NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA __________ MAJADILIANO YA BUNGE _______________ MKUTANO WA KUMI NA TISA Kikao cha Kumi na Sita – Tarehe 24 Aprili, 2020 (Bunge Lilianza Saa Nane Mchana) D U A Naibu Spika (Mhe. Dkt. Tulia Ackson) Alisoma Dua NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, tukae. Katibu. NDG. MOSSY LUKUVI - KATIBU MEZANI: HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na:- WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa mwaka wa fedha 2020/2021. MWENYEKITI WA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA HUDUMA NA MAENDELEO YA JAMII: Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii kuhusu utekelezaji wa majukumu ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa mwaka wa fedha 2019/2020 pamoja na Maoni ya Kamati kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa mwaka wa fedha 2020/2021. 1 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) MSEMAJI MKUU WA KAMBI RASMI YA UPINZANI BUNGENI WA WIZARA YA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Maoni ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa Mwaka wa Fedha 2020/2021. NAIBU SPIKA: Ahsante, Katibu. NDG. MOSSY LUKUVI - KATIBU MEZANI MASWALI NA MAJIBU (Maswali yafuatayo yameulizwa na kujibiwa kwa njia ya mtandao) Na. 143 Ujenzi wa Jengo la Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana MHE. STANSLAUS S. MABULA aliuliza:- Wilaya ya Nyamagana ambayo ni kongwe imeanza kujenga jengo la Wilaya takribani miaka 6 sasa:- Je, Serikali ina mpango gani wa kukamilisha jengo hili ili Mkuu wa Wilaya apate mahali pa kufanyia kazi zake kwa uhuru na eneo rafiki hata kwa watu wenye ulemavu? WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA alijibu:- Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Stanslaus Shing’oma Mabula, Mbunge wa Nyamagana, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Naibu Spika, ujenzi wa ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana ulianza katika mwaka wa fedha 2008/ 2009 chini ya Mhandisi Mshauri Wakala wa Majengo Tanzania - TBA kwa gharama ya Sh.1,836,843,148. Hadi Machi, 2020 2 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) kiasi cha Sh.1,714,812,276 kimetolewa na kutumika katika kazi za ujenzi. Ujenzi wa ofisi hii umekamilika na Mkuu wa Wilaya alikabidhiwa jengo tarehe 23/09/2019 na kuhamia rasmi tarehe 01 Oktoba, 2019. Na. 144 Kuzipandisha Hadhi Zahanati za Mji wa Tarime kuwa Vituo vya Afya MHE. ESTHER N. MATIKO aliuliza:- Zahanati nyingi zilizoko Halmashauri ya Mji wa Tarime zimekuwa zikihudumia wananchi wengi kutoka ndani ya Mji wa Tarime na wengine kutoka Jimbo la Tarime Vijijini na Wilaya ya Rorya, mfano Zahanati ya Gamasara iliyopo Kata ya Nyandoto inahudumia wananchi kutoka Kijiji cha Kongo na Kitere vya Wilaya ya Rorya na Vijiji vya Kewamba na Nyangisya vya Jimbo la Tarime Vijijini kwa zaidi ya 50% na zahanati hiyo ina upungufu mkubwa wa watumishi, dawa pamoja na vifaa tiba:- (a) Je, nini mkakati wa Serikali katika kujenga na kuzipandisha hadhi zahanati hizi kuwa vituo vya afya ili kukidhi mahitaji ya watu wa Tarime Mjini na Majimbo ya jirani? (b) Je, nini mpango wa Serikali katika kuhakikisha zahanati hizi zinakuwa na watumishi wa kutosha, vifaa tiba pamoja na dawa? WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA alijibu:- Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Esther Nicholas Matiko, Mbunge wa Tarime Mjini, lenye sehemu (a) na (b), kama ifuatavyo:- (a) Mheshimiwa Naibu Spika, Mpango wa Serikali ni kuimarisha huduma za afya ya msingi kwa kuhakikisha zahanati na vituo vya afya vinajengwa kwenye mamlaka za 3 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) Serikali za Mitaa ili kuwawezesha wananchi kupata huduma za afya katika umbali mfupi na kupunguza vifo hasa vinavyotokana na uzazi. Katika mwaka wa fedha 2020/2021, Serikali imepanga kujenga zahanati tatu (3) katika Halmashauri ya Mji wa Tarime kwa gharama ya shilingi milioni 150 ili kuboresha upatikanaji wa huduma za afya. Hivyo, mpango wa Serikali siyo kupandisha vituo vya zahanati kuwa vituo va afya badala yake imejielekeza katika kujenga zahanati na vituo vya afya katika mamlaka za Serikali za Mitaa. (b) Mheshimiwa Naibu Spika, kati ya mwaka wa fedha 2016/2017 hadi 2019/2020, Serikali imeajiri na kuwapanga watumishi 35 wa kada za afya katika Halmashauri ya Mji wa Tarime. Aidha, OR-TAMISEMI, imepata kibali cha kuajiri madaktari 610 ambao watapangwa kwenye vituo vya kutolea hduma za afya kwa kuweka kipaumbele katika vituo vyenye upungufu mkubwa wa watumishi. Na. 145 Migogoro ya Wakulima na Wafugaji Kilwa MHE. SELEMANI S. BUNGARA aliuliza:- Wafugaji katika Wilaya ya Kilwa wapo katika maeneo ambayo hayakupangwa kwa ufugaji ikiwemo Vijiji vya Nakiu, Kikole, Nanjirinji na Kiranjeranje hali inayosababisha migogoro ya wakulima na wafugaji:- Je, Serikali haioni sasa ni wakati muafaka wa kulishughulikia suala hili kabla halijaleta uvunjifu wa amani? WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA alijibu:- Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Selemani Said Bungara, Mbunge wa Kilwa Kusini, kama ifuatavyo:- 4 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) Mheshimiwa Naibu Spika, hatua zinazochukuliwa na Serikali katika kudhibiti uingizaji wa mifugo kiholela Wilayani Kilwa ni pamoja na kuendelea kukamilisha uandaaji wa Mipango ya Matumizi ya Ardhi ya Vijiji 60 vikiwemo Vijiji vya Nakiu, Kikole, Nanjirinji na Kiranjeranje. Aidha, limewekwa zuio la uingizaji wa mifugo kwenye vijiji pasipo kibali kutoka Halmashauri na kuondoa mifugo iliyoingia pasipo kufuata taratibu. Vilevile, Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa imekuwa ikitenga fedha ili kufanya mapitio ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi kwa Vijiji ambavyo mipango yake iliandaliwa zaidi ya miaka 10 iliyopita ili iweze kuendana na hali halisi ya sasa na kuepuka mwingiliano wa matumizi ya ardhi kwenye maeneo hayo. Na. 146 Kuboresha Vituo vya Afya – Ngara MHE. ALEX R. GASHAZA aliuliza:- Kituo cha Afya Nyamaga kinakabiliwa na changamoto ya miundombinu ikiwemo ukosefu wa jengo la utawala, jengo la upasuaji, jengo la X-Ray, jengo la wazazi na mochwari:- (a) Je, ni lini Serikali itatenga fedha kwa ajili ya kuboresha hospitali hiyo ikizingatiwa kuwa Wilaya ya Ngara haina Hospitali ya Wilaya? (b) Je, ni lini Serikali itatoa fedha ili kumalizia ujenzi wa Kituo cha Afya cha Nyakisasa, Kata ya Nyakisasa? WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA alijibu:- Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Alex Raphael Gashaza, Mbunge wa Ngara, lenye sehemu (a) na (b), kama ifuatavyo:- 5 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) (a) Mheshimiwa Naibu Spika, ili kuboresha huduma za afya Wilayani Ngara kuanzia mwaka wa fedha 2017/2018 hadi Machi 2020, Serikali imeipatia Halmashauri ya Wilaya ya Ngara kiasi cha shilingi milioni 690 kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa Vituo vya Afya Mabawe, Kiinga na Zahanati ya Nyakisasa. Aidha, katika mwaka wa fedha 2020/2021, Serikali imeweka kipaumbele cha ujenzi wa zahanati tatu (3) katika Halmashauri ya Wilaya ya Ngara utakaogharimu shilingi milioni 150. Serikali itaendelea kuzingatia na kuweka kipaumbele cha ujenzi na ukarabati wa miundombinu ya afya ikiwemo ukarabati wa Hospitali ya Nyamaga ambayo ndiyo Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Ngara kadri fedha zitakavyopatikana. Na. 147 Kujenga Kiwanda cha Samaki Kanda ya Ziwa MHE. LOLESIA J. BUKWIMBA aliuliza:- Mkoa wa Geita umepakana na Ziwa Victoria na Wananchi wa maeneo hayo hujishughulisha na uvuvi:- Je, Serikali ina mpango gani wa kujenga kiwanda cha samaki kwenye maeneo hayo ili kutoa fursa za ajira? WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA alijibu:- Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Lolesia Jeremiah Bukwimba, Mbunge wa Busanda, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali ina jukumu la kuweka mazingira wezeshi ili kuwezesha sekta binafsi kufanya shughuli za maendeleo ikiwemo kujenga viwanda. Tanzania ina viwanda kumi na nne (14) ambavyo huchakata samaki wastani wa tani 350.3 kwa siku. Uchakataji huo wa samaki unahusisha Ukanda wa Pwani ya Bahari ya Hindi, Ziwa Victoria na Ziwa Tanganyika. Kwa hivi sasa kuna viwanda vitano (5) Ukanda wa Pwani; viwanda nane (8) Ukanda wa Ziwa 6 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) Victoria; na kiwanda kimoja (1) na viwanda vidogo 34 vya kuhifadhi samaki hai Ukanda wa Ziwa Tanganyika. Samaki wanaochakatwa na viwanda hivyo ni pamoja na pweza, ngisi, kaa, kambamiti na kambakochi (Ukanda wa Pwani), sangara (Ziwa Victoria) na migebuka (Ziwa Tanganyika). Aidha, kuna maghala 33 ya kuhifadhi mazao hayo ya uvuvi yaliyokaushwa na maghala 23 ya kuhifadhi mazao yaliyogandishwa. Mheshimiwa Naibu Spika, mpango wa Serikali ni kuendelea kuwahimiza wavuvi na wafanyabiashara wa samaki Mkoa wa Geita kutumia fursa za viwanda vya kuchakata samaki vilivyoko Kanda ya Ziwa Victoria na kuhamasisha wawekezaji wa ndani na wa nje kujenga kiwanda cha kuchakata samaki nchini ukiwemo Mkoa wa Geita ili kuongeza fursa za ajira. Na. 148 Hitaji la Soko la Ndizi na Viazi Mviringo MHE. FREDY A. MWAKIBETE aliuliza:- Je, ni lini Serikali itatafuta soko la uhakika la zao la viazi mviringo na ndizi ikiwa ni pamoja na kujenga viwanda kwa ajili ya mazao hayo katika Halmashauri ya Busekelo? WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA alijibu:- Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Fredy Atupele Mwakibete, Mbunge wa Busekelo, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali inaendelea na uhamasishaji wa uwekezaji katika sekta ya viwanda nchini ili kuongezea thamani mazao ya kilimo vikiwemo viazi na ndizi. Lengo ni kukidhi mahitaji ya soko la ndani na nje ya nchi na pia kupata mapato zaidi. Katika zao la ndizi, kuna viwanda vya usindikaji vya Mazimba Company Ltd na Matunda Mema Tanzania Ltd vilivyopo Wilayani Karagwe Mkoani Kagera; Kibo 7 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) Alex Banana Wine Ltd kilichopo Wilayani Rombo, Mkoani Kilimanjaro; Kilimanjaro Banana Wine Ltd na Lumbugani Banana Enterprises Ltd vilivyopo Mwanjelwa katika Jiji la Mbeya; Kasuku Banana Wine Ltd kilichopo Wilayani Rungwe, Mkoani Mbeya na Arusha Banana Investment Ltd kilichopo Jijini Arusha. Hivyo, nawashauri wakulima wa ndizi kutoka Halmashauri ya Busekelo watumie fursa ya uwepo wa soko la viwanda hivyo kuuza mazao ya ndizi katika viwanda hivyo ili yaongezewe thamani.
Details
-
File Typepdf
-
Upload Time-
-
Content LanguagesEnglish
-
Upload UserAnonymous/Not logged-in
-
File Pages295 Page
-
File Size-