NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ____________ MAJADILIANO YA BUNGE ___________ MKUTANO WA KUMI Kikao cha Saba – Tarehe 7 Februari, 2018 (Bunge Lilianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Mwenyekiti (Mhe. Najma Murtaza Giga) Alisoma Dua MWENYEKITI: Waheshimiwa tukae, Katibu. NDG. THEONEST RUHILABAKE – KATIBU MEZANI: HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa mezani na:- WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Muhtasari wa Tamko la Sera ya Fedha (Mapitio ya Nusu mwaka 2017/2018) [Monetary Policy Statement (The Mid – Year Review 2017/2018)]. MHE. PETER J. SERUKAMBA – MWENYEKITI WA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA HUDUMA NA MAENDELEO YA JAMII: Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii kuhusu Shughuli za Kamati kwa mwaka 2017. 1 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) MHE. DANIEL E. MTUKA – K.n.y. MWENYEKITI WA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA MASUALA YA UKIMWI: Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Masuala ya UKIMWI kuhusu shughuli za Kamati kwa mwaka 2017. MWENYEKITI: Asante sana, Katibu tuendelee. NDG. THEONEST RUHILABAKE – KATIBU MEZANI: MASWALI NA MAJIBU Na. 84 Kuimarisha Huduma za Kijamii maeneo ya Vijiji MHE. CECIL D. MWAMBE (K.n.y MHE. UPENDO F. PENEZA) aliuliza:- Je, Serikali imeweka mikakati gani kuimarisha huduma za umeme, maji, afya na elimu katika maeneo ya vijijini ili kuongeza uzalishaji katika maeneo hayo na kuzuia wimbi la watu kukimbilia mijini? NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. JOSEPH G. KAKUNDA) alijibu:- Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Upendo Furaha Peneza, Mbunge wa Viti Maalum kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Mwenyekiti, ili kuongeza uzalishaji katika maeneo ya vijijini kwa kuimarisha huduma za umeme, maji, afya na elimu kwa lengo la kuzuia wimbi la watu kukimbilia mijini Serikali inatekeleza mikakati ifuatayo:- Mheshimiwa Mwenyekiti, moja, kuendelea kuboresha miundombinu ya shule za msingi na sekondari kwa kujenga na kukarabati madarasa, vyoo, maabara, mabweni, nyumba 2 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) za walimu, mabwalo, maktaba kwa kuzingatia mahitaji ya shule husika. Pia kujenga shule mpya katika maeneo ambayo shule za msingi na sekondari ziko mbali. aidha, mkakati wa madawati kwa kila shule, mkakati wa kujenga maabara kwa shule za sekondari na ajira mpya kwa walimu wapya wa michepuo ya sayansi ni miongoni mwa mikakati mahususi ya kuboresha sekta ya elimu. Mheshimiwa Mwenyekiti, mbili, kuendelea kuboresha miundombinu kwenye sekta ya afya ambapo kwa mwaka huu wa fedha pekee Serikali inajenga na kukarabati vituo vya afya 183 kwa gharama ya shilingi bilioni 81 vitakavyokamilika ifikapo tarehe 30/4/2018; ambapo shilingi bilioni 35.7 zimetolewa kwa ajili ya vifaa tiba. Ili kuongeza upatikanaji wa dawa Serikali imeongeza bajeti ya dawa kutoka shilingi bilioni 31 mwaka 2015/2016 hadi shilingi bilioni 260 mwaka huu wa fedha 2017/2018 ambazo zimesaidia sana kuongeza upatikanaji wa dawa mijini na vijijini. Pia kipaumbele maalum kimewekwa kuhusu kuongeza watumishi wa afya. Mheshimiwa Mwenyekiti, katika sekta ya nishati vijiji 7,873 kati ya vijiji 12,545 vya Tanzania Bara vitapatiwa umeme kuanzia mwaka huu wa fedha 2017/2018 hadi 2021. Umeme utasambazwa hadi kwenye maeneo yote ya shule, zahanati, vituo vya zfya, hospitali, mitambo ya maji, viwanda vidogo vidogo, viwanda vya kati na viwanda vikubwa. Aidha, huduma za maji zitaboreshwa zaidi kupitia utekelezaji wa awamu ya pili ya Programu ya Maendeleo ya Sekta ya Maji. Serikali pia itaendelea kuimarisha barabara vijijini ili kupunguza gharama za usafiri na usafirishaji hasa wa mazao kwenda kwenye soko. MWENYEKITI: Mheshimiwa Cecil Mwambe maswali ya nyongeza. MHE. CECIL D. MWAMBE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Nitakuwa nina maswali mawili ya nyongeza kama ifuatavyo:- 3 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la kwanza, pamoja na majibu ya Mheshimiwa Naibu Waziri kwamba Serikali imejipanga kuhakikisha wanafikisha umeme pamoja na maji hasa zaidi kwenye shule pamoja na sehemu zingine za kutolea huduma za kijamii, lakini ningependa kwa uhakika kabisa aseme kwamba ni lini Serikali itatimiza suala hili kwa sababu ni muda mrefu wamekuwa wakiliongea kila mara bila kuwa na tarehe ya uhakika kwamba itakapofika wakati fulani tutakuwa kwa kweli tumetekeleza, bado shule nyingi pamoja na vituo vya afya vinakosa huduma ya umeme pamoja na maji? Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, kuna vijiji vingi sana, kama anavyosema kwamba Serikali imeazimia kupeleka umeme kwenye vijiji vyote zaidi ya 7,000, lakini ukipita Jimbo la Ndanda kwa mfano Vijiji vya Nangoo, Liputu, Ndolo pamoja na Mdenga vinapitiwa na umeme wa msongo wa megawati 33. Sasa Waziri angetusaidia kutueleza ni lini kwa hakika Serikali sasa wako tayari kushusha umeme ule kwa ajili ya matumizi ya watu wale walioko chini ya hizi waya ambazo kwao ni hatari kwa maisha?Ahsante. MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri majibu kwa ufupi. NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. JOSEPH G. KAKUNDA): Mheshimiwa Mwenyekiti, katika maswali yake mawili ya nyongeza aliyouliza Mheshimiwa Cecil Mwambe, Mbunge wa Ndanda yeye mwenyewe ni shahidi anafahamu kwa sababu ameshiriki kupitisha bajeti hapa anajua mipango ya Serikali ilivyo. Sina shaka kwamba anatambua kwamba ahadi iliyoko kwenye Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano inaendelea kutekelezwa vizuri na tuna uhakika vijiji vyote nilivyovitaja kwenye jibu la msingi vitapata umeme pamoja na vitongoji vyake kama ambavyo Wizara ya Nishati imeahidi, na mikakati iko wazi na yeye mwenyewe Mheshimiwa Mbunge ni shahidi. Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu suala la maji, Mheshimiwa Waziri wa Maji ametoa ahadi hapa Bungeni 4 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) kuhusu kutekeleza awamu ya pili ya Programu ya Maendeleo ya Sekta ya Maji, na hii itaongezeka kasi zaidi pale ambapo tutaanza kutekeleza miradi ya maji vijijini kupitia ile Wakala wa Maji Vijijini ambao utafanya kazi sawasawa na REA inavyofanya kazi. Kwa hiyo, ndugu yangu Mwambe ondoa shaka katika swali lako la kwanza. Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, huu umeme ambao umepita kwenye vijiji alivyovitaja na msongo anaujua ameutaja, mimi kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri wa Nishati namuahidi kwamba mikakati ya Serikali itatekelezwa na wanavijiji aliowataja hao watapata umeme. MWENYEKITI: Ahsante, Mheshimiwa Lubeleje. MHE. GEORGE M. LUBELEJE: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana kwa kunipa nafasi ili na mimi niulize swali moja la nyongeza. Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuwa katika mipango yote ya kujenga shule za sekondari, shule za msingi, zahanati, vituo vya afya tunasahau sana huduma za maji, umeme pamoja na afya. Sasa nataka niulize swali kwa Mheshimiwa Waziri na bahati nzuri sana Mheshimiwa Jafo, Waziri wa TAMISEMI Mpwapwa anaifahamu vizuri sana. Katika bajeti ya mwaka 2018/2019; je, Serikali itakuwa tayari kutenga fedha kwa ajili ya kuhakikisha kwamba vituo vya afya, zahanati, shule za msingi, sekondari zote Jimbo la Mpwapwa zinapata huduma ya maji, umeme na afya? MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri majibu kwa ufupi. WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza naomba nimpongeze Naibu Waziri wangu kwa majibu mazuri sana aliyoyatoa hapo awali. Pia naomba kujibu swali la Mheshimiwa Lubeleje kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli ukiangalia hali halisi ya Jimbo la Mpwapwa changamoto hizo alizozungumza 5 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) Mheshimiwa Mbunge ni kweli, lakini hata hivyo tunachokifanya ni kuhakikisha kwamba tunawapatia huduma ya maji. Nafahamu kwamba Jimbo la Mpwapwa, Wilaya ya Mpwapwa ina changamoto kubwa. Tumeweza kuhakikisha kwamba; kwa mfano ile miradi sita na Mzee Lubeleje anafahamu tulivyokuwa kule Mima pamoja katika ujenzi wa Kituo cha Afya, mtandao wa maji ambao kwa muda mrefu wakandarasi walikuwa mradi huo walikuwa hawajaanza sasa wakandarasi wote sita wako site. Mheshimiwa Mwenyekiti, jukumu letu kubwa ni kwamba maji yale yatakapotoka katika jamii kuna water points tutazipeleka katika taasisi hizi za Umma kwa ajili ya kuhakikisha kwamba vituo hivyo vinapata maji. Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu mpango wa REA mnafahamu kwamba Wizara ya Nishati imezungumza wazi katika mpango wa REA Awamu ya Tatu kwamba itahakikisha katika sehemu zote za umma hasa vituo vya afya, shule pamoja na taasisi za dini zote zitapatiwa umeme kupitia katika mpango wa REA III. Isipokuwa katika hili niwaombe Waheshimiwa Wabunge katika ajenda hiyo lazima tuanze maandalizi ya awali ya kuweka wiring katika maeneo hayo, kwa sababu umeme ukishafika hapo ni lazima taasisi yenyewe iwe imeshafanya wiring ili kuhakikisha kwamba huduma hiyo inapatikana vizuri. Ahsante sana. MWENYEKITI: Ahsante sana Mheshimiwa, tunaendelea na Mheshimiwa Ally Seif Ungando Mbunge wa Kibiti sasa aulize swali lake. Na. 85 Mipango Miji MHE. ALLY S. UNGANDO aliuliza:- Maeneo ya Kibiti, Bungu, Jaribu Mpakani na Nyamisati katika Jimbo la Kibiti yanakuwa kwa haraka sana na kuongezeka kwa shughuli za kibinadamu. 6 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) (a) Je, Serikali ina mpango gani wa kupanga mipango miji? (b) Je, Serikali ina mpango gani wa kuweka mitandao na kuchonga barabara za mitaa? NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. JOSEPHAT S. KANDEGE) alijibu:- Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI naomba kujibu swali la Mheshimiwa Ally Seif Ungando, Mbunge wa Kibiti lenye sehemu (a) na (b) kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Mwenyekiti, Halmashauri ya Wilaya ya Kibiti kwa mujibu wa Sheria Namba 8 ya Mipango Miji ya mwaka
Details
-
File Typepdf
-
Upload Time-
-
Content LanguagesEnglish
-
Upload UserAnonymous/Not logged-in
-
File Pages319 Page
-
File Size-