali leo inatoa tamko gani zito hapa ili hii tabia ya kujenga majengo mengi chini ya kiwango iachwe mara moja? NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU- TAMISEMI: Mheshimiwa Spika, kwanza nimshukuru sana Mheshimiwa Spika kwamba amekuwa anafuatilia na pia nimetoka kule kwako, wanakusalimia. (Kicheko/Makofi) Mheshimiwa Spika, Wizara yetu hapa tulipofikia hatutaki hata siku moja tumsikilize Mbunge anazungumza hapa halafu tukampuuza, hatutampuuza kabisa Mbunge yeyote. Hiyo tunasema kabisa, Mbunge yeyote atakayeleta habari yoyote nataka niwathibitishie, hatutampuuza hata kidogo. Ni kweli kabisa kama anavyosema, hali tuliyoikuta katika field kule inasikitisha na inatisha. Hela zilizopitishwa hapa za TAMISEMI zilikuwa trilioni 2.5 ndizo zilizopelekwa kule, kwa nchi changa kama Tanzania ni kweli kabisa kwamba fedha hizi ni nyingi sana. Mheshimiwa Spika, sasa yeye anataka kujua kwamba tunasema nini. Wale watu wote ambao wamehusika na mambo haya ya ujenzi ambayo ni hafifu, tumetoa maelekezo kwa Tawala za Mikoa kwa upande wa Sekretarieti za Mikoa na tumewaandikia barua na tumeipeleka ripoti hiyo kwa Mheshimiwa Waziri Mkuu na Mheshimiwa Mkuchika yuko hapa anasikia tunazungumza habari hiyo, wote wale ambao wamehusika na ujenzi hafifu tutawachukulia hatua kwa misingi ya sheria zilizowekwa. Hilo ndiyo tamko letu. (Makofi) SPIKA: Ahsante. Nilitaka kuwaeleza tofauti ya maswali ya nyongeza wanayouliza wengine na hili alilouliza Mheshimiwa Anna Kilango. Yeye amezungumzia jumla sasa, angeweza kuuliza habari ya Same kule, huyu hakujianda juu ya Same, lakini la ujumla analiweza kwa sababu ndiyo Sera yenyewe. Kwa hiyo, ndiyo utofauti wa maswali ya nyongeza. Nakushukuru kwa hilo swali. (Makofi) 3 Na. 17 Fedha za CDCF Katika Halmashauri za Tanzania Zanzibar MHE. AHMED JUMA NGWALI aliuliza:- Mbunge
Details
-
File Typepdf
-
Upload Time-
-
Content LanguagesEnglish
-
Upload UserAnonymous/Not logged-in
-
File Pages103 Page
-
File Size-