Tarehe 7 Novemba, 2017 (B

Tarehe 7 Novemba, 2017 (B

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ____________ MAJADILIANO YA BUNGE ___________ MKUTANO WA TISA Kikao cha Kwanza – Tarehe 7 Novemba, 2017 (Bunge Lilianza Saa Tatu Asubuhi) WIMBO WA TAIFA (Hapa Wimbo wa Taifa Uliimbwa) D U A Spika (Mhe. Job Y. Ndugai) Alisoma Dua SPIKA: Hawa Wanyamwezi sijui wamefanyaje meza yangu hapa, inaelekea Wanyamwezi wanaroga. Katibu! NDG. STEPHEN N. KAGAIGAI – KATIBU WA BUNGE: KIAPO CHA UAMINIFU Mhe. Janeth Maurice Massaburi SPIKA: Katibu! NDG. STEPHEN N. KAGAIGAI – KATIBU WA BUNGE: TAARIFA YA SPIKA SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, katika Mkutano wa Nane wa Bunge, Bunge lilipitisha miswada mitatu ya sheria kama ifuatavyo; kwanza Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali Na.3 wa mwaka 2017 (The Written Laws Miscellaneous Amendments No. 3, Bill 2017). 1 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) Pili, Muswada wa Sheria ya Reli wa mwaka 2017 (The Railways Bill, 2017) na tatu Muswada wa Sheria ya Madaktari wa Meno na Wataalam wa Afya Shirikishi wa mwaka 2016 (The Medical Dental Allied Health Professionals Bill, 2016). Kwa taarifa hii, ningependa kuliarifu Bunge hili Tukufu kwamba tayari miswada hiyo imepata kibali cha Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kuwa sheria za nchi zifuatazo:- (i) Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali Na.3 ya mwaka 2017 (The Written Laws Miscellaneous Amendments No. 3 Act. No. 9 of 2017); (ii) Sheria ya Reli No. 10 ya mwaka 2017 (The Railways Act. No. 10 of 2017); na (iii) Sheria ya Madaktari, Madaktari wa Meno na Wataalam wa Afya Shirikishi No. 11 ya mwaka 2016 (The Medical Dental and Allied Health Professionals Act. No. 11 of 2017). Baada ya hayo Waheshimiwa Wabunge ningeomba tupunguze sauti kidogo, tumesharudi tena. Tukumbushane wale wote ambao tunaongea ongea, tafadhali. Ningependa kuchukua nafasi hii kuwatambulisha au kumtambulisha rasmi Katibu wa Bunge mpya Ndugu Stephen Kagaigai. (Makofi) Ahsante sana na kwa niaba yenu nimkaribishe sana Bungeni. Ningewaomba sana Waheshimiwa Wabunge wote tumpe Katibu wetu mpya kila aina ya ushirikiano. Lakini pili niwajulishe kwamba ndugu yetu tuliyekuwa naye kama Katibu wa Bunge Dkt. Kashililah yeye ameteuliwa na Mheshimiwa Rais kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Kilimo. (Makofi) Kwa maana hiyo hiyo, nichukue nafasi hii kumshukuru sana Dkt. Thomas Kashililah kwa kazi nzuri sana ambayo 2 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) tulifanya kwa pamoja katika Bunge hili, amefanya kazi kwa karibu miaka 30 katika taasisi hii na tumtakie kila la heri huko kilimo ambako ameenda na ninajua bado tutaendelea kufanya kazi kwa pamoja. (Makofi) Waheshimiwa Wabunge, basi baada ya taarifa hizo nitumie nafasi hii kuwakaribisha tena Dodoma kwa mara nyingine, Dodoma ni njema. Safari hii tumehakikisha Dodoma ni salama zaidi kuliko wakati mwingine wowote, msiwe na wasiwasi na Dodoma. Kwa hiyo, karibuni sana, hizo ndiyo taarifa rasmi. Taarifa zisizo rasmi ni mambo madogo madogo tu, wakati hampo hapa haya mambo Waziri wa Mambo ya Ndani anayajua vizuri zaidi, Mheshimiwa Mwigulu Nchemba, ule uwanja wa shamba la bibi kule Dar es Salaam kulikuwa na mechi moja hivi, Mheshimiwa Nchemba alikuwepo, nilimuona na Mheshimiwa Nape nadhani. Wale jamaa, aah! Wakachomoa lile goli kwa taabu sana. Yaani kwa shida basi ikawa draw! Nikamuona Mheshimiwa Nchemba anacheka meno nje, anashangilia draw. Basi yote mema, hayo ndiyo yaliyotokea katikati wakati hampo jamani. (Makofi/ Kicheko) Basi baada ya hapo, Katibu tunaendelea! NDG. STEPHEN N. KAGAIGAI – KATIBU WA BUNGE: HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa mezani na:- NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa unaokusudiwa kutekelezwa na Serikali kwa mwaka wa fedha 2018/2019. Mwongozo wa Kuandaa Mpango na Bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2018/2019. 3 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) SPIKA: Ahsante sana Naibu Waziri wa Fedha na Mipango. Tunaendelea na Mwenyekiti wa Kamati ya Bajeti, kwa niaba yake tafadhali. MHE. FLATEY G. MASSAY (K.n.y MWENYEKITI WA KAMATI YA BAJETI): Taarifa ya Mwenyekiti wa Kamati ya Bajeti juu ya Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa unaokusudiwa kutekelezwa na Serikali pamoja na Mwongozo wa Kuandaa Mpango na Bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2018/2019. MHE. MASOUD ABDALLAH SALIM (K.n.y MSEMAJI MKUU WA KAMBI RASMI YA UPINZANI WA WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO): Taarifa ya Msemaji Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani wa Wizara ya Fedha na Mipango juu ya Mpendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa unaokusudiwa kutekelezwa na Serikali pamoja na Mwongozo wa Kuandaa Mpango na Bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2018/2019. SPIKA: Ahsante sana. Katibu! NDG. STEPHEN N. KAGAIGAI – KATIBU WA BUNGE: MASWALI NA MAJIBU Na. 1 Ajira kwa Vijana Wanaomaliza Shule Nchini MHE. AIDA J. KHENAN aliuliza:- Je, Serikali ina mpango gani kwa vijana wanaomaliza shule za msingi, sekondari na vyuo kwa kuwawezesha kujiajiri? NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, VIJANA NA AJIRA alijibu:- 4 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri Mkuu, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Aida Joseph Khenan, Mbunge wa Viti Maalum kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Spika, Serikali inayo mikakati mbalimbali ambayo inawezesha vijana wahitimu wa ngazi mbalimbali za elimu kujiajiri. Mheshimiwa Spika, baadhi ya mikakati inayotekelezwa mahsusi kwa ajili ya vijana wanaomaliza elimu ya msingi na sekondari ni kama ifuatavyo:- (i) Ni kutekeleza Programu ya Kukuza Ujuzi nchini, ambapo kupitia programu hii tumeanzisha utaratibu maalum wa kutambua ujuzi uliopatikana kupitia mfumo usio rasmi na kuurasimisha kwa kutoa mafunzo ya muda mfupi kwa wale walio tayari kuhitaji na kuwapa vyeti vinavyotambulika. Utaratibu huu unawapa fursa vijana wetu kuendelea na mfumo rasmi wa mafunzo na pia kutambulika na waajiri au watoa kazi. (ii) Ni kuhamasisha vijana wanaomaliza shule za msingi na sekondari kujiunga katika vikundi vya kuzalisha mali na kusajiliwa rasmi kupitia Sheria ya Usajili wa NGO’s . Hadi sasa jumla ya vikundi vya vijana vya uzalishaji mali 10,200 vimekwishakusajiliwa. Aidha, ipo mikakati ya kuwawezesha wahitimu wa vyuo kujiajiri na kuajiriwa ambayo ni pamoja na:- (i) Ni kupitia Programu ya Kukuza Ujuzi nchini ambayo inawezesha vijana wahitimu wa vyuo kupata ujuzi wa kuwawezesha kujiajiri au kuajiriwa. Programu hii inatoa mafunzo ya uzoefu wa kazi kwa wahitimu (internship) ili kuwapatia uzoefu wa kazi. (ii) Serikali imerahisisha utaratibu wa uundaji wa makampuni kupitia BRELA hivyo vijana wengi wanaomaliza vyuo kuweza kuanzisha makampuni na biashara zinazoweza kuajiri vijana wengine. 5 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) Mheshimiwa Spika, pia ipo mikakati inayowawezesha wahitimu wa ngazi mbalimbali za elimu kujiajiri ambayo ni:- (i) Serikali imeendelea kuimarisha utekelezaji wa Mfuko wa Maendeleo ya Vijana ambao unalenga kuwasaidia vijana wahitimu wa ngazi mbalimbali za elimu kuweza kujiajiri kwa kuwapa mikopo ya mashati nafuu na mafunzo ya ujasiriamali. Katika kipindi cha mwaka 2013/2014 hadi mwaka 2016/2017 Serikali kupitia Mfuko wa Mendeleo ya Vijana imetoa mikopo ya masharti nafuu ya shilingi bilioni 5.8 kwa vikundi vya vijana 6,076 vyenye wanachama 30,380 katika Halmashauri za Wilaya 157 kupitia SACCOS za vijana. (ii) Serikali kupitia Halmashauri zinatenga maeneo kwa ajili a vijana wahitimu wa ngazi mbalimbali za elimu kufanya shughuli za uzalishaji mali ili kujipatia ajira. Katika mwaka 2016, jumla ya hekta 271,882 zilitengwa kwa ajili ya shughuli za vijana. SPIKA: Mheshimiwa Aida, swali la nyongeza. MHE. AIDA J. KHENAN: Mheshimiwa Spika, nakushukuru, naomba kuuliza maswali mawili ya nyongeza. Swali la kwanza, Serikali ya Awamu ya Tano imepunguza wafanyakazi kwenye kada mbalimbali kwa kigezo cha kutokuwa na sifa, ni lini sasa Serikali itatoa ajira kwa kuwapa kipaumbele vijana wa nchi hii ambao kwa sasa ni wengi wamerundikana mtaani? (Makofi) Mheshimiwa Spika, swali la pili; Kwa kuwa mikopo hiyo anayoizungumza Waziri, Halmashauri inatenga asilimia tano ambayo kwa sasa haiwezi kukidhi haja kulingana na idadai au wimbi kubwa la vijana waliopo mtaani. Serikali haioni sasa ni muda muafaka wa kuwa na mpango mkakati wa kuwapa mafunzo maalum au kuanzisha vyuo kwenye mikoa yote ili kuwapa ufanisi vijana waweze kujiajiri? (Makofi) SPIKA: Majibu ya maswali hayo mawili ya nyongeza, Mheshimiwa Antony Mavunde, Mbunge wa hapa tulipo. 6 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, VIJANA NA AJIRA: Mheshimiwa Spika, katika kutekeleza azma ya kutengeneza nafasi nyingi za ajira hasa kwa kundi kubwa hili la vijana, Serikali imekuja na mipango mikakati mbalimbali, si kweli kwamba tunaweza tukawa tuna nafasi za kuwaajiri vijana wote kwenye sekta ya umma, ndiyo maana kupituia program nilizozisema Serikali imeona ni vyema kuendelea kuishirikisha sekta binafsi, lakini vilevile na kwenda na falsafa ya uchumi wetu wa viwanda, lakini vilevile na kuwahimiza vijana kushiriki katika sekta za uzalishaji mali ikiwemo kilimo, ufugaji na biashara ili kwa pamoja tuwe tumetengeneza nafasi nyingi za ajira kwa vijana kuliko kuendelea kuwafanya vijana wengi wa Kitanzania kuamini kwamba nafasi za kazi ni lazima ziwe za maofisini. Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa Sera ya Ajira, imezungumza vyema kabisa tafsiri ya neno ajira maana yake ni shughuli yoyote halali inayompatia mtu kipato. Kwa hiyo, Serikali tunachokifanya ni kuendelea kutengeneza nafasi nyingi zaidi za ajira ili vijana wengi zaidi waweze kupata nafasi ya kujiajiri na kuajiri vijana wengine. Mheshimiwa Spika, swali lake la pili la nyongeza amesema ni lini tutaanzisha mkakati wa kuanzisha vyuo ili kuwajengea vijana

View Full Text

Details

  • File Type
    pdf
  • Upload Time
    -
  • Content Languages
    English
  • Upload User
    Anonymous/Not logged-in
  • File Pages
    235 Page
  • File Size
    -

Download

Channel Download Status
Express Download Enable

Copyright

We respect the copyrights and intellectual property rights of all users. All uploaded documents are either original works of the uploader or authorized works of the rightful owners.

  • Not to be reproduced or distributed without explicit permission.
  • Not used for commercial purposes outside of approved use cases.
  • Not used to infringe on the rights of the original creators.
  • If you believe any content infringes your copyright, please contact us immediately.

Support

For help with questions, suggestions, or problems, please contact us