13 MEI, 2013 MREMA 1.Pmd

13 MEI, 2013 MREMA 1.Pmd

13 MEI, 2013 BUNGE LA TANZANIA ________________ MAJADILIANO YA BUNGE ___________________ MKUTANO WA KUMI NA MOJA Kikao cha Ishirini na Nne - Tarehe 13 Mei, 2013 (Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Spika (Mhe. Job Y. Ndugai) Alisoma Dua Hati Zifuatazo Ziliwasilishwa Mezani na:- NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Ujenzi kwa Mwaka wa Fedha, 2013/2014. MHE. RITTA E. KABATI (K.n.y. MWENYEKITI WA KAMATI YA MIUNDOMBINU): Taarifa ya Kamati ya Miundombinu Kuhusu Utekelezaji wa Majukumu ya Wizara ya Ujenzi kwa Mwaka wa Fedha 2012/2013 na Maoni ya Kamati Kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo kwa Mwaka wa Fedha 2013/2014. 1 13 MEI, 2013 MHE. PAULINA P.GEKUL - MSEMAJI MKUU WA KAMBI YA UPINZANI WA WIZARA YA UJENZI: Taarifa ya Msemaji Mkuu wa Kambi ya Upinzani wa Wizara ya Ujenzi Kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo kwa Mwaka wa Fedha 2013/2014. MASWALI NA MAJIBU Na. 189 Fedha kwa Ajili ya Kuadhimisha Sherehe za Kitaifa MHE. HENRY D. SHEKIFU (K.n.y. MHE. MARY P. CHATANDA) aliuliza:- Katika kuadhimisha sherehe mbalimbali za Kitaifa nchini Serikali imekuwa ikitumia fedha nyingi sana. Je, Serikali itakuwa tayari kuokoa fedha kwa kuachana na Bajeti kubwa zilizotengwa kwa machapisho ya fulana (T- Shirts) na tafrija fupi ili fedha hizo ziweze kusaidia katika shughuli nyingine? WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, URATIBU, SERA NA BUNGE alijibu:- Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu, ninapenda kujibu swali la Mheshimiwa Mary Pius Chatanda, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli maadhimisho ya sherehe za kitaifa nchini yamekuwa yakigharimu Serikali fedha nyingi sana. Hata hivyo Serikali inachukua hatua mbalimbali ili kupunguza gharama hizo, Ofisi yangu imeandaa mapendekezo ya kupunguza idadi ya namna ya kuadhimisha sherehe hizo kwa mwaka. Wizara zimeshatoa mapendekezo kwa Waziri Mkuu ya namna maadhimisho ya sherehe mbalimbali zilizo chini ya Wizara hizo zingeweza kuadhimishwa sasa ili kupunguza gharama. 2 13 MEI, 2013 Kwa mfano baadhi ya sherehe za kisekta zimependekezwa kuanzishwa kila baada ya miaka mitatu mpaka mitano badala ya kila mwaka. Mapendekezo haya yanasubiri kujadiliwa katika vikao vya maamuzi ili yaanze kutumika rasmi. Mheshimiwa Naibu Spika, kwa sasa Serikali imepunguza kwa kiasi kikubwa bajeti ya uchapishaji wa fulana, kanga na vipeperushi kama sehemu ya maadhimisho ya sherehe za kitaifa. Sare zinazotolewa kama T-Shirts zinalenga makundi maalum tu ambayo ni muhimu kwa ajili ya ushereheshaji na kufikisha ujumbe mahsusi (kauli mbiu) kuhusu maadhimisho husika kwa wananchi. Aidha, tafrija fupi hufanyika wakati wa sherehe za Uhuru na Muungano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Tafrija hizi maalumu hasa kwa wageni maarufu wa Kimataifa ambao huwa wanaalikwa na Ikulu na ni wageni wa Mheshimiwa Rais. MHE. HENRY D. SHEKIFU: Mheshimiwa Naibu Spika, ninashukuru kwa majibu mazuri ya Mheshimiwa Waziri. Kwa kuwa sherehe hizi ni muhimu na kufanyika Kitaifa pia ni muhimu, lakini hakuna umuhimu wa kuzihamisha kutoka eneo moja kwenda eneo lingine maana zikihamishwa inabidi kuweka miundombinu mipya kwa ajili ya sherehe hizo, kama vile sherehe za mwenge. Hivi ni kwa nini tusiwe na eneo moja tukajua kuwa hili ndilo eneo litafanyika sherehe hizo ili kupunguza gharama? (Makofi) WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, URATIBU, SERA NA BUNGE: Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu ninapenda kumjibu Mheshimiwa Shekifu, swali lake la nyongeza kama ifauatavyo:- Ni kweli kuwa baadhi ya sherehe huwa zina hama, zinazunguka kila Mkoa na lengo ni kuhamasisha wananchi wa maeneo mbalimbali ili waweze kushiriki katika kutekeleza shughuli zinazoendana na Sera za Sherehe zile. Kwa mfano sherehe za nanenane zinafanywa Kikanda zinazunguka na Mwenge madhumuni yake ni tofauti kabisa na sherehe zingine kwa sababu unahimiza upendo nanupendo huwezi 3 13 MEI, 2013 kuwa katika Mkoa mmoja. Upendo uko kila Mkoa na unahitaji kuhimiza upendo. Unazunguka kuhamisha matumaini kutoka Mkoa mwingine kwenda Mkoa mwingine. Kwa hiyo nilifikiri shughuli za mwenge haziwezi kulinganishwa sana na shughuli zingine. Lakini tunachoangalia katika madhimisho ya Sherehe ya nchi siku nyingine kwa mfano siku ya maziwa, siku ya maji, siku ya nyuki na kadhalika. (Makofi) Mheshimiwa Naibu Spika, hizi zinaweza kuwa fixed katika kipindi fulani lakini baadhi ya sherehe zingine na pengine tunafikiri tunaweza kuangalia kuziunganisha. Kwa mfano Sherehe ya sabasaba sasa imekuwa ya maonyesho ya biashara. Lakini ukienda nanenane na yenyewe ina maonyesho ya biashara. kwa hiyo, kuna sherehe zingine ambazo tunaweza kuziunganisha zikafanyika mahala pamoja kitaifa na nyingine zikawa zinazunguka ili wananchi wote wapate bahati ya kuona na kuangalia maonyesho ya biashara. (Makofi) MHE. PAULINE P. GEKUL: Mheshimiwa Naibu Spika, inashukuru kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali moja la nyongeza pamoja na maadhimisho ya sherehe mbalimbali ambazo Waziri amezitaja lakini kuna hili la uzinduzi wa mwenge wananchi wamekuwa wakichangishwa, lakini wakati huohuo Serikali imekuwa na ndimi mbili kwamba mchango wa mwenge ni hiari lakini wafanyabiashara na wananchi na ofisi mbalimbali wamekuwa wakiandikiwa na Serikali kwamba wachangie. Ninaomba nipate kauli ya Serikali kwa nini wananchi hawa wanachangishwa wakati kuna fungu linatengwa kwa ajili ya kazi hiyo? WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, URATIBU, SERA NA BUNGE: Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli na ninajua kuwa Mikoa huwa inachangisha fedha lakini moja ya kazi za mbio za mwenge siyo zile shamrashamra tu mbio za mwenge mara nyingi huwa zinafanya shughuli nyingine za kuhimiza maendeleo, kama alama ya kichocheo cha kuhimiza shughuli za maendeleo ya kujitolea wannchi katika maeneo yale. (Makofi) 4 13 MEI, 2013 Kwa hiyo, wakati mwingine Mikoa huwa wanachangisha fedha kukamilisha shughuli fulani ambazo kwa pamoja wamezianzisha ili angalau zihitimishwe na shughuli ya mwenge. Mheshimiwa Gekul. Kuandikiwa barua na Serikali kuchangia siyo kosa maana hata kwenye arusi huwa tunaalikwa kuchangia na hatuchangi humu ndani kuna makadi mengi watu wanatuchangisha lakini hatuchangi,kama hupendi huchangi lakini kuandika barua ya mchango kwa Mkoa siyo mbaya. Lakini ungeniambia wanalazimisha hili ni suala jingine. Haturuhusu kulazimishwa lakini wananchi wanaruhusiwa kuchangia maendeleo yao kama pale Manyara wanavyochangia kujenga shule, Zahananti na miundombinu mingine kwa faida yao. Mheshimiwa Naibu Spika, fedha zinazotolewa na Serikali ni kwa ajili ya kugharamia mahitaji ya wale vijana wanaokumbiza mwenge kitaifa, mafuta ya mwenge wenyewe na gharama za usafiri za wale vijana. Lakini kwa maendeleo yanayohamasishwa na mwenge katika eneo lile wananchi lazima wachangie ili miradi yao waliyoibuni wao wenyewe iweze kukamilika. (Makofi) Na. 190 Ujenzi wa Stendi ya Mabasi Ngaramtoni MHE. DKT. AUGUSTINE L . MREMA aliuliza:- Je, Serikali ina mpango gani wa kujenga stendi ya mabasi katika Mji wa Marangu Mtoni ambao unakuwa kwa kasi na una magari mengi? 5 13 MEI, 2013 NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (ELIMU): alijibu:- Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu naomba kujibu swali la Mheshimiwa Dkt.Augustine Lyatonga Mrema, Mbunge wa Vunjo, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli kuwa Mji wa Marangu Mtoni unakuwa kwa kasi kubwa na kusababisha ongezeko la magari yanayotoa huduma katika maeneo hayo. Halmashauri ya Wilaya ya Moshi imeshatembelea eneo hilo la Marangu Mtoni na kulikagua, pamoja na kuandaa michoro na gharama za ujenzi wa stendi hiyo. Mheshimiwa Naibu Spika, gharama za ujenzi wa stendi hiyo zimekadiriwa kuwa shilingi 32,300,000/= pendekezo hili liko katika hatua za awali za kujadiliwa katika vikao vya Halmashauri ili mradi huo uweze kutengewa fedha na kutekelezwa ili kuondokana na msongamano mkubwa wa magari, pikipiki na biashara zilizopo katika eneo hilo. Mradi huu utakapokamilika unakusudiwa kuongeza vyanzo vya mapato kwa Halmashauri kutokana na huduma hiyo. Mheshimiwa Naibu Spika, ili kuhakikisha mpango huo unafanikiwa, Halmashauri imepanga kutumia wadau wengine wa maendeleo kwa kuzingatia Sera ya Public Private Partinership (PPP) ili kujenga na kuendesha mradi huo na kuufanya kuwa endelevu. MHE. DKT. AUGUSTINE L . MREMA: Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Waziri ninaomba kuuliza swali lifuatalo:- Kwa kuwa msongamano pale Marangu mtoni ni mkubwa na pale Marangu Mtoni ni Kituo cha barabara kubwa Himo, kwenda Kilema na kwenda Rombo. 6 13 MEI, 2013 Sasa swali ni kwamba badala ya kungojea Halmashauri ya Moshi ambayo haina hela tena kwenye jibu lako umesema wanapanga, ina maana hizo hela hazipo na mimi ningetaka ile stendi ijengwe haraka na mapema ili kuondoa huo msongamano pale. Ninaomba kujua Serikali kuu ina utaratibu gani wa kusaidia hizi Halmashauri wanapokuwa na miradi mizuri na mikubwa kama huu wa kujenga stendi ya basi Marangu Mtoni. Mnawasaidiaje kutumia benki, kutumia Bank guarantee, pamoja na mambo mengine kama hayo ili miradi iweze kutekelezeka? Mheshimiwa Naibu Spika, lakini kama tunaziachia Halmsahauri uwezo hawana hili swali litasusua hata miaka kumi jibu wewe Naibu Waziri unasemaje hapo (Makofi/ Kicheko). NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri unasemaje kuhusu hilo. Naibu Waziri Majibu tafadhali. NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (ELIMU): Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu ninao0mba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Dkt. Augustine Lyatonga Mrema, ninatambua ni Naibu Waziri Mkuu Mstaafu. Ni kweli

View Full Text

Details

  • File Type
    pdf
  • Upload Time
    -
  • Content Languages
    English
  • Upload User
    Anonymous/Not logged-in
  • File Pages
    256 Page
  • File Size
    -

Download

Channel Download Status
Express Download Enable

Copyright

We respect the copyrights and intellectual property rights of all users. All uploaded documents are either original works of the uploader or authorized works of the rightful owners.

  • Not to be reproduced or distributed without explicit permission.
  • Not used for commercial purposes outside of approved use cases.
  • Not used to infringe on the rights of the original creators.
  • If you believe any content infringes your copyright, please contact us immediately.

Support

For help with questions, suggestions, or problems, please contact us