Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) BUNGE LA TANZANIA _____________ MAJADILIANO YA BUNGE ______________ MKUTANO WA NNE Kikao cha Thelathini na Nane – Tarehe 7 Agosti, 2006 (Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Spika (Mhe. Samuel J. Sitta) Alisoma Dua HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na:- NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA MASOKO:- Hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Viwanda, Biashara na Masoko kwa mwaka wa Fedha 2006/2007. MHE. HERBERT J. MNTANGI (K.n.y. MHE. WILLIAM H. SHELLUKINDO) - MWENYEKITI WA KAMATI YA UWEKEZAJI NA BIASHARA:- Maoni ya Kamati ya Uwekezaji na Biashara Kuhusu Utekelezaji wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Masoko kwa Mwaka wa Fedha uliopita, pamoja na Maoni ya Kamati Kuhusu Makadirio ya Matumizi ya Wizara hiyo kwa mwaka 2006/2007. MHE. LUCY F. OWENYA - MSEMAJI MKUU WA KAMBI YA UPINZANI KWA WIZARA YA VIWANDA, BIASHARA NA MASOKO: Maoni ya Kambi ya Upinzani Kuhusu Utekelezaji wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Masoko kwa Mwaka wa Fedha uliopita, pamoja na Maoni Kuhusu Makadirio ya Matumizi ya Wizara hiyo kwa mwaka 2006/2007. MASWALI NA MAJIBU Na. 355 Umuhimu wa Barabara ya Mbelei – Mayo-Bumbuli MHE. WILLIAM H. SHELLUKINDO aliuliza:- 1 Kwa kuwa, zipo barabara Wilayani Lushoto na hasa Jimbo Bumbuli ambazo zimethibitika kuwa ni za muhimu sana kiuchumi kama ilivyo kwa barabara ya kutoka Mbelei- Kwesiwe-Baga-Mgwashi-Mayo-Bumbuli yenye urefu wa kilomita 50 inayopita kwenye maeneo yanayolimwa Mazao kama Chai, Kahawa, Nyanya, Viazi, Vitunguu, Pilipili, Mahindi, Maharage na kadhalika:- (a) Je, barabara hiyo itatengenezwa lini na kufikia kiwango cha changarawe? (b) Je, Serikali itaitembelea lini barabara hiyo ili ithibitishe na kuona umuhimu wake katika uchumi wa Jimbo la Bumbuli? (c) Je, Serikali itakubaliana nami kwamba, sasa kuna umuhimu wa kukubali kuipandisha daraja barabara hiyo iwe ya Mkoa na kuipunguzia Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto mzigo huo mzito? WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA alijibu:- Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la Mheshimiwa William Shellukindo, Mbunge wa Bumbuli, lenye sehemu (a), (b) na (c) kama ifuatavyo:- (a) Mheshimiwa Spika, ninakubaliana na Mheshimiwa Mbunge kwamba barabara ya Mbelei-Kwesiwe-Baga-Ngwashi-Mayo hadi Bumbuli yenye urefu wa kilomita 50 ni muhimu sana kiuchumi kwa kuzingatia kwamba inapita katika maeneo ya kilimo cha mazao ya biashara na chakula na pia sehemu zenye huduma za Taasisi mbalimbali kama vile Zahanati za Mbelei, Baga-Mwashi na Hospitali teule ya Bumbuli na Kituo cha Utafiti cha Chuo Kikuu cha Sokoine katika msitu wa Mazumbai. Barabara hii ipo katika mpango wa matengenezo kwa kiwango cha changarawe kama ifuatavyo:- Kutoka Mbelei-Kwesiwe-Baga-Mgwashi yenye urefu wa kilomita 26 ipo katika mpango wa matengenezo kwa kiwango cha changarawe chini ya Mpango wa Kilimo na Uboreshaji wa Masoko (Agriculture System Marketing Development Programme) ikiwa ni msaada wa fedha kutoka African Development Bank (ADB). Pia matengenezo makubwa yamefanyika katika sehemu ya Galambo-Bumbuli yenye urefu wa kilomita 5.0, matengenezo hayo yamefanywa na Wakala wa Barabara Mkoa wa Tanga. Sehemu iliyobaki ni Mgwashi –Galambo yenye urefu wa kilomita 19.0 ambazo zipo katika makisio ya mpango wa bajeti ya Halmashauri kwa mwaka wa fedha 2006/2007. Kiasi cha shilingi milioni 8 kimetengwa kwa ajili ya barabara hii. (b) Mheshimiwa Spika, Serikali kwa kupitia Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto mpaka sasa imekwishatambua umuhimu wa barabara hiyo kiuchumi na kijamii, ndiyo maana Halmashauri imependekeza sehemu ya Mbelei-Kwesiwe-Baga- Mgwashi yenye urefu wa kilomita 26 kufanyiwa matengenezo makubwa kwa msaada wa fedha kutoka African Development Bank, kwa kupitia Mradi wa “Agriculture System Marketing 2 Development Programme (ASMDP)” kwa gharama ya shilingi milioni 700. Aidha, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa inakubali kabisa kwamba itatembelea eneo hilo la barabara wakati wa kukagua shughuli za barabara zinazopatiwa fedha kutoka Mfuko wa Barabara katika mwaka wa fedha wa 2006/2007. (c) Mheshimiwa Spika, barabara ya Mbelei-Kwesiwe-Baga-Mgwashi- Mayo- Bumbuli ni miongoni mwa barabara sita za Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto ambazo zimependekezwa kupandishwa daraja kutoka ngazi ya Wilaya na kuwa katika ngazi ya Mkoa. Barabara hizo zilipendekezwa katika kikao cha Bodi ya Barabara ya Mkoa kilichofanyika tarehe 26/9/2003 kama ifuatavyo:- (a) Mlalo – Umba (Mng’aro) kilomita 25.9; (b) Mbelei – Mgwashi-Bumbuli kilomita 50.0; (c) Dochi- Mombo kilomita 20.0; (d) Mlalo- Mlalo-Milingano – Mshewa kilomita 78.1; (e) Soni – Mponde kilomita 14.0; na (f) Vuga – Mponde – Wena Kilomita 22.5. Mheshimiwa Spika, suala la kuzipandisha daraja barabara hizi linashughulikiwa na Wizara ya Miundombinu ili kuona kama upo uwezekano wa kuzihudumia katika ngazi ya Mkoa. Majibu yatakapokuwa tayari, hasa baada ya kupitishwa kwa Sheria inayotarajiwa kuwasilisha hapa Bungeni kupendekeza baadhi ya barabara kuwa za Mkoa. Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto itajulishwa ili iweze kuzikabidhi kwa Wakala wa Barabara wa Mkoa na kuweza kupunguziwa mzigo wa kuzihudumia. Na. 356 Majengo ya Mahakama ya Mwanzo Gairo MHE. AHMED M. SHABIBY aliuliza:- Kwa kuwa, jengo la Mahakama ya Mwanzo Gairo lilithibitishwa na Msajili wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam tarehe 10/3/2006 kuwa haifai kwa matumizi ya Kimahakama; na kwa kuwa, Jaji Kiongozi wa Kanda ya Dar es Salaam alithibitisha pia kuwa, jengo hilo halifai na kwamba, lilijengwa kwa udongo mwaka 1926 likiwa kama Kanisa:- (a) Je, Serikali haioni kuwa, kuna sababu ya kujenga jengo jingine jipya? (b) Je, Serikali haioni kuwa, inahatarisha maisha ya watumishi wa Mahakama na wadau wake? WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA alijibu:- Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Ahmed Shabiby, Mbunge wa Gairo, lenye vipengele (a) na (b) kwa pamoja kama ifuatavyo:- 3 Mheshimiwa Spika, majengo mengi ya Mahakama, hasa Mahakama za Mwanzo, ni machakavu na inawezekana kuwa mengine yanahatarisha maisha ya watumishi na wateja wanaofika kupata huduma za Mahakama. Serikali inatambua hatari hiyo na ndio sababu imeanzisha Mpango Endelevu wa miaka mitano wa ujenzi na ukarabati wa majengo ya Mahakama za Mwanzo. Mpango huu ulioanza Mwaka wa Fedha 2004/2005 utatekelezwa kwa awamu hadi kufikia Mwaka wa Fedha wa 2008/2009. Vilevile kupitia fedha za ufadhili za Maboresho ya Sekta ya Sheria kasi ya ujenzi wa Mahakama za Mwanzo itaongeza. Mahakama ya Mwanzo, Gairo ni moja ya majengo yaliyoingizwa kwenye mpango huu wa miaka mitano ya ujenzi na ukarabati wa Mahakama za Mwanzo. MHE. AHMED M. SHABIBY: Mheshimiwa Spika, ahsante sana kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza. Kwa kuwa, Mahakama ya Mwanzo ya Gairo, inafanana na Mahakama za Mwanzo za Idibo, Chakwale na Nungu, je, hizo nazo zipo katika Mpango wa ujenzi wa miaka mitano? Ahsante. WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA: Mheshimiwa Spika, mpango huu unahusu Mahakama zote za Mwanzo, na kwa hivyo Mahakama alizozitaja nazo zinahusika. SPIKA: Naona leo Waheshimiwa Wabunge hawakuchangamka kabisa. Na. 357 Madai ya Walimu MHE. DIANA M. CHILOLO aliuliza:- Kwa kuwa, wapo walimu ambao hawajalipwa madai yao kama vile ya matibabu, nauli wakati wa likizo na kadhalika, kutokana na sababu ya kupotea kwa viambatanisho vya madai yao; na kwa kuwa, viambatanisho hivyo vimepotelea kwenye majalada mikononi mwa mwajiri:- Je, Serikali haioni kwamba, kuwanyima walimu madai yao ni kutowatendea haki? NAIBU WAZIRI WA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI (MHE. MWANTUMU B. MAHIZA) alijibu:- Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Elimu na Mafunzo ya ufundi, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Diana Mkumbo Chilolo, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Spika, Wizara yangu imekuwa ikilipa madai ya walimu wa Shule za Sekondari, Vyuo vya Ualimu na Wakaguzi wa Shule yakiwa na viambatanisho. Nakubaliana na Mheshimiwa Mbunge kwamba kumnyima mwalimu malipo ya madai 4 yake, endapo ni kweli kuwa viambatanisho vya madai vimepotea mikononi mwa mwajiri ni kutomtendea haki. Mheshimiwa Spika, kwa kuwa madai huwa yana mazingira tofauti, tunawaomba wenye madai ya aina hiyo watuletee ili tuyafanyie kazi. MHE. DIANA M. CHILOLO: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali moja la nyongeza. Nashukuru sana kwa majibu mazuri ya Naibu Waziri. Kwa kuwa pamoja na kulipa madeni ya walimu ya muda mrefu. Vilevile Serikali bado inazalisha madeni mapya badala ya kwenda sambamba na wakati, pale walimu wanapohitaji haki zao. Je, Serikali ni lini basi itaacha tabia ya kuzalisha madeni haya ili walimu sasa wawe wanaenda sambamba kazi na dawa? (Makofi) NAIBU WAZIRI WA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI (MHE. MWANTUMU B. MAHIZA): Mheshimiwa Spika, ni kweli Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, haina namna ya kuepuka kuzalisha madai. Kwa sababu kila mwaka tunaajiri walimu na kila mwaka walimu wanakwenda likizo. Kwa hiyo, sisi tutaendelea kupokea na kwa kadri Mwenyezi Mungu atakavyotujalia uwezo tutayalipa madeni hayo, kwa sababu ni haki zao. MHE. WILLIAM M. NGELEJA: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa kunipa nafasi hii. Mheshimiwa Spika, pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Naibu Waziri, nilikuwa na swali moja dogo la nyongeza. Kwa kuwa Serikali imekuwa ikiahidi kwa muda mrefu na hata katika Mkutano huu wa Bajeti kwamba malipo ya walimu ambayo ni stahili zao yatalipwa ndani ya mwaka huu wa fedha 2006/2007; na kwa kuwa tunafahamu kwamba mwaka fedha utaishia mwezi Juni, mwaka kesho. Je, lini Serikali itakuwa imeishawalipa walimu madai yao ambayo yamekuwepo na yameishathibitishwa ili swali hili lisije likaendelea kujitokeza mara kwa mara katika
Details
-
File Typepdf
-
Upload Time-
-
Content LanguagesEnglish
-
Upload UserAnonymous/Not logged-in
-
File Pages169 Page
-
File Size-