Tarehe 15 Aprili, 2020

Tarehe 15 Aprili, 2020

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA __________ MAJADILIANO YA BUNGE ___________ MKUTANO WA KUMI NA TISA Kikao cha Tisa – Tarehe 15 Aprili, 2020 (Bunge Lilianza Saa Nane Mchana) D U A Spika (Mhe. Job Y. Ndugai) Alisoma Dua SPIKA: Mheshimiwa Wabunge, tukae, Katibu! NDG. LAWRANCE MAKIGI - KATIBU MEZANI: HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI:- Hati zifuatazo ziliwasilishwa mezani:- NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI UTUMISHI NA UTAWALA BORA: Hotuba ya Bajeti ya Ofisi ya Rais (Utumishi na Utawala Bora) kwa mwaka wa fedha 2020/2021. MHE. MWANNE I. MCHEMBA - MAKAMU MWENYEKITI WA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA UTAWALA NA SERIKALI ZA MITAA: Maoni ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa kuhusu Utekelezaji wa Majukumu ya Ofisi ya Rais (Utumishi na Utawala Bora) kwa mwaka wa fedha 2019/2020 pamoja na Maoni ya Kamati kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi hiyo kwa mwaka wa fedha 2020/2021. 1 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) MHE. RUTH H. MOLLEL - MSEMAJI MKUU WA KAMBI RASMI YA UPINZANI BUNGENI KWA OFISI YA RAIS UTUMISHI NA UTAWALA BORA: Maoni ya Kambi Rasmi ya Bungeni kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi ya Rais (Utumishi na Utawala Bora) kwa mwaka wa fedha 2020/2021. MASWALI NA MAJIBU (Maswali yafuatayo yameulizwa na kujibiwa kwa njia ya mtandao) Na. 74 Idadi ya Watu Wenye Ulemavu wa Ngozi Nchini MHE. VENANCE M. MWAMOTO aliuliza:- Je, kuna watu wangapi wenye ulemavu wa ngozi nchini na ni Wilaya gani inaongoza kwa kuwa na idadi kubwa zaidi? WAZIRI MKUU alijibu:- Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Venance Mwamoto, Mbunge wa Kilolo kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa taarifa ya Sensa ya Watu na Makazi iliyofanyika nchini mwaka 2012, idadi ya watu wenye ulemavu wa ngozi nchini ni 16,127 ambapo wanaume ni 8,872 na wanawake ni 7,255. Aidha, kwa mujibu wa taarifa hiyo, mikoa yenye idadi kubwa ya watu wenye ulemavu wa ngozi ni Dar es Salaam yenye watu 1,637; Mwanza 1,063; na Dodoma 1,034. Hata hivyo, taarifa inayoonesha mchanganuo wa watu wenye ulemavu wakiwemo wenye ulemavu wa ngozi kiwilaya haikuandaliwa. 2 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) Na. 75 Hitaji la Vifaa Tiba Kituo cha Afya Igoma MHE. KEMILEMBE J. LWOTA aliuliza:- Mheshimiwa Spika, Serikali imefanya jitihada kubwa katika ujenzi na uboreshaji wa Sekta ya Afya kwa kujenga Vituo vya Afya kikiwemo Kituo cha Afya Igoma:- Je, ni lini Serikali itapeleka vifaa tiba kama vile X-ray, Ultrasound na vifaa vingine vya kiuchunguzi kama ilivyoahidi? WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA alijibu:- Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Kemilembe Julius Lwota, Mbunge wa Viti Maalum kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Spika, Kituo cha Afya Igoma kilipatiwa kiasi cha shilingi milioni 400 kwa ajili ya ukarabati na upanuzi na kazi hiyo imekamilika. Serikali inaendelea kuvipatia vifaa tiba Vituo vya Afya vilivyokamilika ambapo hadi sasa jumla ya shilingi bilioni 27.11 zimetumika. Kituo cha Afya Igoma kitapewa kipaumbele cha kupatiwa vifaa katika awamu zinazofuata ili kukiwezesha kutoa huduma. Na. 76 Kupandisha Hadhi Barabara ya Getifonga, Mabogini, Chekereni na Kahe MHE. ANTONY C. KOMU aliuliza:- Mheshimiwa Spika, barabara ya kutoka Gatefonga, Mabogini, Chekereni, Kahe mpaka Wilaya ya Mwanga ni muhimu kwa uchumi wa Mkoa wa Kilimanjaro lakini haipitiki kipindi cha mvua. 3 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) Je, ni kwa nini Serikali haikubaliani na mapendekezo ya RCC Kilimanjaro ya kuipandisha hadhi barabara hii kwa kuwa chini ya TANROADS? WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA alijibu:- Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Antony Calist Komu, Mbunge wa Moshi Vijijini kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Spika, kwa kuzingatia Sheria ya Barabara Na.13 ya mwaka 2007 Kifungu cha 12(2)- (3), barabara ya Gatefonga, Mabogini, Chekereni na Kahe haina sifa ya kusimamiwa na TANROADS. Hivyo, barabara hiyo itaendelea kufanyiwa matengenezo kupitia Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) ili kuhakikisha inapitika wakati wote. Na. 77 Ujenzi wa Barabara ya Itoni - Lusitu MHE. EDWARD F. MWALONGO aliuliza:- Je, ni lini Serikali itatekeleza ahadi yake ya kujenga kwa kiwango cha lami barabara ya Itoni – Lusitu? WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO alijibu:- Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Edward Franz Mwalongo, Mbunge wa Njombe Mjini kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Spika, Upembuzi yakinifu, usanifu wa kina na uandaaji wa nyaraka za zabuni za Barabara ya Itoni – Ludewa – Manda (kilomita 211.42) umekamilika tangu mwaka 2016 kwa barabara yote. 4 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) Mheshimiwa Spika, kwa kutambua umuhimu wa barabara hii, na kwa vile barabara ya Itoni – Ludewa – Manda (kilomita 211.42) ni ndefu, Serikali iliamua kuijenga kwa awamu. Awamu ya kwanza ni sehemu ya Lusitu – Mawengi (kilomita 50) ambayo ni sehemu korofi. Sehemu hii inajengwa kwa kiwango cha zege la saruji na ujenzi umefikia asilimia 42. Mradi huu wa kilomita 50 za kwanza umepangwa kukamilika tarehe 30 Oktoba, 2020. Mheshimiwa Spika, awamu inayofuata ni ujenzi wa sehemu ya Itoni – Lusitu (kilomita 50) kwa kiwango cha lami. Katika mwaka wa fedha 2020/2021, mradi huu umeombewa shilingi bilioni sita kwa ajili ya kuanza ujenzi. Na. 78 Hitaji la Mahakama ya Wilaya – Mkalama MHE. ALLAN J. KIULA aliuliza:- Mheshimiwa Spika, wananchi wa Jimbo la Iramba Mashariki wanasafiri umbali mrefu na pia kutumia gharama kubwa kufuata huduma ya Mahakama ya Wilaya iliyopo Kiomboi na baadhi yao hukata tamaa na hivyo hupoteza haki zao:- Je, ni lini Mahakama ya Wilaya itajengwa Mkalama kama ilivyoahidiwa Bungeni mwaka 2019? WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA alijibu:- Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Allan Joseph Kiula, Mbunge wa Iramba Mashariki kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Spika, uhaba wa majengo ni moja ya changamoto inayoikabili Mahakama ya Tanzania. Mahitaji ya majengo ya kuendeshea shughuli za Mahakama hapa nchini ni makubwa. Kwa msingi huo, Mahakama imejiwekea 5 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) utaratibu wa kujenga majengo haya kwa awamu kulingana na mpango wa ujenzi na upatikanaji wa fedha. Mheshimiwa Spika, ujenzi wa jengo la Mahakama ya Wilaya Mkalama ni miongoni mwa Majengo ya Mahakama za Wilaya 33 ambayo yatajumuisha Mahakama za Mwanzo katika jengo moja. Ujenzi wa majengo haya umepangwa kuanza mwezi Juni na kukamilika mwezi Disemba, 2020 kwa ufadhili wa Benki ya Dunia. Kwa sasa Mahakama ipo katika hatua za mwisho kukamilisha taratibu za awali ili ujenzi wa majengo hayo uanze kwa muda kama ilivyo katika mpango wa Mahakama. Mheshimiwa Spika, tayari Mshauri Elekezi amefanya mapitio ya michoro na ujenzi unatarajiwa kuanza kama ilivyopangwa. Hivyo, naendelea kumwomba Mheshimiwa Mbunge kuwa na subira ili jengo hili likamilike ambalo litatatua changamoto alizozitaja kwenye swali lake la msingi. Na. 79 Tatizo la Ugonjwa wa Figo MHE. MGENI J. KADIKA aliuliza:- Mheshimiwa Spika, ugonjwa wa figo unakua kwa kasi kubwa sana katika nchi yetu ya Tanzania:- Je, ni mkoa gani katika Mikoa yote Tanzania Bara na Visiwani unaongoza kwa kuwa na wagonjwa wengi wa figo? WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO alijibu:- Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Mgeni Jadi Kadika, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Spika, ugonjwa wa figo husababishwa kwa kiasi kikubwa na magonjwa yasiyoambukiza. Kulingana 6 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) na Utafiti ulioitwa Community Base Survey to assess prevalence of kidney diseases wa mwaka 2013 uliofanyika katika maeneo ya Kaskazini Mashariki ambayo ilihusisha Mikoa ya Kilimanjaro, Arusha, Tanga na Morogoro pamoja na Utafiti uliofanyika mwaka 2015 ulihusisha Mkoa wa Pwani na Dar es Salaam ulionesha asilimia 44 unasababishwa na ugonjwa wa kisukari na shinikizo la damu linachangia asilimia 34. Mheshimiwa Spika, utafiti huo uliofanyika katika Mikoa ya Kilimanjaro, Arusha, Tanga na Morogoro mwaka 2013 ulionyesha tatizo kuwa kubwa asilimia saba na takwimu za utafiti kwenye jamii uliofanyika Kisarawe na Dar es Salaam mwaka 2015 ulionesha tatizo kuwa kubwa kwa asilimia 12.4. Mheshimiwa Spika, magonjwa yasioambukiza husababishwa na mtindo usio bora wa maisha ikiwa ni pamoja na matumizi ya pombe kupita kiasi, matumizi ya tumbaku na bidhaa zake, matumizi ya chumvi ya mezani, kutokufanya mazoezi na kwa ujumla na lishe mbaya, mfano matumizi ya mafuta kupita kiasi. Viashiria vyote hivi huchangia kupata magonjwa ya shinikizo la damu na kisukari ambayo ndio husababisha zaidi ugonjwa wa figo. Mheshimiwa Spika, mtindo usiofaa wa maisha upo mjini na vijijini pamoja na mikoa yote ya Tanzania Bara na Visiwani. Tatizo hilo ni kubwa kwa Mkoa wa Dar es Salaam ambako takwimu za kitabibu zinaonyesha kuwa na wagonjwa 1,234 na mkoa wa pili kuwa na tatizo la wagonjwa wa figo wengi ni Mkoa wa Arusha wenye idadi ya wagonjwa 563 na Mkoa ambao una takwimu chache za wagonjwa wa Figo ni Simiyu wagonjwa 113. Mheshimiwa Spika, nitoe wito kwa wananchi kuendelea kufanya mazoezi kuepukana na magonjwa yasiyoambukiza. 7 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) Na. 80 Chanjo ya Saratani ya Shingo ya Kizazi MHE. MWATUM DAU HAJI aliuliza:- Mheshimiwa Spika, hivi karibuni Serikali ilianzisha mpango wa chanjo ya Saratani ya Shingo ya Kizazi kwa wasichana kuanzia umri wa miaka kumi na mbili:- Je, mafanikio gani yamepatikana kwenye mpango huo? WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO alijibu:- Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Mwatum Dau Haji, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Spika, Wizara ilianzisha chanjo ya HPV dhidi ya saratani ya mlango wa kizazi mwezi Aprili, 2018 kwa wasichana wa miaka tisa hadi 14. Katika kipindi hicho, chanjo hii ililenga kuhakikisha kuwa wasichana 643,383 wenye umri wa miaka 14, ambao wote ni walengwa wa huduma hii, wanapata chanjo kwa wakati. Aidha, kwa kipindi cha mwaka 2019, walengwa wa chanjo hii walikuwa wasichana wapatao 685,580. Mheshimiwa Spika, mwaka 2018 chanjo hii ilianzishwa na jumla ya wasichana 383,683 walifikiwa kwa dozi ya kwanza ya chanjo hii, sawa na asilimia 60 ya lengo la wasichana 643,383.

View Full Text

Details

  • File Type
    pdf
  • Upload Time
    -
  • Content Languages
    English
  • Upload User
    Anonymous/Not logged-in
  • File Pages
    263 Page
  • File Size
    -

Download

Channel Download Status
Express Download Enable

Copyright

We respect the copyrights and intellectual property rights of all users. All uploaded documents are either original works of the uploader or authorized works of the rightful owners.

  • Not to be reproduced or distributed without explicit permission.
  • Not used for commercial purposes outside of approved use cases.
  • Not used to infringe on the rights of the original creators.
  • If you believe any content infringes your copyright, please contact us immediately.

Support

For help with questions, suggestions, or problems, please contact us